Wafuasi wa wahhabi wanaweza kukataa kuwa
hayo si kweli, na wamesha andika vitabu kadhaa wakimsafisha Abdul Wahhab na
hayo niliyo yaeleza, lakini nukta moja ya msingi ambayo wote tunaweza kuitizama
kwa jicho moja ni kuwa, Mashariki ya kati haikuingia kwenye mikono ya
Illuminanti mpaka pale dola ya Kiislam ya Ottoman ilipoangushwa. Pia hakuna
shaka kuwa mataifa ya kigeni peke yao hayakuweza kuiangusha dola hii ila kwa
kutumia sera yao ya ‘divide and rule’ ambapo baadhi ya wananchi waligeuzwa na
kuwapiga wenzao na moja kwa moja kumsaidia mgeni kuwatawala.
BUSINESS KAMA KAWA
Mfalme Saud ambaye
aliahidiwa madaraka na kuhakikishiwa ufalme wake endapo atasaidia kuidhoofisha
na hatimaye kumuangusha ndugu yake wa Kiislam anaye tawala kupitia dola ya
Ottoman. Alilifanya hili kwa uzuri akishirikiana na Abdul Wahhab ambaye yeye
aliweza kutoa tafsiri mpya ya mafunzo ya Kiislam iliyo ruhusu muislamu mmoja
kumuua muislamu mwenzake. Tafsiri hii inatumiwa mpaka leo na vikundi mbalimbali
vinavyo endesha matukio ya ugaidi duniani, ambapo wao kumuwa muislamu mwenzao
kwa tuhuma zisizo na mashiko au bila hata tuhuma ni jambo la kawaida.
Ibn Saud
alipewa ujira wake kwa kupewa nchi iliyoitwa jina lake, yaani Saud Arabia, naye
alilipa fadhila hii kwa kuwaruhusu Illuminanti kushikilia hazina yote ya mafuta
ambayo sasa inatumiwa kwa faida ya New World Order.
Kwa hiyo kazi ya Wahhabi nyuma ya familia ya Saud ilikuwa ni kuwasaidia Freemason
wa Uingereza kuikamata dola ya Ottoman baada ya WWI. Kwa kiasi kikubwa lengo
hilo lilifanikiwa, kwani sehemu kubwa ya Mashariki ya kati ikawa ni makoloni ya
Ungereza, na hivyo Freemason wa Ulaya wakakipata kile walicho kuwa wakikisaka
kwa muda mrefu, moja ya nishati muhimu katika uchumi wa dunia hii, nishati ya
mafuta.
ONE FAMILY
Familia ya Illuminati ya kishetani
ya Rockefeller ndiyo iliyo patiwa funguo za hazina hiyo. Kupitia ushirika huu,
familia ya Saud itapata nafasi ya pekee kwenye muungano huu wa kishetani na
kwenye mpango mkubwa wa New World Order, ambapo familia hii itapewa nguvu juu
ya nishati hiyo, na miaka itakayo fuata faida kubwa itakayo patikana kwenye
mafuta, kati ya mengi itakayo tumiwa kufanya ni kufadhili kazi na tafsiri
potofu za mafunzo ya Uislamu zenye falsafa na mtiririko wa maono ya Khawarij,
Wahhabisim na Assassins kwenye ulimwengu wa Uislamu na ulimwengu kwa ujumla, na
mafundisho hayo yatatoa ruhusa ya kufanyika mauaji yatakayo itwa UGAIDI kama
yalivyo fanyika katika zama za wahhabism, mauaji haya kupitia mafundisho ya
Wahhabisim kwenye kanzu ya Uislamu ni muhimu mno kwa ajili ya ajenda ya New World
Order.
Mipango hii kamambe haitoki kwenye vinara wa Wahhabi na familia ya Saud
ambao wao si chochote si lolote katika mchezo huu mzima, bali ni wanasesere
walio fungwa kamba na mabwana wakubwa ambao huvichezesha viungo vyao namna
kulingana na matakwa ya ajenda.
Mabwana hawa wakubwa utawakuta katika jiji la London, ambalo linaendeshwa
na Bank of England ambavyo kama ilivyo Federal Reserve ya Marekani nayo hii
inamilikiwa na watu binafsi. Jiji hili la London nalo kama lilivyo jimbo la Washington
Marekani na jiji la Vatican Rome ni miji inayojitegemea kwa kila kitu na iko
juu ya sheria kuu za nchi hizo. Miji hii inazo sheria zake yenyewe. Jiji kama
la London liko chini ya meya ambaye ni lazima awe Freemason wa daraja la 33 na
hata Malkia na nguvu aliyopewa na Illuminanti hawezi kuingia ndani ya London
bila idhini ya meya huyu. Hivyo ndivyo ilivyo kwa miji mingine miwili ya
Vatican na Washington zote ni dola zinazo jitegemea kwa kila kitu.
Ni kichekesho kuwa rais Obama ni rais wa USA na kapata kura kutoka
Washington DC, na makao makuu ya serikali yake yapo hapo lakini hana nguvu
yoyote juu ya Washington D.C, na anapo chungulia kwenye moja ya madirisha ya
White House anauona mnara mkubwa mrefu na mweupe wa kimasoni kutoka Egypti
ukimuambia ni nani anaye iendesha Washington.
RAMANI YA MAJENGO MUHIMU YA SERIKALI NDANI AY WASHINGTON YANAPOUNGANISHWA HUTENGENEZA NEMBO YA KISHETANI, HILI SI KWA BAHATI MBAYA!
Kama Freemason walivyoweza kujipenyeza ndani ya ulimwengu wa Kikristo na
kuikamata dini hiyo vilivyo kupitia Kanisa Katoliki na kupitia viongozi wa
madhehebu mengine; kwa njia hiyohiyo wameitumia na kujipenyeza kwenye dini ya Uislamu
na kuweka vibaraka wao katika kila sehemu muhimu na ya kimaamuzi kupitia kwenye
asasi, taasisi, vyuo, nchi na hata dola zinazo dai ziko chini ya dini hii.
Mpango huu kwa upande wa kuivuruga dini ya Kiislamu, hasa kupitia mafunzo yake
ya msingi, Quran na Sunnah kwa ajili ya mpango kamambe, ambao kwa sasa picha
yake inaanza kuonekana, mpango huu ulifahamika kama Oxford Movement, kitovu cha
shughuli ilikuwa ni Egypti. Lengo lilikuwa kuisambaza Scotish Freemason ndani
ya Mashariki ya Kati kwa ajili ya kuandaa vijana watakao kuja na tafsiri
tofauti ya usilaumu. Kupitia Grand Lodge la Egypti chini utawala wa Ismailia, Freemason
ya Egypti iliweza kuvuka bahari na kufika Ulaya ambako ilipelekea kuzaliwa kwa
Scottish Freemason ambayo sasa kupitia Oxford Movement ni kama inarudi nyumbani
kwa wazee wake.
Vinara nyuma ya Oxford Movement alikuwepo mwanachama wa Palladian Rite
Freemason Albert Pike, alikuwepo Lord Palmerston na alikuwepo aliyekuwa waziri
mkuu wa England na Freemason wa daraja la juu Benjamin Disraeli na Edward
Bullwer-Lytton aliyekuwa mwanachama wa asasi ya siri iliyofahamika kama
Rosicrucianism. Mpango huu ulikuja kupewa nguvu na asasi nyingine ya siri inayo
fahamika kama Jesuits.( Dreyfuss, Hostage
to Khomeini)
Oxford Movement ilishughulika na kuingiza mafunzo mapya kwenye Uislamu
ambaye baadaye yalikuja kujulikana kama Salafi (Salafi hii tunayoiona leo au
New Salafisim). Mafunzo na tafsiri hizi mpya kutoka kwenye mahekalu ya kimasoni
yalikuweka msingi wa mbinu mbaya ya illuminanti itakayo kuja kufahamika
kama ugaidi.
Muanzilishi wa Salafi hii mpya anajulikana
kama Jamal ud Din al Afighani, jamaa huyu alikuwa ni jasusi wa Uingereza. Baada
ya Egypti kuingia kwenye mkataba wa kusaidia kuipanua Seuz Canal na baadaye
ikashindwa kulilipa deni hilo iliweka chini ya uangalizi wa Ufaransa na
Uingereza bila nguvu zozote za kiserikali. Chini ya kiongozi aliyefahamika
kama Ahmed Urabi wazalendo wa Egypti
wakajiunga kuyapinga maamuzi hayo na hivyo kuipatia fursa Uingereza kwa
kisingizio cha kulinda maslahi yake ya Suez Canal kuifanya Egypt kuwa ni koloni
lake.
Kijana aliyetumiwa kuchochea vurugu na harakati hizo za wazalendo wa
Egypti na hatimaye Uingereza kufanikisha mpango wake hakuwa mwingine bali ni
Jaml ud Din al Afghani (Ibid)
Baadaye Salafi wakajiunga na Wahhabi wa Saudi Arabia. Wakati Salafi itakuwa
ni chombo muhimu cha kutengeneza tafsiri kutoka kwenye aya za Quran na mafunzo
ya mtume zitakazo ruhusu kile tutakachoiita ugaidi, Wahhabi wa Saud chini ya
utawala wa familia ya Saud wao ndiyo watakao kuwa wadhamini wakubwa wa mpango
huu kupitia faida wanayo kusanya kwenye biashara ya mafuta ambayo nayo haiko
tena kwenye mikono na uma wa Kiislam bali kwenye familia ya kishetani na
illuminati ya Rockefeller. Familia hii ya Saud imepewa nafasi muhimu kwenye
picha kubwa ya New World Order kwani ulimwengu mzima umefanywa utegemee nishati
hiyo ya mafuta peke yake na hivyo kutengeneza faida maradufu na wakati huohuo
kuamua hatma ya uchumi wa dunia kupitia mafuta.
BUSINESS AS USUAL
Mashariki ya kati bado kuliendelea kuchafuliwa. Mwaka 1891 baba yake na Ibn
Saud alilazimika kuikimbilia Kuwait akiiwacha Riyadh imekaliwa na Ottoman.
Baadaye tena Ibn Saud akaanzisha mapambano ya kuikamata Riyaadh akisaidiwa na Uingereza.
Baadaye Uingereza wakaongeza msaada wao kwa Ibn Saud ili komuongezea nguvu
zaidi kisilaha na kifedha dhidi ya dola ya Ottoman.
Mustafa Kemal Ataturk
Hata hivyo ni mpaka mwaka 1918 chini ya mtu aliyeitwa Faisal dola ya
Ottoman ndani ya Mashariki ya Kati ilipinduliwa. Eneo hilo likagaiwa baina ya
mataifa makubwa yaliyo kuwa yakilitolea macho eneo hilo. Mtu aliyeitwa Mustafa
Kemal Ataturk kutoka Uturuki hakukubaliana na mgawanyo huo mpya wa Mashariki ya
Kati. Aliunda jeshi ambalo liliwatimua wa Giriki na wa Italia nje ya Anatolia.
Uingereza na Ufaransa hawakuingilia mpambano huo. Inasemekana Ataturk hakuwa
mfuasi wa Uislamu bali Myahudi. Mwaka 1923 wakati Jamhuri ya Uturuki inaundwa
Ataturk ndiye aliyechaguliwa kuwa rais wa kwanza wa taifa hilo na mwaka 1924
alitumika vizuri kukimaliza kile kilicho fahamika kama Khilafa au Ukhalifa wa
dola ya Kiislam ulio dumu kwa miaka elfu moja na mia tatu.
Wakati WWI inaelekea ukingoni Faisal aliendelea kulikamata eneo kubwa la
Arabia ikiwemo Jordan na sehemu za Syria. Hata hivyo wakati Faisal anaendelea
kujipanua kimipaka Uingereza nao walikuwa na ajenda yao ya siri ya kuigawanya
Mashariki ya Kati kutokana na maono yao. Mwisho wa siku Faisal alikuwa
amesalitiwa na mgawanyo huo mpya ambapo yeye alipewa eneo la Iraq tu. Ili
kuhakikisha Faisal hawi kitisho siku za usoni, Uingereza ikawatumia marafiki
zake wa muda mrefu, Wahhabi wa Saud chini ya Ibn Saud kuyakamata maeneo ya
Penisula yaliyokuwa chini ya Faisal.
Faisal alishindwa na Wahhabi wakaikamata penisula ya Arabia. Ni katika
kipindi hichi makubaliano ya kuungana baina ya Wahhabi na Salafi yalifanyika.
Mwaka 1924 chini ya jasusi wa Uingereza Wahhabi walifanikiwa kuikamata Makkaha
tena. Mwaka 1926 Ibn Saud akaita kongamano la kimataifa kuuarifu ulimwengu kuwa
anaishikilia miji miwili mitakatifu ya Makkah na Medinah. Mwaka 1932 Kingdom of
Saudi Arabia ikaundwa rasmi kwa msaada wa Freemason wa Uingereza, na mfalme
akiwa ni kibaraka wa Uingereza, kiongozi wa Wahhabisim na Salaf na mfuasi wa
sufiism Ibn Saud. Miaka iliyo fuata Ibn Saud alizilipa fadhila hizo za kufanywa
ni mfalme wa Saudi Arabia wakati mababu zake wanadamu ya Kiyahudi toka Ghaibar
kwa kuyagawa mafuta ya eneo hilo takatifu kwa makampuni mbalimbali yaliyo chini
ya Illuminanti na familia zao za kishetani na Rockefeller wakipatia nusu nzima
ya uzalishaji wa mafuta hayo.
.jpg)
NA HII NDIYO NEMBO YA MAPOLISI WA SAUDIA, JE UMEONA ALAMA YA JICHO MOJA KWENYE NEMBO HII, JE UMEONA TAJI LA MFALME JUU YA JICHO HILO, UNADHANI NI MFLAME GANI HUYO MWENYE JICHO MOJA ANAYETAMBULISHWA NA NEMBO HII?
PICHA HII IMEPIGWA NDANI YA MASJID HARRAM, MAKKA, HAPO NI MAALI CHACHE SANA KUTOKA ILIPO AL-KAABAH TUKUFU, NA TIZAMA BEJI YA ASKARI HUYO, NI ILE YA MFLAME MWENYE JICHO MOJA, YAAN MASIH DAJJAL.
PICHA HII NI NJE YA MSIKITI WA MAKKAH, NA HUYU NI ASKARI WA KUFANYA DORIA, LAKINI UMEIYONA NEMBO YA DAJJAL KWENYE VAZI LA ASKARI HUYU? USISAHAU HAPO NI KWENYE MSIKITI MTAKATIFU WA MAKKAH.
Kupitia kwa mtu aliyeitwa Jack Philby, Allen Dulles ambaye alikuwa rais wa Council
on Foreign Relation (CFR) na baadaye kuwa ni kiongozi wa CIA waliisaidia
Rockefeller kuishika Saud Arabia ambaye itakuja kuwa ndiye wazalishaji wakubwa,
karibu nusu ya mafuta yote duniani yatazalishwa ndani ya Saud Arabia. Mwaka
1933 Saud Arabia ikatoa kibali kwa California Arabian Standard Oil Company
(CASOC) ambayo nayo ilikuwa na mahusiano na Standard Oil ya California. Mwaka
1936 Socal na Texas Oil wakatengeneza ushirika mbao baadaye ulikuja kufahamika
kama Arabian-American Oil Company (Aramco).
Makampuni saba makubwa ya mafuta
yakawa pamoja katika kutawala soko la mafuta, makampuni hayo yakaja kufahamika
kama Seven Sisters. Makampuni haya yakishirikiana na utawala wa kifalme wa Saudi
yanamiliki utajiri mkubwa na nguvu kubwa kutokana na faida wanayotengeneza
kwenye nishati hiyo.
DO I NEED TO SAY MORE?
Mpango mzima ni kumsimamisha muislamu kwenye uwanja wa WWIII, uso kwa uso
na yoyote ambaye hatokuwa muislamu na hapa zikiwemo nchi za Ulaya pamoja na
Israeli. Lakini kabla ya kumsimamisha muislamu kwenye uwanja huo wa WWIII
kwanza lazima wamfanye muislamu akubali na kuamini kuwa wazo hili ni lake na
linatoka kwenye vitabu vyake.
HII BENDERA MAHUSUSI UTAWAKUTA NAYO BOKO HARAM, ALSHABAB, AL-QAEEDAH NA WENGINE KANA KWAMBA MBUNIFU NYUMA YA BENDERA HII NDIYO MBUNIFU WA MAKUNDI YOTE HAYA, NA WALA SIYO QURAN, WALA SUNNAH, BALI NI KUTOKA WASHINGTON, NYUMA YA CIA.
Vikundi kama vya Wahhabi, Salafi, Sufi na wengine
tayari wana aina hii ya mtazamo kutokana na kazi kubwa iliyofanyika kwenye
miaka ya ’50 mpaka ’60 baina ya Wahhabi na Salafi. Mpaka kwenye miaka ya ’50
Mashariki ya Kati ilikuwa ikiwaka moto kutokana na nadharia hizi ambazo ni za kimasoni
zaidi kuliko Kiislam. Kipindi hichi ndicho kilicho kuwa kipindi cha vuguvugu la
ukombozi na kupigania uhuru.
Utaona kundi kama la Muslim Brotherhood lilivyo
jishughulisha na harakati za ukombozi zaidi na njia tofauti na imani yao waliyo
tumia kwenye harakati hizo. Kundi hili lilikuwa chini ya uangalizi wa Uingereza
na mahusiano yake na Hitler yalikuwa mazuri kiasi cha kupeana na kubadilishana
mbinu za kijeshi. Muslim Brotherhood iliundwa kwa ajili ya maslahi ya Uingereza
na Illuminanti kwa ujumla na kazi zao zinazo wawakilisha mabwana wakubwa hao
tunaziona mpaka sasa ndani ya Egypti na sehemu mbalimbali ulimwenguni.
MUFTI WA EGYPT ALIPOKUTANA NA HITLER MWAKA 1941. MUFTI ALITAKA MSSADA WA KINAZI DHIDI YA WAYAHUDI WANAO IKALIA PALESTINE. MAHUSIANO HAYO NDIYO YALIYOPALILIA MAHUSIANO KATI YA MUSLIM BROTHERHOOD NA NAZI
MWAKA 1943 MUFTI WA EGYPT ALILITEMBELEA JESHI LA KINAZI ALMAARUF SS, KATIKA KUJENGA MAHUSIANO BAINA YA NAZI NA WANAHARAKATI WA KIISLAM EGYPT, WAKIWEMO MUSLIM BROTHERHOOD.
Ilikuwa ni sera ya Uingereza kuyanyonya makoloni yake na kuyaacha hoi na
machovu kwa kila kitu. Lakini pia ilikuwa ni sera ya Club of Rome na CIA
kutumia mwanya huo wa mgawanyo usio kuwa sawa kwenye mali ghafi za uma kuunda
wapigania uhuru na wanaharakati ambao miongozo yao haitotoka kwa viongozi wao,
bali kutoka kwenye asasi ya Club of Rome, Commitee of 300, CIA na
Freemason. Wana stratejia wa Illuminanti
kama vile Dr. Alexander Kings, Henry Kissinger, Zbigniew Brzezinski na Bernard
Lewis kwa makini na mipango madhubutu wakishirikiana na CIA, utawala wa Saud,
vikundi mbalimbali vya wanaharakati wa kupigania uhuru walitengeneza kile
tunachoita Waislam wenye siasa kali (New Salafi au kizazi kipya cha Khawarij)
ambao watatumiwa kwenye harakati za ukombozi kwenye nchi na sehemu mbalimbali
mashariki ya kati kabla ya kuwapeleka
Afighanistani kuuangusha utawala wa Kisovieti kwa jina lilelile la
Jihad.

PICHA INAYO SEMA MANENO 1000. KWAMBA MUSLIM BROTHERHOOD ILIZALIWA PAMOJA NA UNAZI, IKALELEWA NA UINGEREZA, NA SASA INAFANYA KAZI ZAKE KAMA CHOMBO HURU LAKINI CHENYE KUSUBIRI MIONGOZO KUTOKA WASHINGTON.
Lakini kwanza kabla ya hilo Shah wa Iran alitakiwa aondoke na kibaraka
mwingine wa Illuminanti aliyeitwa Khomeini akalie kiti hicho. Muslim
Brotherhood, CIA na Club of Rome walishirikiana vilivyo kuhakikisha Khomein
anaichukua Iran. Utawala wa Khomein ni muhimu kwa vile utatoa mwanya wa
kutengenezwa kwa makundi mengine ya Kishia ambayo nayo yatakuwa na msimamo
mkali na kuendesha harakati zao kwa namna ileile wanavyo fanya wale ambao
wanajiita kuwa wanapigania Jihad.
Pia Iran utawala huu utatumiwa kama ni
kitisho kwa nchi za Ulaya na washirika wake kwenye kile kitakachoitwa mradi wa
kinyuklia ambayo nayo ni karata muhimu inayosubiri saa na wakati kabla ya
kutupwa mezani na kuipamba ile njia ya kuelekea kwenye WWIII (kwa sasa
unavyosoma makala hii, karata hiyo imeshaanza kuchezwa).
Kwanza walimuweka Shah baada ya kuuondoa utawala wa Mossadegh. Shah akalipa
fadhila kwa kubinafsisha viwanda vya mafuta kwa nchi za magharibi zilizomsaidia
kuingia kwenye madaraka. Miaka ishirini na tano baadaye nguvu iliyo mweka Shah
madarakani ikamuona hafai inabidi aondolewe na nafasi yake akapewa Khomein.
Iraq alikuwepo Saddam muda wake ulipo kwisha walimuondoa na kumuweka Ghazi
Mashal Ajil al-Yawer na sasa Jalal Talabani. Zunguka Mashariki ya kati yote
utakutana na hadithi hii ya aina moja.
Kwa njia hii Iluminanti wanayabakiza mataifa ya Kiarabu kwenye mgawanyiko
na wakati huohuo wao wakitoa mwongozo wa wapi yaeleke; hii tunaiita golden rule
ya ‘Divede and Rule’, na hata sasa inatumika kwenye nchi nyingi za dunia ya
tatu. Kwenye kile ambacho wanastratejia wa Illuminanti walikiita ‘Arc of Crisis’
haikuwa kingine bali kutengeneza mgawanyiko wa kidini, kiitikadi, kisiasa na
kimakabila ndani ya mashariki ya kati, mgawanyiko huu ungepelekea kuwepo kwa
vikundi na makundi yatakayo endesha vuguvugu za aina mbalimbali kutoka zile za
kidini mpaka kisiasa, kijamii na kimakabila.
Makundi haya mitandao yao itaachiwa ikue na ipanuke kwa misaada kutoka kwa
mashirika ya kijasusi ya Illuminanti na baadhi ya nchi za Kiarabu. Makundi haya
yatatumika sehemu mbalimbali kwa ajili ya kufanya mapinduzi, ukombozi na
kutetea uhuru. Baadaye vijana hawa watajulikana kama ni Mujahidina na
watapelekwa Afighanistani kuungusha utawala wa Kisovieti. Kisha baada ya hapo
utaachiwa utanuke na kutangaza vita na mataifa yote ya Ulaya na washirika wake
kokote walipo duniani kwa kile watakachokiita ni Maadui wa Uislamu na Waislam.
Hii ni hatua muhimu ambayo itafanikisha kumsogeza Muislamu kwenye uwanja wa
WWIII. Kwani mpango mzima ni mapinduzi ya mwisho yatakayo zaliwa ndani ya
WWIII. Mapinduzi haya ni muhimu kwa ajili ya kuzifuta serikali na dini zote
duniani, hivyo ni muhimu WWIII kupiganwa kwa kisingizio cha dini kuliko siasa;
huko ndiko ambako vita dhidi ya ugaidi inapo tupeleka.
ILIKUWA NI MWAKA 1983, NDANI YA WHITE HOUSE, DONALD REGERN, RAIS WA MAREKANI WAKATI HUO, ALIPOKUTANA NA WAPIGANAJI WA TALIBANI NA KUWEKA MAKUBALIANO YA KUWASAIDIA DHIDI YA USSR KUPITIA SHIRIKA LA KIJASUSI LA PAKISTANI.
Tukirudi Iran kutizama namna mchezo mzima ullivyo chezwa na namna karata
moja baada ya nyingine ilivyo tupwa na kutenegeza Arc of Crisis, tutizame namna
Khomein alivyosaidiwa na Illuminanti kuichukua Iran. Wakati watu walio msaidia
Shah kuchukua madaraka walipokuwa wakimshawishi Shah kuzibadilisha sera zake
zifanane na zile za kimagharibi kitu ambacho walifahamu kitamsababishia
matatizo yeye na watu wake; wakati huohuo watu haohao walimuwezesha Ayatollah
Khomein kusimama kama alama, nembo na kiongozi wa kidini zaidi na anayejali,
anayeheshimu na anayejitolea kwa kila kitu kusimamia maadili ya kidini ya nchi
hiyo.
Club of Rome wakishirikiana na Muslim Brotherhood waliandaa mikakati ya
kumuondoa Shah madarakani ambaye ni wao ndiyo walio muweka hapo mara ya kwanza
baada ya kumsaidia Shah kumpindua Mossadegh aliyewekwa madarakani kwenye
uchaguzi wa mwaka 1953.
Illuminanti ilibidi kumuondoa Shah kwa vile yeye alikuwa na mpango wa
kuendeleza viwanda vya kinuklia nchini mwake. Shah alikuwa na mtazamo wa
kuifanya Iran kuwa na sura ya kimagharibi kwa maana ya kimaendeleo katika
nyanja mbalimbali. Hili halikuwa jambo zuri kwa Illuminanti kwani Iran itakuwa
na nguvu za kimaamuzi zaidi na kiuchumi kuliko inavyo takiwa kuwa. Kwa kutumia
mawakala wao mbalimbali llluminanti wakaanza kupalilia mbegu zinazo kizana na
mtazamo wa kimaterilisti ambao ndiyo ulikuwa mtazamo wa Shah, mbegu hizo
zilipandwa kwa vijana mbalimbali kupitia taasisi za kimataifa na kitaifa ndani
ya Iran.
Mmoja wa mawakala wa illuminanti waliotumiwa kupanda mbegu ya
antimaterilistik kwa vijana wa Kiirani kupitia kwenye sekta ya elimu ni bwana
Ali Shariati, ambaye naye pia anatajwa kuwa ni Freemason. Kupitia kwake wasomi
wakubwa wa vyuo mbalimbali ndani ya Iran waliingizwa kwenye duara linalo mpinga
Shah na sera zake za materelisim. Kupitia kwa wasomi hawa na kupitia kwenye taasisi muhimu ya elimu
ndani ya Tehran Shariati aliwafunulia vijana wa ki-Iran kazi za waandishi kama
vile Jean-Paul Sartre, Frantz Fanon, Albert Camus, Jacques Berque na Louis
Massignon, waandishi hawa ni wapinzani wa kubwa wa mambo ya ubeberu na
materialist, hata hivyo waandishi hawa wote wanafadhiliwa na kufuata miongozo ya
Club of Rome.( Dobry, Gary. The Body
Politic. <http://www.onthecanvas.com/body_politic.htm>)
TAHRIR SQURE' HAIKUANZIA EGYPT, NA WALA SI LAZIMA IWE NDANI YA EGYPT, POPOTE PALE WANAPO TAKA MABWANA WAKUBWA, PAWE NI 'TAHRIR SQURE' KWA AJILI YA KUMNG'OA WASIYE MTAKA NA KUWEKA WANAYE MTAKA ...
Wanafalsafa hawa hawakuwa chochote zaidi ya wana propaganda wa Illuminanti
na maandishi yao yalifuata mwongozo na matakwa ya Illuminanti. Nadharia yao ya
kupambana na ukoloni ilishikilia msimamo wenye sera za vurugu, kivita na
utumiaji wa nguvu kuliko njia ya amani. Waliamini ni kupitia kwa mtutu wa
bunduki tu ndiyo uhuru utapatikana.
SINA HAKIKA SANA NA PICHA HII, LAKINI MTU ALIYE KUSHOTO KWENYE PICHA HII, AL MAARUF KAMA ZBIG, NDIYE 'THE BRAIN' NYUMA YA MPANGO WA WATALEBANI UPIGANA JIHAD DHIDI YA USSR, NA NDIYE ALIYEKUWA MSHAURI WA REGARN KIPINDI HICHO, NA NDIYE ALIYEMSHAWISHI RAIS HUYO KUWASAPOTI TALIBAN. NA LEO ANAYO NAFASI KAMA HIYO KWA KIJANA NAYEITWA OBAMA, NA NATUMIA MBINU ILEILE KUIWASHA DUNIA MOTO NA HASA AFRIKA KWA MASLAHI YA MAREKANI.
Si kupitia kwenye dini ya Uislamu bali kupitia kwa wanafalsafa hawa wa kimasoni
na nadharia zao za vurugu kama njia ya kuleta amani ndipo vijana wa ki-Iran
walipofunguliwa kwenye utaratibu wa siasa ambao leo tunauita Ugaidi. Ni kwakupitia
kwenye sera hizi za vibaraka na mawakala
wa Illuminanti ndiyo Iran ikaweza kuandaliwa kama kituo muhimu cha
kudhamini na kutoa misaada mbalimbali kwa wale ambao leo tunawaita ni magaidi,
Sera hizo hazikutoka kwenye vitabu na mafunzo ya Kiislam bali yalitoka kwenye
kabrasha na miongozo ya Club of Rome.
Wanafalsafa hawa kwenye maandishi yao wanasisitiza kuwa vurugu ni kitu
kizuri, vurugu nimuhimu kwa nchi za dunia ya tatu endapo zinataka kujitoa
kwenye mikono ya kikoloni, wanadai wana propaganda hao wa Illuminanti kuwa si
kwamba tu vurugu zitatuletea uhuru wetu, bali pia kisaikolojia zitaturudishia
uwezo wetu wa kujiamini dhidi ya mataifa ya kimagharibi.
Hichi ndicho wanacho dai vijana wa Salafi ya sasa, hichi ndicho wanacho
king’ang’ania, wanakuambia hapawezi pakaeleweka hapa mpaka tuchapane kwanza!
Nami narudi nyuma na kuwauliza hicho mnacho kitaka sicho ambacho walichoambiwa
Talibani, wakaambiwa wa Iraq, wakaambiwa wa Iran, wakaambiwa wa Libya, wa
Syria, Boko Haram, Alshabab, Seleka na wengine wengi? Hamuoni, hamtazami mambo
kwa jicho pana na kuona mnachezewa? Majibu yao watazunguka na kuzunguka katika
mazungumzo yao na nukta ya mwisho watarudi palepale, lazima tuchapane, nami
napata hofu kuwa kile tulicho kuwa tukikihofia kipo mbele ya macho yetu
kikitutazama, mitazamo ya Khawarij, Assassin, New Salafi na Wahhabi
zimeshapenyezwa kwenye fikra na mitazamo ya vijana wetu. Zimepenyezwa na nani
na kwa faida ya nani, hapo ndipo palipo na hekima.
Kupitia sera hizi wapigania uhuru wa
nchi mbalimbali ili wabidi kuingia msituni ili kuweza kumng’oa mkoloni, kwa
mtazamo wa karibu nchi hizi zilifanikiwa kumng’oa adui yao, lakini imewachukua
miaka mingi wasomi wetu kutambua kuwa hatukumng’oa mkoloni, imewachukua miaka
mingi kutambua kuwa nchi zetu bado zinatawaliwa na wakoloni, nchi zetu
zimewekwa chini ya mashirika ya kimataifa, wakurugenzi, ma-CO na ma-share
holders wa mashirika hayo ndiyo wasimamizi, waongozaji, wasemaji wa kila
kinacho zihusu nchi hizi, viongozi wa nchi zetu ni kama wamefungwa mikono,
midomo na miguu na wameachiwa macho kutazama tu. Tizama http://salimmsangi.blogspot.com/2014/01/malighafi-za-afrika-na-damu-ya-waafrika.html
nimelielezea hili kwa kina, kwa mtazamo wa mbali nchi hizi zimeweza kupanda ile
mbegu ya ugaidi dhidi ya mataifa ya magharibi. Mbegu hii ni muhimu kwa mataifa
ya Magharibi kuliko nchi zetu zilivyo dhania. Nyingi ya nchi hizi zimeendelea
kuwa ni mawakala wa vitendo vya kigaidi kwa namna mbalimbali kwa vipindi
tofauti katika historia zao.
Khomein alipingana na sera za Shah, lakini yeye alitumia sura ya udini
zaidi ilikuonesha mapungufu ya Shah kwa wa Iran ambao idadi kubwa wanashikilia misingi ya dini ya
Ushia kuliko siasa za kimagharibi, lakini kilichokuwa ni cha ajabu zaidi ni
kuwa miongozo ya Khomein nayo haukutokea kwingine ila kwa wafadhili wake wa
nchi za magharibi. Mpaka mwaka 1964 alipofukuzwa alikuwa bado anaishi kwenye
mji wa kidini wa Qom na alikuwa na mawasiliano mazuri na Uingereza ambayo
inasemwa walimpatia masurufu ya kifedha kila mwezi. Khomein alipofukuzwa Iran
alikimbilia kuishi Iraq mpaka alipotiwa nguvuni na utawala wa Iraq. Utawala wa
Ufaransa ulilazimishwa kumpa hifadhi Khomein. Alipokuwa Ufaransa mambo
yaliendelea kubadilika kwa kasi, na picha kubwa ilisomeka hivi;
Bigbrotherhood / Illuminanti hawamtaki tena Shah na Khomein ndiye atakaye
kuwa kibaraka wao mpya. Akiwa hapo alipokea msururu wa wageni kutoka BBC, CIA
na kutoka kwenye shirika la kijasusi la Uingereza. BBC wakawa ni promota namba
moja wa Khomein. (Goodgame, Globalists
and the Islamists. http://www.redmoonrising.com/Ikhwan/BritIslam.htm)
BBC wakahusika vilivyo katika kusambaza kaseti za Khomein kwa watu
mbalimbali wa Iran hasa kwa viongozi wa kidini. Kwenye kaseti hizo Khomein
alizungumzia kuhusu ubaya wa utawala wa Shah. BBC wakaenda mbali zaidi,
wakauonesha ulimwengu ubaya na mateso yanayo fanywa na kundi la kijasusi la
Shah, kundi la SAVAK, asasi hii ya ujasusi hakuiunda Shah peke yake bali kwa
msaada mkubwa wa nchi zilizo muwezesha kuingia madarakani, lakini kwa vile leo
hatakiwi basi kila ubaya wake ambao mwanzo ulifanywa siri ulianikwa. Mchezo huu
waliufanya tena kwenye miaka ya tisini na elfu mbili pale ajenda ilipomchoka
Saddama Hussein.
Ilipofika September na October 1978 BBC ilianza kurusha matangazo yenye
mawazo na fikra za kimapinduzi moja kwa moja Iran kwa lugha ya Kifursi, lugha
ya taifa la Iran, hivyo kila mtu aliweza kumsikia Khomein kupitia lugha yao ya
asili kupitia BBC. Gazeti la Washington Post likatoka na kichwa cha habari kuwa
‘BBC ni adui namba moja wa nchi ya Iran’.
MWISHO UKAWA NI WIMBO WA KILA MTU, SHAH MUST GO!!
Haikuchukua muda wimbi la watu hasa vijana wanafunzi na wasomi wakachukuliwa
na vuguvugu la kimapinduzi la Khomein ambao kupitia kwa propaganda za BBC
waliona kuna haja ya kurudishwa kwa utawala wa kidini wa Kishia na hivyo Shah
aondoke na Khomein aingie ili atekeleze maono hayo kwa faida ya nchi yao.
Lakini walikosea kitu kimoja, haikuwa kwa faida yao bali kwa faida ya
Illuminanti. Utawala wa Carter kutoka kwenye White House za Marekani, ukifuata
muongozo wa Zbgniew Brzezinski mwanastratejia mkubwa wa Illuminanti na kinara
wa New World Order ulishirikiana na utawala wa Uingereza kumtoa Shaha Iran na
kumuingiza Khomein ndani ya nyumba.
KAMA WALIVYO WALIOMTANGULIA, NAYE MUONGOZO WAKE HAUKUTOKA PENGINE ZAIDI YA UINGEREZA, MAREKANI NA UFARANSA.
Kuanzia kipindi hicho mpaka Khomein alipofariki mwaka 1989, Iran ikawa ni
kituo cha kimataifa cha kuendesha sera za chuki dhidi ya mataifa ya magharibi,
kwa maneno mengine kituo cha kimataifa kwa kuendesha sera za ugaidi dhidi ya
mataifa ya magharibi.
Mtu mwerevu atajiuliza ni vipi utawala wa Khomein uliosaidiwa kuingia
madarakani na nchi za Magharibi leo uendeshe mapambano dhidi ya mataifa hayo
ambayo ndiyo wafadhili wake wakubwa? Jibu ni kuwa utawala huo ulitakiwa uingie
madarakani ili uweze kuendesha vita hivyo na hivyo kutengeneza mazingira ya
kuwepo kwa makundi mbalimbali ya kigaidi ambayo yatategemea msaada wa moja kwa
moja kutoka Tehran, na hapa tunakutana na Hizbullah, tunakutana na makundi
mbalimbali ya kipalestina mbayo yanapokea misaada yao kutoka Tehran kupambana
na adui wa Uislamu na muislamu, kupambana na mataifa ya magharibi, na hapa
tunapata vita dhidi ya ugaidi na hii ndiyo picha kubwa ambayo wengi walishindwa
kuiona, na wengi bado hawaioni, vita dhidi ya ugaidi si kwa faida ya Uislamu,
na kama tulivyona vita hivi havikuzaliwa ndani ya Uislamu na wala havihusiani
chochote na Uislamu, bali ni kwa faida ya Illuminanti, ambao kwao ni hatua
muhimu kulifikia lile lengo la milenia nyingi, lengo la kuwa na serikali moja
na dini moja kwa dunia yote na walimwengu wote, lengo litakalo fikiwa kupitia
mapinduzi na vita vikubwa. Mapinduzi na vita hivyo yamekwisha tokea katika zama
tofautitofauti, na sasa imebaki hatua moja kubwa ya mwisho, nayo ni WWIII,
ambayo itafikiwa kupitia vita dhidi ya Ugaidi.

NA PUNDE MICHAKATO YA KUWAFADHILI MUJAHEEDINA NA WAPIGANIA UHURU IKAANZA ... HILI NDILO WALILOKUWA WAKILITAKA ILLUMINANTI.
Mwaka 1979 Bernad Lewis alipewa fursa ya kuhudhuria kwenye mkutano unao
fanyika mara moja kwa mwaka, mkutano wa siri wa asasi ya Bilderberg, Lewis
alitoa maono yake ya namna gani Mashariki ya Kati itaendelea kutawalika na
wakati huohuo kutumika kuipigisha ajenda hatua kupitia vita dhidi ya ugaidi.
Lewis aliwataka Illuminanti kukitengeneza kile kitakacho itwa ‘Waislam wenye
siasa kali’ ndani ya Mashariki ya kati, Waislam hao watasaidia migawanyiko
mbalimbali yenye sura ya kisiasa, kidini, kiuchumi na kijamii. Migawanyiko hii
pia ipewe fursa ya kuanzisha vuguvugu la kimapinduzi, na kupigania uhuru wa
wachache ambao wanaoneka kunyonywa au kutengwa na wengi, mfano wa Kurdu,
Armeniani, Druze, Azerbaijani Turk, Copto wa Ehiopia, Sudan na makabila yao,
Waarabu na makabila yao.
MWANAJESHI WA KIMAREKANI BEGA KWA BEGA AKISHIRIKIANA NA WAPIGANAJI WA TALIBANI ... JIULIZE NI NANI MLENGWA IKIWA MMAREKANI NA MTALIBANI WAKO JESHI MOJA?
Mpango huu utafanikiwa kwa kutumia mbinu zote chafu na za siri za
Illuminanti kupitia kwa CIA ambao kwa mlango wa nyuma watafadhili na kutoa mwongozo
kwa vikundi hivi. Kupitia mpango huu Iran ilitoa ushirikiano na kuto msaada wa
kiukombozi kwa watu walio itwa wapigania uhuru wa Palestine, Ireland ya
Kaskazini, Sudan na Ivory Cost.( Labeviere, Richard. Dollars for Terror. p. 215)
Illuminanti ndiyo walioitengeneza na kuipa nguvu Urusi na hatimaye kuifanya
kuwa ndiyo taifa lenye nguvu duniani kuliko yote (Super Power), mchakato huo
ulifanyika baada ya WWI na WWII, kati ya sababu moja wapo ya Urusi kufanywa
Super Power ni ili kutengeneza taifa lenye nguvu na lisilo na dini. Hata hivyo
u-super power wa Urusi ulitakiwa kufa na kile kilicho julikana kama vita
baridi.
Ajenda ilikuwa inapiga hatua nyingine kubwa, hatua ambayo itaifikisha
kwenye WWIII. Nchi iliyo chaguliwa kuifikisha ajenda hapo haikuwa Urusi bali
Marekani, taifa teule la Illuminanti, taifa ambalo maelfu ya miaka nyuma, hata
kabla ya zama za Plato tayari lilishateuliwa kuifanikisha kazi hii muhimu na makhususi
kwa Illuminanti. Hivyo vita baridi na harakati za kuliteka anga kwa njia ya
kumfikisha binadamu mwenzini kwa mara ya kwanza katika historia yake vyote
vilikuwa ni maagizo ya kuangusha utawala wa kisoviet na kulikaribisha taifa
teule la Marekani kwenye ulingo wa u-super power.
WAS HE? SURE HE DIDNT, BUT WHY THEY TELLING US THAT HE DID?
Kwa ajili ya kumbukumbu napenda kugusia hapa kuwa hakuna binadamu
aliyekwenda mwezini, si Urusi wala Marekani walioweza kumpeleka binadamu
mwenzini, huu ulikuwa na bado ni uwongo mkubwa katika historia ya binaadam
kupata kutolewa na mataifa makubwa duniani, na bado mpaka sasa unaendelea
kufundishwa kwa namna na njia mbalimbali kuwa binaadam alikwenda mwezini,
lakini ukweli ni kuwa hakuna binaadam aliye kanyaga mwezini, kifupi hakuna
binaadam aliyepata kutoka nje ya orbiti ya dunia. Kwenye vitabu vya kidini
mathalani Biblia na Quran kuna hadithi kuhusu mitume waliopaa kwenda mbinguni,
hii ni hadithi tofauti na ninayo zungumzia , mimi nazungumzia binaadam kwenda
mwezini katika zama zetu zinazoitwa za sayansi na teknolojia, katika zama zetu
hizi ambazo teknolojia yetu inasemwa ipo juu.
Nasikitika kukuambia kuwa
teknolojia hii ni duni mno kiasi cha kwamba haiwezi hata kumtoa binaadam nje ya
orbit ya dunia na kumrudisha akiwa hai achilia mbali kumpeleka mwezini, haiwezi
kufanya hivyo ni duni mno. Hivyo safari ya kwenda mwezini ilikuwa ni danganya
toto. Samahani kama na wewe ni miongoni mwa walio nunua uongo huo.
.jpg)
MOJA YA PICHA ZILIZOPIGWA 'MWEZINI', UNYAYO WA NAMNA HII HAUWEZI KUACHA KWENYE USO WA MWEZI AMBAPO HAKUNA NGUVU ZA MVUTANO, HIVYO USINGEONEKANA KABISA, AU ATHARI YA UNYAYO HUO INGEONEKANA KWA MBALI SANA, LAKINI KWA VILE PICHA HII IMENASWA KWENYE USO WA DUNIA, MAHALI WALIPOIGIZA TUKIO ZIMA LA KWENDA MWEZINI NDIYO MAANA ATHARI YA UNYAYO HUU, NI SAWASAWA NA MTU ANAYEKANYAGA JUU YA ARIDHI NA SIYO MWEZINI.
Hivyo sakata la vita baridi na nguvu zake zilikuwa na lengo la kumuingiza
mwali mpya, Marekani kwenye ulingo wa super power na kumuondoa Urusi. Lakini
Urusi haikuwa imesambaratika mpaka pale watu walio itwa kuwa ni mujaheedina
kutoka Afighanistani , na kutoka katika kila kona ya dunia walipo pambanishwa
na Urusi.
ITAENDELEA HAPA INSHALLAH ...
iyo ya mwezi ndo umeniacha hoi ucsahau na ile ishu ya ndege ya malasyia
ReplyDeleteHaupo mbali sana, kwa mtazamo wangu tukio la kwenda mwezini na hili la ndege kupotea vinawiana sawasawa, nikipata wasaa Mola akipenda huenda nikaishusha hiyo skendo ya mwezini na hapo utanipata vyema ... big up for your observation ...
ReplyDeleteJe hao neo salafy ndo hawa salafy swaleh wenye kufuata kitabu na sunna?
ReplyDeleteHapana! Ispokuwa wanatumia jina hilo zuri ili kuweza kuuhadaa umma.
DeleteNimejaribu kuuliza kwa ahlul elm kuhusiana na huyo mwanzilishi wa muslim brother hood wakathibitisha kweli alikuwa freemason na pia alikuwa akijiita salafy ila katika vitabu vya masalafy wamemthibitisha kuwa yeye ni free mason, ukijaribu kupitia katika kitabu cha aliyeanzisha chuo cha Daarul hadithy (salafiya) fiy dammaj yemen Sheikh Muqbil Rahmahu Allah amemthibitisha na kusema yeye siyo katika wale wenye kujinasibisha na wema walotangulia bali lengo lao lilikuwa ni kudanganya umma ili kuwagawa makundi
ReplyDeleteSuch a good comment from my reader, keep it up Abu Hudhaifa na waelimishe wengine pia.
Deleteyou seem to have a good capacity in analytical journalism. Hongera, lakina hautubainishii vyanzo vya habari zako. Upande wa jinsi uislamu unavyohusishwa na ugaidi wakati magaidi ni wamarekani hapo sina shaka. Lakini hili la safari za mwezini I reserve my comment. Good job keep it up...
ReplyDeleteNakushuru kwa maoni yako, kwenye vyanzo au 'source' ya hizi taarifa sehemu nyingi sana nimeweza kuweka, ila nitaboresha zaidi kwa kuongeza idadi ya vyanzo na kuviweka vionekane kwa wepesi. Karibu sana na endelea kutembelea blogi hii.
ReplyDeleteThis is all shia propaganda.
ReplyDeleteHivi Iran wangekuwa chini ya ottaman wangekubali kuendeshwa kutokaa ankara?
Basi zimbabwe au namibia wangeacha tu wazungu watawale kule kwa vile ni wakristo wenzao ?
Ottoman ilikua dola ya kituruki zaidi kuliko ya kiislam. Hakuna cha illuminati wala nini , dunia hii ya sasa ni maslahi na wenye nguvu ndio wamehodhi rasilimali zote.
Ghadafi na Assad wa syria hawana tofauti na Shah w iran , wote ni madictactor tu.
Huku shah kaondolewa na mashia na ghadafi na assad ataondoles na ameondolewa na mussuni , yanayotekea sasa ya isis ni harakati za wengine kuzuia suni wasitawale kule sasa wana upaka matope uislam.
N hi zote hizi ni maslah na zote zinafadhili vikundi vya kigaidi kuifkia maalendo y kisiasa ni kiuchumi
Iran ina hizbollah , houthi na vikundi vya mauaji kule bahrAin, sawa na saudi na alqaeeda.
Kuweka photo shop za bush na abdalla wakibusiana ni kuonesha kiwango cha namna gani mtu unaweza kukubali kutumiwa kufanya propaganda za kijinga ambazo hazimsaidi miislam wala mtanzania
Nakushukuru kwa maoni yako Riyadh Seif,
DeleteIla Umekosea Riyadh hizi siyo propaganda za Kishia hata kidogo.
Maoni yako yako vizuri kabisa na kwa namana fulani maoni yako yapo sawa ispokuwa kwenye nukta ya HIZI NI PROPAGANDA ZA KISHIA.
Sina cha kusema Ikiwa Ottamn ilikuwa ni dola ya Kituriki zaidi kuliko Kiislam, sababu ilibidi Wazayani kufanya njama za kuanzisha WWI na moja ya malengo yake ilikuwa ni kuiangusha dola hiyo, na Uturuki ilikuja kuzaliwa baada ya kuanguka kwa Ottaman, na wanazuoni wa Kiislam kutoka Azhar Cairo ilibidi kukutana kutoa msimamo wao juu ya hilo, na kwa miaka 2 Uingereza walipambana kumshinikiza rais wa Egypt wa wakati huo kuhakikisha mkutano huo haufanyiki, na ulipofanyika walito msisimamo wao kwamba Kuvunjwa kwa Khilafah Ya Ottaman ni Bid'aa na Haram.
Japo Ottaman ilikuwa na mapungufu yake kama zilivyokuwa dola zingine za Kiislam baada ya makhalifa wa 4 kuondoka, lakini bado ilikuwa ni nembo na alama ya Dola ya Kiislam na Uingereza kwa kushirikiana na Ibn Saud, ndiyo waliweza kuiangusha dola hiyo.
Kwanini basi Ibn Saud akishirikiana na Wahhab hawakuisimamisha Khilafah baada yakuanguka kwa Ottaman? Mpaka leo hakuna Khilafah, au haikuwa kwenye mpango wao kuisimamisha tena dola hiyo? Na vipi wataisimamisha ikiwa watu waliowawezasha kupambana na dola hiyo ndiyo bado wanaishikilia.
Ni kweli unavyosema kuwa dunia ya leo ni mwenye nguvu ndiye anayefanya atakavyo, na vikundi vingi vya kigaidi vinafadhiliwa na serikali mbalimbali kama ulivyo ainisha, LAKINI KUFIKIRI KWAMBA VURUGU YA MASHARIKI YA KATI HIVI SASA NI SUNNI KUZUILIWA KUTAWALA, NADHANI UTAKUWA UMEFIKIRI CHINI YA KIWANGO CHAKO, NI KWELI KWENYE USO WA MBELE NDIVYO INAVYOONEKANA, LAKINI MALENGO MAKUU SIYO HAYO, MALENGO MAKUU NI KUWA MAREKANI SASA ANAILINDA 'PETRO DOLAR' AMBAYO MCHINA, MRUSI, MVENEZUELA, MJAPAN, MUIRAN WAMESHAITUPA, SASA MAREKANI ANAFANYA KILA ANALOWEZA KUNUSURU MKTABA BAINA YAKE NA NCHI ZA MAFUTA ULIOFANYA NA KISSINGER CHINI YA NIXXON MWAKA 1973 KUHAKIKISHA KUWA MAFUTA YOTE YATAUZWA KWA DOLA, NA MAREKANI ITATOA SILAHA NA ULINZI KWA NCHI HIZO. lIBYA ALITAKA KUUZA KWA DINAR, AKANG'OLEWA, SADDAM ALIANZA KUUZA KWA ERO, AKATOLEWA, NILIO WATAJA HAPO JUU WAMESHA ACHANA NA SARAFU YA DOLA KATIKA BIASHARA ZAO WENYEWE, SASA MAREKANI LAZIMA APAMBANE KUHAKIKISHA MAFUTA YATAENDELEA KUUZWA KWA DOLA AMA VINGINEVYO SARAFU YA DOLA HAINA THAMANI YEYOTE KOKOTE. SO KINACHOENDELEA MASHARIKI YA KATI SIYO ISHU YA SUNNI AU SHIA, AU ISIS, AU YEYOTE YULE, KINACHOENDELEA NI HARAKATI ZA KUINUSURU PETRO DOLLAR.
KUHUSU PICHA YA BUSH NA ABDALLA KUBUSIANA SIYO USHAHIDI JUU YA POSTO HII. NADHANI SEHEMU NYINGI NIMEWEKA REFERENCE KAMA USHAHIDI, PICHA ZA KWENYE MTANDAO HATA KIDOGO HAZIWEZI KUTUMIKA KAMA USHAHIDI, ITS JUST A DECORATION, ILA NASHUKURU KWA KULIONA HILO.
ENDELEA KUSOMA BLOGI YETU KARIBU SANA.
Daaah dunia inafikia mwisho
ReplyDeleteBado unayo nafasi ya kufanya kitu. Think BiG
Delete