Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Showing posts with label Masih Dajjal. Show all posts
Showing posts with label Masih Dajjal. Show all posts

Friday, August 5, 2016

MFALME OBAMA: Ep 2


Mungu anapo wateuwa mitume wanakuwa wanatoka katika mkondo wa damu maalum, anakuwa chini ya uangalizi wa Muumba wake kuanzia maisha ya wazee wake, maisha yake akiwa tomboni, utoto wake, ujana wake mpaka anapo kabiziwa jukumu hilo zito na tukufu kwa ajili ya kuwaongoza watu wake. 

Monday, November 2, 2015

DOLA YA KISHETANI NA USHOGA



ILANI YA MASHOGA



Leo nataka tuongele suala la Mashoga!

Kwa waaumini wa dini mbalimbali suala hili ni moja ya alama za siku za mwisho. Kwa maadui zetu ni alama muhimu ya kufikia kwenye malengo yao mahususi.

Ushoga kwanza unaingia kwenye ile mbinu ya  kupunguza idadi ya watu duniani. Pili ushoga unachangia kusambaza nguvu hasi (negative energy) kwenye uso wa dunia ambalo hilo ni muhimu sana kwa dola la Shetani kusimama.
BENDERA YA MASHOGA

Mtandao wa mashoga haujapata nguvu na sauti kwa bahati mbaya, na sasa nguvu na sauti hiyo inasukumwa ionekane na kusikika katika kila kona ya dunia. Lakini wenye hekima na busara tunafahamu kabisa kuwa nguvu na sauti hizo si zakwao hata kidogo. Lakini ni watu wachache tulio wapa nguvu na sauti hiyo kama viongozi ndiyo wameruhusu mashoga kupaza sauti katika kila uchochoro wa dunia.

Sunday, June 22, 2014

USICHO KIJUA KUHUSU VITA DHIDI YA UGAIDI NA UISLAM Pt 2


Wafuasi wa wahhabi wanaweza kukataa kuwa hayo si kweli, na wamesha andika vitabu kadhaa wakimsafisha Abdul Wahhab na hayo niliyo yaeleza, lakini nukta moja ya msingi ambayo wote tunaweza kuitizama kwa jicho moja ni kuwa, Mashariki ya kati haikuingia kwenye mikono ya Illuminanti mpaka pale dola ya Kiislam ya Ottoman ilipoangushwa. Pia hakuna shaka kuwa mataifa ya kigeni peke yao hayakuweza kuiangusha dola hii ila kwa kutumia sera yao ya ‘divide and rule’ ambapo baadhi ya wananchi waligeuzwa na kuwapiga wenzao na moja kwa moja kumsaidia mgeni kuwatawala. 
BUSINESS KAMA KAWA


Mfalme Saud ambaye aliahidiwa madaraka na kuhakikishiwa ufalme wake endapo atasaidia kuidhoofisha na hatimaye kumuangusha ndugu yake wa Kiislam anaye tawala kupitia dola ya Ottoman. Alilifanya hili kwa uzuri akishirikiana na Abdul Wahhab ambaye yeye aliweza kutoa tafsiri mpya ya mafunzo ya Kiislam iliyo ruhusu muislamu mmoja kumuua muislamu mwenzake. Tafsiri hii inatumiwa mpaka leo na vikundi mbalimbali vinavyo endesha matukio ya ugaidi duniani, ambapo wao kumuwa muislamu mwenzao kwa tuhuma zisizo na mashiko au bila hata tuhuma ni jambo la kawaida. 

Ibn Saud alipewa ujira wake kwa kupewa nchi iliyoitwa jina lake, yaani Saud Arabia, naye alilipa fadhila hii kwa kuwaruhusu Illuminanti kushikilia hazina yote ya mafuta ambayo sasa inatumiwa kwa faida ya New World Order.


Sunday, June 15, 2014

USICHO KIFAHAMU KUHUSIANA NA VITA DHIDI YA UGAIDI Pt 1


Ningependa kuianza makala hii kwa hadithi mbili,

Hadithi ya kwanza

Hudhaifa (ra) anasema kwamba, amesema mtume (saw): “Kwa hakika, nahofia kati yenu yule mtu ambaye ataisoma Quran kiasi kwamba nuru ya Quran itaonekana kwenye uso wake ... halafu neema hii itaondolewa pale atakapoidharau na kuipa mgongo na atabeba upanga wake kumshambulia jirani yake na kumtuhumu kuwa ni mshirikina.” Mtume (saw) akauliza ni nani kati ya wawili hao atakuwa anazistahiki hizo tuhuma? -  Mwenye kutuhumu au mtuhumiwa? Mtume (saw) akajibu ni, “mwenye kutuhumu.”

Hadithi ya pili.

Imam Bukhari (Allah amrehemu) ameeleza, “Umar ibn al-Khattab (ra), ambaye alikuwa akizungumza na masahaba, aliwauliza, ‘Ni nani kati yenu mwenye elimu zaidi kuhusiana na fitnah?’ Hudhaifah (ra) akajitokeza na kusema, ‘Mimi ewe Ameer ul-Muumini! Kisha akaanza kuzitaja baadhi ya fitnah Umar ibn al-Khattab (ra) akasema, ‘Siyo fitnah hizo ningependa kufahamu kuhusiana na fitnah ambazo wimbi lake litakuwa kama wimbi la bahari.’ Hudhaifa (ra) akauliza ‘Kwanini unataka kujua kuhusina na hizo fitnah ewe Ameer ul-Muuminin? Kati yako na hizo fitnah kuna mlango ulio fungwa.’ Umar (ra) akauliza ‘Je mlango huo utavunjwa au utafunguliwa?’ Hudhaifah (ra) akajibu, ‘Utavunjika’ Umar (ra) akajibu, ‘Basi hautafunga mpaka siku ya kiyamah..’

KUNA AMBAYE YUPO BIZE SANA KUFITINISHA IMANI HIZI MBILI.

Monday, December 2, 2013

NAMBARI TISA (9) NA KUMI NA MOJA (11) KWENYE DUNIA YA KIMASONIA

LEOTUTAZUNGUMZIA ALAMA NEMBO ZA KIMASONIA, NA LEO TUTATIZAMA KWA UNDANI NAMBARI TISA (9), KISHA KUMI NA MOJA (11), HALAFU MWENGE …

Kwa freemasonry lugha yao ipo mahususi kwenye maumbo na alama mbalimbali lakini pia bila kusahau nambari, umuhimu wa nambari kwa freemasonry na asasi nyingine za siri unakuja pale ambapo elimu ya kale kabisa ilihifadhiwa katika nambari na kwa watu hawa hisabati limekuwa ni somo muhimu mno,

“Elimu ya kwanza duniani imekuja Kwa alama mbalimbali, hekima za watu wa Chaldean, Phoenician, Egypty, Kaanani, wanafalsafa kama akina Zoroaster, Sanchoniathon, Pherecydes, Syrus, Pythagoras, Socrates na Plato, vyote vya zamani vilivyokuja katika mikono yetu, vimekuja kwa njia ya alama”

Tuesday, August 13, 2013

HATUA NNE KABLA YA UJIO WA MASIHDAJJAL/KRISTO WA UWONGO/MPINGA KRISTO/666


PROJECT BLUE BEAM

Waandishi wawili wa habari waliokuwa wakifuatilia sakata ya hichi tunacho kizungumzia hivi sasa au maarufu kama Blue Beam wote wawili walikutikana wamekufa kwa ‘ugonjwa wa moyo’ ingawa kwenye historia yao hawakupata kuwa na magojwa ya moyo. Vifo vyao vilitofautiana kwa wiki kila mmoja.

Sege Monast alikuwa ni mwandishi wa Internationa Free Press Canada, huyu ni mmoja kati ya waandishi wawili walio kutwa wamekufa kwa ‘ugonjwa wa moyo’.

Moja ya wadau wanao isimamia Project Blue Beam ni NASA, na mradi huu umegawanywa katika sehemu nne ambazo zitafanikisha kuisimamisha New World Order na Masih Dajjal/Kristo wa Uwongo akiwa ndiye kiongozi wa serikali hiyo.

Wednesday, July 3, 2013

MAANA HALISI YA 666

Wapendwa!
Tarehe ambayo 666 Ilikuwa ubaoni ....

Sehemu hii ndogo kuhusiana na nambari 666 nimeitoa kwenye, sura moja ndani ya kitabu kinacho kwenda kwa jina la “FREEMASON; Dunia usiyo ifahamu”, 

kitabu hichi ni nimeandika mwenyewe, na soon Maulana akipenda mtakiona mtaani, hivyo sehemu hii kuitoa kwenye kitabu na kuwamegea ni zawadi kwenu wasomaji wangu, please ipokeeni ....

.... Kwa watafiti huru wa mambo ya UFO na New World Order ni kuwa serikali na ‘sayansi’ wanapigia debe taarifa hizo kwa lengo lilelile la New World Order ambayo kiongozi wake atakuwa na ‘damu takatifu’ na mwenye nguvu za maajabu.

Mmoja anaye tegemewa ni wazo ambalo liko kwenye imani ya dini mbalimbali duniani, ikiwemo kwenye Uyahudi, Uislamu na Ukristo na bila kusahau kwenye imani na dini za kishetani ukiwemo Freemasons.