Ningependa kuianza makala hii kwa hadithi mbili,
Hadithi ya kwanza
Hudhaifa (ra) anasema kwamba, amesema mtume (saw): “Kwa hakika, nahofia
kati yenu yule mtu ambaye ataisoma Quran kiasi kwamba nuru ya Quran itaonekana
kwenye uso wake ... halafu neema hii itaondolewa pale atakapoidharau na kuipa
mgongo na atabeba upanga wake kumshambulia jirani yake na kumtuhumu kuwa ni
mshirikina.” Mtume (saw) akauliza ni nani kati ya wawili hao atakuwa
anazistahiki hizo tuhuma? - Mwenye
kutuhumu au mtuhumiwa? Mtume (saw) akajibu ni, “mwenye kutuhumu.”
Hadithi ya pili.
Imam Bukhari (Allah amrehemu) ameeleza, “Umar ibn al-Khattab (ra), ambaye
alikuwa akizungumza na masahaba, aliwauliza, ‘Ni nani kati yenu mwenye elimu
zaidi kuhusiana na fitnah?’ Hudhaifah (ra) akajitokeza na kusema, ‘Mimi ewe
Ameer ul-Muumini! Kisha akaanza kuzitaja baadhi ya fitnah Umar ibn al-Khattab
(ra) akasema, ‘Siyo fitnah hizo ningependa kufahamu kuhusiana na fitnah ambazo
wimbi lake litakuwa kama wimbi la bahari.’ Hudhaifa (ra) akauliza ‘Kwanini
unataka kujua kuhusina na hizo fitnah ewe Ameer ul-Muuminin? Kati yako na hizo
fitnah kuna mlango ulio fungwa.’ Umar (ra) akauliza ‘Je mlango huo utavunjwa au
utafunguliwa?’ Hudhaifah (ra) akajibu, ‘Utavunjika’ Umar (ra) akajibu, ‘Basi
hautafunga mpaka siku ya kiyamah..’
KUNA AMBAYE YUPO BIZE SANA KUFITINISHA IMANI HIZI MBILI.
Hadithi hizo mbili tutakuwa tukizirejelea kila pale zitakapo hitajika,
lakini kwanza tuanze na hii ya pili. Hadithi hii inatuthibitishia kuwa fitnah
katika Uislam imeingia baada ya kufa kwa Umar (ra) ambaye katika hadithi hiyo
hapo juu mpaka mwisho wake inamtaja Umar (ra) kuwa ndiye mlango baina ya fitnah
na umma wa kiislam. Fitnah ya kwanza katika umma ni kuuwawa kwa Umar (ra), kitu
kinacho ashiria kuvunjika kwa mlango ulikuwapo baina ya fitnah na dini hii ya
Uislamu, hivyo baada ya hapo fitnah zinazo kwenda kama mawimbi ya bahari
zikaanza kumiminika.
Fitnah iliyofuatia ni kuwawa kwa khalifah watatu wa Waislamu, Uthman bin
Khafan (ra), kwa kiasi kikubwa kifo chake kilitokana na Myahudi aliye ingia
katika Uislam kwa nia ya kuubomoa Uislamu akiwa ndani.
Wauwaji wa Uthman (ra) wakamfuata Ali (ra) na kumtaka awe Khalifah, Ali
(ra) alikataa, lakini waliendelea kumsihi na kumsisitizia mpaka akakubali.
WANASHIRIKIANA NA WASIYO WAISLAM KUUBOMOA UISLAM
Muawiyah (ra) kama ndugu wa karibu wa Othumani (ra) alikuja kutaka haki
itendeke dhidi ya wauaji wa ndugu zake, lakini Ali (ra) akimsihi achukue kiapo
kwanza cha kumtii kabla hajaanza kazi ya
kutafuta haki ya ndugu yake, na hapo ikawa mvutano ambao ulipelekea fitna kubwa
baina ya Waislam, kwanza Mama wa Waumini Aisha (ra) na Ali, baadaye
vilimalizika vita hivyo na Ali (ra) akamsindikiza Aisha (ra) kurudi nyumbani,
halafu vita vya Suffin baina ya Muawiyah na Ali (ra) ambavyo pamoja na hasara
kubwa iliyo patikana katika umma wa kiislam, Muawiya alisalimu amri na Ali (ra)
alikubaliana na hilo.
Lakini watu waliomuwa Othaman (ra), na ambao walikuwa wamejipenyeza kwenye
jeshi la Ali (ra) na ambao ndiyo waliyo anzisha vita hivyo vya Suffin, watu
hawa wakaondoka kwenye jeshi la Ali (ra) kwa kutumia kauli maarufu (la hukm illa lillahi) ‘Hukmu ni ya Mwenyeezi Mungu peke yake’ na kwamba Ali amefanya makosa
kupatana na Muawiya (ra), amefanya makosa kwa kutumia ‘maoni’ yake dhidi ya
amri ya Allah. Hapo ndipo walipo pata jina la Khawarij, likiwa na maana ya wale
wenye kujitenga.
MWISHO WA YOTE NI MUISLAM KUMUUWA MUISLAM.
Utakumbuka watu hawa ndiyo waanzilishi wa fitna hii, na ndiyo waliyo
pelekea vita baina ya Waislam kwa Waislam, na kila wakiona damu wanashiriki,
wakiona amani, wanajitenga.
NYUMA YAKE KUNA MNARA WA MSIKITI MKONONI KUNA KITABU CHA QURAN NA MKONO MWINGINE KUNA BUNDUKI. HII NDIYO PICHA WANAYO PANDIKIZWA WATU KUWA NAYO DHIDI YA UISLAM.
Lakini mzizi wa kundi hili ulikuwepo tangu wakati wa Rasulullah (saw), kutokana
na hadithi iliyo simuliwa na Said Khudhuri, kutoka kwenye kitabu cha Bukhar,
kwamba wakati mtume (saw) anagawanya ngawira, alikuja mtu kutoka kwenye kabila
la Tamim na jina lake ni Dhul-Khuwaisar, mtu huyu kwa jeuri na kiburi
akamuambia mtume (saw) tenda haki!, mtume wa Allah akamuambia, ole wako, ni
nani atakaye tenda haki kama mimi sitaitenda. Omar (ra) akataka ruhusa kwa
mtume (saw) ili aweze kukitenganisha kichwa na kiwiliwili cha mtu huyo, lakini
mtume akamuambia, Muache. Atakuwa na wafuasi. Na mtakapo linganisha swala zao
na zenu mtaiona ya kwenu si chochote kitu, na saumu yenu si chochote
ukilinganisha na ya kwao, wataisoma Quran lakini haitavuka koromeo lao.
Watatoka na kuiacha dini yao kama mshale unavyo wacha shabaha yake. Abu Saiid
akaendelea kusema, Naapa nilikuwepo wakati Ali ibn Abi Talib alipopambana nao
na kuwapiga. Ali (ra) alitoa amri kuwa kiongozi wao atafutwe katika maiti wao,
na alipatikana kama ambavyo Mtume (saw) alivyo muelezea sifa zake.
.jpg)
KHAWARIJ WANAPIGANA JIHAD NA WAISLAMU WENZAO, TANGU ZAMA HIZO MPAKA LEO.
Watu hawa walikuja kupigana na Ali (ra) katika vita vya Naharwan baada ya
kumkamata sahaba na familia yake na kuwaua, mke wa Sahaba alikuwa na ujauzito,
walimpasua tumbo na kukitoa kichanga hicho na kukiuwa. Baada ya hapo Ali (ra)
alipambana nao, na hatimaye mwili wa kiongozi wao ukaletwa mbele ya Ali (ra) kama
nilivyo taja hapo juu.
Khawari waliendelea kuwepo hata baada ya vita hivyo, na wanaendelea uwepo
hata mpaka sasa, na siku zote hawakuwa wakipambana na yeyote isipokuwa Waislam.
Yeyote aliyewapinga walimuita ni Kafir na ni haki kwao kuwapiga watu wao na
hata kuuwa wanawake zao na watoto wao na kuchukua mali zao. Nafi ibn al Azraq
mmoja wa viongozi wa moja ya makundi ya Khawarij alikuwa akisema ‘wapinzani
wetu ni washirikina na hivyo hatupaswi kurudisha chochote tunacho kaishikilia
dhidi yao.’ (Abd al-Qahir 82-84)
Baada ya kifo chake Nafi Ibn Azraq, katika vita wafuasi wake wakampa
utawala Ubaydallah ibn Ma’mun al-Tamimi. Naye huyu Ubaydallah akauwawa katika
vita vingine pamoja na kaka yake Uthman ibn Ma’mun. Baada ya hapo wakampa
uongozi wao bwana Qatari ibn al Fuj’a, ambaye walimuita Amir al-Muuminina. (Abd al-Qahir 85-86)
MSAHAFU NA BUNDUKI, HUU NDIYO UISLAM WA LEO.
Kwenye mikono ya watu hawa ambao nao walijiita ni ‘waislamu’, maelfu kwa
maelfu ya waumini wa Kiislamu waliuwawa, mali zao kuporwa na heshima zao
kuvunjwa, Khawarij walifikia kuwaita waumini wa Kiislamu ni makafiri na wenye
kustahiki kuwawa kwa vile hawakukubaliana na mtazamo wao wa kiitikadi.
Lakini tumeona kisa cha Dhuli-Khuwaysira, ambaye alidiriki kusimama mbele
ya mtukufu wa daraja (saw) na akamuambia kwa ukali na kwa dharau, “tenda haki”
naye huyu anahisabiwa kuwa Khawarij wa mwanzo kabisa, na ambako misimamo ya
viongozi wengine wa Khawarij ilifuata nyayo zake, na watu hawa hawakuwa ni
fitina kwa kipindi fulani tu cha historia ya umma huu, lakini unapo itazama
historia ya umma na fitina zake utaona Khawarij walikuwa ni njia au mawimbi ya
fitina hizo. Mtume (saw) amesema, fitna ya watu hawa itaendelea, haikatiki.
Kizazi kimoja cha watu hawa kinapo toweka, basi kingine kinakuja, mpaka katika
zama za Dajjal zitakapo fika. Mtume (saw) amesema kizazi kimoja kinapo toweka
kwa maana ya kuwa hawafuatani katika mstari ulionyooka, kizazi kimoja kinakuja
kisha kinaondoka, sababu mwisho wa yote watu hawa wakikosa watu wakupingana
nao, wanaishia kupingana, kuuwana wao kwa wao, kisha kizazi hicho kinatoweka,
halafu kinakuja kuibuka tena kingine baada ya kitambo fulani, tena huenda
kikaibukia sehemu nyingine kabisa. Hadithi kutoka kwa Ibn Maaja, kutoka kwa Ibn
Omar anasema alimsikia mtume (saw) akisema “ ... kila kizazi kimoja kinapo tokea,
hutoweka ( eidha kwa kuuana wao kwa wao au kwa nguvu pinzani) kisha kingine
kitafuata nacho kitatoweka, Ibn Omar anasema mtume wa Allah alirudia hivyo
zaidi ya mara 20 kisha akasema mpaka Dajjal atakapo tokea.
Ibn Omar akaendelea kusema kuwa, Khawarij ni watu wabaya zaidi, kwani
wanazichukua aya za Quran zinazo walenga makafiri na kuwashambulia nazo
waumini. Wanawashutumu waumini kuwa ni makafiri kwa kutumia ayah ambazo misingi
yake inawalenga makafiri. Ni wepesi sana kwa kuwahukumu watu na kuwaita makafiri.
Rejea hadithi ya kwanza ya mtume niliyo itaja katika makala hii nayo ikielezea
jambo hilohilo kutoka kwenye kinywa cha Rasullullah.
SURA MBILI.
Nayo hiyo ndiyo moja ya sifa zao kubwa, moja kuwa na msimamo mkali
kupitiliza (extremisim), pili kuwatuhumu Waislamu kuwa ni makafiri na tatu
kumwaga damu ya Waislamu, kuchukua mali zao na kuwavunjia heshima zao. Na ni
kwa sifa hizo kuu tatu utaona imekuwa ni rahisi kwa wao kumwaga damu ya maelfu
na malaki za Waislamu kuanzia pale walipomuua Othman (ra).
Ingawa kwa ujumla
wao wanafahamika kama Khawarij, lakini kwa sifa au tabia hizo nilizo zitaja
wamekuwa wakija na majina tofauti katika zama na maeneo mbalimbali kwenye historia
ya umma.
HIZI NI SURA MAARUFU KWENYE HARAKATI ZA KIISLAM, LAKINI NAMNA YA HARAKATI HIZO ZILIVYO NA ZINAVYOFANYIKA ZINATIA SHAKA NA DOA KWENYE MAFUNZO HALISI YA UISLAM, NA YANABEBA KILA RANGI YA KHAWARIJ.
Kuna kundi lilikuwa likifahamika kama Assassin, kundi hili unapotembelea
Mashariki ya kati basi utakutana na hadithi zao za kutosha tu.
Kundi hili la kigaidi la Assassins lilikuwa ni moja ya makundi mengi ya
waliokuwa wafuasi wa dini ya kiislam ambao walijitenga na mafunzo sahihi ya
dini hii na kuzitafsiri aya pamoja na mafunzo ya mtume Mohammad kutokana na
maono yao.
Kama tutakavyo kuja kuona, kundi hili la Assassins lilikuja kukutana
na kikundi maarufu cha Knights Templars ambao hawa Knight Tempars ndiyo walio
kuwa vinara wa vita vile vya msalaba. Kupitia kwa Assassins; Knight Templars wakajifunza uchawi na
ushirikina wa mashariki ya kati na wao wakaupeleka uchawi huo katika nchi za
Ulaya. Baadaye ushawishi huo utaingia mpaka kwenye Scottish Rite Freemasonry na
baadaye kwenye karne ya ishirini tutaona athari ya mahusiano haya baina ya Assassins
na Knight Templar ambayo yatapelekea kuunda kwa makundi mengine ya kigaidi na
Freemasonry wa Magharibi kupitia jina la Uislamu kwa malengo makubwa ya New
World Order
Ugaidi ambao hauna nafasi yoyote katika mafunzo ya Kiislam ulirudishwa mara
ya pili kwa freemason wa Egypt kutoka Ulaya ambapo mbinu hiyo ilipelekwa na
Knights Templar ambao nao walichukua kutoka kwa Assassins. Ismailia ndiyo
waliyo boresha mbinu hii ya ugaidi na baadaye itachukuliwa na Illuminanti ambao na wataitumia kwa karne zitakazo fuata.
Ismailia haikuwa imepotea sana kwenye
misingi ya Uislamu mpaka pale uongozi wa kundi hili ulipo chukuliwa na mtu
aliyeitwa Abdullah Ibn Maymun mnamo mwaka 872. Jamaa huyu alipouchukua utawala
wa kundi hili si kwamba Ismailiya walibadilika na kuwa ni adui wa Uislamu
lakini adui wa dini zote duniani. Ibn Maymun alikuwa ni Myahudi ambaye alifuata
imani za kipagani za Mesopotamia ya kale, imani ya kuabudu nyota, ushirikina,
uchawi na mazingaombwe ndizo alizo fuata Ibn Maymun. Lakini jamaa huyu alikuwa
pia na elimu ya dini zingine mbalimbali duniani ikiwemo Uislamu na Ukristo,
hivyo alikuwa vizuri, alikuwa yupo vyema na alijua anachofanya.
Mmoja wa walio kuwa wanafunzi wazuri sana
wa Ibn Maymun ni Hamdan Qarmat, ambaye alianzisha hekalu kama yale ya kimasoni,
hekalu hilo liliitwa Qaramitah ambapo katika zama hizo lilipata sifa pande za
Arabuni na warabu wengi walisimikwa katika asasi hiyo, mafunzo na maono yake
yalikuwa sawa na ya mwalimu wake mkuu. Kwa vile wengi wa wafuasi wake walikuwa
ni waumini wa dini ya Uislamu aliamua kuwafundisha namna ya kuachana na misingi
ya dini hiyo lakini wakati huohuo wakiendelea kujitambua kuwa wao ni Waislamu.
Aliwapa nadharia za upagani zilizo waruhusu kuachana na sala, ibada ya kufunga
pamoja na ibada zingine. Kutokana na aina hii ya mafundisho kundi hili likawa
ni kitisho dhidi ya waumini wa kweli wa Uislamu. Wale walio pinga mafunzo ya
kikundi hichi waliuwawa, kikundi hichi kilisimamia kile ambacho leo tunaita ni
ugaidi dhidi ya yeyote aliye onekana ni kitisho au kuwapinga. Kundi hili
lilifanikiwa kuishika Iraq, Yemen na Bahrain na baadaye walilikamata jiji
takatifu kwa dini ya Uislamu, jiji la Makka ambapo hapo waumini wa kweli
wapatao elfu thelathini waliuwawa na kundi la Qaramitah. (David Livingstone ‘TERRORISM
AND THE ILLUMINATI’ A Three Thousand Year History)
Ismailia nao wakagawanyika makundi mawili
juu nani ashike uongozi wa dini hiyo baada ya kufariki kiongozi wao
al-Mustansir mwaka 1094 AD. Kundi la Ismailia wa Egypti walimtambua mtoto wa
al-Mustansir bwana al Mustali kuwa ndiye anayefaa kushika hatamu, kundi jingine
la Ismailia kutoka Iran na Syria wao walimtaka mtoto mkubwa wa Al-Mustansir
bwana Nizari ndiye ashike hatamu. Waliomuunga mkono Nizari waliongozwa na Hasan
Sabbah.
.jpg)
Mahusiano haya baina ya Freemason wa Ulaya
na wale wa Mashariki ya Kati yalitengeneza njia ambayo Illuminanti wataitumia
kutengeneza kile kitakacho itwa ugaidi na baadaye vita vya tatu vya dunia
vitakavyo jengwa kwenye msingi huu wa vita dhidi ya ugaidi. Mpango huu mahiri
ulichorwa na vichwa vinne vya Illuminanti vya wakati huo, Alikuwepo Muzzin
mwenyewe kutoka Italia, Lord Henry Palmerston wa England, Otto von Bismarck wa
Ujerumani na Albert Pike mwenyewe, jamaa wote hawa walikuwa ni Freemason wa Scottish
Rite wa daraja la 33. Walikubaliana kutengeneza chombo kikuu cha Freemason
kitakacho kuwa na nguvu ya kuwaingilia, kuwahoji na hata kutengua maamuzi ya Freemason
wengine kokote walipo duniani, chombo hichi ndicho kitakacho kuwa kikitazama na
kuongoza mchezo mzima, walikiita chombo chao hichi Palladium Rite Freemason.
Hivyo basi Grand Lodges, Grand Orient. Memphis Rite, Mizraim Rite, Scottish
Rite na Egptian Freemason au Primitive Rite zote zililetwa chini ya Palladium
Rite. (Three World Wars”. “Who Was Albert
Pike?” <http://www.threeworldwars.com/albert-pike.htm>)
.jpg)
Wakati Freemason wa Egypt wakiwa ni msingi mzuri wa mahusiano baina yao na
wale wenzao wa Ulaya, mshikamano ambao kwa karne zitakazo fuata utatengeneza
vikundi na mitandao ya ugaidi kwa mbinu ileile iliyo tumiwa na Hasan Sabbah. Nadharia
na sababu ya kutumika kwa mbinu hiyo ya ugaidi inazaliwa katika nchi ya Saudi
Arabia kupitia kwa mtu aliye itwa Mohammed Abdul Wahhab na nadhari ya Wahhabism
iliyo tengenezwa na mtumishi wa Illuminati.
Kazi ya Abdul Wahhab dhidi ya umma
haikuwa na tofauti na zile kazi za Khawarij, na hata hivyo anafahamika pia kama
mtu aliyeifufua Khawarij tena.
Kabla Wahhabism haijafanya kazi nzuri
iliyokusudiwa ya kuliharibu kabisa jina la Uislamu na kutilia mashaka mafunzo
yake itakapofika karne ya ishirini na moja, kwanza ilitumiwa katika ile mbinu
maridadi ya Uingereza ya ‘divide and rule’, ambapo Waarabu waliuwana na ndugu
zao wa Uturuki,
Mwaka 1453 Waturuki waliikamata Constantinople na kuanzisha dola maarufu
kwenye historia ya Uislamu, dola ya Ottoman ambayo iliweza kupanuka na
kuzifikia mpaka nchi za Ulaya. Dola hii ya Ottoman ilishikilia maeneo mengi
ambayo pia dola ya Uingereza iliota ndoto za kuyashika maeneo hayo. Hivyo njia
iliyo kuwa bora kwa Uingereza kuweza kuizorotesha dola hii kamambe ya Ottoman
ilikuwa ni kutumia njia yao marufu ya ‘divide and rule’. Freemason na jasusi wa
Uingereza ndiye aliye pewa kazi hiyo ya kuwagawa na hatimaye kuwa pambanisha
ndugu wawili wa Uislamu, yaani Mwarabu wa Saudi na Mturuki.
Katika Uislamu ni haram na dhambi kuu, kupigana
na hatimaye kumuua ndugu yako wakiislamu. Kwa hivyo ilikuweza kumpambanisha
Mturuki na Mwarabu ambao wote ni ndugu katika Uislamu, aina mpya na tofauti ya kutafsiri
Quran na mafunzo ya mtume ilihitajika kufanikisha hilo, tafsiri ambayo itatoa
ruhusa kwa ndugu muislamu kumuua ndugu yake.
Historia ya Uislam inathibitisha kuwa
hakuna watu bora zaidi wa kufanya fitna hii zaidi ya Khawarij. Hivyo kwa
mtazamo wa Uingereza hilo lingewezekana kutokea tena endapo tu atapatikana mtu
muhimu wa kuanzisha moto huo, na safari hii mtu huyo hakuwa mwingine bali ni
Mohammed Abdul Wahhab na mbinu au tafsiri aliyoitumia kufanikisha hilo ilikuja
kufahamika kama Wahhabisim.
Kama walivyo kuwa Assassin na wengine mfano wa hao, Abdul Wahhab naye
alitangaza kuwa yeyote asiye mfuata katika imani yake hiyo mpya ni kafiri na
yeye Abdul Wahhab ana haki ya kumuua mtu huyo, kuteka mali zake, kumvunjia
heshima yake na kumuuza kwenye soko la watumwa.
Alitumia nafasi ya hali duni waliyo kuwa nayo Waislam wa hapo kutokana na
uongozi wa dola ya Ottoman na hivyo kuwataka waumini wasimtii Sultani wa Istanbul.
Abdul Wahhab akasema kuzitukuza sehemu takatifu ni ushetani, akamtukana mtume
na wafuasi wake waliomfuata kwa haki, wakiwemo viongozi wa kiroho na wasomi wa Kiislam.
Akachochea vurugu baina ya miji na nchi za Kiislam na hasa dhidi ya dola ya
Ottoman. Kokote kuliko kuwa na mwanya au jambo lenye shaka Abdul Wahhab
alilitumia hilo kuwa pambanisha ndugu wawili wa Kiislam. Mwisho alitangaza
jihadi dhidi ya Waislam wote. (Shaykh
Juri, Muhammad bin Abdul Wahab)
Uingereza waliweza kumshawishi Mohammad ibn Saud, kiongozi wa Dariyah
kumuunga mkono Ibn Abdul Wahhab. Inasemekana pia pande hizi mbili ya Saud na
Wahhab walikubaliana kuwa kuanzia hapo madaraka yatagawanya baina ya familia
hizo mbili tu. Wakati Saud wao watashikiliwa utawala kwenye mambo ya siasa,
Wahhab wao watabakia na nguvu kwenye masuala ya kidini. (Madawi al-Rasheed, A History of
Saudi Arabia: )
TAHADHARI NA MCHUNGAJI HUYU ...
Wahhabi wakishirikiana na Saud wakatangaza kuwa utawala wa Ottoman ni wa
kinafki, wakatangaza jihad kwa yoyote asiye kubaliana na madai yao kuwa utawala
huo haufai. Katika mafunzo ya Uislamu ni kosa zito kumuita muislamu mwenzako
mnafiki, na ili kuthibitisha uzito wa kosa hilo, mafundisho ya Uislamu
yanasema, muislamu anapo mtuhumu mwenzake kwa unafiki, basi kwa uhakika anaye
tuhumiwa au anayetuhumu mmoja wao ni mnafiki. Lakini uzito wa kosa hilo
haukumzuia Abdul Wahhabi kuwaita wale wasiomuunga mkono kuwa ni makafiri. (The Wahhabi Threat)
Mwaka 1746 kabla hata Abdul Wahhab
hajaonganisha nguvu zake na zile za Ibn Saud, yeye Abdul Wahhab alituma wanaume
thelathini kwenda kuomba ruhusa ya kufanya ibada ya Hajj. Uongozi wa Makkah
uliwakubalia kwani waliona huo utakuwa ni wakati muafaka kwa wanazuoni wa kweli
wa Kiislam kutoka Makkah na Medina kufanya mjadala wa wazi na Abdul Wahhab
mbele ya hadhara kubwa na hapo watu wote watakao hudhuria na wasio hudhuria
watafahamu ukweli ni upi baina ya madai ya Abdul Wahhab na mafunzo ya kweli ya
dini anayo dai kuitetea. Abdul Wahhab alishindwa vibaya katika mjadala huu na
alishindwa kabisa kutetea hoja zake. (Algar,
Hamid. Wahhabism: A Critical Essay, uk. 23.)
VIJANA WETU WANAKUJA WAKIWA WAZURI KABISA, LAKINI WANAPO PITA CHINI YA MTU HUYU WANATOKA WAKIWA NA MABOMU NA SHIDA ZINGINE
Tukio hili lilizidisha chuki za Wahhab dhidi ya uma wa Kiislam. Ibn Saud
alipofariki mtoto wake Abdul Aziz akawa mtawala wa Dariyah. Kipindi cha miaka
ishirini iliyofuata Wahhabi walizidi kutanuka, kila sehemu Mwingereza
alipoingia nao walikuwa nyuma. Mara kadhaa Mwingereza alijaribu kuichukua
Kuwait lakini kila wakati alizidiwa nguvu na dola ya Ottoman. Mwaka 1775 wakati
Uingereza ikiuguza majeraha iliyo yapata toka kwa Ottoman, mshirika wake Abdul
Wahhab alijitangaza kuwa ni kiongozi wa waislam wote duniani, na wakati huohuo
akiwa ametangaza vita ya Jihad dhidi ya utawala wa Ottoman. Mwaka 1788
Uingereza ukamsaidia Abdul Aziz ibn Saud kuichukua Kuwait.
Mwaka 1792 Abdul Wahhab alifariki na Abdul Aziz akawa kiongozi wa
Wahhabisim ambapo kwa miaka mitatu iliyo fuata aliweza kupenyeza vuguvugu la
Wahhabisim kwenye mji wa pili kwa utukufu katika dini ya Uislamu, mji wa Medina
kisha Syria na mwaka 1801 Iraq.

Saud ibn Abdul Aziz ibn Saud akawa kiongozi
wa Wahhabi baada ya baba yake. Baada ya kuuvuruga vibaya mji mtakatifu wa dini
ya Shiah, Wahhabi wakahamia katika mji wa kwanza kwa utakatifu kwa dini ya Kiislam,
mji wa Makkah. Utawala wa Ottoman wa kwenye mji wa Makkah haukuweza kupambana
na jeshi la Wahhabi bali walikimbilia kwenye ngome yao iliyoko Taif. Hata hivyo
jeshi hilo la Wahhabi lilifanikiwa kuichukua ngome ya Taif. Kisha kama walivyo
fanya uharibifu katika mji wa Karbala ndivyo walivyo uvuruga mji huo mtakatifu
wa Makkah. Kutoka kwenye makaburi ya waumini mpaka kwenye madrassah na
misikiti. Vitabu mbali mbali vya dini waliviharibu na inasemekana walitengeneza
malapa kwa kutumia vitabu hivyo. ( Part
Two: The Beginning and Spreading of Wahhabism, by Ayyub Sabri Pasha [1888
-1893])
Wahhabi wakiwa wameishikilia miji hiyo miwili mitakatifu ya Makkah na
Medina chini ya kiongozi wao Saud ibn Abdul Aziz bin Saud wakapitisha sheria
zao mpya za Uislamu. Ikiwemo kuzuia Waislamu kufanya ibada ya Hijja, walidai
zama hizo hakukuwa na Waislam wasafi wa kuweza kufanya ibada hiyo, wakaifinika
Al-Kabbah na kitambaa chakavu na cheusi na wakipanga namna ya kuivunja nyumba
hiyo tukufu.
Mkono wa Freemason wa Uingereza ulikuwa nyuma ya haya yote na
Wahhabisim nyuma ya viongozi wao walikuwa wakitekeleza maelekezo toka kwenye
nyumba za ibada za kimasoni. Wakati dola ya Uingereza ikipanuka na kuchukua
aridhi za Waislam Wahhabisim wao walikuwa bize
wakifanya Jihad dhidi ya uma wa Kiislam.(Ibid)
NI KAMA VIJANA WETU WANATOLEWA BONGO ZAO NA NAFASI YAKE INAWEKWA BOMUU!!!! HATARI SANA!
ITAENDELEA INSHAALAH ...
Inalillah wainailah rajiun sasa n vipi tutazitambua jihad ya kwel na kwa namna hii xaxa uiclam utaitawalaje dunia kama umeshaharibiwa ivi inaskitisha sana
ReplyDeleteMafunzo ya Uislam yapo wazi kabisa kwenye hili. Kwanza ni kuitafuta elimu sahihi ya kiislam, kisha ifundishe elimu hiyo kwa familia yako na jamaa zako wa karibu, na fanya juhudi kwa namna nzuri utakayo weza ya kuuelimisha umma dhidi ya njama hizo mbovu. Uma ukifahamu kipi ni kipi basi hiyo yenyewe itakuwa ni moja ya jihadi kubwa umeifanya.
ReplyDeleteWewe shia eeh! hapana shaka shia ni wapinga jihad hakuna muumin walweli asie wafahamuni! ni nyinyi mnaotoa fatwa za uongo kupinga jihad! mkasmea kunjiahd nnafsi ambayo ni kubwa kuliko jihad ya silaha! hadithi ambayo si sahihi! muhaddithiina wote wamekosa kuipatia dalili kua ni hadithi sahihi! Shia c waislamu ninyi japokua mnakuja kwa sura za kiislamu! hilo ulifaham so hakuna unchoelezea za maana zaidi ya upotoshaji dhidi ya umma wa kiislam! Allah ndiye mjuzi zaidi!
DeleteKuwa huru wakati unasoma posti hizi, achia akili yako ichanganue yenyewe. Usiwe na msimamo ambao hautaki utizamwe na kuoneshwa kasoro zako, msimamo wa namna hii haumsogezi mtu popote katika kutafuta elimu na uelewa zaidi ya kupingana kugombana na kuwapachika watu majina na sifa zisizo zao. Kaachini, kuwa mpole pima kwa akili yako mwenyewe, usipime kwa akili au mtazamo wa fulani, halafu mwisho njoo na utafiti wako binafsi juu ya kile unacho kisema, usikimbile kupinga tu.
Deleteasalaam alaikum, Salim, naomba nisaidie juu ya hili, UKIWAANGALIA ALSHABAAB, NI WASOMALI NA WAPO NDANI YA ARDHI YAO, NA WANANYANYASIKA NA WAGENI, NA UKIZINGATIA WANAJITAWALA ASILIMIA KUBWA KWA SHARIA YA KIISLAM, ASILIMIA TISINI NI WAISLAM, SERIKALI YAO NI CORRUPTED, ....JE KAMA ALSHABAAB HAWAPIGANI JIHAD, ....IPI ITAKUWA NI JIHAD YA KWELI? NA JE, DHULMA IWE YA KIWANGO KIPI NDIPO WAISLAM WANARUHUSIWA KUPIGANA JIHAD?,.....NA JE, JIHAD YA UPANGA KATIKA QURAN INAMAANISHA NINI?......
ReplyDeleteNdugu nashukuru kwa maswali yako.
DeleteKitu cha kwanza waislam tumehusiwa kufuata vitu viwili, Quran na Sunnah.
Kwa kutumia viwili hivyo ndipo Mbora na mtukufu wa daraja (SAW) alifanikiwa kusimamisha Dola ya Kiislam. Sasa rudi kwenye sira na utizame sera ya bwana mkubwa huyo (SAW) na tizama falsafa ya mwenendo wake kutoka Makkah mpaka Madinah na hatimaye dola ya Kiislam ikasimama. Halafu rudi na utizame wanacho fanya hawa wanajihad wa CNN na FOX News na upime kwa akili yako mwenye halafu uniambie hiyo ndiyo JIHAD????
Na uislam haukuenezwa kwa UPANGA, hizo ni misconception na propaganda zilizofanywa kazi kwa muda mrefu hata kabla ya first Crussade, na imeendelea hivyo na kuingizwa kwenye mafunzo mbalimbali na watu wameaminishwa hivyo, na sasa wanapotengenezwa watu wanao taka kusimamisha dola ya ‘kiislam’ kwa njia ya upanga vitendo vyao vinathibitisha na kutilia nguvu uongo na urongo na uzandiki waliopandikizwa watu kwa muda mrefu na hivyo kuichora picha mbaya ya dini yetu kwamba ilienezwa kwa upanga.
Ukikwama rudi hapa tujadiliane.
In short JIHAD maana yake ni "STRIVING AGAINST EVILS" .........JE IWAPO MUISLAM NDIYE ANATENDA MACHAFU, NA WEWE NI MUISLAM, MAANA YAKE USIMKANYE??
ReplyDeleteUnapaswa kumkanya.
DeleteSwali linakuja,
Unamkanya vipi?
Kuna mengi ya kutizama katika hili na kuna njia nyingi za kupita katika hili, lakini kumkata ndugu yako shingo kwa sababu anafanya ‘machafu’ hilo litakuwa na mashaka yake makubwa. Labda ungefafanua ni aina gani ya ‘MACHAFU’ unayo yakusudia. Lakini kwa maarifa madogo niliyo nayo ni kuwa kwanza tizama aina ya kosa, pili kosa limefanywa na nani, na tatu kosa limefanywa katika mazingira gani, yote hayo matatu yatakusaidia katika aina ya njia inayofaa kuondoa uovu huo