Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Showing posts with label blue degree. Show all posts
Showing posts with label blue degree. Show all posts

Sunday, November 27, 2016

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? S02, Ep1 (Ujio wa Wageni kutoka Sayari ya Mbali)

Bandiko la Queen Replaced, bado linaendelea, nadhani linaweza kuwa moja ya bandiko refu kupata kubandiko kwenye blogi hii. Muandishi anaendelea kukusanya ushahidi na taarifa zingine kuhusiana na kitimbi hichi cha Queen Replaced, na kadiri taarifa zenye mashiko zitakapo patikana basi nitaendelea kuririka hapa kwenye bandiko hilo, nadhani litaendelea na episode moja baada ya nyingine mpaka Mfalme Trump atakapo ondoka au kuthibitisha vinginevyo.

Leo nazungumzia kitu nilicho pata kukigusia hapoa nyuma kidogo kwenye bandiko hili ‘Je Tupo Wenyewe Kwenye Ulimwengu?’ unaweza kulipitia hapa http://salimmsangi.blogspot.com/2015/04/je-tupo-wenyewe-kwenye-ulimwengu.html
Leo nataka tuizungumzie mada hiyo kwa kina zaidi ...




“Historia ni mtazamo wa zama zilizopita ambapo watu wamekubaliana juu ya mtizamo huo”- Nepoleon Bonaparte

“Wanao tawala wakati wetu ulio kuwepo ndiyo wanao tawala wakati wetu uliopita, (na wanao tawala historia yetu, ndiyo wanao tawala hatma yetu) ” - George Orwell

Monday, December 2, 2013

NAMBARI TISA (9) NA KUMI NA MOJA (11) KWENYE DUNIA YA KIMASONIA

LEOTUTAZUNGUMZIA ALAMA NEMBO ZA KIMASONIA, NA LEO TUTATIZAMA KWA UNDANI NAMBARI TISA (9), KISHA KUMI NA MOJA (11), HALAFU MWENGE …

Kwa freemasonry lugha yao ipo mahususi kwenye maumbo na alama mbalimbali lakini pia bila kusahau nambari, umuhimu wa nambari kwa freemasonry na asasi nyingine za siri unakuja pale ambapo elimu ya kale kabisa ilihifadhiwa katika nambari na kwa watu hawa hisabati limekuwa ni somo muhimu mno,

“Elimu ya kwanza duniani imekuja Kwa alama mbalimbali, hekima za watu wa Chaldean, Phoenician, Egypty, Kaanani, wanafalsafa kama akina Zoroaster, Sanchoniathon, Pherecydes, Syrus, Pythagoras, Socrates na Plato, vyote vya zamani vilivyokuja katika mikono yetu, vimekuja kwa njia ya alama”