Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Showing posts with label freemaosn. Show all posts
Showing posts with label freemaosn. Show all posts

Sunday, November 27, 2016

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? S02, Ep1 (Ujio wa Wageni kutoka Sayari ya Mbali)

Bandiko la Queen Replaced, bado linaendelea, nadhani linaweza kuwa moja ya bandiko refu kupata kubandiko kwenye blogi hii. Muandishi anaendelea kukusanya ushahidi na taarifa zingine kuhusiana na kitimbi hichi cha Queen Replaced, na kadiri taarifa zenye mashiko zitakapo patikana basi nitaendelea kuririka hapa kwenye bandiko hilo, nadhani litaendelea na episode moja baada ya nyingine mpaka Mfalme Trump atakapo ondoka au kuthibitisha vinginevyo.

Leo nazungumzia kitu nilicho pata kukigusia hapoa nyuma kidogo kwenye bandiko hili ‘Je Tupo Wenyewe Kwenye Ulimwengu?’ unaweza kulipitia hapa http://salimmsangi.blogspot.com/2015/04/je-tupo-wenyewe-kwenye-ulimwengu.html
Leo nataka tuizungumzie mada hiyo kwa kina zaidi ...




“Historia ni mtazamo wa zama zilizopita ambapo watu wamekubaliana juu ya mtizamo huo”- Nepoleon Bonaparte

“Wanao tawala wakati wetu ulio kuwepo ndiyo wanao tawala wakati wetu uliopita, (na wanao tawala historia yetu, ndiyo wanao tawala hatma yetu) ” - George Orwell

Friday, August 5, 2016

MFALME OBAMA: Ep 2


Mungu anapo wateuwa mitume wanakuwa wanatoka katika mkondo wa damu maalum, anakuwa chini ya uangalizi wa Muumba wake kuanzia maisha ya wazee wake, maisha yake akiwa tomboni, utoto wake, ujana wake mpaka anapo kabiziwa jukumu hilo zito na tukufu kwa ajili ya kuwaongoza watu wake. 

Monday, March 7, 2016

NAMTAFUTA MUNGU

“Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima.”

“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakuhitilafiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.” (Quran 3:18-19)

Leo nataka tuzungumzie mada moja tata kidogo, pana lakini iliyofanywa ndogo na akili zetu ... nataka tumtafute Mungu



     Je ni kweli kuna ‘Mungu’ yaani yule mbaye aliyeumba vyote tuvionavyo na tusivyo viona, tunavyo fahamu na tusivyo fahamu. Au ni ‘ulevi’ wa imani za kidini unao tufanye tuamini kuwa Mungu yupo.

Sunday, June 15, 2014

USICHO KIFAHAMU KUHUSIANA NA VITA DHIDI YA UGAIDI Pt 1


Ningependa kuianza makala hii kwa hadithi mbili,

Hadithi ya kwanza

Hudhaifa (ra) anasema kwamba, amesema mtume (saw): “Kwa hakika, nahofia kati yenu yule mtu ambaye ataisoma Quran kiasi kwamba nuru ya Quran itaonekana kwenye uso wake ... halafu neema hii itaondolewa pale atakapoidharau na kuipa mgongo na atabeba upanga wake kumshambulia jirani yake na kumtuhumu kuwa ni mshirikina.” Mtume (saw) akauliza ni nani kati ya wawili hao atakuwa anazistahiki hizo tuhuma? -  Mwenye kutuhumu au mtuhumiwa? Mtume (saw) akajibu ni, “mwenye kutuhumu.”

Hadithi ya pili.

Imam Bukhari (Allah amrehemu) ameeleza, “Umar ibn al-Khattab (ra), ambaye alikuwa akizungumza na masahaba, aliwauliza, ‘Ni nani kati yenu mwenye elimu zaidi kuhusiana na fitnah?’ Hudhaifah (ra) akajitokeza na kusema, ‘Mimi ewe Ameer ul-Muumini! Kisha akaanza kuzitaja baadhi ya fitnah Umar ibn al-Khattab (ra) akasema, ‘Siyo fitnah hizo ningependa kufahamu kuhusiana na fitnah ambazo wimbi lake litakuwa kama wimbi la bahari.’ Hudhaifa (ra) akauliza ‘Kwanini unataka kujua kuhusina na hizo fitnah ewe Ameer ul-Muuminin? Kati yako na hizo fitnah kuna mlango ulio fungwa.’ Umar (ra) akauliza ‘Je mlango huo utavunjwa au utafunguliwa?’ Hudhaifah (ra) akajibu, ‘Utavunjika’ Umar (ra) akajibu, ‘Basi hautafunga mpaka siku ya kiyamah..’

KUNA AMBAYE YUPO BIZE SANA KUFITINISHA IMANI HIZI MBILI.

Wednesday, July 3, 2013

MAANA HALISI YA 666

Wapendwa!
Tarehe ambayo 666 Ilikuwa ubaoni ....

Sehemu hii ndogo kuhusiana na nambari 666 nimeitoa kwenye, sura moja ndani ya kitabu kinacho kwenda kwa jina la “FREEMASON; Dunia usiyo ifahamu”, 

kitabu hichi ni nimeandika mwenyewe, na soon Maulana akipenda mtakiona mtaani, hivyo sehemu hii kuitoa kwenye kitabu na kuwamegea ni zawadi kwenu wasomaji wangu, please ipokeeni ....

.... Kwa watafiti huru wa mambo ya UFO na New World Order ni kuwa serikali na ‘sayansi’ wanapigia debe taarifa hizo kwa lengo lilelile la New World Order ambayo kiongozi wake atakuwa na ‘damu takatifu’ na mwenye nguvu za maajabu.

Mmoja anaye tegemewa ni wazo ambalo liko kwenye imani ya dini mbalimbali duniani, ikiwemo kwenye Uyahudi, Uislamu na Ukristo na bila kusahau kwenye imani na dini za kishetani ukiwemo Freemasons.