“Wale ambao hawawezi kukumbuka historia, ndiyo ambao kimakosa wanarudia
makosa ya kihistoria” - George Santayana
Rais wa 40 wa taifa la Marekani,
mwenye daraja la 33 kwenye asasi ya Freemasons na pia mwanachama wa asasi
nyingine ya siri inayokwenda kwa jina la Knights of Malta na mwenye damu ya
kifalme ya kishetani, Ronald Reagan mara kwa mara amekuwa akizungumzia ni namna
gani dunia nzima itaweza kuungana endapo patakuwepo na kitisho cha uvamizi wa
viumbe kutoka sayari nyingine.
Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1987, Septemba 21 alisema;
“Katika hali yetu kubwa ya chuki na utengano tuliyo nayo hivi sasa, mara
kwa mara tunasahau ni kiasi gani binaadam tumeungana. Huenda tunahitaji kitu
kutoka nje, kitisho cha ulimwengu kitakacho tufanya sisi kuweza kutambua umoja
huu tulio nao. Nimekuwa nikifikiria ni namna gani tofauti zetu zitatoweka pale
ambapo tutakuwa tunapambana na kitisho cha viumbe kutoka nje ya sayari yetu”.( http://www.bibliotecapleyades.net/exopolitica/exopolitics_reagan03.htm)
Mwaka 1988 Mei 5, White House, kwenye chumba kilicho jaa waandishi wa
habari, Reagan alisema,
“Nimekuwa nikijiuliza mwenyewe kwamba itakuwaje
kama sisi sote hapa duniani tukagundua ya kuwa kuna kitisho dhidi yetu kutoka
nje ya dunia yetu … nguvu ya kutoka kwenye sayari nyingine. Je si mara moja tu
tutaweza kutambua kuwa hatuna tofauti yoyote baina yetu, kwamba wote tu
binadamu, wananchi wa dunia na je, hatutaungana kupambana na kitisho hicho?”( http://www.bibliotecapleyades.net/exopolitica/exopolitics_reagan03.htm)
Wazo hili la kuwa kuna au kutakuwa na kitisho kutoka nje ya dunia yetu, nje
ya mfumo wetu wa jua, yaani nje ya galaxy ya Milk Way, raisi huyu amekuwa
akilitaja mara kwa mara wakati na baada ya uongozi wake.
Henry Kissinger Kwenye mkutano wa Bilderberger, Evians, Ufaransa mwaka 1992
alisema,
Katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani vyombo kadhaa vya habari
na mitandao ya kijamii vimekuwa vikiripoti kuwa wananchi wa Marekani
wangelipendelea kumpa Obama ushindi kwenye uchaguzi huo kama shujaa ambaye
mwenye uwezo wa kuliokoa taifa hilo kwenye shambulizi la viumbe wasio julikana
kutoka kwenye sayari nyingine. Asilimia 72 ya wananchi wataifa hilo wanaamini
juu ya kuwepo kwa viumbe hao na uwezekano wa kutokea kitisho hicho.
Kwenye miaka ya karibuni neno ‘UFO’ (Unidentified flying object) limechukua
kasi kwenye vyombo vya habari, hasa nchi za Magharibi, Asia, na Marekani.
Vyombo hivi mwonekano wake ni duara lakini pia vinaweza kuwa na umbo jingine
tofauti na hilo kama tutakavyo ona. Taarifa zisizo rasmi kutoka kwenye vyombo
mbalimbali vya habari na maelezo ya watafiti mbalimbali kwenye suala hili ni
kuwa UFO hutumika kama chombo cha anga cha kusafiria kwa viumbe hao wasio
julikana kutoka sayari ya mbali. Lakini tabia yake ni tofauti sana na vyombo
vyetu vya anga.
UFO haionekani kuathiriwa na nguvu za mvutano, inakwenda kwa
mwendo kasi mkubwa sana ambao hakuna vyombo vyetu vya kusafiria vilivyo pata
kurikodiwa kuwa na mwendo kasi huo, huweza kubadili mwelekeo wake katika nukta
yoyote ya safari yake, na inaweza kutoweka machoni pa mtazamaji ndani ya
sekunde na asijue ameona nini.
Baadhi ya vyombo vikubwa vya habari, wanasiasa, wasomi, wanafunzi na
viongozi wanauchukulia huu mtazamo mpya wa nafasi yetu na sayari yetu kwenye
ulimwengu utatuletea amani ya kidunia ambayo haijapata kuwepo, umoja na udugu
na maendeleo makubwa. Lakini kwa upande mwingine hasa watafiti huru na wasomi
kadhalika wanaamini kuwa huu mtazamo mpya utatupeleka kwenye wakati mgumu na
changamoto nzito tulizo pata kukutana nazo kwenye sayari yetu hii.
UFO kweli zipo au ni aina fulani ya udanganyifu?
Asilimia 72 ya wananchi wa Marekani wanaamini juu ya kuwepo kwa uhai nje ya
sayari yetu na kwamba kuna viumbe wengine wanaishi huko. Asilimia 48 wanaamini
juu ya kuwepo kwa UFO na asilimia 15 wanaamini kuwa wameona UFO. Asilimia 2-3
wanaamini kuwa wamewahi kutekwa na viumbe hao na kuingizwa kwenye UFO na baadaye
kurejesha walipo kuwa.
Kuhusiana na UFO kumekuwepo na taarifa nyingi mno, kutoka kwenye magazeti
mpaka majarida. Vijitabu na mavitabu. Kutoka kwenye taarifa za watu waliona
UFO, walio waona viumbe hao, mpaka wale walio kamata na kupakiwa kwenye UFO.
Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kuzithibitisha taarifa hizo, wakati mwingine
taarifa zinakuzwa kubwa kushinda tukio lenyewe, wakati mwingine kwa makusudi
zinakuwa ni taarifa za kutengeneza au zenye upotoshaji. Lakini bado kuna wakati
tukio moja linakuwa na mashahidi zaidi ya mmoja, linakuwa limeacha ushahidi
wenye kuonekana, ushahidi unao weza kuugusa kwa mkono, ushahidi ambao ni zaidi
ya maneno ya shuhuda.
UFO kwa wanahistoria zimerekodiwa kwenye majalada ya historia tangu enzi na
enzi ya historia ya mwanadamu. Ingawa haipo kwenye mitaala ya somo la historia
yenyewe, na hivyo ni kama hakuna kitu kama hicho.
Kuanzia mwaka 1991 mpaka 1993 jiji la Mexico lilifunikwa na taarifa za
kuonekana kwa UFO. Julai 11, 1991. Watu 17 ambao hawana mahusiano yoyote katika
maeneo tofauti ya jiji hilo wakiwa na kamera zao, waliweza kunasa picha ya
diski kubwa la chuma karibu kabisa na usawa wa jua mbalo muda mfupi nyuma
lilikuwa limepatwa na mwezi. Diski hilo lilikuwa limening’inia angani kwa muda
bila kusogea upande wowote ule. Lakini watu hawa hawakujua kama wamepiga picha
UFO mpaka watu wengine walipo ng’amua wakati wanaoneshwa video hizo.
Kutoka hapo watafiti wakaanza kupokea video na picha nyingi zinazo onesha
umbo la duara kubwa la chuma, UFO zikiwa kwenye anga la Mexico ambazo picha
zake zilipigwa na watu binafsi. Vyombo vya rada na hata marubani kadhaa
wameripoti kuviona vyombo hivyo vikivinjari katika anga la Mexico. Kutoka
kwenye uwanja wa Benito Juárez International Airport Machi 4-5, 1992
iliripotiwa marubani wawili na kuthibitishwa na rada ya uwanja huo juu ya
kuionekana kwa UFO. Mmoja wa rubani
aliyehojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema;
Tukiwa bado tupo hapo Mexico, ripoti nyingine inasema,
Jeshi la anga la Mexico limetoa kaseti ya video ambayo wataalam wa UFO
wamedai ni UFO kumi na moja zilizo naswa na kamera zilipokuwa zikiizonga zonga
ndege ya jeshi hilo iliyo kuwa ikifanya doria. Jaime Maussan ambaye anaamini
juu ya kuwepo kwa vyombo vinavyo ruka vya viumbe wengine kwenye sayari yetu
alisema alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, vitu hivyo ni vya
kweli na vinaonekana kusimamiwa na viumbe huru kutokana na tabia viliyo onesha.
Vyombo hivyo vilikuwa vikifukuzwa na ndege ya doria baada ya kudhaniwa ni ndege
za wabeba dawa za kulevyea, lakini ghafla zilitoweka na zilipo onekana tena
zilikuwa zimeizunguka ndege ya doria ya jeshi la anga la Mexico.
Mexico imekuwa na historia ndefu ya kuonekana kwa UFO, nyingi kati ya hizo
zimekuwa zikidharauliwa na wana sayansi kama ni vipande vya uchafu ama vumbi
kutoka kwenye anga, roketi za kivita, Maputo ya hali ya hewa au uzushi.
Januari 2, 1993, kila gazeti kubwa ndani ya Mexico na taarifa za vyombo
vingine vya habari viligubikwa na habari moja tu ya chombo kisicho fahamika na
chenye tabia zisizo lingana na chombo chochote kinacho julikana na wakazi wa
sayari hii. Chombo hicho kilibaki kwenye anga la Mexico kwa masaa matano.
Gazeti moja kubwa la Mexico linalo kwenda kwa jina la, La Prensa lilikuwa na
kichwa cha habari kilichosema, ‘Maajabu!
UFO kwenye anga la Mji Mkuu’. Tukio hilo pia lilirekodiwa na rada kutoka
kwenye uwanja wa kimataifa wa jiji la Mexico.( Gary Bates: UFOs and the Evolution Connection Uk 179)
Brit Elders mtafiti kwenye masuala ya UFO, alipokuwa akizungumzia tukio la
UFO kunasa kwenye rada kwenye jiji la Mexico alisema,
“… rada ya Mexico imefuatilia na kurekodi UFO
sawa na yale yanayo semwa na watu waliyo ona kwa macho yao wenyewe kutoka
aridhini na kutoka kwa marubani wa ndege wakiwa angani.”( Chuck Missler na Mark Eastman ‘ALIEN ENCOUNTERS’)
Serikali ya Mexico ilipo shinikizwa na wadau mbalimbali juu ya kulifanyia
uchunguzi suala hili la UFO ilifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo
serikali ilitambua juu ya kuonekana kwa vyombo hivyo lakini ikasema – UFO
hazina madhara yoyote kwa wananchi.
Tukitoka Mexico tunaelekea kwenye nchi inayo kaliwa kimabavu na utawala wa
Kizayuni, Palestina. Septemba 17, 1996 kituo cha Polisi cha Tel Aviv kilipokea
dazeni za simu toka kwa wakazi ambao wameona kitu chenye mwanga mkali kikifanya
sarakasi kwenye anga lao kwa namna ambayo hakuna ndege wala helikopta ambayo
ingeweza kufanya kitu kama hicho.
Mwaka 1997 kwenye mahojiano na jarida la British Journal UFO Reality, Rnen
alisema yafuatayo kuhusiana na kile kinacho tokea kwenye aridhi hii inayo
kaliwa kimabavu na Wazayuni,
“Vyote kwa pamoja UFO zimeanza kuonekana kwenye maeneo ya Israel, na pia
Iran na Australia kwa wakati mmoja. Agosti mwaka 1996 wimbi la mashahidi walio
ona kwa macho UFO, na haikuwa watu wa kawaida peke yao, hata maofisa wa polisi
na jeshi. Taarifa zilizo pokelewa ni nyingi na zilikuwa zikiongezeka siku hadi
siku na hata kuwa ni vigumu kuweka taarifa ya mtu mmojammoja.”(
Chuck Missler na Mark Eastman ‘ALIEN ENCOUNTERS’ uk 14-17)
Tukio hilo lilishuhudiwa na maelfu ya watu ambao waliona UFO ikisafiri
taratibu mita 200 kutoka aridhini. Vituo vya polisi na vituo vingine vya
dharura vilipokea simu za kutosha kutoka kwa watu ambao walitaka kujua kulikoni
na wengine wakishuhudia kuyaona hayo. Ilikuwa ni usiku wa manane, saa nane na
nusu usiku, watu walisimama na kutizama UFO kama kitu kubwa mno lilio na taa na
muangaza wa kutosha kumulika anga la vitongoji viwili kwa mpigo. Tukio hili
lilishuhudiwa kwa takribani dakika kumi, halafu ghafla, bila tahadhari yoyote
chombo hicho kikatoweka kwenye macho ya watazamaji wake.( Chuck Missler na Mark Eastman ‘ALIEN ENCOUNTERS’ uk 14-17)
Machi 13, 1997 jimbo la Arizona kwa dakika 106 midaa ya saa mbili na robo
usiku lilishuhudia kile ambacho baadaye kilijulikana kama ni UFO. Baada ya
tukio hilo simu zilimiminika kwenye vituo vya dharura vya jimbo hilo kutoka kwa
mashuhuda wa maeneo kadhaa ikiwemo
Prescott, Wickenburg, Glendale, Phoenix, Scottsdale na Tempe.
Kutoka kwa
mashuhuda ni kuwa chombo hicho kilikuwa karibu kabisa na kituo cha Luke Air
Force, ndege aina ya F-16 tatu zilitoka kwenda kukifuatilia chombo hicho kujua
kulikoni. Hata hivyo ndege hizo za kijeshi zilipo karibia chombo hicho
kilitoweka ghafla kama kupepesa mboni ya jicho. Hata hivyo maafisa wa kituo
hicho cha Luke kama ilivyo tegemewa walikataa kuwa hakuna ndege za kijeshi
zilizo tolewa kwenda kukifuatilia chombo hicho na wala hawafanyi tafiti juu ya
UFO.
Peter Davenport kutoka kwenye kituo cha taifa cha kutoa taarifa za UFO
kilichopo Seattle, Washington alipokea mamia ya simu kuhusiana na tukio hilo na
maoni yake binafsi ni kuwa,
‘Tukio la Arizona lilikuwa wazi kabisa kati ya
matukio niliyo pata kuyaona … tulicho kiona pale ni kitu cha kweli kabisa.
Tayari wako hapa (viumbe kutoka sayari nyingine)’(Chuck Missler na Mark
Eastman ‘ALIEN ENCOUNTERS’ uk 14-17)
Miezi mitatu baada ya tukio, Juni 18, 1997 tukio hilo lilianza kuzungumziwa
kwenye vyombo vikubwa vya habari duniani na kuanza kupata mvuto na kuvuta hisia
za watu. Liliripotiwa kwenye NBC, MSNB,CNN na ABC.
Mike Fortsen, ambaye alishuhudia tukio hilo kwa jicho lake mwenyewe
alipokuwa anahojiwa na CBS kuhusiana na tukio lenyewe la Arizona alisema hivi,
‘Ninayo uhakika kabisa na kushawishika kuwa
kile kilikuwa ni chombo cha viumbe kutoka kwenye ulimwengu mwingine. Ni na
hakika kabisa viumbe hawa si kwamba wametoka kwenye sayari nyingine, bali
kutoka kwenye uwanda mwingine.( Chuck Missler na Mark Eastman ‘ALIEN ENCOUNTERS’ uk 14-17)
Kitu kidogo nikiweke sawa hapa kabla ya kuendelea mbele, ingawa na amini
kitu hicho nitakizungumzia kwa mapana zaidi mbele, lakini ili nisikuache sana
ngoja nikigusie kidogo. Fortsen amesema ‘kutoka kwenye uwanda mwingine’. Neno ‘uwanda’ ni neno ambalo utalikuta sana kwenye aina
hii ya habari. Dunia tunayo ishi sasa ni maarufu kama ‘pande tatu’ au ‘miwanda
mitatu’ miwanda ni wingi wa uwanda. Wanaita ‘Three Dimensional’ au 3D. Yaani kimo,
urefu na upana. Hivyo kutoka uwanda mwingine ni kutoka nje ya mfumo wetu wa
jua wa Milk Way, kwamba ni kutoka kwenye galaxy nyingine isiyokuwa na 3D!
Tukio hili la Arizona liliripotiwa pia na USA Today kwenye kurasa nzima
iliyojaa mnamo Juni 18, 1997. Kwenye
makala hiyo mwandishi na mtafiti Richard Price ameliita tukio hilo,
“Tukio la ajabu na kushangaza la UFO tangu miaka 50 iliyopita.”(
USA Today Juni 18, 1997)
Kitu kimetokea kwenye anga la Arizona usiku wa Machi 13. Hakuna mwenye
uhakika wa kwamba kilikuwa ni kitu gani, lakini maelfu walikiona, dazeni kadhaa
walikirekodi kwa njia ya video na watu kwenye jimbo zima bado fikra zao
zimenaswa kwenye tukio hilo ….
Mashuhuda hao wanakubaliana kwenye vitu vitatu juu ya tukio hilo. Kwanza
jichombo lenyewe lilikuwa ni jikubwa mno. Makadirio ya karibu ni kuwa ukubwa
wake ulikuwa ni sawa na urefu wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu.
Uchambuzi wa kompyuta kupitia video zilizo rekodiwa wamekadiria ni sawa na
futi 6000, au zaidi ya maili moja.
Pili chombo hicho hakikutoa ukulele wowote, kipo kimya kama hakipo.
Tatu kilikwenda taratibu juu ya eneo
la Phoenix, imekadiriwa kuwa na mwendo kasi wa 30 mph. Mara kadhaa kilikuwa
kikinata kwenye anga.( Chuck Missler na
Mark Eastman ‘ALIEN ENCOUNTERS’)
Venezuela, eneo la Maracaibo, Oktoba 24, 1886.Turkey eneo Istanbul, Mei
2008 – Septemba 2009.Portugal eneo la Fatima, Agosti 13, 1917, Septemba 13,
1917, Oktoba 13, 1917.Marekani, Aurora, Texas, Aprili 19, 1897.Urusi,
Podkamennaya Tunguska River, Juni 30, 1908. Marekani, Stephenville, Texas,
Dublin, Texas, Crawford, Texas, Januari 01, 2008 – Februari 09, 2008. Mexico,
jiji la Mexico, Agosti 6, 1997. Brazil, Varginha, Minas Gerais, Januari 20,
1996. Australia, Victoria, Agosti 8, 1993. Uingereza, London, Aprili 21, 1991.
Kanada, Montreal, Quebec, Novemba 7, 1990. Belgium, Ans, Wallonia, Machi 30,
1990. New Zealand, South Island, Disemba 21, 1978.
Kwa takribani miaka hamsini sasa tangu serikali mbalimbali duniani na
watafiti walipoamua kulishughulikia suala la UFO na kutafuta majibu ya maswali
kuhusiana na asili yake ni nini na tija au madhara yake kwa binadamu ni yapi
hakuna kati ya hao walio kuja na majibu ya kuridhisha au majibu rasmi kuhusiana
na suala hilo.
Kama UFO zitakuwa ni kweli zipo, na asili yake hasa ni kutoka nje eidha ya
sayari yetu au galaxy yetu, ukweli huo hapana shaka utakuwa ni changamoto ya
namna yake kwa binadamu wote. Kwa upande mwingine, ikiwa UFO si hivyo tunavyo
ambiwa na si hivyo inavyo elezewa na wale walio shuhudia , basi vyombo hivyo
vitakuwa ni ushahidi tosha wa mpango kamambe ambao mabilioni ya binadamu
hawafahamu hatima na malengo yake ni nini na ambao athari yake huenda
ikamuathiri kila binadamu aliyepo kwenye sayari hii.
NDIYO KWANZA TUNAANZA ..... NGOMA INAENDELEA HAPAHAPA ... CATCH YOU NEXT TIME ...
Mmh sasa izi ufo mbona n za ajabu zimetengezwa na nani na zinahifadhiwa wapi
ReplyDeleteEndelea kufuatilia hii blogi na utapata majibu yako na zaidi ...
DeleteUFO is man made so the eliens .... mengi yanaendelea ulimwengu huu elimu nyingi imefichwa ili kuamini wanachotaka kuamini... nimesoma mengi unajua vingi Bro Salim hongera, elimu yako itoe kwa jamii tafuta njia hii ya blog haitoshi. Reptilian r real ! Weka tofauti dunia inahitaji watu kama nyinyi. Mi niko nafanya kwa kadri yangu kuiokoa dunia yetu ...
ReplyDelete