Tangu Agosti 2914, Jeshi la Anga la Marekani na washirika wake, nchi 19 kwa
pamoja bila kuchoka wamekuwa wakifanya mashambulizi ya nguvu dhidi ya Syria na
Iraq, kwa dhana kwamba wana walenga Islamic State, wanamgambo wenye ‘msimamo wa
kati’ ambao nguvu na silaha zake wamezipokea kutoka kwa Marekani na kwa nchi
washirika.
Kutokana na mashambulizi hayo, mashambulizi ya anga yapatayo 16,000
yamefanywa kwa kipindi cha Agosti 2015 mpaka katikati ya Januari 2015 (Defense
News)
Asilimia sitini (60%) ya mashambulizi hayo, yalifanywa na Jeshi la anga la
Marekani kwa kutumia ndege za kisasa za kivita. Vyombo vya habari za magharibi
vimekuwa vikiripoti kuwa vita hivyo ni dhidi ya wanamgambo wa ‘Islamic State’.
Lakini kinyume chake ndiyo sahihi vita hivyo vimekuwa dhidi ya viwanda, miundo
mbinu, makazi ya watu, hospitali na kila aina ya uharibifu kwa rai wa nchi hizo
kuliko ‘Islamic Satate.’
Lakini pamoja na yote hayo, bado serikali ya Marekani inafikiria uwezekano
wa kufanya mashambulizi makubwa zaidi, yenye nguvu zaidi, sababu ‘islami state’
ni kitisho dhidi ya utawala wa magharibi na ustaarabu wake.
Mpaka sasa ndege ambazo zimetumiwa kwenye kampeni hii za kuwapiga watu wa
Syria na Iraq ni F-16 Fighting Falcon, F-15 Strike Eagle, The a-10 Warthog, na
F-22 Raptor.
SWALI LA MSINGI LA KUJIULIZA?
Kwanini Jeshi la Marekani na washirika wa nchi 19 wameshindwa kuwafuta
wanamgambo wa ‘ISALMIC STATE’ ambao, kwanza ni wanamgambo, pili silaha walizo
kuwa nazo mwanzo zilikuwa ni silaha ndogondogo.
Tangu yalipoanza mashambulizi, ni wazi kabisa walengwa hawakuwa ISLAMIC
STATE, lakini kinyume chake kabisa mashambulizi hayo yalilenga miundo mbinu ya
Iraq na Syria.
Tizama hii picha hapa chini na utafakari! Picha hii inaonesha siku ambayo kundi
la Islamic State lilisafiri KM 200, mchana kweupe, kwenye jangwa pana linalo
gawa nchi mbili, kutoka Syria mpaka Iraq. Salama salmini wanamgambo hao wakiwa
na msururu mrefu wa magari aina ya ‘Toyota Pickup’ waliingia Iraq Juni 2014.
Nini kilicho kosekana kwa ndege hizo za kivita za Marekani na nchi 19 washiriki
kuufutilia mbali msafara huo kwenye janga jeupe lisilo na kichaka?
Kama kweli vita hivyo ni dhidi ya ISIS, basi kwenye jangwa hilo, na kwa
silaha walizo nazo Marekani na washirika wake, hilo lingekuwa ni kaburi la
ISIS, lakini wapi walimaliza km 200 wakiwa na msafara mrefu wa magari meusi,
kwenye jangwa jeupe na kuingia Iraq, lakini ni wakati huohuo, ndege zisizo na
rubani ‘drone’ zilikuwa zikiendelea mashambulizi ya nguvu Pakistani.
Yes! walikuwa bize Pakistani wakiwatwanga raia wasiyo na hatia, huku ISIS
wakivuka jangwa salama salmini.
Ajabu nyingine ni kuwa hakuna chombo chochote cha habari kilicho ripoti
msafara huo. Msafara hewa wa Boko Haram kupotelea msituni na binti zaidi ya
270, iliripotiwa na kila chombo cha habari, ingawa hakuna hata gari moja la
Boko Haram lililonaswa na kamera ilikuwa na mabinti hao.
Lakini ISIS na msafara mrefu wa magari kutoka Syria mpaka Iraq kuvuka
jangwa jeupe, hakuna chombo hata kimoja
kilicho ripoti.
F15, f22 Raptor, F16 zilitosha kabisa kuwazika ISIS ndani ya saa moja.
Lakini kinyume chake ni vita vinavyo kwenda mwezi wa 9 sasa na ISIS inazidi
kupata nguvu na kutanua mipaka yake. Ikilinganisha na NATO, 1999 iliwachukua
miezi mitatu tu na YOGOSLAVIA ikawa nchi nyingine kabisa.
Lakini vyombo vya habari vinatuaminisha kuwa ISIS hawawezwi kumalizwa na
jeshi kubwa la anga la Marekani na la nchi 19 washiriki!
Hivyo basi utaona vita hivi walengwa si ISIS, bali Syria na Iraq. ISIS
wanatoa sababu maalum na mahususi kwa Mrekani na washirika kuzichanachana nchi
hizo. Hivyo ISIS wanafanya kile ambacho Marekani na washirika wake wanacho
taka, hivyo ISIS na Marekani na washirika wao lao ni moja. Lakini pia situmeona
vile ISIS walivyo patiwa silaha kupitia kwa Seneta McCain mwenyewe, na fedha
kuoka kuwait na nchi zingine za kiarabu.
Hivyo basi ISIS ni adui nambari moja wa WAISLAM na UISLAM, ISIS HAWAPIGANI
DHIDI YA MAREKANI, LAKINI SAFU MOJA NA MAREKANI DHIDI YA UMMA WAKIISLAM, AMKA
WEWE KIJANA UNYEOTA NDOTO ZA KUSIMAMISHa khilafa kwambinu za kina isis,
alshabab, boko haram n.k, huo ni mtego na fitna kubwa kwa umma.
No comments:
Post a Comment