Ushirika wa US-NATO 2011 ulianza kuwagawia silaha vikundi vya kigaidi
wakiwemo Al Qaeda kwa ajili ya kuangusha utawala wa Libya.
Silaha hizo nzito
zilisafirishwa kutoka Libya kupitia Kusini mwa Uturiki kisha zikavushwa mipaka
na kuingia Syria mpaka kwenye mikono ya ‘FREE SYRIAN ARMY (FSA), JABHAT AL
NUSRA (AL Qaeda wa Syria) na vikundi vingine vya ugaidi ambavyo Obama anaviita
‘Magaidi wenye Msimamo wa Wastani’ ambao wanastahiki kupewa silaha. AJABU SANA YULE AMBAYE UMEKUWA KWA SIKU ZOTE UKIMUITA ADUI, NA AMBAYE IMEBIDI KUIITA DUNIA NZIMA WAKUSAIDIE JUMPIGA, LEO UNASEMA NI SAWA AKIPEWA SILAHA?!!! AMA KWELI UKISTAAJABU YA MUSA ...
Kwa upande mwingine FSA, NUSRA pamoja na ISIS wanafanya kazi pamoja na
kushirikiana na June 2014 NUSRA na ISIS zilisimama pamoja kama kikundi kimoja.
Mtandao wa magaidi kwa makusudi makubwa kabisa, umeachiwa huru ukuwe na
ukomae kiasi cha kuchinja mamia kwa maelfu ya watu na dunia nzima kunyamaza
kimya.
Mtandao huu tangu ulipoanza kwenye miaka ya mwishoni mwa 70 wakati
Mmarekani anapambana kumtoa Mrusi kwenye U-super Power, ulitumia jina la ‘HOLY
WAR’ yaani ‘VITA VITAKATIFU’ au JIHAD, Kiongozi akiwa ni Osama Bin Laden,
lakini nyuma yake wakiwemo, akina Abu Bush, Abu Kissinger, Abu Jimm Carter, Abu
CIA na Abu Zbig mwenyewe,
Mtandao huo hivi sasa umetanuka na ukiwa na kisingizio cha ‘KHILAFA’ hivi
sasa ni Jihadi ya kusimamisha KHILAFA, lakini sura za wafadhili zikibakia zile
zile, Abu Obama, Abu Nato, Abu Zbig, Abu CIA, Abu Israel na wengine.
Kwa sasa mtandao huu umeweza kukusanya wanachama kutoka zaidi ya nchi 80,
zikiwemo nchi za Ulaya na Marekani.
Marekani imekiri kupitia Retd. Lt.Gen. Ian Mclnerny kuwa ilishiriki vilivyo
kuiyandaa, kuitengeneza na kuiacha ifikie hapo ilipo, ISIS.
Ukiacha taarifa hizo za kiongozi wa jeshi kukiri kuhusika katika
kuitengeneza ISIS, taarifa zingine zinamuonesha Seneta John Mcain waziwazi
akiwa amepiga picha na waasi wa Syria, ambao Marekani inakataa kuwaita magaidi.
Kwenye Picha hiyo yupo mtu mashuhuri na maarufu ambaye Marekani inamtafuta, AL
BAKR AL BAGHDADI aka ‘NEW OSAMA’
MCCAIN AKIWA NA AL BAGHDAD, BAADA YA KIKAO HICHI AL BAGHDAD AKAJITANGAZA KUWA KHALIFA NA MUDA SI MUDA ISIS IKAANZA KUPATA 'COVAREGE' KWENYE VYOMBO VYOTE VYA HABARI VYA MAGHARABI, NA HUKU KWETU IKAWA NI 'KU-COPY' N 'PASTE' HABARI HIZO NA GHAFLA ISIS IKIWA SI KITU KINACHO WEZEKANA KUSHINDWA TENA,
Lakini mbali na hili pia imefahamika kwamba Marekani imeshirikiana kwa
karibu sana na Saudi Arabia, Jordan na Israel kuwasaidia waasi hao katika
mipango yao ya kuivamia Syria.
Waasi hao wa Mr. Obama walipata mafunzo yao ya kijeshi katika kambi
zilizopo Jordan, Uturuki na Qatar kabla hawajaingia Syria. Maeneo hayo yapo
chini ya uangalizi wa NATO. Lakini zaidi waasi hao wa Obama, ISIS, FSA, JABHAT
AL NUSRA walipopata majeraha walikwenda kutibiwa kwenye kambi za Israel
zilizopo kwenye maeneo ya Golani yanayo milikiwa na Israel.
ALBAGHADAD ILIUNDA ISIS MWEZI MMOJA KABLA YA KIKAO HICHI CHA MCCAIN. NI KAMA KHALIFAH HUYO ALIKUWA AKIPOKEA MUONGOZO KUTOKA WASHINGTON KUWA KITU GANI AFANYE WAKATI GANI.
Msemo maarufu wa ‘Marekani hana adui/rafiki wa kudumu’ umedhihiri kwenye
sera zake za mambo ya nje, hasa nafasi ambayo Seneta John Mcain aliyoitumia
kuhakikisha ISIS na wenzake wanapata ‘Khilafa’ yao.
4 Februari 2011, NATO iliandaa mkutano kwa ajili ya kuanza mkakati wa kuishughulikia
Syria na Libya. Mkutano huo mwenyekiti wake alikuwa ni John Mcain.
22 Februari 2011, McCain alikutana na Saad Harir Beirut na kumpatia jukumu
la kuhakikisha waasi wa Obama wanapata silaha ambazo zitapelekwa Syria.
April 2013, Seneta McCain alitembelea kwa siri mji wa Idlib uliopo
Kaskazini Magharibi mwa Syria na kufanya kikao na makamanda wa waasi na
wanajeshi wao, ambao yeye McCain kupitia serikali ya Marekani anahakikisha kuwa
wanapata silaha, fedha, matibabu na kila wanacho taka ilimradi eneo hilo la
Mashariki ya kati liendelee kuwaka moto kwa jina la ‘Khilafa’.
Katika watu ambao McCain alikutana nao siku hiyo alikuwepo pia Abu Bakr al
Baghdad, mtu aliye jitangaza mwenyewe kuwa ni Khalifa. Wakati McCain anakutana
na AlBaghdad Marekani ilikuwa imeshatangaza zawadi ya dola milioni 10 kwa
yeyote atakaye leta kichwa cha Albaghdad au atakaye pelekea kutoa taaria za
kukamatwa kwake. McCain angeweza kushtakiwa kabisa kwa kushirikiana na Magaidi.
Lakini McCain si wa kwanza kufanya hivyo, wala hilo si jambo geni kwenye
sera za mambo ya nje za Marekani. Bush alifanya hivyo kabla ya 9/11.
Ajabu ni kuwa ISIS baada ya ‘kuteka’ silaha hizo, walipita nazo mitaani
waziwazi, wakijitapa na kuringa nazo. Lakini Marekani kinyume na sera zake za
kivita, haikujaribu hata kuwashambulia ilikuharibu au kurudisha silaha zao, waliwaacha
kama hawajui vile.
Muda huohuo Marekani ilikuwa ikiendesha mashambulizi ya drone Pakistan,
lakini haikutumia drone zake kuwagusa ISIS katika mitaa ya Mosoul au
kwengineko.
No comments:
Post a Comment