IS (Islamic State) inatoa upenyo sawia kwa majeshi ya NATO na Marekani
kuwepo na kuendelea kuafanya ‘kazi’ zao ndani ya Mashariki ya Kati.
Kila aina ya vita ya Ugaidi, inazalisha mamia kwa maelfu ya magaidi na
kuwahakikishia majeshi ya nchi za Marekani za Ulaya kuendelea kuwepo katika
eneo hilo. Nchi kama Iraq, Syria na Libya ambazo hazikuwa na watu wanao itwa Al
Qaeda, lakini baada ya uvamzi wa wa majeshi ya US-NATO kumekuwa na kila aina ya
Al Qaeda katika maeneo hayo na zaidi.
Sasa tunaiona IS kwenye uso wa dunia, kwa furaha, uhuru wanacheza ‘wimbo’
wowote wanao taka bila kuguswa na yeyote. Limekuwa ni jeshi kubwa kutoka kwenye
mitandao ya kijamii, mpaka kwenye maisha halisi, wanamiliki silaha nzito na
zile za kisasa. Wanapokea misaada ya kutosha kutoka baadhi ya nchi za Kiiarabu,
Ulaya na Marekani.
Kukuwa kwa IS swali moja ni lazima tujiulize wenyewe, ‘Hivi inawezekana
kweli kwa kikundi cha ugaidi kama IS kukuwa na kumiliki nguvu zote hizo za
kifedha na kisilaha bila kuwa na msaada wowote kutoka nchi yeyote, shirika
lolote?
Unapoitazama IS na vikundi mfano wake na maeneo ambayo shughuli zao za
kusimamisha Khilafa zinalenga, utaona kuna maeneo manne mahususi ambayo
yanalengwa.
Mwaka 2007 kiasi kukubwa cha gesi kiligundulika Mashariki mwa eneo la
Mediterania ikihusisha Syria, Lebanon, Palestine, Israel na Cyrups, lakini pia
Iran na Qatar.
Kisha vita vya kumiliki njia ya bomba la mafuta linalofahamika kama ‘Bomba
la Iran-Iraq-Syria’ na ‘Bomba la Qatar’ ambayo kufika nchi za Ulaya ibidi
yapitie Syria kwenye pwani ya Mediterani halafu Uturuki kisha Ulaya.
Kama Urusi na Ulaya watakuwa na umiliki wa gesi zao, watakazo safirisha
kupitia kwenye mabomba yao, hiyo ni kusema kuwa Urusi na Irani watamiliki mpaka
50% ya mafuta yatakayo kwenda Ulaya. Kwa maneno mengine Urusi na Iran kwa
pamoja zitakuwa zinatoa changamoto kwa Marekani ikiwa inastahiki kukalia kiti
cha Super Power au La?
Upande mwingine wa habari ni kuwa si muda mrefu sana Marekani ataendelea
kukalia kiti hicho, kama tunavyo jua kwa upande wa Biashara tayari Marekani
imeshapitwa na China, lakini anayeandaliwa kuchukua kiti hicho baada ya
Marekani si Mchina, wala Mrussi bali ‘Mwiisrael’.
Lakini Israel mwali mpya kwenye nyumba ya ‘Usuper Power’ hatoweza kupendaza
na kukalia kiti hicho kwa imani ikiwa kuna nchi kama Iran, Iraq, Syria na
washirika wao bado wako hai. Nchi hizi inabidi zivurugwe na kuchanwa chanwa
kama makaratasi kwa kutumia aina yeyote ya mbinu, njia na mipango itakayo
zalisha matokeo hayo, iwe ni Jihadi, iwe ni Khilafa, iwe ni Shia vs Sunni
chochote kile, ilimradi mwali mpya akiingia akalie kiti chake kwa amani.
Qatari ilitoa dola milioni 2.5 kwa Abu Bakr al-Baghdad iliaweze
kuitengeneza ISIS na yeye awe ni Khalifa wa eneo hilo.
Baada ya kugundulika kuwepo kwa kiasi kikubwa cha gesi 2007, Qatari ilianza
kwa kumshawishi rais Assad kuachana na bomba la gesi la Iran-Iraq-Syria na
ajiunge na Bomba la Qatar. Assad akajibu kuwa hawezi kumsaliti Mrussi ambaye ni
rafiki na mshirika wake.
Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa bwana Roland Dumas mwaka 2009,
akasema kuwa Qatar ililipa dola bilioni 10 kwa waziri wa mambo ya nje wa
Uturuki Mr. Dovutoglu kwa ajili ya mpango wa kuivunja vunjia Syria kama siyo
kuipindua kabisa.
Baada ya mpango wa Saudia wa kuiangusha Syria kushindikana, na wapiganaji
wa kulipwa wapatao 20,000 kuchakazwa na jeshi la Syria, na propaganda za
kuichafua serikali hiyo kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani kugonga
mwamba, ndipo Saudia ilipongia kwenye kila mtaa wa dunia hii kuwasaka ‘magaidi’
ambao watakwenda kusimamisha Khilafa Syria chini ya Al-Baghdad, hata hapa kwetu
Tanzania waliingia, na vijana wengi wanao fuata mkumbo tukawapoteza eidha
kwenye magereza au kutaka kwenda kwenye nchi hizo zinazo taka kusimamisha
Khilafa ya McCain na Obama. Mpaka sasa wengi wapo jela na wengine wameuwawa.
Saudi na timu yake ya kusaka vijana walipita kwenye nchi zaidi ya 80
ikiwemo nchi za Ulaya na Marekani ambako huko walifanikiwa kwa kiasi kikubwa
kupata vijana wa kwenda kupigana Syria kwa maslahi yao, lakini kwa kutumia jina
la dini yetu tukufu; Uislam.
Jeshi la Iraq lililo pewa mafunzo kwa gharama kubwa na serikali ya
Marekani, pamoja na kupatiwa silaha za kisasa kabisa, halikuweza kusimama mbele
ya wanamgambo wa ‘kiislam’
wa Obama. Wakati mwingine wanajeshi hao walikimbia na kuziacha silaha zao,
na vijana wa Obama wakaziokota.
Nigeria nako tumeona mchezo kama
huo, na sasa maafisa kadhaa wa jeshi la Nigeria wako ndani kujibu tuhuma za
kwanini jeshi lao lilikimbia na kuwaachia Boko Haram silaha.
Ni kama mchezo wa kiigiza, hivi inakuingia akilini kabisa kuwa jeshi la
nchi linazidiwa nguvu na kuacha silaha zao na kukimbia? Au ni njia za
kuhakikisha kuwa magaidi wanamiliki silaha sawa na serikali wanayo pambana
nayo?
Ghafla ISIS wanaonekana wako mtaani na vifaru, makombora ya kutungulia
ndege, bunduki nzito, Helikopta nzito. Vyote wameteka kutoka kwenye jeshi la
Iraq. Mara mji mmoja baada ya mwingine ukaanza kuanguka kwenye mikono yao.
... ITAENDELEA ...
No comments:
Post a Comment