Kuonekana kwa UFO kwenye anga la sayari yetu ya dunia siyo jambo jipya na
geni. Katika kumbukumbu nyingi za kale kumekuwa na rekodi za vyombo mbalimbali
vya kusafiria vya kale ambavyo vilikuwa na sifa za kupaa kama gari za angani,
diski zenye mbawa, ndege na vyombo vingine vya angani vyenye mwanga mkali.
Jacques Vallee mtafiti kwenye mambo yahusiayo UFO na ambaye moja ya kazi
zake ni ile inayo patikana kwenye filamu maarufu ya mwaka 1997, ‘Close
Encounters of the Third Kind’ Mwaka 1969 Vallee aliandika kitabu chenye mvuto wa aina yake kwenye masuala
hayo kilicho kwenda kwa jina la ‘Passport to Magonia’, Vallee anasema,
“….
Hadithi za kufikirika kwenye jamii mbalimbali duniani, imeonekana kuwa, zina kiasi
kikubwa cha wapokeaji wa hadithi zinazo husu viumbe wanao karibiana na binadamu
walio kuwa wakiruka angani na wakitumia vyombo na nyenzo zilizo onekana ni bora kiteknolojia
ukilinganisha na zama hizo.”( Jacques Vallee ‘Passport to Magonia’)
Watafiti wa UFO John Weldon na Zola Levitt ambao utafiti wao wameuweka
kwenye kitabu walicho kiita, ‘What on Earth Is Happening?’ wanasema,
“UFO zinaonekana kuwepo kwa
muda mrefu. Tunaweza kupata hadithi za kushangaza zinazo husu ‘maduara ya moto
angani’ kwenye kumbukumbu nyingi za kihistoria na hata kwenye michoro ya
mapangoni. Wakati tukijiona kuwa na taarifa nyingi zinazo husu UFO katika zama
zetu, kila zama zinaonekana kuwa na hadithi kama hizi za kwetu (tunazo ripoti
sasa kuhusu UFO)”( John Weldon
na Zola Levitt, ‘What on Earth Is Happening?)
Kama tutazungumzia kuwepo kwa viumbe wengine ambao ni huru kama binadamu
basi Misri ni nukta ambayo haiwezekani kuachwa kwenye mazungumzo hayo, hapa
nitazungumzia kitu kingine kidogo tu kwenye mstari huohuo wa viumbe huru mbali
na binadamu na mahusiano yake na vyombo visivyo fahamika kwenye anga la dunia.
Kwenye utamuduni wa kale wa kutoka Egypt na watu wake kumejaa visa vingi
vinavyo wahusu ‘miungu wenye kupaa’ ambao walikuja duniani na kati ya mambo
mengi ni kuwatawalia binadamu mambo yao na kuwaongoza. Vyombo walivyo tumia miungu
hao ni ‘diski za duara’ na ‘ngalawa zenye kupaa’ ambazo mwonekano wake ni sawa na maelezo
ya watu wa zama zetu walio ona UFO.
Kutokana na hadithi za kale za watu wa Misri, mungu jua ambaye alifahamika
kama Ra, alikuwa ndiye mungu wa ulimwengu wote na alikuwa akisafiri kwa kutumia ‘ngalawa
inayo paa’ Mungu huyu huoneshwa
akiwa na mwili wa binadamu na kichwa cha ndege tai. Mungu mwana wa Ra aliitwa Horus, ambaye alizaliwa na mungu mama, bikira Isis. Mungu mwana huyu alikuwa ndiye mungu wa
mbingu, mungu mwangaza na wema. Horus huoneshwa akiwa na umbile la binadamu na
kichwa cha kipanga. Horus naye alisafiri angani akitumia diski yenye mbawa.( E. A. WALLIS BUDGE ‘THE
BOOK OF THE DEAD’, The Papyrus of Ani).
Isis mungu mama, bikira aliyemzaa mungu mwana
Horus, wakati anatoroka kumuokoa mwanae ambaye ni Horus asiuwawe na Seth
alisaidiwa na mungu Thoth kutoroka kwa kutumia boti yenye muundo wa disk inayo
paa angani. Chombo alicho safiria angani mungu baba Ra, kilikuwa kiking’aa kwa
rangi nyingi, maelezo ambayo yanafanana na chombo cha UFO.
Kuonekana kwa vyombo hivi vya ajabu Mashariki ya Kati viliendelea muda
mrefu baada ya matukio kama hayo kwenye jamii ya watu wa Egypt wakale.
Katika kipindi cha dola ya wa Giriki na ile ya Roma kutoka karne ya nne BC
mpaka kwenye karne ya 17 BC mara kadhaa vitu vya ajabu ambavyo muambilie na
teknolojia yake ilikuwa hailingani hata kidogo na zama zenyewe vilionekana
katika anga hizo.
Kutoka kwenye kazi ya Weldon Levitt kuhusiana na zama hizo na vyombo vya
usafiri vya anga ambavyo havifahamiki wanasema,
Zama zilizo fuata na karne zake ambazo zilishuhudia kunyanyuka na kuanguka
kwa dola ya Roma, bado rekodi ya vyombo visivyo fahamika katika anga la sayari
yetu iliendelea kuingizwa kwenye vitabu vya kihistoria duniani kote mpaka
kwenye zama zetu hizi.
Nukta ambayo ingefuatia hapa baada ya hiyo historia fupi ni shuhuda rasmi
kutoka katika serikali mbalimbali duniani na taasisi zake. Lakini huenda ni
kutokana na muda au mchezo unao chezwa kuhusiana na suala hili binafsi sijaweza
kupata ushuhuda huo, ingawa kupitia milango ya nyuma, vyanzo visivyo rasmi na
wafanyakazi wa kiserikali kutoka eidha serikalini au taasisi na mashirika ya
kiserikali yanayo husiana na masuala haya upo ushuhuda wa kutosha kwamba
lisemwalo lipo.
Hivyo nukta hii nitaiacha ikining’inia kama haipo lakini nitakuwa nikiigusa
moja kwa moja, au kupitia kwa katika mfululizo wa kazi yetu hii. Nitakuwa
nikiigusa kwa namna ambayo baadhi ya serikali, taasisi na watendaji wao
wanakiri waziwazi juu ya vyombo hivi na shughuli zake.
Ikiwa UFO ni vyombo ambavyo
havijulikani, na ikiwa vinaweza kufanya vitu vya ajabu na hatari kushinda hata
vile ambavyo vyombo vyetu vya anga na vile vya kivita vinavyo weza kufanya,
basi hapana shaka vyombo hivyo vinamilikiwa au vipo nyuma ya viumbe ambao ni
huru. Swali la msingi ni; Je kuna viumbe huru katika sayari yetu na kutoka nje
ya sayari yetu kama binadamu?
Kwa ajili ya somo letu kuweza
kueleweka vyema, na muhimu lieleweke vyema kwa sababu kama tulivyo ona kwenye posti
hii (HATUA NNE KABLA YA UJIO WA MASIHDAJJAL/KRISTO WA UWONGO/MPINGA
KRISTO/666) icheki hapa, http://salimmsangi.blogspot.com/2013/08/hatua-nne-kabla-ya-ujio-wa.html
ni kuwa karata ya mwisho itakayo chezwa na maadui zetu kwa ajili waweze
kututawala chini ya utawala wa kishetani ni kutuletea kitisho kutoka nje ya
sayari yetu. Hivyo kati ya mengi hapa pia tutaangalia ikiwa kuna kiumbe kingine
huru mbali na binaadamu, si kutoka kwenye sayari yetu tu, bali hata nje ya
galaxy yetu ya Milk Way, Inshallah.
Maoni ya wengi ni kuwa ‘viumbe
kutoka nje ya sayari yetu’ na ambao wanatumia UFO ni wageni kutoka kwenye
Galaxy nyingine mbali na hii ya kwetu. Viumbe hao husafiri mamilioni ya maili
kwa muda mchache sana, kitu ambacho kinapingwa kutokana na ukweli kwamba
kusafiri tu kutoka kwenye dunia yetu kuelekea kwenye nyota iliyo karibu sana na
dunia yetu huenda ikachukua kwa uchache miaka 70,000. Kizingiti kikubwa
kuhusiana na usafiri huu wa kutoka achilia mbali galaxy moja kwenda nyingine
lakini kwenye nyota tu zilizo kwenye galaxy yetu ni nishati kiasi gani
itahitajika kwenye safari kama hiyo ambayo mwendo kasi wake ni ule wa umeme.
Kumbuka safari ya mwezini waliirekodi kwenye jangwa la Nevada na kudai ni
mwezini. Nimeshalieleza hilo kwa kina kwenye posti hii, HATUKWENDA MWEZINI, unawweza kuipata
hapa, http://salimmsangi.blogspot.com/2014/12/hatukwenda-mwezini.html
Lakini huenda ‘ viumbe’ wanao
endesha UFO wanayo teknolojia hiyo ya maajabu.
Lakini kuna ‘shortcuts’, Wormholes.
Kabla hatujaanza kuitizama ‘shortcuts’ kuna misamiati mitatu ambayo inabidi
tuitizame na tuielewe kabla ya kuzama kwenye somo letu. Misamiati hiyo ni
Wormhole,
Timerelativity, na
Blackhole.
Blackhole ni hali inayo tokea au ni mazingira yanayo patikana baada ya kifo
cha nyota angani. Nyota hiyo ambayo utakuta ukubwa wake unazidi nyota yetu ya
jua mara tatu mpaka kumi na zaidi. Nyota hiyo inapoishiwa na ‘mafuta’ yake
inaongezeka ukubwa. Joto lake ambalo lilikuwa ni nyuzi milioni 15, linaongezeka
na kufikia nyuzi milioni 100. Nyota hiyo hubadilika na kuwa nyota kubwa na
nyekundu, ukubwa wake unazidi ukubwa wa nyota yetu ya jua mara milioni 60. (ametakasika
Mola wangu Mbora wa Uumbaji) Kutokana na
kuwa nyota hii imeishiwa na mafuta yake inakuwa haina nguvu ya kuzishinda nguvu
zake za mvutano na hivyo inajimeza yenyewe, inanyonywa na nguvu zake za mvutano
na kutengeneza Blackhole.
Tukio hili muhimu kwenye maisha
ya nyota katika ulimwengu wetu limeelezewa katika Quran 56:75-76;
“Basi naapa kwa maanguko ya
nyota,”
“Na hakika bila ya shaka
hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngelijua!”
Blackhole unahusiana vipi na mada
yetu hii? Kifizikia inafahamika kuwa hakuna chenye kukatisha Blackhole hata mwanga
wenye kusafiri kwa kasi ya kilometa 300,000 kwa sekunde haukatizi kwenye shimo
hilo! Lakini nadharia mbayo haijathibitishwa kabisa ni kuwa Blackhole inayo upande
wa pili ambapo ni Whitehole. Utakapo zama kwenye blackhole
utaunganishwa kupitia ‘Wormhole’ kufika kwenye Whitehole ambapo hapo
utakuwa umetokea kwenye ulimwengu mwingine. Lakini nadharia hii haikamiliki
mpaka kweli kuwepo na Whitehole mwisho wa blackhole na kuwepo na Wormhole
ambavyo hivi vyote vipo kwenye nadharia.
Kutokana na itikadi kwamba huenda
kukawa na viumbe wengine ima katika galaxy au sayari nyingine walio piga hatua
na maendeleo makubwa kiteknolojia na kiustaarabu kutushinda sisi, huenda hivi
ambavyo katika ulimwengu wetu ni nadharia kwao vikawa ni maarifa yanayo fanyika
kivitendo na vyenye ukweli wa msingi, hivyo kwa wao kutumia, blackhole,
Whitehole, Wormholes ni kitu kinacho wezekana kabisa. Lakini swali ni je viumbe
hao wapo? Kwa ushahidi upi tutatambua kama wapo?
Wormhole kama tulivyoona nayo ni tobo la kufikirika ambalo linasemwa
linaweza kuunganisha sehemu mbili tofauti kwenye galaxy mbili tofauti, sayari
au nyota na muda.
Safari kuelekea kwenye nyota nyingine au galaxy kupitia Wormhole inakuwa
fupi sana. Lakini kwa sharti ya kuwepo kwa hiyo Wormhole. Katika ulimwengu wa
dunia yetu hii ya tatu kutoka kwenye mfumo wetu wa jua, Wormhole bado ni
nadharia piwa, hatujui kwa ‘hao’
wanao tajwa kuwa ni viumbe kutoka ulimwengu mwingine labda kwao ni ukweli wa
msingi na wanaweza kusafiri kutoka kona moja ya galaxy, nyota au sayari kwenda
nyingine kwa kutumia Wormholes. Lakini swali letu linabaki palepale, viumbe hao
wapo? Ushahidi ni upi kuwa wapo?
Hivyo kupitia kwenye Wormhole,
sehemu mbili za ulimwengu tofauti yaani galaxy au nyota zinaweza kufikiwa,
lakini zaidi pia muda tofauti na kwenye nukta ambayo safari imeanzia. Kabla
ilikuwa ikichukuliwa kuwa muda upo sawa sehemu zote kwenye Milkway na kwenye
galaxy nyingine. Lakini baadaye ikaja kuthibitika kuwa muda unatofautiana
sehemu mbalimbali kwenye galaxy, sayari na nyota zingine, na hapa ndipo
ugunduzi mkubwa wa watu kama Einstein, Galileo, na Aristotle ulipo kuja na ‘theory of relativity’ au ‘time relativity theory’.
Ingawa wanasayansi na wanafizikia
hawa nadharia hii imebaki bado ni nadharia, kwenye kitabu kitakatifu cha Quran
mahali pengi ‘time
relativity’
haikutajwa kama nadharia bali; ukweli wa msingi. Tizama Quran 70: 4, Quran 32: 5, Quran 10: 45, Quran
23: 112-113.
Kabla ya kulitizama hili la time relativity kwa mustakabali wa mada yetu,
kwanza tujiulize swali moja tata kidogo;
Wakati, muda, saa ni nini? Au What is Time?
Kama unatembea barabarani halafu mtu akakusimamisha, akakuomba samahani
halafu akakuliza what is time? Hapana
shaka utanyanyua mkono wako utatizama mashine iliyoko mkononi mwako au
utalitizama jua na kisha utamuambia ni saa kadha, na dakika kadha halafu kila
mtu ataendelea na ustaarabu wake.
Kiasi fulani hichi ndicho tunacho kijua kuhusiana na saa. ‘Muda hautoshi bana, tutaonana kesho.’ Utawasikia watu wakisema, kila mtu
anatamani lau tungelikuwa na muda zaidi, kila siku, muda, saa, wakati hautoshi,
lakini what is time?
Kuna leo, kesho na jana. Je muda
ndiyo kizingiti kwamba hatuwezi kwenda kuiona kesho, kurudi kuioyana jana? What is time? Je tunaweza kurudi nyuma kwenda kumuona
Yesu (Rehma na Amani ziwe juu yake) alivyo kuwa anahubiri na alikuwa akihubiri
kitu gani? Je tunaweza kurudi nyuma na kwenda mwona Muhammadi (Rehma na Amani
Ziwe Juu yake) na masahaba zake (Radhi za Mola wetu ziwe juu yao) katika moja
ya vikao vyao? Lakini what
is time? Ndiyo inayo tuzuia tushindwe kumuona Hitler? Ndiyo inayo tuzuia tusiende
mwaka 2090 na kujua dunia itakuwaje? What is time? Kuweza kurudi nyuma kwenda kuiona ‘jana’ au kwenda mbele na kuweza kuiona
‘kesho’ wanasayansi wa leo katika fani husika wameiita hiyo hali ni ‘time traveling’.
Eidha time traveling inawezekana
ama la lakini kwanza what is time?
Inavyofahamika kisayansi saa ipo kwenye mstari ulionyooka, yaani ina mwanzo,
kati na mwisho. Lakini relativity theory
inatupa mtazamo mwingine juu ya saa. Kwamba hali inayo itwa saa si kitu unacho
weza kukishika, saa imeongezwa kwenye ulimwengu wetu wa 3D, na kuifanya kuwa ni
4D kwa dharura na kwenye mazingira fulani ingawa kiuhalisia na kimantiki hasa
ulimwengu wetu ni 3D. Saa kwa mtazamo wa
sayansi ya kifizikia na kifalsafa ndiyo hali inayo tufunga tushindwe kusafiri
kwenda kuiona kesho na kurudi nyuma kuiona jana.
Kwa vile kimaumbile kitendo
kilicho kwisha pita hata ndani ya sekunde iliyogawanywa hakiwezekani kamwe
kubadilishwa, sekunde (saa) imeshapita, hatuwezi kimaumbile kurudi nyuma kabla
ya tukio kufanyika na kuzuia lisifanyike au kulirekebisha namna ambayo linapasa
kufanyika.
Kama kilivyo kitu chochote ambacho
kimerikodiwa iwe ni Quran katika CD, filamu au chochote kile, hata posti hii
unayo soma, utaona kina mwanzo, kati na mwisho lakini kiasilia ni kitu ambacho
kinapatikana katika hali ya ukamilifu wake, mathalani unaposikiliza CD hiyo
kutakuwa na mwanzo, kati na mwisho wa kile ambacho unasikiliza au kutizama
lakini kitu chenyewe kilivyo hifadhiwa kwenye chombo hicho hakina mgawanyo huo,
bali mgawanyo wa eidha upo mwanzo au mwisho unategemewa na muda ambao muhusika
anasikiliza/tizama kitu hicho. Ndivyo ulivyo wakati/saa, haina mwanzo wala
mwisho bali sisi wahusika ndiyo tunaipa hali hiyo au aina hiyo ya mtazamo.
Na maanisha wewe hapo ulipo unapo soma posti hii, maisha yako na vyote
vinavyo kuzunguka, na vitakavyo kuja au utakavyo fanya baada ya kumaliza kusoma
hapa unapo soma ni kama kitu kilicho hifadhiwa kwenye CD, wewe unaona maisha
yako yana mwanzo, yana kati na yatakuwa na mwisho, lakini kuna ambaye
anayatizama maisha yako bila kuathiriwa na kitu ambacho wewe unakiita wakati/
muda/ saa, yeye anayaona hayo maisha yako yaliyopita, ya sasa na yanayo kuja
kwa pamoja bila kuwa na mwanzo wala kati wala mwisho. Hii ni sifa ya MUNGU
MMOJA ALIYETUKUKA, uonaji wake yeye hauathiriwi na muda.
Ingawa kwenye kalenda yako wewe
inasoma umezaliwa miaka 20, 30 au 40 iliyo pita, lakini machoni pa Mungu Mmoja
wa Haki, tendo la wewe kuzaliwa linaonekana kama ndiyo unazaliwa sasa, ingawa
utakufa miaka 20, 5, au 1 baadaye lakini machoni pa Mungu Mmoja wa Haki tendo
la wewe unakufa linatokea au linaoneka hivi sasa. Hakuna mwanazo wala mwishoni
machoni pa Mungu, hali zote, vitendo vyote, vinaoneka kwa wakati mmoja. Maumbile
yetu hayaturuhusu sisi kuona hali katika sifa hiyo.
Ukiwa na mantiki hiyo kichwani mwako, kwamba wakati hauko kwenye hali ya
mstari mmoja, hivyo hauna mwanzo wala mwisho bali ni hali itakayo pewa mtazamo
huo na wahusika tofauti, mahala tofauti na mazingira tofauti, hapa ndipo inapo
kuja nadharia nyingine kuhusiana na UFO. Kwamba je UFO na viumbe wanao endesha
wanatokea katika wakati ujao.
Nadharia hiyo inadai kuwa UFO
watakuwa ni binadamu wa zama zijazo ambao teknolojia yao imekuwa ya hali ya juu
kiasi kwamba wameweza kusafiri kutoka kwenye hali tunayo ita ‘wakati
ujao’ na kuja kwenye
‘wakati uliopita’ ambao kwa wao ‘wakati uliopita’ ni ‘wakati uliopo’ kwetu sisi. Hivyo ni binadamu
wanao toka katika wakati ujao, au pia inawezekana kuwa ni viumbe wanao toka
kwenye ulimwengu mwingine ambao maendeleo yao ya teknolojia yana wawezesha
kusafiri kutoka kwenye ‘wakati ujao’ na kuja kwenye ‘wakati ulio pita’ ambao
kwetu sisi ni wakati uliopo kwa vile kitu unacho kiita ‘saa’ hakina mwanzo,
kati wala mwisho na hakipo kwenye mstari ulio nyooka.
Lakini kama watakuwa ni binadamu
ambao maarifa yao yame wafikisha hapo na kuweza kufanya ‘time
traveling’ yaani kutoka
kwenye ‘hali’ moja ya ‘saa’ kwenda nyingine, haikubaliki kwa vile ‘mashuhuda’
wa vyombo hivyo na wale walio wahi ‘kutekwa’ na viumbe hao wanasema siyo binadamu!
Lakini juu ya yote ‘time traveling’ kwa binadamu haliwezi kufanyika KIMWILI
bali KIROHO, kila mmoja wetu kwa nyakati tofauti amefanya ‘time traveling’
kiroho, yaani bila kiwiliwili, na hapo ni wakati unapokuwa NDOTONI, ambapo ‘unaota’
tukio ambalo linakuja ‘kutokea’ sehemu fulani kwenye nukta ya maisha yako.
Lakini kimwili inakuwa ni vigumu mno na sina muda wa kutosha kukuelezea kwa
nini inakuwa vigumu, unless kama mada hiyo ikija kwa mfumo wa swali.
Lakini kama itakuwa ni viumbe wengine kutoka nje ya ulimwengu huu kama
inavyo semwa basi, ushahidi wenye mashiko na misingi inayo eleweka na
kukubalika lazima uwekwe mezani kuthibitisha kuwepo kwa viumbe hao, kitu
ambacho mpaka sasa bado hakijafanyika.
Tumetoka nje kidogo na somo letu la UFO, ila nukta nilizo zitaja hapo juu
tutakuwa tukizirudia mara kwa mara kutoka hapa na kuendelea.
Kitendo kinacho fanywa na UFO au tabia za UFO ambapo huweza kujitokeza na
kupotea kwa kipindi cha kupepesa jicho tu, kusafiri kwa mwendo kasi mkubwa na
kupinduka chini juu na juu chini au kugeuka katika nukta mbayo vyombo vyetu
haviwezi zimechukuliwa kuwa ni tabia za ‘hyperdimensional’ au tabia kutoka
kwenye galaxy nyingine.
Maumbile yetu au tabia zetu sisi binamu tunaweza kuutambua au kuuona
ulimwengu wetu na vile vyote vinavyo tuzunguka kwenye mfumo wa ‘three
dimensional’ (3D) yaani, urefu, upana na kimo. Chochote chenye zaidi ya 3D
hatuwezi kukiona. Mazingira ambayo kuna
zaidi ya 3D yanafahamika kama ‘hyperspace’ au ‘hyperdimensional’. Ni vigumu mno
na ngumu sana kwa mtu wa kawaida kuweza kuingiza kwenye akili yake na ‘kupiga
picha’ kwenye ubongo ya namna ulimwengu wenye zaidi ya 3D unavyo onekana.
Mathalani tunapo zungumzia ‘two dimensional’ (2D) tunakuwa na ‘upana’ na
‘urefu’ tu. Tuashumu kuna ulimwengu wa kufikirika wa 2D ambapo kuna viumbe wanaishi kwenye
ulimwengu huo. Ni wazi kuwa kile ambacho wanaweza kuona na kuhusu viumbe hawa
ni kile tu ambacho kitakuwa kwenye 2D. Tuashumu kinakuja kiumbe kutoka kwenye
ulimwengu wa 3D na hapo kiumbe hichi kinachomeka kidole chake kwenye ulimwengu
wa 2D. Kile ambacho viumbe wa ulimwengu wa 2D watakacho ona si kidole bali
duara, kwani uwezo wao wa kutambua kitu umesimamia kwenye ‘urefu’ na ‘upana’
hamna ‘kimo’ .Duara hilo (kidole) hicho kitaonekana kuwa kimetokea ghafla
kusiko julikana na pia kupotelea kusiko julikana. Lakini ni kuwa mwenye kidole
hicho anaweza kuwatisha na kuwasumbua wa kazi wa 2D kwa vile tu yeye ana 3D.
Anaweza kukitoa hapo na kukipeleka sehemu nyingine yoyote apendayo katika
ulimwengu wa 2D kwa tabia na sifa ambazo kwenye ulimwengu huo ni kitu ambacho
hakiwezekani.
Tunapolitazama suala la UFO leo hii ambapo mfumo wa mawasiliano na vyombo
vya habari umewafungua kwa kiasi fulani walimwengu kuhusiana na elimu ya anga
na uwezekano wa kuwepo viumbe wengine nje ya dunia yetu, katika ulimwengu wa
leo ambao mambo ya ‘New Age’ na imani
yake inakaribia kuchukua nafasi ya imani za kidini kwa baadhi ya dini na
madhehebu, suala la UFO nalo lina waumini wake wanaolikubali kiimani zaidi
kuliko . Hivyo kuliachia suala la UFO kwenye ulingo wa teknolojia peke yake
bado hatutakuwa tumelitendea haki.
Tukiacha upande wa sayansi na tekinolojia au ‘bati na nondo’, UFO kwa
baadhi ya wachambuzi ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko uhalisia wa kitu
chenyewe. Wachambuzi hao wana simamia kuwa
suala la UFO ni hitajio la kisaikolojia ambalo limetengenezwa na maono ya mtu
binafsi au imani yake na kutimilizwa na ubongo wake. Ubongo kama ulivyo na
ufanyaji kazi yake ni fumbo ambalo utatuzi wake bado umbali sana kutatuliwa.
Kile ambacho tunacho kifahamu kuhusiana na ubongo, hasa kwa kutegemea kile
ambacho tuna pata kupitia mitaala iliyopo kwenye ngazi mbalimbali zilizopo
katika mfumo wetu wa elimu ni kidogo sana.
Ubongo si mada kuu hapa hivyo nachilia kukutwika maelezo ambayo yatakutoa
nje ya somo letu, hivyo kwa wakati wako binafsi kajifunze hilo, isipokuwa ubongo unaweza kukuletea au kukutengeneza
umbo la kitu au kiumbe kilichopo kwenye 3D na kikasimama mbele yako. Mathalani
nimepata kusoma maandishi ya mtu mmoja aliye dai kuwa yeye binafsi
amekwenda ‘mbinguni’ na kukanyaga aridhi
yake aliyo sema ni dhahabu tupu na waka shikana
mikono na Yesu. Lakini pia nimepata kusikia mfano wa hayo kutoka kwa watu
mbalimbali. Leo kwenye fukuto la ’New Age’ hadithi kama hizo zinajaza maelfu ya
vitabu, lakini je, zina beba ukweli wowote wa msingi?
Jibu ni hapana.
Lakini kuliweka sua la UFO kwenye
uchambuzi wa kisaikolojia peke yake pia unashindikana kutokana na kwamba baadhi
ya UFO zilizo pata rikodiwa kuna zile ambazo zilizo dondoka au dondoshwa na
makombora na baadhi ya masalio yake kuokotwa kwa ajili ya uchambuzi na
kumbukumbu.
Tunaweza kusema kuwa UFO na viumbe wanao vimiliki vyombo hivyo wanatokea
katika Hyperdimensional. Lakini swali ni moja tu, je kuna viumbe wengine kwenye
hiyo hyperdimensional, je wapo viumbe wengine katika sayari za mbali, nyota au
kwenye galaxy?
Katika zama zetu hii leo ‘zama za
sayansi na teknolojia’ na sakata la kuwepo kwa viumbe wengine huru ni suala
ambalo limekuwa likielezewa zaidi na filamu za Hollywood kuliko kwenye maabara
za sayansi hiyo. Ni suala ambalo limeandikwa sana kwenye hadithi za kufikirika
kuliko vitabu rejea vya mashuleni. Ni suala ambalo halijathibitishwa rasmi
katika maeneo karibu yote ya hatua
mbalimbali za mifumo mbalimbali ya elimu tuliyo nayo. Zaidi ya maelfu kama siyo
mamilioni ya filamu na tamthilia kutoka maeneo mbalimbali ya dunia zinazo
elezea juu ya kuwepo kwa viumbe hao, mamilioni ya nakala zikiwemo vitabu na
makala zenye maudhui ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia juu ya kuwepo kwa
viumbe hao, hakuna ukweli wa msingi uliothibitishwa rasmi na vyombo huru
vinavyo tegemewa kwenye fani hiyo hasa ya elimu ya anga juu ya kuwepo kwa
viumbe hao.
Ni suala ambalo limemeza fikra na
mitazamo ya watu hasa katika karne hii, na hivyo inaniwia vigumu binafsi
kulipinga kwa aya moja tu hapo juu, lakini hata hivyo fikra na mitazamo hiyo
juu ya kuwepo kwa viumbe hao huru kama binadamu haijasimamia kokote zaidi ya
kwenye ulimwengu wa filamu, katuni, tamthilia na vitabu vyenye hadithi za
kufikirika zaidi.
Karibu kila filamu, tamthilia au
kipindi cha luninga kinacho zungumzia kuhusu ujio wa viumbe kutoka nje ya
sayari yetu, utakuta kiongozi wakazi hiyo ni Freemasons. Mathalani Close Encounters of the Third Kind, ET,
Taken, Alien 14, Independence Day, 2001: Space Odyssey, Star Wars, Star Trek,
Men In Black, From the Earth to the Moon, Apollo 13, War of the Worlds, na
XFiles.
Gene Roddenberry, mtengenezaji wa Star Trek alikuwa ni Freemasons wa daraja
la 33. Hii ndiyo sababu ya kuwepo kwa alama nyingi za kimasoni kwenye filamu
hiyo. George Lucas. mtengenezaji wa Star War naye alimimina alama na nembo
nyingi za kimasoni kwenye kazi yake hiyo.
Alama hizo za kishetani na kimasoni kwenye kazi zao mbalimbali zinazo
patikana katika ulimwengu wa burudani, zinaeleweka vyema kwa wafuasi wa taasisi
hizi za kishetani kuliko kwa watazamaji na wasikilizaji wa kawaida ambao kwa
wao zinabaki kama fumbo lisilo na mtatuzi. Hata hivyo nembo na alama hizo
zinalenga kabisa kupandikiza maudhui hayo ya kishetani na kimasoni katika hatua
mbalimbali za maisha yetu na katika harakati mbalimbali za kila siku za maisha
yetu. Zinalenga kutufanya tuwaze, kufikiri na kutenda kama wanavyo taka maadui
zetu na watawala wao bila sisi wenyewe kufahamu.
Spielberg ambaye pia alikuwa ni mtengenezaji mkuu wa Men in Black II,
filamu inayo zungumzia serikali ya siri ambayo kazi yake kubwa ni kuwalinda
watu kutokana na kitisho cha viumbe kutoka nje ya dunia. Februari 1997 shirika
la filamu Uingereza lilivujisha habari kwamba Spielberg na viongozi wenzake wa
Dream Works kwa siri walikutana na viongozi
wa Pentagon ndani ya Los Angeles. Viongozi hao walimuambia ‘acha kila
kitu’ na atengeneze filamu ambayo maudhui yake yatakuwa yanahusu vimondo.
Mwaka mmoja baadaye filamu ya Deep Impact ilitengenezwa. Filamu ambayo
inazungumzia vimondo vinavyo anguka kwenye uso wa dunia yetu. Ni akina nani hao
viongozi wa Pentagon na kwa nini walikuwa na hamu kubwa kwa Spielberg
kutengeneza filamu inayo zungumzia kitisho kutoka nje ya dunia?
Spielberg amehudhuria mkutano wa asasi ya siri ya Bilderberg wa mwaka 1999
na mikutano mingine ya asasi hiyo. Disemba ya mwaka 2002, mtandao wa luninga wa
SciFi ulionesha dokumentari, zilizomo kwenye utaratibu wa wa miniseries ya masaa 20, ambazo zililenga
kuonesha uvamizi wa viumbe toka nje ya sayari yetu wakiwateka binadamu. Gharama
za utengenezaji wa kazi hiyo ilifikia dola za Marekani Milioni 120 na kuifanya
kuwa ni moja ya miniseries yenye gharama kubwa sana kupata kutengenezwa.
Unaweza kudhani kuwa Spielberg kwa sasa amechoka na kutengeneza kazi za namna
hii. Lakini mabwana wakubwa waliomshika akili yake kiukweli wanayo hamu kubwa
sana ya kuona fikra hizi za kuwa kuna viumbe wengine nje ya sayari yetu (na
ambao ni hatari mno na wanao weza kutuvamia na kutushambulia na
kutusambaratisha kabisa tusipo ungana, kuwa fikra hizi zinaingia kwenye akili
za watu na kuwa ni sehemu ya maisha yao ya kila siku).
Kwa hivi sasa wale watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wao wakiwa ni
vijana, na wale wenye matumizi ya kutumia barua pepe, na wale wanao shusha
huduma mbalimbali kutoka kwenye mitandao ya intaneti wataona kabla hawajafanya
yoyote kati ya hayo kuna hatua ya kujisajili ambayo kwanza lazima uipitie,
katika hatua hiyo kuna mahala ambapo utatakiwa kuingiza aina fulani ya herufi
na tarakimu ambazo ziime changanywa na kutakiwa kuziingiza kwa usahihi. Unajua
ni kwa nini unatakiwa kuingiza namba na tarakimu hizo? Kwa sababu wanataka
kuhakikisha anayetaka kutumia huduma hiyo ni binaadamu. Nambari hizo na
tarakimu kwa namna zilivyo andikwa zitatambuliwa na binadamu tu, hivyo ndivyo
wanavyo sema. Sasa jiulize ni nani atakayetumia huduma hii ya kompyuta na
intaneti zaidi ya binadamu? Wanadhibiti viumbe kutoka nje ya sayari yetu ambao
inasemekana tayari wapo na wanaishi na sisi katika dunia yetu hii ya tatu
kutoka kwenye jua ndani ya galaxy ya Milkway, wasitumie huduma hizi za
mawasiliano kwa sababu mbalimbali. Lakini je ni kweli wapo?
Itaendelea Inshallah ....
hii mada ni ngumu sana kuielewa hususani sisi ambao hatukuenda shule sana. lakini mkuu umeelezea vizuri kwa kiasi kikubwa sana , naomba nikupongeze na kukushukuru na kukutakia kila la heri .
ReplyDelete