“Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi,
basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka (uwezo wa kufanya hivyo).”
“Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?” Qur’an 55: 33-34
“Ukweli wowote ni rahisi kufahamika pale unapopatikana, nukta ya msingi ni
kuupata” - Galileo Galilei
Mbio za angani katika zama ambazo binadamu ataikanyaga sayari nyingine nje
ya orbit ya dunia, na tukio hilo litashuhudiwa na kusikilizwa na mamilioni ya
watu. Lakini ni kweli binaadam amefika mwezini?
Zama hizo ushindani wa nani ataliteka anga baina ya mataifa makubwa ulikuwa
hauna mfano.
Mabilioni ya dola yalitumika kuhakikisha ushindi baina ya mataifa hayo.
Umoja wa Kisovieti walikuwa ni wa kwanza kutuma satelaiti kwenye obirt ya dunia, halafu mnyama; mbwa,
halafu binaadam.
Mwezi mmoja kabla Marekani hawajarusha Appolo
11 Mungano wa Kisovieti walirusha chombo kisicho kuwa na mtu mpaka mwezini
kwenda kuchukua mchanga kutoka kwenye mwezi wenyewe, chombo hicho kisingeanguka vibaya kwenye uso wa mwezi, basi jiwe la
kwanza kutoka nje ya sayari yetu, kutoka mwezini lingeletwa duniani na Umoja wa
Kisovieti. Hivi ndivyo kasi ya kuliteka anga ilivyokuwa siku hizo.
Binaadam hakatai kuwepo kwa Mungu Mmoja mpaka pale kiburi chake kinapokuwa
na kukomaa, mara nyingi kiburi hicho hutokana na vitu vya kuonekana alivyo
ruzukiwa binaadam na huyo Mungu anayemkataa, lakini kiburi hicho hakiishi hapo,
binaadam huyu hufikia kujiita kuwa yeye ni mungu, lakini hilo halitoshi binaadam
huyu hutaka kupambana hata na Mungu Aliyetukuka mwenyewe.
Hili tumeliona vema kwenye historia za watu wa zama zilizo pita na watu wa
zama zetu vilevile.
Kutoka Babyloni zama hizo ambazo hata ilikuwa ni milenia gani bado
haifahamiki, kiburi kilipozidi wakazi wa jiji hilo walisema wajenga mnara mrefu
kufika mbinguni, watengeneze jina na hata wamuone huyo Mungu Mmoja wapambana
naye. Mnara ule haukukamilika.
Egypt kwa mfalme wa mapiramidi, ambayo aliyarithi kutoka kwa viumbe wasio
fahamika (mashetani), kiburi chake kilivuka mpaka naye akajiita ni mungu
aliyetukuka, alimaliziwa baharini na ajabu Mungu Aliyetukuka alimtoa na
akamkausha na mwili wake akauweka kwenye jumba la makumbusho kwa kila mtu
kuona, na zaidi iwe ni somo kwa vizazi vyote na hasa wale wenye maono kama ya
Firauni.
Lakini hiyo haikutosha majuzi tu, binaadam alitengeneza meli kubwa;
Titanic, wakasema hata Mungu mwenyewe hawezi kuizamisha, haikumaliza safari
yake ya kwanza, ilizama au kwa uwazi zaidi ilizamishwa.
Katika zama za mashine palipo zaliwa mbio za kwenda angani, kiburi cha binaadam
hakijaisha, wala kujifunza chochote kutoka kwa vizazi vilivyo tangulia. Binaadam
anataka kwenda mwezini na kurudi pasina mashaka, akiwa salama. Lakini chombo
walicho kitumia walikiita Apollo 11.
Apollo ni jina la mungu wa kipagani katika dola ya Roma, nambari 11 ni
namba ya kishetani na maana yake kuu ni ‘afananaye na Mungu’ yaani namba moja
(1) ni namba ya Mungu Mmoja tu, lakini kwenye taaluma ya kishetani namba hiyo
ukiipangwa na nambari moja (1) nyingine na kutengeneza 11 basi hiyo iliyo
ongezeka inamaanisha mmoja afananaye na Mungu, yaani shetani mwenyewe, au
mpinga Kristo ambaye naye anajifananisha na Kristo (Yesu) (Jay-Z Hip Hop Master Mason. (Exposed)).
Lakini chombo kilicho tumika kuisukuma Apollo 11 kinaitwa Sartun, jina
ambalo Kilatini ni Shetani.
Mpango mzima ulianza mwaka 1961 na kumalizika mwaka 1972 kwa hivyo ulidumu
kwa miaka 11! Wanaanga wote wa mwanzo kwenda mwezini walikuwa ni Freemasons na
wengine picha zao zimebandikwa katika mahekalu ya kimasoni, yafuatayo ni baadhi
tu ya majina ya wanaanga ambao ni Freemasons na walifanya safari za kwenda
angani ikiwemo mwezini, kwenye mabano ni jina la chombo kilicho tumika kwenye
safari hiyo.
Buzz Aldrin Jr. (Apollo 11), Gordon Cooper Jr., (Mercury 9, Gemini 5), Donn Eisele (Apollo 7), John Glenn Jr., (Mercury 6), Virgil Grissom (Apollo 1&15, Mercury 5, Gemini 3), James Irwin (Apollo 15), Edgar Mitchell (Apollo 14), Walter Schirra Jr. (Apollo 7, Sigma 7, Gemini 6, Mercury 8), Thomas Stafford (Apollo 10&18, Gemini 7&9) na Paul Weitz (Skylab 2, Challenger). (Eric Dubay ‘The Atlantean
Conspiracy-Exposing the Illuminati from Atlantis to 2012)
Tukio zima lilikuwa ni la kiibada za kishetani na kipagani zaidi kuliko
ulimwengu ulivyo fahamu. Hivyo Mungu wa kipagani aitwaye Apollo aliyepewa
heshima ya kufanana na Mungu kwa kuongezea namba 11 kwenye jina lake anasukumwa
kwenda mwezini na Shetani mwenyewe. Je Apollo alifika?
Ilipofika 4:17 p.m EST Julai 20, 1969, Apollo 11 ilitua kwenye uso wa jirani
yetu wa karibu, Mwezi, kwa mara ya kwanza binadamu akaweka mguu wake kwenye
dunia nyingine kabisa, mwezini. Neil Armstrong, binadamu wa kwanza kuweka mguu
wake kwenye uso wa mwezi akasema maneno maarufu, ‘One small step for man, one giant leap for
mankind.’
Muungano wa Kisovieti walianza mbio hizi mapema zaidi, wakiweka rekodi moja
baada ya nyingine. Lakini karibu miaka 3 na nusu baadaye tangu Umoja wa
Kisovieti ulipoanza mbio hizo, raisi John F. Kennedy akaweka hadharani tangazo
lake ambalo wengi walilichukulia kama ni kichekesho, alisema Marekani
imeanzisha mradi ambao utampeleka binadamu mwezini na kumrudisha duniani salama
kabla ya mongo huo kumalizika.
Miaka kadhaa baada ya tangazo la
Kennedy, wazo la kwamba Marekani itafanikiwa kumpeleka binaadam mwezini kabla
ya Umoja wa Kisovieti lilizidi kuonekana ni kituko, kwani teknolojia ya Umoja
huo kwenye elimu ya anga ilikuwa ni kubwa kushinda ile ya Marekani na walikuwa
wakiweka rekodi moja baada ya nyingine kwenye mbio hizo.
Lakini walikuwa ni Marekani walio kuwa wa kwanza kuweka rekodi ya pekee,
kumpeleka binadamu mwezini na kumrudisha akiwa hai. Umoja wa Kisovieti mbio zao
ziliishi kwenye Orbit ya dunia na kukipeleka chombo kisicho kuwa na mtu mwezini
ambacho nacho hakikurudi, hata kidogo hawakuonekana kama walikuwa na mpango wa
kumpeleka binaadam mwezini. Julai 20, 1969, ndoto ya kufikirika ya Marekani
ikawa ni kweli, baada ya miaka 8 na kutumia gharama zilizo fika $24,000,000,000
hatimaye Apollo 11 ilitua mwezini.
.jpg)
Umoja wa Kisovieti ulihuzunika kwa kushindwa mbio hizo, Red China waliita
tukio zima ni uwongo mtupu na danganya toto, lakini dunia nzima ilisherehekea,
na kila Mmarekani alijivunia kuwa Mmarekani. Halafu ghafla Marekani ikachana na
mradi huo, walisema wanajaribu kuokoa pesa, wamesha peleka vyombo sita mwezini
na kurudi salama, safari tatu za mwisho zilikuwa na tija nzuri na mafanikio
makubwa kushinda zote. Juu ya yote kila mtu alijua Marekani wamefanikiwa kwenda
mwezini, na kuokota vijimawe kadhaa kwa ajili ya maabara.
Ndugu yangu! Hivyo ndivyo tulivyo ambiwa, lakini hicho sicho kilicho tokea!
Ha haha ha! Kucheka ni afya bwana wacha ni cheke kwa raha zangu.
Kwa miaka mingi sasa kumekuwa na maswali yasiyo na majibu kuhusiana na
safari hiyo na ikiwa kweli kama binaadam ameukanyaga mwezi? Idadi ya waandishi
na watafiti huru na wale wadadisi wa mambo na idadi kubwa ya Wamarekani wenyewe
ni kuwa, hatukuenda mwezini.
Miaka ishirini baada ya mradi wa kwenda mwezini kufungwa, na mwaka mmoja
nyuma ya ratiba, NASA na kitengo chake cha anga hakikuweza kuweka kwenye Orbit
ya dunia mtambo wa teleskop wenye kamera ya uhakika. Lakini miongo miwili
kabla, mradi kamambe, mradi mgumu mara 100 kushinda ule wa kuweka teleskop
kwenye Orbit ya dunia, ulifanikiwa kwa asilimia mia moja. (The Funny Thing
Happened On The Way To The Moon)
Marcus Allen mchapishaji wa jarida la Nexus ana wasiwasi ikiwa binaadam
alifikika mwezini, anasema;
“Kwenda mwezini kiuhakika siyo tatizo kubwa, Urusi
ilifanya hivyo mwaka 1959, ambalo ni tatizo kubwa ni kuwapeleka watu hapo.” (Jim Marrs ‘ABOVE TOP SECRET’ - Uncover the Mysteries of the
Digital Age)
Ni wendawazimu nadhani haikuingii akilini na wala haileti maana kitu
ambacho umeambiwa na kuambiwa, ukahadithiwa na kupata ushahidi wa kila namna
mpaka mwisho ukaamini nawe ukawa nabii mzuri wa imani hiyo kwa kuwaambia
wengine kuwa Binaadam ameukanyaga Mwezi.
Leo unatakiwa kuachana na imani hiyo kuwa haikuwa ya kweli na ulilokuwa
ukijivunia kama maendeleo na mafanikio ya hali ya juu kabisa kwa binaadam
kukanyaga mwezini hayajapata kutokea. Lazima ikuchanganye.
Lakini kwa nini isikuchanganye ikiwa
wewe haukuelewa kabisa suala la kwenda mwezini isipokuwa ulichofanya ni kuamini
baada ya kuambiwa, kusimuliwa na kusoma kutoka kwa watu na vyombo vya habari
ambavyo wewe unaviamini mia kwa mia na wala hukuwa na haja ya kuuliza swali
lolote kuhusiana na tukio zima, hivyo ukaamini, kama ambavyo ulivyoamini nadharia
ya kuwa wewe ulikuwa ni nyani, Ukimwi unatokana na Green Monkey, Osama ndiyo
kalipua WTC, na mengine mengi.
Sasa nataka kukibadilisha kile
ulichokuwa unakiamini lakini tafadhali safari hii sitaki uamini nataka uelewe
kwa kutumia uwezo wako wa ufahamu uliopewa na Muumba wako. Kuamini ni suala
linalo kuja mwisho kabisa baada ya kuuzuia uwezo wako wa kufahamu kufanya kazi
yake kadiri uwezavyo kinachofuata ni
kuamini na ukisha amini hutauliza swali utafuata tu kila unachoambiwa na wewe
hutakuwa huru tena, bali mtumwa anayelaghaiwa kuwa yuko huru.
.jpg)
Tuanze na Umoja wa Kisovieti. Propaganda za Umoja wa Kisovieti kuhusu
safari za anga ulirushwa kwa nguvu sana na nchi za kikomunisti kama vile
Hungary, Estonia, na Poland. Kila mmoja aliamini habari hizi kuwa afisa wa Jeshi
la Anga la Soviet Yuri Gagarin alikwenda kwenye anga na kuifikia Orbit ya
dunia kama zilivyo aminiwa na kukubaliwa zile za washindani wenzake; Marekani.
Nchi nyingi za Kimagharibi zilifahamu Umoja wa Kisovieti ulikuwa unarusha
propaganda, lakini ofisa wao wa anga hakufanya safari ya anga lakini hili
hawakutaka kulizungumzia. (Juri Lina ‘
Archtect s of Deception’)
Mpaka mwaka 1961 Marekani ilikuwa imeshapeleka setelaiti 42 kwenye anga
wakati Muungano wa Kisovieti ulipeleka satelaiti 12 tu, Marekani ikauwambia
ulimwengu kuwa mwana anga wao Alan Shepard atasafiri kwenda kwenye anga mnamo
mwezi Mei 1961, hali hii ikawa inalazimisha Muungano wa Kisovieti ulifanya kitu
ili kuokoa sura yao kutokana na upinzani unaoletwa na Marekani.
Ilipofika Aprili 7, mwaka 1961 Muungano wa Kisovieti ikamtuma mwana anga
wao Vladimir Ilyushin kwenda kwenye anga. Safari haikufanikiwa na wakati wa
kutua Ilyushin alipata majeraha makubwa kutokana na kuwa chombo chake
kilishindwa kutua kama ilivyo pangwa. Ikasemwa kuwa amepata ajali ya gari na
hivyo akapelekwa China kwa ajili ya matibabu zaidi.( Juri Lina ‘ Archtect s of
Deception’)
Gagarin hakuwahi hata kupiga picha alipokuwa katika anga, alipoulizwa
katika mahojiano ya luninga akadai kuwa hakuwa amebeba kamera, ajabu sana hata
chombo chake hakikuwa na kamera pia? Katika safari muhimu na ya heshima kubwa
kwenye historia ya maendeleo ya Binaadam wasahau kitu muhimu kama kamera ni
kweli hilo linaingia akilini?
Gazeti moja liitwalo Sovetskaya Rossiya lilidai kuwa Gagarin alivaa suti ya
angani ya rangi ya bluu, lakini katika mahojiano Gagarin akasema alivaa ya
rangi ya chungwa. Katika mahojiano hayo Gagarin alikuwa anajibu maswali kwa
kutegemea dondoo alizo andikiwa na pia akisaidiwa na wataalam kadhaa
waliomzunguka lakini juu ya yote hayo bado alikuwa akikosea kujibu maswali hayo
kinyume na alivyotarajiwa kama mtu aliyekwenda angani.
Alidai kuwa kutokuwepo na nguvu za mvutano angani hilo halikuwa tatizo kila
kitu kilikuwa kama kawaida, lakini ni uwongo mwana anga wa Kijerumani bwana
Titov alipojaribu kufanya safari kama hiyo hali hiyo ilimsumbua na baadaye
alipata maradhi ya moyo, tatizo ambalo pia walilipata wana anga wa Kimarekani.
Kabla ya hadithi ya Gagarin kuchapishwa wanaanga kadhaa wa Kirusi walisha tumwa
kwenye safari kama yake na wengi walikufa lakini hili halikusemwa mpaka mwaka
2001.
.jpg)
Baada ya majaribio ya muda mrefu mnamo mwaka 1961 ndoto ikatimia, hivi
ndivyo ilivyoelezewa, ndoto ya binaadam kutembea juu ya mwezi. Lakini nyuma ya
mapazia mahala fulani kwenye uso wa dunia mchezo wa kuigiza ulikuwa unaendelea
chini ya ulinzi na siri kubwa, picha zilipigwa, filamu zikarekodiwa na vyombo
vizito kiubora wakati huo na hatimaye muda ulipofika ‘mchezo’ huo wa kuigiza
ukazinduliwa rasmi ukarushwa moja kwa moja na vyombo vikubwa vya habari
duniani, vyombo vyao, mamilioni wakitizama na kusikiliza redioni, hatua kwa
hatua binaadam ‘akiukanyaga’ mwezi na Apollo 11.
Ilikuwa ni hatua ndogo ya maendeleo ya Sayansi na elimu ya anga na uwongo
mkubwa kwenye historia ya binaadam.
Ajabu mpaka leo mamilioni ya watu wanaushikilia uwongo huu.
Majina, vituo vilivyo tajwa, maeneo waliyoshukia vinahusiana na alama,
nembo, ibada na mila za dini yao ya siri dini ya kishetani. Lakini hivi sivyo
vinavyo pelekea tuwe na mashaka na safari hiyo lakini vina nafasi kwenye
walakini huo.
Kwa sasa tunaona harakati za kwenda mwezini zimefifia kabisa, umewahi
kujiuliza ni kwa nini? Ni kwa sababu ni vigumu kuendelea na mpango huo bila
kugundua vitu vipya na vipi watagundua ikiwa hawajafika na pia kuna uwezekano wameishiwa na picha pamoja na filamu
hivyo hawana jipya.
TUKUTANE TENA HAPA TUICHAMBUE KINAGAUBAGA SAFARI NZIMA YA MWEZINI ... HIYO
ILIKUWA NI INTRO ....
Mbona kuna mataifa mengine kama china yanadai bado yanaenda mwezin
ReplyDeleteUkiacha Marekani hakuna taifa jingine lolote duniani lililokuja na UWONGO huo kwamba limpeleka binadamu mwezini. Usichanganye safari ya kwenda mwezini na TAFITI ZA KUTUMA VYOMBO ANGANI HUSUSAN KWENYE ORBIT YETU. HIVYO YATIZAME MADAI YAKO VIZURI KABLA YA KUYAANDIKA.
DeleteUkiacha Marekani hakuna taifa jingine lolote duniani lililokuja na UWONGO huo kwamba limpeleka binadamu mwezini. Usichanganye safari ya kwenda mwezini na TAFITI ZA KUTUMA VYOMBO ANGANI HUSUSAN KWENYE ORBIT YETU. HIVYO YATIZAME MADAI YAKO VIZURI KABLA YA KUYAANDIKA.
DeleteOky nimekuelewa sasa mbona habari ya malaysia air way hujatumalizia kaka
Deletehii makala safari ya mwezini unaweza kunitumia
ReplyDelete