Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Thursday, December 11, 2014

HATUKWENDA MWEZINI ...

“Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka (uwezo wa kufanya hivyo).”
“Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?” Qur’an 55: 33-34

“Ukweli wowote ni rahisi kufahamika pale unapopatikana, nukta ya msingi ni kuupata” - Galileo Galilei



Mbio za angani katika zama ambazo binadamu ataikanyaga sayari nyingine nje ya orbit ya dunia, na tukio hilo litashuhudiwa na kusikilizwa na mamilioni ya watu. Lakini ni kweli binaadam amefika mwezini?


Zama hizo ushindani wa nani ataliteka anga baina ya mataifa makubwa ulikuwa hauna mfano.
Mabilioni ya dola yalitumika kuhakikisha ushindi baina ya mataifa hayo. Umoja wa Kisovieti walikuwa ni wa kwanza kutuma satelaiti kwenye obirt ya dunia, halafu mnyama; mbwa, halafu binaadam.



Mwezi mmoja kabla Marekani hawajarusha Appolo 11 Mungano wa Kisovieti walirusha chombo kisicho kuwa na mtu mpaka mwezini kwenda kuchukua mchanga kutoka kwenye mwezi wenyewe, chombo hicho kisingeanguka vibaya kwenye uso wa mwezi, basi jiwe la kwanza kutoka nje ya sayari yetu, kutoka mwezini lingeletwa duniani na Umoja wa Kisovieti. Hivi ndivyo kasi ya kuliteka anga ilivyokuwa siku hizo.

Binaadam hakatai kuwepo kwa Mungu Mmoja mpaka pale kiburi chake kinapokuwa na kukomaa, mara nyingi kiburi hicho hutokana na vitu vya kuonekana alivyo ruzukiwa binaadam na huyo Mungu anayemkataa, lakini kiburi hicho hakiishi hapo, binaadam huyu hufikia kujiita kuwa yeye ni mungu, lakini hilo halitoshi binaadam huyu hutaka kupambana hata na Mungu Aliyetukuka mwenyewe.


Hili tumeliona vema kwenye historia za watu wa zama zilizo pita na watu wa zama zetu vilevile.
Kutoka Babyloni zama hizo ambazo hata ilikuwa ni milenia gani bado haifahamiki, kiburi kilipozidi wakazi wa jiji hilo walisema wajenga mnara mrefu kufika mbinguni, watengeneze jina na hata wamuone huyo Mungu Mmoja wapambana naye. Mnara ule haukukamilika.

Egypt kwa mfalme wa mapiramidi, ambayo aliyarithi kutoka kwa viumbe wasio fahamika (mashetani), kiburi chake kilivuka mpaka naye akajiita ni mungu aliyetukuka, alimaliziwa baharini na ajabu Mungu Aliyetukuka alimtoa na akamkausha na mwili wake akauweka kwenye jumba la makumbusho kwa kila mtu kuona, na zaidi iwe ni somo kwa vizazi vyote na hasa wale wenye maono kama ya Firauni.


Lakini hiyo haikutosha majuzi tu, binaadam alitengeneza meli kubwa; Titanic, wakasema hata Mungu mwenyewe hawezi kuizamisha, haikumaliza safari yake ya kwanza, ilizama au kwa uwazi zaidi ilizamishwa.

Katika zama za mashine palipo zaliwa mbio za kwenda angani, kiburi cha binaadam hakijaisha, wala kujifunza chochote kutoka kwa vizazi vilivyo tangulia. Binaadam anataka kwenda mwezini na kurudi pasina mashaka, akiwa salama. Lakini chombo walicho kitumia walikiita Apollo 11.



Apollo ni jina la mungu wa kipagani katika dola ya Roma, nambari 11 ni namba ya kishetani na maana yake kuu ni ‘afananaye na Mungu’ yaani namba moja (1) ni namba ya Mungu Mmoja tu, lakini kwenye taaluma ya kishetani namba hiyo ukiipangwa na nambari moja (1) nyingine na kutengeneza 11 basi hiyo iliyo ongezeka inamaanisha mmoja afananaye na Mungu, yaani shetani mwenyewe, au mpinga Kristo ambaye naye anajifananisha na Kristo (Yesu) (Jay-Z Hip Hop Master Mason. (Exposed)).

Lakini chombo kilicho tumika kuisukuma Apollo 11 kinaitwa Sartun, jina ambalo Kilatini ni Shetani.



Mpango mzima ulianza mwaka 1961 na kumalizika mwaka 1972 kwa hivyo ulidumu kwa miaka 11! Wanaanga wote wa mwanzo kwenda mwezini walikuwa ni Freemasons na wengine picha zao zimebandikwa katika mahekalu ya kimasoni, yafuatayo ni baadhi tu ya majina ya wanaanga ambao ni Freemasons na walifanya safari za kwenda angani ikiwemo mwezini, kwenye mabano ni jina la chombo kilicho tumika kwenye safari hiyo.

 Buzz Aldrin Jr. (Apollo 11), Gordon Cooper Jr., (Mercury 9, Gemini 5), Donn Eisele (Apollo 7), John Glenn Jr., (Mercury 6), Virgil Grissom (Apollo 1&15, Mercury 5, Gemini 3), James Irwin (Apollo 15), Edgar Mitchell (Apollo 14), Walter Schirra Jr. (Apollo 7, Sigma 7, Gemini 6, Mercury 8), Thomas Stafford (Apollo 10&18, Gemini 7&9) na Paul Weitz (Skylab 2, Challenger). (Eric Dubay ‘The Atlantean Conspiracy-Exposing the Illuminati from Atlantis to 2012)


Tukio zima lilikuwa ni la kiibada za kishetani na kipagani zaidi kuliko ulimwengu ulivyo fahamu. Hivyo Mungu wa kipagani aitwaye Apollo aliyepewa heshima ya kufanana na Mungu kwa kuongezea namba 11 kwenye jina lake anasukumwa kwenda mwezini na Shetani mwenyewe. Je Apollo alifika?

Ilipofika 4:17 p.m EST Julai 20, 1969, Apollo 11 ilitua kwenye uso wa jirani yetu wa karibu, Mwezi, kwa mara ya kwanza binadamu akaweka mguu wake kwenye dunia nyingine kabisa, mwezini. Neil Armstrong, binadamu wa kwanza kuweka mguu wake kwenye uso wa mwezi akasema maneno maarufu, ‘One small step for man, one giant leap for mankind.’


Muungano wa Kisovieti walianza mbio hizi mapema zaidi, wakiweka rekodi moja baada ya nyingine. Lakini karibu miaka 3 na nusu baadaye tangu Umoja wa Kisovieti ulipoanza mbio hizo, raisi John F. Kennedy akaweka hadharani tangazo lake ambalo wengi walilichukulia kama ni kichekesho, alisema Marekani imeanzisha mradi ambao utampeleka binadamu mwezini na kumrudisha duniani salama kabla ya mongo huo kumalizika.


 Miaka kadhaa baada ya tangazo la Kennedy, wazo la kwamba Marekani itafanikiwa kumpeleka binaadam mwezini kabla ya Umoja wa Kisovieti lilizidi kuonekana ni kituko, kwani teknolojia ya Umoja huo kwenye elimu ya anga ilikuwa ni kubwa kushinda ile ya Marekani na walikuwa wakiweka rekodi moja baada ya nyingine kwenye mbio hizo.

Lakini walikuwa ni Marekani walio kuwa wa kwanza kuweka rekodi ya pekee, kumpeleka binadamu mwezini na kumrudisha akiwa hai. Umoja wa Kisovieti mbio zao ziliishi kwenye Orbit ya dunia na kukipeleka chombo kisicho kuwa na mtu mwezini ambacho nacho hakikurudi, hata kidogo hawakuonekana kama walikuwa na mpango wa kumpeleka binaadam mwezini. Julai 20, 1969, ndoto ya kufikirika ya Marekani ikawa ni kweli, baada ya miaka 8 na kutumia gharama zilizo fika $24,000,000,000 hatimaye Apollo 11 ilitua mwezini.

Umoja wa Kisovieti ulihuzunika kwa kushindwa mbio hizo, Red China waliita tukio zima ni uwongo mtupu na danganya toto, lakini dunia nzima ilisherehekea, na kila Mmarekani alijivunia kuwa Mmarekani. Halafu ghafla Marekani ikachana na mradi huo, walisema wanajaribu kuokoa pesa, wamesha peleka vyombo sita mwezini na kurudi salama, safari tatu za mwisho zilikuwa na tija nzuri na mafanikio makubwa kushinda zote. Juu ya yote kila mtu alijua Marekani wamefanikiwa kwenda mwezini, na kuokota vijimawe kadhaa kwa ajili ya maabara.

Ndugu yangu! Hivyo ndivyo tulivyo ambiwa, lakini hicho sicho kilicho tokea!

Ha haha ha! Kucheka ni afya bwana wacha ni cheke kwa raha zangu.

Kwa miaka mingi sasa kumekuwa na maswali yasiyo na majibu kuhusiana na safari hiyo na ikiwa kweli kama binaadam ameukanyaga mwezi? Idadi ya waandishi na watafiti huru na wale wadadisi wa mambo na idadi kubwa ya Wamarekani wenyewe ni kuwa, hatukuenda mwezini.

Miaka ishirini baada ya mradi wa kwenda mwezini kufungwa, na mwaka mmoja nyuma ya ratiba, NASA na kitengo chake cha anga hakikuweza kuweka kwenye Orbit ya dunia mtambo wa teleskop wenye kamera ya uhakika. Lakini miongo miwili kabla, mradi kamambe, mradi mgumu mara 100 kushinda ule wa kuweka teleskop kwenye Orbit ya dunia, ulifanikiwa kwa asilimia mia moja. (The Funny Thing Happened On The Way To The Moon)
Marcus Allen mchapishaji wa jarida la Nexus ana wasiwasi ikiwa binaadam alifikika mwezini, anasema;

“Kwenda mwezini kiuhakika siyo tatizo kubwa, Urusi ilifanya hivyo mwaka 1959, ambalo ni tatizo kubwa ni kuwapeleka watu hapo.” (Jim Marrs ‘ABOVE TOP SECRET’ - Uncover the Mysteries of the Digital Age)

Ni wendawazimu nadhani haikuingii akilini na wala haileti maana kitu ambacho umeambiwa na kuambiwa, ukahadithiwa na kupata ushahidi wa kila namna mpaka mwisho ukaamini nawe ukawa nabii mzuri wa imani hiyo kwa kuwaambia wengine kuwa Binaadam ameukanyaga Mwezi.



Leo unatakiwa kuachana na imani hiyo kuwa haikuwa ya kweli na ulilokuwa ukijivunia kama maendeleo na mafanikio ya hali ya juu kabisa kwa binaadam kukanyaga mwezini hayajapata kutokea. Lazima ikuchanganye.

 Lakini kwa nini isikuchanganye ikiwa wewe haukuelewa kabisa suala la kwenda mwezini isipokuwa ulichofanya ni kuamini baada ya kuambiwa, kusimuliwa na kusoma kutoka kwa watu na vyombo vya habari ambavyo wewe unaviamini mia kwa mia na wala hukuwa na haja ya kuuliza swali lolote kuhusiana na tukio zima, hivyo ukaamini, kama ambavyo ulivyoamini nadharia ya kuwa wewe ulikuwa ni nyani, Ukimwi unatokana na Green Monkey, Osama ndiyo kalipua WTC,  na mengine mengi.

 Sasa nataka kukibadilisha kile ulichokuwa unakiamini lakini tafadhali safari hii sitaki uamini nataka uelewe kwa kutumia uwezo wako wa ufahamu uliopewa na Muumba wako. Kuamini ni suala linalo kuja mwisho kabisa baada ya kuuzuia uwezo wako wa kufahamu kufanya kazi yake  kadiri uwezavyo kinachofuata ni kuamini na ukisha amini hutauliza swali utafuata tu kila unachoambiwa na wewe hutakuwa huru tena, bali mtumwa anayelaghaiwa kuwa yuko huru.

Tuanze na Umoja wa Kisovieti. Propaganda za Umoja wa Kisovieti kuhusu safari za anga ulirushwa kwa nguvu sana na nchi za kikomunisti kama vile Hungary, Estonia, na Poland. Kila mmoja aliamini habari hizi kuwa afisa wa Jeshi la Anga la Soviet Yuri Gagarin alikwenda kwenye anga na kuifikia Orbit ya dunia kama zilivyo aminiwa na kukubaliwa zile za washindani wenzake; Marekani. Nchi nyingi za Kimagharibi zilifahamu Umoja wa Kisovieti ulikuwa unarusha propaganda, lakini ofisa wao wa anga hakufanya safari ya anga lakini hili hawakutaka kulizungumzia. (Juri Lina ‘ Archtect s of Deception’)

Mpaka mwaka 1961 Marekani ilikuwa imeshapeleka setelaiti 42 kwenye anga wakati Muungano wa Kisovieti ulipeleka satelaiti 12 tu, Marekani ikauwambia ulimwengu kuwa mwana anga wao Alan Shepard atasafiri kwenda kwenye anga mnamo mwezi Mei 1961, hali hii ikawa inalazimisha Muungano wa Kisovieti ulifanya kitu ili kuokoa sura yao kutokana na upinzani unaoletwa na Marekani.

Ilipofika Aprili 7, mwaka 1961 Muungano wa Kisovieti ikamtuma mwana anga wao Vladimir Ilyushin kwenda kwenye anga. Safari haikufanikiwa na wakati wa kutua Ilyushin alipata majeraha makubwa kutokana na kuwa chombo chake kilishindwa kutua kama ilivyo pangwa. Ikasemwa kuwa amepata ajali ya gari na hivyo akapelekwa China kwa ajili ya matibabu zaidi.( Juri Lina ‘ Archtect s of Deception’)


Gagarin hakuwahi hata kupiga picha alipokuwa katika anga, alipoulizwa katika mahojiano ya luninga akadai kuwa hakuwa amebeba kamera, ajabu sana hata chombo chake hakikuwa na kamera pia? Katika safari muhimu na ya heshima kubwa kwenye historia ya maendeleo ya Binaadam wasahau kitu muhimu kama kamera ni kweli hilo linaingia akilini?

Gazeti moja liitwalo Sovetskaya Rossiya lilidai kuwa Gagarin alivaa suti ya angani ya rangi ya bluu, lakini katika mahojiano Gagarin akasema alivaa ya rangi ya chungwa. Katika mahojiano hayo Gagarin alikuwa anajibu maswali kwa kutegemea dondoo alizo andikiwa na pia akisaidiwa na wataalam kadhaa waliomzunguka lakini juu ya yote hayo bado alikuwa akikosea kujibu maswali hayo kinyume na alivyotarajiwa kama mtu aliyekwenda angani.

Alidai kuwa kutokuwepo na nguvu za mvutano angani hilo halikuwa tatizo kila kitu kilikuwa kama kawaida, lakini ni uwongo mwana anga wa Kijerumani bwana Titov alipojaribu kufanya safari kama hiyo hali hiyo ilimsumbua na baadaye alipata maradhi ya moyo, tatizo ambalo pia walilipata wana anga wa Kimarekani. Kabla ya hadithi ya Gagarin kuchapishwa wanaanga kadhaa wa Kirusi walisha tumwa kwenye safari kama yake na wengi walikufa lakini hili halikusemwa mpaka mwaka 2001.


Baada ya majaribio ya muda mrefu mnamo mwaka 1961 ndoto ikatimia, hivi ndivyo ilivyoelezewa, ndoto ya binaadam kutembea juu ya mwezi. Lakini nyuma ya mapazia mahala fulani kwenye uso wa dunia mchezo wa kuigiza ulikuwa unaendelea chini ya ulinzi na siri kubwa, picha zilipigwa, filamu zikarekodiwa na vyombo vizito kiubora wakati huo na hatimaye muda ulipofika ‘mchezo’ huo wa kuigiza ukazinduliwa rasmi ukarushwa moja kwa moja na vyombo vikubwa vya habari duniani, vyombo vyao, mamilioni wakitizama na kusikiliza redioni, hatua kwa hatua binaadam ‘akiukanyaga’ mwezi na Apollo 11.
Ilikuwa ni hatua ndogo ya maendeleo ya Sayansi na elimu ya anga na uwongo mkubwa kwenye historia ya binaadam. 

Ajabu mpaka leo mamilioni ya watu wanaushikilia uwongo huu.

Majina, vituo vilivyo tajwa, maeneo waliyoshukia vinahusiana na alama, nembo, ibada na mila za dini yao ya siri dini ya kishetani. Lakini hivi sivyo vinavyo pelekea tuwe na mashaka na safari hiyo lakini vina nafasi kwenye walakini huo.

Kwa sasa tunaona harakati za kwenda mwezini zimefifia kabisa, umewahi kujiuliza ni kwa nini? Ni kwa sababu ni vigumu kuendelea na mpango huo bila kugundua vitu vipya na vipi watagundua ikiwa hawajafika na pia  kuna uwezekano wameishiwa na picha pamoja na filamu hivyo hawana jipya.


TUKUTANE TENA HAPA TUICHAMBUE KINAGAUBAGA SAFARI NZIMA YA MWEZINI ... HIYO ILIKUWA NI INTRO .... 

5 comments:

  1. Mbona kuna mataifa mengine kama china yanadai bado yanaenda mwezin

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukiacha Marekani hakuna taifa jingine lolote duniani lililokuja na UWONGO huo kwamba limpeleka binadamu mwezini. Usichanganye safari ya kwenda mwezini na TAFITI ZA KUTUMA VYOMBO ANGANI HUSUSAN KWENYE ORBIT YETU. HIVYO YATIZAME MADAI YAKO VIZURI KABLA YA KUYAANDIKA.

      Delete
    2. Ukiacha Marekani hakuna taifa jingine lolote duniani lililokuja na UWONGO huo kwamba limpeleka binadamu mwezini. Usichanganye safari ya kwenda mwezini na TAFITI ZA KUTUMA VYOMBO ANGANI HUSUSAN KWENYE ORBIT YETU. HIVYO YATIZAME MADAI YAKO VIZURI KABLA YA KUYAANDIKA.

      Delete
    3. Oky nimekuelewa sasa mbona habari ya malaysia air way hujatumalizia kaka

      Delete
  2. hii makala safari ya mwezini unaweza kunitumia

    ReplyDelete