Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Sunday, September 21, 2014

IKO WAPI NDEGE YA MALYSIA MH 370? pt2


Ndege hiyo haijadondoka kokote pale, haijazama baharini, Kisanduku cheusi nacho kimakata mawasiliano yake ghafla, 

IMETOWEKA ANGANI.

NI VIPI NDEGE INAWEZA KUTOWEKA HEWANI?




Uwezekano mkubwa ni kwamba ndege hiyo imetekwa kwa njia ya Remote Control na kupelekwa kutua mahala ambapo mtekaji anataka itue.

Hakuna kingine chochote kinacho weza kuingia akilini kwamba ndege imetoweka kwenye anga na isifahamike ilipo.


Watafiti wengine wamefikia kusema ni wapi ndege hiyo ilipo sasa. Wanasema ipo kwenye kiwanja cha jeshi cha Marekani kilichomo sehemu fulani kwenye bahari ya hindi, mahala hapo panaitwa DIEGO GARCIA. Sina mpango wa kuelezea madai hayo hapa, labda wakati mwingine lakini mwenyewe kwa wakati wako unaweza kutembelea ukurasa huu na kujishibisha maelezo na kuyapima mwenyewe kama mwandishi yupo sahihi ama la, ukurasa ni






Labda swali la msingi sasa ni WHY?

Kwanini aliyenyuma ya mchezo huo aamue kufanya hivyo?
Ninacho ona mimi binafsi ni kwamba huo ni mwanzo wa vita vipya, au mwanzo wa adui mpya wa kutengenezwa.
Ninacho maanisha hapa ni hichi,

Utakumbuka kipindi fulani kwenye historia kulikuwa na kitisho cha Nyuklia, matokeo yake tukatengenezea UN na kupewa mamlaka ya kupitiliza.

Unakumbuka tulipata kuwa na vita kati ya UJAMAA na UBEPARI, vijinchi vyetu visivyo jielewa vikaunda MUUNGANO USIO FUNGAMANA NA KOKOTE.
Unakumbuka tulipata kuwa na vita baridi ...
Orodha ni ndefu sana mpaka sasa TUNAVYO VITA DHIDI YA UGAIDI.
Ukichukua muda wako na kupitia aina zote hizi za vita, mapinduzi, mirongo ya kisiasa, kiuchumi na kiitikadi, mwisho wa siku utakubaliana kwamba hayakuwa chochote mambo hayo ISPOKUWA NI HATUA MUHIMU ZA KUISOGEZA AJENDA MBELE.
Vita vya Ugaidi kama nilivyo zungumza kwenye posti zilizo pita havina chochote kutoka kwenye Uislamu, bali ni hatua muhimu ya kuisogeza ajenda mbele.


Sasa adui hewa huyu anayeitwa UGAIDI soon atafikia tamati, na ADUI MPYA ataingiza ulingoni.
Kupotea kwa ndege ya Malaysia, ‘safari ya mwezini’, kuonekana kwa vyombo vinavyo fahamika kama UFO, YOTE HAYO NI HATUA MUHIMU ZA KUMTAMBULISHA HUYO ADUI MPYA.

Matukio niliyo yataja hapo juu kwa kiasi kikubwa yanahusishwa na UJIO WA VIUMBE KUTOKA SAYARI NYINGINE.



Kama binadamu anaweza kwenda mwezini, ingawa HATUJA KWENDA MWEZINI KIUKWELI, ISPOKUWA ILIKUWA NI DANGANYA TOTO KAMA ZILIVYO NYINGINE, Basi na viumbe kutoka sayari nyingine wanaweza kuja hapa duniani. Ingawa mpaka sasa hakuna ushahidi wenye mashiko kama kuna viumbe katika sayari nyingine.
Lengo ni nini basi kutupatia aduo kutoka sayari nyingine?

Adui kutoka sayari nyingine, kumbuka atakuwa ni adui hewa, hatokuwepo kabisa, kama ambavyo HAKUNA KITU KINACHO ITWA UGAIDI KAMA KINAVYO SEMWA, Ipokuwa adui huyo atakuwa ni muhimu awepo ili kukamilisha kazi ambayo haiwezi kufanywa na VITA DHIDI YA UGAIDI.


KAZI YENYEWE NI KUWAONGANISHA WALIMWENGU WOTE DHIDI YA ADUI MMOJA KUTOKA NJE YA SAYARI YETU.
SASA NDEGE YA MALYSIA WATATUJIA NA TAARIFA NA KUTUAMBIA NI VIUMBE WA SAYARI NYINGINE NDIYO WALIYO ITEKA NDEGE HIYO, ABIRIA NAO WATAPATIKANA HAI NA WATATHIBITISHA HILO KWAMBA WALIKUWA NI MATEKWA WA VIUMBE KUTOKA SAYARI NYINGINE, MATUKIO MENGINE MAKUBWA ZAIDI YA HILI YATAFUATA NA MATOKEO YAKE ITABIDI BINADAM TUUNGANE KULILINDA ANGA LETU DHIDI YA VIUMBE WAVAMIZI ....


UNAKUMBUKA SERIES INAYO KWENDA KWA JINA LA THE EVENT ..... HUWEZI ACHA KUITIZAMA TAMTHILIA HII MPAKA UJUE MWISHO WAKE NI NINI, LAKINI KWENYE NUKTA MOJA KWENYE TAMTHILIA HIYO NDEGE INAPOTEA ANGANI MCHANA KWEUPE ... BAADAE INAKUJA KUFAHAMIKA KUWA NI VIUMBE KUTOKA SAYARI YA MBALI NDIYO WALIYO FANYA TUKIO HILI ... VIPI INAFANANA NA TUKIO LA KWELI ULILOONA CNN?


ADUI HUYU NIME MGUSIA KIDOGO KATIKA POSTI HII __ salimmsangi.blogspot.com/2013/08/hatua-nne-kabla-ya-ujio-wa.html

ISPOKUWA NITAMZUNGUMZIA KWA KINA ZAIDI HUKO MBELE NITAKAPO ZUNGUMZIA SUALA LA SAFARI YA MWEZINI.

 “Katika hali yetu kubwa ya chuki na utengano tuliyo nayo hivi sasa, mara kwa mara tunasahau ni kiasi gani binaadam tumeungana. Huenda tunahitaji kitu kutoka nje, kitisho cha ulimwengu kitakacho tufanya sisi kuweza kutambua umoja huu tulio nao. Nimekuwa nikifikiria ni namna gani tofauti zetu zitatoweka pale ambapo tutakuwa tunapambana na kitisho cha viumbe kutoka nje ya sayari yetu”

Nimekuwa nikijiuliza mwenyewe kwamba itakuwaje kama sisi sote hapa duniani tukagundua ya kuwa kuna kitisho dhidi yetu kutoka nje ya dunia yetu … nguvu ya kutoka kwenye sayari nyingine. Je si mara moja tu tutaweza kutambua kuwa hatuna tofauti yoyote baina yetu, kwamba wote tu binadamu, wananchi wa dunia na je, hatutaungana kupambana na kitisho hicho? – MANENO YA REGAN ALIYEKUWA RAIS WA MAREKANI

3 comments:

  1. Hiv kaka awa aliens wapo kwel naomba pia post juu y hawa viumbe

    ReplyDelete
  2. hii ni hatua ya tatu ya kuja kws Masiihh Dajjal/Mpinga kristoo

    ReplyDelete
  3. Kaka hebu ongelea hi big brother manake hii nembo yake ya jicho moja ciielewi

    ReplyDelete