Mimi binafsi nililitilia shaka suala zima la ndege ya Malaysia kutoweka
angani na isipatikane kokote kwenye uso wa dunia mpaka hivi leo, bado nalitia
mashaka suala hilo kwamba halina ukweli wowote ndani yake, bali ni moja kati ya
filamu zao nyingi wanazo ziigiza ilikuendelea kuulaghai umma, lakini zaidi mimi
naona ni hayo ni MAANDALIZI YA KUMTAFUTA ADUI MPYA ATAKAYE CHUKUA NAFASI YA ‘VITA
DHIDI YA UGAIDI’.
Kaa vizuri hapo ulipo ...
Wakati ndege hiyo ya Malaysia ikipotea ndani yake kuliwa na abiria 227,
nambari hiyo ni sawa na 2+2+7=11, ndege yenyewe ni Boeing 777 nambari
inayogawika kwa 11.
Ndege hiyo ya Malaysia ilipatwa na ‘ugonjwa’ kama ule uliozipata ndege za
9/11 ambayo tunajua kuwa tukio lile lilifanywa na utawala wa Bush mwenyewe.
1.
Ndege hiyo ya Malaysia ilipoteza mawasiliano kama zilivyokuwa ndege za
9/11. Masaa mawili baada ya ndege hiyo kuondoka ilipoteza mawasiliano kabisa na
kitengo cha anga ambacho ndicho kilicho kuwa na dhamana ya kuiongoza ndege
hiyo.
2.
Ndege hiyo iliacha njia yake ya safari kama ilivyokuwa kwenye 9/11. Ndege
hiyo ya Malaysia ikaendelea kusafiri maelfu ya maili nje ya njia yake
iliyopaswa kupita bila hata ya kutuma taarifa za tahadhari na msaada kwenye
kituo chochote cha kuongezea ndege na kisha ‘ikatoweka’ kama mazingaombwe vile.
3.
Ndege hiyo ikapotea kabisa na isionekane kama zilivyo potea ndege iliyo
gonga Pentagon na ile ya Pennsylvania kwenye tukio hilo la 9/11.
4.
Kama ilivyokuwa kwenye 9/11, kwenye ndege ya Malaysia nako abiria simu zao
zilikuwa hewani!!!!!
Kila mtu anajiuliza ni nini hicho? Ndugu na jamaa wa abiria kwenye ndege
iliyo potea wamethibitisha kusikia milio ya simu walipojaribu kuwapigia
wapendwa wao. Na pia baadhi ya kurasa za fecebook za abiria hao zimeonesha kuwa
wapo ‘online.
Shirika hilo la ndege la Malaysia limethibitisha pia simu ya mhudumu
aliyekuwepo kwenye ndege hiyo nayo iliita tu bila kupokelewa na mtu yeyote mpaka
ikakata kama zilivyo fanya simu 19 za abiria walio kuwepo kwenye ndege hiyo
baada ya kupigia na ndugu na jamaa. Hayo yalisemwa na msemaji wa shirika hilo
bwana Hugh Dunleavy.
Lakini pia hadithi ya simu za abiria na ile ya muhudumu kuita inatupatia
mwanga wa jambo moja, kwamba ndege hiyo haipo ndani wala chini ya bahari! Simu
haiwezi kuita kama ipo ndani ya maji, lakini zaidi simu hiyo lazima iwepo karibu
na mnara wa simu, ambao tunajua hauwezi ukawepo chini ya bahari isipokuwa
aridhini.
5.
Kama ilivyokuwa kwenye 9/11 hapa napo kwenye ndege ya Malaysia mapema
kabisa Illuminanti walianza kutoa dondoo za tukio zima takribani miaka minne
kabla. Tizama picha hii inayofuata na linganisha na tukio lenyewe kisha kuna
kichwa na kujiuliza ikiwa tangazo kwenye picha hiyo limetokea kwa bahati mbaya?
Tunapoendelea kulitolea macho suala hili, tunayo maswali ya msingi ya
kujiuliza, kumbukua hapa tunazungumzia ndege kubwa aina ya Boeng, ndege ya
kisasa kabisa, ndege hii haijalipuka, haijaanguka mahala kokote, si nchi kavu
si baharini, imetoweka ghafla, narudia tena IMETOWEKA GHAFLA ikiwa angani, na
haijapatikana mpaka hivi leo.
Vipi kama vile MUVI linajirudia ...?
Vipi wanataka kututengenezea Spetemba Ileveni nyingine au?
Swali # 1
Ndege zote aina ya Boeing 777 zimetengenezwa pamoja na ‘Black Box’ ambayo
inaweza kuhimili mlipuko wa aina yeyote ule utakaoipata ndege hizo. Kisanduku
hicho kinabeba taarifa zote muhimu yakiwemo mawasiliano ya hatua kwa hatua
tangi ndege inapotokea mpaka inapo elekea.
Swali linakuja NI VIPI KIBOKSI HICHO KIMESHINDWA KUTUELEKEZA WAPI NDEGE
ILIPO?
Swali # 2
Black Box zote zinayo uwezo wa kuendelea kusafirisha mawasiliano na kutambua
wapo kilipo hata kwa muda wa siku 30 hata kama ndege ikiwa imezama baharini.
Swali linakuja ni kitu gani hicho kilicho zima ‘signal’ ya kisanduku hicho
kiasi kwamba shughuli za kuipata ndege yetu zimekuwa ni ndoto. Tunajua ndege
hiyo haijawaka moto wala kuzama baharini, sababu simu za abiri na wafanyakazi
wa ndege zilikuwa zikiita kila zinapo pigwa. Sasa inakuwaje simu zinaweza
kuendelea kuleta mawasiliano lakini kisanduku cheusi kipoteze mawasiliano
kabisa?
Swali # 3
Ndege inapokuwa imepotelea baharini, mara zote kuna sehemu na mapande ya
ndege hizo yataonekana yakielea baharini.
Kama ndege ya Malaysia ingekuwa imetungulia na kushushwa chini basi vipande
lazima vingeonekana vikielea baharini, lakini viko wapi vipande hivyo? Ndege ya
Boeing 777, imetoweka ghafla kwenye uso wa dunia, IMETOWEKA, ama kweli
ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
Swali # 4
Mahala ambapo ndege hiyo ‘imepotelea’ panafahamika. Waongozaji wa ndege wanakuwa
taarifa zote za ndege husika, kumbuka wao ndiyo waongozaji, hivyo nukta ambayo
ndege inakata mawasiliano na wao wanakuwa wanafahamu ilikuwa eneo gani, ilikuwa
kwenye mwendo kasi wa aina gani, vyote hivyo vinaweza kutumika kuelekeza ni
wapi mapande ya ndege hiyo yanaweza kuwa yameangukia. Lakini ni vipi ndege hii
ya Malaysia imeshindwa kupatikana chochote pamoja na kwamba inafahamika ni wapi
nukta ya mwisho ilionekana kwenye rada?
Swali #5
Tuseme Ndege 370 ya Malaysia imetekwa, lakini ndege haipotei kwenye rada
hata kama ikitekwa. Sasa inakuwaje ipotee hata kwenye rada isionekane?
Ndege nambari 370 ya Malaysia aina ya Boing 777 HAIJALIPUKA, HAIJANGUKA
KOKOTE, ILA IMETOWEKA?
HOW?
TUKUTANE TENA HAPA TO FIND THE HOW ...
hahahaa c walisema mabaki yameonekana Australia
ReplyDeleteWalisema yameonekana Australia lakini wamekuonesha hayo mabaki? Kama walivyo sema wanafahamu walipo wasichana wanao shikiliwa na Bokoharam lakini wamekuonesha hao wasichana? They Just think your fool to buy anything the y sell, no matter how crap it is ... so sad
DeleteUmesikia eti tena wanahisi mabaki ya ndege hiyo yanaweza kuwa haya yaliyoonekana Ktk kisiwa fulani huko Zanzibar!!
DeleteHebu tujiulize,kama simu za abiria zilikua hewani kwanini wasiwasiliane na watu wa mitandao ili kujua simu hizo ziko wapi?halafu ulimwengu huu tulionao uko juu sana kwa sasa kiteknolojia,ni kweli kabisa teknolojia imeshindwa kabisa?
ReplyDeletedaaaahh hii ni vita na wanatamani malengo yao yakamilike kwa her au kwa shar,na wanapambana usiku na mchan kukamilishsha makusudio yao,hakika imani zetu za kwelii ndo mkomboz wetuuu
ReplyDeleteAsee inatisha
ReplyDelete