Hadithi moja ya kweli nilisikia kuhusu mtoto wa miezi kadhaa ambaye
alipelekwa kwa daktari mwenye uchu wa pesa aliyempima na kumuambia mlezi wa
mtoto yule kuwa ana Malaria na kisha akampatia dozi ambayo hata baada ya muda
haikuwa imetatua tatizo, hivyo kitoto kile kikarudishwa kwa daktari yule ambaye
tena akamuandikia dozi nyingine, mwendo ukawa ni huo kila anaporudishwa ni dozi
na hata mwisho akamua kukatundikia dripu na kalizidi kudhoofu karibu ya kufa,
walipopata wazo la kumpeleka kliniki zinazotumia dawa za asili mtoto yule
alikutwa anafunza mwili mzima, kila anapopasuliwa panafunza hivyo utaratibu
mpya wa kumtibu mtoto huyo ukaanza na alipochunguzwa hakuwa akiumwa malaria isipokuwa
sikio, masikini. Lakini hapa mtoto huyu tayari keshaupata UKIMWI, sababu kinga
zake za mwili zimeshavunjwa vunjwa ila kwa sababu akipimwa hana virusi vya HIV
basi hutambiwa kuwa ana UKIMWI , lakini hata kama unakohoa na ukawa na virusi
vya HIV utaambiwa una UKIMWI na hiyo peke yake inatosha kukumaliza kabla
hujaanza kutumia hizo dawa zenye sumu ambazo hazikutengenezwa ili kutibu
UKIMWI, bali kukupa UKIMWI ufe.
Mgonjwa anapo bainika kuwa na kile ambacho jamii inakiita ni virusi vya
Ukimwi au kwa jina lingine V.V.U, kitu ambacho hakipo; anaanza utaratibu wa
kupima damu yake mara kwa mara kwa ajili ya kuangalia uwezo wa mfumo wake wa
ulinzi mwilini dhidi ya maradhi unavyoweza kupambana na mashambulizi ya
maradhi. Vipimo hivyo vya damu ambavyo vinatizama kiwango cha T-Seli au kwa
jina maarufu CD4 ndivyo vinavyoamua kuwa mtu huyu mwenye V.V.U sasa anaweza
kuanza safari ya kutumia madawa ya kurefusha maisha. Hata hivyo ni makosa
makubwa yanayofanywa na wauguzi katika vituo vya afya, vituo vya kupima na
kutoa ushauri nasaha kwa kutumia kigezo cha T-Seli kama ndiyo kipimo cha kuweza
kutoa tiba kwa mwatahirika kwa sababu kwa mtu mwenye afya peke yake T-Seli
zinaweza kushuka mpaka 200 na kupanda mpaka kufikia 2000 ndani ya siku moja ya
kawaida tu. Profesa Ian Weller ambaye alikuwa akihisika na mpango wa majaribio
wa kutumia madawa ya kuongeza maisha ya AZT kwa wanajeshi wa Uingereza wenye VVU
na ambao walijitolea kwa ajili ya majaribio hayo anasema.
“Kitu ambacho tunapaswa
kukumbuka kuhusu idadi ya CD4 (T-cell) ni kuwa idadi yake inapishana kila mara.
Zinaweza kupishana kiidadi katika siku moja kwa mtu mmoja.... zinaweza kuwa
chache wakati wa asubuhi na kuongezeka wakati wa jioni. Idadi yake inaweza
kuathiriwa na vitu mbalimbali anavyofanya muhusika katika siku”.
Mazingira haya yasiyo sahihi juu ya upimaji wa kile wanachokiita VVU
ambacho kiuhakika hakipo kumepelekea mamilioni ya watu kuhesabiwa kuwa na
Ukimwi. Katika nchi zetu zinazoendelea kama vile nchi nyingi za Afrika kuna
maradhi mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza kusababisha mtu kuwa na
Ukimwi.
Maradhi yatokanayo na kujamiiana na suala zima la mtu kuwa na upungufu wa
kinga katika mwili wake si swala geni masikioni pa wengi, lakini hili suala la
HIV kusababisha huo upungufu wa kinga katika mwili na upimaji wake hapana shaka
ni suala jipya kwa wachunguzi wa mambo na wadadisi. Mwaka 1989 Luc Montagnier mshirika wa karibu
Robert Gallo ambaye kwa pamoja na Montagnier ndiyo waliokuja na nadharia ya kibubusa
kuwa HIV inasababisha Ukimwi alisema hadharani kuwa,
“HIV haina uwezo wa kusababisha
maangamizi ya mfumo wa ulinzi mwilini ambayo yanaonekana kwa watu wenye
Ukimwi.”[1]
Dr. Duesberg anatambulika duniani
kama mmoja wa wataalam au miongoni mwa wajuzi wachache wa virusi aina ya
retrovirus ambao wanatajwa kama aina ya virusi vinavyosababisha HIV ana haya ya
kutuambia,
“AZT ni muwaji wa seli hai za
mwili zilizo ambukizwa na ambazo hazijaambukizwa. AZT haiwezi kuzibagua seli
hai mbili hizi wala kuzitofautisha. Inauwa T- cell, B-cell, red cell, inauwa
seli zote haina kizuizi. Inafuta kila kitu na baada ya muda fulani zinamuua
mbebaji wa seli hizo. AZT ni muwaji halisi ambaye anahusika na mauwaji ya mamia
elfu ya watu wanaotubiwa na madawa hayo na mbao tayari wameshakufa kutokana na
sumu yake dhidi ya celi hai za mwili... HIV au (kama inavyotambulika sasa VVU)
haisababishi Ukimwi... nukta ya msingi ambayo kila mtu anaikosa ni kuwa
makaratasi ambayo yaliandikwa na Gallo kuhusu HIV yote yamepatikana kuwa ni ya
kughushi (feki)... na nadharia ya HIV kusababisha ukimwi imeegemea katika
makaratasi hayo (AMBAYO NI FEKI, YA KUGHUSHI).”[2]
Sasa mbona bado yanaendelea kupigiwa zumari? Sababu hiyo ni business ya
mabilioni ya dola, unataka tuseme kuwa HIV haisababishi UKIMWI au hakuna VVU
unadhani sisi tutaenda kula wapi? Taasisi na NGo zinazo zaliwa kila uchao kupambana
na UKIMWI zitapatia wapi pesa, watu wanajenga majumba, watu wanapaki BMW kwa
takwimu hizo feki halafu wewe unasema tutangaze kuwa HIV haisababishi ukimwi,
hivi wewe unayo akili kweli? Jifikirie vizuri kama unajipenda ua Hujipendi sisi
tunaendelea kuvuta FUND za maana kwa ajili ya ishu hiyo sasa kama wewe
unajifanya unajua sana kaa kushoto usituekee inzi hapa.
Dawa hizi zenye madhara mengi kuliko faida zinapojazana mwilini
zinaudhofisha na kuumaliza nguvu mfumo wa ulinzi mwilini katika viungo fulani
au maeneo fulani ya mwili na kisha kufanya aina fulani ya minyoo kuzaliana
katika maeneo hayo, daktari mmoja ambaye amekuwa akiwatibu mamia ya wagonjwa wa
Kansa na UKIMWI amewakuta wote wana aina hiyo ya minyoo na mifumo dhaifu na
iliyoharibiwa kabisa ya ulinzi mwilini kutokana na kutumia madawa hayo yasiyo
faa kwa binaadam, daktari huyo aliweza kuiua minyoo hiyo kwa dawa asili na
kuwapatia virutubisho na dawa zingine zenye kulenga katika kujenga mfumo wa
ulinzi mwilini.
Tukumbuke kuharibiwa kwa mfumo huo wa ulinzi au kuvunjwa vunjwa kabisa
ndiko kunako sababisha maradhi ya UKIMWI na ikiwa dawa tunazopewa za kuongeza
maisha kwa waathirika zinakwenda kuvunja mfumo je hizo ni dawa za kutibu UKIMWI
au kukuua kwa UKIMWI?
Hii ndiyo maana wagonjwa wengi wa UKIMWI huzidi kupata matatizo ya kiafya
na kudhoofu pale tu wanapoanza kutumia dawa hizo wakati kabla hawakuwa na
matatizo wanayo yapata. Ni vigumu kwa mtu mwenye fikra huru kukubaliana na
msemo wa mashirika ya UKIMWI duniani kuwa UKIMWI hauna tiba na uchunguzi bado
unaendelea. Hivi inawezekana vipi kwa maprofesa na watu wenye PhD za udaktari
,na M.D wanaoishi katika nchi zilizoendelelea zenye vifaa vya kutosha na vya
kisasa, malighafi na kiwango kikubwa cha fedha kushindwa kupata tiba ya maradhi
haya tangu yalipotangazwa rasmi mwaka 1981 wakati tuna waona madaktari
mbalimbali wa tiba za asili katika nchi zetu wenye vifaa duni, malighafi chache
wasio maprofesa na wasio na fedha za kutosha wakitengeneza dawa za asili ambazo
zimekuwa zikileta manufaa makubwa kwa wagonjwa hao.
Kama umepata kutizama kipindi cha City Sound kilicho kuwa kina rushwa na
East Afrika Television cha chanel 5 ambacho mtangazaji wake alikuwa ni Seki (sikumbuki
hasa ni mwaka gani kilikuwa kikirusha kipindi kile, lakini kilikuwepo) katika
kipindi hicho tuliona daktari mmoja wa hapa nchini kwetu, daktari wa tiba
asilia namna anavyofanya kazi yake kuwatibu wagonjwa hawa wa UKIMWI na
mafanikio wanayoyapata, daktari wetu huyu hana vifaa bora na vya kisasa, wala
bado hajawa na ofisi rasmi anawatibia wagonjwa hawa nyumbani kwake na
alichokuwa anaomba yeye ni ofisi tu na yeye yuko tayari kufanya kazi hii ngumu,
hana fedha nyingi kama walizonazo hao wanaoa jiita wapiga vita UKIMWI wa nchi za magharibi na wa hapa kwetu, ikiwa
kweli serikali ina nia ya kupiga vita UKIMWI kwa nini wasimpatie vitendea kazi
mtu huyu alionesha mwanga katika kiza kinacholigubika anga la dunia nzima?
Ikiwa ni kweli mashirika hayo yenye nia ya kutokomeza UKIMWI duniani
yamedhamiria hilo kwa nini wasiwaunge mkono watu kama hawa ambao wameanza
kuwaonesha njia ambayo wao kwa zaidi ya miaka 25 sasa bado wanaendelea
kuitafuta? Ukweli ni kuwa mashirika hayo na madaktari wao hawana nia ya
kuutokomeza UKIMWI, kwa sababu ya umasikini wetu wanapotuletea vifaa na fedha
ambazo miaka kadhaa nyuma walizipora hapa kwetu na bado wanaendelea kuzipora
basi tunaona kuwa wanania ya kuutokomeza maradhi hayo hatakama vifaa hivyo na
dawa walizoleta ni sehemu ya ajenda yao ya kutuangamiza.
Vidonge hivi wanavyo pewa wagonjwa wa UKIMWI kwa kuwaambia kuwa
vitawaongezea siku za kuishi kama vile AZT vimeonekana vinayo madhara makubwa
kama UKIMWI wenyewe. Vidonge hivi vilizuiliwa na kupigwa marufuku mwaka 1957
na Full Form of Food and Drug
Adminstration (FDA) kwa sababu vilikuwa vikiuwa watu ambao vilipaswa
kuwasaidia. Leo hii waathirika wa UKIMWI wamekuwa ndiyo maabara za kujaribia
kila aina ya madawa sumu, na vipi itaingia akilini kuwa wanawajaribia kama siyo
makusudi.
Sote tunajua kabla dawa haijathibitishwa kwa matumizi ya binaadam lazima
ipitishwe kwenye majaribio kadhaa na kuonekana ni salama kwa binaadam, lazima
ijaribiwe kwa panya wa maabara na viumbe wengine wenye maumbile na mifumo kama
yetu kabla haijaruhusiwa leo vipi shirika kubwa la afya duniani lishughulike na
kutoa aina hii ya dawa, je tutasema wamekosea, au wanafanya majaribio? Hapana
ukweli uko wazi na nchi zinazo endelea ndizo hasa zilizo lengwa, kama vitu
vidogo mfano wa mitambo fulani au mashine fulani zisizo na ubora zitaweza
kuingizwa kwa mkataba wa mamilioni ya shilingi ambao thamani yake ni kubwa
kushinda chombo chenyewe kwa vile tu wananchi hawatajua je vipi kuhusu madawa
yanayoingia bure nani atasema nini juu ya hili?
Waliotusaliti wameungana kukataa kata, kata kuwa asili hasa ya Ukimwi ni
maabara. Docta Seale J, wa Royal Society of Medicine anasema greenmonkey wa
Afrika hawawezi kupata virusi vinavyosababisha ukimwi. Anasema hata kama
watachomwa sindano yenye virusi hivyo. Kwa taarifa yako ni kuwa virusi hao
walijaribiwa kwa chimpanze hao na hakuna hata mmoja aliyepata ukimwi.
Ushahidi wa kisayansi unathibitisha kuwa wanawake wengi wajawazito
wanaathirika kwa kiasi kikubwa na madawa haya ya kuongeza muda wa kuishi kwa
waathirika. Ni kwa miaka mingi imekuwa ikijulikana kisayansi kuwa seli hai
changa zinazo kuwa zinaathirika haraka na sumu mbalimbali zinazokutana nazo.
Huu ndiyo msingi wa juhudi ya kuwaepusha wa mama wajawazito na vibeba sumu
vyovyote kwa kadiri inavyowezekana, huu ndiyo msingi wa mama wajawazito
kutakiwa kuwa chini ya uangalifu mkubwa katika kipindi cha ujauzito na mara
baada ya kujifungua.
MOJA YA MADHARA YA DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA
Lazima pia tutambue kwamba mfumo wa ulinzi katika mwili wa mtoto unaanza
kukomaa pale mtoto anapofikia umri wa miaka 10. Lakini ajabu ni kuwa katika
suala hili la Ukimwi wauguzi wa afya wamekuwa sheria hizi wanazibadilisha,
madawa yenye sumu kali na madhara kwa mtumiaji yamekuwa yakihalalishwa kwa mama
wajawazito pamoja na watoto duniani kote. Hata watoto ambao wamezaliwa na mama
ambao tayari wameathirika lakini watoto wao wakawa hawajaathirika, ajabu ni kuwa
na watoto hao nao wanaandikiwa dozi ya AZT kwa wiki sita baada ya kuzaliwa.
Watoto ambao wanazaliwa tayari wana Ukimwi wanakuwa wanaandikiwa dozi ambazo
msingi wake ni kwenda kuuwa mfumo wa ulinzi wa mtoto yule na hivyo baadaye
kumsababishia Ukimwi. Kana kwamba madaktari hao wamesahau kuwa seli changa za
watoto hao zinaathirika haraka na upesi zaidi kwa madawa hayo.
AZT pia inaiathiri vibaya DNA ya muhusika na ushahidi unathibitisha kuwa
AZT inaweza kuibadilisha DNA. Pia AZT inaweza kusababisha kutoka kwa mimba,
madhara kwenye uti wa mgongo wa mtoto, mtoto kuzaliwa na viungo ambavyo
havijajipanga sehemu yake, uso kukaa vibaya, maradhi ya moyo na aina nyingine
za ulemavu, pia mtoto huzaliwa akiwa na kiasi kidogo cha Haemoglobin. Katika
mazingira mengine ukuaji duni wa mtoto pia hutokea.
UKIMWI umekuwa ni biashara kubwa, biashara ya vifo, ni miaka michache tu
nyuma ilitangazwa kwenye vyombo mbali, mbali vya habari kuwa kuna makahaba wa
Nigeria ambao wamepatika na aina fulani ya damu, damu maalum ambayo haiathiriwi
na virusi vya HIV, kuwa makahaba hao wanatembea na virusi hivyo ila
haviwasababishi UKIMWI kutokana na damu yao ilivyo ila wanapo kutana na watu
wengine kimwili wanaweza kuwaambukiza virusi hivyo vya HIV na baadaye
kuwasababishia UKIMWI watu hao, bali wao hao makahaba wataendelea kuwa salama,
nilishangaa sana niliposikia hadithi hii na kuona kweli hao makahaba
wamebarikiwa.
Halafu hadithi nyingine ikavuma na bado tunayo hapa kwetu kwamba kuna watu
ambao wao ni “kerea” yaani wabebaji tu wa virusi vya HIV lakini wao haviwapatii
UKIMWI ila wakikutana na watu wengine kimwili wanaweza kuwapatia virusi hivyo
vya HIV na hatimaye UKIMWI ila wao kama kawaida wako salama, eti hii ni kwa sababu
ya damu yao.
Mungu wangu uwongo mwingine huo. Kama tunavyojua UKIMWI anaupata mtu au
kutokuupata mtu kutokana na kinga zake za mwili zilivyo, kama ni imara
kupambana na mashambulizi ya maradhi au ni duni na haziwezi kupambana na
mashambulizi hayo, suala la damu maalum linatoka wapi? Labda hata wangesema
wanakinga maalum katika mwili wao lakini damu kwa maana ya damu bado haijaingia
akilini. Lakini hiyo ni harakati za kutokupoteza wewe mteja wa dawa za kurefusha
maisha, sababu watakapo kupima na kuonekana una virusi vya HIV ndipo utakapo
kwenda kununua hizo dawa zao, sababu sisi ni masikini na madawa hayo ni ghali
hivyo mpango wa kutupunguza unaweza kusuasua ndiyo maana wakatuleta bure na kwa
sababu HIV siyo inayosababisha UKIMWI hii ndiyo maana watu fulani wanaweza kuwa
na HIV na wasiwe na UKIMWI sababu watu hawa hawajaamua kutumia hizo dawa za
kurefusha maisha ili kuzidi kukupotosha wanakuambia watu hawa wana damu maalum
na au watu hawa ni “kerea”, halafu mtu mwingine anapo jamiiana na watu hawa na baadaye
akapima na kujikuta kapata virusi vya HIV anapo pewa ushauri nasaha anaambiwa aanze
kutumia dawa za kurefusha maisha kwani tayari ana UKIMWI, lakini ukweli hana
UKIMWI hali yake ni sawa na ya wale wanaoitwa watu wenye damu maalum au “kerea”
ila baada ya muda fulani wa matumizi ya madawa hayo ndipo sasa anaupata UKIMWI.
Hii ndiyo maana mgonjwa yoyote anapokwenda kupima afya yake na akakutwa ana
malaria, daktari atampatia dawa za malaria na atamuambia tumia hii dozi vizuri
utapona usijali wala usiwe na shaka utapona kabisa. Lakini mgonjwa huyo, huyo
inapobainika kuwa ana virusi vya VVU baada ya kwisha kupewa dawa daktari
atamuambia nenda na uishi kwa matumaini. Kwa nini kule ameambiwa atapona na
huku anaambiwa aishi kwa matumaini? Kwa sababu hiyo aliyopewa ni sumu tofauti
ni kuwa mtoaji na mpokeaji hawajui kuwa ni sumu wao wanafuata vile
walivyoambiwa kufanya, na hivyo baada ya muda fulani mgonjwa yule atakufa tu,
kwa hiyo hakuna haja ya kumuambia atapona wakati anachopewa kitamuongezea sumu
bali aishi kwa matumaini kwani muda si mrefu ataondoka. Na hiyo kauli peke yake
hata kabla ya kuanza kunywa hizo dawa inatosha kuanza kumdhoofisha na kumuwa
kisaikolojia.
UKIMWI ni silaha ya kibaiolojia iliyolengwa kuwamaliza watu wa namna fulani
duniani, wafutike au idadi yao ipungue kufikia kiwango kinachotakiwa na Freemasons.
Na watu weusi ni miongoni mwa walengwa na hii ndiyo maana UKIMWI unayo makazi
ya kudumu Afrika.
Inashangaza pale watu wanapomfurahia kiongozi wa Marekani kwa jitihada zake
za kupunguza makali ya janga hili barani Afrika wakati watu walio nyuma ya
kiongozi huyu na nchi yake yaani Freemasons wamedhamiria kuwatokomeza watu wa
bara hili. Ikiwa kweli rais Bush na serikali yake wanania ya kutokomeza UKIMWI
duniani ilikuwaje serikali yake ikiongozwa na yeye mwenyewe ichukue dhamana ya
maisha kwa madaktari wale walio waambukiza mamia ya watoto virusi vya HIV?
Madaktari wale ni wauaji na walistahiki kifo kama sheria ilivyopitishwa, kwa sababu
walifanya kwa makusudi kama ushahidi
ulivyoonesha na walikuwa wakijua matokeo yake nini baada ya kuwa ambukiza
watoto wale virusi hivyo lakini serikali ya Marekani kwa vile inapesa
ikaingilia kati na kutoa mamilioni ya dola za Kimarekani kama fidia kwa watoto
wale na dhamana kwa wauaji wale wachiwe huru na kununua urai wa daktari mmoja
wa Palestina ili na yeye akaishi huru Bulgaria kwa kazi nzuri waliyoifanya. Madaktari
hawa wana tofautiana gani na wale wanao chafua majina ya dini zetu kwa mabomu
ya kujitoa muhanga? Wote ni wauaji ikiwa ugaidi unayo maana ya kumletea mtu
khofu, mashaka na wasiwasi katika uhai wake na mali zake basi na hawa madaktari
ni magaidi sababu tayari watoto wale na familia zao watakuwa na mashaka juu ya
uhai wa watoto wao, mbona basi
anayepigana vita dhidi ya ugaidi ndiye anayewakingia kifua? Aha! kumbe kwa
sababu madaktari hawa wamewasaidia Brotherhood katika ajenda yao ya kupunguza
idadi ya watu duniani.
Ikumbukwe UKIMWI hautokani na Sokwe ni Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa
msaada mkubwa wa Marekani ndiyo waliouleta kupitia chanjo ya Smallpox mwaka
1978 mpaka 1980, ndiyo hao, hao wakawagawia maradhi hayo kwa chanjo nyingine ya
Homa ya Manjano watu Weusi wa marekani, mashoga na Wahispania. Lengo la UKIMWI
ukishirikiana na Vita, Njaa na Kampeni za Uzazi wa Mpango ni kupunguza idadi ya
watu bilioni 2.5 ifikapo mwaka 2000, ambao tayari tumeshaupita na takwimu za
Shirika la Afya Duniani (WHO) na lile la Umoja wa Mataifa la UKIMWI na HIV (UNAAIDS)
zinaonesha kutoka mwaka 1981 mpaka 2002 UKIMWI ulikuwa umeshakula watu milioni
20 na hizi ni zile zinazoitwa taarifa za kiserikali ambazo mara nyingi huficha
mengi, Njaa yenyewe kila mwaka inakula watu milioni 20, Vita kama mauwaji ya
halaiki ya Rwanda yalikula watu zaidi ya milioni moja, kuna Sudan, kuna Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Kongo, kuna Sierra Leone, kuna Mashariki ya Kati na
kwengineko, kuna Kampeni za Uzazi wa Mpango hatufahamu mpaka sasa zimeshakula
maisha ya watu wangapi, na swali ni je Brotherhood/Freemasonry/Illuminants
kutokana na ajenda yao wamesharidhika na idadi ya watu waliokwisha wauwa, ikiwa
tuna mashaka juu ya majibu kutokana na swali hilo iweje tusiwe na mashaka juu
ya muwaji huyo anapokuja na sura ya kutibu maradhi aliyoyaleta yeye, tutajuaje
kama hizo za safari hii si sumu kama zilivyokuwa za mwaka 1978, lakini AZT
imeshajulikana ni sumu bado tunanyoosha mikono kuzipokea, Mungu atusaidie
tufungue macho kwani tumelala vibaya mno lakini naye hawezi kutusaidia kama
sisi hatuko tayari kusaidiwa, kuna jambo kubwa linaloendelea nyuma ya kivuli
cha janga hili la UKIMWI na tusipofungua macho tutajikuta tumekwisha ni vyema
tukaanza utaratibu wa kuwa ni wachunguzi wa mambo, kufuatilia jambo na kujua
ukweli wake kabla ya kulikimbilia na kuanza kulifanya kwa sababu tu limeletwa
na fulani au limeletwa katika sura fulani, kuna haja kubwa ya kutafuta elimu
sahihi, na kufungua uwezo wetu wa kufikiri.
Hello,
ReplyDeletenaomba mawasiliano yako, mkuu haswa sim no. nahitaji kukuliza jambo.
nitumie email, tuanzie hapo kwanza ...
Delete