Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Monday, December 2, 2013

NAMBARI TISA (9) NA KUMI NA MOJA (11) KWENYE DUNIA YA KIMASONIA

LEOTUTAZUNGUMZIA ALAMA NEMBO ZA KIMASONIA, NA LEO TUTATIZAMA KWA UNDANI NAMBARI TISA (9), KISHA KUMI NA MOJA (11), HALAFU MWENGE …

Kwa freemasonry lugha yao ipo mahususi kwenye maumbo na alama mbalimbali lakini pia bila kusahau nambari, umuhimu wa nambari kwa freemasonry na asasi nyingine za siri unakuja pale ambapo elimu ya kale kabisa ilihifadhiwa katika nambari na kwa watu hawa hisabati limekuwa ni somo muhimu mno,

“Elimu ya kwanza duniani imekuja Kwa alama mbalimbali, hekima za watu wa Chaldean, Phoenician, Egypty, Kaanani, wanafalsafa kama akina Zoroaster, Sanchoniathon, Pherecydes, Syrus, Pythagoras, Socrates na Plato, vyote vya zamani vilivyokuja katika mikono yetu, vimekuja kwa njia ya alama”


Nembo/Alama ni muhimu sana kwa wamasonia na freemason wanajifunza maana mpya ya kila nembo, nambari kila wapandapo daraja moja (degree), hivyo nembo moja au nambari inaweza kuwa na maana zaidi ya moja na maana tofauti kwa masonia wa daraja tofauti, ni wale freemasons walio katika daraja ya juu tuu ndiyo wanao jua maana halisi ya nembo hizo na wengine hawajui kwani hao hawastahiki chochote ila kupotezwa.

Katizame ile Filamu ya Davinci Code, Jina la Filam hii linatokana na jina Leonard da Vinci mtu huyu ambaye huenda tukaja kuisoma hadithi yake huko mbele. Filamu iliyozua utata kwenye Kanisa na kuzusha mkanganyiko, Freemason wenyewe ndiyo waliotengeneza Filam hii na ina mengi kuelezea kuhusu freemason hasa kwa watu wanao wajua freemason lakini kwa mtu wa kawaida anaweza kuona ni sinema ya kawaida yenye lengo ya kulipaka matope Kanisa mbali na vitu kadhaa vilivyoelezea filamu hii pia inaelezea jinsi gani nembo/ alama zilivyo na umuhimu kwa Freemason katafute uitizame kama hujapata kuitizama.

Katika hili leo ningependa kuitizama nambari hizi mbili, 9 na 11 maarufu kama ‘NINE, ELEVEN’ ingawa sitazungumzia tukio muhimu katika historia yetu la minara miwili kule Washington D.C. mpaka baadae kidogo.

Tuanze na nambari tisa (9)

Kutoka kwenye kitabu kilicho itwa A lexicon of Freemasonry, kilichoandikwa na Freemason mkubwa na maarufu, Albert G Mackey, MD, anasema,
“ ... kutoka kwa wafuasi wa Pyhagoras ni kuwa namba tisa (9) inayo uwezo na nguvu ya kujizalisha yenyewe kwa kuizidisha, ichukulie nambari hii mfano wa kitu chenye au kisicho na uhai, ingawa umbile lake litakuwa ni lenye kubadilika, lakini kitu hicho hakitofutika kamwe (sababu kinayo uwezo wa kujizalisha chenyewe.) Pia nambari hii inayo maana aya ndani zaidi kwenye umbo la duara, ambalo kimahesabu umbile hili lina nyuzi za digrii 360 ambayo ni sawa na kuchukua 3+6+0= 9 ..”


Maana yake ni nini hasa, hii inatueleza kuwa freemasonry wanapo itzama nambari tisa (9) kwa ni kama wanakitazama kitu ambacho hakiwezi kufutika, kumalizika, kufa au kuondolewa, kitu ambacho daima kinajizalisha chenyewe. Hivyo kwa freemasonry nambari tisa (9) ni alama ya umilele.

Apron hiyo hapo juu ya kimasonia huvaliwa na mwana masonia mbaye ameingia daraja la tisa (9), hufungwa kiunoni, mwanachama huyo hujulikana kama Memphis-Misraim, utaona kwenye Apron hiyo kumechorwa ibada mahususi ya kimasonia, ‘ibada ya kuchinja mtu’

Tunapo ichambua Aproni hiyo inayovaliwa na mfuasi wa kimasonia laiyefikia daraja la tisa (9), tunakutana na hayo yafutayo,

Kwanza mkono ambao umeshika kisu ni mkono wa kulia, ambao nao kwa freemasonry mkono wa kulia ni ‘mkono wa utii,’ ‘mkono wa uaminifu,’ na pia ndiyo mkono unao tumika kuchukulia kiapo.
Jambia ambalo limeshikwa na mkono huo kikawaida hushikwa na mtu maalum anayefahamika kama ‘Grand Sword Bear’ na jambia lenyewe huitwa ‘Sword of the State’.

Kichwa nacho kwenye Aproni hiyo kinayo maana yake mahususi, kichwa hicho kinamaanisha ‘utawala ambao upo’ yaani utawala ambao siyo ule wa kimasonia, kwa vile siku zote vita vyao freemasonry ni dhidi ya watu na serikali zao.

Kichwa kinapo katwa kama inavyo oneshwa kwenye aproni hiyo, hushikiliwa kichwa hicho na kuacha damu itiririke bila kizuizi na hapo ikimaanisha ‘maisha mapya’ au ‘utawala mpya’ au NEW WORLD ORDER’ inakuja kuchukua nafasi ya kiuatawala.


Unakumbuka kile kilicho tokea Mei 29, 2004, raia mmoja wa  Marekani na ambaye anayo asili ya ‘Uyahudi’ bwana Nick Berg, alikamatwa na kuchinjwa ‘live’ na watu wanao jiita nia ‘magaidi.’ Vidio ya kuchinjwa kwake ilirushwa kwenye kila kituo kikubwa duniani cha Luninga, 


Kila kituo cha luninga duniani kilionesha habari hii. Kama kawaida wauwaji walijitambulisha kuwa wao ni kikundi cha kislam, ambacho kimekerwa nay ale wanayo yafanya Wamarekani na majeshi yao kwenye aridhi ya Iraq.

Tukio hilo lilikuwa ni la aina yake kwenye historia ya vyombo vya habari, kwani hakuna kabla ya hapo na baada ya tukio hilo kulipatwa kuoneshwa tukio lenye maudhui ya kuogofya na kutisha kama hayo kwenye mtandao wa luninga kwa kiasi kikubwa kama hicho.

SWALI: KWA NINI TUKIO HILO LILIONESHWA NA KUONESHWA KWA KIWANGO HICHO KOTE DUNIANI?

Tukio hili lilioneshwa kwa sababu, wakati walimwengu wasiyo jua chochote wakiendelea kuaminishwa kuwa waliyo fanya hayo ni Waislam, na ndivyo kitabu chao kinawataka wafanye hivyo, upande mwingine wa shilingi ni kuwa, huo ulikuwa ni ujumbe kwa fremasonry wa daraja la juu, illuminanti na wengine wote wanao shiriki katika kufanikisha NWO.
Tukio hilo lilikuwa sawasawa na ibada ya kimasonia ambayo inaonekana kwenye Aproni ya mfuasi aliyefikia daraja la tisa (9)

Nick Berg alikatwa kichwa chake na kwa kutumia kisu kilicho shikwa na mkono wa kulia wa muuaji wake.
Kishwa Muuwaji akakishika kichwa cha Nick kwa mkono wa kushoto, akakining’niza kuachia damu itiririke kama ilivyo kwenye Aproni ya kimasonia, 

SITAWEKA PICHA HIYO YA NAMNA KICHWA CHA NICK KILIVYO NING'INIZWA BAADA YA KUTENGENISHWA NA KIWILIWILI KWA SABABU ZA KIMSINGI KABISA. HUWEZI KUONDOA UOVU KWA KUUONESHA KIVITENDO UOVU HUO, BALI UTAKUWA UNAUSAMBAZA ZAIDI.

Muaaji akiwa amekining’iniza kichwa cha Nick Berg kwa mkono wake wa kushoto baada ya kukikata kwa mkono wake wa kulia. Hii ilikuwa ni picha mbaya sana kwenye historia ya luninga.

Ujumbe waliokuwa wanapewa watu hao, kote duniani, katika majukumu na nafasi zao ni kuwa, muda umefika kwa wao KUONESHA UTII WA KIAPO CHAO, UAMINIFU KWENYE NCHI ZAO, KWA KUING’OA UTAWALA ULIOPO SASA KOTE DUANIANI, MA KUWEKA MAZINGIRA YA UJIO WA NWO.
Cha kuvutia zaidi ni kuwa, miaka miwili baada ya tukio hilo, yaani baada ya ibada hiyo ya kimasonia iliyofanywa ‘LIVE’ kwenye mitandao yote ya Luninga duniani, ambalo lilikuwa ni ujumbe mahususi kwa wafanyakazi wote wa NWO kokote walipo kuamka na kuanza kazi ya kuandaa mazingira ya NWO, au kwa jina lingine kama wanavyoiita wao ‘NEW INTERNAL KINGDOM,’ ambayo wanaamini kuwa huko wataishi milele au watapata uwezo wa kuishi milele, kama ambavyo uwezo huo unavyo wakilishwa na nambari tisa (9). Cha kuvutia ni kuwa Mwanamasonia mmoja ambaye mpaka sasa inasemekana yupo kwenye daraja la tatu (3) kwenye mtandao huo, daraja la wale wanao faa kudanganywa, au maarufu kama Blue Degree, mimi huwaita ni mauwa kwenye ukuta wa kimasonia,    mwanachama huyo hakuwa mwingine bali mwanamuziki maarufu wa Hip Hop JAY-Z.
Unajua Jay Z, alifanya nini?


Jay Z, alikuja na albamu yenye jina la ‘KINGDOM COME’, hii inavutia sana, sababu ujumbe ulikuwa unapatikana kwenye ibada ile ya kimasonia iliyofanywa ‘LIVE’ kote duniani, ni kuwataka wanachama, vibaraka na wafanyakazi wa NWO, kuonesha utiifu wa kiapo chao, uaminifu kwa kuzivuruga na kuzimaliza serikali zilizopo sasa, na kuweka mazingira ya ujio wa ‘NEW INTERNAL KINGDOM’ halafu miaka miwili tu baada ya tukio, mwanamasonia huyo akaja na albamu yake inayo kwenda na jina ambalo moja kwa moja linawiana na matakwa, au amri ambayo ilitolewa na wauwaji wale wa kimasonia miaka miwili kabla.


Kwa hiyo nambari tisa (9) ni moja ya namba zenye nguvu sana kwa freemasonry, halikadhalika nambari ambayo inagawanyika kwayo yaani nambari tatu (3).
Nambari hii tisa (9) kama tulivyoona ni namba inayo ashiria hali ya ‘UMILELE’ kwa chochote kile chenye kuhusishwa nacho, na hapa tumeona kati ya vitu ambavyo jamaa hawa wanavihusisha na umilele ni ‘NEW INTERANAL KINGDOM’ au ‘NEW WORLD ORDER’ ambayo wanaifanyia kazi na ambayo waliombwa rasmi kupitia kwenye luninga kuandaa mazingira ya KINGDOM hiyo KWA IBADA YA KIMASONIA ILIYO FANYWA LIVE KWENYE LUNINGA, IBADA AMBAYO ILIFAHAMIKA KWA WANAMASONIA ZAIDI, TENA MASONIA WA DARAJA LA JUU KUANZI 30 NA KUENDELEA.

TUMEONA MMOJA WA WANACHAMA WALIYO UFANYIA KAZI UJUMBE HUO KWA NAFASI NA KAZI YAKE NI MSANII JAY-Z ALIPOKUJA NA ALABAMU MIAKA MIWILI BAADA YA TUKIO, ALBAMU AMBAYO KIMAJABU AJABU, IMEBEBA JINA SAWIA NA UJUMBE ULIOTOLEWA NA WAUWAJI WA NICK ‘KINGDOM COME’

JAY-Z NI MFUASI WA DARAJA LA CHINI ASINGEWEZA KUELEWA MAANA HALISI YA IBADA ILE YA KIMASONIA, LAKINI KIKAWIDA WATU KAMA JAY-Z NA WENZAKE VILE WANAVYO VIFANYA, KAMA WALIVYO FANYA WAUWAJI WALE HUWA NI AMRI AU MAELEKEZO KUTOKA JUU, AU KUTOKA KWA YULE AMBAYE ANASIMAMIA SHUGHULI ZAO, AMBAO WAO WANAKUWA NA PICHA KUBWA YA NINI KINAENDELEA.


Katika ulimwengu wa kishirikina na ulimwengu wa kimasonia nambari kumi na moja (11) inafahamika kama nambari kuu ya kishetani, katika kazi yetu hii ya leo, tutaitizama nambari kumi na moja na kazi yake kwenye tukio la kupigwa kwa minara miwili ya WTC.

Nambari 11, kwenye duara la wenye kufuata elimu ya kishetani inafahamika pia kama zawadi na urithi kutoka kwa yule anayefahamika kama ‘LIGHT BEARER’ au ‘MBEBA NURU’, hili ni jina kabisa lililotafsiriwa kutoka kwenye lugha ya Kiyahudi, unajua kwenye Kiyahudi LIGHT BEARER NI NANI?


LIGHT BEARER NI LUCIFER


Lakini pia unapotizama duara la vikundi vya nyota 12, maarufu kama Zodiac, kikundi cha 11 kwenye duara hilo kinafahamika kama AQUARIUS, na kipindi tulicho nacho sasa utakuwa umeshasikia na utaendelea kusikia mengi kuhusiana na kiile kinacho fahamika kama ‘NEW AGE’ au zama mpya, hii ni kwa vile freemasonry na wale wote wenye kufuata mila za kishetani kutoka Babiloni wanaamini kuwa tupo kiuhakika katika zama za AQUARIUS, tupo kwenye ZAMA MPYA, zama za kumpokea Masih, Masih wa zama mpya, masih wa NWO.
JE UNAMJUA MASIH WA NWO?

NAJUA UTAULIZA HILO SWALI!

SI MWINGINE BALI NI DAJJAL, PIA ANAJULIKANA KAMA ANTI-CHRIST, AU MPINGA KRISTO.


Lakini kile ambacho wengi wanashindwa kukifahamu au wanasema kile ambacho hawakifahamu ni kuwa MASIH-DAJJAL AU ANTI-CHRIST SIYO SAWA TUNAVYO TAFSIRI MAJINA YAKE HAYO AMBAYO YAMEKUJA KUTOKANA NA SIFA ZA MAUMBILE NA TABIA ZAKE. KABISA, KABISA NAFASI YAKE NA SHUGHULI ANAZO TARAJIWA KUZIFANYA HAZIMUWEKI KWENYE CHEO CHA KUMPINGA KRISTO (ISSA MWANA WA MARIAM), HAPANA NA HII NDIYO HASA MAANA YA NAMBARI 11.


MAANA YAKE NI IPI?
MAANA YAKE NI KUWA, NAMBARI 11, INASIMAMA KAMA ALAMA YA MFANANO, UWILI, KINZANI AU NGUVU MBILI ZENYE UWIANO ULIO SAWA LAKINI ZINAZO KWENDA NJIA MBILI TOFAUTI, YAANI NYEUPE NA NYEUSI, MCHANA NA USIKU, KIZURI NA KIBAYA N.K.

HIVYO BASI TUNAPO SEMA TUPO KWENYE ZAMA AMBAZO ILLUMINANTI WANAMTEGEMEA KRISTO WAO KUWA YUPO NJIANI, DAKIKA YEYOTE ATAINGIA KWENYE ULIMWENGU WETU HUU WA 3D, ZAMA AMBAZO KWENYE DUARA LA ZOADIC ZINAWAKILISHWA NA ALAMA YA AU KIKUNDI CHA NYOTA CHA AQUARIUS, ZAMA AMBAZO NAFASI YAKE NI NAMBARI 11, ZAMA ZA DAJJAL, HAIMAANISHI KUWA DAJJAL NAFASI ATAKAYO KUJA KUICHUKUA NI KUMPINGA ISSA MWANA WA MARIAM, HAPANA LAKINI ATAKUJA KUJIFANANISHA NA ISSA MWANA WA MARIAM.

Na hii utaona katika kazi ambazo Dajjal atakuja kuzifanya ni kuwarubuni watu kuwa yeye ni Kristo, na hatofanya chochote kumpinga, ila Kristo mwenyewe, Issa mwana wa Mariam ndiye atakaye kuja kumpinga na hatimaye kumuuwa Dajjal. Hivyo Dajjal atakapo kuja, kama ilivyo nambari kumi na moja, atakuja kujifananisha na Kristo. Kama ambayo maana nambari kumi na moja inavyo tumika kumfananisha Shetani na Mungu Mmoja, na kumpa Shetani nguvu na mamlaka sawa na yale ya Mungu Mmoja.
Katika kitabu cha Isaya tunakutana na maneno haya,

“Nawe ulisema moyoni mwako (Lucifer), nitapanda mpaka mbinguni, nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; nami nita keti juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vua mawingu. NITAFANANA NA YEYE ALIYE JUU.” Isaya 14:13


Umemsikia Lucifre baada ya kushushwa kutoka mbinguni kile alicho kisema, kwamba ANATAKA KUFANANA NA YEYE ALIYE JUU, tunafahamua aliye juu ni ninani, ni MUNGU MMOJA, hivyo Lucifer anataka kujifanannisha na MUNGU MMOJA, kama Dajjal anavyo taka kujifananisha na Masih mwana wa Mariam, na hii ndiyo maana hasa ya nambari 11.





Hivyo basi unapo chukua nambari 9 ukaiweka pamoja na nambari 11, kwenye ulimwengu wa kishetani unapata zaidi ya nambari zilizo pangwa. Kama tulivyo ona nambari 9 kazi yake ni, au maana yake halisi ni kuharibu, utawala uliuopo, mfumo uliopo kwa kukisimamia kiapo cha kimasonia, na wakati huo huo, nambari 11, ikiwa na maana ya kusimamisha utawala mpya, utawala ambao utakuwa sawa na utawala wa Mungu Mmoja, lakini huu ni wa kishetani.

 Hivyo kuangushwa kwa minara ile miwili, hii ilikuwa ni ujumbe kuwa tumeshaibomoa, au tumeshauvunja utawala wa Mungu Mmoja na sasa tunasimamisha Utawala wa Lucifer, na tangu baada ya tukio lile tumeona dunia imegeuka kuwa mbaya mara dufu, serikali moja baada ya nyingine zinapinduliwa kutengeneza njia ya ujio wa serikali moja duniani kote, serikali ya Illuminanti, serikali ya Dajjal.

MPENDWA MSOMAJI NISINGEPENDA UAMINI HAYA NINAYO YAANDIKA HUMU, LAKINI NATAKA UYAELEWE ... KWA AJILI HIYO BASI HAPA CHINI NITAWEKA KWA UPANA ZAIDI NAMBARI 11 na maana yake HALISI YA KUTUMKA KATIKA KUFANIKISHA TUKIO LA WTC...

Kilicho tokea 9/11 ilikuwa ni moja ya ibada kuu kuliko za kishetani.... moja ya ibada muhimu kuliko kutiririsha nguvu za kiza kwenye uso wa dunia....

Kwa kawaida nembo au alama fulani huwa ni mbadala au kiwakilishi cha kitu fulani, hivyo navyo nembo za kimasonia popote zinapo kuwepo, huwepo kama mbadala wa kile kilicho kusudiwa, mathalani katika kila hekalu la kimasonia panakuwepo na nguzo mbili zimesimama, nguzo hizo wanasema zinawakilisha nguzo zinazo patikana ndani ya hekalu la Mfalme Solomoni (Freemasonry ni wazushi na waongo na wamemzushia mtume huyu wa Mungu Mmoja kwamba alikuwa ni mchawi na mshirikina na kwamba alikuwa ni freemason).

Hivyo basi nguzo hizo mbili kwa namna mbalimbali kote duniani zimekuwa zikisimamishwa kwa njia mbalimbali, na katika miji ya kisasa hutakosa aina hii ya majengo ambayo huwakilishwa na majengo pacha, na minara miwili ya WTC, ni mfano mzuri wa nguzo hizo mbili ambazo freemason wanaziitikadia. Lakini pia kwa upande mwingine nguzo hizo mbili huhesabiwa kama tatu, na hii ni kwa uwiano wa Piramidi tatu zinazo patika kwenye uwanda wa Gaza, Egypty. Unapo jumlisha uwazi uliopo baina ya nguzo mbili hizo, basi huhesabiwa kama ni nguzo tatu.


Kama tutarudi kwenye asili hasa ya nguzo hizo mbili, ambako ni Egypty, ni kwamba Piramidi zile moja ya kazi yake kubwa ni kufungua kile kinacho fahamika kama ‘STAR GATE’

STAR GATE, ni njia ya kuelekea kwenye uwanda mwingine wa kimaumbile, sisi tupo kwenye uwanda wa 3D. Lakini pia ni mlango wa kuelekea kwenye kile kinacho fahamika kama ‘Higher Counseousness’

Hivyo basi kuangushwa kwa minara ile miwili pia tunaweza kusema ni alama ya kufunguliwa kwa Star Gate.


Jua hukamilisha mzunguko wake baada ya miaka 11, hata hivyo mzunguko wa mwisho wa jua ulikadiriwa utatokea baina ya mwaka 1989 au 1990. Halafu mzunguko utakao fuata utakuwa ni mwaka 2000 au 2001.
Mwaka 1990, katika bunge la Marekani, raisi wa kipindi hichi, Bush Sr. Alitoa hotuba maarufu, hotuba ambaye iliashiria kutangazwa kwa mchakato wa kuelekea kwenye New World Order, hutuba hiyo ilikuwa ni tarehe 9.11.1990, baadhi ya vitu alivyo sema kwenye kauli hiyo ni “... what it takes ? It’s more than a small country, it’s a big idea, a NEW WORLD ORDER ...”

Halafu baada ya miaka 11 kamili, au baada ya jua kukamilisha mzunguko wake, ibada kubwa ya kishetani ikafanyika kufungua milango kuelekea kwenye NEW WORLD ORDER. Ikafanyika tarehe 9.11.2001


Unamkumbuka babu yake na Bush Jr, au Baba yake na Bush Sr, ambaye aliandika kitabu cha kishetani alicho kiita ‘Book of Law’ wakati alipokuwa ndani ya Piramid la Gaza, hiyo ilikuwa ni mwaka 1904 baada ya kufanya meditation ndani ya King Chember, kwenye Piramid la Gaza, alipokea ufunuo wa kitabu hicho, huyu ni Aleister Crowley, 

Au pia alifahamika kama 666, alisema kuwa aliwasiliana akiwa hapo na kiumbe kinacho fahamika kama Oz, kwenye kazi zake pia alitumia alama hii...




Moja ya maana inayo patikana kwenye nambari hii Ni sawa na nambari 777 na pia kuwa na mahusiano na mungu anaye fahamika kama PAN.




Aleister Crowley akachora aina hichi cha kiumbe chenye maarifa lakini kisicho kuwa binadamu ambacho alikiri kukiona wakati akifanya ibada zake humo.



Sasa turudi kwenye 9/11
Kabla tukio lile halijatokea, au kabla ibada ile ya kishetani haijaanza, mjukuu wa Aleister Crowley alikuwa kwenye shule ya watoto na alikuwa akiwasomea hadithi...



... Unafahamu ni hadithi gani Bush alikuwa akiisoma, kabla ya kufanyika kwa ibada kuu ya kishetani, ibada ambayo itaadhimisha miaka 11 ya mzunguko wa jua, ibada ambayo itafungua milango ya NEW WORLD ORDER, Ibada ambayo itafungua mlango wenye nguvu za giza katika uso wa dunia ... unajua ni hadithi gani Bush Jr, alikuwa akiisoma?

Kwa vile ushahidi upo wa kutosha kwamba si kwamba tu Bush alifahamu juu ya tukio hilo, lakini zaidi ni kwamba yeye na utawala wake walishiriki kikamilifu kuhakikisha hilo linatokea kama lilivyo pangwa, na zaidi ya yote kwake yeye na familia yake, na Illuminanti wengine tukio lile lilikuwa ni ibada maalum ya kufungua milango hiyo niliyo itaja hapo juu, Je katika wakati muhimu kama huo unadhani Bush alikuwa akisoma hadithi gani kwa watoto wale...?

Alikuwa anasoma kitabu kinachoitwa ‘MY PET GOAT’, Kitabu hichi kilisha pigwa marufuku kutokana na maudhui yake ya kishetani na ibada za kishetani zinazo tajwa humo kama zawadi kwa mungu anayefahamika kama PAN.



Utamkumbuka mungu huyu PAN ndiye aliyempatia Aleister Crowley babu yake na Bush ufunuo wa kuandika kitabu cha kishetani kinacho kwenda kwa jina la ‘BOOK OF LAW’, na mungu huyu huchorwa au kuoneshwa katika maumbile mbalimbali lakini akiwa na KICHWA CHA MBUZI, hivyo kichwa cha mbuzi pia hufahamika kama ‘GOAT OF MEANDEZ’ na huwakilishwa na picha au mchoro wa nyota yenye ncha TANO lakini iliyo elekezwa chini, nacho hufahamika kama ni kichwa cha SHETANI.




Hivyo basi wakati na kabla ibada hiyo kuu ya kishetani haijaanza, Bush Jr, alishatia ‘Tabaruk’ ya tuko hilo kwa kuanza kuwasomea watoto hadithi za MBUZI, ambazo ni zawadi kwa mungu PAN, kwa maneno mengine Bush Jr, aliaanza kumtukuza mungu PAN, au shetani mwenyewe, hadharani, mbele ya vyombo vya habari, mbele ya watoto wadogo, mungu PAN, na kuzitaka baraka zake kabla ya tukio lenyewe kuanza.
Huwezi kuamini, nami sitaki uamini, ILA uelewe, kwamba katika vitabu vyote vya watoto vilivyopo kwenye uso wa dunia, Bush hakuona kitabu bora zaidi cha kuwasomea watoto asubuhi ile, isipokuwa kitabu ambacho ni zawadi kwa mungu PAN, mungu aliyempatia Babu yake na Bush ufunuo wa kuandika kitabu cha kishetani.

Maneno yaliyopo kwenye kitabu hicho, ndiyo maneno ambayo darasa zima lilikuwa likiyatamka, wakiongozwa na Bush mwenyewe wakati tukio hilo, au wakati ibada hiyo kuu ikichukua nafasi yake. Unaweza kuona ni namna gani maadui zetu walivyo jipanga, ni namna gani walivyo makini katika kutekeleza ibada kwa miungu yao, tukio kubwa kabisa la kufungua milango ya kiza linafanyika, na mungu mwenye dhamana hiyo, au shetani mwenyewe anaombwa, tena na watoto, walimu, na kiongozi wa taifa kubwa duniani, mbele ya kamera, kuikubali na kuipokea ibada hiyo ‘takatifu.’



BUSH, AKILIONGOZA DARASA KUMTUKUZA PAN, MUDA MCHACHE KABLA YA 9/11

Freemasonry na wafuasi wengine wa aina hii ya ibada hupendelea kuzigeuza alama zao kinyume nyume, au juu chini, na chini juu, hii ni desturi ya kishetani, na Bush hakuwa amelisahau hili, pia, hasa kwenye tukio muhimu na ibada ‘takatifu’ kama hiyo, desturi hii ya kishetani haikurukwa ... Bush alikuwa akikisoma kitabu kile CHINI JUU, JUU CHINI.


UMEONA HAPA BUSH ANAKISOMA KITABU JUU CHINI NA CHINI JUU, MILA NI MUHIMU SANA KWA HAWA JAMAA ...

Utakumbuka moja ya vitu ambavyo tulivitaja huko nyuma kuwa vinawakilishwa na ile minara miwili ni NGUZO MBILI KWENYE HEKALU LA ‘SULEIMAN’ au KWENYE HEKALU LA KIMASONIA,




Pia nguzo hizo zinafahamika kama JACHIN na BOAZ,





Minara hiyo miwili pamoja na sehemu ya kuingilia ndani ya hekalu la ‘suleiman’ ilifahamika kama ‘THE GATE’ kwenye lugha yetu tungeita ‘MLANGO’

Minara hii miwili inafahamika kama Emirate Tower




DUBAI YA LEO HIYO


Ila utajiuliza swali moja, mbona ni kanuni hiyo hiyo ya ujenzi wa minara miwili mirefu utaikuta kwenye kila kona ya majengo katika miji yetu ya kisasa?










Lakini unafahamu wanaiita jina gani, wanapo jumuisha minara hiyo na sehemu yake ya kuingilia?


Wanaiita jina lilelile walilo kuwa wakilitaja huko Egypty kwenye dunia ya kale, ‘THE GATE’


Kama minara ile miwili ilikuwa ni MLANGO, basi ulikuwa ni mlango wa kwenda wapi?, Sote tunajua unapovunja mlango basi unapita au kitapita kile kilicho kusudiwa kupita au kilicho kuwa kikizuiliwa kisipite kwenye MALANGO huo.

Unakumbuka ni eneo gani lingine liligongwa na ndege zile?

Sehemu nyingine iliyogongwa ilikuwa ni PENTAGON.

Pentagon nayo umbo lake ni mfano wa nyota, lakini siyo nyota ya kawaida, bali nyota inayo itikadiwa kuwa ni nyota ya KISHETANI, Nyota yenye ncha tano, nyota ya kichwa cha mbuzi.


Ibada hii ililenga kufungua kile kinacho fahamika kama STAR GATE, Kwa madhumuni ya kufungua chaneli za kiza katika uso wa dunia zitakazo wawezesha ILLUMINANTI kusimamisha NEW WORLD ORDER, kwa vile kadiri kunapo kuwepo na nguvu za kiza nyingi ndipo na nguvu za hawa jamaa zinapo zidi juu yetu, na sote tumeshuhudia ni damu kiasi gani imemwagika na inaendelea kumwagika baada ya tukio lile, ni uharibifu kiasi gani umefanyika na unaendelea kufanyika kwa jina la tukio lile, ni vifo kiasi gani vimetokea na vinaendelea kutokea kutokana na tukio lile, ni vilema wangapi wanazaliwa na wataendelea kuzaliwa kutokana na tukio lile na ... na ... na ...


Ninacho kieleza hapa kwa mnasaba wa 9.11, ni kuwa pale ambapo unapo taka kuwatambua maadui zetu, kuwatambua viumbe wanao shirikiana nao, viumbe kutoka kwenye uwanda mwingine, viumbe kutoka kwenye dimensional tofauti na hii ya kwetu, yaani unapo shughulika na majini au mashetani. Unapo taka kuwafahamu Illuminanti au watu ambao wanayo aina fulani ya elimu na maarifa ambayo kwa wengine hawana ...


Jamaa hawa wamechagua lugha nyingine tofauti kabisa na lugha inayo fahamika kote ulimwenguni, lakini ni lugha ambayo ni wachache sana wanaifahamu, lugha ambayo imevuka mipaka, mataifa na makabila, lugha ya nambari na maumbo.


Utakuta wanafanyia kazi aina hii ya elimu ambayo utaisikia wakiita SECRET NUMEROLOGY na SECRET GEOMETRY.

Hii inamaanisha nini basi, hii inamaanisha kuwa kila nambari, inayo maana yake maalum iliyo pewa, kila umbo limepewa maana yake maalum, maana ambayo inawasilishwa au inakuwa ndiyo ujumbe au mawasiliano ambayo yanapatikana pale ambapo nambari au umbo linapo wekwa, andikwa au kuchorwa.

Hivyo basi katika maana hizo, tunakuta kuwa nambari 10, ni ALFA na OMEGA, au Mungu, na nambari 11, ni hatua au sehemu iliyopo juu ya Mungu, au 101 ni juu ya Mungu.


Hivyo basi unapo toka kwenye na kurukia kwenye 11 bila kwenda kwenye 10, ni sawa kwenye lugha hii na kumruka Mungu, umetoka kwenye na hukwenda kwenye 10, bali umekwenda kwenye 11, yaani umemruka Mungu na kwenda kwa yule ambaye eidha anajifananisha na Mungu au anajinasibisha au wewe unamnasibisha kuwa yeye yupo juu ya Mungu.




Hapa tunasema unamjaribu Mungu, unampa Mungu changamoto, ndicho wanacho kifanya katika lugha hii. Hivyo tukio la 9.11 lililotokea kwenye 9.11 yenyewe lilikuwa ni jaribio kwa Mungu na kwa wale wanao muamini Mungu ... na historia inathibitisha hii haikuwa mara ya kwanza kumjaribu Mungu ...
Ukiwa unafahamu nini maana hasa ya 9.11, jiulize kwanini nambari ya dharura, nambari ya kutaka msaada kwa baadhi ya nchi ni 911?
Yaani unapo taka msaada, unapokuwa kwenye wakati wa shida usielekee kwa mwingine ila kwa yule ambaye wao wana muitikadia kuwa yupo juu ya Mungu ...

















Ukiwa na shida elekea kwa Shetani na utasaidiwa, hii ndiyo maana ya kupiga 911 wakati wa dharura.

Sasa mpaka utakapo elewa ni namna gani adui yako anafikri ndipo utakapo weza kupambana naye, na hivyi ndivyo maadui zetu wanavyo fikiri 

1 comment:

  1. ASANTE SANA KWA POST ZAKO!
    NIMEKUA NIKIFUATILIA MAMBO MENGI SANA JUU YA HAWA MABWANA!TOKA 2012!
    PIA UMENISAIDIA KUPATA VIPYA THAT I DIDNT GET BEFORE!

    SASA NAWEZA PATA SABABU YA MICROSOFT WINDOWS KURUKA *WINDOWS 9* BADALA YAKE WINDOWS 10

    ReplyDelete