Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Tuesday, August 13, 2013

HATUA NNE KABLA YA UJIO WA MASIHDAJJAL/KRISTO WA UWONGO/MPINGA KRISTO/666


PROJECT BLUE BEAM

Waandishi wawili wa habari waliokuwa wakifuatilia sakata ya hichi tunacho kizungumzia hivi sasa au maarufu kama Blue Beam wote wawili walikutikana wamekufa kwa ‘ugonjwa wa moyo’ ingawa kwenye historia yao hawakupata kuwa na magojwa ya moyo. Vifo vyao vilitofautiana kwa wiki kila mmoja.

Sege Monast alikuwa ni mwandishi wa Internationa Free Press Canada, huyu ni mmoja kati ya waandishi wawili walio kutwa wamekufa kwa ‘ugonjwa wa moyo’.

Moja ya wadau wanao isimamia Project Blue Beam ni NASA, na mradi huu umegawanywa katika sehemu nne ambazo zitafanikisha kuisimamisha New World Order na Masih Dajjal/Kristo wa Uwongo akiwa ndiye kiongozi wa serikali hiyo.



HATUA YA KWANZA
Hatua ya kwanza kabisa ya NASA Project Blue Beam inahusiana na  uharibifu wa elimu sahihi ya historia na ushahidi wake. Kimsingi hatua hii itakuwa inashughulikia kuonesha au kuthibitisha kuwa maneno, hadithi na utabiri wa vitabu vya dini ni makosa ya kufasiriwa vitabu hivyo au pia ni uwongo kwamba vitabu hivyo havina dira sahihi kwa mwanaadamu.



Hatua hii itahusisha ‘matetemeko ya aridhi’ ya kutengeneza, ‘ugunduzi mpya’ ambao utakuja na taarifa tofauti na zile zinazo patikana katika vitabu vya dini mbalimbali. ‘Ugunduzi’ huo utakuwa ukiwaambia watu kuwa vitabu hivyo havina usahihi wala umakini wowote, kwa maneno mengine ulimwengu uachane kabisakabisa na vitabu hivyo pamoja na imani ya kuwa kuna Mungu Mmoja kwa vile vitabu hivyo kwenye ‘ugunduzi’ mpya vinaonekana siyo kitu bali urongo mtupu.



Mathalani eneo fulani kutokana na vitabu vya dini fulani waumini wake wanaamini kulitokea tukio fulani, au kutatokea tukio fulani, Project Blue Beam kazi yake ni kuonesha mambo tofauti na vitabu hivyo, na mambo hayo yataitwa ‘ugunduzi wa kisayansi’ na hivyo dini ambazo wakati mwingine zinaonekana kimakosa kuwa zinakwenda kinyume na sayansi zitakuwa zinasambaratishwa hatua kwa hatua na waumini wake kukosa imani na dini zao.



Hiyo ndiyo hatua ya mwanzo kwenye Project Blue Beam kwa vile kile ambacho wao wanataka kukiondoa si kingine bali ni imani za dini zote ulimwenguni na kuwapatia imani ya dini mpya, New Age Religion’ ambayo itakuwa si nyingine bali ni dini ya ‘Ushetani.’
Kwa sasa Illuminanti wanamiliki teknolojia ya kutengeneza ‘Mitetemeko ya Aridhi,’ na pia teknolojia ya kubadilisha hali ya hewa, wanayo na wamepiga kimya kwa vile hiyo ni silaha na mara kwa mara wamekuwa wakizitumia au kuzijaribu maeneo mbalimbali duniani, wanataka wao wawe ndiye mungu kabla ya kumsimamisha mungu wao ambaye ni Masih Dajjal/ Kristo wa uwongo.



Hatua hii inahusisha vita vya kisaikolojia ambavyo vitakuwa vikiandaa akili za watu kukubalina na hatua tatu za mwisho zitakazo fuata.

Kuna kile kinacho fahamika kama HAARP, KIFUPI MTAMBO HUU UMETENGENEZWA KUFANYA KAZI UKIWA NA NGUVU MFANO WA ZILE ZA JUA. NAKUACHIA HOMEWORK, NENDA KATAFUTE KUHUSIANA NA HAARP, NAMNA IANVYO FANYA KAZI NA MADHARA YAKE.

HATUA YA PILI.
SPACE SHOW
Anga litakuwa ni mfano wa kioo kikubwa cha luninga, kama umepta kutizama ‘series inayo kwenda kwa jina la V’  Series hii ni moja ya kazi zao dhidi yetu sisi, maadhui yake tutayazungumzia huko mbele isipokuwa hapa nataka nikukumbushe tukio moja kwenye series hiyo ambapo ‘wageni’ wale kutoka sayari ya mbali walipofika, kwanza kabisa walizungumza na walimwengu kwa kutumia chombo chao ambacho kiligeuka na kuwa mfano wa luninga kubwa iliyopo angani, na luninga hiyo iliweza kuonekana kupitia vyombo vyao vingine vilivyo kuwa katika miji mingine duniani. Watu waliwaona ‘wageni’ na kusikia sauti zao.


SPACE SHOW ya Project Blue Beam nayo itakuwa hivyohivyo, ispokuwa yenyewe itakuwa bora zaidi kwa vile hakutakuwa na chombo cha wageni na maumbile ya wahusika wataonekana kwenye maumbo ya 3D na sauti zao zitasikika vyema.
Sehemu tofauti za dunia wataona maumbo tofauti kulingana na imani za watu husika la lugha zao. Kuna ambao wataletewa umbile la Yesu, wengine Mahdi, wengine Krishina, wengine Budha na wengine Muhammad, na ‘watu’ hawa yatazungumza kwa lugha mbalimbali kulingana na jamii husika.


Silaha itakayo tumika kufanya kazi hiyo si nyingine bali ni HAARP. Itatengeneza kile kinacho fahamika kama HOLOGRAM angani.
‘Wateule’ hao watakuwa na ujumbe wa aina moja ingawa katika lugha na tafsiri tofauti kuwalika watu kwenye New World Order, walimwengu wataambiwa wale ambao mlio kuwa mnawangojea kwa ajili ya kuwaokoa wameshafika, wapokeeni, Mashia watapelekewa Mahd wao ambaye wanasema yupo pangoni anasubiri tu muda ili aje, Waislamu wa madhehebu mengine watapelekewa, Mahd ambaye tunaitikadia atakuja, Wakristo na Wayahudi watapelekewa Yesu. Anga ndilo litakalo tumika kama kioo cha sinema hizo.

Kama tulivyo ona leo kuna watu wanasikia sauti zikiwaongoza na wanaamini kuwa wao ni ‘wateule’ au wao ni watu maalum, kuna ambao wanakuambia wameshamuona Yesu (Rehma ziwe juu yake) kwa macho yao na wanazungumza naye, kuna wanao kuambia wao kila siku wanaonana na Muhammadi (Rehma na Amani ziwe Juu Yake) na anawapa miongozo mbalimbali, lakini tutafikia mahala matukio hayo yatakuwa ni ya kiulimwengu zaidi, kila mtu ataona kama tunavyo liona jua, na atasikilizishwa kwa lugha yake kama tunavyo sikiliza redio juu ya ujio wa mwokozi wetu, ambaye hatakuwa mwingine bali ni Dajjali / Mpinga Kristo/Kristo wa Uwongo.



Kama kawaida tutakuwepo wale tutakao pinga, wale ambao tutasema hilo silo ni uwongo mtupu, lakini taarifa zetu hazitopewa maana yoyote ile kwenye chombo chochote cha habari na tutaonekana kama wavunjaji sharia, au magaidi. Pia watakuwepo ‘waumini’ bandia, ambao wao watatumia vitabu hivyohivyo vitakatifu kukubaliana na hali hiyo ya kutengenezwa, hawa taarifa zao zitapewa kipao mbele kwenye vyombo vyote vya habari, huo utachukuliwa kama ukweli wa msingi. 

aina hii ya mfumo wa habari si ngeni hasa kwa wanaharakati, hapa kwetu tume uona na bado tunaendelea kuona ukifanywa dhidi ya jamii fulani kwa ajili tu ya kuendelea ‘kuwachinjia baharini’.

Mwaka 1974 mtafiti G.F Shapits alisema,

“… katika utafiti huu itaonekana kuwa ile sauti ambayo mlengwa anaisikia ni kuwa inaweza kuwekwa katika hali ya kiumeme na kutumwa moja kwa moja kwenye subconscious level ya ubongo bila kutumia kifaa chochote cha kimakanika kwa ajili ya kupokea na kutafsiri ujumbe huo kwenye ubongo na bila ya muhusika kuweza kuzizuia taarifa hizo zilizotumwa kwenye ubongo wake bila yeye kufahamu…”
Blue Beam Project pia itatumika kupandikiza mawazo ya uwongo na mawasiliano yasiyo sahihi kwa kutumia mawimbi ya mawasiliano yatakayo tumwa kupitia ELF, VLF, na LF yatawafikia kila mtu na kwenda moja kwa moja kugonga kwenye ubongo kana kwamba hicho anacho kiona au kukisikia muhusika ni kweli, na taarifa hizo zitamfanya ahisi kuwa anaongea eidha na Muhammad, Yesu, Buddha, Jah na hata Mungu mwenyewe, teknolojia hii ipo na siyo hadithi za kufikirika za kisayansi. Sehemu mbalimbali duniani zipo kompyuta kubwa ambazo zimebeba taarifa za kila raia duniani na mpaka lugha zao, kompyuta hizi hufanya kazi kwa kutumia satelaiti ni kwa kutumia kompyuta hizo ndipo aina hizi za taarifa hutumwa kwa walengwa.


Sizungumzii mambo yatakayo kuja kufanyika siku zijazo, ila mambo yanayo fanyika sasa. Binafsi nimeshakutana na watu wawili ambao wanapokea aina hizi za taarifa, na ninakueleza ni vigumu kumshawishi mtu huyo vinginevyo, ni vigumu kumuambia kuwa anacho kisikia ni kazi ya watu fulani mahala fulani, ni ngumu. Si wote wanao sikia sauti kwenye akili zao ni mawasiliano ya ELF, VLF na LF, hapana wengine ni kweli akili zao tayari zina matatizo na wengine ni ushawishi wa majini ambao wao wanadhani ni neema. Hivyo inahitaji uangalizi wa kina kabla ya kufahamu athari iliyo tengenezwa kwa mtu kupitia Illuminati na teknolojia yao na athari iliyo tengenezwa na mashetani.

Kibaya zaidi na cha kutisha zaidi kwenye aina hii ya teknolojia, hasa inapo tumika dhidi ya binadamu, na rafiki yangu nakuambia hajatengenezewa mwingine ila binadamu ni kuwa inanyakua thamani yako wewe kuitwa binadamu. Inanyakua uhuru wako. Uhuru wako ndiyo mstari mnene na mweusi tii, unao kutofautisha wewe na viumbe wengine, ukiwaacha majini ambao nao wana sifa hiyo. Kama kuna kitu ambacho thamani yake ni kubwa kuliko vyote ulivyo navyo ni; Uhuru, yote uliyo pewa na majukumu yako yote ni kwa sababu wewe u-huru. Bila ya uhuru tofauti yako wewe na kiumbe chengine chochote ukitoa majini, haipo.


 Teknolojia hii itakuja kuuchukua uhuru wako, utadhani mawazo na maneno unayo toa ni yako, utadhani nguo unazo vaa ni chaguo lako nakadhalika, lakini hayo ni maamuzi ya watu Fulani walio kwisha amulia maisha yako na wanakuongoza vile watakavyo. Hautakua huru kuamua unacho taka kama binadamu bali utaongozwa punde tu kama kundi la kondoo nyuma ya mchungaji wao, wakati huo wachungaji ni Babyloni Brotherhood.


Walimwengu haiwaingii akilini kama kuna aina hii ya teknolojia achilia mbali kuamini, na mimi sitaki uamini bali uelewe na akili yako huru. Watu wanapo dhani aina hii ya teknolojia haiwezekani kwa sababu yoyote ile, watu hawa wanawarahisishia kazi maadui zetu, kwani pale silaha hizo zitakapo anza kutumika kwa ajili ya kuwafunga walimwengu wote kwa ujumla wake, watu hawa watakuwa upande wa Babyloni Brotherhood, watu hawa wataamini kile wanacho kiona na kukisikia, watawapokea Masihi na mitume wa uwongo na watachana na imani zao kwa ‘kufikiri’ mafundisho yake yalisha kosewa tangu zamani.

HATUA YA TATU
ALIEN INVASION

Kwa kutumia Blue Beam Project maadui zetu watatengeneza kile ambacho dunia wataona ni uvamizi kutoka ‘nje’ ya sayari yetu, ‘uvamizi’ wa viumbe wasio julikana. ‘Uvamizi’ huo wa kutengeneza utasababisha mataifa yote yenye silaha za nyuklia kutumia silaha zao dhidi ya ‘uvamizi’ huo na ambapo maafa makubwa yatakuwa dhidi ya binadamu kwani kiuhakika kabisa hakuna uvamizi wowote. Mahakama ya Umoja wa Mataifa itazitaka nchi ambazo zimetumia silaha zao za kinuklia dhidi ya ‘uvamizi’ huo feki, kuziharibu silaha hizo mara moja. Hii itakuwa ni hatua muhimu sana nchi mbalimbali duniani zina nyang’anywa silaha zao, hii ni kwa ajili ya kuondoa kitisho chochote kile dhidi ya serikali mpya ambayo punde tuu itawekwa hadharani. 



Sharia hii haitazigusa nchi peke yake bali mpaka wananchi wake, watu wote duniani hawatatakiwa kumiliki silaha, lengo ni lile, lile kuondoa aina yoyote ile ya vikwazo kwa serikali inayo ngojewa.
Kwa Wakristo kuna kitu kinaitwa ‘unyakuo’ kwamba Yesu atakapo rudi atawanyakua wale wateule na kuwapeleka mbinguni kuwaepusha na mabalaa yatakayo fuata kwani hizo ni siku za mwisho na mabalaa yake ni mengi. Wakati Illuminati wakitengeneza ‘uvamizi’ feki pia watatengeneza na ‘unyakuo’ wao, ambapo baadhi ya watu watanyakuliwa na kutiwa kwenye vyombo ambavyo wao wataona ni UFO nakadhalika, kwani Masiha wao amekuja kuwaokoa kutokana na kitisho cha ‘wavamizi’ kutoka nje ya dunia. Lengo la unyakuo huu wa Illuminati ni kuivunja kabisa imani ya Kikristo kwani baadaye unyakuo huo utaonekana ni feki na mafundisho ya Kikristo yata chukuliwa eidha yalidanganya au yalitafsiriwa vile ambavyo sivyo.

Wakati hayo yanatokea, ‘viumbe’ hao ambao wataitwa ‘wavamizi’ toka sayari ya mbali wataonekana katika kila kona ya uso wa dunia, lakini hawatakuwa viumbe asili bali ni maumbo ya holographic ya viumbe hao na mapicha yao kupitia Blue Beam Project, kupitia vyombo na vifaa vingine vya mawasiliano kama nyaya, simu na Luninga vitu hivyo ulimwengu mzima utaonekana kama umepagawa, watu watakuwa wendawazimu, wahubiri wasio jua wanacho kihubiri au kwa makusudi na wasemaji wa dini nyingine wataibuka na kusema huu ndiyo mwisho wa dunia, ni kama wanamwagia mafuta kwenye moto unao waka, watu watajiua, wengine watauwana na kuua wenzao, wengine kisaikolojia watamalizika kabisa na madhila mbali, mbali yatatokea na wakati huo wengine wakishuhudia ‘unyakuo’ wa Illuminati.



Baada ya zahama hili dunia nzima itakuwa tayari kumpokea Masih mpya kwa ajili ya kuwaongoza, kwa ajili ya kuwatoa kwenye zahama hili, hatokuwa mwingine ile ‘mnyama’ ambaye jina lake ni K-F-R au 666 au Masih Dajjal au Mpinga Kristo.

HATUA YA NNE
ANGUKO LA KIUCHUMI LA KIDUNIA.

Kama kawaida zahama hili litaanzia kwenye uchumi, fedha! Kutakuwa na anguko la kiuchumi, nalo la kutengeneza, kama walivyo zoea kuyatengeneza mengine. Nalo hili litapiga dunia nzima, benki zote za kwao, au zinafanya kazi kwa kufuata sharia zao, anguko hili litatengeneza njia kwa ajili ya aina mpya ya sarafu mpya. Lakini kinyume na sarafu tulizo zoea, sarafu hii mpya itakuwa ‘ki-elktronik’. Hutaiona pesa hiyo, wala hutaishika lakini itakuwepo. Baada ya anguko hili watu watazitoa fedha zao kokote zilipo na kununua vile ambavyo wataweza kuvinunua kabla pesa zao hazijapoteza thamani kabisa. 



Watu watatumia fedha zote kununua vitu ambavyo wanadhani baadaye wataviuza na kurejesha pesa zao. Lengo ni kuhakikisha hakuna yoyote anaye bakiwa na hata sumuni ili watu wasije kuzichanga fedha zao na kudhamini watu watakao pambana na serikali mpya. Kila kikwazo kinaondolewa kwa umakini kabisa. Kiasi kwamba kusibakiwe na hata mtu mmoja mwenye uwezo wa kujilisha mwenyewe, pesa haina thamani tena, kila mtu atakuwa anategemea aina fulani ya uongozi ambao utapatiwa mamlaka na nguvu ya kutoa mahitaji ya muhimu kwa watu.


Kuhakikisha kuwa kila mtu atakuwa ameuweka uhai wake chini ya serikali mpya ya Masih Dajjal, Illuminati wamesha tengeneza mpaka Microchip ambazo zitawekwa kwa wanyama pori, ndege na samaki kiasi kwamba ukijifanya wewe huhitaji uwepo wao kuishi na kwamba utakwenda kuwinda au kuvua, na hii inamaanisha kuwa wewe utakuwa umekataa kuwekewa chip, basi punde tu unapo mshika mnyama huyo au samaki au ndege baada ya kumuua kwa kutumia chip ambayo imewekwa kwa viumbe hao watakunasa, sababu itawajulisha wewe ni nani na muhimu kabisa upo eneo gani kwenye uso wa dunia, utakamatwa kwa kuitwa ‘gaidi’ utafungwa au utauwawa.



Hizi ni baadhi ya filamu zinazo elezea ujio wa ‘wageni’ au ni baadhi ya silaha zinazo tumika kwako na kwa familia yako na kwa nchi yako kisaikolojia kukubaliana na ujio huo na kujiandaa kupambana nao, au kujiandaa kuutoa uhuru wako kwa Illuminati na uwe mtumwa wao. 

Baadhi tu ya filamu zao ni hizi, The Day the Earth Stood Still  ya mwaka 1951, War of the Worlds ya mwaka 1953, Close Encounters of the Third Kind  ya mwaka 1977, Star Wars  ya mwaka 1977, Invasion of the Body Snatchers  ya mwaka 1978, E.T.  ya mwaka 1982, Cocoon ya mwaka 1985, Independence Day  ya mwaka 1996, Dark City ya mwaka 1998, Dreamcatcher  ya mwaka 2003, District 9  ya mwaka 2009, Avatar ya mwaka 2009, Cowboys and Aliens  ya Julai 29, 2011, Monsters  ya Oktoba, 2010, Megamind  ya Novemba 5, 2010, Battle: Los Angeles  ya Novemba 12, 2010, Battleship  ya Mei 25, 2012, Paul ya  Machi 18, 2011, Alien 5 ya mwaka 2012, Super 8  ya mwaka 2011, Area 51  ya mwaka  2010-2011, The Darkest Hour ya  Aug 5, 2011, Skyline ya mwaka 2010

Hollywood na makampuni yote ya filamu yapo chini ya Illuminati. Idadi hii kubwa ya filamu na tamthilia kuhusiana na viumbe hawa wa kufikirika, ingawa sasa ulimwengu unaamini kuwa wapo ni kuonesha jinsi gani maadui zetu walivyo jiandaa katika kututengeneza kukubaliana na uwongo wao, kuwa kuna viumbe wengine nje ya sayari yetu ambao muda wowote wanaweza kutuvamia na viumbe hawa ni hatari na mwokozi wetu ni umoja wetu chini ya serikali moja ya dunia.


Lengo si kukufanya uamini haya, narudia tena, lengo si kukufanya uamini haya niliyo yaandika, kuna mabuku rejea ipomitandao ya internet, chukua muda wako, kafanye utafiti wako binafsi na huenda ukaja na suluhisho bora juu ya tatizo linalo ikabili dunia, kuliko kupinga na kubisha kibubusa.


1 comment:

  1. Nakubaliana na unachokisema 99%,kwani nimechunguza,na hadithi zimeshafika kila kona ya dunia

    Na nakuomba kushare nakala zako kwenye mitandao ya kijamii,mfano Facebook.

    ReplyDelete