Laika ni mbwa wa kwanza kwenda mwezini kwa majaribio na alikufa baada ya
masaa machache ya kuizunguka dunia nje ya anga lake kama ambavyo walivyokufa
wanaanga wa Kirusi waliojaribu kufanya hivyo mpaka mwana anga mwingine wa
Kirusi Yuri Alekseyevich Gagarian alipofanikiwa kutudanganya kuwa amefanikiwa
kufanya hivyo mnamo mwaka 1961 baada ya kuruka katika upeo ambao ulikuwa ni
salama, hakufika mwezini ila anahisabiwa kama binaadam wa kwanza kwenda kwenye
anga (Space). Uwongo hata katika hilo anga hakufanikiwa kufika.
Ukitizama picha ya mfumo wa Jua na sayari zake utaziona hazitofautiani
sana, lakini ukiitizama sayari moja kati ya hizo utaiona hii imejitenga zaidi
na nyingine kwa utofauti, sayari hii ni Dunia yetu, imejaa maji kuliko aridhi,
ina hewa mbalimbali ambazo zinasaidia kuwepo kwa maisha kwenye nyumba hii,
wingu hilo la hewa mbalimbali limekaa kama blanketi ambalo linaikinga Dunia
yetu na miali ya moja kwa moja ya Jua.
Blanketi hilo la hewa linapoharibiwa
basi hatari ya maisha kutoweka inakuwa
kubwa, mnamo mwaka 1981 nchini Japan wajasiria mali wa kule waligundua biashara
ya kuuza hewa ya Oxygen baada ya kuwa adimu katika baadhi ya maeneo nchini
humo, mteja aliingia katika chumba maalum chenye hewa ya Oxygen na kufungiwa
kwa muda mbao fedha zake zinaruhusu hii inatokana na kuharibiwa kwa blanketi
hilo la hewa ambalo halipo kabisa kwenye mwezi kwa hiyo binaadam kuishi mwezini
walau kwa sekunde chache inahitaji
teknolojia ya juu kuliko ile iliyoelezewa na NASA.
Miale
mikubwa na ya ajabu inayokutana kwenye eneo linaloitwa Van Allen Belt huko
angani, Miale mikubwa ya Jua isiyo na kizuizi, miale kutoka kwenye Vimondo,
uwezo wa kuimudu miale hiyo na matatizo mengine mengi yatokanayo na uwezo
hafifu wa binaadam na ugeni kwenye mazingira hayo ni vitu vinavyo sababisha
safari nzima ya binaadam kuliacha anga letu na kwenda kwenye anga jingine iwe ni ndoto ambayo kwa uwezo wa
teknolojia iliyoelezewa na NASA bado ina endelea kuotwa.
Wanaanga hawawezi kusafiri kwenda kwenye mwezi kwa sababu ya hii mionzi
kwenye Van Allen Belts, mionzi kwenye huu uwanda, ipo mara mbili, kuna mionzi
ya kati na ile ya nje, mionzi ya kati inakadiriwa ni urefu wa km 2400 mpaka
5600 kutoka duniani, na upana wa km 3200. Na Mionzi ya nje ni urefu wa km 12000
mpaka 19000 kutoka Duniani. Vipande chanya na hasi vya umeme vinavyopatikana
katika uwanda huu vinakwenda kwa kasi mno na vinasafiri katika njia tatu kwa
wakati mmoja, zinakwenda kwa kuzunguka katika maeneo/njia za nguvu kizani za
dunia, pia zinakwenda mbele na kurudi nyuma kwa wakati huohuo katika mistari ya
nguvu kizani na katika njia ya dunia zikiizunguka jua.
Uwanda ambao unao vipande ambavyo vinayo mionzi yenye nguvu na ya hatari ni
vile vya uwanda na au mionzi ya kati, eneo ambalo wanaanga ni lazima waliepuke katika
safari yao ama sivyo watapata madhara makubwa na hata kufa mara tu baada ya
kugusana na mionzi hiyo, na picha ambazo nazo zitachukuliwa nazo zitaharibiwa
na mionzi hiyo. Mionzi hiyo inakuwa na nguvu mara elfu pale Jua linapokuwa
kwenye kipindi cha kurusha mionzi yake kwa wingi. Ni kutokana na mionzi hiyo
ndiyo warusi waliona ni wendawazimu kumpeleka binaadam mwezini.
Ni vipi wana anga hao wameweza kutembea juu ya mwezi wakiwa wamefunikwa
gubigubi na kile kilichoitwa Space Suit (Nguo maalum wavaazo wanaanga) katika
eneo ambalo mionzi ya jua inapiga moja kwa moja kwenye kiwango cha 265°C, kama linavyoitwa
Space hakuna chembechembe za hewa, ni pa wazi (vacuum) hakuna joto wala baridi.
Tunaposema Hali ni ya joto tunamaanisha, mtetemo au mwendo wa chembechembe
(molecules) ndani ya kitu. Kadiri mwendo wa chembechembe hizo unavyokuwa mkubwa
ndivyo joto linapoongezeka, na mwendo huo unapokuwa mdogo joto nalo hupungua.
Joto linapokuwa sifuri ni kwamba hakuna chembechembe zinazo safiri kabisa. Kwa
hiyo ili kuwepo na joto au baridi molecules lazima ziwepo. Vacuum ni ile hali
ya kuwa hakuna kitu chochote, hakuna, hakuna kabisa na kama ndivyo hata molecules nazo zinakuwa hakuna na hali hii haipatikani katika dunia yetu ila
kwenye Space (anga) nako wataalam wanadai pia si kwamba hakuna molecules
kabisa, hapana zipo ila ni chache mno hivyo zinaondoa uwezekano wowote wa
kuweza kupima kile kinachoitwa ‘Joto’ au ‘Baridi’. Na hii ndiyo maana chombo
tunachokitumia kuhifadhia joto au baridi kwa muda mrefu bila kupunguza au
kuongeza joto au baridi la kitu hicho
mathalani chupa ya chai vinafanya kazi mfano wa vacuum. Mionzi mbalimbali
itaweza kusafiri kwenye vacuum lakini haitaweza kuleta athari ya joto au
baridi.
Mionzi ya joto kutoka kwenye Jua inasafiri kwenye uwazi (vacuum) ya Space
bila kuliathiri anga la space kwa joto la mionzi yake, hivyo mionzi hiyo haina
athari yoyote mpaka pale inapogongana na kitu au inapotua juu ya kitu na
molecules za hicho kitu zitaanza kutetema au kusogea kulingana na kiwango cha
miali kilichogonga juu ya kitu hicho. Muda ambao mionzi hiyo itachukua
kukipasha joto kitu chochote cha angani itakayo gongana nacho itategemea na ni
kwa kiasi gani kitu hicho kimejiweka wazi kwenye mionzi hiyo, rangi ya kitu
chenyewe, vitu ambavyo vimekitengeneza kitu hicho, umbali wake kutoka kwenye
Jua na uwezo wake wa kuakisi mionzi ya Jua. Anga (Space) haina kitu kinachoitwa
“Joto” na wala haina kitu kinachoitwa “Baridi”
Kwa hiyo kitu ambacho kina joto hakiwezi kikapoozwa kwenye Space ili kitu
hicho kiweze kupoozwa inabidi kwanza kiondolewe kutoka kwenye Mionzi ya moja
kwa moja ya jua, kitu ambacho kiko kwenye kivuli ya kitu kingine kitaanza
kupoa, lakini si kwa sababu space ni ya baridi hapana bali kwa sababu kwa
wakati huo kitu hicho kitakuwa kinapambana na molecules zingine ambazo kasi
yake si kubwa kutokana na kuwepo mbali na mionzi ya moja kwa moja ya jua na
ambapo baada ya muda mitetemo yote itasimama kukiwa na sharti la kuwa kitu
hicho kimeondolewa kwenye mionzi ya moja kwa moja au ya kupitia kwa ya Jua na
kwamba hakuna kitu kingine cha kuweza kusababisha joto. Kwa kuwa anga halina
molecules kabisa ama ambazo ziko ni chache sana basi inachukua muda mrefu sana
kwa kitu kuweza kupoa katika space hata baada ya kuondolewa katika kila aina ya
chanzo cha joto. Hayo ndiyo mazingira yaliyopo mwezini na angani kwa ujumla.
NASA wanasisitiza kwamba Space Suit (nguo za wanaanga) walizo vaa
walipokuwa mwezini zina Air Condition,
kiyoyozi, lakini kiyoyozi hakiwezi na hakitaweza kufanya kazi bila kuwepo na
mazingira ya kubadilishana hewa. Mazingira hayo yanaruhusu kiyoyozi kuweza kuchukua hali joto kutoka
sehemu moja na kupeleka sehemu nyingine hii inahitaji kuwa na molecule ambazo zitaakisi na kusafirisha
joto kama ambavyo inavyoweza kufanyika kwenye blanketi letu la hewa au kwenye
maji kwani hapo kuna molecule za
kuweza kuruhusu hilo. Hivyo Kiyoyozi hakiwezi kufanya kazi kwenye space iliyozungukwa na vacuum. Space Suit iliyozungukwa na vacuum
haiwezi kusafirisha joto kutoka ndani ya nguo hizo maalum kwenda sehemu
nyingine, kumbuka vacuum ni ile hali ambayo hakuna kabisa kabisakabisa chembechembe
za hewa ambazo zingesaidia hata hicho kiyoyozi kufanya kazi na kama hivyo
ndivyo basi binaadam anaweza kuiva katika mazingira hayo, inakuaje wameenda wakarudi
na hawajaiva, sababu hawakuenda walikuwa sehemu fulani kwenye uso wa Dunia na
kutudanganya kuwa ni mwezini!
NASA wanadai kuwa wanaanga hao walifungiwa mabomba maalum ya kupitisha maji
katika miili yao ilikowapooza na joto la ndani ya Appolo, hilo si tatizo lakini swali
linalotokana na kubebwa kwa kiasi cha maji kwenda angani linaposhindwa kujibika
hapo ndipo tatizo linapotokea. Ikiwa maji yanageuka na kuwa hewa (everporation) iwapo yatachemka kwa
kiwango cha 55
kutoka kwenye usawa wa bahari, je ni kiasi gani cha maji
yatahitajika kwenye mazingira ambayo mionzi ya jua inapiga moja kwa moja kwa
kiwango cha nyuzi joto 265〫kwa ajili ya safari ya kwenda tu ambayo iliwachukua siku tano na masaa
mawili na dakika thelathini juu ya mwezi kama walivyo danganya.
Hawakusema ni maji kiasi gani yaliyo bebwa na chombo hicho, lakini maji
ambayo yangehitajika katika mazingira waliyoyaelezea ilikusababisha kuendelea
kuwepo kwa uhai kwa wanaanga hao walau kwa muda mfupi sana wa sekunde chache
tu, basi vitu viwili vingetokea, Huenda Apollo 11 isingeweza kuruka kutokana na
uzito kuwa mkubwa, au ingeruka na hii ingeifanya iruke kwa kasi kubwa mno
ambayo ingeweza kuzizidi nguvu za mvutano baina ya chombo hicho na Dunia na
hivyo kusababisha chombo hicho kupotolea kwenye Space kama jinsi vilivyopotea
vyombo vingine.
Vipi wanaanga hao baada ya kurejea na kuanza kudai kuwa chombo chao kilikuwa
kikizunguka taratibu sana sababu ya baridi kali iliyokuwepo kwenye Space,
Uwongo, kwanza kwenye Space kama sheria ya Fizikia ilivyotuonesha ni kwamba
hakuna baridi wala joto sababu hakuna molecules wao hiyo baridi wameihisi
kutoka wapi kama hawakuwa hapahapa duniani ambapo kumejaa molecules za kila
aina. Pili air condition walibeba ya
nini ikiwa kuna baridi kali, na tatu chombo hicho kwenda taratibu tofauti na
mahesabu ya mwendo yaliyowekwa kukiwezesha kuendelea kukaa kwenye Space na
kusonga mbele kuelekea mwezini basi kitu kingine kingetokea nacho ni kuwa
chombo hicho kingezidiwa na nguvu za mvutano za dunia na kurudishwa aridhini
kama ilivyotokea kwa vyombo vilivyotangulia ambavyo baadhi viliokotewa
baharini, cha Gagarin wa USSR kiliokotewa China.
Hii ni kwa sababu dunia ndiyo sayari ambayo ni kubwa na yenye nguvu kubwa
ya ukinzani na ndiyo ambayo bado iko karibu na chombo hicho ambacho
kimeshapoteza mahesabu ya mwendo kasi unaotakiwa kukiwezesha kuendelea na
safari yake kutokana na kuvamiwa na hali ya hewa ya ubaridi ambayo hawakuitarajia na hivyo kusababisha
mwendo kupungua, na hivyo nguvu za mvutano wa dunia zingekivuta chombo hicho,
lakini ni baridi gani hiyo ikiwa angani
hakuna joto wala baridi?
Kutokana na maelezo ya William Cooper, mtaalam aliyelivalia njuga suala la
kwenda mwezini anadai kuwa hata nguo walizovaa (space suit) zimetengenezwa
na malighafi za kawaida ambazo hata kidogo haziwezi kuhimili mikikimikiki na
dhoruba za angani hivyo kama nguo hizo ndizo walizo kwenda nazo angani basi
hadithi yao isingetofautiana na ile ya wanaanga wa Kirusi, wangekufa mara moja
wote.
Kwa upande wa pili picha nyingi kama si zote zinazo semwa zimepigwa mwezini
zimebainika si za kweli, yaani kama picha hizo zilitakiwa kupigwa mwezini basi
ni za kughushi, hii zikiwemo pamoja na baadhi ya vidio, na sauti walizo rekodi
na walizo zaionesha. Baada ya taarifa za kwenda mwezini na kurudi kushamiri,
mgongano mkubwa wa mawazo ukaanza katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo
vya kwao vikihoji,
“je ni kweli wamekwenda mwezini au hawakuenda?”
hata hivyo ilichukuliwa kama changamoto ya kawaida mpaka pale mwaka 2001
kipindi cha habari maalum kilipo rushwa hewani na Fox Televisheni kikienda kwa
jina la “Did we Land on the moon?” (Je tulitua mwezini?) Ndipo jamaa mmoja
aliyeitwa Jack White mwenye stashahada ya uandishi wa habari, na ambaye kwa
nusu karne amekuwa akionesha ujuzi wake mkubwa kuhusu mambo yahusiayo picha,
kwani yeye ni mtaalamu katika masuala ya kuichambua picha.
Alichaguliwa kama mjuzi wa kuchambua picha kwenye kamati iliyoundwa
kuchunguza mauwaji ya Rais F Kennedy, White House wakatengeneza Vidio mbili
kutokana na uchunguzi wake kuhusu mauwaji ya Kennedy, hivyo ni mtu
anayekubalika katika taaluma za picha, alipoamua kuzichambua picha hizo
zinazosemwa zimepigwa mwezini alikuta mamia ya picha hizo zimeghushiwa, maswali
mengi yakazuka kutokana na uchunguzi wa jamaa huyu kama vile alivyozusha
maswali hayo alipozichambua picha zihusiazo muwaji ya rais Kennedy.
Swali likawa, ikiwa ni kweli wamekwenda mwezini kwa nini watumie picha za
kughushi na za uongo kuelezea matukio mbalimbali, vituo na safari walizozifanya
wakiwa huko walipo paita mwezini?
Picha hizo zimejaa mapungufu mengi na wala hazihitaji elimu kubwa kwenye
masuala ya picha ili kuweza kutambua mapungufu hayo.
Kuna mambo mengi ambayo yasingeonekana kwenye picha hizo ikiwa kama kweli
zimepigwa mwezini. Mfano kwenye baadhi ya picha hizo kuna alama ya matairi ya
magari tofauti na tairi za kigari walichosema wamekwenda nacho mwezini,
zimetoka wapi? Unaweza kusema ni kitu kidogo hicho lakini kwa watu makini hakuna
kitu kidogo na kikubwa vyote vina nafasi yake katika jambo, hivyo watu wenye
fikra huru lazima tuhoji matairi hayo
yametoka wapi?
Sehemu zingine kigari hicho kili[ita bila hata kuacha alama ya matairi? Kana kwamba kamewekwa hapo kapigwe picha kisha kaondolewe. Unalielezeaje hili, hasa mahala ambapo picha zinanesha unyayo wa wanaanga, lakini hakuna unyayo wa matairi ya kigari cha mwezini,
DONT MISS IT, MTANANGE UNAENDELEA HAPAHAPA ... CATCH YOU NEXT TIME ...
ASANTE KAKA ENDELEA KUTUPA VITU
ReplyDeleteMUNGU AKUBARIKI
Kaka makala hizi zimenifungua ubongo sana. nimejaribu kuwajuza na wale wasioufahamu ukweli kwa kuziandika katika blog yangu.
ReplyDeletewww.robhinsontz.blogspot.com
Nafurahi kwa kuongezeka idadi ya watu wanao zifurahia kazi zangu. Ila bwana Robhin nina vitu viwili ambayo ningependa uzingatie wakati unapo chapisha kazi hizi kwenye blogi yako. Moja ni chapisha kama ilivyo usibadili chochote kwenye maudhui ya kazi yenyewe, yaani usiongeze neno au kupunguza. Pili si vibaya ukimtaja mwandishi wa kazi hizo, thanks and keep it up.
DeleteEnter your comment...pamoja kaka
ReplyDelete