Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Thursday, December 18, 2014

HATUKWENDA MWEZINI ... Pt 2



Laika ni mbwa wa kwanza kwenda mwezini kwa majaribio na alikufa baada ya masaa machache ya kuizunguka dunia nje ya anga lake kama ambavyo walivyokufa wanaanga wa Kirusi waliojaribu kufanya hivyo mpaka mwana anga mwingine wa Kirusi Yuri Alekseyevich Gagarian alipofanikiwa kutudanganya kuwa amefanikiwa kufanya hivyo mnamo mwaka 1961 baada ya kuruka katika upeo ambao ulikuwa ni salama, hakufika mwezini ila anahisabiwa kama binaadam wa kwanza kwenda kwenye anga (Space). Uwongo hata katika hilo anga hakufanikiwa kufika.


Ukitizama picha ya mfumo wa Jua na sayari zake utaziona hazitofautiani sana, lakini ukiitizama sayari moja kati ya hizo utaiona hii imejitenga zaidi na nyingine kwa utofauti, sayari hii ni Dunia yetu, imejaa maji kuliko aridhi, ina hewa mbalimbali ambazo zinasaidia kuwepo kwa maisha kwenye nyumba hii, wingu hilo la hewa mbalimbali limekaa kama blanketi ambalo linaikinga Dunia yetu na miali ya moja kwa moja ya Jua. 

Blanketi hilo la hewa linapoharibiwa basi hatari ya maisha kutoweka  inakuwa kubwa, mnamo mwaka 1981 nchini Japan wajasiria mali wa kule waligundua biashara ya kuuza hewa ya Oxygen baada ya kuwa adimu katika baadhi ya maeneo nchini humo, mteja aliingia katika chumba maalum chenye hewa ya Oxygen na kufungiwa kwa muda mbao fedha zake zinaruhusu hii inatokana na kuharibiwa kwa blanketi hilo la hewa ambalo halipo kabisa kwenye mwezi kwa hiyo binaadam kuishi mwezini walau  kwa sekunde chache inahitaji teknolojia ya juu kuliko ile iliyoelezewa na NASA.

     Miale mikubwa na ya ajabu inayokutana kwenye eneo linaloitwa Van Allen Belt huko angani, Miale mikubwa ya Jua isiyo na kizuizi, miale kutoka kwenye Vimondo, uwezo wa kuimudu miale hiyo na matatizo mengine mengi yatokanayo na uwezo hafifu wa binaadam na ugeni kwenye mazingira hayo ni vitu vinavyo sababisha safari nzima ya binaadam kuliacha anga letu na kwenda kwenye  anga jingine iwe ni ndoto ambayo kwa uwezo wa teknolojia iliyoelezewa na NASA bado ina endelea kuotwa.

Wanaanga hawawezi kusafiri kwenda kwenye mwezi kwa sababu ya hii mionzi kwenye Van Allen Belts, mionzi kwenye huu uwanda, ipo mara mbili, kuna mionzi ya kati na ile ya nje, mionzi ya kati inakadiriwa ni urefu wa km 2400 mpaka 5600 kutoka duniani, na upana wa km 3200. Na Mionzi ya nje ni urefu wa km 12000 mpaka 19000 kutoka Duniani. Vipande chanya na hasi vya umeme vinavyopatikana katika uwanda huu vinakwenda kwa kasi mno na vinasafiri katika njia tatu kwa wakati mmoja, zinakwenda kwa kuzunguka katika maeneo/njia za nguvu kizani za dunia, pia zinakwenda mbele na kurudi nyuma kwa wakati huohuo katika mistari ya nguvu kizani na katika njia ya dunia zikiizunguka jua.

Uwanda ambao unao vipande ambavyo vinayo mionzi yenye nguvu na ya hatari ni vile vya uwanda na au mionzi ya kati, eneo ambalo wanaanga ni lazima waliepuke katika safari yao ama sivyo watapata madhara makubwa na hata kufa mara tu baada ya kugusana na mionzi hiyo, na picha ambazo nazo zitachukuliwa nazo zitaharibiwa na mionzi hiyo. Mionzi hiyo inakuwa na nguvu mara elfu pale Jua linapokuwa kwenye kipindi cha kurusha mionzi yake kwa wingi. Ni kutokana na mionzi hiyo ndiyo warusi waliona ni wendawazimu kumpeleka binaadam mwezini.



Ni vipi wana anga hao wameweza kutembea juu ya mwezi wakiwa wamefunikwa gubigubi na kile kilichoitwa Space Suit (Nguo maalum wavaazo wanaanga) katika eneo ambalo mionzi ya jua inapiga moja kwa moja kwenye kiwango cha 265°C, kama linavyoitwa Space hakuna chembechembe za hewa, ni pa wazi (vacuum) hakuna joto wala baridi.

Tunaposema Hali ni ya joto tunamaanisha, mtetemo au mwendo wa chembechembe (molecules) ndani ya kitu. Kadiri mwendo wa chembechembe hizo unavyokuwa mkubwa ndivyo joto linapoongezeka, na mwendo huo unapokuwa mdogo joto nalo hupungua. Joto linapokuwa sifuri ni kwamba hakuna chembechembe zinazo safiri kabisa. Kwa hiyo ili kuwepo na joto au baridi molecules lazima ziwepo. Vacuum ni ile hali ya kuwa hakuna kitu chochote, hakuna, hakuna kabisa na kama ndivyo hata  molecules nazo zinakuwa hakuna  na hali hii haipatikani katika dunia yetu ila kwenye Space (anga) nako wataalam wanadai pia si kwamba hakuna molecules kabisa, hapana zipo ila ni chache mno hivyo zinaondoa uwezekano wowote wa kuweza kupima kile kinachoitwa ‘Joto’ au ‘Baridi’. Na hii ndiyo maana chombo tunachokitumia kuhifadhia joto au baridi kwa muda mrefu bila kupunguza au kuongeza joto au baridi la kitu hicho  mathalani chupa ya chai vinafanya kazi mfano wa vacuum. Mionzi mbalimbali itaweza kusafiri kwenye vacuum lakini haitaweza kuleta athari ya joto au baridi.

Mionzi ya joto kutoka kwenye Jua inasafiri kwenye uwazi (vacuum) ya Space bila kuliathiri anga la space kwa joto la mionzi yake, hivyo mionzi hiyo haina athari yoyote mpaka pale inapogongana na kitu au inapotua juu ya kitu na molecules za hicho kitu zitaanza kutetema au kusogea kulingana na kiwango cha miali kilichogonga juu ya kitu hicho. Muda ambao mionzi hiyo itachukua kukipasha joto kitu chochote cha angani itakayo gongana nacho itategemea na ni kwa kiasi gani kitu hicho kimejiweka wazi kwenye mionzi hiyo, rangi ya kitu chenyewe, vitu ambavyo vimekitengeneza kitu hicho, umbali wake kutoka kwenye Jua na uwezo wake wa kuakisi mionzi ya Jua. Anga (Space) haina kitu kinachoitwa “Joto” na wala haina kitu kinachoitwa “Baridi”

Kwa hiyo kitu ambacho kina joto hakiwezi kikapoozwa kwenye Space ili kitu hicho kiweze kupoozwa inabidi kwanza kiondolewe kutoka kwenye Mionzi ya moja kwa moja ya jua, kitu ambacho kiko kwenye kivuli ya kitu kingine kitaanza kupoa, lakini si kwa sababu space ni ya baridi hapana bali kwa sababu kwa wakati huo kitu hicho kitakuwa kinapambana na molecules zingine ambazo kasi yake si kubwa kutokana na kuwepo mbali na mionzi ya moja kwa moja ya jua na ambapo baada ya muda mitetemo yote itasimama kukiwa na sharti la kuwa kitu hicho kimeondolewa kwenye mionzi ya moja kwa moja au ya kupitia kwa ya Jua na kwamba hakuna kitu kingine cha kuweza kusababisha joto. Kwa kuwa anga halina molecules kabisa ama ambazo ziko ni chache sana basi inachukua muda mrefu sana kwa kitu kuweza kupoa katika space hata baada ya kuondolewa katika kila aina ya chanzo cha joto. Hayo ndiyo mazingira yaliyopo mwezini na angani kwa ujumla.


NASA wanasisitiza kwamba Space Suit (nguo za wanaanga) walizo vaa walipokuwa mwezini zina Air Condition, kiyoyozi, lakini kiyoyozi hakiwezi na hakitaweza kufanya kazi bila kuwepo na mazingira ya kubadilishana hewa. Mazingira hayo yanaruhusu  kiyoyozi kuweza kuchukua hali joto kutoka sehemu moja na kupeleka sehemu nyingine hii inahitaji kuwa na molecule ambazo zitaakisi na kusafirisha joto kama ambavyo inavyoweza kufanyika kwenye blanketi letu la hewa au kwenye maji kwani hapo kuna molecule za kuweza kuruhusu hilo. Hivyo Kiyoyozi hakiwezi kufanya kazi kwenye space iliyozungukwa na vacuum. Space Suit iliyozungukwa na vacuum haiwezi kusafirisha joto kutoka ndani ya nguo hizo maalum kwenda sehemu nyingine, kumbuka vacuum ni ile hali ambayo hakuna kabisa kabisakabisa chembechembe za hewa ambazo zingesaidia hata hicho kiyoyozi kufanya kazi na kama hivyo ndivyo basi binaadam anaweza kuiva katika mazingira hayo, inakuaje wameenda wakarudi na hawajaiva, sababu hawakuenda walikuwa sehemu fulani kwenye uso wa Dunia na kutudanganya kuwa ni mwezini!



NASA wanadai kuwa wanaanga hao walifungiwa mabomba maalum ya kupitisha maji katika miili yao ilikowapooza na joto la ndani ya  Appolo, hilo si tatizo lakini swali linalotokana na kubebwa kwa kiasi cha maji kwenda angani linaposhindwa kujibika hapo ndipo tatizo linapotokea. Ikiwa maji yanageuka na kuwa hewa (everporation) iwapo yatachemka kwa kiwango cha 55 kutoka kwenye usawa wa bahari, je ni kiasi gani cha maji yatahitajika kwenye mazingira ambayo mionzi ya jua inapiga moja kwa moja kwa kiwango cha nyuzi joto 265kwa ajili ya safari ya kwenda tu ambayo iliwachukua siku tano na masaa mawili na dakika thelathini juu ya mwezi kama walivyo danganya. 

Hawakusema ni maji kiasi gani yaliyo bebwa na chombo hicho, lakini maji ambayo yangehitajika katika mazingira waliyoyaelezea ilikusababisha kuendelea kuwepo kwa uhai kwa wanaanga hao walau kwa muda mfupi sana wa sekunde chache tu, basi vitu viwili vingetokea, Huenda Apollo 11 isingeweza kuruka kutokana na uzito kuwa mkubwa, au ingeruka na hii ingeifanya iruke kwa kasi kubwa mno ambayo ingeweza kuzizidi nguvu za mvutano baina ya chombo hicho na Dunia na hivyo kusababisha chombo hicho kupotolea kwenye Space kama jinsi vilivyopotea vyombo vingine.

Vipi wanaanga hao baada ya kurejea na kuanza kudai kuwa chombo chao kilikuwa kikizunguka taratibu sana sababu ya baridi kali iliyokuwepo kwenye Space, Uwongo, kwanza kwenye Space kama sheria ya Fizikia ilivyotuonesha ni kwamba hakuna baridi wala joto sababu hakuna molecules wao hiyo baridi wameihisi kutoka wapi kama hawakuwa hapahapa duniani ambapo kumejaa molecules za kila aina. Pili air condition walibeba ya nini ikiwa kuna baridi kali, na tatu chombo hicho kwenda taratibu tofauti na mahesabu ya mwendo yaliyowekwa kukiwezesha kuendelea kukaa kwenye Space na kusonga mbele kuelekea mwezini basi kitu kingine kingetokea nacho ni kuwa chombo hicho kingezidiwa na nguvu za mvutano za dunia na kurudishwa aridhini kama ilivyotokea kwa vyombo vilivyotangulia ambavyo baadhi viliokotewa baharini, cha Gagarin wa USSR kiliokotewa China.


Hii ni kwa sababu dunia ndiyo sayari ambayo ni kubwa na yenye nguvu kubwa ya ukinzani na ndiyo ambayo bado iko karibu na chombo hicho ambacho kimeshapoteza mahesabu ya mwendo kasi unaotakiwa kukiwezesha kuendelea na safari yake kutokana na kuvamiwa na hali ya hewa ya ubaridi  ambayo hawakuitarajia na hivyo kusababisha mwendo kupungua, na hivyo nguvu za mvutano wa dunia zingekivuta chombo hicho, lakini ni baridi gani hiyo ikiwa angani  hakuna joto wala baridi?
Kutokana na maelezo ya William Cooper, mtaalam aliyelivalia njuga suala la kwenda mwezini anadai kuwa hata nguo walizovaa (space suit) zimetengenezwa na malighafi za kawaida ambazo hata kidogo haziwezi kuhimili mikikimikiki na dhoruba za angani hivyo kama nguo hizo ndizo walizo kwenda nazo angani basi hadithi yao isingetofautiana na ile ya wanaanga wa Kirusi, wangekufa mara moja wote.

Kwa upande wa pili picha nyingi kama si zote zinazo semwa zimepigwa mwezini zimebainika si za kweli, yaani kama picha hizo zilitakiwa kupigwa mwezini basi ni za kughushi, hii zikiwemo pamoja na baadhi ya vidio, na sauti walizo rekodi na walizo zaionesha. Baada ya taarifa za kwenda mwezini na kurudi kushamiri, mgongano mkubwa wa mawazo ukaanza katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya kwao vikihoji,

“je ni kweli wamekwenda mwezini au hawakuenda?”



hata hivyo ilichukuliwa kama changamoto ya kawaida mpaka pale mwaka 2001 kipindi cha habari maalum kilipo rushwa hewani na Fox Televisheni kikienda kwa jina la “Did we Land on the moon?” (Je tulitua mwezini?) Ndipo jamaa mmoja aliyeitwa Jack White mwenye stashahada ya uandishi wa habari, na ambaye kwa nusu karne amekuwa akionesha ujuzi wake mkubwa kuhusu mambo yahusiayo picha, kwani yeye ni mtaalamu katika masuala ya kuichambua picha.

Alichaguliwa kama mjuzi wa kuchambua picha kwenye kamati iliyoundwa kuchunguza mauwaji ya Rais F Kennedy, White House wakatengeneza Vidio mbili kutokana na uchunguzi wake kuhusu mauwaji ya Kennedy, hivyo ni mtu anayekubalika katika taaluma za picha, alipoamua kuzichambua picha hizo zinazosemwa zimepigwa mwezini alikuta mamia ya picha hizo zimeghushiwa, maswali mengi yakazuka kutokana na uchunguzi wa jamaa huyu kama vile alivyozusha maswali hayo alipozichambua picha zihusiazo muwaji ya rais Kennedy.

Swali likawa, ikiwa ni kweli wamekwenda mwezini kwa nini watumie picha za kughushi na za uongo kuelezea matukio mbalimbali, vituo na safari walizozifanya wakiwa huko walipo paita mwezini?

Picha hizo zimejaa mapungufu mengi na wala hazihitaji elimu kubwa kwenye masuala ya picha ili kuweza kutambua mapungufu hayo.

Kuna mambo mengi ambayo yasingeonekana kwenye picha hizo ikiwa kama kweli zimepigwa mwezini. Mfano kwenye baadhi ya picha hizo kuna alama ya matairi ya magari tofauti na tairi za kigari walichosema wamekwenda nacho mwezini, zimetoka wapi? Unaweza kusema ni kitu kidogo hicho lakini kwa watu makini hakuna kitu kidogo na kikubwa vyote vina nafasi yake katika jambo, hivyo watu wenye fikra huru lazima tuhoji matairi hayo yametoka wapi?



Sehemu zingine kigari hicho kili[ita bila hata kuacha alama ya matairi? Kana kwamba kamewekwa hapo kapigwe picha kisha kaondolewe. Unalielezeaje hili, hasa mahala ambapo picha zinanesha unyayo wa wanaanga, lakini hakuna unyayo wa matairi ya kigari cha mwezini,



DONT MISS IT, MTANANGE UNAENDELEA HAPAHAPA ... CATCH YOU NEXT TIME ...

4 comments:

  1. ASANTE KAKA ENDELEA KUTUPA VITU

    MUNGU AKUBARIKI

    ReplyDelete
  2. Kaka makala hizi zimenifungua ubongo sana. nimejaribu kuwajuza na wale wasioufahamu ukweli kwa kuziandika katika blog yangu.
    www.robhinsontz.blogspot.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nafurahi kwa kuongezeka idadi ya watu wanao zifurahia kazi zangu. Ila bwana Robhin nina vitu viwili ambayo ningependa uzingatie wakati unapo chapisha kazi hizi kwenye blogi yako. Moja ni chapisha kama ilivyo usibadili chochote kwenye maudhui ya kazi yenyewe, yaani usiongeze neno au kupunguza. Pili si vibaya ukimtaja mwandishi wa kazi hizo, thanks and keep it up.

      Delete
  3. Enter your comment...pamoja kaka

    ReplyDelete