Kama tunavyojua mwezi haujazungukwa na blanketi la hewa kama hili la kwetu
hivyo anga zima (Space) linaonekana jeusi tii hivyo hakuna kitu chochote
kitakachoweza kurikodiwa nyuma ya weusi huo mpaka miale ya kamera iwe na nguvu
ya kupenya weusi huo, lakini cha ajabu baadhi ya picha baada ya kuchunguzwa
zimekutwa na duara kubwa nyuma wa weusi huo wa anga, duara mbalo kwenye picha
zingine limetumika kama jua au chanzo cha mwanga wa jua.
PICHA UNAZO ZIONA ZIMETUMIKA KAMA JUA KWENYE PICHA ZA APOLLO 11 NA APOLLO NYINGINE. LAKINI PICHA HIZO ZILIPONYAMBULIWA KWA KUTUMIA PROGRAMU NYINGINE KILICHO ONEKANA SI JUA BALI NI 'SPOT LIGHT' ZINAZOTUMIKA KURIKODIA MUVI.
Ni vipi duara hilo
limeweza kurikodiwa nyuma ya kiza kinene cha kwenye anga?
PICHA HII INAJIELEZEA YENYEWE
Ingawa picha hizo zinaonesha anga likiwa safi na ndivyo lilivyo hatutegemei
mawingu kwenye space lakini hakuna hata moja iliyonasa picha ya nyota za
angani, ni ajabu sana katika weusi huo wa angani miongoni mwa vitu ambavyo
vingeonekana kwa haraka na kwa wepesi zaidi ni nyota kwa sababu zinauwezo wa
kuzalisha nuru mfano wa Jua lakini haikuonekana hata moja,
cha ajabu zaidi
kilichoonekana ni uso wa Dunia, kitu ambacho hakiwezi kuelezeka labda kwa
nadharia za kibususa, Dunia haizalishi mwanga na katika mazingira hayo kuipata
picha yake ni vigumu zaidi kuliko kuipata picha za nyota zilizoko angani, ni
vipi katika umbali wa maili zote hizo waliweza kuipata picha ya dunia
wakashindwa kuzipata picha za Nyota?
MAAJABU DUNIA INAONEKANA VIZURI KABISA, LAKINI NO STAR?
Katika picha ambayo Luna Module (LM) inaonekana ikikaribia kutua juu ya
mwezi na kwa mbali dunia yetu na rangi yeka nzuri inaonekana kama jua
linalozama, ni kitu gani kinachosababisha dunia isiyo zalisha mwanga wowote
iweze kuonekana katika mazingira hayo na nyota yenye kuzalisha mwanga
isionekane.
MWISHO WA SIKU TUNAONA HATA HIYO INAYO ONEKANA NI 'DUNIA' NI KITU KILICHO ONGEZEWA KWENYE PICHA HIZI. KWAMBA HAKIKURIKODIWA MWEZINI BALI STUDIO.
Mazingira hayo ni magumu kwa mwanga kupenya kutokana na weusi mzito
wa anga lililo izunguka dunia yetu kama picha inavyo onesha hivyo dunia yetu
isingeweza kuonekana kutokana na kwamba haizalishi mwanga kama nyota wala
haihakisi mwanga kama mwezi na hivyo ingekuwa ni sehemu ya weusi huo mzito wa
anga na isingerikodiwa katika picha hii.
Halafu ni kitu gani kilichozuia nyota
ambazo zina uwezo wa kuzalisha mwanga zisirikodiwe katika picha hii. Hapana,
tunaweza kuziona kwa jicho la kawaida wakati wa usiku iweje kwenye kamara hii zisirikodiwe.
Picha hii ni maalum kwa kurubuni mawazo ya watu, lakini kiuhakika kitu kilicho
rikodiwa kwenye picha hii hakiwezi kuelezeka na kuleta maana kwenye elimu ya
mambo ya picha na wala kwa mtu mwenye mawazo na fikra huru, ni picha ya
kughushi.
Picha zingine zimekuwa zikionesha mwanga wa Jua mahala ambapo wanaanga
wamesimama juu ya mwezi na kwengine kote ni giza hii inakuwaje, ina maana huko
angani jua linabagua kumulika baadhai ya sehemu na kuacha kwengine, baadhi ya
picha utaona kuna mwanga mkali mahala waliposimama wanaanga na kama baada ya m
10 hivi kuna kiza totoro hili ni jua la aina gani jamani? Nisaidieni labda mimi sizifahamu tabia za jua
vizuri.
Mahala pengine utaona vivuli vinapishana, yaani kuna vyanzo vya mwanga
zaidi ya kimoja hili unaweza kuelezea vipi, inamaana huko mwezini kuna majua
mawili au matatu au manne? Jamani hivi ni kweli wametuona kuwa sisi ni wajinga
kiasi hichi.
Picha za vidio zinazo daiwa kurikodiwa mwezini wanaanga wakitembea mwezini
zikioneshwa kwa kasi ya mara mbili (fast forwad) basi wanaanga hao wanaonekana
wakikimbia kama ambao wako duniani ambako nguvu yake ya mvutano inasababisha
kukimbia au kutembea kwa namna hiyo na si kwenye mwezi.
Safari nzima ilijaa vituko, picha zingine imeonekana chupa ya Coca cola
sasa hatujui kama na huko mwezini walienda kuziuza ama vipi, alama za matairi
ya gari tofauti na kile kilichokwenda mwezini hatujui kama na yenyewe
yalipelekwa na hizo Apollo ama vipi, alama za miguu yao na matairi ya chombo
chao vinaonesha alama ambazo uzito wake ni sawa na ule wa mtu anayetembea juu
ya uso wa dunia kitu ambacho hakiwezekani kabisa sababu kwenye mwezi uzito
unapungua maradufu kutokana na kutokuwepo kwa nguvu kizani.
Mahala ambapo Apollo imetua hapa oneshi shimo lolote kutokana na kishindo
cha kutua kwake, na inaponyanyuka utadhani inavutwa na uzi kwenda juu, mahala
pengine tunakuta alama za matairi mawili wakati chombo kilichopita kina matairi
manne hii inakuwaje.
Lakini baada ya mambo kuwekwa wazi na NASA kuonekana wamedanganya kwenye
safari ya mwezini, shughuli nyingine ikaanza ya propaganda na vipindi maalum
kwenye televisheni na filam vyikielezea safari hiyo ilikuendelea kuwalaza
mamilioni katika usingizi wa ujinga na imani wasiyoijua uhakika wake, imani ya
kuwa tulikwenda mwezini. Mfano wa filamu hizo ni ile iliyoitwa Apollo13, na ile
ya Froma the Earth to the Moon.
MZIKI HAUJAISHA ...... UNAENDELEA HAPA HAPA .....
Kazin nzuri sana kaka! Bravoh.
ReplyDeleteNingependa tuwasiliane zaidi ili unifundishe mambo mengi, navutiwa sana na kazi yako.
tupakule@gmail.com, robhinson.edson@gmail.com +255 756891212
Ñna mm ningeomba uwe unarusha kweny google +
ReplyDeleteipo kwenye google+ unless kama kuna tatizo, na akama lipo just tuambie na litafanyiwa kazi ASAP
ReplyDeleteUwongo huu ushaota mizizi kwenye jamii kwani tumeaminishwa tangu wadogo unazani jamii itatuelewa tukiwaambia n uwongo
ReplyDelete