Lengo hasa ni kutengeneza kiu ya kutaka kujua juu hasa ya kuwepo kwa
‘wageni’ hao na kuwafanya watu wafikiri na kudhani kuwa ni kweli, viumbe hao
kutoka sayari ya mbali wapo, ni kweli kuwa ‘wageni’ wamerudi tena. Mwaka 1947
aliyekuwa rais wa Marekani na Freemasons kwenye daraja la 33, Harry S. Truman
alitengeneza kile kilicho itwa Majestic 12 au MJ12, kamati ya siri ya
wanasayansi ikishirikiana na serikali, ilichaguliwa kulifanyia utafiti na
uchunguzi suala Roswell, UFO na viumbe kutoka nje ya sayari yetu.
Richard Hoagland mzungumzaji wa Umoja wa Mataifa na pia amekuwa akialikwa
katika vituo na vipindi vya redio kufanya mahojiano juu ya kuwepo kwa viumbe
wengine kutoka nje ya sayari yetu. ‘Bahati’ nzuri Hoagland amekuwa na ‘mtu wa
ndani’ kutoka NASA ambaye amekuwa akimmegea siri na mambo ambayo NASA hawataki
walimwengu wafahamu. Amekuwa akizungumzia kuhusu kuwepo kwa viumbe hao na alama
kama za piramidi, na uso wa mtu kwenye sayari ya Mars ambazo NASA hawataki watu
wafahamu. Anasema NASA wanaufunika ukweli kwamba wanasayansi wetu wa anga wanao
ushahidi juu yakuwepo kwa viumbe hao na kwamba binadamu (wanasayansi na
viongozi wa Illuminati) wamesha anza kuwasiliana na kushirikiana na viumbe hao
kwa namna mbalimbali.
Je ni kweli Hoagland anafichua siri za NASA juu ya kuwepo kwa ‘wageni’ hao
katika sayari yetu au galaxy nyingine au ni mtumishi anaye fanya kazi yake
vyema ya kuwapandikiza walimwengu dhana na nadharia kuwa kweli viumbe hao wapo,
kweli wapo na serikali hawataki watu mfahamu.
NASA walitoa taarifa rasmi za kukataa juu ya kuwepo kwa viumbe hao kutoka
nje ya sayari yetu, walikataa kuwa viumbe hao hawapo kwenye mwezi wala kwenye
sayari ya Mars. Ghafla Richard Hoagland na wenzake wanao ‘megewa’ habari za
ndani wakaja na taarifa kuhusiana na UFO, ‘wageni’ hao na picha mbalimbali za
kwenye mwezi na kwenye sayari ya Mars zinazo elekeza na kuonesha juu ya kuwepo
kwa viumbe hao katika maeneo hayo na alama zao, yaani kama vile NASA hawataki
walimwengu kufahamu chochote juu ya ukweli huo. Hoagland na wenzake wana watu
wao ndani ya NASA, walio wamegea picha hizo na taarifa zingine, hivyo ‘watu wa
ndani’ wanautoa ukweli NASA wasio taka watu kufahamu kupitia kwa Hoagland na
wenzake.
Hivyo hapa Hoagland anaonekana kama whistleblower, yaani mfichuaji mambo ya
ndani na mtu mzuri kwa wale wasio na sauti. Lakini kwanza, na cha kwanza NASA
wanafunika ukweli juu ya safari ya kwenda mwezini, tunajua hawajakwenda,
tunajua hakuna binadamu aliyekanyaga mwezini kupitia teknolojia ya NASA,
ulikuwa ni uwongo mtupu na danganya toto, hili NASA wanalifunika walimwengu
wasijue, lakini Hoagland na wenzake wanakubali kuwa tulikwenda mwezini, na
kutuonesha picha na alama za ‘wageni’ toka mbali zikiwa mwezini ambazo
zilipigwa na wanaanga wa NASA walipo kwenda ‘mwezini’. Sasa Hoagland ni NASA au?
Anaonekana kama ni adui namba moja wa NASA, na anawapinga NASA na mambo yao ya
kufunika ‘ukweli’ na anakuwa ni tumaini na tegemeo la watu duniani kote
kuhusiana na ukweli juu ya UFO na madereva wake. Lakini mwenye jicho haambiwi
tazama.
Kama kwenye filamu ya Indepencence Day ambapo binadamu wote waliunganishwa
kupitia majeshi ya nchi mbalimbali kupambana na kitisho kipya kilicho jitokeza,
kitisho kutoka nje ya sayari yetu, ‘wageni’. Usidanganywe na taarifa za kupikwa
kisayansi na uwongo juu ya UFO vitu ambavyo vitaonekana ni vitu vya kutisha.
Lakini lango ni kutengeneza adui mwenye nguvu kutoka nje ya dunia (kwa ajili ya
kutuunganisha, kwa sasa adui tuliye naye ambaye naye ni wa kutengeneza ni
ugaidi)
Nazikubali kazi za David Icke, kiukweli kazi zake ni miongoni mwa kazi za
mwanzo kabisa zilizo ni fungua akili kuhusiana na ulimwengu wa kimasoni na
njama zao, lakini sikubaliani na Icke kwenye nukta hii ya kwamba kuna viumbe
wengine kutoka au ndani ya sayari yetu ambao kwenye sura hii tumewaita ni ‘wageni’.
Wako watafiti wengi ambao kazi zao nazikubali vizuri, lakini kwenye nukta hii
nakwenda nao njia tofauti, achilia mbali kuwa ni suala linalo husu mtazamo
zaidi, lakini bado hakuna ushahidi wa kutosha na wenye mashiko juu ya kuwepo
kwa viumbe hao na kazi zao.
Unaposikiliza na kusoma taarifa za wale ambao wanadai kukutana na ‘wageni’
hao labda kwa kutekwa au kutokewa kwa njia za ajabu na ‘wageni’ na taarifa
walizozipata au maelekezo kutoka kwao utaona hazina tofauti hali ya kukutana
kwao na aina za taarifa na utaratibu wa kuzipata hizo taarifa na ule wa viumbe
tunavyoviita ni majini au mashetani!
Mwaka 1969, Lynn Catoe alikuwa ni miongoni mwa watu wenye jina katika watu
walio kuwa wakilifanyia kazi suala la UFO na ‘wageni’. Baada ya miaka miwili ya
utafiti wake na maelfu ya makabrasha na vitabu alivyo pitia kuhusiana na somo
hilo, alihitimisha kuwa kuna mahusiano ya msingi na ya muhimu baina ya suala la
UFO na uchawi. Alisema,
“Sehemu kubwa ya maandishi yanayo patikana kuhusiana na UFO … yameegemea
kwenye hali ya kusoma akili, kalamu inayo andika yenyewe bila mwandikaji
kuonekana, kujitokeza kwa kiumbe cha maajabu kama jini, muhusika kuwa na hali
sawa na ya mtu aliye ingiliwa na pepo, hali zinazo elezeka kisaikolojia zaidi
(kusikia sauti kwenye masikio/akili yako bila kumuona anayekusemesha)”
Profesa Elizabeth L Hillstrom naye katika kitabu chake alicho kiita
‘Testing the Spirits’ amehitimisha kuwa taarifa na habari za UFO zikiwemo tabia
zake zinalingana sana na zile za mashetani ambao utakuta hadithi zao katika
kila utamaduni duniani, ikiwemo kwenye vitabu vya dini mbalimbali.
Pierre Guerin mwanasayansi anaye husiana na French National Council for
Scientific Research, na mtafiti wa masuala ya UFO anasema,
“Yanayo husiana na UFO leo hii na matukio ya majini katika zama zilizo pita
ni mambo yanayo fanana”
Mtafiti na mwandishi John Keel aliye andika vitabu mbalimbali kikiwemo kile
cha UFOs: Operation Trojan Horse amekuja na majibu sawa na hayo hapo juu,
kwamba UFO na viumbe wake tabia zao zinawiana na zile za viumbe wanao fahamika
kama majini.
Kwa sababu sayansi kwa namna mbalimbali haina sheria wala taratibu au
muongozo wakukubaliana na kuwepo kwa viumbe wengine kama Malaika, Majini au
nguvu za kiimani, basi inakuwa ni vigumu kwa wale ambao tunawaita wanasayansi
kukubaliana na hili, labda wanapo kuwa nje ya magwanda yao ya sayansi hapo
watakubaliana na hilo, kwani mbali ya vingi katika maisha yao ya kila siku kama
binadamu wanakutana na hali, vitu na matukio ambayo kisayansi huwezi kuyaeleza
yakaeleweka mpaka utakapo toka nje ya ‘sayansi’ na kutumia njia na taratibu
mbadala kujifunza na kuyaelezea hayo. Hii ndiyo moja ya sababu ya kutokuwa na
taarifa rasmi juu ya kuwepo viumbe wengine kutoka nje ya sayari yetu, kwa vile
kisayansi imeshindikana kuthibitisha badala yake wakaamua kuitumia Hollywood kama
kitengo mbadala cha kuwapandikiza walimwengu nadharia kwamba kuna viumbe
wengine mbali na binadamu, kutoka nje ya sayari yetu, hata kutoka nje ya galaxy
yetu na ambao siyo majini, wala mashetani, wala malaika wanao ishi na sisi na
wanao tutembelea kupitia UFO.
Wakati watafiti wa mambo ya UFO wakiwa wamegawanyika makundi mawili, wako
wanao dhani kuwa matukio yanayo semwa kuwa ni hali ya kutembelewa na ‘wageni’
kutoka mbali au baadhi ya binadamu wenzetu kukamatwa na viumbe hao na baadaye
kuachiliwa kuwa hii ni kazi ya mashetani mia kwa mia, mashetani ambao wanalenga
kuwaharibu binadamu kiroho, kukivuruga kizazi cha binadamu na kupandikiza mbegu
zao za uzazi kwa binadamu kama walivyo fanya awali na kuzaana na mabinti wa
binamu. Watafiti wengine wa UFO wanaliona hili tofauti, wanadai kuwa waandishi
wa biblia walitafsiri matukio wasiyo yafahamu kwa namna ileile kama ambavyo
sisi tunavyo tafsiri matukio haya kwamba hawa ni mashetani, lakini kumbe huo si
ukweli bali uoni wetu wa kiimani ndivyo unavyo tuongoza.
Sasa kipi ni kipi hapa? Katika rekodi za kale na zile zinazo patikana
kwenye kitabu cha Mwanzo, zinadai kuwa malaika wasio kuwa watiifu pamoja na
shetani mwenyewe walifukuzwa na kushushwa kutoaka mbinguni kuja aridhini, (hili
la malaika kuasi halikubaliki kwenye mafundisho ya Kiislamu, kwani malaika
hawana sifa hiyo ya kuasi. Bali kutokana na mafunzo ya Kiislamu Shetani
mwenyewe ndiye aliye asi na kufukuzwa kutoka kwenye rehema za Muumba wake,
Kutokana na mafunzo ya biblia viumbe hawa walipofika aridhini walizaana na
mabinti wa binadamu na kutengeneza ‘viumbe wenye sifa’ yaani wenye sifa na
nguvu za maajabu, viumbe hao waliitwa wana miungu.
Katika mafundisho ya
Kiislamu ni kwamba mpaka leo hii majini bado wanazaana na binamu katika hali
mbalimbali, na viumbe hao wanao zaliwa na binadamu akishirikiana na mashetani,
wanaweza wakaonekana au wasionekane, na kwenye mafunzo haya jambo hilo halifai
kwa binadamu kufanya ngono na kiumbe chochote isipokuwa binamu mwenzake tena wa
jinsia tofauti na yake tena kwa sheria, yaani ndoa. Binafsi hadithi kama hizi
nimepata kuzisikia kwa mtu ambaye yeye anasema amemsikia muhusika mwenyewe
akidai juu ya kuwa amezaa na jini ila watoto hajawaona, jini lenyewe ndilo
lilimpatia hizo taarifa.
Lakini watafiti wa UFO wengine wanadai kuwa, tukio lililo elezewa kwenye
kitabu cha ‘Kutoka’, ambalo viumbe hao walizaana na mabinti wa binadamu si
kweli, bali ‘wageni’ hao walichukua genetiki kutoka kwao wenyewe na kumuumba
binamu wa mwanzo wa kike na wakiume ambao sisi tunawaita (Adamu na Hawa) na
wanasema hii ndiyo maana ya maneno yanayo sema ‘tumuumbe mtu’ kwa mfano wetu.
Viumbe hao ndiyo wanao rudi tena na bado wanaendeleza tafiti zao na majaribio
juu ya binadamu hasa kutokana na hadithi nyingi za wale walio kamatwa na viumbe
hao kudai kuwa kuna wakati wanalazwa kwenye meza na kuchukuliwa damu zao na
kufanyiwa vitu ambavyo madaktari wetu huvifanya katika tafiti zao mbalimbali.
Je ni kweli tumekwisha vamiwa na ‘wageni kutoka mbali’ au
Shetani/Ibilisi/Lucifer yuko kwenye mpango kamambe wa ajenda yake ya
kusimamisha utawala wake kwenye dunia yetu?
Inahitaji zaidi ya jicho la kawaida kwa mtoto kubaini kuwa zawadi anazo
pewa wakati wa sikukuu ya Krismasi hazitoki kwa Santa, bali wazazi. Nchi za
Ulaya wana utamaduni wa kuwanunulia watoto wao zawadi na kuzificha na kuwapatia
siku ya Krismasi kwa kuwaambia kuwa zimeletwa na Santa. Je unawezaje kumuambia
mtoto huyu kuwa hakuna kitu”/mtu kama ‘Santa’ ikiwa shuleni kafundishwa hivyo,
anamuona Santa kwenye filamu na katuni na anamuona Santa kwenye matangazo mbalimbali
ya biashara na anamuona Santa akimpatia zawadi wakati wa sikukuu ya
Krismasi. Lakini mbaya zaidi ni mimi
ndiye ninaye paswa kumuambia mtoto kuwa hakuna Santa na zawadi hizo wamenunua
wazazi. Upo tayari … usingekuwa unasoma posti hii kama hujawa tayari,
twende nitakuonesha njia lakini ni wewe utakaye paswa kupita kwenye njia hiyo.
Kama zilivyo zawadi za mtoto kabla ya Krismasi kuwa hununuliwa na wazazi wa
mtoto na baadaye kumdanganya mtoto kuwa zimenunuliwa na Santa, UFO nazo ni kazi
za binadamu wenyewe, ni kazi ya serikali za kimasoni kote duniani ambazo
wanazifanya kwa siri katika maeneo mbalimbali duniani waliko weka ngome na
himaya zao, hasa zilizo chini ya aridhi, na baadaye huvirusha vyombo hivyo
wakijifanya hawavijui ni vya nani na vimetoka wapi Kwa kutumia mtandao wao
mpana wa vyombo vya habari hutuambia kuwa vyombo hivyo ni UFO na huenda ni kazi
ya viumbe wasio julikana.
Kwa kutumia aina mbalimbali za vituma taarifa kama tutakavyo ona punde,
hutuma picha, sauti na hata sura ya kitu kamili katika baadhi ya akili za watu
na kuwarubuni kuwa wamesikia sauti za viumbe hao zikiwa elekeza kufanya kadha
wa kadha, au wamepata ufunuo au wamepata upako. Hii tu ni baadhi ya misamiati
inayo tumika kuelezea aina hii ya matukio. Lakini hata hivyo matukio kama haya
wakati mwingine yana kwenda mbali zaidi na kuwahusisha mashetani yenyewe kuliko
vyombo maalum vinavyo tumika kurubuni akili za watu.
Kuhusu mashimo yaliyomo aridhini na himaya pamoja na kambi za kijeshi
huenda tukalitazama katika kazi zingine au yeyote akajitolea na kulielezea hili
katika lugha yetu ya Kiswahili.
Tangu wazee wetu walipoanza kurekodi matukio ya UFO, tangu hadithi za
kufikirika kuhusiana na viumbe hivi zilipo anza kurikodiwa tabia na hali zao
zimekuwa zikifanana na zilezile za viumbe tunao wafahamu kama majini. Jacques
Vallee kwenye kitabu chake alicho kiita Passport to Magonia ameonesha uwiano na
ufanano wa hali ya juu baina ya matukio ya UFO na yale ya mashetani, anasema,
“Pia nina shawishika kukubaliana na nadharia kwamba zamani sana mawasiliano
yalipatikana baina ya binadamu na viumbe wengine ambao walifahamika kama
majini, malaika au kama tunavyo waita leo, viumbe toka nje ya dunia yetu.”
John Keel kwenye kitabu chake cha Operation Trojan Horse, amesema,
“Ushetani siyo kitu cha kibubusa. Ni elimu ya kale ambayo watu walikaa na
kujifunza kuhusiana na mashetani na majini ambao walionekana kuwepo pamoja na
binadamu kote kwenye historia … namna ambavyo walijitokeza na kuonekana kama
ilivyo elezewa kwenye nakala hizo za kale kuna wiana, kama siyo kufanana kabisa
na tabia za UFO zenyewe. Wahanga wa mashetani (wale wanao pandisha mashetani au
kuingiliwa na hayo mashetani) wanapata taabu na matatizo yaleyale ya
kisaikolojia, kihisia na kiafya kama yanayo wapata watu ambao wanasema wamekutana
au kuwasiliana na ‘wageni…”
“Mashetani na majini wanaweza, kutokana na maandishi mbalimbali, kujionesha
wenyewe katika aina ya umbile lolote lile na kimaumbile wanaweza kuvaa taswira
yoyote ile kutoka ile ya malaika mpaka ile ya kiumbe chenye kutisha na chenye
macho yenye kutoa nuru kali. Vitu vya ajabu na viumbe vinatokeza na kupotea
katika hadithi hizo, kama ambavyo UFO na
wamiliki wake wanavyo jitokeza na kupotea, kupita kwenye ukutani (siyo
dirishani wala mlangoni na kufanya mambo mengine ya kimaajabu)”
Ingawa kwenye duara la ‘sayansi’ hatuna viumbe kama majini na malaika
ijapokuwa ‘wana wa sayansi’ kwa namna na njia tofauti wanakubaliana juu ya
kuwepo kwa viumbe hao, na kwa kuwa ‘serikali’ kivitendo haikubaliani na athari
yoyote inayo tokana na viumbe hao, na hivyo kwa njia ya mkato inakataa juu ya
kuwepo kwa viumbe hao, ingawa watumishi wa serikali kama walivyo ‘wanasayansi’
wanakubaliana na kuwepo kwa viumbe hao na athari zao, nafasi ya UFO kwenye
macho ya ‘wanasayansi’ na ‘serikali’ inakuwa ya mkanganyiko zaidi hasa kutokana
na kwamba ‘serikali’ na ‘wanasayansi’ wanalitazama jambo hili kama ‘kitisho cha
viumbe’ kutoka nje ya sayari yetu bila kuweka hadharani ushahidi usio na shaka
na wakati huohuo watafiti huru wakiweka hadharani ushahidi wa kutosha kuwa
viumbe hao si wengine bali ni ‘maswahiba’ wetu wa muda mrefu tangu enzi na
enzi, yaani majini.
Swali ni je ‘serikali’ na baadhi ya taasisi zake za sayansi zinapatia wapi
ushahidi kiasi cha kuweza kuwaambia walimwengu, ingawa si kwa njia ya moja kwa
moja, lakini kwa namna tofauti kuonekana kukubaliana na taarifa hizo juu ya
kuwepo kwa viumbe toka nje ya sayari yetu na kwamba ni kitisho, kwa nini
serikali na ulimwengu wa sayansi ya anga wanakubaliana na hili, na ikiwa huo
siyo ukweli wa msingi kama tulivyo ona, ni nini ajenda ya siri nyuma ya hili la
kudai viumbe hao wapo?
Lakini si unajua kuna New World Order? Lakini si unajua kuwa karata ya
mwisho itakuwa ni ‘vita baina ya binadamu na viumbe toka mbali’? Kwa watafiti
huru wa mambo ya UFO na New World Order ni kuwa serikali na ‘sayansi’ wanapigia
debe taarifa hizo kwa lengo lilelile la New World Order ambayo kiongozi wake
atakuwa na ‘damu takatifu’ na mwenye nguvu za maajabu.
Mmoja anaye tegemewa ni wazo ambalo liko kwenye imani ya dini mbalimbali
duniani, ikiwemo kwenye Uyahudi, Uislamu na Ukristo na bila kusahau kwenye
imani na dini za kishetani ukiwemo Freemasons. Wote wanasubiri juu ya kuja kwa
Messiah, ambaye atakaye kuja kuuokoa ulimwengu. Kutokana na mafunzo na falsafa
za kimasoni ni kuwa Masiha wa kwanza, yaani Yesu alikuja kwa ajili ya
kusimamisha ufalme wa mbinguni, lakini Masiha wa mara ya pili ambaye ni …?
Atakuja kuisimamisha New World Order chini ya utawala wake.
Kuhusiana na Masiha huyo, Freemasons wa daraja la 33 Manly P. Hall, katika
kitabu chake cha “The Secret Destiny of America ameandika hivi,
‘’Jawabu la mpango huu wa siri ni World Order chini ya mfalme mwenye nguvu
za kimaajabu. Mfalme huyu anatokana na ukoo wa wenye damu tukufu; hii ni
kusema, anatokea kwenye asasi ya Illuminati na walio na hekima, anatokana na
familia ya mashujaa ya binadamu walio wakamilifu’’
Mtu aliyetajwa na Hall sote tunamjua ni nani, ametajwa vizuri kwenye vitabu
vitakatifu, hasa kwenye mafundisho ya Kiislamu. Wasomi na watafiti huru dini zote watakubaliana na mimi kwamba hakuna
dini iliyo weza kuelezea vyema maisha yatakayo kuja na alama zake, maisha ya
kaburi na maisha ya motoni na peponi kama Uislamu, na mtu huyu ametajwa vilivyo
na alama zake mbalimbali katika mafunzo hayo ya Uislamu.
Duuh mungu atunusuru jmn!ila mi naomba unieleweshe kuhusiana na kuona future yani ndoto inatokeaje had unaona yatakayo kuja
ReplyDeleteKuona kitu ndotoni na kisha ukaja kukiona ‘live’ ni katika maumbile ya mwanadam ambayo Mola katuumba hivyo.
DeleteISPOKUWA KUNA TANBIHI
Si kila ndoto unayoiyona ni ndoto ya kweli.
Si kila anayeota ndoto kaota kitu cha kweli.
Na sikila mtu anaweza kukueleza maana hasa ya ndoto.
Binaadam anapokuwa kiroho, kiakili na kimwili yupo sawa sawa, basi anayo nafasi kubwa sana ya kuiyona ndoto, na baadae akaiyona katika masiha halisi. Kuwa sawa kwenye maeneo hayo ni kuwa maisha yako yamefungamana na mfumo sahihi wa maisha masaa ishirini na nne. Yaani wewe ni muumin safi, ingawa silazima uwe muumin ndiyo uote ndoto ya kweli.
Hivyo utaona hii ni neema katika neema za Mola wetu na humpa amatakaye kwanamna anavyo taka.
KINGINE
Maisha yetu ya siku zote tangu unazaliwa mpaka unakufa ni NDOTO…….?????!!!!!!!!!!!
kak 2pe tofaut kat ya ibilisi, lucifer na dajjal
ReplyDeleteIblis au Ibilisi ndiye anayefahamika kama Lucifer, huyu ndiye kiongozi wa vita dhidi ya mwanga (Muongozo sahihi wa Maisha uliowekwa na Mola Mwenyewe).Ni kiongozi wa vita hivyo tangu alipowateremsha wazee wetu kutoka Peponi na ataendelea kuvisimamia vita hivyo mpaka mtu wa mwisho atakapokufa hapa duniani.
DeleteDajjal, au Masih Dajjal, au Mpinga Kristo au Ant Christ, huyu naye ni kama msaidizi wa Iblisi kwenye vita hivi, atakapofika kazi na malengo yake yanaowana na yale ya Iblis, kuwatoa watu kwenye Nuru na kuwapeleka kwenye Kiza, na hata sasa Iblis akishirikiana na majini wengine na binaadam wenzetu wanaandaa zulia jekundu ambalo Dajjal atakuja kupita juu yake wakati wa kutekeleza misheni yake.
Iblis atakufa kifo cha kawaida kabla ya Kiyama kusimama na Dajjal atauwawa Jerusalem na Issa mwana wa Mariam (Yesu) Jerusalem, mahala panapoitwa Baab Lud, Telavivi, na hapo Issa (AS) ataanza kuhubiri mfumo sahihi maisha na kuwarudisha watu kwenye nuru, nako ni kwenye dini inayowiana na maumbile kamili ya binadam, dini ya Kiislam.