AJABU ILIYOJE KWA MAFUNZO HAYA MAPYA NDANI YA UISLAM, NI KINYUME KIASI GANI MAFUNZO HAYO NA DINI WANAYO DAI KUITETEA?
Hii ndiyo iliyo kuwa picha kubwa ambayo CIA na mawakala wengine wa
Illuminanti walifahamu. Kupitia sera chafu za kupigania uhuru kwa njia ya
silaha, kupitia mafunzo yaliyo potoshwa ya dini ya Uislam waliweza kuwaandaa
vijana hawa kutoka sehemu mbalimbali kwenye uso wa dunia na kuwaleta mahala
pamoja kama wapigania jihadi.
Vijana hawa wa Mujaheedina watakapo maliza kazi
yao ya kuiangusha USSR kama super power, watapewa kazi nyingine na wajiri wao, kazi
ambayo katika zama zetu tunaifahamu vyema kama Ugaidi. Kazi hii mwongozo wake
pamoja na maudhui yake havitoki kwenye mafunzo ya dini ya Uislamu bali kwenye
mahekalu ya kimasoni na mawakala wa Illuminanti.
Mwanastratejia wa Illuminanti bwana Brzezinski ambaye kwa sasa anashikilia
wadhifa muhimu kwenye serikali ya kibaraka mwingine wa Illuminanti na Freemason
wa daraja la 32 bwana Barak Obama, alipokuwa akihojiwa mwaka 1998 kwenye
mazungumzo aliyo yafanya na Le Nouvel Observateur alikiri kuwa CIA iliwasaidia
mujaheedina kwenye mapambano dhidi ya USSR. Alisema kuwa July 3, 1979 aliyekuwa
rais wa Marekani kipindi hicho Jimmy Carter alisaini na kupitisha mwongozo wa
kwanza wa kuwasaidia Mujaheedina kwa siri.( “Interview
With Zbigniew Brzezinski”, Le Nouvel Observateur.<http://members.aol.com/bblum6/brz.htm>)
.jpg)
Ni katika kipindi hichi mwanastratejia huyu alianza kuziita nchi za Iran,
India na Afighanistani kuwa ni muhimili wa maovu duniani, sera ambazo
zimeendelea kutumia hata na rais Bush na sasa zinatumiwa na Obama pia.
Kuzipachika nchi hizo jina hilo sababu yake ni kutengeneza na kuwapa nafasi ya
kutanuka kwa vikundi vinavyo julikana kama ‘Waislam wenye siasa kali’, hivyo
nchi hizi zilijukana na bado zinafahamika kwa mujibu wa sera za Marekani kuwa
ni nchi zenye kusaidia ugaidi duniani.
Lakini hayo hayakumzua Carter kusaini mwongozo wa kuvisaidia vikundi hivyo
ambapo kitendo hicho ni kinyume na katiba ya Marekani na ni kinyume na mwongozo
wa UN. Kwa nini basi Carter aliwasaidia, Carter aliwasaidia kwa vile vikundi
hivi ni wao ndiyo wamevianzisha kupitia mtandao mpana unao zahusisha nchi
kadhaa za bara la Ulaya na mashirika yao ya kijasusi na pia zikiwemo nchi za Kiarabu
na malengo ya vikundi hivi si kuusaidia Uislamu kwa kupambana na nchi za Ulaya
na washirika kama watu walivyo fanywa waamini, bali kuubomolea mbali Uislamu na
wakati huohuo vikitekeleza matakwa mengine ya Illuminanti kama lile la
kuiangusha USSR ili Marekani inyanyuke kama super power, na kwa sasa vikundi
hivi kama tunavyo ona vinashirikishwa vilivyo kuhakikisha vinaukokota uma wa Kiislamu
kwenye uwanja wa WWIII.
HII NDIYO PICHA AMBAYO WATU WANAPASWA KUWA NAYO, KILA JINA 'UISLAM na MUISLAM' LINAPOTAJWA. JUHUDI KUBWA IMEFANYIKA HATA SASA NI VIGUMU KUONA AU KUSEMA TOFAUTI NA PICHA HIYO.
Mpango huu wa CIA kuwasaidia Mujaheedina Afighanistan ulikuja kufahamika
kama Iran-Contra-Affair ambapo mbali na mambo mengine Marekani walihusika na
kuwauzia Iran silaha kwa ajili ya kupambana na Iraq na pia ikawauzia Iraq nao
silaha katika mpango ulio itwa Iraq-Gate, huu ni mchezo wa kawaida kwa Marekani
na Illuminanti kufadhili pande mbili za vita kwa wakati mmoja, kwani mwisho wa
siku ni wao wanao faidika na vita hivyo. Hapa utaona Marekani inaziuzia silaha
nchi ambazo yenyewe inazitambua kuwa ni nchi za kigaidi duniani.
NI WAPI WANATOLEA SILAHA HIZI?
Mkutano wa asasi ya siri ya Bildeberg uliofanyika mwaka 1973 ambapo kwenye
mkutano huo walijadili kuhusu kupandishwa kwa bei ya mafuta duniani na baadaye
mwaka 1974 bei hiyo ikapanda kwa kasi sana, faida kubwa iliyopatikana katika
ongezeko hilo la bei ya mafuta ilitumika kati ya mengi ni ufadhili shughuli ya
Iran-Contra-Affair, na mipango mingine michafu ya kuunda vikundi vya kigaidi
sehemu mbalimbali duniani. Wakati haya yote yanafanyika mshirika mkubwa wa
Marekani kwenye hili alikuwa na bado anaendelea kuwa ni Saudi Arabia chini ya
uongozi wa Wahhabisim.
Kwenye utawala wa Saud Arabia alikuwepo mtu aliyeitwa Prince Bandar
aliyetumiwa na CIA kwa niaba ya utawala wa Saud kuufadhili mpango mzima wa
Contra, Prince Bandar bin Sultan ambaye alikuwa ni mjukuu wa Ibn Saud na Hassa
bint Ahmed al-Sudairi, mmoja wa wanawake wenye kuheshimika sana ndani ya Saud
Arabia. Prince Bandar aliteuliwa kuwa balozi wa Saudia ndani ya Marekani mwaka
1983 na alishikilia wadhifa huo kwa miaka 20. Alikuwa ni rafiki wa karibu na
familia ya Bush. Bandar alitumiwa kama kiunganisha baina ya serikali ya Marekani na Saddam, pale uongozi wa Saddam
alipoonesha nia ya kupokea msaada kutoka kwa Marekani. Kwa siri utawala wa
Regan uliziruhusu nchi za Saud Arabia, Egypt na Kuwait kusafirisha silaha
zilizo tolewa na Marekani kwenda kwa Saddam, silaha zingine zikauzwa kwa Iran
ambazo ziliwafikia Mujaheedina wa Afighanistan. Saud Arabia ilichangia kiasi
cha dola za kimarekani milioni thelathini na mbili kwenye Contra. (U.S. News & World Report, 15 December
1986)
.jpg)
WAKATI WOTE WAMEVAA MAVAZI YA KIISLAM, LAKINI KAZI YAO NI KUUBOMOA HUO UISLAM WANAO DAI KUUTETEA.
Contra haikuishia kwenye fedha za mafuta peke yake, fedha za dawa za kulevyea
ambazo ziliuzwa kwenye mtandao mpana kwenye majiji na mitaa mbalimbali duniani
nazo ziliingizwa kudhamini Contra, Mujaheedina walio kuwa wanadai wanapigana
Holy War walikidhi mahitaji yao na kuendeleza mapambano kwa muda mrefu kwa
kutumia fedha za dawa za kulevyea zilizo wafikia kupitia kwa CIA, kupitia kwa
shirika la kijasusi la Pakistan, na kupitia kwa mawakala na vibaraka wengine wa
Illuminanti. Ni vipi unapigana Holy War kwa kutumia pesa za dawa za kulevyea?
Wakati wa vita ya Vietnam, CIA wakishirikiana na makabila ya Vietnam
walishiriki kwa kiasi kikubwa kusafirisha dawa za kulevyea kutoka kwenye eneo lilioitwa
Triangle Kusini mwa Asia. Kabla ya hapo ni Ufaransa ndiyo waliokuwa
wakiishikilia biashara hiyo katika eneo hilo. Hata baada ya vita na Vietnam
kumalizika Marekani bado waliendelea kuishikilia biashara ya mihadarati eneo
hilo.
YES, THIS IS CIA ... OR WAS IT CONFISCATED EVIDENCE ...? I DON'T KNOW, BUT IT WAS ON THEIR PLANE!!!
Tangu mwanzo wa vita baina ya USSR na Mujaheedina, CIA walikuwa wamesha
tengeneza mahusiano mazuri na Pakistani kupitia shirika la kijasusi la Pakistan
la ISI. Benki iliyotumiwa kuwafikishia Mujaheedina fedha za dawa za kulevyea na
fedha ambazo zililengwa kwa ajili ya misaada sehemu mbalimbali duniani ni Bank
of Credi and Commerce International, BCCI. Benki hii ilianzishwa mwaka 1972 na
Agha Hasan Abedi kutoka Pakistan akiwa amepokea fungu kutoka kwa Sheik Zayed wa
Abu Dhabi ambaye alitegemea kuitumia benki hiyo vilivyo kutokana na fedha za
ziada zitakazo zalishwa kwenye mfumuko wa bei ya mafuta kwenye miaka ya 70. (The Outlaw Bank, uk. 109.)
MWANZILISHI WA BENKI YA BCCI
Utakumbuka mfumuko huo wa bei ulipangwa kwenye mkutano wa asasi ya siri wa
Bilderberg, na mwaka ulio fuata mfumuko wa bei ukatokea na mabilioni ya dola ya
ziada yaliyo zalisha hapa yalikwenda kuwafadhili mujaheedina kupitia BCCI na
nyingine ziligawiwa kama mikopo kwa nchi zinazoendelea kupitia WB na IMF, deni
ambalo mpaka sasa ni jinamizi lililozimeza nchi zetu.
Unapo zungumzia mchezo mchafu wa kusafisha pesa za dawa za kulevyea na
kutumia pesa za misaada na pesa za mafuta kwa ajili ya kuwadhamini watu walio
itwa mujaheedina basi huwezi kuwacha kuzungumzia kuhusu BCCI. Benki hii ilikuwa
ni benki ya kwanza yenye nguvu kuliko benki zote katika nchi zinazoendelea
kutokana na utajiri mkubwa uliomiminika kutokea Mashariki ya Kati kutokana na
ongezeko la bei ya mafuta kwenye miaka ya 70. Pesa chafu za CIA kwa ajili ya
kudhamini magaidi ambao waliitwa mujaheedina au wapigania uhuru zilipata njia
nzuri kwenye benki ya BCCI. Wauza silaha za magendo, wauza dawa za kulevyea
kutokea Asia mpaka Amerika ya Kusini, makundi ya wahalifu na mashirika ya
kijasusi kama vile ISL, Mossad, M16 na CIA yote yalipata kimbilio kwenye benki ya
BCCI. (Richard H. Curtiss, “What You
Won’t Read About Michael Harari, Noriega Is Israeli Adviser Who Got Away”.
Washington Report. February 1990)
BCCI ilikuwa na tawi Panama, ambapo kibaraka wa serikali ya Marekani na
nyenzo muhimu kwa CIA, Manuel Noriega ambaye pia alikuwa ni kiungo muhimu kwa
biashara za dawa ya kulevyia baina ya CIA na wadau wengine eneo hilo, alitumia
tawi hilo la Panama kupitisha fedha hizo kutoka nchini humo. Alikuwepo mtu
aliyeitwa Michael Harari, jasusi wa Mossad ambaye baada ya kumaliza kazi yake
ndani ya Palestina alipelekwa Amerika ya Kati na Kusini ambapo aliunda mtandao
uliofanya kazi ya kusafirisha bunduki na dawa za kulevyea baina ya wateja
mbalimbali walio hitaji bidhaa hizo na kutengeneza faida kubwa ambayo ilifuata
njia ya moja kwa moja mpaka kwenye mifuko ya kanzu za wa Taliban. Kipindi hichi
Marekani na CIA waliacha kununua dawa za kulevyea kutoka kwa watu mmojammoja
bali waliwashauri vinara hawa kuungana na kuwauzia bidhaa hizo kama kikundi au
kampuni badala ya mtu mmoja mmoja. (Uri
Dowbenko, “Book Review”, Conspiracy
Digest.http://www.conspiracydigest.com/bookdefrauding.html)
.jpg)
Harari alipokuwa anazungumzia biashara hii
alisema hivi,
“Tunachokifanya
hakihusiani chochote na kulinda maslahi ya nchi, hii ni biashara tu na nchi za
dunia ya tatu ...Tunawapatia mafunzo ya kijeshi na kuwapatia silaha na wao kama
njia ya biashara wanatupatia bidhaa yenye thamani kubwa zaidi kushinda silaha
na fedha. Tizama thamani ya bunduki moja na risasi zake ni dola 1200. Kilo moja
ya Cocain ni kama dola 1000. ... Kwa upande wetu tunatumia dola 1200 kwa kila
kilo moja ya Cocain na tunakuja kuuza hiyo kilo moja kwa dola 12,000 mpaka
15,000. Hichi ni kituo cha kutengeneza faida na soko la cocain ni kubwa
kushinda soko la silaha. Kwa hiyo hii ni biashara tu. Umeelewa?” (Ibid)
Alichokisema Hariri si kigeni katika nchi
zetu za duniani ya tatu, bado kinaendelea kufanyika na bado kitaendelea sana tu
kufanyika, daima vikundi vyote vya waasi katika nchi za dunia ya tatu vimekuwa
vikifanya biashara ya namna hii na Marekani pamoja na washirika wake
wakishirikiana na mashirika yao ya kijasusi. Eidha ni silaha na mafunzo kwa
dawa za kulevyea, au silaha na mafunzo kwa rasilimali zingine za nchi kama
madini, mafuta, aridhi na vinginevyo. Daima utajiuliza swali moja, watizame
waasi wa Kongo, watizame waasi wa Somali, waliokuwa waasi wa Ivory Cost,
watizame waasi wa Sudan na kwengineko duniani, utawaona wamevaa nguo safi
nadhifu, wamebeba silaha nzitonzito, lakini nchi nzima imemezwa na umasikini,
imefunikwa na kiza cha shida, ukosefu wa huduma za kijamii, miundo mbinu
mibovu, njaa na umasikini wa kutisha, lakini waasi na washirika wao utadhani
hawaishi hapo wako safi kisilaha na kimavazi ya kivita, kwa nini? Kwa vile watu
walewale wanao dai kuwakalisha kwenye meza
kwa ajili ya mazungumzo ya amani ndiyo watu haohao kupitia mawakala wao
wanawapatia waasi na washirika na hata serikali zao silaha na mafunzo kwa ajili
ya kurefusha mapambano, kwani kama walivyo sema wahenga, vita vya Panzi .... Naam kama alivyo sema Hariri, it is just a business.
.jpg)
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA
Kuzaliwa kwa BCCI na kukuwa kwake kuna mahusiano makubwa na vita baina ya
USSR na Mujaheedina. Bhuto wa Pakistan alikuwa ni kila kitu Bigbrother
wasichokihitaji na hivyo aliondolewa na nafasi yake ikachukuliwa na Zia ambaye
alimuweka mtu aliyeitwa Fazle Haq kuwa msimamizi kwenye jimbo la Kaskazini
Magharibi mwa Pakistan mwaka 1978. Eneo hili linapakana na Afighanistan na
ndilo liliokuwa uchochoro wa kupitisha tani na tani za dawa za kulevyea na
silaha. Fazle Haq pia anatajwa kwamba alikuwa ni rafiki mkubwa wa mwanzilishi
wa BCCI bwana Hasan Abedi. Pesa za dawa za kulevyea kwa ajili ya watu walio
itwa mujaheedina zilipitishwa na kusafishwa na BCCI.( Time magazine, “The Dirtiest Bank of All”, 7.29.91)
October 13, 1996 jarida la Executive Intelligence Review liliandika habari
yenye kichwa cha habari, “Anglo-Amerika imekuwa ni kifaa cha kuwasaidia
Mujaheedina wa Afighanistan” Ni katika kipindi hichi kulianzishwa redio
iliyoitwa “Radio Free Kabul” ambayo ilitumika kama sauti kwa mujaheedina, mwanzilishi
wa redio hiyo hakuwa mwingine bali ni jasusi wa Uingereza bwana Lord Nicholas
Bethell. Hapa unaona Mujaheedina wanapigana holy war na USSR, lakini unakuta
wahusika wakubwa kuanzia kwenye udhamini wa vifaa vya kivita, gharama za
kuendeshea hivyo vita, na mpaka wapiganaji wenyewe wanatolewa na nchi za Ulaya,
Marekani na washirika wao, na unakuta nchi hizo zinafanya mengi makubwa,
zinakiuka katiba zao, na katiba za kimataifa kama za UN ambazo ni wao
wameziweka ili kuwasaidia hao wanao itwa ni mujaheedina ambao kwenye katiba zao
wanatajwa wazi kuwa ni magaidi, hapa utajiuliza swali moja la msingi ‘Je hivi
ni vita vitakatifu au kuna mazingaubwe ambayo jicho la kawaida haliyaoni?”
.jpg)
Ndani ya miaka miwili tu ya CIA kufanya kazi kwenye mpaka baina ya
Afighanstan na Pakistan hatimaye Pakistan wakaibuka wazalishaji namba moja wa
dawa za kulevyea kwa ajili ya soko la Marekani ambapo Pakistani alizalisha
kadiri ya asilimia 60 ya soko zima. Wahanga wa dawa za kulevyea ndani Pakistan
peke yake iliongezeka kutoka idadi inayo karibiana na sifuri mwaka 1979 mpaka
milioni 1.2 mwaka 1985. (Alfred McCoy,
Drug fallout: the CIA’s Forty Year Complicity in the Narcotics Trade. The
Progressive; 1 August 1997.)
Hivyo unapotizama vikundi mbalimbali vya kigaidi kote duniani utakuta si
kwamba tu havifanyi kazi vyenyewe lakini pia mitandao ya vikundi hivyo imepenya
kwenye nafasi za juu za serikali za nchi kubwa za kimagharibi ambazo ndizo
zilizopo mstari wa mbele kupambana na ugaidi.
Watu wa kawaida kwenye vikundi hivyo wanaonekana ni waumini wazuri wa dini
ya Kiislam, lakini kama ulivyo utaratibu wa vikundi hivyo, wafuasi wa kawaida haambiwi
yote kuhusiana na kikundi chake na hii ni asili ya vikundi vyote vilivyo jengwa
kwenye nadharia ya kimasoni. Lakini wale viongozi wakubwa wa vikundi hivyo
ambao hutawaona kwenye maandamano wala kwenye uwanja wa vita, ni watu wenye
suti zao nadhifu, leo wako New York kesho wako London, keshokutwa wako Abu Dhabi
mwezi ujao wanayo mkutano Durban, wanafanya business
za mabilioni na wanachama wengine wa Illuminanati. Wanamiliki mabenki,
wanamiliki mali za mabilioni kutoka kwenye biashara za mafuta mpaka kwenye
uuzaji haram wa silaha, dhahabu na dawa za kulevyea. Wako juu, wanapokea
mipango kamambe ya namna gani vikundi vyao vya kigaidi vitafanya kazi kutoka
kwenye mahekalu ya kimasoni, na wao wana wadondoshea wanachama wao wa kawaida
vijisenti ili waendeleze miradi ya kibinadamu na kijamii kwa jina la vikundi
hivyo. Kile ambacho jicho la kawaida halioni ni nguvu kubwa ya vikundi hivyo
kupitia serikali mbalimbali za kimasoni duniani. Kile ambacho jicho la kawaida
halioni ni kuwa wale wanajulikana kama magaidi na wale ambao wanaupinga ugaidi
na magaidi wote ajenda yao ni moja.
.jpg)
Wakati Marekani na washirika wake walipo taka kuing’oa USSR kupitia kwa
Mujaheedina ili wabidi CIA kushughulika vilivyo katika kuwaandaa, kuwapa
mafunzo, kuwalipa na hatimaye kuwasafirisha watu ambao waliitwa wapigania
uhuru, au ukipenda mujaheedina na au kwa uwazi zaidi magaidi kutoka sehemu
mbalimbali duniani kuja Afighanstan kuuangusha utawala wa USSR. Mpango Huu
ulifanyika ukiwashirikisha Muslim Brotherhood. Watu walitolewa kutoka Ulaya,
Afrika ya kaskazini, Afrika Mashariki, Mashariki ya Kati, Asia na ndani ya
Marekani kwenyewe. Mpango huu ulilenga kuwaandaa watu watakao tumika kama
mawakala wa ugaidi kote duniani pale vitakapo malizika vita baina ya wapigania
uhuru na USSR kupinduliwa.
TUMIA AKILI YAKO HURU KUNG'AMUA KAMA KUNA TOFAUTI YEYOTE NA SIYO AKILI YA CNN, AU ALJAZEER AU FOX NEWS
Hivyo vijana hawa waliojitolea kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa nia
safi kabisa ya kupigana holy war kwa kipindi hicho walifahamika kama wapigania
uhuru, lakini baadaye watatumika kutengeneza mtandao utakao fahamika kuwa ni wa
kigaidi dhidi ya Marekani na marafiki zake, na hiyo ndiyo picha kubwa ambayo
wengi hatukuiona kipindi hicho.
Msingi waliopatiwa vijana hawa kutoka sehemu mbalimbali duniani ulilingana
na mafunzo ya karne ya kumi na nane yaliyotolewa na wakala wa Uingereza bwana
Mohamed Abdul Wahhab. Uongozi wa Saudi Arabia nao haukuwa nyuma kwenye hili
King Fahd naye akazimwaga dola kupitia kwenye benki ya BCCI kuwasaidia Mujaheedina.
Haikuishia hapo, shirika la kijasusi la Pakistan lilihitaji mwana wa mfalme wa
Saud Arabia kuviongoza vita hivyo vya jihad dhidi ya USSR. Hata hivyo hakuna
aliyejitolea kutoka kwenye familia hiyo hivyo viongozi wa Saud wakampendekeza
kijana kutoka kwenye familia tajiri na ambayo ipo karibu na familia ya kitawala
ya Saud, naye hakuwa mwingine bali ni Osama Bin Laden.
KAA TAYARI KWA SEHEMU YA MWISHO YA POST HII ... INSHAALLAH....
sasa hii dhulma itaondoshwaje katka dunia mpaka lini
ReplyDeleteDhulma hii inaweza kuondosha na mimi na wewe. Cha kwanza kabisa binadamu lazima tuamke kwenye usingizi tulio lala, cha pili lazima tujifunze elimu sahihi, maarifa sahihi yanayo husu kwanini tuko hapa duniani na wapi tunakwenda na tatu lazima tuchukue uwajibikaji kwa kila kile tunacho paswa kufanya, muda wa kumlaumu huyu na yule haupo, lazima tuwajibike wenyewe kubadilisha hali hii na ndipo NUSRA YA MUUMBA ITAKAPO KUJA.
DeleteVp kuhusu shehe dkt Abdullah Aazam ambae alifariki kwa kupigwa na bomu na kuchanguka vpande huko afghanistani nayeye alikua akitumiwa?
ReplyDeleteLakin je? Unaweza kunithibitishia kuwa osama na marekani lao lilikua ni moja?
Mwisho naomba unitumie makala kadhaa zenye kuonyesha kuwa hv vikundi vya mujahidiina vinavyooendelea dunia vmeundwa kwa manufaa yya nchi za magharib?
Swali lako limejibiwa na baadhi ya Post kwenye blogi hii kama itazipitia moja moja utaona, lakini pia kuna post ya Ossama itakayo kuja baadae nayo italijibu tena swali lako kwa upana, stay Tune here here.
Delete