Pyramid za Mexico
Kama utakumbuka tulikuwa Peru, tulipokutana na mapiramidi matatu yaliyo
jengwa kule ndiyo tukaamua kuja Gaza ambako nako kuna mapiramidi mfano wa yale
ya Nazca, hakuna tulichopata kuhusu wajenzi wa majengo hayo ila maajabu ya kazi
zao.
The work of unknown civilazation of inkown epoch.
Mapiramidi ya Mexico yanakwenda kwa jina la Temple of Quetzalcoat, Pyramid
of the Sun na Pyramid of the Moon. Majengo hayo yana wiana kwa vipimo na yale
ya Misri kana kwamba mjenzi wake ni mmoja. Tofauti ni kuwa kwa hapa Mexco ukuta
wake yamejengwa mfano wa ngazi wakati Misri ukuta wake umenyoka moja kwa moja,
ingawa yapo mapiramidi madogo kule Misri yaliyojengwa mfano wa haya ya Mexico.
Thousands of miles away, different epoch, yet quite similar as if they were in contact with one another. Who are these engineers?
Mapiramidi ya Mexico yanakwenda kwa jina la Temple of Quetzalcoat, Pyramid
of the Sun na Pyramid of the Moon . Majengo hayo yana wiana kwa vipimo na yale
ya Misri kana kwamba mjenzi wake ni mmoja. Kwenye mapiramidi hayo ya Mexico,
kuna kitu kinachoitwa Street of the Dead, tafiti zinatuonesha kitu kingine cha
maajabu kwenye mahusiano ya kimahesabu baina ya mapiramidi hayo , Street of the
Dead na mfumo wa jua, ni kanakwamba mjenzi wako alikuwa anaichora solar system.
Mfumo wetu wa Jua na uwiano wa Majengo na mapiramidi ya mexico.
Kama piramid la Temple of
Quetzalcoatl tukilichukulia ndiyo jua, Street of the Dead itakuwa ikiwakilisha
Asteroid Belt na sayari zilizopo ndani ya ukanda huo wa asteroid, Jupiter na
Saturn ziliwakilishwa na Pyramid of Sun, Uranus ikiwakilishwa na Pyramid of
Moon wakati Neptune na Pluto
zikiwakilishwa na kilima kilichoko kilometa kadhaa kaskazini mwa eneo hilo,
kilima hicho bado hakija pekuliwa na watafiti kuona kina nini.
Muonekano na mpangilio kutoka angani, wa Mapiramidi na majengo mengine ikiwemo street of the dead, mpangilio huo unawiana kabisa na nyota tatu za orion belt, lakini pia unawiana na mfumo wetu wa jua.
Majengo haya ya
piramidi, kilima ambacho bado hakija pekuliwa pamoja na Street of the Dead kwa
kutumia vipimo vya skeli uwiano wake na nafasi yake kutoka jengo moja kwenda
jingine unawiana na nafasi pamoja na umbali wa sayari kama ulivyo katika solar
system .
Muonekano wa Pyramid za mexico kwenye mchoro wa 3D.
Ni mwaka 1787 ndiyo watalam wetu waligundua kuwepo kwa sayari ya Uranus,
Neptune tumekuja kuigundua mwaka 1846 na Pluto tumeigundua juzi tu mwaka 1930.
Hakuna ustarabu wa zama zozote katika historia binadam uliopata kurikodiwa kuwa
na elimu ya sayari zote katika solar system achilia mbali kufahamu nafasi baina
ya sayari hizo.
Mfumo wetu wa jua na sayari zake ikiwemo dunia yetu.
Samahani kidogo, naomba tutoke nje ya sayari yetu lakini ndani ya mfumo
wetu huu wa jua (milk way) tuingie kwenye sayari nyekundu, maarufu kama
sayari ya Mars, bado tuna ndoto za kuikanyaga sayari hiyo, lakini kabla
hatujafungasha mizigo yetu na kwenda kwenye sayari hiyo, tumegundua kuwa kuna
vitu vya ajabu ambavyo vinatushangaza kuwepo hapo.
Yes, next to the Earth before you reach Jupiter~
Mwanzoni wanasayansi wetu
walidhani kuwa vitu hivyo kuwepo kwake vimefanywa na mabadiliko mbalimbali ya
hali ya hewa vikisaidiana na vitu kama upepo na kadhalika, lakini hata hivyo imebainika
kuwa vitu hivyo vimefanywa kwa ustadi, malengo, vipimo sahihi na kwa ujuzi wa
hali ya juu, kwa maneno mengine vitu hivyo ni kazi ya mikono ya viumbe Fulani …
viumbe gani hao? …
Ni kweli picha hii ni ya kwenye Mars? Ni kweli kuna kinyago cha sura binadam hapo? Sijuiii !!!!
swali hili tumetoka nalo kwenye sayari yetu ya dunia mpaka
hapa kwenye sayari ya Mars lakini na kuahidi kwa mapenzi yake Mungu kabla ya
kuifunga sura hii tutapata jibu kuwa ni
viumbe gani hao waliofanya kazi hizi.
Hat Sphinx wanasema lipo, Je ni kweli??!! Bado tuko mbali sana na kupata jibu la masawali hayo.
Katika eneo linalo itwa Cydonia kwenye sayari ya Mars picha iliyo pigwa na
vyombo vya anga ilionekana uso wa mtu kwenye eno hilo . NASA wakiwa mstari wa
mbele waliipinga picha hiyo na kuseam kuwa kinacho onekana siyo uso wa binaadam
bali ni matokeo ya mwanga wa kamera na kivuli cha eneo hilo ndiyo vilivyo
tengeneza picha mfano wa uso wa mtu, kwa maneno mengine kutokana na NASA picha
hiyo siyo halisi.
Was it or Is it? I dont know.
Hata hivyo nadharia hiyo ya NASA iliishiwa nguvu pale picha
nyingine iliyopigwa kwenye Mars, katika eneo tofauti kwa viwango tofauti vya
mwanga kulinganisha na ile ya kamera ya mwanzo, na picha hiyo ilionesha tena uso
wa binaadam ukiwa umechongwa kama kichwa cha Sphnix kwenye aridhi ya Egypt,
lakini hapa ni kwenye Mars ambapo hatuna ndoto za lini tutaikanyaga aridhi hii
nyekundu .
Ni kwa kiasi gani hii picha kutoka kwenye syari nyekundu ina ukweli? Ni vigumu kuithibitisha, lakini pia si hekima kuikataa moja kwa moja.
Uso huo kwenye Sayari nyekundu unasemwa una urefu wa maili 1.6 kutoka
kichwani mpaka kwenye kidevu na upana wa maili 1.2. Watafiti wanasema uso huo una muonekano wa
uso wa kawaida wa binadam na hivyo inakuwa ni vigumu kusema uso huo umechongwa
na mazingira yake yenyewe kwa nasibu tu .
Tulicho nacho ni dhana tu, kiasi gani zina ukweli, bado ni swali ambalo linaweza kujibiwa na yeyote na kukataliwa na yeyote kuhusiana na Pyramid ndani ya Mars.
Lakini tukiwa na uso unao karibiana na uso wa Sphinix Egypt, hapa kwenye
sayari nyekundu tunakutana na kitu kingine ambacho nacho hakiko mbali sana na
uso huo kama ambavyo kilivyo karibu na Sphinix pale Geza, Egypt kweney sayari
ya dunia. Kitu hichi si kingine bali ni Pyramid! Linaitwa D&M Pyramid, jina
hili linatokana na majina ya watu wawili ambao walivumbua Pyramid hilo, nao ni
Gregory Molenaar na Di Pietro, wote walikuwa waajiriwa wa NASA . Pyramid hili limesimamishwa umbali wa maili
kumi kutoka eneo ulipo ule uso wa binaadam, na kama lilivyo Pyramid kubwa la
Egypt hili nalo hapa kwenye sayari nyekundu liko sambamba na muhimili wa sayari
ya Mars.
We are stranger indeed.
Ni kama mjenzi wa kazi ile ya
Egypty ndiye yule yule aliyefanya kazi ile pale Mexico, ndiyo yule yule aliye
chora zile ramani, ndiye yule yule aliyechora ile mistari ya Nazca, na hapana
shaka ndiye huyu huyu tunaye ikuta kazi yake hapa kwenye sayari nyekundu,
sayari ya Mars, kama kweli ipo.
Swali la kujiuliza ni kuwa kama kuliwa na viumbe wenye teknolojia kubwa ya
kuweza kufika kwenye sayari ya Mars au walikuwepo hapo toka awali na wakafanya
vitu hivyo tunavyo viona, wamekwenda wapi viumbe hao? Kumbuka pamoja teknolojia
tuliyo nayo bado hatujaweza kutoka nje ya obiti ya dunia! Achana na hadithi za
kwenda mwezini, ulidanganywa mpaka sasa hakuna binadam aliyekanyaga mwezini!
Kuna mengi ya kuandika kuhusu ustaarabu huu ambao hatujafahamu ni kazi ya
kizazi gani katika zama zipi, nilikuwa napitia kitabu kinachoitwa The
Prehistoric Alignment of the World Wonders kilicho andikwa na Jim Allison
ambacho kimezama kwa kina kuelezea maajabu ya kazi za wajenzi wasiofahamika,
nilistajabishwa na yaliyo elezwa humo, itahitaji makala nyingine kama hii
kuelezea yote hayo na muda hauko upande wetu ila yoyote mwenye kutaka kuzama zaidi
na kufamu ni namna gani historia imepotoshwa hana budi kukipitia kitabu hicho.
Bada tunaendelea na safari ya kumtafuta mjenzi wa kazi hizo za maajabu, bado swali letu la msingi ni kutaka kujua 'JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU?
Tukutane tena hapa next safari bado inaendlea ....
Ukiangalia picha zote ni zakuchora,au zile zinazofanana kama zile zilizoonyesha Obama kumuua Osama Bin Laden,(1)Jee hawa viumbe wanatokea wapi?(2)wanaishi kwa kutumia nini ikiwa binaadamu anatumia Oxygen? (3)Ikiwa wanateknolojia ya hali ya juu,wapi wamesoma hiyo sayansi?(4)Na tecknolojia yao ilianzia wapi na kipindi gani?(5)Ikiwa hawa viumbe wapo wanaishi ulimwenguni,ni ipi nisabu yao?
ReplyDeleteKaka nashukuru kwa maswali yako mazuri, ila muelekeo wa posti yetu soon itajibu maswali yako, endelea kufuatilia.
DeleteDuuuh
ReplyDelete