Ili tuweze kuwa na hitimisho lenye vigezo vya kitaaluma na kisomi hapana budi kuchambua kila aina ya ushahidi tunao upata, hivyo bado tunaendelea kuvipitia hivi vielelezo, ingawa unacho kiona hapa kwenye hizi posti ni kama 'karanga kwenye dafu la nazi' hivyo ni wajibu wako msomaji kuzama kwenye bahari pana ya vyanzo mbalimbali uweze kujiridhisha.
TIAHUANACO,
BOLIVIA
Yale ambayo hayawezi kutokea, yametokea hapa.
Ni eneo ambalo mkandamizo wa hewa ni mkubwa mno, kiasi kufanya hewa ya oksijeni
kuwa ndogo sana. Lakini tofali lenye uzito wa tani 200 limekokotwa kwa umbali
unao kadiriwa kufikia maili 90, kwenye eneo ambalo hewa ya oksejeni ni ndogo
mno ni vipi kazi hii ilifanyika.
Jengo lililobaki kama masalia limejengwa kwa
utaalam ambao hauwezwi kulinganishwa na teknolojia yetu, mbele ya ujenzi huo
utaalam wetu wa ujenzi unasimama kama kituko.
Maheka na maheka maumbo ya jabu yamesimama,
mapyramid, vyumba chini ya aridhi, mageti makubwa mno ambayo vyote hivyo
vinathibitisha kutumika kwa taaluma ya hali ya juu mno kwenye Sanaa ya ujenzi,
na si ya hali ya juu tu, lakini pia ambayo katika zama zetu leo, bado sana
kuifikia.
Mageti mengi hapa utayaona yamejengwa kwa jiwe
moja tu. Mathalani ‘Gate of the Sun’ ni jiwe kubwa mno kupata kuchongwa duniani
na kusimamishwa kama geti. Futi 10 kwenda juu na upana wa futi 6.
Ukubwa wa majengo mengine hapa ni maajabu
ndani ya maajabu. Hekalu la Jua limejengwa kwa mawe ambayo kila moja uzito wake
ni baina ya tani 100 mpaka 200. Kuta za hekalu hilo zimejengwa kwa mawe yenye
uzito wa tani 60 kila moja, ngazi zake zimetandazwa kwa mawe yenye ujazo wa
tani 50 kila moja.
Mawe yamechongwa
kwa ustadi mkubwa kiasi huwezi kuona ni wapi ynaungana na yakapigwa polishi.
SACSAYHUAMAN, PERU
Inatamkwa ‘sexy woman’ ingawa haimaanishi
hivyo. Ni kama ngome, juu kileleni kwenye mlima utaona mji wa zamani wa Cuzco.
Mawe yenye ujazo ule ule wa tani 50 mpaka 200 unayakuta hapa. Hayapo chini,
bali juu kusimamisha majengo yenye mvuto wa kipekee.
Mawe hayo yameonganishwa
moja juu ya jingine au pembeni kwa ustadi ambao huwezi kupitisha kisu au wembe
baina yake.
Jiwe moja unakuta limechongwa sawa sawa ili kuwezesha mawe mengine
kumi na zaidi kuunganishwa na hilo ili kwa pamoja yatengeneze ukuta.
Tizama
picha hiyo hapo chini na uone jinsi gani kila jiwe limeweza kufiti na mwenzake
sawia kwa kila upande na kwa ndani pia! Hi si kazi ya asili, yupo aliye nyuma
ya kazi hii, yupo ambaye aliifanya kazi hii.
Ni nani huyo, na katika zama zipi?
Kwa umbali wa kama yadi 100 kwenye eneo hilo
pamelala pande linguine la jiwe lenye ukubwa sawa na jingo la ghorofa 5, lenye
uzito unao fika tani 20,000!
Halionekani kuwa ni kazi ya asili kwenye mazingira
yake, bali kazi iliyofanywa kwa makusudio maalum, nani mfanyaji wake? Hata sasa
hatuna mashine ya kusogeza uzito wa namna hiyo.
BAALBEK, LEBANON
Mahekalu mawili ya
warumi yamejengwa juu ya msingi wa kale mno ulio kuwepo hapo kabla ya mahekalu
hayo kujengwa. Mahekalu hayo makubwa kupata kuwepo kwenye dola ya warumi hata
kidogo hayawiani na msingi unayo yabeba.
Msingi huu
unadhihirisha taaluma ya hali ya juu kwenye fani ya ujenzi, ujuzi ambao mpaka
leo historia haijatengeneza kopi yake.
Jiwe moja kwenye
msingi huo linaukubwa sawa na basi, urefu wa futi 82 na kimo cha futi 15,
likikadiriwa kuwa na zito baina ya tani 1,200 mpaka 1,500.
Mapande hayo ya mawe uliyatizama utaona yame nyanyuliwa kutoka aridhini kwa
futi 20. Hata kwa kutumia zana za sasa, na teknolojia yetu ni kichekesho,
hatuwezi kusogeza mapande hayo ya mawe. Lakini yalinyanyuliwa na yakawekwa kwa
vipimo sahihi, mahala sahihi yaliyopaswa kuwekwa, na kuunganisha moja na
lingine kiasi baina yake huwezi kupenyeza makali ya kisu kilicho nolewa.
Ni akina nani hao waliyo fanya kazi hii iliyo lenga kubakizwa hapo milele?
Ni vigumu mno kumuweka binadam wa sasa kwenye picha hii, wala si binadam wa
Darwin anayefit hapo. Inahitaji watu 40,0000 kulisogeza jabali hilo, hata kama
watapatikana na walisogeze ni vipi wau 40,0000 wanaweza kutosha kwenye eneo
hilo la ujenzi na kuweza kulinyanyua jabali hilo?
Haiwezekani, kifupi
inakuambia si binadam walio fanya kazi hiyo, wala hakuna mashine yeyote, kokote
duniani kwenye majengo haya ambayo imeachwa kama alama ya namna gani
walifanyiza kazi hizo. Fumbo juu ya fumbo.
Ni viumbe gani hao, katika zama
zipi? Mbona teknolojia yao na yetu ni kama nazi na karanga unapolinganisha na
yetu.
EASTER
ISLAND
Mbali kwenye kisiwa kilicho tengwa.
Mamia ya mawe ya ajabu yenye sura zinazo
lingana na binadam, kila moja lina uzito baina ya tani 35 mpaka 50. Sura hizo
zingine zimevalishwa kofia nyekundu. Kofia peke yake zinafikia uzito wa tani 10
kwa kofia moja. Kipenyo cha duara kwenye kofia hizo ni futi 25 na kimo cha futi
7. Kofia hizo ‘zilivalishwa’ baada ya masanamu hayo kusimamishwa.
Masanamu hayo yalichongwa karibu na mlima,
kisha yakabebwa kutoka hapo umbali wa maili 5 mpaka mahala yalipo sasa bila
kuacha alama yeyote. Masanamu mengine ni makubwa mno kukaribia jengo la kisasa
la ghorofa saba.
Swali ni vipi waliweza kuchonga masanamu hayo,
na vipi waliyabeba kutoka yalipochongewa mpaka yalipo sasa bila kuvunjika, na
vipi waliweza kuyachomeka aridhini mithili ya vijiti?
Lakini swali la muhimu na msingi zaidi ni
AKINA NANI HAO WALIO FANYA KAZI HIYO?
WALIIFANYA KATIKA ZAMA ZIPI?
YU WAPI
MWALIMU WA SOMO LA HISTORIA ATUSAIDIE KUTUPA MAJIBU?
YU WAPI DARWIN ATUAMBIE BINADAM HUYO ALIISHI
ZAMA GANI?
Guys we are stilling build our case ...but worry not, at the end Inshallah we will find WHO is behind these, and if possible WHEN ... so stay tune till next time....
Ahsante kaka kwa kutuelimisha ila utata juu ya utata
ReplyDeleteEndy chande amefarika je unaweza kutupa info kidogo
ReplyDeleteKuhusu Endy Chande unaweza kutizama posti za awali kabisa kwenye blogi hii, sikumzungumzia yeye mahususi, lakini nilizungumzia freemason wa aina yake, ambao ni maarufu kama blue degree freemason, au freemason ambao hawavuki daraja la 3. Hawa wanatumika kama mauwa kwenye ukuta, hawa ni kinga ya kile ambacho freemason wa daraja la juu wanacho fanya, na hawa huwa hawafaham ubaya wowote wa freemason, sababu hawa ndiyo kazi yao kutoa misaada mbalimbali ya kijamii. Zaidi unaweza ukazitazama hizo posti.
DeleteJee hawa viumbe wapo duniani tayari au wanaandaliwa mazingira ya kuja?
ReplyDeleteJee kuna ushahidi wa picha za ukweli na sio za kuchora,kwamba hawa viumbe wanapatika sayari flani?
Endelea kufuatilia posti hizi mpaka mwisho maswali yako yote yatakuwa yamejibiwa.
DeleteInavyoonyesha hivo viumbe ni vikubwa (GIANTS) kuliko binaadamu wa kawaida kwa kujenga majengo hayo yenye matufali ya uzito wa tani,Jee hao viumbe waliishi mwaka gani?
ReplyDeleteInavyoonyesha hivo viumbe ni vikubwa (GIANTS) kuliko binaadamu wa kawaida kwa kujenga majengo hayo yenye matufali ya uzito wa tani,Jee hao viumbe waliishi mwaka gani?
ReplyDeletesoon we will have the answer, keep on visit our blog.
DeleteAhsantul
ReplyDeleteAssalaaam alaykum warahmatu llaaaah wabarakaaatuh,mbona sijauona mwisho wa maswali haya? Nani aliejenga piramidi,mchora ramani na elimu ya sayari na hao Kizazi cha Nyoka
ReplyDeleteMbona haiendelei Post hii tukapata majibu ya waliofanya kazi hii
ReplyDeleteInakuja ....
DeleteMbona Post hii haiendelei tukawajua wahusika wa Kazi hii
ReplyDeleteInakuja ....
DeleteMbona kimya kaka tuhabarishe!!
ReplyDeleteInakuja ....
DeleteMbona kimya kaka tuhabarishe!!
ReplyDeletenarudi baba nilikuwa nafuta grease. Lol
Delete