Ni lini binadam wa zama za mawe alianza kuchimba chuma?
Kulingana na Darwin, zana zake zilikuwa bado ni duni, na alitumia mawe butu siyo chuma.
Haiwezekani alichimba chuma katika zama za mawe, kulingana na Darwin na
kulingana na historia wanayo tufundisha.
Bado aliishi mapangoni kama wanyama wengine.
Lakini cha jabu kote duniani kumekuwa na mashimo makubwa ya kale mno, ya
kale kuzidi historia ya ‘binadam wa leo’ mashimo hayo madini na vito mbalimbali
vilikuwa vikichimbuliwa ikiwemo chuma.
Lion Cave, Swaziland, Afrika Kusini, moja ya mashimo ya kale mno, shimo hilo limekwenda chini zaidi ya futi 30, maelfu na maelfu ya tani za chuma zilichimbwa zama hizo. Wanahistoria wetu wanakuambia walitumia mawe na mifupa kuchimba chuma. Si kichekesho hicho, tani zote hizo walizifanyia nini? Maswali ni mengi yasiyo jibika.
Je binadam wa zama za mawe alikuwa akichimba chuma? Lakini si walichimba tu
bali pia walisafirisha biadhaa hizo sehemu mbalimbali, maelfu ya mali kutoka
eneo walilochimbia. Si kwamba walichimba, kusafirisha lakini pia waliweka
kumbukumbu ya maandishi, na kimahesabu ya kazi yao hiyo. Kweli zama za mawe, au
... hivi ni kweli tulikuwa na zama za mawe? Darwin uko wapi mbona mambo magumu
huku na vitu vingine hatuvielewi, au hukutufundisha vitu vyote?
Mathalani shimo hili lipo Marekani, Michigan, moja ya mashimo ya kale sana kuchimbwa chuma kabla ya zama za chuma. makabila ya Marekani ya kaskazini hayakuwa kuchimba chuma wala hakuna rikodi zozote zinazo onesha kuwa walikuwa na taaluma hiyo. Swali lile lile, nani alichimba na lini?
Kote duniani, Afrika, Ulaya, Amerika na mabara mengine, mashimo mengi ya chuma na madini mengine yalikuwa tayari yameshaanza kuchimbwa kabla ya sisi kuendelea nayo.
USAFIRI WA BAHARINI.
Kwenye miaka ya 1920, meli mbili za Kirumi zilipatikana chini kwenye ziwa
Nemi, Italy. Kama kawaida meli hizo zikatajwa kuwa ni kazi ya moja ya viongozi
wa dola ya Roma. Lakini kama yalivyo ma Pyramid ya Egypt na kwengineko, dai
hilo halina mashiko.
Masalio ya moja ya meli hizo ilipo ibuliwa kutoka chini ya ziwa Nemi.
Meli hiyo ilionekana kuwa na uwezo wa kubeba watu 120. Inayo kebini 30,
yenye bafu 4, eneo la wafanyakazi wa meli, sakafu ya marumaru (tiles), nguzo za
chuma, maktaba, mgahawa, jiko n.k. Ni vigumu kuamini kuwa meli hiyo inaweza
kuwa ni ya kale kuliko dola ya Roma, ingawa huduma zilizomo ni kama meli ya
kitalii.
Muonekano wa meli hiyo endapo ingefanyiwa ukarabati. Ilifanyiwa lakini akaja kulipuliwa wakati wa WWII.
Ukienda Egypty unakutana na meli yanye urefu wa futi 350 na upana wa futi
60, yenye mgawanyo wa sehemu nne ya abiria kukaa juu ya wengine, kama vile
first class, economy n.k. Lakini si ya kwenye milenia yatu, hapa bali maelfu ya
miaka nyuma kabla ya Kristo.
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.
China, Ugiriki vimepatikana vyombo vya usafiri kwenye maji ambavyo vina
urefu kati ya futi 250 mpaka 600 na vyenye uwezo wa kubeba karibu watu 600 kwa
wakati mmoja, ambazo ni kubwa mno hata ukilinganisha na zile ambazo wazungu
waliaanza kuzitumia baada ya kufanya uvumbuzi wa usafiri wa bahari.
Ukija Sumeria, kamusi ya watu wa Akkadia (Akkadian) inajumuisha sehemu
maalum kwa ajili ya meli, ambapo imetaja majina mpaka 105 kwa ajili ya meli
mbalimbali kulingana na ukubwa, kazi, kituo, safari inazofanya, mpaka nyambizi
(submarine) n.k.
India nyaraka inayo kadiriwa kuwa ya miaka 3000 nyuma, inayo sura nane
maalum zinazo zungumzia vyombo vya usafiri vinavyo safiri angani, juu ya maji
na ndani ya maji.
Mfano wa nyambizi katika zama zetu za leo.
Wakati kwenye historia wanatufundisha kuwa watu wa kale hawakuwa na
maarifa, walianza kwa kuzigeuza meza zao na kuziweka kwenye maji wakaanza
kusafiri nazo na taratibu ndiyo wakagundua majahazi, lakini historia nyingine
inatuambia hapana, walikuwa na taaluma kubwa hata kutushinda kwa upande huo wa
usafiri wa anga na maji.
Je tumekopi kutoka kwenye dunia isiyo fahamika?
Kwenye usafiri na mawasiliano vitu mbalimbali kutoka sehemu moja ya bara
vilipatikana kwenye bara jingine. Mathalani maandishi, kazi za sanaa, bidhaa
zinazo fahamika asili yake ni kona flani ya dunia, vimepatikana kwenye kona
nyingine ya dunia vikiwa na kumbukumbu za maelfu ya miaka kabla ya Kristo.
Lakini ni wazi kwa teknolojia tuliyo iyona na tutakayo endelea kuiyona ya
viumbe hao, suala la usafiri kutoka kona moja ya dunia kwenda nyingine haliwezi
kuwa na alama ya kuuliza.
Miji kama ya, TENNESSEE, GEORGIA, GUATEMALA, MEXICO, PERU, PANAMA, MEXICO, ECUADOR
kutaja kwa uchache sana, kumepatikana vitu kutoka maelfu ya maili na vingine
kutoka mabara mengine, vinavyo ashiria kuwepo kwa mawasiliano baina ya jamii
hizo.
Lakini pia ukitazama ujenzi wa Pyramidi, ingawa nimetaja miji michache
kuhusiana na hili, ila ukweli ni kuwa yalijengwa dunia nzima, kwenye mabara
yote kwa muundo na utaratibu unao wiana, na hata maeneo ambayo yaliyo jengwa
yalikuwa yanawiana kimazingira, au kinajimu, au kivipimo kwa maana ya latitude
na longitude, na mengine unaweza kuchora mstari ulio nyooka kutoka jengo moja
kwenda jingine kuzunguka dunia nzima.
Ngano za kale haziwezi kuwa za jabu zaidi ya hivi. Lakini hizi si ngano za
kale, bali ukweli wa msingi, takwimu moja baada ya nyingine, kielelezo kimoja
baada ya kingine, maisha ya watu maelfu ya miaka, kama siyo maelfu, elfu ya
miaka kabla ya Kristo, hadithi zao, kazi zao, maisha yao na juu ya yote
ushahidi wa hayo.
Wanahistoria, wanasayansi, wanajiografia, na wengine wabobezi katika fani
zao wanazipokea habari na ushahidi huu kwa ukimya usio elezeka, hakuna katika
nyuso zao ila macho ya kusalitiwa, moyo uliovunjika na ubongo uliofikia tamati.
Kuukubali ushahidi huu ni kutoa kibali cha kuandika upya historia ya dunia, na
hasa ya binadam ambayo kwa maelezo yao ni kuwa hauna zaidi ya miaka 4000
iliyopita.
Hatujafika bado, safari inaendelea, safari ya kukusanya ushaidi wa kutosha
kabla ya kutoa hukumu.
Ni juzi tu wanasayansi wetu walikuwa wakisema dunia haiwezi kuwa tufe,
sababu walio sehemu ya chini wangeanguka na kupotelea pasipo fahamika.
Ni juzi
walikuwa wakisema nyota za angani haziwezi kuzidi 1,500! Lakini uvumbuzi wetu
wa leo unatuonesha kama ni watu wa nyuma mno kwa kila kitu ukilinganisha na
maarifa na taaluma ya watu walio ishi miaka 15,000 KK au zaidi!
Wanajimu wa Babiloni, Egypt, Kaanani, Sumeria, Mesopotemia, India kutaja
kwa uchache walimiliki zana bora na zali hali ya juu kwenye masuala ya anga, au
kuwa wakweli zaidi kwenye hili, walirithi zana bora na za hali ya juu kwenye
mambo mbalimbali kutoka kwa jamii isiyo fahamika.
Miji ambayo naitaja katika posti hizi ni kwasababu baada ya maelfu na
maelfu ya miaka kupita ushahidi ulitufikia ni vipande vipande, ingawa kuna kila
dalili kuwa maarifa na taaluma hiyo ilikuwa ulimwenguni kote zama hizo.
Maeneo kama EGYPT, CHINA, ENGLAND, GUATEMALA, TIAHUANACO, BOLIVIA, GREECE, INDIA,
SUMERIA, BABILONI, SSYRIA, HITTITE, na SASIA MINOR; walikuwa na rikodi au
walirithi rikodi zilizo kuwa zikionesha kuwa dunia ni duara, imezungukwa na
mbingu.
Wasumeria wao rikodi zao zilikuwa mpaka na majina ya nyota, na majina
ya vikundi vya nyota vya anga la kusini na kaskazini. Wajenzi wa Pyramid kama
tulivyoona hapo nyuma, wao walijua mpaka ukubwa wa kipenyo cha dunia, ukubwa wa
duara la dunia, sehemu nyota zilipo, safari za nyota hizo zama hadi zama.
Vipimo vyao vilikuwa sahihi kuliko vipomo tulivyo kuwa navyo karne ya 19!
Miji kama INDIA, CHINA, GREECE na ROME walikuwa wakifaham kuwa dunia ni
duara na inaelea angani, inajizungusha kwenye mhimili wake kwa masaa 24, na
inalizunguka jua, njia yaje ya kulizunguka jua imekaa kama yai. Wapi walirithi
haya maarifa, kutoka kwa nani? Ghafla mbona yamepotea? Ghafla mbona tunakutana
na binadam wa Darwin ambaye hajui chochote?
Ukija tena kwenye miji niliyo itaja yaani, unakuta vipimo vya dunia kwa
maana ya uzito wa tufe la dunia lina uzito kiasi gani, hapo ni GUATEMALA.
BABILONI NA EGYPTY vipimo sahihi vya
siku ngapi dunia inachukua kulizunguka jua, wameandika siku 365.2420, mahesabu
yetu ya leo ni 365.2422!
Ni kweli kulikuwa na binadam wa zama za mawe a.k.a
binadam wa Darwin? Kwa taaluma hiyo katika zama hizo, binadam wa leo
tungetegemea awe ameanzisha makazi kwenye Mars, sayari nyingine na hata
kuvumbua ulimwengu (Universal) mwingine, ambayo kwenye sayansi ya leo bado ni
nadharia.
KUHUSU MWEZI
INDIA wao walikuwa na vipimo kuhusu umbali wa kutoka kwenye mwezi kuwa ni
maili 253,000. Vipimo vyetu vya leo vinatuambia ni 252,710. Watu wa mahesabu za
makadirio na waachia mnipe jibu. Vipi walijua
hivyo vipimo za ambazo wanahistoria wetu wanatuambia ni zama za giza na ujinga?
CHINA, UGIRIKI, INDIA, CHALDEA, walikuwa na elimu kuwa mwanga wa mwezi si
wakwake, kwamba mwezi hauzalishi mwanga, inaukopa mwanga huo mahali. Leo
tunafaham kuwa mwezi unaakisi nuru yake kutoka kwenye jua!
Walifahamu njia inayopita mwezi kuizunguka dunia ipo kama yai, na kuna
wakati mwezi unakuwa karibu na dunia, na wakati mwingine inakuwa mbali na
dunia. Walikuwa na hesabu ya siku ambazo mwezi inazitumia kulizunguka jua.
Mathalani watu wa MAYA walirikodi ni siku 29.53020, kwa mahesabu ya zama zetu
ni siku 29.53059.
Naweza kuendelea zaidi na zaidi kwenye Jua na kila sayari unayoijua kwenye
mfumo huo, hawa jamaa rikodi hizo walikuwa nazo, tena kwa usahihi wake.
NJE YA MILK WAY
Nje ya galaxy yetu inayo fahamika kama milk way. CHINA walikuwa na rikodi
kuwa kile kinachonekana kama anga la buluu si chochote bali ni rangi inayo
tengenezwa na ufinyu wa macho kuona. Leo tumejua kwamba buluu tunalo ona angani
siyo mbingu ile, ni mtazamo wa mwenye kutazama kutokana na mchanganyiko wa gesi
mbalimbali.
INDIA na UGIRIKI walikuwa wakitambua kwamba ulimwengu hauna mwisho, leo
tumejua kwamba ulimwengu unatanuka na hauna mwisho.
Kabila la wa Dogoni walio ishi MALI, wao walikuwa wanajua kuwa nyota ziko
mbali zaidi kuliko sayari. Leo huo ndiyo ukweli wa msingi kwenye sayansi yetu
ya anga.
INDIA na UGIRIKI walikuwa na elimu kuwa nyota za angani hazihesabiki. Sisi
tulikuwa tunasema hazi zidi 1,500. Lakini sasa inafahamika kuwa nyote zote
kwenye ulimwengu (universal) huu hazihesabiki na idadi yake inazidi idadi ya
michanga ya pwani zote za bahari zote za dunia hii.
Yes sijakosea, idadi ya
nyota zote kwenye ulimwengu (universal) zinazidi idadi ya michanga yote (kama
utaweza kuhesabu kimchanga tu moja mpaka tu ngine) yote ya pwani zote za bahari
zote kwenye dunia yote!
Ukifikia nukta hiyo kwanza mtukuze Mola wako mbora wa waumbaji.
SUMERIA na UGIRIKI walifahamu kuwa kila nyota ni mfumo kamili wa jua wenye
sayari zake. Ni Juni 1984, American Astronomical Society walitangaza kuwa nyota
40 ambazo zipo karibu na sisi zimeonesha kutoa milipuko kama inayo tolea na
nyota yetu kubwa inayo itwa JUA, na hivyo inaashiria kuwa nyota hizo zitakuwa
zinayo vitu vigumu na hata sayari zinayo zizunguka.
Watu wa Dogoni walio ishi MALI, Africa walikuwa wakifahamu kuwa galaxy
yetu, milk way ipo kwenye umbo mithili ya dawa ya mbu (dawa ya mbu ya zamani)
umbo hilo kwenye lugha ya kigeni ni spiral, kwenye karne hii ndiyo sisi
tumethibitisha hayo!
EGYPT, SUMERIA, WATU WA DOGONI walioishi MALI, watu wa fupi (mbilikimo) wa ITURI, walio
ishi ZAIRE, leo Demokrasia ya watu wa Kongo; walikuwa na rikodi kuhusiana na Nyota
ya SIRIUS A.
Wameitaja nyota inayo izunguka Sirius A. Nyota hiyo ni nyeupe
lakini haionekani, njia yake ni kama yai, umbali ilipo Sirius A na njia ya hiyo
nyota inayoizunguka pia waliujua, inazunguka kuizunguka nyota inayo ng’ara sana
ambayo ndiyo Sirius A kila baada ya miaka 50, pia nyota hiyo ni nyota nzito
mno.
Kwa kutumia mashine ya telescope yenye nguvu na taaluma yetu ya leo
tumeweza kuthibitisha kila taarifa iliyo tajwa na watu hao wa kale kuwa ni ya
kweli na sahihi. Kale yenyewe si ya juzi, bali ya maelfu na maelfu ya miaka
kabla ya Kristo, lakini leo sisi ndiyo tumekuwa na teknolojia ya kuthibitisha
hayo.
Hatukuweza kuiyona kwenye teleskopi zetu mpaka mwaka 1862, na hatukuweza
kipindi hicho kuipiga picha mpaka mwaka 1970. Nyota hiyo inayo izunguka Sirius
A, uzito wake ni mkubwa kiasi kwamba mchanga au jiwe dogo unaloweza kuliweka
kwenye kijiko kidogo cha chai kutoka kwenye sayari hiyo, kijiwe au mchanga huo
ni sawa na tani 20,000 za mchanga au mawe kwenye sayari yetu! Nguvu zake za
mvutano ni kubwa mara milioni 100 ukilinganisha na nguvu za mvutano za dunia
yetu.
Jiulize ni wapi watu hawa katika zama hizo waliweza kufanya utafiti na
gunduzi ambazo ndiyo kwanza tunazithibitisha leo? Walizirithi kutoka kwa nani?
Mmiliki wa taaluma na teknolojia hiyo ni nani na alishi katika zama zipi?
Ndiyo kwanza kuna kucha, unajua kwamba watu hawa walikuwa na kompyuta? Unabaki
mdomo wazi, vipi kuhusu ndege, vipi kuhusu njia chini ya bahari, vipi kuhusu
barabara za mwendo kasi?
afKama ni safari hata bado hatujaanza, tunaiandika upya historia ya binadam
...
Stay tune ushahidi bado haujatosha TUKUTANE NEXT TIME NA VIELELEZO VINGINE
.... TCHAO.
Makala hii imekata kiu ya wanafunzi,Walimu wa ngazi ya Elimu ya msingi ,sekondari na vyuo.Mungu ibariki blog hii,Mungu mbariki Salim Msangi.
ReplyDeleteA nice scholarly work
ReplyDeleteAppreciate
DeleteWell done
ReplyDelete:s
DeleteHongera kaka kwa kutufumbua macho
ReplyDeleteBig up to you kwa kutafuta haya maarifa.
DeleteHongera kaka kwa kutufumbua macho
ReplyDeleteHongera kwa kuwa mdau wa blogi hii.
Deletehongera bro kwa kazi nzr sana unayoifanya tupo tunajifunza mingi sana kupitia ww.
ReplyDeleteKaribu sana mdau
Deletemkuu mungu akubariki sana
DeleteMbona haiendelei hii Post
DeleteEndelea kutuelimisha kaka
DeleteGd
DeleteUbarikiwe sana kaka Salim kwa Makala nzuri na ya aina yake.
ReplyDeleteJe suis ni kina nani? Ni kweli walihusika na kuzama kwa meli ya Titanic? Niko katika kujifunza ndugu yangu bwana Salim na ningeshukuru mno kupata ukweli na ufafanuzi juu ya hili. Ahsante!
ReplyDeleteMbona sehemu ya 10 haiendelei
ReplyDeletembona haiendelei sehemu ya 10
ReplyDeleteMuendelezo wa sehemu ya 10
ReplyDeleteInakuja ....
DeleteInakuja ....soon
DeleteNzuri sana endelea kaka
ReplyDeleteT
ReplyDeleteHii ya barabara chini ya bahari nayo kali wapo waliokuwepo kabla yetu
ReplyDelete