Wakati wa harakati nyingi katikati ya mji, baadhi ya mitaa inabadilishwa na
kufanywa njia moja (One way street), alama za barabarani, alama za mitaa,
‘service road’, mji wa kisasa kabisa, unaweza fikiri ni New York au Madrid kama siyo Kuala lumpur, lakini unaonaje nikikuambia kuwa hiyo inaweza kuwa ni ni Babiloni ya
kale, Nineveh, au Aztec Mexico?
Yees, here we go like this ...
TOLTECS, MEXICO mpango mji wa miaka 400 mbele. Hata leo hatuna mpango mji
wa miaka 50, pengine hata wa miaka 10 hatuna. Lakini Mexico maelfu ya miaka
nyuma mipango mji ulilenga kukidhi mahitaji ya miaka 400 mbele!
PAKISTANI, GUATEMALA, BABILON walijenga miji na mitaa yenye barabara pana
kama miji na barabara za nchi tunazoita ‘zilizoendelea.’
Mpango mji wa jiji la kale la Roma, POMPEII, ambao kimakosa 'unadhaniwa' kuwa ulijengwa na waroma.
ANTIOCH, SYRIA walikuwa na taa za barabarani. INDUS VALLEY, PAKISTAN,
MEXICO walikuwa na mfumo imara wa maji taka, mitaro mikubwa na mambomba katika
kila mtu. Miji mikubwa ya kisasa kwenye ‘nchi zinazo endelea’ hakuna mifumo
imara ya maji taka ukilinganisha na zama hizo.
Masalio ya mji wa kale Pompeii, nyuma yake ni Mlima wa Volcano wa Vesuvius, ambao mlipuko wake umeuzika sehem kubwa ya mji huo.
Dalili ya mvua ni mawingu, panapo fuka moshi pana moto chini. Kinukta
kiduchu cha mpango miji nilicho kigusa, ni kama ‘tip of iceberg’ kwenye hili
linalofuata, are you ready ...
Barabara zao zilikuwa pana, na imara, masalio ya barabara katika eneo la Leptis Magna, Libya. Aina hii ya ujenzi wa barabara hizi unaweza ukaikuta Cairo, Lebanon na hata kwenye baadhi ya mitaa ya Zanzibar.
BARABARA
COLOMBIA, ECUADOR, PERU, CHILE,BOLIVIA NA ARGENTINA.
Ustaarabu na miji ya Amerika ya kusini, mpaka leo kwenye somo rasmi la
‘historia’ inafundishwa kuwa ulianzishwa na watu wa INCA, kama ambavyo wanavyo
fundisha ustaarabu wa Egypty na Mafarao.
Luxor Temple, Egypty. Mpaka sasa wanahistoria hawajaja na maelezo yenye kuridhisha juu ya ujenzi wa majengo ya namna hii katika Egypt ya kale ambayo ni kama 'yalishuka kutoka mbinguni.'
Lakini ushahidi wa kutosha unaeleza
kuwa Inca kama walivyo mafarao miji hiyo waliikuta, hawakuijenga wao. Barabara
za ‘highway’ zilikuwepo Peru kabla ya watu wa Inca kufika. Barabara hizo ndizo
tunazo zijenga sasa katika miji yetu mikubwa ili kuweza kukidhi mahitaji ya
vyombo vya usafiri, wingi wa watu, kupunguza ajali, na kusafiri kwa kasi na
salama.
Kwenye ramani hii, unachoona kama mstari mwekundu ni barabara za Inca, ambapo urefu wake unakadiriwa kufika zaidi ya kilometa 40,000!
Miaka mingi kabla hajazaliwa Kristo barabara hizo zilikuwepo Peru,
Colombia, Chile na kwengineko. Baadhi ya barabara hizo zinatumika mpaka sasa
kuendeshea magari yetu.
Hiyo siyo mito, ni barabara za Inca, ambazo wamezirithi kutoka kusiko julikana ... lakini haikuwa kazi ya Inca wala mababu zao, ni kazi ya nani?
Mh! Kulikuwa na magari kabla ya kuja Kristo?
Tulia bado tunakusanya ushahidi ...
Barabara hizo katika maeneo niliyo yataja, zinaungana na mtandao wa
barabara nyingine ndogo na kutengeneza mtandao mpana wa barabara za kuingia na
kutoka ndani ya mji. Barabara hizo zinafika mpaka kando ya mto Amazoni, halafu
zinanyanyuka kuelekea kwenye vilele vya milima na kuteremkia pwani. Hazijatokea
kwa nasibu, zimejengwa.
Urithi wa barabara kutoka kwa kizazi kisichojulikana, mpaka kwa watu wa Inca walizitumia kuendeshea magari ya farasi na farasi, mpaka kwenye zama zetu ambapo tunazitumia kuendeshea magari!
Wajenzi wa barabara hizo walipokuta mlima, hawaku uzunguka, bali walitoboa
katikati na barabara ikapitishwa! Zipo tunazitumia leo, tunajiuliza ni nani
walifanya haya, yakuwapi magari yao, au walifanya kazi hiyo kwa ajili ya
kuendeshea magari ya punda na farasi?
Machu Picchu, huwezi kwenda Peru halafu usifike Machu Picchu.
Si barabara tu, na madaraja yake, madaraja imara ambayo bado tunayatumia
mpaka leo hii.
Miji mingine yenye barabara za kisasa kama za karne 21, lakini zikiwa
zimejengwa maelfu ya miaka kabla hatujaanza kuetengeneza kalenda ni EGYPT,
ROMA, MEXICOSANTA CRUZ,
GREECE, ENGLAND, kutaja kwa uchache sana. Barabara
pana, zimenyooka, sehemu nyingine ni pana zaidi sawa na ‘highway’ zetu za sasa
zinazo ruhusu magari manne kupita kwa wakati mmoja.
Majumba yao tumeona ni makubwa, barabara zao nazo ni pana, huwezi sema
zilijengwa kwa waenda kwa miguu au njia ya farasi.
MIFEREJI YA MAJI.
NORTH COAST, PERU. Mfereji wenye urefu wa maili 70, ujengwa katika ubora ambao mpaka leo bado unatumika.
YUCATAN, MEXICO, kunayo mtandao wa mifereji 30, ambapo mingine inayo upana
wa mpaka futi 160, mifreji hiyo inatoa maji kwenye vyanzo vikubwa kama mito,
maziwa na bahari kisha inakwenda kuyamwaga maji hayo kwenye mabwawa makubwa,
kabla ya kuyasambaza katika mji! Hii ni taaluma ya Hydraulic Engineering,
lakini hapa tunazungumzia kipindi ambacho hata binadam wa leo tunamashaka kama
alikuwepo.
GUATEMALA.
Picha ya karibuni iliyo pigwa na satelite kwenye misitu ya eneo
hilo imenasa na kuonesha mifereji iliyo jengwa kwa ustadi na utaalam wa hali ya
juu. Mifereji hiyo imechukua eneo la squre maili 11,185, kwa kilimo cha
umwagiliaji, mifereji hiyo inaweza kuwatosheleza mamilioni ya watu!
CARTHAGE, TUNISIA. Mfereji wenye urefu wa maili 87.6 na uwezo wa kubeba
galoni 7,000,000 kwa siku moja.
Muundo wa mifereji ya chini ya aridhi wa Qanat uliopo Iran, asilimia 75 ya maji ya Iran yanatoka humu, lakini nani mjenzi wa mifereji hii ya chini ya aridhi, siyo wa Persia wala binadam wa Darwin.
PERSIA. Mifereji iliyo enda chini ya airdhi maili 170,000 kwa ajili ya
kukusanya maji kutoka milimani na kuyaleta tambarare jangwani! Pamoja na
teknolojia na maendeleo, na rasilimali walizo nazo Iran ya sasa, lakini asilimia
75 ya maji yao yote wanayo yatumia sasa, wanayategemea kutoka kwenye mifereji
hiyo ambayo hatujajua mpaka sasa mjenzi wake ni nani. Yes mifereji hiyo iko safi
na inafanya kazi yake tangu maelfu ya miaka huko nyuma, mpaka sasa. Hatumjui
huyo injinia bado.
Kulingana na muandishi huyu, Qanat na mifereji mingine ya chini ya aridhi kwenye jangwa hilo ni kama mishipa ya damu kwenye mwili. Lakini nani mjenzi wa kazi hii?
MOROCCO. Mtandao wa njia za chini ya aridhi, kwa umbali wa futi 250 kwenda
chini, na hapa ni chini ya jwangwa, ulitengenezwa kwa ajili ya kukusanya maji
kutoka chini ya aridhi. Njia hizo kila baada ya maili 100 kumewekwa mabomba kwa
ajili ya kuingiza na kutoa hewa.
Morocco, kama Iran.
Hata sasa, na maarifa, elimu, teknolojia na rasilimali tulizo nazo kufanya
mradi kama huu chini ya jangwa ni vigumu mno kuliko kuufanya sehemu zisizo na
jangwa. Lakini ulifanyika na uko hapo.
Ukiwa juu ya aridhi, mifereji hiyo imejengewa ukuta kama kisima, lakini hicho siyo kisima ni shimo la kuingiza na kutolea hewa.
EGYPT. Maandishi haya, yananifanya nikifikirie tena ikiwa mfereji wa Suez
maarafu (Suez Canal) kama kweli ulijengwa na mafarao! Utakumbuka kwenye posti
za nyuma tumezungumzia kupatika meli za kale mno hapo Egypt kushinda kipindi
cha utawala wa mafarao.
Ukiwa ndani ya mifereji hiyo, chini ya aridhi hichi ndicho unacho kiona, ni kama upo kwenye mji mwingine kabisa, lakini hapa ni chini ya aridhi yenye jangwa kubwa barani Afrika.
MAPANGO, MAHANDAKI NA NJIA ZA CHINI YA ARIDHI
DOMINICA. Shimo la dhahabu, lina kina cha urefu wa futi 16,000 kwenda chini
na upana wa mile 6. Tuliligundua shimo hili kwenye karne ya 15, kipindi hicho
habari za hili shimo ndiyo ilikuwa ‘story’ ya mjini.
Lakini kwenye mabara yote saba, kumekuwa na taarifa na ushahidi pia wa
kuwepo kwa mapango makubwa, mahandaki na njia pana za chini ya aridhi na chini
ya bahari pia, zinazo kwenda maelfu ya maili kwa urefu. Njia hizo za chini ya
aridhi na chini ya bahari zipo zinazo unganisha bara moja na jingine!
Ramani hii inaonesha namna dunia nzima inavyo weza kuonganishwa kwa kutumia mahandaki na njia za chini ya aridhi
Haya si kwamba ni moja ya maajabu makubwa, lakini ni moja ya habari zinazo
fichwa kwa kila hila na mbinu ilimradi tu watu tusifahamu.
Utawaambia nini watu? Kwamba watu wa kale tunao ambiwa walitumia zana duni
za mawe na vijitu waliweza kutengeneza si tu majumba makubwa, ambayo bado yapo
mpaka leo, barabara pana na imara tunazo zitumia mpaka leo, mifereji na mabwawa
makubwa yanayotumika mpaka leo, lakini eti kwamba walijenga barabara chini ya
aridhi, na si chini ya aridhi tu, na chini ya bahari pia, na si chini ya bahari
tu, lakini refu kiasi cha kuonganisha mabara mawili au zaidi?
Njia 'mpya' za chini ya aridhi na chini ya bahari zinazo pendekezwa kwenye mchoro huu, karibu asilimia 80, zinafuata njia za kale mno, ambazo mpaka sasa hatuja fahamu wachimbaji wake ni akina nani, na kwa vile 'serikali' zote na taasisi zao elimu zeme linyamazia hilo, inaonekana kuwa wao ndiyo wavumbuzi au teknolojia imekuwa kubwa kiasi wameweza kutengeneza njia za chini ya aridhi, lakini si kweli, ni njia ambazo wamaezikuta na kwa makusudi hawasemi kuwa zilichimbwa na nani.
Whaaaaaaaat! Are you talking
about?
Yeah! The truth is stranger
than fiction dear!
Habari ya barabara na njia za chini ya aridhi na chini ya bahari tumekuwa
tukizisikia kwenye hadithi za kufikirika na ngano za kale, na sote tukidhani ni
hadithi za kufikirika, lakini kuna ukweli zaidi ya ngano na hekaya.
Mtambo wa kisasa kwenye teknolojia yetu, unao tumika kuchimbia njia za chini ya aridhi. Mtambo huu haujafikia ubora wa zana zilizotumika makumi elfu ya miaka huko nyuma katika kufanya kazi hiyo. Ni zana gani walitumia.
AFRIKA.
Tuanzie nyumbani, mcheza kwao hutuzwa. Utakumbuka kwenye posti iliyopita
tulizungumzia watu wa Mali na mbilikimo wa Zaire, ambao walikuwa na ujuzi na
taaluma ya nyota na sayari mbalimbali ambazo ni majuzi tu ndiyo tumekuja
kuzigundua na kuthibitisha. Kwenye hili la njia za chini ya aridhi Afrika
hatupo nyuma, na siyo Afrika tu, hata hapa kwetu Tanzania hatupo nyuma.
MOROCCO mpaka SPAIN. Ipo njia kubwa chini ya bahari siyo chini ya aridhi,
narudia tena, chini ya bahari, ambayo inaiunganisha Morocco na Spain, au kwa
uwazi zaidi Afrika na Ulaya. Yaani unapo tembea kwenye njia hiyo unaanzia chini
ya aridhi, kwenye handaki halafu unakwenda mpaka unaifikia bahari, lakini hapa
bahari inakuwa juu, wewe unakuwa chini, moja kwa moja mpaka Ulaya.
Kama unavyoona, bahsri ipo juu, njia ipo chini ya bahari.
Serikali ya Spain na Morroco wanaangalia uwezekano wa kuonganisha tena
Ulaya na Afrika kupitia eneo hilo. Lakini wataalam walio pewa kazi hiyo ya
utafiti na kuja na suluhisho, wanaitilia mashaka njia ya chini ya bahari, si
kwamba si salama, lakini wanasema ‘Hatuna teknolojia ya kuweza kuitoboa miamba
hiyo ambayo ni migumu sana.’
Morocco na Spain wana pendekeza njia ya namna hii, ambapo itapita ndani ya maji, na siyo chini ya maji, sababu hatuna teknolojia ya kuchimba chini ya maji! Je waliochimba chini ya maji ni akina nani, wa zama gani, kwa teknolojia ipi?
Hivyo wanapendekeza pajengwe mfano wa bomba kubwa ndani ya bahari, lakini
siyo chini ya bahari, hapana, ndani ya maji ya bahari ambalo ndilo liwe njia ya
treni kutoka Morocco mpaka Spain.
Swali la kujiuliza ni wakina nani waliichimba hiyo njia ya chini ya bahari
ya kutoka Morocco mpaka Spain, waliichimba kwa teknolojia gani, ya zama gani,
kiasi kwamba leo sisi kwenye zama tunazo ita za teknolojia tunashindawa kufanya
kitu kama hicho?
Mwandishi wa kitabu cha The Lost World of Agharti, anasema kunazo taarifa za wasafiri wa
kiafrika juu ya kuwepo kwa uwanda mkubwa wa njia, mahandaki na mapango chini ya
aridhi ya bara hilo, ambazo msafiri anaweza kwenda mamia ya maili. Anasema
mathalani upande wa Malawi, kusini mwa ziwa Tanganyika, chini ya mto Kaoma,
kuna handaki na njia za chini ya mto huo ambazo msafiri anaweza kwenda kuanzia
alfajiri mpaka jua la utosi ndiyo anaweza kutokea upande wa pili.
Amboni
Tanga, kunako mapango ya Amboni, mengi yameandikwa, hasa kuhusu vinyago na
baadhi ya michoro na kipindi fulani makazi ya wahalifu, mashujaa n.k. Lakini
kimoja ambacho hakijaandikwa sana ni kuhusu mahandaki na njia zinazo anzia
kwenye mapango hayo na kukupeleka mpaka chini ya Mlima Kilimanjaro!
Ni maneno ya wakazi wa maeneo hayo, na baadhi ya ‘tour guider’. Wanasema
kuna ambazo zitakupeleka mpaka Kilimanjaro na zitakazo kupeleka mpaka Mombasa.
Hakuna taarifa rasmi ya kiserikali juu ya njia hizo, lakini ni juu ya watafiti
na wanahistoria kujitupa kwenye hilo na kulifanyia kazi.
AFRIKA YA KASKAZINI.
Mmisionari, David Livingstone anaandika, “Makabila yanaishi chini ya aridhi,
kwenye mahandaki na wamejenga nyumba humo chini ya aridhi.” (The
Lost World of Agharti,)
NIGERIA
Kwenye wilaya ya Wama, kume patikana mapango ya kale na mahandaki yenye
njia za chini ya aridhi, ambazo wakazi walitumia pia kama sehemu za kujifichia,
njia zingine zinakwenda mamia ya maili mpaka kwenye bahari ya Atlantik, karibu
na nchi ya Guinea.
EGYPT
Handaki ambalo mlango wake umefungwa, chini ya moja ya Pirami la Geza.
Handaki hilo inasemekana linakwenda mpaka Tibet, kunako milima ya Himalaya.
ULAYA
GREAT BRTITAIN. Kuna mahandaki makubwa na ya kutosha kwenye eneo la
Yorkshire. Kumekuwa na ngano na hadithi za kale mno kwa wakazi wa hapo juu ya
jamii inayo ishi chini ya mahandaki hayo.
FRANCE
Mwaka 1834 kanisa la Gapennes katika eneo la Picardy lilipo dondoka
ikafahamika kuwa kanisa hilo lilikuwa limejengwa juu ya mtandao mpana wa
mahandaki na njia za chini ya aridhi, utafiti ulipofanyika zaidi ya mahandaki
100 yalipatikana eneo hilo.
Moja ya mahandaki yanayo patikana Ufaransa, hili limejengwa upya na kutiwa nakshi, lakini asili yake ni la kale mno. Bado tunawatafuta wajenzi wa asili wa kazi hizi.
UJERUMANI
Ushahidi wa kutosha unathibitisha uwepo wa mahandaki na njia za chini ya
aridhi ambazo katika vipindi mbalimbali vya vita yalitumika na wakazi kwa ajili
ya kujifichia. Wakazi wa maeneo husika wanayafahamu mahandaki hayo kwa jina la
‘Southern Siberia’ sababu mtu anaweza kutembea kwenye mahandaki hayo kutoka
Ujerumani mpaka mpaka Siberia, hayo ni maelfu kama siyo malaki ya kilometer,
chini ya aridhi, kutoka Ulaya mpaka Asia.
Handaki hili Ufaransa walilibadilisha na kufanya ni kama kaburi, wakajaza mifupa na mafuvu ya watu, na sasa limegeuka kuwa kivutio cha utalii. Lakini ukilitazama unaona kabisa ni njia inayo elekea mahala fulani.
SOUTH AMERICA
Juu kabisa kwenye vilele vya milima ya Andes, mahandaki yana iunganisha
milima hiyo na Machu Picchu, na maeneo mengine, ambapo kuta za mahandaki hayo
zimechongwa vizuri kwa ustadi mkubwa, huwezi kuiita ni kazi ya mazingira yake,
bali ni kazi ya kizazi fulani cha zama za kale, lakini ni kizazi gani?, Kwenye
zama zipi? Handaki jingine linapita chini ya mto Urubamba.
ECUADOR
Yamepatikana mahandaki na mtandao mpana wa mahandaki kwa urefu wa maelfu ya
maili, kutoka Ecudor mpaka Peru. Na pia inaunganisha Lima mpaka Cuzco na
inaendelea mpaka Bolivia au hata mpaka baharini.
PERU
Baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 1972 kwenye mji wa Lima, wataalam wa
uwokozi waligundua kuwa sehemu kubwa ya jiji hilo, chini ya aridhi kuna
mahandaki na njia za chini ya aridhi zenye mtandao mpana za kuonganisha handaki
moja na jingine na zote zikiwa zinaelekea milimani.
Hadithi na ushahidi wa kushikika kuhusiana na barabara, njia, mahandaki ya
chini ya aridhi, chini ya bahari na chini ya mito mikubwa na midogo; ni nyingi
na za kale mno, kiasi watu wakizipuuza na kudhani ni ngano za kale za
kufikirika, lakini; HAPANA, nenda Peru, Brazil, South America yote, Ulaya,
Asia, Afrika.
Mchoro huu ukionesha baadhi ya mji ulio patikana chini ya aridhi Uturuki, huu ni mji chini ya aridhi.
Lakini wakati unafikiri juu ya mahandaki hayo ya chini ya aridhi.
Nikuongezee tu kuwa kwa maeneo kama Amerika ya Kusini,Afrika, Amerika ya
Kaskazini, Ulaya, Asia kifupi kwenye mabara yote, mpaka kwenye bahari ya
Pasifiki na visiwa vyake kumepatikana pia mahandaki na njia chini ya aridhi, na
miji mikubwa chini ya aridhi ... Tunaiandika tena historia ya binadam ...
Kama huwezi kuamini mpaka uguse, kama Thomas, basi andaa mabegi nafunga safari mpaka Uturuki, Jiji chini ya aridhi. Kwa Teknolojia yetu sasa hivi tunajenga ghorofa mbili mpaka tano au kumi chini ya aridhi, lakini siyo jiji. Jiji kamilifu lenye njia nyumba za wakazi, maduka, sehemu ya mifugo mifumo ya hewa na maji taka, chini ya aridhi. Najiuliza ikiwa binadam tuna 'evolve' kwenda mbele kama alivyo tuambia Darwin au tuna 'evolve' kurudi nyuma?
Naweza kuendelea na kuendelea, lakini kwanini nikuchoshe, bahari ya maarifa
imejaa na kumwagika mpaka kwenye pwani, upatikanaji wa taarifa tangu binadam wa
‘Darwin’ aanze kutumia zana za mawe haujawahi kuwa mpana hivi, fanya utafiti
wako binafsi, kisha ulete hapa kuthibitisha haya au kuyapinga, uhuru ni wako.
Guys till next ... still there is so much to cover on subject and I am working on it ... our goals is to found who was behind all these and if possible to rewrite the history of a man on earth ... Tchaoooo
Enter your comment...kaka umetutupa xana xx ni watu wakalibu tunafatilia unachokiandika
ReplyDeleteHaya mambo kwanini wanayaficha?
ReplyDelete