Time Traveling ni moja ya nyanja zenye kusisimua kwenye sayansi ya
kosmolojia. Tafiti zinaonesha ‘time traveling’ ipo, lakini inafanyikaje kwa
zana gani, bado teknolojia yetu haijaweza kulijibu swali hilo.
Lakini kwenye nakala za kale mno, ambazo bado waandishi wake bado hatuwajui
kuwa ni viumbe gani na wazama zipi, zinaelezea matukio yanayo husiana na ‘time
traveling’.
Wanasayansi wa Marekani kwa wiki mbili walisafiri angani kuizunguka dunia
wakiwa na madege yao aina ya Jets, moja ya ndege zinazo kwenda kwa kasi mno
kwenye teknolojia yetu ya leo ya usafiri wa anga. Walibeba katika ndege hizo
saa za atomiki. Lengo likiwa ni moja tu, kuthibitisha nadharia ya Einstein ya
‘time relativity’.
ambayo inasema kuwa, saa/muda/wakati unakwenda taratibu,
unapokuwa kwenye chombo kinacho safiri kwa kasi, kadiri chombo hicho kinavyo
kuwa na kasi kubwa ndivyo muda unavyo zidi kwenda taratibu. Walithibitisha hilo
ni kweli baada ya wiki mbili kuizunguka dunia wakiwa na jeti na saa za atomiki.
Wanaanga ambao watasafiri kwenye chombo ambacho kina kasi inayo karibia
kasi ya umeme, umri wao utaenda taratibu kulinganisha na wale ambao wamewaacha
kwenye uso wa dunia.
Kwenye chombo kinacho kwenda kwa kasi inayo karibiana na umeme, wakiwa huko
angani wataona kuwa muda unakwenda sawa na walio kuwa duniani, lakini ndani ya
miaka michache watakuwa wamezikaribia nyota za mbali mno.
Aliporudi kutoka angani, alimkuta ndugu yake kazeeka, yeye bado ni kijana vilevile.
Baada ya miaka
ishirini na moja ndani ya chombo chao hicho watakuwa wapo katikati ya galaxy
yetu inayo fahamika kama milk way, lakini hapa duniani itakuwa imepita miaka
75,000!
Lakini nadharia hii, tunayoiita ya Einstein ya ‘Time Relativity’
ilithibitishwa kuwa ni kweli, ilifahamika huko nyuma katika zama ambazo
kulingana na Darwin binadam bado alikuwa ni kiumbe duni anayetumia zana duni.
Kwenye ngano za wa Japan, wanayo hadithi ya mtoto ambaye alisafiri kwenda angani miaka 3, aliporudi duniani alikuta miaka 300 imeshapita.
Mtume Isaya anazungumzia safari ya mbinguni, alipo ambiwa anarudi duniani, akauliza mbona imekuwa haraka hivyo nimekuwepo hapa kwa masaa mawili tu, malaika akamuambia, siyo masaa mawili bali miaka 32, Isaya akawa anahofia akirudi duniani atazeeka haraka na kifo, akaambiwa asiwe na wasiwasi akirudi duniani atabaki kama alivyo. (Tomas Endrew- We are not the First)
INDIA, walikuwa na taaluma ya ‘law of gravity’. Maarifa haya ndiyo msingi
wa safari za anga na kasi ya usafiri wenyewe. Law of Atraction, pia ilifahamika
India, sasa hivi inahubiriwa sana kwa namna mbali mbali na hasa kutoka nchi za
Mashariki ya mbali, ambapo watu wa Magharibi wamechukua mafunzo hayo na kufanya
moja ya biashara kubwa, na sasa watu wa New Ages na makanisa yao wamefanya kama
moja ya misingi ya mafunzo ya dini yao, lakini kinacho fundishwa ni kama
mchicha, kulinganisha na mbuyu.
Greece, Britain, Egyty, Guatemala kutaja kwa uchache walikuwa na maarifa
juu ya ‘anti gravity, vacuum, na mahesabu ambayo yana vipimo vya kasi ya umeme!
Guatemala walitumia neno ‘kinchiltun’ kumaanisha miaka 57,600,000. Ni kitu
gani walikuwa wakikipima kwa miaka hiyo? Walitumia neno ‘alautun’ wakimaanisha
siku 23,040,000,000 au miaka 63,123,000! ‘Kalpa’ ikimaanisha kipindi cha miaka
bilioni 4.32. Aina hii ya vipimo ndiyo inayo tumiwa na wanasayansi wetu wa anga
kupima umbali wa baina ya nyota, galaksi na sayari mbalimbali. Mathalani umbali
baina ya nyota tunatumia neno ‘light years’ ambayo ni mamilioni ya miaka,
umbali baina ya galaksi tunatumia neno ‘parsecs’, ambalo ni kipimo kinacho
unganisha 3.26 light years.
Unaweza kufanya nini ndani ya sekunde moja? Unaweza ukakonyeza jicho lako
mara sita, kusogea urefu wa nchi sabini. Unaona ni kitu kidogo sana unaweza
kufanya ndani ya sekunde moja. Lakini unaweza kufikiri ni nini kinaweza
kufanyika kwenye ‘tatu ya mamilioni ya sekunde’, soma vizuri siyo sekunde
milioni tatu, hapana, ‘TATU YA MILIONI YA SEKUNDE’ Yaani muda utakao utumia
kukonyeza jicho lako mara moja, kabla hujaanza kulifunga jicho, tayari 1/300,000,000
ya sekunde imeshapita! Ni kitu cha namna gani unacho weza kukipima kwenye muda
huo, na kwa nini utake kukupima kitu hapo, unatumia nini kukipima? Maswali ni
mengi na siyoni wa kuyajibu. India walifanya kipimo hicho, na wakakirikodi,
lakini ni zamani hasa, makumi elfu ya miaka nyuma! Walikiita ‘Kashta’ kipimo
hicho.
Wagiriki walipokuwa wakirikodi tarakimu, hawakuweza kuzidi ’10,000’
kilichozidi hapo kwa wagiriki kilirikodiwa sawa na ‘infinity’, yaani kisicho na
mwisho.
Ajabu ni kuwa watu walio ishi Syria ya kale, milenia kadhaa kabla ya
Wagiriki walirikodi nambari zenye tarakimu kumi na tano! Hata kompyuta haiwezi
kurikodi tarakimu kumi na tano! Hawa watu si walikuwa mbali kushinda wagiriki,
lakini mbali kutushinda sisi kwenye zama za sayansi na teknolojia? Who are
they?
Peru walifahamu matumizi ya ‘sifuri’, 0 ni tarakimu muhimu katika mahesabu
yoyote yale, bila hiyo hakuna haesabu inayofanyika, kompyuta na program zake
zinajengwa kwenye msingi wa 0 na 1. Siyo Peru peke yake, India, Mexico,
Babiloni, China kutaja kwa uchache.
Ni kweli Darwin alikuwa najua anacho kisema?
Pythagoras alikuwa ni mwanachama wa secrete society, hii ni mada nyingine, lakini kwenye sanamu hilo hapo kuna alama mahususi inayo mtambulisha kama mwanafunzi wa secrete society, umeiyona alama hiyo?
Hesabu za maumbo, hesabu za desimali, zilikuwa zinafahamika maelfu ya miaka
hata kabla ya wale walio itwa ‘wavumbuzi’ wa hesabu hizo kuzaliwa! Mara nyingi
wanao itwa ‘wavumbuzi’ unakuta ni watu walio tafsiri kazi hizo kutoka kwenye
vyanzo vingine na hasa vya kale mno na kuleta kwenye lugha inayofahamika wakati
huo, lakini hawasemi ni wapi wametolea kazi hizo.
Hakuna jipya chini ya Jua.
Hesabu hizo zilifahamika Mexico, Egypty, Peru, Babilon, Ur, Chaldea.
Kipenyo cha ‘Great Pyramid’ la Gaza, Kairo, Misri na kipenyo cha ‘King
Cahmber’ kilichomo ndani ya Piramidi vinahusisha pembe tatu ya ‘3 by 4 by 5 na
2 by 3. Aina hii ya pembe tatu ndiyo ile iliyotumiwa na mwana mahesabu wa
Kigiriki Pythagoras ambaye kwa kufuata historia ya kiserikali aliishi miaka
2000 baada ya Pyramid kujengwa, na yeye eti anaitwa ‘muasisi’ wa hesabu hizo za
pai. Lakini tukifuata historia ‘mpya’ isiyo na ukakasi ni kuwa mwana mahesabu
huyo aliishi miaka 15,000 baada ya Piramidi hizo kujengwa. Niambie ni wapi
Pythagoras ‘alivumbua’ hesabu hizo?
Ukija kwenye hesabu za ‘phi’, aljebra, trigonometry, squre roots, cube
root, na Logarithims tunakuta jamii za kale mno kushinda hata hao wanao itwa ‘wavumbuzi’
wa hesabu hizo walikuwa wanazijua. Egypty, Mesopotamia, Ur, Babilon, India,
Peru, China kutaja kwa uchache. Ni kama hizi kazi tunazikopi kutoka mahala
fulani, ni kama kuna wateule fulani wanao teuliwa kupitia miiko na taratibu
fulani ambao wanakwenda kujifundisha maarifa haya kwa siri ikisha baadae
wanakuja kutuambia kuwa fulani, ‘kavumbua’ kitu fulani.
Egypty ya kale walikuwa na alama fulani ya kimahesabu waliyo itumia kuonesha
‘mamilioni’ yaani badala ya kila wakati kuandika tarakimu yenye masufuri mengi,
walibuni alama ya kimahesabu ya kuonesha kitu hicho. Hilo linaweza kufanyika
endapo kitu hicho kinayo matumizi ya mara kwa mara na hivyo kumrahisishia
mtumiaji wake asipate tabu, kama vile ambavyo leo tunatumia, MB, GB, TB n.k.
Lakini cha ajabu ni kuwa dhana ya mamilioni sisi tumeanza kuitumia kwenye karne
ya 17, yaani juzi tu; sasa ni akina nani hao ambao walikuwa Egypty na katika
zama zipi ambazo mamilioni kilikuwa kitu cha kawaida mno kiasi kuwekewa alama
mahususi kumrahisishia mtumiaji?
Niendelee kukuchosha na ugonjwa wa taifa, a.k.a ‘Hisabati’?
Twende kwingine usije ukakimbia blogi yangu bure kwa kudhania nafundisha
hisabati hapa.
ROBOTIKA
Ni majuzi tu hapa robotika linalo itwa Sophia limepewa uraia katika nchi za
Kiarabu. Yeah, kabla ya hapo tulizoea kuyaona kwenye viwanja vya Hollywood
marobotika kama Cyborg, Terminator, Iron Man, Transformer, i, Robot, Robo Cop,
A.I Artificial, Star Wars ... niendelee? Kuna vitabu vya kutosha na cartoon na vitabu
vya komiki, lakini yote hayo tulidhani ni ‘fiction’, ngano au hekeya ...
tulikuwa tumekosea.
Hawa jamaa ni kama walikuwa wanajua juu ya teknolojia hiyo, halafu
wanatengeneza filamu na vitabu kuziandaa akili zetu juu ya hicho wanacho
kificha, akili zetu zikisha kubaliana nao, kisha sasa wanakileta kitu chenyewe.
Ni nani ambaye mwaka 1953 alikuwa anaitazama filamu ya Robot Monster ambaye
angefikiri kuwa mwaka 2017, robotika anaye itwa Sophia angepewa uraia na kualikwa
kwenye mahujiano na vituo mbalimbali vikubwa vya luninga ulimwenguni? Nani?
Labda huko mbali, ni nani ambaye mwaka 1999 alikuwa anatizama filam ya
Matrix, ulidhani kweli 2012 tungekuwa na ‘smartphone’, lakini kwenye Matrix
walionesha ‘Touch Computer’, teknolojia ambayo inaonekana kuja baada ya ‘smart
phone’, hivyo 1999, sehemu fulani kwenye pembe nne za dunia palikuwa na
teknolojia hii ambayo mpaka 2012 ndiyo ikafanywa ‘biashara.’
Sijui tunaelewana, nataka tupate picha kwamba kila unacho kiona, kwenye
vitabu au filamu kama ‘science fiction’ kitazame vizuri kwa jicho la tatu,
huenda ni bidhaa itakayo ingizwa sokoni miaka kumi ijayo. Lakini kwanini SIRI?
Hatukuwa na hatujawahi kuwa wa kwanza kutengeneza Robotika.
Whaaaaaaatsss?!
Yes, you read it correct, we were never the first? Somebody else already
beat us on that too.
Unataka kujua kuhusiana na Robotika za kale?, luninga je?, Kompyuta? Ndege
kama bombadia je? ...
Hey lets catchup soon for another episode ...Tchaaaooooo....
Enter your comment...dah tunakukubali sana naomba utupe ukweli wa taifa la israil na Donald trump
ReplyDeleteSasa ndugu Hawa jamaa kumbe hawana discovery yeyote mpya zaid ya kutuzingua2
ReplyDeleteHahahaa so funny
ReplyDelete