Robotika, Kompyuta, Luninga, Redio vilikuwepo zama hizo kabla hajaja
Masihi, vilikuwepo zama za nyuma zaidi kabla ya Abraham wa Uru, leo tunaita
Iraq. Historia ya vifaa hivyo kwenye uso wa dunia ni ya zamani mno kama ilivyo
historia ya binadam mwenyewe.
Kwenye karne ya pili kabla ya zama zetu, mahekalu ya Egypt yalikuwa na
mashine ya kutolea maji ‘matakatifu’, ujazo wa maji yatakayo toka kwenye
mashine, yanawiana na uzito wa sarafu iliyotumbukizwa kwenye mashine. Mashine
hizi utazikuta sana kwenye nchi zilizo endelea na kwenye masuper market
makubwa, mteja unadumbukiza sarafu, aina fulani ya bidhaa, inatoka,
‘automatiki.’ Lakini hapa ni kwenye Egyty ya kale kabla ya kuja Masihi na siyo
Mlimani City.
Dispensa ya kutolea maji matakatifu
Wachina walikuwa na taaluma moja waliyo iita, ‘Khwai-shuh’ ikiwa na maana, kulitia sanamu uhai
limsaidie kazi mmiliki wake, tafsiri ya karibu ni ‘kutengeneza robotika’,
Kwenye mji wa Alexandria, zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, palikuwa na aina
kwa aina ya vifaa vya ‘automatiki’ zaidi ya 100.
Sarafu inadumbukizwa kwenye Dispensa
Plato, mmoja wa mababa wa Ugiriki ya kale, anasema, robotika lake lilikuwa
na pilika nyingi kiasi walibidi kulizuia lisikimbie! Whaaaats?
Mshairi wa Kitaliano, Garcilaso de la Vega anaandika kuwa, watu wa Inca
walikuwa na sanamu ambalo lilikuwa linaongea na kutoa majibu ya maswali; Je
hivyo si ndivyo zifanyavyo Kompyuta zetu leo?
Baada ya sarafu kudumbukizwa maji yanatoka
Ugiriki, Marekani ya Kusini, Egypty, Ulaya, China kunayo hadithi na ngano
za kale, lakini pia yapo maandishi na kazi za wasomi wa zama zetu wanao sadiki
juu ya kuwepo kwa marobotika katika zama za kale.
Kama ambavyo Pythogoras hawezi kusema ni wapi alizipata hesabu za Phi, au
Alogorithm na hesabu za Logarithim, ndivyo ambavyo Plato hawezi kusema ni wapi
alilipata roboti ambalo wakati mwingi ilibidi kulizuia lisikimbie!
Katika zama zao, ukiwataja madaktari, wanasayansi, wanahisabati na wanajimu
wa zama za kati, unakuta ni kikundi fulani cha wateule wachache wenye maarifa
makubwa si kupita watu wote, lakini kupita zama zao. Ni wapi waliyanyakua
maarifa hayo na kuyafanya ya wateule wachache?
‘Siku moja itabidi tuzungumzie Mystery schools
and secret society’
Ni wazi maarifa hayo yalikuwa ni urithi wa kutoka zama zilizopita. Sababu
si kijamii, iuchumi, wala kisiasa kwamba teknolojia hiyo ilihitajika au kuzuka
ghafla kusiko julikana, hapana, haikuwa katika zama zao.
Zama gani, za akina nani sasa?
We are still lokingiii,
here here!
Kitengo cha historia na makumbusho nchini Ugiriki, wanacho chombo ambacho
kime tengenezwa na vyuma, ambacho kiliokotwa baharini kwenye kisiwa cha
Antikythera mwaka 1900. Chombo hicho kilikuwa na vitufe vya kubonyeza na gia
ambavyo havifananani chochote na masalio ya kale yaliyo wahi kukusanywa kutoka
Ugiriki ya kale.
Mwaka 1959 Dr. Derik J. Solla Price, mwanasayansi wa Uingereza, aliyekuwa
anafanya kazi kwenye chuo cha Priaceton alipotazama kifaa hicho, alikiita ni ‘Babu
wa Kompyuta’ aliendelea kusema, kifaa hichi ni aina ya Kompyuta ambayo kazi yake
ilikuwa ni kufuatilia mwenendo wa sayari na nyota, na mwezi. Aliandika hayo
kwenye jarida la Natural History Juni 1959.
Ilituchukua miaka 70, kutambua kwamba kifaa hichi cha Antikythera, ni Kompyuta.
Kifaa hichi kilicho patikana Antikythera kilibadilisha mtazamo wa
wanasayansi kuhusiana historia ya sayansi, sababu hakiwezi kuwa ndiyo cha
kwanza wala cha mwisho.
Stonehenge, kwenye ukamilifu wake, kama tunaweza kuwa na teknolojia ya kuyapanga mawe hayo upya.
Mwana anga Gerald Hawkins, ambaye ni profesa katika chuo cha Boston anasema
kuwa, ‘Stonehenge’ zilizopo uingereza ambazo hazijulikani nani alijenga na lini
zilijengwa, kazi yake kubwa ilikuwa ni kwa ajili ya unajimu. Alifanya kazi ya
kukusanya taarifa za kimahesabu za angani kwa kutumia ‘stonehenge’, alipoingiza
taarifa hizo kwenye Kompyuta, majibu aliyo yapata ni kwamba, ‘Stonehenge’
yenyewe ni Kompyuta
Ni kama 'US Space Center' moja ya vituo vikubwa vya anga duniani, ndiyo kinacho onesha na Stonehenge, ingawa Stonehenge ikiwa na uwezo mkubwa wa kukusanya taarifa kuliko vituo vyetu.
Profesa anasema, wajenzi wa ‘Stonehenge’ walikwenda mbali zaidi kwenye
sayansi ya anga, sababu kupitia taarifa hizo aliweza kupata taarifa za kinajimu
ambazo sayansi yetu ya leo ya anga haikuwa imeweza kuing’amua.
Kutoka kwenye ‘babu wa kompyuta’ mpaka kwenye vifaa vinavyo zungumza.
Whaats? Mobile Phone?
I dont know, lets ride along to see ...!
Sanchuniathon wa Mesopotamia, aliishi mwaka 1193 KK, na Philo Byblos wa
mwaka 150 BK, wanazungumza juu ya kuwepo kwa vifaa vinavyo zungumza! Mwana
historia wa kikristo Eusebius wa mwaka 260 – 340 BK, alikuwa anabeba aina hiyo
ya vifaa kifuani mwake, na vilikuwa vinajibu swali lolote alilouliza. Anorbius,
mchungaji mwingine wa Kikristo anakiri kuwa ameshawahi kuwa na kifaa cha namna
hiyo na akakitumia. Je ndiyo vifaa hivyo ambavyo leo tunaita ‘mobile phone’?
Kitu
kimoja ambacho msomaji ningependa uwe nacho kichwani wakati unasoma maandishi
haya ni kuwa, hichi kilicho andikwa hapa, kimefasiriwa kutoka lugha mbalimbali,
vyanzo tofauti vya kale mno, ambavyo ni vigumu kwenye zama za kati au KK, kuwa
walikuwa na wazo au mtazamo wa Robotika au simu za mkononi kama tulivyo nao
sasa. Lakini maandishi hayo pamoja na uduni wa vyanzo vyake, asili yake,
unakupa mtazamo wa vifaa hivyo kama ambavyo tuko nao sasa!
Tumeona huko nyuma ramani za kale zilizo na ubora kushinda za kwetu za
karne ya 19. Tumeona vifaa vya baharini na vya kuongezea meli vya kale mno,
tumeona mahesabu ya ajabu, ujenzi wa maajabu, mpangilio wa miji, barabara za
Peru, njia za kurushia ndege za Nazca, mitambo ya kinajimu, kompyuta na sasa
simu za mkononi.
Vitu hivyo ungevizungumza kwenye karne ya 18, unge onekana mchawi, kama
alivyo onekana Galileo, mwendawazimu, ilimradi hakuna ambaye angekuelewa.
Kwenye karne ya 18 Ufaransa waliwaona
watu ambao waliwaletea wazo la simu kama wahuni fulani, wanao taka
kuwadanganya watu.
Hivyo mpaka kwenye karne za karibuni kabisa 18 mpaka 19 bado tulikuwa
gizani ukilinganisha na maandishi haya, ambayo yanatoa mwango wa sauti kutoka
karne na hata milenia za nyuma kabisa! Ni nini kilitokea baina yetu na maarifa
haya, mbona kama tumeenda kuanza si moja, bali sifuri kabisa, yalitokea wapi
maarifa haya, kisha yakaenda wapi na sasa yanakuja kwetu kwa jina la ‘uvumbuzi’,
kweli?
Darwin huko uliko ...?!
Kuna kile kinachoitwa ‘Magic Mirror’, hadithi zake utazisikia sana Ulaya,
hasa Uingereza na Mashariki ya Kati, na Afrika kwa uapande wa Egypty. Kuna
filam kadhaa zime tengenezwa zikiwa na maudhui ya ‘magiz mirror’, lakini zikiwa
na dhana ya ushirikina zaidi kuliko teknolojia.
Kwenye kitabu cha Enoch imeandikwa kuwa Azazel aliwafundisha watu
kutengeneza ‘magiz mirror’ ambayo watu wa mbali na miji ya mbali na matukio yao
yalionekana kwenye hiyo, ‘magic mirror’.
Mwana historia Vera wa Luciana, anasema ‘magic mirror’ ilikuwa ni kioo
kinacho weza kuonesha matukio ya mbali au matukio yajayo. Aina hii ya ‘magic
mirror’ inataka kufanana na ile ya kwetu ya kule Tanga na Sumbawanga na maeneo
mengine maarufu Afrika kwa aina hii ya ‘magic mirror’.
Aliyetajwa kwenye kitabu cha Enoch, yaani Azazel kwenye ngano za kale
amekwenda kwa sifa tofauti lakini moja wapo ikiwa ni jini au mchawi mkuu. Kama
yeye ni mwalimu ni wazi ‘magic mirror’ haito tofautina sana na zile za
Sumbawanga, lakini bado, ukitazama suala la vifaa vinavyo zungumza, kompyuta za
kinajimu, na mengine na tilia shaka kama ‘magic mirror’ hii inafanana na zile
za kwetu kulee ...
Kwenye ‘magic mirror’ hiyo mtu angeweza kuona na kusikia yote yanayo
endelea duniani. Ukitazama filamu ya Sherk, Fellowship fo the Ring na zingine
utaona ‘magic mirror’ lakini kwenye maudhui ya ushirikina fulani kuliko teknilojia.
Lakini ‘magic mirror’ hiyo ilikuwa inaweza onesha matukio ambayo bado
hayajatokea, unaweza sema utabiri? Mathalani mwanafunzi wa ‘secret Society’ Nastrodums,
katafute kazi moja inayo sema ‘The Man Who Sawa Tommorrow.’, utamtambua na kumuelewa
Nastrodums, daktari wa kifaransa na mfuasi alieandika kazi maarufu ya Century,
ambapo, ‘alitabiri’ matukio makubwa yaliyo tokea na yanayo subiriwa kutokea,
kifaa alichotumia kupata taarifa hizo anasema ni ‘magic mirror’?
Was it a time machine tooo?!
I dont know?
Shida tunayo kumbana nayo kwenye kujenga hoja kwenye maandishi na kazi za
namna hii ni kwamba asilimia 90 ya ushahid wa kushikika haupo, kwenye hitimisho
tutajua ni kwanini tumebakiwa na vipande vipande tu vya ushahidi ambavyo vinatupatia
tabu kutengeneza picha kubwa. Lakini utamuona hapa Nastrodumas, kama alivyo
kuwa Einstain, Plato, na wavumbuzi wengine na yeye alikuwa ni mwanafunzi kwenye
‘secret society’.
Kifaa cha kuima tetemo la aridhi, kilikuwepo China maelfu ya miaka kabla ya kuja Kristo!
Na nikutoka kwao tu
ndiyo tunapata maarifa hayo, na kujinadi wao ndiyo wavumbuzi au wa mwanzo
kufanya vitu hivyo, lakini maelezo yao hayajitoshelezi.
Are we there yet ....
Patient my dear we are closer now ... stay put ...
Tutakwenda kutazama kwenye post zitakazo fuata, umeme, electricity, kamera,
ndege, safari za mwezini nyuma huko kabla hatujajua kwamba dunia ni duara, na
mengine na mengine kisha tutaweka nanga tukiwa na ushahidi huo, tutamtafuta ni
nani wa zama zipi aliyefanya kazi hiyo na wapi maarifa hayo yalipotelea au
kufichwa mpaka tukageuka na kuwa binada wa Darwin .....
See you soon my dear reader ....
Tupo pamoja sana
ReplyDeleteAllahu akbar
ReplyDeleteInaogopesha
Allahu akbar
ReplyDeleteHongera sana