Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Saturday, January 27, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? S02, Ep13 (Nyayo za Wageni Kutoka Sayari Ya Mbali - Taa Zisizo Zimika Milele ...)



Mwaka 1938-39 Wilhelm Konig, mwana historia wa Kijerumani aliokota ‘betri’ zilizo tengenezwa kwa kopa na udongo na kuwa mfano kama wa jagi au kibuyu, aliokota vifaa hivyo maeneo ya Baghdad, vifaa hivyo vilikariwa kuwa ni vya zaidi ya miaka 2000 iliyopita.



Baada ya WWII, Willard Gray wa kampuni ya General Electric, aka-copy na ku-paste aina hiyo ya betri ya miaka 2000 iliyopita, na ilipojaribiwa ilifanya kazi. Ushahidi kuwa Babiloni zama hizo walikuwa wanatumia betri!

Ikumbukwe kuwa utengenezaji wa betri katika zama zetu ulianza mwanzoni mwa karne ya 19.
Uatikanaji wa Betri hizo za Baghdad ni uthibitisho kuwa, kwenye zama ambazo tulidhani ni zama za kiza, kiuhakika zilikuwa zama za ‘mwanga’ sababu walitumia vifaa vya umeme.

Denis Saurat, mwandishi na mtafiti wa Kifaransa alipata ushahidi wa kuwepo vifaa vya kiumeme Egypt.
Lakini kwa upande mwingine kumekuwa na hadithi juu ya uwepo wa taa za kale zinazo waka milele bila kuzimika. Imeshindwa ‘kufahamika’ ni aina gani ya nishati hasa ambayo ilitumika kuziwasha taa hizo zisizo zimika.

Luciana, (120-180 BK) mwandishi maarufu wa zama hizo, anaandika katika kusafiri kwake kwenye miji ya Hierapolis, Syria, kwenye hekalu lilikuwepo sanamu ambalo liliwekwa kifaa ambacho giza linapoingia, kifaa hicho kililiangaza hekalu lote kwa nuru iliyo itoa!

Hekalu jingine la Hadad au Jupiter lilikuwa na kifaa kama hicho ambacho giza linapoingia basi hekalu zima linajazwa nuru na kifaa hicho.
Pausanias mwana jeografia wa kigiriki anaandika juu ya dhahabu iliyokuwa ikiwaka kwa mwaka mzima kwenye hekalu la Minerva.


St. Augustine wa 354-430 BK, aliandika juu ya taa ya ajabu ambayo si mvua wala upepo uliyo weza kuizima taa hiyo iliyo kuwepo Egypt kwenye hekalu la mungu Isis. Aina hii ya taa ilipatikana Antioch wakati dola ya Bezantiya ilipokuwa moja ya super power ya dunia, karne ya 6; juzi tu hapo. Taa hiyo ilikuwa ikiwaka kwa zaidi ya miaka 500.


Hadithi za taa zinazo waka maelfu ya miaka utazikuta, katika miji ya kale ambayo ustaarabu wao haujulikani ni wapi hasa ulitokea.
India pia zimepatikana aina hizo za taa, ambazo zinadaiwa zilikuwa ni taa za waungu wao walio itwa nagas, waungu nyoka, na ziliwaka kwa mamia kama siyo maelfu ya miaka.

Mahekalu yaliyo patikana kwenye miji ya Sumeria, Egypty, Babiloni, India, Himalaya, Tibet, Peru, Mexico kutaja kwa uchache makuhani na makaburi ya makuhani hao kume kutikana taa zilizo weza kuwaka kwa mamia kama siyo maelfu ya miaka.

Taa hizo mahali pengine zinatajwa kama aina fulani ya mawe, katika miji mingine ya kale na kwenye miji ya chini ya aridhi kumekuwa na maansidhi kwamba kuna ‘mawe’ yanayo ning’inia hewani na yakitoa nuru wakati wa usiku kama mwezi!

Maswali ni mengi, si kwamba zama hizo zilizo sahaulika walikuwa wanatumia umeme na betri, lakini walitumia umeme na betri bora kuliko ambazo tulizowahi kutengeneza kwenye zam zetu.
Betri yenye zaidi ya miaka 2000 inajaribiwa kwenye karne ya 20 na inawaka! Makaburi na mahekalu yamewekwa taa zinazo waka mamia na maelfu ya miaka! Hatujawahi kuwa na betri au taa za namna hii, au kuwa na mawe yanayo waka kama mwezi wakati usiku.


Ni teknolojia gani hii ilitumika, waliitolea wapi ina hii ya teknolojia, ikapotelea wapi aina hiyo ya teknolojia.

Next post we are going to catch a plane back in time ... planes of ancient world and perhaps destination to the moon...

See yaaaa .... there!

3 comments:

  1. Allahu akbar
    Allah akufungulie mengi nasi 2pate faida

    ReplyDelete
  2. Shegh 2pe vitu tupate faida koz nataman kujua huyo mjenzi wa haya yote

    UPO KIMYA SANA MAALIM

    ReplyDelete