Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?
Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.
Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.
Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!
Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%
Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...
Thursday, March 16, 2017
JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? S02, Ep6 (Nyayo za Wageni Kutoka Sayari Ya Mbali - Egypt )
Mapiramidi matatu ndani ya Geza.
Bado tukiwa tunamtafuta mwandishi wa kazi hizi katika maeneo ya Marekani ya
Kusini, tunakutana na kitu ambacho tumepata kukiona na kukusikia huku kwetu
Afrika, Piramidi, kwenye eneo hili kuna mapiramidi kadhaa, lakini kuna matatu
yanayo vutia zaidi ambayo mwonekano wake hautofautiani na ule wa mapiramidi
matatu ya Gaza.
Mapiramidi matatu ndani ya Mexico.
Turudi Egypt kidogo ambako kuna maandishi mengi kuhusu piramidi
kubwa la Gaza tutafute kama tutapata chochote kitu kuhusu kazi hizi za maajabu
halafu tutarudi Peru kwenye haya mapiramidi matatu kabla hatujatoka nje ya
dunia na kuitembelea sayari ya Mars ambako nako eti kuna Piramidi.
Je ni viumbe kutoka sayari ya mbali ndiyo waliyo jenga Pyramid ndani ya Mars?
Daima majengo hayo ya Gaza yamekuwa yaki washangaza wanasayansi, hasa
kutokana na ukamilifu wa muundo wake ambao unathibitisha utumikaji wa elimu
kubwa ya mahesabu na elimu ya maumbo.
Uyakinifu wa mahesabu yaliyotumika kusimamisha kuta za Pyramid, hata kwa theluthi ya sekunde haikubaliki kwamba, eti yalijengwa na watumwa walioshinikizwa kwa adhabu na viboko, bali ni kazi ya kitaalam ambayo taaluma yetu ya leo ya ujenzi, ikishirikiana na mahesabu, elimu ya nyota na vifaa tulivyo navyo hatujaweza kutengeneza nakala (copy) ya mfano wa jengo hilo.
Kamwe hayakujengwa kama makaburi ya
Mafarao kama wanavyo tufundisha katika mitaala yao, wala hayakujengwa na
Mafarao wenyewe, wala watumwa, bali ni hazina waliyo irithi, wameirithi kutoka
wapi, hilo ndilo swali tunalo litafutia jibu katika mtiririko wa posti hizi.
Ndani ya Pyramid kuna vyumba (vyemba) vilivyo jengwa juu, chini ya pyramid, kuna milango kama huo hapo kwenye picha ambao haujulikani unafunguliwaje na ndani ya chumba hicho kuna nini? Maduara meusi unayo ona ni matobo ambayo kamera imepenyezwa kuona kuna nini ndani. Walichoona ni mlango mwingne kama huo. Hakuna kibali kilichotolewa kuendelea kufanya utafiti kujua kuna nini ndani. Ni kipi tunacho ogopa?
Uwanda wa Gaza, nyumbani kwa Great Sphinx, na nyumbani kwa mapiramidi
makubwa matatu ya Egypt, kwa kila hali ujenzi huo wakale ni fumbo kwenye sanaa
ya ujenzi wa zama zetu, fumbo ambalo teknolojia yetu haijafikiriwa kulifumbua.
Hii ni kwa sababu ni vichache sana vinavyo fahamika kuhusiana na mapiramidi
hayo.
Muonekano wa Great Pyramid
Mapiramidi hayo matatu makubwa yanahusishwa na makaburi ya mafirauni
watatu, yaani Khufu, Khafre na Menkaure ingawa hakuna mwili wala alama yoyote
ya ustaarabu wa Egypt wa zama hizo iliyo pata kupatikana ndani ya maumbo hayo
ambayo kama ilivyo michoro na mapiramidi ya Nazca nayo mjengaji wake hajulikani
ni nani.
Khufu, Khafre na Menkaure
Katika Great Piramidi kuna alama ya mfalme Khufu ambayo inalenga kuashiria
kuwa yeye ndiye mjenzi wa kazi ile au walau kazi ile ilifanyika katika zama
zake, lakini utafiti unaonesha kuwa alama hiyo iliwekwa makusudi mwaka 1837 na
mtu aliyeitwa Howard Vyse.
Jina la mfalme Khufu liliwekwa hapo kwa kughushi ili ionekane kanakwamba yeye ndiye muhusika wa ujenzi huo au ulifanyika katika zama zake.
Mengi yamesemwa kuhusu jamaa huyu kuamua kuipa nguvu
ile nadharia ya kuwa Khufu ndiye mjenzi wa kazi ile kwa kuweka alama yake
kwenye ukuta wa Great Pyramid. Hata hivyo lilokubwa ni kuwa Howard Vyese si wa
kwanza kuingia ndani ya Pyramid na kutoa hadithi zake, na alama hizi za Khufu
zimeonakana katika vyemba vinne vilivyo gunduliwa na Howard na alama hizo
hakuzitaja popote katika maandishi yake mpaka siku ya pili alipokwenda na mtu
mwingine katika vyemba hivyo.
Mwaka 1765 mtu aliyeitwa Davison alipogundua
kuwepo kwa vyemba hivyo hakuona wala kutaja kwenye kazi zake jina la Khufu .
Hivyo jina hilo lililenga kumpa mfalme sifa isiyo yake. Lakini katika mtirirko
wa sura hii tutakuja kuona kuwa Piramidi zilikuwepo hata kabla ya kuja
binaadam, lakini ni kazi ya nani hiyo ndiyo jukumu letu kwa sasa kumtafuta
mjenzi wa kazi hizi za maajabu.
Baadhi a vyemba ndani ya Pyramid. Ustadi na maarifa yaliyo tumika kuvichonga vyemba hivyo, bado unavitia soni vyombo nza zana za kwenye zama zetu katika ujenzi na uchimbaji.
Uzito wa jengo hilo unakaribia kufikia tani milioni 6! Leo hii kwa
teknolojia tuliyo nayo, na maendeleo katika fani ya ujenzi, mahesabu na elimu
ya nyota bado itahitajika maajabu kusimamisha jengo mfano wa hili. Great
Pyramid linafahamika kuwa ndiyo jengo kubwa, bora zaidi duniani na lililojengwa
kwa mahesabu na vipimo yakinifu.
Ni vigumu kukubaliana na wanahistoria wanao dai kuwa majengo hayo
yalijengwa na mafirauni watatu walio tajwa hapo juu. Mawe mengine ni makubwa
mno ambayo teknolojia tuliyo nayo haiwezi kuyanyanyua,achilia mbali binaadam wa
kawaida, ndani ya mapiramidi hayo, wajenzi wake wamechimba, njia, vyumba na
korido za haja kuelekea chini ya aridhi na kufunikwa na mawe mazito mfano wa
mlango ambayo mingine mpaka hivi leo haijaweza kufunguliwa(watu fulani hawataki
vyemba hivyo vifunguliwe).
Bado unafikiri kuwa mawe hayo makubwa yalikokotwa na watumwa na kupangwa moja juu ya jingine na kutengeneza Pyramid, ambopo jiwe lenye uzito mdogo kwenye jengo hilo linakadiriwa kufikia tani 20.
Mapande ya mawe yalitumika kama matofali
hayafahamiki waliyatolea wapi, kwani eneo hilo halina asili ya kuwa na mawe
hayo zaidi ya mchanga, na wala hakuna alama ya kuonesha kuwa mawe hayo
yaliburuzwa kutoka sehemu yoyote ile, mawe hayo makubwa yakanyanyuliwa na
kupangwa kwa ustadi na maarifa makuu na kuunganishwa kiasi kwamba huwezi hata
kupenyeza wembe baina ya mawe mawili.
Historia wanayo tufundisha ni kama kwenye hiyo picha hapo. Lakini inashindwa kujibu maswali ya msingi kabisa kama vipi waliweza kuburuza jiwe lenye uzito wa tani 20? Hakuna eneo lolote kuzunguka Egypt ambako imeonekana kuwa ndipo mawe hayo mazito yalichimbwa. Hakuna alama yeyote au zana yeyote iliyopatikana ambayo inaweza kunasibishwa na ujenzi au wajenzi wake. Ni kifaa gani kilitumika kunyanyua mawe mengine yanayofikia tani 200?
Aina ya tabaka la aridhi mahali pa ujenzi wa mapiramidi hayo ni lile eneo
linajulikana kuwa na mawe aina ya diorite, kwa wataalam wa tabaka la aridhi,
mawe na mchanga aina hii ya mawe ndiyo mawe magumu mno kwenye uso wa aridhi,
hutumika kujengea barabara kabla ya kuweka lami. Ni katika aridhi ya aina hii
ambapo chini ya mapiramidi ndiko utakuta njia, korido na vyumba kadha na ambavyo
vingine milango yake bado haijaweza kufunguliwa.
Uwanda wa Gaza
Muandishi wa kitabu cha Fingerprints of the gods bwana Graham
Hancock,anasema kuwa,
“Hakukuwa na teknolijia ambayo ilipata kujulikana kwenye Egypt ya kale
kwamba ina uwezo wa kufanya kazi za namna hii, na wala si katika zama zetu
ambapo tutapata mhunzi wa kufanya kazi ya aina hii...”
Ikiwa hata kwenye teknolojia ya leo hatuwezi kufanya kopi ya kazi ile, ni vipi tuseme ilejengwa na watumwa, waliolazimishwa kwa mijeledi, ni vipi tuseme ilifanyika kibususa?
Kusema kwamba Pyramid zilitengenezwa kwa zana duni na watu wenye maarifa duni kama wanavyo sisitiza. Ni sawa na kusema mtoto mchanga anaweza kutengeneza engine ya ndege!!!!!
Chini ya aridhi ndani ya mapiramidi mamia ya mita kadhaa kwenda chini
utakutana na korido hizo zilizo chongwa vizuri na kwa usatadi mkubwa na hata
kutengeneza pembe ya nyuzi 90. Aina hii ya teknolojia ndiyo kwanza inapatika katika zama
zetu.
Maajabu na maswali yasiyo jibika kuhusu Pyramid.
Utafiti unaonesha kuwa drili iliyotumiwa na wajenzi hao
ilikuwa na uwezo wa kutoboa shimo lenye nchi 0.100 kwa kila mzunguko mmoja
uliofanya, ilikuwa ni vigumu kueleweka teknolojia hii ya hali ya juu waliipata
vipi kwa sababu ni mwaka 1983 kwa viwanda vya dhahabu vya nchi zilizo endelea
kiviwanda tulikuwa tukitumia drili inayoweza
kuchimba shimo lenye nchi 0.0002 kwa mzunguko mmoja, kwa maneno mengine
teknolojia waliyotumia wajenzi wa mapiramidi ilikuwa ni ya hali ya juu mara 500
kulinganisha na teknolojia tuliyokuwa nayo mwaka 1983.
Karibu ndani ya Great Pyramid.
Lakini ukishangaa hili
kwa nini usishangae barabara za kurushia ndege zinazo patikana Nazca, Peru
ambapo sisi tulizigundua kwenye karne ya ishirini baada ya ndege kuanza
kurushwa kupita eneo hilo!
Kuna mengi ya kujaza vitabu kuhusu malighafi na teknolojia
iliyotumika,kusimamisha majengo hayo, ili kufanya somo liwe rahisi tuhamie
kwenye kitu kingine, na hapa na zungumzia eneo lililochaguliwa kwa ajili ya
ujenzi wa mapiramidi haya.
Majengo haya yapo kwenye degree 30 ya latitude
ambayo iko sawa na dakika 3 za arc kwenye true north. Arc ni sawa na 1/360 ya
mzunguko wa duara zima. Ambayo hugawanywa kwa dakika 60 ambapo kila dakika moja
ni sawa na 1/21600 ya mzunguko wa duara zima, kwa sekunde 60 kila sekunde moja
ni sawa na 1/1296000 ya mzunguko wa duara zima. Hii ina tuonesha kuwa viumbe
hao walikuwa na uwezowa kupima latitude na longitude kwa usahihi kabisa.
Ni
mwaka 1761 ndiyo tumeanza kutumia mistari hii ya kufikirika, na kabla ya hapo
safari za kupitia kwenye maji zilikuwa za mashaka makubwa.
Ukilipima Great Pyramid kutoka kwenye kitako chake kuelekea mpaka juu
unapata ni sawa na Pi ( π ) 3.14. Aina hii ya mahesabu yaani, Pi ( π ) haikuwa
ikifahamika mpaka pale wa Giriki walipoanza kuitumia karne ya 3 BC nao hawana
maelezo ya kueleweka kuwa waliitoa wapi, ni ajabu kuwa urefu wa Great Pyramid
kutoka kwenye kitako chake ni sawa na futi 481.3949 ambao una wiana na mzunguko
wa kwenye kitako chake yaani futi 3023.16, hesabu ambayo unaweza kuipata kwenye
mzunguko wa duara lolote kuwiana na kipenyo chake. Uwiano huo uko hivi 2pi
(481.3949×2×3.14= 3023.16). Kwa kutumia skeli ya 1:43,200 kwenye kipenyo cha
dunia yetu na kipenyo cha Great Pyramid, kisha tukazidisha skeli hiyo na urefu
wa Grat Pyramid kutoka kwenye kitako kwenda juu, yaani 481.3949×43200=3938.685.
Hii namba tuliyopata yaani 3938.685 kwa makadirio machache ya pungufu ya maili
11 ni sawa na kipenyo sahihi cha dunia yetu ambacho ni maili 3949. Na hivyo
hivyo ukichukua kitako cha jengo hilo ambacho tulipata ni futi 3023.16
ukazidisha na ile skeli yetu ya 1:43200, utapata 24734.94 ambayo nayo kwa
makadirio machache ya pungufu ya maili 170 ni sawa na mzunguko wa duara la
dunia yetu ambao ni maili 24902.
Kumbuka pungufu ya maili 11 na au maili 170 kwenye skeli yetu ni kitu
kidogo mno, yaani ni sawa na tofauti ya vipimo vya sehemu ya nchi kwenye
piramidi zima. Hapa unajiuliza swali moja. Je viumbe hawa walikuwa wakifahamu
vipimo vya duara la dunia na kipenyo chake?
Kwanini yana wiana sana na nyota za angani?
Mundo wa Great Pyramid una siri kubwa kuhusu elimu ya nyota. Jengo hilo lina kile kinacho julikana kama
shaft ambazo wachunguzi wengi walidhani ziliwekwa kwa sababu ya kuingiza mwanga
ndani ya jengo hilo, lakini zina kazi kubwa zaidi ya kuingiza mwanga.
Hatukujua na bado hatujui kazi za shafti hizo, hivyo jibu rahisi ikawa ziliwekwa ili kupitisha hewa, je ni kweli?
Kila
shaft inaonekana kulenga nyota maalum inapo pita kwenye meridian. Kutoka kwenye
Queen Chamber, shaft ya kaskazini iliyo lala kwenye engo ya nyuzi 39 imelenga
nyota ya Kochab na mara nyingine hutamkwa kama Kocab na zaidi ni maarufu kama
Beta Ursa Minor ni nyota ya pili kati ya nyota zinazo ng’ara sana kwenye
kikundi cha nyota za Kaskazini zinazo julikana kama Little Bear. Shafti ya
upande wa kusini kwenye Queen Chamber ambayo iko kwenye engo ya nyuzi 39 na
dakika 30 imelenga nyota ya Sirius inayo patikana kwenye kikundi cha nyota za
Alpha Canis Major, hii ni nyota inayo ng’ara kushinda nyota zote angani.
Je yalijengwa kwa ajili ya kufuatilia mambo ya angani, je watumwa walikuwa wanajua kile kilichopo nje ya galaxy ya milk way? Bado unafikiri Mapiramidi yalijengwa na watumwa wasio jua kuvaa nguo na waliyo kokota mawe hayo kwa kamba? Fikiri tena.
Kutoka kwenye King Chamber, shaft ya kaskazini iko kwenye engo ya nyuzi 32
na dakika 28 imelenga nyota ya Thuban iliyo kwenye kikundi cha Alpha Draconis.
Shafti ya kusini kwenye King Chamber iko kwenye engo ya nyuzi 45 na dakika 14
ina lenga nyota ya Al Nitak iliyopo kwenye kikundi cha nyota cha Zeta Orionis,
ni nyota ya tano kwa mng’aro na pia ni moja ya nyota tatu zilizo chini kwenye
kikundi hicho.
Vipi walijua juu ya uwepo wa nyota hizo, na eneo zilipo kwa vipimo sahihi, wakati sayari ya 12 kwenye milk way tumeigundua kwenye karne ya 19. Ni kweli hii ilikuwa ni kazi ya watumwa kwa ajili ya makaburi ya wafalme?
Shafti hizo nne kwa msaada wa kompyuta zinaweza kutuonesha nafasi za kila
nyota mahala zilipokuwa mara ya kwanza wakati ujenzi wa piramid ulipo kamilika,
kwani hakuna shaka muelekeo wa shafti hizo ulilenga eneo zilipo kuwepo nyota
hizo. Kumbuka nyota hizo ziko nje ya Milk Way, yaani nje ya mfumo wetu wa Jua.
Kutambua ni wapi zilipo nyota hizo si kazi ya kibususa, ni kazi ya kitafiti na mahesabu ya hali ya juu, vipi watumwa waliosimamiwa na mijeledi waliweza kuyatambua mahesabu hayo na kusimamisha jengo lenye uwiano na nyota hizo kwa usahihi wake.
Zipo kwenye njia ambayo Jua letu, mwezi, na sayari nyingine tano ukiacha dunia
yetu zinapo pita, nyota hizo zipo karibu na njia ya nyota kubwa tunayoiitwa Jua
na sayari za Mercury, Venus, Mars, Jupiter, na Saturn pamoja na mwezi wa sayari
yetu. Mzunguko wa jua kuzunguka nyota hizo huu unachukua muda mrefu wa miaka
25,950 kukamilika. Inachukua miaka 12,960 kwa nyota hizo kuteremka kutoka juu
kuja chini na miaka mingine 12,960 kurudi juu kutokea chini.
Safari ya milenia kadhaa.
Ukitizama mpangilio wa mapiramidi matatu ya Misri yamepangwa kwenye
utaratibu ambao unawiana na nyota tatu zilizoko kwenye kundi la Orion. Great
Pyramid na lile la pili kwa ukubwa yako kwenye nyuzi 45 kusini mashariki.
Copy 'n' Paste from above so high to deep below Geza.
Wakati lile la tatu liko upande wa mashariki. Muonekano huo ndiyo muonekano wa
nyota tatu angani kwenye kundi la Orion , ni kama wajenzi wake walikopi
muonekano wa nyota hizo. Nyota mbili za mwanzo yaani Al Nitak na Al Nilam
zimejipanga moja kwa moja kama piramidi kubwa la kwanza na lile linalofuatia,
na nyota ya tatu Mintaka imekaa kuelekea mashariki kulingana na muhimili
uliwekwa na nyota mbili za mwanzo.
Kazi hii ni kazi ya kizazi kipi au viumbe gani katika zama zipi. Ni vipi waliweka alama hii inayoonekana ni ya milele kwenye macho yetu?
Kwa msaada wa kompyuta simulesheni iliyotengenezwa maalum kwa kazi kama
hizi ikisaidiana na picha za satelaiti tunarudi nyuma mpaka mwaka 10500 KK ambapo ndipo wakati hasa ujenzi huo yakinifu ulifanyika. Tunasema ndipo wakati
ujenzi huu ulifanyika kwa sababu uwiano wa moja kwa moja bila kukosea baina ya
piramidi na shafti zake ulilinganisha na nyota nilizo zitaja hapo juu, uwiano
huu haukupatikana kokote katika historia ila mwaka 10500BC.
Inamaana majengo hayo hayakujengwa mwaka 2500 KK kama tunavyo fundishwa ispokuwa 10500 KK, ni nani alikuwepo zama hizo? Binadam anakadiriwa kufika hapa duniani miaka 4000 KK iliyopita, ni nani huyo aliyekuwepo 10500 KK?
Hivyo zama hizo zilizo gandishwa katika
aridhi ya Misri kwa mfumo wa piramidi, yani mwaka 10500 ndicho kipindi nyota
hizo zilikuwa zikianza safari yake ya kutoka chini kwenda juu safari ambayo
itakamilika mwaka 2500AD kabla ya kuanza tena safari ya kushuka chini kwa mara
nyingine. Kikundi hichi cha nyota kipo mashariki mwa Milk Way, na aridhini wajenzi wasiyo fahamika wakayalaza Mapiramidi yale mashariki wa mto Nile. Nivigumu mno kuelezea uwiano huu umetokea kwa nasibu.
As above so below, only in 10500 BC was the alignment of three brightest stars was reflected perfectly to the three Pyramid on Geza plateau.
Bado tukiwa hapo kwenye aridhi ya Egypt, aridhi ya mapiramidi, kuna kitu
kingine ambacho ni vigumu kukidharau na kukifumbia macho, unapotokeza kwenye
aridhi hii ya Egypt kabla hujayafikia mapiramidi, upande wa mashariki utakutana
na kitu hicho, kikutazama na macho mawili, hayaangalii kushoto wala kulia, ni
kama mlinzi anayetizama mlango ambao anajua punde utafunguliwa na hapaswi
kutizama pembeni kabla ya hapo, Sphinx.
Kichwa cha mtu lakini mwili ni wa simba, limelala kwenye aridhi hii, macho
yake yanatizama mashariki. Kama walivyo elezea uwongo kuhusu mapiramidi, ndivyo
wanavyo endelea kufundisha uwongo wao kuhusu Sphinx kwamba na lenyewe ni moja
ya kazi za waegypt wa zama flani, ni kazi ya mfalme fulani wa Egypt.
Watu kutoka nje ya Egypty walipoliona kwa mara ya kwanza, mwili wake wote ulikuwa umefunikwa na mchanga ispokuwa kichwa chake, ni kama unatazamana na zimwi linalotoka chini ya aridhi.
Lakini hakuna
ushahidi wenye mashiko kuhusiana na dai lao hilo, ispokuwa kuna ushahidi wa
kutosha kwamba Sphinx lilikuwepo hapo hata kabla ya mapiramidi yenyewe, ni la
kale kushinda historia ya binadam mwenyewe.
Yu wapi mjenzi wake, kwa malengo yapi au kwa sababu zipi aliamua kulitengeneza sphinix.
Kama yalivyo mapiramidi yale Sphinx nayo ni alama ya nyota maarufu ya Leo,
au nyota ya Simba iliyoko katika kundi la nyota kumi na mbili maarufu kama
Zodiac. Nyota hizi tunaweza kuzichukulia sawa na masaa 12.
Mjenzi wa Sphinix alifahamu juu ya nyota za Zodiaki? Na juu ya nyota ya Leo, alifahamu elimu ya nyota nje ya milk way? Na alifahamu ni lini nyota ya Leo inakuwa sambamba na uwanda wa Gaza? Je alikuwa mnajimu aliyebobea kwenye mahesabu na elimu ya nyota au mtumwa?
Muhimili wa dunia
yetu unafanya kazi ya kuhama kutoka kwenye nyota moja kwenda nyingine, au kazi
ya kutoka kwenye nyumba moja ya Zoadic kwenda kwenye nyingine kwa muda wa miaka
25,920 mpaka 25,925, unapokamilika mzunguko huu dunia yetu inapambana na
mabadiliko makubwa ambayo nitayazungumzia hivi punde.
Najua umefundishwa juu ya dunia kulizunguka jua, dunia kujizungusha kwenye mhimili wake, na pia jua kuzunguka. Lakini najua hili la mhimili wa dunia kuzunguka nyota ya Zodiak ni geni kwako. Tulia upate darsa.
Wakati nguvu za jua zinaivuta dunia upande wake na nguvu za mwezi zinaivuta
dunia upande wake, muhimili wa dunia ulio lala nyuzi 23.5 kuelekea njia ya
dunia kulizunguka jua taratibu,kwa taratibu mno unajizungusha kwenda kinyume na
njia hiyo ya dunia kulizunguka jua na kufuata kwa taratibu sana kuelekea katika
vikundi vya nyota vilivyoko katika great cirlce, mzunguko huu unaitwa
Precessional cycle ambao unaichukua dunia miaka 25920 kukamilisha kuzipitia
nyumba zote 12 zilizoko katika zodiac.
Mchoro huu unaonesha mhimili wa dunia kwenye safari yake ndefu ya miaka 25,920.
Mtu aliyekuwepo duniani anapolitizama
jua linapo chomoza asubuhi kwa zama tofauti na kwa vipindi tofauti atagundua
kuwa jua halichomozi katika sehemu moja miaka yote, bali linahama kutegemea na
kituo lililopo kwenye kikundi flani cha nyota katika ujumla wa safari yake
hiyo.
Mchoro unaonesha mhimili wa dunia katika nukta mbili za zama mbili tofauti.
Muhimili wa dunia kule uliko elekea na ambao taratibu sana na wenyewe
unahama kwenye muelekeo zilizopo nyota hizo za angani unatufanya tudhani kuwa
jua linachomozea sehemu moja, lakini mhimili huo unapo kuwa umekamilisha sehemu
kubwa ya mzunguko wake tuna anza kuona tofauti ya vitu mbalimbali ikiwemo
nafasi ya jua kuwa lilipokuwa likichomozea kabla sipo linapo
chomozea sasa.
The big Clock in the Sky, unajua sasa hivi ni saa ngapi? Sasa hivi ni PISCES NA NUSU. I like that clock!!
Hivyo katika safari hiyo ndefu kuna kipindi jua lilikuwa likichomozea nyuma ya
kikundi cha nyota ya Leo kama inavyo julikana kwa watu wa fani ya mambo ya
nyota na baadae mpaka inamaliza vikundi vyote na kisha inaanza upya tena.
Our Heavenly Clock is ticking.
Ikiwa binadam wa kwanza kukanyaga dunia hii tunamuweka kwenye kipindi cha baina ya miaka ya 6900 mpaka 6000 KK. Hii inamaana kuwa binadam alingia kwenye zama za Germin, au kipindi ambacho jua linachomozea kwenye kikundi cha nyota cha Germin. Hii inamaanisha kuwa tangu binadam wa kwanza akanyage aridhi hii, mpaka leo hii ni kama tumeishi masaa manne na nusu tu!!!!
Hatukuwepo wakati jua linachomoza nyuma ya nyota za kikundi cha Leo, ni nani aliyekuwepo zama hizo na kuliweka Sphinx hapo.
Muhimili wa dunia kwa kuchukua njia ya mzunguko tofauti na ambayo unazunguka
kuifata great cycle ndiyo inayo iwezesha dunia kuhimili nguvu za mvutano za jua
na mwezi bila kutoka kwenye muhimili wake kwa miaka bilioni 4.2 tangu ilipo
anza kufanya mzunguko huo. Kwa sababu muhimili wa dunia unavutika kuifuata
great cycle ambayo imeundwa na vikundi 12 vya nyota tofauti tofauti, hivyo zama
hadi zama muhimili huo nao utakuwa sambamba na kikundi flani cha nyota moja
baada ya kingine kutoka kaskazini mwa great cycle na baadae kusini mwa great
cycle mpaka ikamilishe mzunguko huo, na wakati mwingine mhimili huo utakuwa
ukilenga anga tupu pale unapokuwa kwenye daraja la kuvuka kutoka kikundi kimoja
kwenda kingine.
Katika zama zetu leo jua linachomoza baina ya Pisces na Aquarius. Kwa
maneno mengine mhimili wa dunia umelenga anga tupu, kutokana na kwamba tuko
kwenye kivuko tunamalizia zama za Pisces
na muda si mrefu tutaingia kwenye zama za
Aquarius, hivyo tuko kati na kati. Ama new
age na au zama mpya.
Hivyo alama 12 za Zoadic
ni kama masaa kumi na mbili na kama yalivyo mapiramidi, Sphinx nalo lililenga
kugandisha katika aridhi ya Egypt moja ya alama ya Zoadic au moja ya lisaa
katika masaa 12 ya Zoadic kwenye aridhi ya Egypt. Hivyo basi ni lini Sphinx
liliwekwa rasmi katika aridhi hiyo hapana shaka itakuwa ni kipindi ambacho jua
lilikuwa likichomoza nyuma ya alama ya Leo (Simba).
As the above, so below.
Hivyo basi Sphinx ilijengwa kutizama jua lilipokuwa
likichomoza nyuma ya nyota ya Leo kitu ambacho kilitokea maelfu ya miaka nyuma
hata kabla binaadam hajakanyaga nyumba hii inayoitwa dunia. Ajabu sana
ukizitumia nyumba 12 za zoadic kama masaa 12, utashangaa kuona kuwa binadam
tuna masaa machache sana tangu tulipoingia kwenye nyumba hii inayo itwa dunia,
kifupi hatuna zaidi ya masaa manne tangu binadam wa kwanza akanyage nyumba
hii.
Tuna masaa mangapi kabla hatujafutika.
Nisiwachoshe, msinichoshe, ngoja niweke pause kidogo hapa ... tutaendelea next time....
Aya haikumtaja Firauni kama 'MJENZI' bali mfalme wa 'VIGINGI' Kuwa mfalme wa mahala fulani haimaanishi kuwa wewe ndiye mjenzi wa mahala hapo, wafalme wengi wanarithishwa ufalme na wanakuta miji au mji ulishakuwepo hata kabala wazee wake hawajawa wafalme.Kairudie tena na ujiridhishe na upitie fasiri mbalimbali na ut
Ukifatilia sana mwisho utatambua we are nothing nasisi ni kama wageni katika nyumba tusio wafahamu wamiliki.
ReplyDeleteAtuna Budi kumludia mungu.
ReplyDeleteEnter your comment...kaka natamani siku moja nije nikuone physically nijifunze kitu
ReplyDeleteShukran kaka Ila mbona kuna aya kwenye Quran inasema firauni aliyejenga vigingi je c hizo pyramid
ReplyDeleteAya haikumtaja Firauni kama 'MJENZI' bali mfalme wa 'VIGINGI'
DeleteKuwa mfalme wa mahala fulani haimaanishi kuwa wewe ndiye mjenzi wa mahala hapo, wafalme wengi wanarithishwa ufalme na wanakuta miji au mji ulishakuwepo hata kabala wazee wake hawajawa wafalme.Kairudie tena na ujiridhishe na upitie fasiri mbalimbali na ut
Katika majuwa mimi mmoja wao ila umenitoa ujuwa naanza kuelewa mambo ambayo nilikuwa siyajui mapka ningeungiavkwenyevtumbo la aridhi
ReplyDeleteuko vzuri sana bro.
ReplyDelete