Mistari yenye maumbo ya ajabu ambayo haifahamiki ni lini hasa ilichorwa na viumbe gani, wa zama zipi.
Tukiwa tunaendelea kusaka jibu la swali letu, tuelekee Amerika ya Kusini,
Peru kwenye ustaarabu mwingine ambao mwandishi wake hafahamiki ni nani, huenda
kwa kuongoanisha kazi hizi mbili tukapata mwanga wa swali letu. Kwenye uwanda
wa Nazca.
Uwanda wa Mazca kwenye ramani.
Eneo hili lenye aridhi yenye ukame mkubwa ambao hata kidogo hauwezi
kumvutia binaadam kuishi katika uwanda huo, wala haifikiriwi kama patakuja
kumvutia binaadam kufanya makazi hapo, lakini ajabu kuna maajabu ambayo katu
huwezi kusema ni kazi iliyojifanyiza yenyewe kutokana na hali mbalimbali za
kimazingira za eneo hilo, bali kuna ambaye aliyo fanya kazi hiyo ya usatidi wa
ajabu.
Ni nani msanii wa kazi hizi, ni katika zama zipi aliishi msanii huyu, kwanini alichukua shida, kama basi hata ilikuwa nishida kuifanya kazi hii katika aridhi ambayo haitafutika kwa milenia zenye kutajika?
Yu wapi mkandarasi huyu na ujuzi wake wa ajabu?
Mistari ya Nazca ipo kwenye jangwa la Nazca, kwenye uwanda wa juu wa unao
jumuisha miji mbalimbali ya Nazca na sehemu kubwa ya tambarare iliyopo kusini
mwa Peru, eneo hili lote linafikia kilometa za mraba 520. Eneo hilo lote
limejaa michoro ya maumbo tofauti tofauti, iliyochorwa kwa mistari mirefu, kuna
iliyonyooka kwa takribani kilometa 8, na kuna inayo endelea na kufikia kilometa
65, michoro hiyo inaonesha maumbo ya vitu mbalimbali kama, mimea , barabara
zinazo dhaniwa kutumiwa kurushia ndege na mapiramidi, michoro kwenye uwanda wa
ukame wa Nazca inakadiriwa kufikia 300.
wazo la msanii aliyefanya kazi hii ni kama wazo kutoka dunia nyingine, ngumu kuelezeka kwenye dunia yetu.
Maumbo hayo yamechorwa kwa kupitia
mistari iliyonyooka na kuonganishwa pamoja ambayo inaonekana ukiwa angani tu,
ni mipana sana hivyo huwezi kuona chochote mpaka unapokuwa angani.
Hawakufundishi kwenye somo la historia kuhusiana na hii mistari, ambayo tumejua si mistari iliyochorwa kibususa, bali ni mistari inayo tengeneza maumbo ya viumbe wa ajabu kabisa. Kikubwa unach fundishwa ni kuwa babu yako alikuwa ni sokwe.
Mchoraji wa michoro hiyo hakuchagua eneo hilo kwa kubahatisha, eneo hili ni
la ukame linalo pokea mvua ya dakika ishirini tu kwa mwaka, aridhi yake ni
tambarare na ngumu mno na hii inapunguza kiasi cha mmomonyoko wa aina yoyote
ile, hakuna vumbi wala mchanga wa kufukia alama hizo, hakuna upepo wala mvua wa
kumomonyoa kazi hiyo ya ajabu, aridhi hiyo ngumu ilichimbwa kwa teknolojia
tusiyo ifahamu mpaka kufikia tabaka la chini ambapo kuna aridhi yenye tabaka lenye
kung’ara, si kuwa mchoraji alitaka kazi yake ibaki zama hadi zama bali pia
alitaka iyaonekane daima.
Zaidi watakuambia kwamba mistari hiyo ilichorwa na watu wa zamani, watu wenye maarifa duni kwa kutumia zana duni, walijichorea chorea tu na kisha yakatokea maumbo hayo kwa nasibu. Wakati katika zama zetu na teknolojia tuliyo nayo hatujaweza kutengeneza kopi ya kazi hiyo kokote pale.
Kwa zama zote iliyoishi mistari hiyo, na kwa dhoruba na mabadiliko ya hali
mbalimbali za dunia, mistari hiyo imebaki kama alama ya maarifa, elimu na
teknolojia ya juu kabisa kwa viumbe ambao hatuwafahamu. Ni vigumu katika zama
zetu kupata jengo lililo ratibiwa kudumu japo kwa milenia moja, lakini kazi za
Nazca zimepita milenia kadha wa kadha mpaka leo zimetufikia.
Yu wapi msanii wa michoro hii, je mwalimu wako wa historia anaweza kutusaidia kujibu swali hili. Au tumuulize mwalimu wako wa Jiografia na nadharia ya mmomonyoko wa udongo labda anaweza kutupa majibu ya mistari hii ya Nazca?
Maumbo mengine
yana urefu wa mita 285. Maumbo ya viumbe wengine si ya asili kwa hapo Nazca,
kama vile umbo la Buibui mwenye urefu wa mita 45 ambaye ni wa kundi la
Ricinulei wanao patikana sehemu ya ndani kabisa katika pori la Amazon kwenye
maeneo ambayo ni vigumu kuingilika, kikawaida buibui hawa wanakuwa na urefu wa
milimita 5-10.
Buibui aina ya Ricinulei, aliyechorwa kwenye jangwa hilo kwa urefu wa mita 45.
Mguu wao mmoja ni mrefu mno ambao nchani mwa mguu huo ndipo
kilipo kiungo cha uzazi cha mdudu huyu, na haionekani mpaka kwa microscope,
lakini viumbe hawa waliona vyote hivyo na kumchora juu ya aridhi ngumu kama tunavyo
andika juu ya karatasi.
Mchoro wa buibui huyo kama alivyochorwa na viumbe tusiowajua, katika aridhi ngumu ya Nazca, tizama hawakuacha hata kiungo cha uzazi wa kiumbe hicho kulichopo kwenye ncha ya mguu wake wa kulia, wala hapatikani eneo hilo buibui huyo.
Michoro hii huonekana ukiwa angani tu, ni sehemu ndogo sana ya michoro hii
unaweza kuiona unapokuwa tambarare, michoro mikubwa kabisa ambayo inaonekana
ukiwa juu angani, michoro hiyo inatokea sehemu moja ya uwanda huo na kumalizikia
upande mwingine kana kwamba ni mtu aliye chora juu ya karatasi laini kwa
kutumia penseli iliyochongwa vizuri, lakini hapo ni juu ya aridhi ngumu yenye
ukame na juu ya yote ina miinuko na maporomoko lakini katu michoro hiyo
haikupinda wala kukesewa shabaha yake kutokana na hali ya aridhi hiyo.
Kabla ya kuanza kurusha ndege kwenye karne ya ishirini, ndege zilipoanza kupita eneo hilo, hatukuwa tukifahamu chochote juu ya mistari hiyo. Vizazi na vizazi vilivyo ishi hapo vilichukulia mistari hiyo kama aina fulani ya barabara ambazo hawazijui mjengaji wake ni nani. Tulipoanza kurusha ndege eneo hilo tulidhani ni njia za kurushia ndege, ;Air Line Strip'
Ni
michoro ya wanyama na ndege wa aina tofauti tofauti, na pia kuna michoro ya
maumbo na mistari mirefu ambayo inafanana na barabara za kurushia ndege.
Kabla hatujaanza kurusha ndege, mistari hii ilidhaniwa ni barabara zisizo na muelekeo maalum.
Michoro na mistari hiyo ilianza kujulikana mnamo karne ya 20 baada ya
binaadam kuanza kurusha ndege, ni lini imechorwa nani kachora hakuna anayejua.
Moja ya mchoro maarufu kwenye uwanda wa Nazca ni mchoro wa nyani, ambaye umbo lake kukamilika mchoraji alionganisha mistari mirefu iliyopanda na kushuka juu ya vilima na mabonde.
Kuna mchoro unao muonesha nyani, mistari inayopita juu ya mapiramidi, na
kushuka na kupanda juu ya mabonde bila kukatika hatimaye unatoa umbo kamilifu
la nyani mwenye urefu wa futi 400 na upana wa futi 300. Michoro hii moja ya
vitu ilivyo hitaji ni taaluma ya kuruka angani itakayo muwezesha mchoraji
kupata picha kamili ya mchoro wake, teknolojia ambayo ilipo anza kushika kasi
karne ya ishirini ndiyo ilituwezesha kugundua kuwa kuna viumbe walioishi kabla
na walikuwa na teknolojia bora kushinda ya kwetu ya kuchora picha kubwa juu ya
aridhi kama ambavyo tunavyo chora picha hizo leo juu ya karatasi kwa kutumia
kalamu.
Yuwapi mchoraji huyu, ni katika zama zipi aliishi na kwa teknolojia gani aliweza kuwacha alama ya namna hii?
Kazi hiyo haiwezi kusemwa ni ya zama fulani katika historia, na wala ya
utamaduni fulani uliopata kurikodiwa, ni kama ni kazi ya wageni kutoka sayari
nyingine.
Ndege maarufu, 'homebird' lakini hapo si kwenye karatasi bali kwenye aridhi ngumu ya Nazca.
Inawezekana wachoraji wa michoro hiyo ndiyo wa choraji wa ramani zile za
kale ambazo nazo hazijulikani mchoraji wake ni nani? Ramani zinazo onesha kwa
ukamilifu na kwa vipimo sahihi bara la Antarctica, Amerika ya Kusini na sehemu
ya Afrika?
Viumbe wengine hawafahamiki ni viumbe gani na wazama zipi.
Katika michoro hiyo hakuna ambao ni mdogo unaoweza kuonekana katika ukiwa
unatembea juu ya aridhi, lazima uwe juu ya chombo angani ndiyo utaweza kupata
picha kamili ya mchoro.
Its a piece of art, but who and where is the artist of that magnificent piece of work?
Mbali na michoro hiyo ya wanyama na barabara za
kurushia ndege, pia kuna maumbo ya kuchonga mfano wa yale yanayo fahamika kama
megalithic cultures, maumbo ambayo masalio yake yame pata pia kupatikana chini
ya bahari kwenye maeneo ya Cuba. Maumbo hayo yanakadiriwa kuwa na uzito zaidi
ya tani 100, yamepangwa kwa ustadi katika mstari ulio nyooka, mengine
yamepangwa vizuri juu ya mengine, si kazi iliyofanywa na mazingira yake, wala
si kazi iliyofanywa na binaadam.
Peru, Italy, Turkey, Egypt ... mapande hayo ya miamba hayakujifanyiza yenyewe, labda kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa au mfano wa hayo, wala si kazi ya uwoo wa asili, mapande hayo ya mawe ni makubwa menfine kufikia mpaka tani 1000. Hakuna ustaarabu wowote uliopata kurikodiwa kokote pale kuwa waliweza kumiliki mshine za kunyanyua uzito hata wa tani 1. Lakini hapa tunazungumzia tani 1000 na zaidi, zimenyanyuliwa kwa ustadi na mahesabu ya hali ya juu, jabali moja likapangwa juu ya jingine na kutengeneza ukuta, piramidi au chochote kile alichokitaka mjengaji. Kwa maelfu ya miaka kazi hizo zikabaki kwenye uso wa dunia na kuhimili kila aina ya dhoruba na misiguano iliyougusa dunia hii tangu enzi na enzi, na leo zimesimama mbele ya macho yetu kama zilivyokuwa hapo mwanzo, na swali moja likigonga vichwa vya wahandisi waliobobea, wanahistoria na wanasayansi wakijiuliza, 'waliwezaje'? Wengine wakiliuza walifanya haya lini? Lakini swali la muhimu zaidi ni akina nani hao? Kuna wakutujibu swali letu?
Huwezi kufika Peru halafu isipelekwe Machu Pic'Chu, palipo jengwa mji na ngome ya ajabu kabisa, si wajenzi wake wala zama za lini palijengwa havijulikani.
Stay tuned tunakwenda Egypt kwanza, halafu tutarudi tena hapa Peru, lakini hatutizama Mistari ya Maajabu ya Nazca, bali maajabu mengine kabisa yatakayo tikisa msingi wa imani yako na msingi wa mafunzo yote uliyowahi kupatiwa kwenye 'indoctrination camps' wewe unaziita shule au chuo. Lengo ni kujua je Tupo wenyewe?
No comments:
Post a Comment