Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?
Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.
Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.
Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!
Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%
Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...
Saturday, December 24, 2016
QUEEN REPLACED ... ep: 3
What's wrong with the
world, mama
People livin' like they
ain't got no mamas
I think the whole world
addicted to the drama
Only attracted to things
that'll bring you trauma
Overseas, yeah, we try to
stop terrorism
But we still got terrorists
here livin'
In the USA, the big CIA
The Bloods and The Crips
and the KKK
But if you only have love
for your own race
Then you only leave space
to discriminate
And to discriminate only
generates hate
And when you hate then
you're bound to get irate, yeah
Madness is what you
demonstrate
And that's exactly how
anger works and operates
Man, you gotta have love
just to set it straight
Take control of your mind
and meditate
Let your soul gravitate to
the love, y'all, y'all
People killin', people
dyin'
Children hurt and you hear
them cryin'
Can you practice what you
preach?
Or would you turn the other
cheek?
Father, Father, Father help
us
Send some guidance from
above
'Cause people got me, got
me questionin'
Where is the love (Love) .... (From Black Eyed Peas)
These are strange days!
Ni nini kinaendelea, sijui.
Mwili wa balozi wa Urussi kwenye Jeneza, Andrey Karlov
Je Urusi inacheza karata ya ‘false Flag’? Sijui?
Au kuna ambalo hatulijui kuhusiana na ‘mauwaji’ ya balozi wa Urussi ndani
ya Uturuki? Sijui.
Kuna kubwa zaidi ya picha ya kijana ‘akimuuwa’ balozi wa Urussi na kuanza kutamka ‘Allahu Akbar! Kumbuka Allepo? Sijui.
Mwili wa Andrey Karlov ukiagwa
Ninacho jua ni kwamba Urussi kwa namna yeyote ile kuhusiana na Syria hakuwa
na haja ya kutengeneza ‘False Flag’ ya namna ile. Urussi ilishashinda vita
dhidi ya wana mgambo wa ISL, Assad anajiamini zaidi sasa kuliko vurugu hizo
zilipokuwa zikianza. Hawana haja yeyote ya kutengeneza ‘False flag’ hiyo.
Au Uturiki itapata nini kwa kuja na kituko hicho?
Andrey Karlov mwili wake kwenye jeneza kutoka kanisani.
Kama kweli mauwaji yale yametokea pale kwenye jumba lile la sanaa, kama
tulivyo oneshwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani, basi pasingekuwa na
haja ya kujiuliza maswali yote hapo juu. Sababu dunia imesha gawanywa kati ya
‘mashetani’ ambayo ni mataifa ya magharibi na washirika wake, na ‘malaika’
ambao ni Urrusi, China na washirika wao, moja kwa moja tungeona ni ‘mashetani’
yanaanza chokochoko zao za ugomvi.
Mwili wa Andrey Karlov ukiagwa na Putin
Au tungeona ni mbinu za ‘mashetani’ za
kutaka kuwa sambaratisha ‘malaika’ kwa kuwa gawanya baina yao, sababu mjumbe wa
‘malaika’ kauliwa na ndani ya nyumba ya ‘malaika’ kupitia kwa pandikizi
lililovaa sura ya ‘malaika’
Muuwaji Mevlut Mert Altintas akiwa nyuma ya windo lake, balozi Andrey Karlov
Lakini ambacho kimetokea kwenye jumba lile, kwa jicho huru, siyo kwa jicho
la vyombo mbalimbali vya habari ni kuwa hakuna ‘mauwaji’ yaliyo tokea pale.
Basi ikiwa hivyo ndivyo iweje ‘malaika’ waseme uwongo kwamba mjumbe wao kauwawa
na ajenti wa ‘shetani’ ikiwa hajauwawa?
Mwili wa balozi Andrey Karlov ukiagwa
Mbona hatuna historia ya ‘malaika’ kusema uwongo? Ni nini kinaendelea
kwenye uso huu wa dunia? Russia, Syria, na Uturiki wanafaidika na kitu gani kwa
kusema uwongo kuwa balozi yule kauwawa ndani ya jumba lile?
Vita havina macho
Urrusi kwa kazi iliyoifanya na inayo endelea kuifanya Syria ya kuwaondoa
wanamgambo walikuwa wakidhaminiwa na Marekani na NATO, kila mwenye jicho na
akili huru alimuunga Urrusi mkono, na kila mmoja alijuwa kwamba jambo lile
limeiudhi sana ngome ya ‘shetani’; Marekani, NATO, na washirika wao. Wala
Urrusi haikuhitaji baraka za yeyote kufanya kile ilicho kifanya, na wala
hawakujali nani anasema nini juu ya hilo, hivyo haikuwa inahitaji kumridhisha
au kumshawishi yeyote yule ili iendelee na hicho inacho kifanya huko Syria.
So sad
Mauwaji yale yangekuwa yametokea ndani ya jumba lile kama tunavyo ambiwa,
basi moja kwa moja, kauli ya Putin kwamba mauwaji yale yanalenga kuzorotosha
kazi anayo ifanya Syria, kauli hiyo ingekuwa nzito, yenye mashiko na kila mmoja
wetu angekaa tayari kusubiri kuona nini kitafuata. Na kila mmoja wetu
angeonganisha tukio hilo na lile la kuuwawa kwa mwana mfalme Archiduke Ferdinand kuliko
pelekea kuibuka kwa WWI.
Habari ilivyokuwa baada ya kifo cha Archiduke, tukio hilo likawa chachu ya WW1
Lakini hakuna mauwaji yaliyo tokea kwenye jumba lile,
je Putin naye sasa anatumia ‘false flag’? Je anataka amsingizie nani tukio lile
ili amvamie? Lakini Putin kesha sema ni magaidi na ‘watai-feel it’ hicho
kichapo atakacho wapa, lakini hii haina maana yeyote kwasababu Putin tayari
amesha washughulikia magaidi vya kutosha, na wameshai-feel it, vya kutosha,
mpaka wakina Obama na Kerry wamei-fee it, sasa kuna haja gani ya kutengeneza
tukio kama lile, kwa faida ya nani, kwa malengo yapi? Au hii ni aina mpya ya
Archiduke bado hatujaing’amua?
Time will tell.
Kikaragosi kikimuonesha muuwaji wa mwana mfalme akitekeleza kazi aliyo tumwa.
Sanaa ndani ya jumba la sanaa.
Wakati muvi lenyewe linaanza, hali yakuwa najua ni vidio inayo husu ‘mauwaji’
ya balozi wa Urusi macho yangu yakikaza kutazama muuwaji ataokea kwa wapi,
sababu mbali na waandishi wa habari, ‘muwaji’ hakuonekana kama anayo ajenda
nyingine yeyote zaidi ya ‘mlinzi.’
Muuwaji Mevlut Mert Altintas akiwa nyuma ya windo lake, balozi Andrey Karlov
Ninacho sema hapa ni kuwa, mtu ambaye anayo
silaha na mlengwa yupo mbele yake lakini haonishi hali yoyote ya wasiwasi,
hofu, kuzidiwa na shauku au hamu ya kitu, yupo sooo calm to be a real killer.
Hakuwa kama mtu ambaye sekunde chache zijazo atafanya tukio la kuishtua dunia,
bali kama mtu aliyekuwa anasubiri maelekezo kutoka kwa ‘camera man.’
Muuwaji Mevlut Mert Altintas akiwa nyuma ya windo lake, balozi Andrey Karlov, ukitazma kushoto unamuona mpiga picha, na utaona mguu wa mwandishi wa kike, ni kama 'muuwaji' alikuwa akisubiri mpiga picha huyu aondoke, lakini hakuna vidio inayo muonesha mwandishi wa kike akiondoka hapo alipo, ispokuwa kamera man alipokuwa anachukua 'muvi' hii alimkata kwa makusudi asionekane, sababu kungeongeza maswali.
Ijapokuwa balozi alikuwa mbele ya muuwaji, lakini kwenye kona ambayo ‘muuwaji’
alikuwa amesimama angeweza kuonekana na watu wote wa mbele waliokuwa
wanamsikiliza, mwandishi wa kike aliyekuwa karibu kabisa na ‘muuwaji’ na hata
balozi mwenyewe. Watazamaji na mwandishi wa kike wangekuwa wa kwanza kushtuka
au kutahayari kwa kumuona ‘muuwaji’ anatoa bastola kumlenga balozi.
Mpiga picha ameondoka, mwandishi wa kike amebaki, lakini mbele ya balozi Andrey Karlov waaandishi wengine bado wanaonekana, na hivyo wanamuona yeye na muuwaji Mevlut Mert Altintas pia, ni sekunde chache kutoka hapo muuwaji ataanza igizo lake.
Kushtuka
kwao kungemshtua balozi naye angeweza kuona nini kinaendelea. Hivyo
tungetegemea kuona mshtuko huo kwa balozi, mwandishi wa kike na watazamaji
kabla ya milio ya risasi kuanza kusikika.
Muuwaji Mevlut Mert anaingiza mkono kwenye mfuko wa koti kutoa silaha yake, ukitazama kwenye hiyo kona, aliyosimama mtu wa kwanza ambaye angehisi kitu ni waandishi waliokuwa mbele ya balozi, wapili ni mwanadada mwansidhi ambaye naye alikuwa karibu naye, lakini wote walikuwa kimya, lakini kama hatua ya 'muuwaji' kuingiza mkono kwenye koti lake haikuwashtua, hatua iliyo fuata ilikuwa na kila sababu ya kuwashtua.
Lakini haikuwa hivyo wote walikuwa
kimya kama wanaigiza, of-course walikuwa kwenye jumba la sanaa ulitegemea nini
zaidi ya maigizo?
'Action', muuwaji Mevlut Mert keshaitoa silaha yake kumlenga balozi, ukitazma macho ya balozi na mwenyeji wake hayaoneshi kupata 'alert' yoyote kutoka kwa waandishi wa habari wanao watazama, lakini kwa makusudi kabisa, kamera man akamtoa kwenye 'scene' mwandishi wa kike ambaye alikuwa karibu kabisa na muuwaji na ambaye angetupa 'clue' ya nini kinaendelea. Ingawa muuwaji alikuwa 'very fast' lakini ilikuwa haitoshi kwa watu walio mbele yake kutoona kitu. Kimaumbile mwandishi wa kike alipaswa atahayari, shtuke, aruke au asogee kwa woga, kitu ambacho kinge 'wa-signal' balozi na mwenyeji wake kufanya the same, na kama angeonekana kwenye scene na kubaki kimya kama balozi na mwenzake pia ingezua maswali, kukata mzizi wa fitina 'camera man' akamdelete mwandishi huyo kwenye scene. Lakini bado waandishi walio mbele yake wangetosha 'kuwa-alert' balozi na mwenzake.
Tamthilia hiyo ikaendelea. Tizama vidio hiyo kwenye ‘slow motion’ au weka ‘pause’
baada ya milio ya risasi, utaona balozi alianguka baada ya mlio wa tatu wa
risasi. Sehemu aliyosimama ‘muuwaji’ namna alivyo ielekeza bastola yake kwa
balozi ni eidha risasi ingempata kichwani au mgongoni, lakini hapakuwa na
nafasi ya kumkosa. Lakini ni kama risasi mbili za mwanzo hazikumpata balozi,
sababu bado alikuwa amesimama baada ya milio hiyo miwili, kitu ambacho
hakiwezekani kabisa kwa ‘muuwaji’ aliyepewa kazi hiyo, na ukichukulia umbali
aliyekuwepo kati yake na windo lake. Maana yake ni kuwa eidha muuingizaji wa
sauti kwenye vidio hiyo aliwahi kuiingiza au balozi mwenyewe hakusikia sauti ya
‘director’ aliposema ‘action.’
wa Ukitazama kwa makini hii vidio, vizuri kama utakuwa na headphone au earphone utumie kusikiliza sauti ya mlio wa risasi mbili za mwanzo, utagundua kuwa balozi hakufanya reaction yeyote kwenye risasi mbili za mwanzo. Ukitumia earphone au headphone utaona hicho ninacho kisema. Wakati kamera man anarudisha kamera kwa muuwaji milio ya risasi inaendelea kusikika kanakwamba muuwaji anaendelea kupiga risasi, lakini utaona kwenye frame hiyo japo risasi zinasikika wakati kamarea inahama, muuwaji hakuwa anapiga risasi bali alikuwa kanyanyua mkono mmoja juu na mwingine umeshika bastola ingawa hauoneshi kama ndiye yeye alikuwa anapiga. Inahitaji umakinifu unapo tazama ung'amue hivyo vitu viwili nilivyo taja hapo, hii inamaa sauti ya mlio wa risasi imefanywa kurikodiwa, lakini si risasi iliyopigwa humo ndani.
Kitu cheupe mithili ya mwanga kinatokea ghafla na kupotea kwenye kifua cha
balozi. Mithili ya filamu za Holywood, mwanga huo ulilenga kuonesha athari ya
risasi iliyotokeza kwa mbele kutoka mgongoni.
Mwanga huo mweupe kwenye vidio hiyo umefanywa kuongezwa, 'edited' ili kuonesha athari ya risasi inayo tokeza mbele ya kifua cha balozi.
Lakini ikiwa ni risasi iliyokuwa ikitokeza au iliyotokeza kwa mbele kutoka
mgongoni tungetegemea kuona damu pamoja na mwanga huo, lakini si kwamba tu
hapakuwa na damu lakini athari hiyo ya risasi haijaonekana hata mwili wa balozi
ulipokuwa sakafuni. Suti yake ilikuwa bado safi na haina tundu lolote la risasi
iliyotegemewa kuwa imetokezea kifuani.
Mwili wa balozi sakafuni, athari ya weupe ule labda ni nguo umechanika au hivi havionekani kwa hapo sakafuni alipolala.
Sababu balozi hakuonekana kujeruhiwa kichwa, maana yake ni kuwa risasi hizo
zimempiga mgongoni. Imesikika milio sita ya risasi baada ya ile miwili ambayo
balozi alichelewa kujirusha chini, hivyo jumla ya risasi nane tuseme zime mlenga
balozi. Risasi nane zimemlenga na kumpta mgongoni, ukimtazama balozi wakati
anaenda chini utamuona anashika tumbo!
Rwaction ya balozi kushika tumbo wakati weupe ule ulilenga kuonesha risasi inatokea kifuani, ni ngumu kuielezea iingie akilini.
Reaction hii ni ngumu kuingia akilini.
Jaribu kufikiri umesimama mahala pa wazi, anakuja mtu nyuma yako na kukusukuma
kwa nguvu, ‘reaction’ yako itakuwa ni ipi? Risasi nane mgongoni si sawa na
sindano mgongoni kwamba utasimama pale pale ikichome moja baada ya nyingine,
zitakusukuma mbele kama siyo kukurusha, lakini alicho fanya balozi ni kushika
tumbo! Nadhani hakusikiliza vizuri maelekezo ya director.’
alikwenda chini so smothly kama mtu aliyechomwa sindano ya nusu kaputi, hata microphone aliyokuwa anaitumia haikuanguka, achilia mbali vitu vingine vilivyokuwa mbele yake.
Tulitegemea angerushwa mbele kidogo na angeanguka kwa tumbo, lakini
ukitazama vidio hiyo utaona baada ya kushika tumbo, balozi alifanya kama
kuchuchumaa, kisha, ‘cut.’ Kamera iliporudi kwake balozi alikuwa amelala kwa
mgongo na siyo kwa tumbo, kama kwenye movie vile. Kapigwa risasi nane mgongoni,
tulicho tegemea ni kuanguka kwa tumbo na siyo kwa mgongo kama inavyo onekana.
Hatujui ni vipi balozi alilipata hili pozi la kulala kwa mgongo, lakini ni pozi sahihi, sababu angelala kwa tumbo tungeona mgongo wake hauna hata tundu moja la risasi na hiyo ingezuwa maswali. Pozi hilo hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharam apite.
Hakuna damu. Tulitegemea kwa milio nane ya risasi, balozi angekuwa amelala
kwenye dumbwi la damu. Lakini haikuwa hivyo, hapakuwa na tone la damu. Kilicho
onekana kichwani kwake kama damu kinatiashaka kwa sababu hakuna risasi iliyo
mlenga kichwani.
e.Kumbuka Allepo! Allah Akbaru! yote hayo ni kuongeza kachumbari kwenye pilau yetu ili inoge. Walinzi nao walihakikisha wanamuacha jamaa azungumze yake yote bila kujali kuwa anaweza kusababisha madhara zaidi, picha za muuwaji akiwa amekufa zimepigiwa , ingawa picha hizo ukizitazama nazo zina maswali ya kutosha na hitimisho moja kama kwenye muvi yenyewe ya kuuwawa balozi, yaani nazo zimefanyiwa adobe-shop.
Mwili wa balozi wakati unatolewa kwenye amblence alikuwa
umetolewa shati, na bado hapakuwa na jeraha lolote la risasi iliyopaswa kutokea
kifuani, wala haukuwa na tone hata moja la damu!
uuKwenye vidio hii mwandishi kaelezea details nyingine ambazo sijazitaja hapa, ambazo nazo zinaendelea kutilia shaka tukio zima la balozi huyi kuwawa ikiwemo hilo la kukosekana kwa damu kwenye mwili wa balozi hata alipokuwa kifua wazi akitolewa kwenye amblence kwenda hospitali.
Baada ya ‘mauwaji’ hayo ‘muuwaji’ aliendelea kuranda randa kwenye eneo la
tukio mpaka akakaribia kuishiwa na pozi ndio waka-cut. Tukio lile tulitegemea
linarushwa live lakini mpaka wana-cut hapakuwa na maafisa usalama wowote
waliovamia jengo hilo kukabiliana na ‘muuwaji’.
Muuwaji anaendelea kufika ujumbe kwa raha zake. Kamera man wetu alikuwa ni shujaa sana, sababu aliendelea kumrikodi muuwaji licha ya kuwa kwenye hatua hiyo kila mtu alikimbia kunusuru uhai wake lakini yeye alibaki bila kutishika akaendelea kurudi muvi hiyo.
Sababu ‘muuwaji’ aliachiwa muda wa kutosha, akaanza kuweka pozi kwenye
kamera kama zile za James Bond kwenye 007. Pozi nyingine zilionekana kurikodiwa
kabla ya ‘tukio’ hilo, nadhani waliamua kutuwekea ‘behind the scene’ ili
kukoleza utamu wa tukio.
Piccha hii ni ya 'behind the scene', kunauwezekano mkubwa ilirikodiwa kabla ya tukio lenyewe kutokea, sababu kwenye tukio halisi muda wote muuwaji alionekana ana silaha baada ya tukio, lakini kwenye picha hii silaha hiyo emefanyiwa 'adobe photoshop', huwezi kugundua hilo mpaka ui-zoom kwenye mikono yake.
Kama kweli balozi amekufa, hakuuliwa ndani ya jumba la sanaa bali chochote
ambacho kitakuwa kimepelekea kifo chake kitakuwa kimetokea baada ya tukio hilo
la risasi.
Unapo ikuza picha hiyo kwenye mikono iliyo paswa kushikilia bastola utaona kuwa mikono hiyo haikuwa imeshika bastola, huwenda ni wakati wa kufanya rehersal ndiyo picha hiyo ilipigwa, kisha baadae ikafanyiwa photoshop na kuwekewa bastola. Mwenye macho haambiwi tazama, labda kama huyaamini macho yako.
Hatujui wala hakuna picha wala vidio yoyote ya kile kilicho kuwa
kinaendelea kwenye gari la wagonjwa, tulichoona ni balozi akitolewa kalazwa
kwenye kitanda, kifua wazi na kukimbizwa ndani ya hospitali. Wala hatujui nini
kiliendelea huko hospitali. Lakini filamu iliyochezwa kwenye jumba lile
haitoshi kuelezea kifo cha balozi.
Muuwaji akiendelea kuweka mapozi kama kwenye 007, wala kamera man hashtuki anaendelea kurikodi muvi yake.
Tukio hili bado lina maswali mengi, hasa kila ukitumia akili huru inakuthibitishia kuwa mauwaji hayakufanyika ndani yajumba la sanaa, zaidi ya usanii kwenye jumba la sanaa. Lakini Putin anapo thibitisha kuwa kauwawa, Kerry naye na maafisa wengine wakuu wa serikali zingine duniani wanapo fanya hivyo, wakati mazingira ya kifo chake yaki kataa hilo inakuwa vigumu kuelewa nini hasa lengo la 'false flag hiyo'.
007 in action
Ikiwa kweli balozi huyo amekufa basi pana hitajika ushahidi HURU kuanzia anaingizwa kwenye gari la wagonjwa na kile kilicho endelea baada ya hapo.
Next week tutaendelea na posti yetu ya 'Je Tupo Wenyewe?'kuhusiana na Queen Replaced itaendelea kuja kila pale panapo kuwa na haja mpaka na tutakapo fahamu sababu hasa za maagizo haya. Tchao ...
Sasa ndugu Salim unataka kutuambia nini.? Ni kwamba balozi ameuwawa au yupo hai hadi sasa..? na kama hayupo aliwawa kivingine ni kwanini hii unayosema ni movie isiwe ndio ya kumuua kweli.? maana kwa vyovyote vile balozi na muuwaji wote walitakiwa wage.. Na kweli wote walikufa haijalishi waliwawa kwa staili gani. Suala ambalo tunataka utuchunguzie ni kuwa ni nani kweli alihusika na kifo cha balozi?? na kwanini afanye hivo?? Issue si kwamba et aliwawa kwa staili gani. I
DUNIA INAHITAJI WASOMI WENYE AKILI HURU KAMA OMAR MSANGI ILI KUIFANYA JAMII IWEZE KUSALIMIKA NA PROPAGANDA ZA KIMATAIFA
ReplyDeleteSasa ndugu Salim unataka kutuambia nini.? Ni kwamba balozi ameuwawa au yupo hai hadi sasa..? na kama hayupo aliwawa kivingine ni kwanini hii unayosema ni movie isiwe ndio ya kumuua kweli.? maana kwa vyovyote vile balozi na muuwaji wote walitakiwa wage.. Na kweli wote walikufa haijalishi waliwawa kwa staili gani. Suala ambalo tunataka utuchunguzie ni kuwa ni nani kweli alihusika na kifo cha balozi?? na kwanini afanye hivo?? Issue si kwamba et aliwawa kwa staili gani. I
ReplyDeletesijaelewa swali lako mdau ...
Delete