Kama tulivyoona, kama tulivyo fundishwa na tunavyo endelea kufundishwa
kwamba mara ya mwisho kabisa kwa maji kupata kuwepo kwenye maeneo haya tajiri
kwa barafu ni mamilioni ya miaka iliyo pita. Kutokana na hivyo elimu hiyo hiyo
pia inatuambia kwamba kwenye mamilioni hayo ya miaka yaliyopita, hakuna binadam
au ustaarabu wowote ule ulio pata kuwepo zama hizo, achilia mbali binadam au
ustaarabu ambao ungeweza kuzichora ramani hizo kwa ustadi tuliyo uona.
Ujazo wa barafu uliolifinika bara hilo tangu miaka ya 4000 Kabla ya Kristo mpaka sasa.
Shida au mzizi wa tatizo ni kwamba ramani hizo zilichorwa kipindi ambacho
maeneo hayo hayakuwa na barafu. Ikiwa ndiyo hivyo inamaana Darwin na wenzake
kwenye misingi ya Evulution wamefanya makosa makubwa sana kama siyo wamefanya
uwongo mkubwa sana. Kwa mujibu wa Darwin na wenzake ni kwamba binadam wa zama
hizo hakuwa na uwezo hata wa kutengeneza nguo ya kuusitiri mwili wake hivyo
haiwezekani awe ndiye aliye chora ramani hizo.
Kulingana na Darwin, binadam wa zama hizo alikuwa bado ana 'evolve' na hakuwa hata kidogo na taaluma ya kijiografia ya mazingira yake achilia mbali kuchora ramani.
Swali lisilo na jibu la kueleweka, basi ni nani katika zama hizo aliyechora
ramani hizo? Je ni viumbe kutoka sayari ya mbali? Ni nani anayeweza kuwa ndiye
mwanajiografia wa kazi zile?
Michoro ya kale kwenye baadhi ya jamii duniani, inaelezea ujio wa viumbe wa ajabu kutoka sayari za mbali.
Je tuamini kwamba binadam mwenye ustarabu na teknolojia kama tuliyo nayo
sasa katika karne hii waliishi pia katika miaka ya 13,000 Kabla ya Kristo kisha baadae
wakatoweka ndiyo tukaja sisi kizazi cha Darwin? Kama ndivyo ni lini kizazi
hicho kilitoweka?
Kwenye jamii mbalimbali zenye tamaduni tofauti kwenye kona tofauti za dunia kumekuwepo na hadithi ambazo zimegeuka kuwa ngano za kale juu ya uwepo wa viumbe vya kale wenye maumbo na taaluma kubwa kushinda zama zetu za sasa, je jamii hiyo ndiyo wachoraji wa ramani zile?
Ukizitazama ramani za Piri Reis, Oronteus Finaeus, Mercator na Buache zinasisitiza
kuwa bara la Antaktika limekuwa likifanyiwa ‘survey’ kwa zaidi ya maelfu ya
miaka tangu lilipokuwa halina barafu,
barafu ilivyoanza kutokea, na barafu ilipokuwa inaelekea kuzifunika pwani zake
na mwisho kabisa ni mpaka mwaka 4000KK ndiyo bara zima likawa limefunikwa na
barafu mpaka hivi leo.
Picha hii inaonesha maeneo ambayo yamechorwa kwenye ramani ya Reis kwa usahihi wake ikiwemo pwani ya Antractika ikiwa haina barafu.
Vyanzo vya asili vya ramani za Piri Reis na Mercator zilitengenezwa kipindi
ambacho pwani za Antarktika hazikuwa na barafu kabisa. Vyanzo vya ramani ya Oronteus
Finaeus kwa upande mwingine ni vya kale zaidi, sababu zinalionesha bara hilo
kipindi ambacho barafu ndiyo inaanza ndani kabisa na hasa katikati ya bara
hilo. Wakati vyanzo vya ramani ya Buache vyinaonekana ni vya kale zaidi mno
kushinda wenzake sababu zinalionesha bara la Antarktika likuwa halina barafu
kabisa, kipindi kinacho kadiriwa kuwa ni 13,000 Kabla ya Kristo!
Hapa zinaonekana ramani mbili , moja ya rangi ya kijani ni ya zama zetu, nyingine ni ile iliyo chorwa na Finaeus. Ya zama zetu bara lote ni barafu, ya Finaeus barafu inaonekana sehemu ya kati na ndani kabisa kwenye bara hilo, milima na mito inaonekana ikiwa haina barafu.
Bado ukizitazama ramani za Piri Reis zinayo maajabu mengine mbali na bara
la Antarktika. Ramani ambazo zinapaswa kuwa zimechorwa mwaka 1513 zinayo
taarifa ya kutosha juu ya bara la Amerika ya Kusini, ukiachilia pwani zake za
mashariki, lakini pia milima maarufu ya bara hilo, milima ya Andes iliyopo
upande wa mashariki mwa bara hilo, ambayo katika kipindi cha 1513 haikuwa
inafahamika uwepo wake. Ramani pia zinauonesha mto maarufu duniani, mto wa Amazoni
ukinyanyuka kutoka kwenye milima hiyo na kuelekea upande wa mashariki.
Amerika ya kusini na tabia yake ya nchi ikionekana vyema kwenye rama ya Reis kanakwamba ni ramani iliyotengenezwa kwenye zama zetu. Lakini Ramani hii ni ya karne ya 16 karne nne na nusu baadae ndiyo tulipo weza kutengeneza ramani za namna hii!
Ramani za baharia wetu Piri Reis zimeuonesha mto wa Amazoni mara mbili na
hili likithibitisha uwepo wa vyanzo zaidi ya kimoja vilivyo tumiwa na Reis
kuzichora rama hizi, chanzo kimoja kikiwa ni cha kale zaidi kushinda kingine.
Ikiwa jiografia yako ya Amerika ya Kusini siyo imara sana, basi tazama kulia mwa ramani hiyo, hilo ni bara la Afrika, tizama pwani za Afrika Magharibi zinavyo onekana kwa usahihi wake ikiwemo mito mbalimbali.
Moja inauonesha mto wa Amazoni ukielekea kwenye mdomo wa mto Para, lakini
kisiwa muhimu cha Marajo kikiwa hakionekani hapo. Mtaalam Hapgood aliyezipitia
ramani hizi akasema, ramani ambayo haina kisiwa cha Marajo ni ya kale zaidi ya
miaka 15,000 iliyo pita ambapo kisiwa cha Marajo kikiwa ni sehemu ya bara la
Amerika ya kusini. Ramani nyingine kisiwa cha Marajo kinaonekana tena kwa
taarifa sahihi za kijiografia, lakini cha ajabu ni kuwa kisiwa hichi
kimegunduliwa mwaka 1543 yaani zaidi ya miaka 30 baada ya ramani hizi kuchorwa
na Piri Reis na zaidi ya karne nne baadae ndiyo tulipo anza kuchora ramani na
hatukujua uwepo wa bara la Antarktika. Tunarudi kwenye swali lile lile, ni wapi
baharia huyu alizitoa hizi ramani?
Ramani hiyo ikiwekwa kwenye vipimo vya ramani zetu za sasa, na usahihi wake ukawa kama ramani zinazo chorwa kwenye teknolojia tuliyo nayo sasa.
Visiwa vya Falkland havikuwa vikifahamika mpaka kwenye miaka ya 1592,
lakini visiwa hivi si kwamba tu vinaoneka kwenye ramani za Piri Reis, lakini
pia kwenye usahihi wake wa latitude. Ramani hizi za Piri Reis ni za mwaka 1513
wakati taaluma ya mistari hii ya latitude sisi tumekuja kuifahamu kwenye miaka
ya 1770!
Mistari ya Longitude na latitude nayo ikihakikiwa kwenye ramani hizo na kukurwa kwenye usahihi wake.
Mpaka karne ya 18 ndipo usafiri wa baharini ulipoweza kuchukuliwa upo
salama baada ya ugunduzi wa kifaa ambacho kiliwawezesha wana jiografia kuiweka
mistari ya longitude na latitude mahala pake pa usahihi. Ilihitaji maarifa
makubwa, tafiti na majaribio ya kutosha kuweza kukivumbua kifaa cha namna hiyo.
Isaac Newton alipoulizwa na serikali ya Uingereza kuhusiana na kifaa hicho
mwaka 1714 aliwajibu, “Hath not uet been made ...” (Simon Bethon and Andrew Robinson, The Shape of
the World: The Mapping and
Discovery of the Earth, Guild Publishing, London, 1991, p. 117.)
Zama hizo usafiri wa bahari ulikuwa ni kitu cha bahati nasibu, sababu hapakuwa na ramani za uhakika na mistari ya longitude ambayo ingerahisisha safari hizo hatukuweza kuiweka kutokana na uduni wa teknolojia yetu.
Mpaka mwaka 1720 kipaji cha mtengeneza saa ambaye alikuwa nawania donge
nono la £ 20,000 lililoahidiwa na Bodi ya Longitude ya kipindi hicho, kwa
yeyote atakaye kuja na kifaa ambacho kitawezesha kwa meli kutambulika ipo
sehemu gani kwenye uso wa bahari baada ya wiki sita ya kuanza safari yake.
Jambo hilo lilikuwa ni gumu kiasi ikaonekana kuvumbua kifaa hicho ni sawa na
kusema ‘nguruwe anaweza kupaa’.
Kifaa cha Harrison kilicholeta mapinduzi kwenye safari za baharini.
Iliwachukua miaka 40 ya majaribio na kushindwa
mpaka John Harrison, mtengeneza saa
ambaye alikuja na kifaa ambacho kilikidhi vigezo hivyo. Kwa kutumia kifaa hicho
ndipo safari za baharini zikawa salama, wachora ramani wakaweza kuchora ramani
sahihi za maeneo mbalimbali zikiwa na mistari sahihi ya latitude na longitude.
Mgunduzi wa Kronometa, John Harrison aliyeleta mapinduzi ya bahari kwenye zama zetu.
Ugunduzi huo ukatuambia kuwa ili uweze kutengeneza ramani kwa usahihi
kunahitajika vitu vitatu, kwanza safari ya eneo husika, pili mahesabu ya hali
ya juu na utaalam wa jiografia, na tatu kifaa matata ‘chronometers’ kama alicho
gundua John Harrison. Kitu ambacho hakuna ustaarabu uwe wa watu wa Egypty,
Roma, Fursi, Giriki au Sumeria ambao walikuwa na utaalam huo.
Kiasi alicholipwa Harrison kwa thamani ya pesa ya sasa ni Paundi milioni mbili nukta nane saba, ukizileta hizo kwenye pesa yetu ya Tz, utaona ni kiasi gani dunia ya kipindi hicho ilivyokuwa na uhitajio wa kifaa hicho na ambacho iliwachukua karibu nusu karne kukitengeneza, na Harrison hakupewa fedha hizo mpaka miaka mitatu kabla ya kufa kwake, na ndipo alipo waambia siri ya ubunifu huo na kutoka hapo dunia ya bahari ikawa salama.
Ramani tulizo ziona za mwaka 1513 ambazo moja ya sifa zake bara la Amerika ya
kusini na la Afrika yamechorwa kwenye longitude zake sahihi, kitu ambacho
kilikuwa hakiwezekani kabisa kwenye zama hizo, lakini Piri Reis alikuwa muwazi
zaidi alipo sema ramani zake zinatokana na vyanzo vya kale zaidi, je ni katika
vyanzo hivyo vya kale alikopi pia usahihi wa mistari ya Longitude?
Kwenye ramani ya Oronteus Finaeus pwani za Antarktika zipo kwenye usahihi
wake kulingana na mistari ya Latitude na Longitude, na bara lote likiwa kwenye
vipo vyake sahihi, kitu ambacho kilihitaji taaluma kubwa ambayo haikuwepo zama
hizo mpaka kwenye karne ya ishirini.
Wapi asili ya ramani hizi, katika zama gani zilichorwa, nani mchoraji wake?
Tunabaki na swali lilelile ni nani wachoraji wa ramani hizo katika kipindi
ambacho hapakuwa na ustaarabu wala teknolojia ya kutuwezesha kufanya hivyo, na
hata kutia wasiwasi ikiwa kipindi hicho binadam alishakanyaga uso wa dunia hii.
Historia ya binadam hapa kwa mujibu wa sekula na vitabu vya dini kama tutakavyo
ona kwenye posti zijazo ni kuwa zama hizo binadama alikuwa hajafika hapa
duniani bado.
Kwenye historia tunafundishwa kuwa ustaarabu wa mwanzo ulianza kwenye miaka ya 3000 - 2500 Kabla ya Kristo. Lakini ramani hizi za kale zinaonekana zimechorwa miaka 4000 Kabla ya Kristo na zingine mapema zaidi mpaka mpaka miaka 9000 Kabla ya Kristo. Nani alikuwepo kwenye zama hizo jamani, akazichorwa kwa usahihi kama ambavyo tunafanya katika zama zetu kwa teknolojia ya karne ya 21?
Ikiwa hivyo ndivyo nani mchoraji wa ramani hizo. Nani aliyekuwa na taaluma
ya mistari ya Latitude na Longitude zama hizo. Nani aliishi kipindi ambacho
Antarktika haikuwa na barafu, halafu akaishi maelfu ya miaka baadae barafu
ilipoaanza kujitokeza, alafu maelfu ya miaka tena barafu ilipoanza kulimeza
bara zima na kuacha maeneo ya pwani? Nani huyo.
Hawezi kuwa ni binadam wa Darwin ambaye kipindi hicho bado hata hajawa binadam kamili kulingana na Darwin na wenzake. Lakini kulingana na vitabu vya dini kipindi hicho binadam hajafika bado duniani. Swali linarudi, ni nani alikuwepo na akazichora?
Je tupo wenyewe kweli?
Tutaendelea kutazama kazi zingine za maajabu kwenye uso wa dunia zilizo
achwa na viumbe wasiyo fahamika, katika zama ambazo hazifahamiki, katika kukusanya vithibitisho ikiwa binadam tupo wenyewe au kuna ambaye tupo
naye aliyeishi zama hizo na labda anaishi na sisi mpaka leo.
Till next time tchaooo
yan bro cjawaza kukosa post yako hata moja, nataman ukitupia tu unishtue kwny mkabalaa@gmail.com "thanks be to allah who gave u this exiting abilities"
ReplyDeletekeep coming some day I may put that auto application which will inform you when new post is available. But I cant keep on missing you till I have new post I would like you to show up everyday hah hah lol
Deletesalim msangi wewe ni chuo kikuu kinachotembea
ReplyDeletesalim msangi wewe ni chuo kikuu kinachotembea
ReplyDeleteThanks
DeleteHata mimi naomba uweke App yako ili tuweze kupata kwa urahisi
ReplyDelete