Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Thursday, July 3, 2014

USICHO KIJUA KUHUSU VITA DHIDI YA UGAIDI NA UISLAM Pt 4

THREE ... TWO ... ONE ... ACTION!!! YES CIA WAKIPROJUZI MUVI ZA BIN LADEN.

Hadithi ya Osama ni moja ya hadithi zilizofanywa ni za kusisimua kwelikweli na vyombo vya magharibi, nami kuielezea kwa kina chake itahitaji makala nyingine kama na ninahofia muda haupo upande wangu. Isipokuwa Osama alishakufa tangu 2001, lakini kwa takribani miaka 10, CIA wamekuwa wakirusha kaseti ‘mpya’ za audio na vidio za Osama Bin Laden, na kila CIA ‘walipozindua’ kaseti hizo zilipata mauzo ya kutosha kwenye vyombo vya habari vya magharibi na muuzaji wa ‘jumla’ wa kaseti hizo walikuwa ni Al-jazeera. Tizama posti hii salimmsangi.blogspot.com/2013/07/obama-alazimika-kumfufua-osama-bin-laden.html

Kwa muda wote huo hakuna kiongozi wowote wa Talibani au wa Al-Qaeedah aliyejitokeza hadharani na kusema kaseti hizo ni uzushi na urongo, walikaa kimya kama ambavyo Washington walivyo taka wawe kimya. 


MWAKA 2004 OSAMA ALIKUWA MZEE, NA MWAKA 2007 OSAMA KARUDI KUWA KIJANA ZAIDI, MAAJABU, KADIRI UMRI UNAVYOKWENDA YEYE ANAKUWA NI KIJANA TU.


Obama alipokuja kutangaza kifo cha ‘kutengeneza’ cha Osama bin Laden, na ambacho mpaka sasa kinapigiwa zumari watu wacheze kwa namna mbalimbali, ikiwemo kuandika kitabu cha uzushi kuhusiana na namna Osama alivyo uliwa na kikosi maalum, filamu na taarifa mbalimbali, Al-Qaeedah wakaibuka huko walipotoka na kusema watalipiza kifo hicho cha kiongozi wao?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


NEXT TIME CIA WANIPE MIMI KAZI YA KUCHANGANYA PICHA, HUYU JAMAA ALIYECHANGANYA HIZI AMEKULA PESA YAO BURE, HII HATA MTOTO ANAISHTUKIA KUWA NI FEKI, NADHANI WANAHITAJI MTU MWENYE MASTER YA PHOTOSHOP KUTUDANGANYA VIZURI.

UMEIYONA NA HII, KAMA VILE IMEPIGWA KWENYE MAKAMERA YAO YALE YA KIVITA NA NINI ... KUMBE URONGO MTUPU, TIZAMA PICHA INAYO FUATA.....

PICHA INAYO ONEKANA NI MAITI YA OSAMA HAPO JUU IME-EDITIWA KUTOKA KWENYE PICHA HII HAPA, MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA. TIZAMA PICHA INAYOFUATA ... 
MCHANGANYA PICHA WETU AMETUMIA PICHA HII NA HIYO YA PILI KUTUPATIA 'UTHIBITISHO' WA KIFO CHA OSAMA, LAKINI PICHA HII TUNAIPATA KATIKA MOJA YA MUVI ZA HOLLYWOOD. KAMA KWELI WALIMUUWA KWA 'KIKOSI MAALUM' MBONA PICHA WANAZO TUPATIA NI FEKI?

Inashangaza, mbona mtu huyu alishakufa kifo cha kawaida tangu 2001, ni kifo kipi mnacho kwenda kulipiza? Au kwa vile mnacheza nyimbo za Washington basi mnataka kila mtu acheze? You can fool some people sometimes, but you cant fool all the people all the time.

Al-Qaeedah, makundi ya waasi, Al-shabab, Boko Haram na makundi mengine yanayoitwa ya kigaidi, lao, na Washington, lao na Ulimwengu wa kimataifa wa kimasonia, lao na Illuminanti ni moja! Wewe ndiye adui, wanapigana vita, na ni vita dhidi yako na familia yako, Watch out!!!!!!!!!!!
TUTUMIE AKILI ZETU NA SIYO ZILE ZA KUSHIKIWA NA VYOMBO VYA HABARI NA WANASIASA ...

Mpango wa Brzezinski kupitia kwa Obama ni kutengeneza mitandao ya kisiasa ambayo itaweza kuiporomosha Urusi, utakumbuka mpango wake huu ulianza tangu wakati wa Jimmy Carter ambapo yeye alikuwa ni msimamizi wa siasa za mambo ya nje za Marekani ambapo akapelekea kuundwa kwa Taliban ambao waliifanya kazi hii vizuri sana nyuma ya kile kilichoitwa ‘Holy War’, lakini safari hii mpango huu hautailenga Urusi peke yake bali pia China nayo itaingizwa ndani ya nyumba.

 Brzezinki amekuwa makini akisambaza propaganda zinazo lenga kuchora msitari wa kutokuelewana baina ya Umoja wa Ulaya na Urusi kupitia Kosovo ambayo mustakabali wake wa kisiasa unaonekana kuachwa katika hali ya utata kwa makusudi ili Moscow iweze kunyooshewa vidole kwa aina yoyote ya uwozo unaotokea hapo. Sasa hivi ni Cremea na unaona hali ya mambo inavyo kwenda.

Lakini kwanza Obama anatakiwa kuwatoa wa China nje ya Afrika kwa namna yeyote inayo wezekana. Hata hivyo Brzezinki ana picha kubwa zaidi juu ya hili la kuwafukuza wa China nje ya Afrika. Kupitia kwa Obama, almaaruf, Kennedy Mweusi kama alivyoitwa wakati wa uchaguzi, Brzezinki anao mpango wa kuwapora Wachina kila aina ya rasilimali wanayonunua kutoka Afrika, ikiwemo mafuta, gesi za asili, madini na kila kile ambacho kimebakia kama makombo baada ya vile walivyo pora wakati wa ukoloni, baada ya ukoloni na kwenye ukoloni mambo leo. Tizama posti hii kwa uhondo kamili juu ya vita vya Obama na wachina ndani ya Afrika, http://salimmsangi.blogspot.com/2014/05/boko-haram-mshirika-wa-marekani-nigeria.html

Mpango ulio chaguliwa juu ya hili ni njia ile, ile iliyopendekezwa na mababu wa Freemasons, Priory of Sion kwenye kile walichokiita Protocal of Sion, njia hiyo ni kuzivunja vunja nchi za ki Afrika kupitia vita vya wenyewe kwa wenyewe kitu kitakacho wakimbiza wa China nje ya Afrika. Na hili litasimamiwa vilivyo na kile kinachoitwa Africom ambayo imeundwa na Marekani na mawakala wao wengine.

AFRIKA MOTO


Kupitia mpango wa Brzezinki Afrika itakuwa ni uwanja wa mapambano baina ya Marekani na China, na maanisha mapambano ya kiuchumi na siasa, lakini mapambano ya bunduki itakuwa ni baina ya wa Afrika sisi kwa sisi. Afrika itawaka moto, mauaji ya watu chini ya jangwa la Sahara yatakuwa ya kutisha. CIA wataingilia kati na hata kuingilia siasa za nchi za ndani za Afrika kwa uwazi kabisa nyuma ya kile kitakachoitwa vita vya ugaidi ambavyo wakala wake ni Al-Qaeda ambao kwa sasa kutokana na taarifa za vyombo vya habari za kimagharibi na hata vya hapa Afrka Al-Qaeda tayari wako ndani ya nyumba, wako Afrka, Algeria na Tunisia na kazi zao chafu zimeshaanza kuonekana, kumbuka Algeria ni moja wapo ya nchi zinazo zalisha mafuta kwa wingi Afrika. 

Utakumbuka Al-Qaeda ilikuwa ikidhaminiwa na CIA kupitia hela za dawa za kulevyea wakati Taliban wakidhaminiwa na Brzezinki na mtandao wake wa Trilateral Commission. Hakuna Holy War wala Jihadi kama alivyo Kennedy Mweusi vikundi hivi ni sawa na mwanasesere anayechezeshwa kwa kamba zilizoshikiliwa na bwana wakubwa hawa. Moto umeshawaka Nigeria moja ya wazalishaji wakubwa wa Mafuta Afrika, Boko Haram wananguruma na wanao kufa ni wa Afrika.
 (sehemu hiyo hapo juu niliandika muda kabla moto haujawaka Afrika, lakini yametokea, moto umewaka, serikali zimepinduliwa, Wachina wamekimbia, Illuminati wanabeba chao na Waafrika bado tunapigana risasi kwa faida yao)

Uingereza na Israeli kwa pamoja kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiivunja vunja Sudan, lakini leo picha iliyoko Darfur inatumiwa na Marekani pamoja na Uingereza kama kisingizio cha kuitawalia nchi hiyo mambo yake nyuma ya kile wanacho tuambia  kuwa kuna uvunjaji mkubwa wa haki za binaadam katika eneo hilo.

Kusema Sudan inakiuka haki za binaadam hakuhusiani kabisa na mpango wa kuondoa zahama hilo kama vyombo vya habari vya kimagharibi na mawakala wao wanavyo dai lakini zaidi inahusiana na mpango wa kukata 7% ya mafuta ya China ambayo yanatoka Sudan. Habari zinasambazwa kwa kasi kuwa shughuli za kiuchumi za China nchini Sudan zinazorotesha kwa kiasi kikubwa utaratibu wa kuondoa baa la njaa na tatizo la mafuta duniani. ( Tarpley, Webster Griffin Barack H. Obama: the unauthorized biography / Webster Griffin Tarpley ISBN-13: 978-0-930852-91-7 (Digital), 978-0-930852-81-8 (Offset edition) Uk 376)

 Aina hii ya propaganda muda si mrefu inapokelewa na vikundi vinavyojiita vinasimamia haki za binaadam ambavyo ni vikundi vya watu wale, wale katika sura tofauti lakini nyuma ya ajenda ileile.


Nchi yoyote duniani ambayo kwa namna moja ama nyingine inanufaika kiuchumi na au kiviwanda kutokana na ushirika wake na China na kwa maneno mengine China nayo inajijenga misuli yake ya kiuchumi na viwanda kutokana na miradi yake mbalimbali iliyomo nchini humo, nchi hiyo haiwezi kuepuka mpango huo wa Brzezinki. Mfano ni Burma na Venezuela ambazo historia ya maendeleo yao kiuchumi haijakamilika bila kuitaja China. Shughuli inayo endelea Pakistan ambapo Kennedy mweusi amekiri yuko tayari kuipiga bomu la nyuklia Pakistan endapo itaonekana kushindwa kupambana na Taliban na Al-Qaeda, shughuli hiyo haina lolote kwenye kile kinachosemwa vita dhidi ya ugaidi bali zaidi, ni vita vya kuizorotesha nchi hiyo ambaye muda mrefu imekuwa mshirika wa China, vurugu hizo ni za kuwakimbiza wa China kutoka humo. Tunaona siasa za vuta ni kuvute baina ya Pakistan na Marekani sasa.

China itakapo tengwa na kupokonywa washiriki wake wote wa kiuchumi, na kunyimwa uwezekano wowote wa kupata mafuta na malighafi zozote kutoka nje ya China, hatua itakayo fuata ni kuizorotesha serikali ya China na wakati huo, huo kuipambanisha na Urusi, suala la kuizorotesha serikali hiyo tumeliona linavyoshika kasi kupitia Tibet kwa kiongozi wao wa kiroho Dalai Lama.  Lakini kwa vile Urusi na China zote zinafahamu kuhusu njama hizi za Brzezinki mchezo  unakuwa mgumu ,na hasa pale utakapo jenga mazingira ya kuanganisha mahusiano yenye chuki ya Urusi na China dhidi ya Marekani na washirika wake wapya. Upande mwingine wa shilingi mwanasesere huyu atakuwa na kazi ya kuiunganisha Iran na Syria na kwa pamoja zisimame kuwapinga wa China na wa Rusi. Kinachotakiwa ni Bashir Al Assad atoke pale na paweke kibaraka mwingine, ambaye moja kwa moja atakuwa ni adui wa Urusi na China, kama tunavyo ona, anayempa kiburi Assad ni Mchina na Urusi, sasa hali hiyo inabidi ibadilike, halikadhalika kwa Iran, soon she is next baada ya Syria.


HAIJALISHI NI SHIDA NA MADHARA KIASI GANI YATAPATIKA KWA UMMA, KINACHO JALISHA NI MALENGO YA MILENIA NYINGI KUTIMIA, THE END JUSTFY THE MEANS ... NOTHIN MORE


Mwandishi wa kitabu cha Barack H. Obama: anajaribu kutupa taswira ya mchezo mzima kuhusu Iran na Marekani kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa dhidi ya Urusi na China namna utakavyo kwenda, haya ndiyo maoni yake,

Iran itashawishiwa wawe rafiki na Marekani kwa ahadi ya kupewa nguvu sawa na Marekani ndani ya Mashariki ya kati, si m China wala m Rusi, si m Pakistan wala Egypt atakaye kuwa na sauti ila Iran mshirika wake mpya, Marekani. Rasilimali ngapi za Iran zinazozuiliwa na Marekani kwa muda wote huo sasa zinafikia thamani ya dola bilioni mia na zaidi, vipi unaonaje Iran akipewa na ahadi hii ya kupata rasilimali zake hizo. Unaonaje ahadi ya kutolewa kwenye orodha ya nchi zinazo dhamini ugaidi na vikundi vyake (hatua hii imeshaanza kufanyiwa kazi). Bila kuwasahau washirika wakubwa wa Iran Hezbollah kuwa na wao watapata chochote. Lakini hayo ni mambo madogo tu, unaonaje ishu ya nuklia kama alivyo fanya Bush Baba alimkabidhi Saddam silaha nyuma ya mapazia halafu Bush mwana akaja kuzidai mbele ya hadhara, unaonaje Iran akapewa ruhusa ya kuendeleza mradi wake huo nyuma ya mapazia (Hili nalo limeshapatiwa baraka na Washington). Tunaweza kukupatia teknolojia bora kushinda hii uliyonayo, silaha bora na mabomu ambayo unaweza kuyarusha kokote pale duniani na yakafika Moscow, sema tu kama ndiyo hilo unalo taka, sasa hivi tutakupatia. Ujue tu kwamba adui yako mbaya kuliko wote hajawahi kuwa Marekani bali Urusi. Si unakumbuka namna walivyo kufanya walipo chukua baadhi ya maeneo yako wakati wa WWII, ule ulikuwa ni uharibifu mkubwa. Sisi hatujawahi kufanya kitu kama hicho na wala hututa jaribu kufanya hivyo. Tunachotaka sisi ni kuwa marafiki  na kukusaidia kuwa na nguvu za kutosha kupambana na adui yako wa kweli, Moscow... kama unavyo fahamu mheshimiwa rais wananchi wako wanaichukia Urusi kuliko wanavyoichukia Marekani na Uingereza na wakati wowote utakapo wachukia wa Rusi ujue unawaridhisha watu wako na sisi tutakusaidia... sema tu unataka nini... unaonaje kuhusu manuwari, tukakupatia manuwari inayokwenda mpaka bandari za kusini ya Urusi zikiwa na mizinga ya kinuklia ,hapo utawazuia Urusi wasiendelee kukuibia mafuta yako kutoka kwenye bahari ya Caspian, na kama wakijaribu kujibu mapigo usiwe na hofu tutakuwepo kukupa sapoti. Fikiri mwenyewe kuhusu hili. Halafu kuna hawa wa China, kwa nini unapenda kufanya nao biashara sana, muda si mrefu watakuweka kwenye mfuko wao wa suruali yao kutokana na jinsi unavyo wauzia, halafu tunajua hulipendi hilo... bora ufanye biashara na sisi hata kama ni kwa dola. Tunachotaka ni kuwa ufahamu kwamba sisi ni wa kweli vibaya mno. (Ibid)

UNADHANI NI KWELI OBAMA ALIKUJA KUCHEZA MPIRA NA KIKWETE KWENYE ILE MITAMBO YETU YA UMEME ISIYO ISHIWA NA KASHFA?


Jamaa huyu hayuko mbali sana na ukweli kwa sababu ni mchezo huu, huu aliufanya Brzezinki kwa wa Afghanistan kupitia Mujaheedina ambao ni zao la mpango wake, akawa pambanisha na Urusi na kilichobakia hapo ni historia, alifanya hivyo kupitia kwa Jimmy Carter, leo mchezo uleule wa mtu yule, yule utafanyika kupitia kwa Obama. Halafu wa Syria nao watafuatwa, (tayari Syria kumesha waka moto) watashikwa kama walivyo shikwa kwenye Gulf War ya mwaka 1991. Lengo si kuwapambanisha wa Iran na Syria bali kuwa unganisha dhidi ya China na Urusi. Usisahau Khomeini kufanya mapinduzi yale ulikuwa ni mpango wa Freemasons nyuma ya asasi zake za siri.

Kinacho endelea Afrika na duniani leo ni kazi mahususi ya kuandaa pande za mahasimu kwa ajili ya WWIII, Pakistani tunajua anazo nyuklia, Iran nyuma ya mapazia kama ilivyo kuwa kwa Iraq keshapatiwa ‘green light’ kuendelea na mradi wake, zinazojiita nchi za kiislamu, na zile ambazo tunaona zinapinduliwa na waasi kama Egypti, Libya, Syria, Iraq, Pakistani, Iran na wengine watakao pitiwa na upepo huu, wanaandaliwa kuunda upande mmoja au muungano mmoja dhidi ya maadui wa Uislamu na Waislam. Utasikia vikundi hivi vikija na dai la Khilafa kote duniani, hivyo hawataishia, Syria au Libya au Somalia, hapana wataingia kila pale watakapo ruhusiwa na mabwana zao wakubwa kuingia, kumbuka upande mmoja wa vita unaandaliwa, dhidi ya Ulaya, Marekani, Israeli na washirika wao.


Kipindi hichi siyo Marekani wala Uingereza atakaye anzisha vita hivyo, chokochoko baina ya Israel na Iran ndiyo cheche zitakazo washa moto huo ambapo baadaye kila mmoja ataita washirika wake, Israel washirika wake wapo tayari na tunawafahamu, lakini washirika wa Iran ndiyo kwanza wanaanza kupanga safu, kitakacho fuata ni WWIII.

Malengo ya makuu ya vita hivyo ni kuisimamisha Israel kama ‘New Super Power’, hii ni muhimu kwa vile ni kutokea hapo Jerusalem ndipo Dajjal anatakiwa atawale, na tunajua Illuminanti kwa zaidi ya miaka 2000 wamekuwa wakiandaa zulia ambalo Dajjal atatembea juu yake, na mahala ambapo dola ya Dajjal itakapo anzia ni Israel, na kama yeye atataka kuwa kiongozi wa dunia na hatimaye kujiita mungu, hili haliwezekani kama atasimama nyuma ya dola dhaifu, lazima asimame nyuma ya dola yenye nguvu na iliyoundwa kwa na kuandaliwa kwa muda mrefu kwa ajili hiyo, dola hiyo si nyingine ila ni Israel, na hapo ndipo patakapo kuwa makao makuu ya serikali ya dunia. Hivyo basi Issa (as) atakapo kuja kazi ya kwanza ni kumuondoa Dajjal ndani ya Israel, hichi ndicho kipindi ambacho miji mitakatifu itaachwa na waumini wa kweli kwa ajili ya kwenda kuungana na jeshi la Issa (as) dhidi ya Dajjal. Mpinga Kristo huyu atauwawa sehemu inayo itwa Baablud, leo hii panaitwa Telaviv, na hapo itakuwa ndiyo mwisho wa kitimbi hichi cha Babylon Brotherhood kilichofanyiwa kazi kwa zaidi ya miaka 2000 na vizazi kadha wa kadha vya Illuminanti.  Kazi ambayo imekuwa ndiyo mzizi na chemchem ya kila dhila, mateso, shida, chuki matatizo na kila baya unaloliona leo kwenye uso wa dunia. Kazi hiyo mbaya iliyofanywa kwa milenia nyingi itakwisha pale Baablud. Freemason, Illuminanti, Babilon Brotherhood, asasi zao nyingine nyingi za siri na kazi yao ya milenia nyingi itazikwa hapo.

“Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo.”
“Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyo kuwa wakiyafanya.”
“Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote.”

“Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa. Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?”- Quran 63:1-4

KAA MKAO WA KULA KWA AJILI YA ZILE POSTI NILIZO AHIRISHA ....

2 comments:

  1. naomba niwe napost hizi habari kwa blog yangu kaka yangu! nimezipenda xana na nimekua nikitafuta sehem ya kuzipata.
    www.robhinsontz.blogspot.com
    0756 891212.
    Ur fans from Utegi Rorya Tz.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unakaribishwa mdau na wazo lako ni zuri sana, unaweza kunirushia email kwenye anuani hii, kitabuchetu@yahoo.com, halafu tutajadiliana namna ya kulifanikisha hilo.

      Delete