Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Friday, June 27, 2014

USICHO KIJUA KUHUSU VITA DHIDI YA UGAIDI NA UISLAM Pt 3


AJABU ILIYOJE KWA MAFUNZO HAYA MAPYA NDANI YA UISLAM, NI KINYUME KIASI GANI MAFUNZO HAYO NA DINI WANAYO DAI KUITETEA?

Hii ndiyo iliyo kuwa picha kubwa ambayo CIA na mawakala wengine wa Illuminanti walifahamu. Kupitia sera chafu za kupigania uhuru kwa njia ya silaha, kupitia mafunzo yaliyo potoshwa ya dini ya Uislam waliweza kuwaandaa vijana hawa kutoka sehemu mbalimbali kwenye uso wa dunia na kuwaleta mahala pamoja kama wapigania jihadi. 

Vijana hawa wa Mujaheedina watakapo maliza kazi yao ya kuiangusha USSR kama super power, watapewa kazi nyingine na wajiri wao, kazi ambayo katika zama zetu tunaifahamu vyema kama Ugaidi. Kazi hii mwongozo wake pamoja na maudhui yake havitoki kwenye mafunzo ya dini ya Uislamu bali kwenye mahekalu ya kimasoni na mawakala wa Illuminanti.


Mwanastratejia wa Illuminanti bwana Brzezinski ambaye kwa sasa anashikilia wadhifa muhimu kwenye serikali ya kibaraka mwingine wa Illuminanti na Freemason wa daraja la 32 bwana Barak Obama, alipokuwa akihojiwa mwaka 1998 kwenye mazungumzo aliyo yafanya na Le Nouvel Observateur alikiri kuwa CIA iliwasaidia mujaheedina kwenye mapambano dhidi ya USSR. Alisema kuwa July 3, 1979 aliyekuwa rais wa Marekani kipindi hicho Jimmy Carter alisaini na kupitisha mwongozo wa kwanza wa kuwasaidia Mujaheedina kwa siri.( “Interview With Zbigniew Brzezinski”, Le Nouvel Observateur.<http://members.aol.com/bblum6/brz.htm>)

Ni katika kipindi hichi mwanastratejia huyu alianza kuziita nchi za Iran, India na Afighanistani kuwa ni muhimili wa maovu duniani, sera ambazo zimeendelea kutumia hata na rais Bush na sasa zinatumiwa na Obama pia. Kuzipachika nchi hizo jina hilo sababu yake ni kutengeneza na kuwapa nafasi ya kutanuka kwa vikundi vinavyo julikana kama ‘Waislam wenye siasa kali’, hivyo nchi hizi zilijukana na bado zinafahamika kwa mujibu wa sera za Marekani kuwa ni nchi zenye kusaidia ugaidi duniani.

Lakini hayo hayakumzua Carter kusaini mwongozo wa kuvisaidia vikundi hivyo ambapo kitendo hicho ni kinyume na katiba ya Marekani na ni kinyume na mwongozo wa UN. Kwa nini basi Carter aliwasaidia, Carter aliwasaidia kwa vile vikundi hivi ni wao ndiyo wamevianzisha kupitia mtandao mpana unao zahusisha nchi kadhaa za bara la Ulaya na mashirika yao ya kijasusi na pia zikiwemo nchi za Kiarabu na malengo ya vikundi hivi si kuusaidia Uislamu kwa kupambana na nchi za Ulaya na washirika kama watu walivyo fanywa waamini, bali kuubomolea mbali Uislamu na wakati huohuo vikitekeleza matakwa mengine ya Illuminanti kama lile la kuiangusha USSR ili Marekani inyanyuke kama super power, na kwa sasa vikundi hivi kama tunavyo ona vinashirikishwa vilivyo kuhakikisha vinaukokota uma wa Kiislamu kwenye uwanja wa WWIII.

HII NDIYO PICHA AMBAYO WATU WANAPASWA KUWA NAYO, KILA JINA 'UISLAM na MUISLAM' LINAPOTAJWA. JUHUDI KUBWA IMEFANYIKA HATA SASA NI VIGUMU KUONA AU KUSEMA TOFAUTI NA PICHA HIYO.

Mpango huu wa CIA kuwasaidia Mujaheedina Afighanistan ulikuja kufahamika kama Iran-Contra-Affair ambapo mbali na mambo mengine Marekani walihusika na kuwauzia Iran silaha kwa ajili ya kupambana na Iraq na pia ikawauzia Iraq nao silaha katika mpango ulio itwa Iraq-Gate, huu ni mchezo wa kawaida kwa Marekani na Illuminanti kufadhili pande mbili za vita kwa wakati mmoja, kwani mwisho wa siku ni wao wanao faidika na vita hivyo. Hapa utaona Marekani inaziuzia silaha nchi ambazo yenyewe inazitambua kuwa ni nchi za kigaidi duniani.
NI WAPI WANATOLEA SILAHA HIZI?

Mkutano wa asasi ya siri ya Bildeberg uliofanyika mwaka 1973 ambapo kwenye mkutano huo walijadili kuhusu kupandishwa kwa bei ya mafuta duniani na baadaye mwaka 1974 bei hiyo ikapanda kwa kasi sana, faida kubwa iliyopatikana katika ongezeko hilo la bei ya mafuta ilitumika kati ya mengi ni ufadhili shughuli ya Iran-Contra-Affair, na mipango mingine michafu ya kuunda vikundi vya kigaidi sehemu mbalimbali duniani. Wakati haya yote yanafanyika mshirika mkubwa wa Marekani kwenye hili alikuwa na bado anaendelea kuwa ni Saudi Arabia chini ya uongozi wa Wahhabisim.

Kwenye utawala wa Saud Arabia alikuwepo mtu aliyeitwa Prince Bandar aliyetumiwa na CIA kwa niaba ya utawala wa Saud kuufadhili mpango mzima wa Contra, Prince Bandar bin Sultan ambaye alikuwa ni mjukuu wa Ibn Saud na Hassa bint Ahmed al-Sudairi, mmoja wa wanawake wenye kuheshimika sana ndani ya Saud Arabia. Prince Bandar aliteuliwa kuwa balozi wa Saudia ndani ya Marekani mwaka 1983 na alishikilia wadhifa huo kwa miaka 20. Alikuwa ni rafiki wa karibu na familia ya Bush. Bandar alitumiwa kama kiunganisha baina ya serikali ya  Marekani na Saddam, pale uongozi wa Saddam alipoonesha nia ya kupokea msaada kutoka kwa Marekani. Kwa siri utawala wa Regan uliziruhusu nchi za Saud Arabia, Egypt na Kuwait kusafirisha silaha zilizo tolewa na Marekani kwenda kwa Saddam, silaha zingine zikauzwa kwa Iran ambazo ziliwafikia Mujaheedina wa Afighanistan. Saud Arabia ilichangia kiasi cha dola za kimarekani milioni thelathini na mbili kwenye Contra. (U.S. News & World Report, 15 December 1986)
WAKATI WOTE WAMEVAA MAVAZI YA KIISLAM, LAKINI KAZI YAO NI KUUBOMOA HUO UISLAM WANAO DAI KUUTETEA.

Contra haikuishia kwenye fedha za mafuta peke yake, fedha za dawa za kulevyea ambazo ziliuzwa kwenye mtandao mpana kwenye majiji na mitaa mbalimbali duniani nazo ziliingizwa kudhamini Contra, Mujaheedina walio kuwa wanadai wanapigana Holy War walikidhi mahitaji yao na kuendeleza mapambano kwa muda mrefu kwa kutumia fedha za dawa za kulevyea zilizo wafikia kupitia kwa CIA, kupitia kwa shirika la kijasusi la Pakistan, na kupitia kwa mawakala na vibaraka wengine wa Illuminanti. Ni vipi unapigana Holy War kwa kutumia pesa za dawa za kulevyea?

Wakati wa vita ya Vietnam, CIA wakishirikiana na makabila ya Vietnam walishiriki kwa kiasi kikubwa kusafirisha dawa za kulevyea kutoka kwenye eneo lilioitwa Triangle Kusini mwa Asia. Kabla ya hapo ni Ufaransa ndiyo waliokuwa wakiishikilia biashara hiyo katika eneo hilo. Hata baada ya vita na Vietnam kumalizika Marekani bado waliendelea kuishikilia biashara ya mihadarati eneo hilo.
YES, THIS IS CIA ... OR WAS IT CONFISCATED EVIDENCE ...? I DON'T KNOW, BUT IT WAS ON THEIR PLANE!!! 

Tangu mwanzo wa vita baina ya USSR na Mujaheedina, CIA walikuwa wamesha tengeneza mahusiano mazuri na Pakistani kupitia shirika la kijasusi la Pakistan la ISI. Benki iliyotumiwa kuwafikishia Mujaheedina fedha za dawa za kulevyea na fedha ambazo zililengwa kwa ajili ya misaada sehemu mbalimbali duniani ni Bank of Credi and Commerce International, BCCI. Benki hii ilianzishwa mwaka 1972 na Agha Hasan Abedi kutoka Pakistan akiwa amepokea fungu kutoka kwa Sheik Zayed wa Abu Dhabi ambaye alitegemea kuitumia benki hiyo vilivyo kutokana na fedha za ziada zitakazo zalishwa kwenye mfumuko wa bei ya mafuta kwenye miaka ya 70. (The Outlaw Bank, uk. 109.)

MWANZILISHI WA BENKI YA BCCI

Utakumbuka mfumuko huo wa bei ulipangwa kwenye mkutano wa asasi ya siri wa Bilderberg, na mwaka ulio fuata mfumuko wa bei ukatokea na mabilioni ya dola ya ziada yaliyo zalisha hapa yalikwenda kuwafadhili mujaheedina kupitia BCCI na nyingine ziligawiwa kama mikopo kwa nchi zinazoendelea kupitia WB na IMF, deni ambalo mpaka sasa ni jinamizi lililozimeza nchi zetu.

Unapo zungumzia mchezo mchafu wa kusafisha pesa za dawa za kulevyea na kutumia pesa za misaada na pesa za mafuta kwa ajili ya kuwadhamini watu walio itwa mujaheedina basi huwezi kuwacha kuzungumzia kuhusu BCCI. Benki hii ilikuwa ni benki ya kwanza yenye nguvu kuliko benki zote katika nchi zinazoendelea kutokana na utajiri mkubwa uliomiminika kutokea Mashariki ya Kati kutokana na ongezeko la bei ya mafuta kwenye miaka ya 70. Pesa chafu za CIA kwa ajili ya kudhamini magaidi ambao waliitwa mujaheedina au wapigania uhuru zilipata njia nzuri kwenye benki ya BCCI. Wauza silaha za magendo, wauza dawa za kulevyea kutokea Asia mpaka Amerika ya Kusini, makundi ya wahalifu na mashirika ya kijasusi kama vile ISL, Mossad, M16 na CIA yote yalipata kimbilio kwenye benki ya BCCI. (Richard H. Curtiss, “What You Won’t Read About Michael Harari, Noriega Is Israeli Adviser Who Got Away”. Washington Report. February 1990)

BCCI ilikuwa na tawi Panama, ambapo kibaraka wa serikali ya Marekani na nyenzo muhimu kwa CIA, Manuel Noriega ambaye pia alikuwa ni kiungo muhimu kwa biashara za dawa ya kulevyia baina ya CIA na wadau wengine eneo hilo, alitumia tawi hilo la Panama kupitisha fedha hizo kutoka nchini humo. Alikuwepo mtu aliyeitwa Michael Harari, jasusi wa Mossad ambaye baada ya kumaliza kazi yake ndani ya Palestina alipelekwa Amerika ya Kati na Kusini ambapo aliunda mtandao uliofanya kazi ya kusafirisha bunduki na dawa za kulevyea baina ya wateja mbalimbali walio hitaji bidhaa hizo na kutengeneza faida kubwa ambayo ilifuata njia ya moja kwa moja mpaka kwenye mifuko ya kanzu za wa Taliban. Kipindi hichi Marekani na CIA waliacha kununua dawa za kulevyea kutoka kwa watu mmojammoja bali waliwashauri vinara hawa kuungana na kuwauzia bidhaa hizo kama kikundi au kampuni badala ya mtu mmoja mmoja. (Uri Dowbenko, “Book Review”, Conspiracy Digest.http://www.conspiracydigest.com/bookdefrauding.html)

Harari alipokuwa anazungumzia biashara hii alisema hivi,
 “Tunachokifanya hakihusiani chochote na kulinda maslahi ya nchi, hii ni biashara tu na nchi za dunia ya tatu ...Tunawapatia mafunzo ya kijeshi na kuwapatia silaha na wao kama njia ya biashara wanatupatia bidhaa yenye thamani kubwa zaidi kushinda silaha na fedha. Tizama thamani ya bunduki moja na risasi zake ni dola 1200. Kilo moja ya Cocain ni kama dola 1000. ... Kwa upande wetu tunatumia dola 1200 kwa kila kilo moja ya Cocain na tunakuja kuuza hiyo kilo moja kwa dola 12,000 mpaka 15,000. Hichi ni kituo cha kutengeneza faida na soko la cocain ni kubwa kushinda soko la silaha. Kwa hiyo hii ni biashara tu. Umeelewa?” (Ibid)

Alichokisema Hariri si kigeni katika nchi zetu za duniani ya tatu, bado kinaendelea kufanyika na bado kitaendelea sana tu kufanyika, daima vikundi vyote vya waasi katika nchi za dunia ya tatu vimekuwa vikifanya biashara ya namna hii na Marekani pamoja na washirika wake wakishirikiana na mashirika yao ya kijasusi. Eidha ni silaha na mafunzo kwa dawa za kulevyea, au silaha na mafunzo kwa rasilimali zingine za nchi kama madini, mafuta, aridhi na vinginevyo. Daima utajiuliza swali moja, watizame waasi wa Kongo, watizame waasi wa Somali, waliokuwa waasi wa Ivory Cost, watizame waasi wa Sudan na kwengineko duniani, utawaona wamevaa nguo safi nadhifu, wamebeba silaha nzitonzito, lakini nchi nzima imemezwa na umasikini, imefunikwa na kiza cha shida, ukosefu wa huduma za kijamii, miundo mbinu mibovu, njaa na umasikini wa kutisha, lakini waasi na washirika wao utadhani hawaishi hapo wako safi kisilaha na kimavazi ya kivita, kwa nini? Kwa vile watu walewale wanao dai kuwakalisha kwenye  meza kwa ajili ya mazungumzo ya amani ndiyo watu haohao kupitia mawakala wao wanawapatia waasi na washirika na hata serikali zao silaha na mafunzo kwa ajili ya kurefusha mapambano, kwani kama walivyo sema wahenga, vita vya Panzi .... Naam kama alivyo sema Hariri, it is just a business.
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA

Kuzaliwa kwa BCCI na kukuwa kwake kuna mahusiano makubwa na vita baina ya USSR na Mujaheedina. Bhuto wa Pakistan alikuwa ni kila kitu Bigbrother wasichokihitaji na hivyo aliondolewa na nafasi yake ikachukuliwa na Zia ambaye alimuweka mtu aliyeitwa Fazle Haq kuwa msimamizi kwenye jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Pakistan mwaka 1978. Eneo hili linapakana na Afighanistan na ndilo liliokuwa uchochoro wa kupitisha tani na tani za dawa za kulevyea na silaha. Fazle Haq pia anatajwa kwamba alikuwa ni rafiki mkubwa wa mwanzilishi wa BCCI bwana Hasan Abedi. Pesa za dawa za kulevyea kwa ajili ya watu walio itwa mujaheedina zilipitishwa na kusafishwa na BCCI.( Time magazine, “The Dirtiest Bank of All”, 7.29.91)

October 13, 1996 jarida la Executive Intelligence Review liliandika habari yenye kichwa cha habari, “Anglo-Amerika imekuwa ni kifaa cha kuwasaidia Mujaheedina wa Afighanistan” Ni katika kipindi hichi kulianzishwa redio iliyoitwa “Radio Free Kabul” ambayo ilitumika kama sauti kwa mujaheedina, mwanzilishi wa redio hiyo hakuwa mwingine bali ni jasusi wa Uingereza bwana Lord Nicholas Bethell. Hapa unaona Mujaheedina wanapigana holy war na USSR, lakini unakuta wahusika wakubwa kuanzia kwenye udhamini wa vifaa vya kivita, gharama za kuendeshea hivyo vita, na mpaka wapiganaji wenyewe wanatolewa na nchi za Ulaya, Marekani na washirika wao, na unakuta nchi hizo zinafanya mengi makubwa, zinakiuka katiba zao, na katiba za kimataifa kama za UN ambazo ni wao wameziweka ili kuwasaidia hao wanao itwa ni mujaheedina ambao kwenye katiba zao wanatajwa wazi kuwa ni magaidi, hapa utajiuliza swali moja la msingi ‘Je hivi ni vita vitakatifu au kuna mazingaubwe ambayo jicho la kawaida haliyaoni?”

Ndani ya miaka miwili tu ya CIA kufanya kazi kwenye mpaka baina ya Afighanstan na Pakistan hatimaye Pakistan wakaibuka wazalishaji namba moja wa dawa za kulevyea kwa ajili ya soko la Marekani ambapo Pakistani alizalisha kadiri ya asilimia 60 ya soko zima. Wahanga wa dawa za kulevyea ndani Pakistan peke yake iliongezeka kutoka idadi inayo karibiana na sifuri mwaka 1979 mpaka milioni 1.2 mwaka 1985. (Alfred McCoy, Drug fallout: the CIA’s Forty Year Complicity in the Narcotics Trade. The Progressive; 1 August 1997.)
Hivyo unapotizama vikundi mbalimbali vya kigaidi kote duniani utakuta si kwamba tu havifanyi kazi vyenyewe lakini pia mitandao ya vikundi hivyo imepenya kwenye nafasi za juu za serikali za nchi kubwa za kimagharibi ambazo ndizo zilizopo mstari wa mbele kupambana na ugaidi.
Watu wa kawaida kwenye vikundi hivyo wanaonekana ni waumini wazuri wa dini ya Kiislam, lakini kama ulivyo utaratibu wa vikundi hivyo, wafuasi wa kawaida haambiwi yote kuhusiana na kikundi chake na hii ni asili ya vikundi vyote vilivyo jengwa kwenye nadharia ya kimasoni. Lakini wale viongozi wakubwa wa vikundi hivyo ambao hutawaona kwenye maandamano wala kwenye uwanja wa vita, ni watu wenye suti zao nadhifu, leo wako New York kesho wako London, keshokutwa wako Abu Dhabi mwezi ujao wanayo mkutano Durban, wanafanya business za mabilioni na wanachama wengine wa Illuminanati. Wanamiliki mabenki, wanamiliki mali za mabilioni kutoka kwenye biashara za mafuta mpaka kwenye uuzaji haram wa silaha, dhahabu na dawa za kulevyea. Wako juu, wanapokea mipango kamambe ya namna gani vikundi vyao vya kigaidi vitafanya kazi kutoka kwenye mahekalu ya kimasoni, na wao wana wadondoshea wanachama wao wa kawaida vijisenti ili waendeleze miradi ya kibinadamu na kijamii kwa jina la vikundi hivyo. Kile ambacho jicho la kawaida halioni ni nguvu kubwa ya vikundi hivyo kupitia serikali mbalimbali za kimasoni duniani. Kile ambacho jicho la kawaida halioni ni kuwa wale wanajulikana kama magaidi na wale ambao wanaupinga ugaidi na magaidi wote ajenda yao ni moja.

Wakati Marekani na washirika wake walipo taka kuing’oa USSR kupitia kwa Mujaheedina ili wabidi CIA kushughulika vilivyo katika kuwaandaa, kuwapa mafunzo, kuwalipa na hatimaye kuwasafirisha watu ambao waliitwa wapigania uhuru, au ukipenda mujaheedina na au kwa uwazi zaidi magaidi kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja Afighanstan kuuangusha utawala wa USSR. Mpango Huu ulifanyika ukiwashirikisha Muslim Brotherhood. Watu walitolewa kutoka Ulaya, Afrika ya kaskazini, Afrika Mashariki, Mashariki ya Kati, Asia na ndani ya Marekani kwenyewe. Mpango huu ulilenga kuwaandaa watu watakao tumika kama mawakala wa ugaidi kote duniani pale vitakapo malizika vita baina ya wapigania uhuru na USSR kupinduliwa.
TUMIA AKILI YAKO HURU KUNG'AMUA KAMA KUNA TOFAUTI YEYOTE NA SIYO AKILI YA CNN, AU ALJAZEER AU FOX NEWS

Hivyo vijana hawa waliojitolea kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa nia safi kabisa ya kupigana holy war kwa kipindi hicho walifahamika kama wapigania uhuru, lakini baadaye watatumika kutengeneza mtandao utakao fahamika kuwa ni wa kigaidi dhidi ya Marekani na marafiki zake, na hiyo ndiyo picha kubwa ambayo wengi hatukuiona kipindi hicho.

Msingi waliopatiwa vijana hawa kutoka sehemu mbalimbali duniani ulilingana na mafunzo ya karne ya kumi na nane yaliyotolewa na wakala wa Uingereza bwana Mohamed Abdul Wahhab. Uongozi wa Saudi Arabia nao haukuwa nyuma kwenye hili King Fahd naye akazimwaga dola kupitia kwenye benki ya BCCI kuwasaidia Mujaheedina. Haikuishia hapo, shirika la kijasusi la Pakistan lilihitaji mwana wa mfalme wa Saud Arabia kuviongoza vita hivyo vya jihad dhidi ya USSR. Hata hivyo hakuna aliyejitolea kutoka kwenye familia hiyo hivyo viongozi wa Saud wakampendekeza kijana kutoka kwenye familia tajiri na ambayo ipo karibu na familia ya kitawala ya Saud, naye hakuwa mwingine bali ni Osama Bin Laden.


KAA TAYARI KWA SEHEMU YA MWISHO YA POST HII ... INSHAALLAH....

4 comments:

  1. sasa hii dhulma itaondoshwaje katka dunia mpaka lini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dhulma hii inaweza kuondosha na mimi na wewe. Cha kwanza kabisa binadamu lazima tuamke kwenye usingizi tulio lala, cha pili lazima tujifunze elimu sahihi, maarifa sahihi yanayo husu kwanini tuko hapa duniani na wapi tunakwenda na tatu lazima tuchukue uwajibikaji kwa kila kile tunacho paswa kufanya, muda wa kumlaumu huyu na yule haupo, lazima tuwajibike wenyewe kubadilisha hali hii na ndipo NUSRA YA MUUMBA ITAKAPO KUJA.

      Delete
  2. Vp kuhusu shehe dkt Abdullah Aazam ambae alifariki kwa kupigwa na bomu na kuchanguka vpande huko afghanistani nayeye alikua akitumiwa?

    Lakin je? Unaweza kunithibitishia kuwa osama na marekani lao lilikua ni moja?

    Mwisho naomba unitumie makala kadhaa zenye kuonyesha kuwa hv vikundi vya mujahidiina vinavyooendelea dunia vmeundwa kwa manufaa yya nchi za magharib?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swali lako limejibiwa na baadhi ya Post kwenye blogi hii kama itazipitia moja moja utaona, lakini pia kuna post ya Ossama itakayo kuja baadae nayo italijibu tena swali lako kwa upana, stay Tune here here.

      Delete