Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Sunday, June 22, 2014

USICHO KIJUA KUHUSU VITA DHIDI YA UGAIDI NA UISLAM Pt 2


Wafuasi wa wahhabi wanaweza kukataa kuwa hayo si kweli, na wamesha andika vitabu kadhaa wakimsafisha Abdul Wahhab na hayo niliyo yaeleza, lakini nukta moja ya msingi ambayo wote tunaweza kuitizama kwa jicho moja ni kuwa, Mashariki ya kati haikuingia kwenye mikono ya Illuminanti mpaka pale dola ya Kiislam ya Ottoman ilipoangushwa. Pia hakuna shaka kuwa mataifa ya kigeni peke yao hayakuweza kuiangusha dola hii ila kwa kutumia sera yao ya ‘divide and rule ambapo baadhi ya wananchi waligeuzwa na kuwapiga wenzao na moja kwa moja kumsaidia mgeni kuwatawala. 
BUSINESS KAMA KAWA


Mfalme Saud ambaye aliahidiwa madaraka na kuhakikishiwa ufalme wake endapo atasaidia kuidhoofisha na hatimaye kumuangusha ndugu yake wa Kiislam anaye tawala kupitia dola ya Ottoman. Alilifanya hili kwa uzuri akishirikiana na Abdul Wahhab ambaye yeye aliweza kutoa tafsiri mpya ya mafunzo ya Kiislam iliyo ruhusu muislamu mmoja kumuua muislamu mwenzake. Tafsiri hii inatumiwa mpaka leo na vikundi mbalimbali vinavyo endesha matukio ya ugaidi duniani, ambapo wao kumuwa muislamu mwenzao kwa tuhuma zisizo na mashiko au bila hata tuhuma ni jambo la kawaida. 

Ibn Saud alipewa ujira wake kwa kupewa nchi iliyoitwa jina lake, yaani Saud Arabia, naye alilipa fadhila hii kwa kuwaruhusu Illuminanti kushikilia hazina yote ya mafuta ambayo sasa inatumiwa kwa faida ya New World Order.


Kwa hiyo kazi ya Wahhabi nyuma ya familia ya Saud ilikuwa ni kuwasaidia Freemason wa Uingereza kuikamata dola ya Ottoman baada ya WWI. Kwa kiasi kikubwa lengo hilo lilifanikiwa, kwani sehemu kubwa ya Mashariki ya kati ikawa ni makoloni ya Ungereza, na hivyo Freemason wa Ulaya wakakipata kile walicho kuwa wakikisaka kwa muda mrefu, moja ya nishati muhimu katika uchumi wa dunia hii, nishati ya mafuta.

ONE FAMILY

 Familia ya Illuminati ya kishetani ya Rockefeller ndiyo iliyo patiwa funguo za hazina hiyo. Kupitia ushirika huu, familia ya Saud itapata nafasi ya pekee kwenye muungano huu wa kishetani na kwenye mpango mkubwa wa New World Order, ambapo familia hii itapewa nguvu juu ya nishati hiyo, na miaka itakayo fuata faida kubwa itakayo patikana kwenye mafuta, kati ya mengi itakayo tumiwa kufanya ni kufadhili kazi na tafsiri potofu za mafunzo ya Uislamu zenye falsafa na mtiririko wa maono ya Khawarij, Wahhabisim na Assassins kwenye ulimwengu wa Uislamu na ulimwengu kwa ujumla, na mafundisho hayo yatatoa ruhusa ya kufanyika mauaji yatakayo itwa UGAIDI kama yalivyo fanyika katika zama za wahhabism, mauaji haya kupitia mafundisho ya Wahhabisim kwenye kanzu ya Uislamu ni muhimu mno kwa ajili ya ajenda ya New World Order.

Mipango hii kamambe haitoki kwenye vinara wa Wahhabi na familia ya Saud ambao wao si chochote si lolote katika mchezo huu mzima, bali ni wanasesere walio fungwa kamba na mabwana wakubwa ambao huvichezesha viungo vyao namna kulingana na matakwa ya ajenda.

Mabwana hawa wakubwa utawakuta katika jiji la London, ambalo linaendeshwa na Bank of England ambavyo kama ilivyo Federal Reserve ya Marekani nayo hii inamilikiwa na watu binafsi. Jiji hili la London nalo kama lilivyo jimbo la Washington Marekani na jiji la Vatican Rome ni miji inayojitegemea kwa kila kitu na iko juu ya sheria kuu za nchi hizo. Miji hii inazo sheria zake yenyewe. Jiji kama la London liko chini ya meya ambaye ni lazima awe Freemason wa daraja la 33 na hata Malkia na nguvu aliyopewa na Illuminanti hawezi kuingia ndani ya London bila idhini ya meya huyu. Hivyo ndivyo ilivyo kwa miji mingine miwili ya Vatican na Washington zote ni dola zinazo jitegemea kwa kila kitu.

Ni kichekesho kuwa rais Obama ni rais wa USA na kapata kura kutoka Washington DC, na makao makuu ya serikali yake yapo hapo lakini hana nguvu yoyote juu ya Washington D.C, na anapo chungulia kwenye moja ya madirisha ya White House anauona mnara mkubwa mrefu na mweupe wa kimasoni kutoka Egypti ukimuambia ni nani anaye iendesha Washington.
RAMANI YA MAJENGO MUHIMU YA SERIKALI NDANI AY WASHINGTON YANAPOUNGANISHWA HUTENGENEZA NEMBO YA KISHETANI, HILI SI KWA BAHATI MBAYA!

Kama Freemason walivyoweza kujipenyeza ndani ya ulimwengu wa Kikristo na kuikamata dini hiyo vilivyo kupitia Kanisa Katoliki na kupitia viongozi wa madhehebu mengine; kwa njia hiyohiyo wameitumia na kujipenyeza kwenye dini ya Uislamu na kuweka vibaraka wao katika kila sehemu muhimu na ya kimaamuzi kupitia kwenye asasi, taasisi, vyuo, nchi na hata dola zinazo dai ziko chini ya dini hii.

Mpango huu kwa upande wa kuivuruga dini ya Kiislamu, hasa kupitia mafunzo yake ya msingi, Quran na Sunnah kwa ajili ya mpango kamambe, ambao kwa sasa picha yake inaanza kuonekana, mpango huu ulifahamika kama Oxford Movement, kitovu cha shughuli ilikuwa ni Egypti. Lengo lilikuwa kuisambaza Scotish Freemason ndani ya Mashariki ya Kati kwa ajili ya kuandaa vijana watakao kuja na tafsiri tofauti ya usilaumu. Kupitia Grand Lodge la Egypti chini utawala wa Ismailia, Freemason ya Egypti iliweza kuvuka bahari na kufika Ulaya ambako ilipelekea kuzaliwa kwa Scottish Freemason ambayo sasa kupitia Oxford Movement ni kama inarudi nyumbani kwa wazee wake.

Vinara nyuma ya Oxford Movement alikuwepo mwanachama wa Palladian Rite Freemason Albert Pike, alikuwepo Lord Palmerston na alikuwepo aliyekuwa waziri mkuu wa England na Freemason wa daraja la juu Benjamin Disraeli na Edward Bullwer-Lytton aliyekuwa mwanachama wa asasi ya siri iliyofahamika kama Rosicrucianism. Mpango huu ulikuja kupewa nguvu na asasi nyingine ya siri inayo fahamika kama Jesuits.( Dreyfuss, Hostage to Khomeini)

Oxford Movement ilishughulika na kuingiza mafunzo mapya kwenye Uislamu ambaye baadaye yalikuja kujulikana kama Salafi (Salafi hii tunayoiona leo au New Salafisim). Mafunzo na tafsiri hizi mpya kutoka kwenye mahekalu ya kimasoni yalikuweka msingi wa mbinu mbaya ya illuminanti itakayo kuja kufahamika kama  ugaidi.

 Muanzilishi wa Salafi hii mpya anajulikana kama Jamal ud Din al Afighani, jamaa huyu alikuwa ni jasusi wa Uingereza. Baada ya Egypti kuingia kwenye mkataba wa kusaidia kuipanua Seuz Canal na baadaye ikashindwa kulilipa deni hilo iliweka chini ya uangalizi wa Ufaransa na Uingereza bila nguvu zozote za kiserikali. Chini ya kiongozi aliyefahamika kama  Ahmed Urabi wazalendo wa Egypti wakajiunga kuyapinga maamuzi hayo na hivyo kuipatia fursa Uingereza kwa kisingizio cha kulinda maslahi yake ya Suez Canal kuifanya Egypt kuwa ni koloni lake.

Kijana aliyetumiwa kuchochea vurugu na harakati hizo za wazalendo wa Egypti na hatimaye Uingereza kufanikisha mpango wake hakuwa mwingine bali ni Jaml ud Din al Afghani (Ibid)

Baadaye Salafi wakajiunga na Wahhabi wa Saudi Arabia. Wakati Salafi itakuwa ni chombo muhimu cha kutengeneza tafsiri kutoka kwenye aya za Quran na mafunzo ya mtume zitakazo ruhusu kile tutakachoiita ugaidi, Wahhabi wa Saud chini ya utawala wa familia ya Saud wao ndiyo watakao kuwa wadhamini wakubwa wa mpango huu kupitia faida wanayo kusanya kwenye biashara ya mafuta ambayo nayo haiko tena kwenye mikono na uma wa Kiislam bali kwenye familia ya kishetani na illuminati ya Rockefeller. Familia hii ya Saud imepewa nafasi muhimu kwenye picha kubwa ya New World Order kwani ulimwengu mzima umefanywa utegemee nishati hiyo ya mafuta peke yake na hivyo kutengeneza faida maradufu na wakati huohuo kuamua hatma ya uchumi wa dunia kupitia mafuta.
BUSINESS AS USUAL

Mashariki ya kati bado kuliendelea kuchafuliwa. Mwaka 1891 baba yake na Ibn Saud alilazimika kuikimbilia Kuwait akiiwacha Riyadh imekaliwa na Ottoman. Baadaye tena Ibn Saud akaanzisha mapambano ya kuikamata Riyaadh akisaidiwa na Uingereza. Baadaye Uingereza wakaongeza msaada wao kwa Ibn Saud ili komuongezea nguvu zaidi kisilaha na kifedha dhidi ya dola ya Ottoman.

Mustafa Kemal Ataturk


Hata hivyo ni mpaka mwaka 1918 chini ya mtu aliyeitwa Faisal dola ya Ottoman ndani ya Mashariki ya Kati ilipinduliwa. Eneo hilo likagaiwa baina ya mataifa makubwa yaliyo kuwa yakilitolea macho eneo hilo. Mtu aliyeitwa Mustafa Kemal Ataturk kutoka Uturuki hakukubaliana na mgawanyo huo mpya wa Mashariki ya Kati. Aliunda jeshi ambalo liliwatimua wa Giriki na wa Italia nje ya Anatolia. 
Uingereza na Ufaransa hawakuingilia mpambano huo. Inasemekana Ataturk hakuwa mfuasi wa Uislamu bali Myahudi. Mwaka 1923 wakati Jamhuri ya Uturuki inaundwa Ataturk ndiye aliyechaguliwa kuwa rais wa kwanza wa taifa hilo na mwaka 1924 alitumika vizuri kukimaliza kile kilicho fahamika kama Khilafa au Ukhalifa wa dola ya Kiislam ulio dumu kwa miaka elfu moja na mia tatu.

Wakati WWI inaelekea ukingoni Faisal aliendelea kulikamata eneo kubwa la Arabia ikiwemo Jordan na sehemu za Syria. Hata hivyo wakati Faisal anaendelea kujipanua kimipaka Uingereza nao walikuwa na ajenda yao ya siri ya kuigawanya Mashariki ya Kati kutokana na maono yao. Mwisho wa siku Faisal alikuwa amesalitiwa na mgawanyo huo mpya ambapo yeye alipewa eneo la Iraq tu. Ili kuhakikisha Faisal hawi kitisho siku za usoni, Uingereza ikawatumia marafiki zake wa muda mrefu, Wahhabi wa Saud chini ya Ibn Saud kuyakamata maeneo ya Penisula yaliyokuwa chini ya Faisal.
Faisal alishindwa na Wahhabi wakaikamata penisula ya Arabia. Ni katika kipindi hichi makubaliano ya kuungana baina ya Wahhabi na Salafi yalifanyika. Mwaka 1924 chini ya jasusi wa Uingereza Wahhabi walifanikiwa kuikamata Makkaha tena. Mwaka 1926 Ibn Saud akaita kongamano la kimataifa kuuarifu ulimwengu kuwa anaishikilia miji miwili mitakatifu ya Makkah na Medinah. Mwaka 1932 Kingdom of Saudi Arabia ikaundwa rasmi kwa msaada wa Freemason wa Uingereza, na mfalme akiwa ni kibaraka wa Uingereza, kiongozi wa Wahhabisim na Salaf na mfuasi wa sufiism Ibn Saud. Miaka iliyo fuata Ibn Saud alizilipa fadhila hizo za kufanywa ni mfalme wa Saudi Arabia wakati mababu zake wanadamu ya Kiyahudi toka Ghaibar kwa kuyagawa mafuta ya eneo hilo takatifu kwa makampuni mbalimbali yaliyo chini ya Illuminanti na familia zao za kishetani na Rockefeller wakipatia nusu nzima ya uzalishaji wa mafuta hayo.

NA HII NDIYO NEMBO YA MAPOLISI WA SAUDIA, JE UMEONA ALAMA YA JICHO MOJA KWENYE NEMBO HII, JE UMEONA TAJI LA MFALME JUU YA JICHO HILO, UNADHANI NI MFLAME GANI HUYO MWENYE JICHO MOJA ANAYETAMBULISHWA NA NEMBO HII?

PICHA HII IMEPIGWA NDANI YA MASJID HARRAM, MAKKA, HAPO NI MAALI CHACHE SANA KUTOKA ILIPO AL-KAABAH TUKUFU, NA TIZAMA BEJI YA ASKARI HUYO, NI ILE YA MFLAME MWENYE JICHO MOJA, YAAN MASIH DAJJAL.

PICHA HII NI NJE YA MSIKITI WA MAKKAH, NA HUYU NI ASKARI WA KUFANYA DORIA, LAKINI UMEIYONA NEMBO YA DAJJAL KWENYE VAZI LA ASKARI HUYU? USISAHAU HAPO NI KWENYE MSIKITI MTAKATIFU WA MAKKAH.

Kupitia kwa mtu aliyeitwa Jack Philby, Allen Dulles ambaye alikuwa rais wa Council on Foreign Relation (CFR) na baadaye kuwa ni kiongozi wa CIA waliisaidia Rockefeller kuishika Saud Arabia ambaye itakuja kuwa ndiye wazalishaji wakubwa, karibu nusu ya mafuta yote duniani yatazalishwa ndani ya Saud Arabia. Mwaka 1933 Saud Arabia ikatoa kibali kwa California Arabian Standard Oil Company (CASOC) ambayo nayo ilikuwa na mahusiano na Standard Oil ya California. Mwaka 1936 Socal na Texas Oil wakatengeneza ushirika mbao baadaye ulikuja kufahamika kama Arabian-American Oil Company (Aramco). 

Makampuni saba makubwa ya mafuta yakawa pamoja katika kutawala soko la mafuta, makampuni hayo yakaja kufahamika kama Seven Sisters. Makampuni haya yakishirikiana na utawala wa kifalme wa Saudi yanamiliki utajiri mkubwa na nguvu kubwa kutokana na faida wanayotengeneza kwenye nishati hiyo.


DO I NEED TO SAY MORE?

Mpango mzima ni kumsimamisha muislamu kwenye uwanja wa WWIII, uso kwa uso na yoyote ambaye hatokuwa muislamu na hapa zikiwemo nchi za Ulaya pamoja na Israeli. Lakini kabla ya kumsimamisha muislamu kwenye uwanja huo wa WWIII kwanza lazima wamfanye muislamu akubali na kuamini kuwa wazo hili ni lake na linatoka kwenye vitabu vyake. 


HII BENDERA MAHUSUSI UTAWAKUTA NAYO BOKO HARAM, ALSHABAB, AL-QAEEDAH NA WENGINE KANA KWAMBA MBUNIFU NYUMA YA BENDERA HII NDIYO MBUNIFU WA MAKUNDI YOTE HAYA, NA WALA SIYO QURAN, WALA SUNNAH, BALI NI KUTOKA WASHINGTON, NYUMA YA CIA.

Vikundi kama vya Wahhabi, Salafi, Sufi na wengine tayari wana aina hii ya mtazamo kutokana na kazi kubwa iliyofanyika kwenye miaka ya ’50 mpaka ’60 baina ya Wahhabi na Salafi. Mpaka kwenye miaka ya ’50 Mashariki ya Kati ilikuwa ikiwaka moto kutokana na nadharia hizi ambazo ni za kimasoni zaidi kuliko Kiislam. Kipindi hichi ndicho kilicho kuwa kipindi cha vuguvugu la ukombozi na kupigania uhuru. 

Utaona kundi kama la Muslim Brotherhood lilivyo jishughulisha na harakati za ukombozi zaidi na njia tofauti na imani yao waliyo tumia kwenye harakati hizo. Kundi hili lilikuwa chini ya uangalizi wa Uingereza na mahusiano yake na Hitler yalikuwa mazuri kiasi cha kupeana na kubadilishana mbinu za kijeshi. Muslim Brotherhood iliundwa kwa ajili ya maslahi ya Uingereza na Illuminanti kwa ujumla na kazi zao zinazo wawakilisha mabwana wakubwa hao tunaziona mpaka sasa ndani ya Egypti na sehemu mbalimbali ulimwenguni.


MUFTI WA EGYPT ALIPOKUTANA NA HITLER MWAKA 1941. MUFTI ALITAKA MSSADA WA KINAZI DHIDI YA WAYAHUDI WANAO IKALIA PALESTINE. MAHUSIANO HAYO NDIYO YALIYOPALILIA MAHUSIANO KATI YA MUSLIM BROTHERHOOD NA NAZI

MWAKA 1943 MUFTI WA EGYPT ALILITEMBELEA JESHI LA KINAZI ALMAARUF SS, KATIKA KUJENGA MAHUSIANO BAINA YA NAZI NA WANAHARAKATI WA KIISLAM EGYPT, WAKIWEMO MUSLIM BROTHERHOOD.


Ilikuwa ni sera ya Uingereza kuyanyonya makoloni yake na kuyaacha hoi na machovu kwa kila kitu. Lakini pia ilikuwa ni sera ya Club of Rome na CIA kutumia mwanya huo wa mgawanyo usio kuwa sawa kwenye mali ghafi za uma kuunda wapigania uhuru na wanaharakati ambao miongozo yao haitotoka kwa viongozi wao, bali kutoka kwenye asasi ya Club of Rome, Commitee of 300, CIA na Freemason.  Wana stratejia wa Illuminanti kama vile Dr. Alexander Kings, Henry Kissinger, Zbigniew Brzezinski na Bernard Lewis kwa makini na mipango madhubutu wakishirikiana na CIA, utawala wa Saud, vikundi mbalimbali vya wanaharakati wa kupigania uhuru walitengeneza kile tunachoita Waislam wenye siasa kali (New Salafi au kizazi kipya cha Khawarij) ambao watatumiwa kwenye harakati za ukombozi kwenye nchi na sehemu mbalimbali mashariki ya kati kabla ya kuwapeleka  Afighanistani kuuangusha utawala wa Kisovieti kwa jina lilelile la Jihad.
PICHA INAYO SEMA MANENO 1000. KWAMBA MUSLIM BROTHERHOOD ILIZALIWA PAMOJA NA UNAZI, IKALELEWA NA UINGEREZA, NA SASA INAFANYA KAZI ZAKE KAMA CHOMBO HURU LAKINI CHENYE KUSUBIRI MIONGOZO KUTOKA WASHINGTON.

Lakini kwanza kabla ya hilo Shah wa Iran alitakiwa aondoke na kibaraka mwingine wa Illuminanti aliyeitwa Khomeini akalie kiti hicho. Muslim Brotherhood, CIA na Club of Rome walishirikiana vilivyo kuhakikisha Khomein anaichukua Iran. Utawala wa Khomein ni muhimu kwa vile utatoa mwanya wa kutengenezwa kwa makundi mengine ya Kishia ambayo nayo yatakuwa na msimamo mkali na kuendesha harakati zao kwa namna ileile wanavyo fanya wale ambao wanajiita kuwa wanapigania Jihad.

Pia Iran utawala huu utatumiwa kama ni kitisho kwa nchi za Ulaya na washirika wake kwenye kile kitakachoitwa mradi wa kinyuklia ambayo nayo ni karata muhimu inayosubiri saa na wakati kabla ya kutupwa mezani na kuipamba ile njia ya kuelekea kwenye WWIII (kwa sasa unavyosoma makala hii, karata hiyo imeshaanza kuchezwa).

Kwanza walimuweka Shah baada ya kuuondoa utawala wa Mossadegh. Shah akalipa fadhila kwa kubinafsisha viwanda vya mafuta kwa nchi za magharibi zilizomsaidia kuingia kwenye madaraka. Miaka ishirini na tano baadaye nguvu iliyo mweka Shah madarakani ikamuona hafai inabidi aondolewe na nafasi yake akapewa Khomein. Iraq alikuwepo Saddam muda wake ulipo kwisha walimuondoa na kumuweka Ghazi Mashal Ajil al-Yawer na sasa Jalal Talabani. Zunguka Mashariki ya kati yote utakutana na hadithi hii ya aina moja.

Kwa njia hii Iluminanti wanayabakiza mataifa ya Kiarabu kwenye mgawanyiko na wakati huohuo wao wakitoa mwongozo wa wapi yaeleke; hii tunaiita golden rule ya ‘Divede and Rule’, na hata sasa inatumika kwenye nchi nyingi za dunia ya tatu. Kwenye kile ambacho wanastratejia wa Illuminanti walikiita ‘Arc of Crisis’ haikuwa kingine bali kutengeneza mgawanyiko wa kidini, kiitikadi, kisiasa na kimakabila ndani ya mashariki ya kati, mgawanyiko huu ungepelekea kuwepo kwa vikundi na makundi yatakayo endesha vuguvugu za aina mbalimbali kutoka zile za kidini mpaka kisiasa, kijamii na kimakabila.

Makundi haya mitandao yao itaachiwa ikue na ipanuke kwa misaada kutoka kwa mashirika ya kijasusi ya Illuminanti na baadhi ya nchi za Kiarabu. Makundi haya yatatumika sehemu mbalimbali kwa ajili ya kufanya mapinduzi, ukombozi na kutetea uhuru. Baadaye vijana hawa watajulikana kama ni Mujahidina na watapelekwa Afighanistani kuungusha utawala wa Kisovieti. Kisha baada ya hapo utaachiwa utanuke na kutangaza vita na mataifa yote ya Ulaya na washirika wake kokote walipo duniani kwa kile watakachokiita ni Maadui wa Uislamu na Waislam. 

Hii ni hatua muhimu ambayo itafanikisha kumsogeza Muislamu kwenye uwanja wa WWIII. Kwani mpango mzima ni mapinduzi ya mwisho yatakayo zaliwa ndani ya WWIII. Mapinduzi haya ni muhimu kwa ajili ya kuzifuta serikali na dini zote duniani, hivyo ni muhimu WWIII kupiganwa kwa kisingizio cha dini kuliko siasa; huko ndiko ambako vita dhidi ya ugaidi inapo tupeleka.
ILIKUWA NI MWAKA 1983, NDANI YA WHITE HOUSE, DONALD REGERN, RAIS WA MAREKANI WAKATI HUO, ALIPOKUTANA NA WAPIGANAJI WA TALIBANI NA KUWEKA MAKUBALIANO YA KUWASAIDIA DHIDI YA USSR KUPITIA SHIRIKA LA KIJASUSI LA PAKISTANI.

Tukirudi Iran kutizama namna mchezo mzima ullivyo chezwa na namna karata moja baada ya nyingine ilivyo tupwa na kutenegeza Arc of Crisis, tutizame namna Khomein alivyosaidiwa na Illuminanti kuichukua Iran. Wakati watu walio msaidia Shah kuchukua madaraka walipokuwa wakimshawishi Shah kuzibadilisha sera zake zifanane na zile za kimagharibi kitu ambacho walifahamu kitamsababishia matatizo yeye na watu wake; wakati huohuo watu haohao walimuwezesha Ayatollah Khomein kusimama kama alama, nembo na kiongozi wa kidini zaidi na anayejali, anayeheshimu na anayejitolea kwa kila kitu kusimamia maadili ya kidini ya nchi hiyo.

Club of Rome wakishirikiana na Muslim Brotherhood waliandaa mikakati ya kumuondoa Shah madarakani ambaye ni wao ndiyo walio muweka hapo mara ya kwanza baada ya kumsaidia Shah kumpindua Mossadegh aliyewekwa madarakani kwenye uchaguzi wa mwaka 1953.

Illuminanti ilibidi kumuondoa Shah kwa vile yeye alikuwa na mpango wa kuendeleza viwanda vya kinuklia nchini mwake. Shah alikuwa na mtazamo wa kuifanya Iran kuwa na sura ya kimagharibi kwa maana ya kimaendeleo katika nyanja mbalimbali. Hili halikuwa jambo zuri kwa Illuminanti kwani Iran itakuwa na nguvu za kimaamuzi zaidi na kiuchumi kuliko inavyo takiwa kuwa. Kwa kutumia mawakala wao mbalimbali llluminanti wakaanza kupalilia mbegu zinazo kizana na mtazamo wa kimaterilisti ambao ndiyo ulikuwa mtazamo wa Shah, mbegu hizo zilipandwa kwa vijana mbalimbali kupitia taasisi za kimataifa na kitaifa ndani ya Iran.

Mmoja wa mawakala wa illuminanti waliotumiwa kupanda mbegu ya antimaterilistik kwa vijana wa Kiirani kupitia kwenye sekta ya elimu ni bwana Ali Shariati, ambaye naye pia anatajwa kuwa ni Freemason. Kupitia kwake wasomi wakubwa wa vyuo mbalimbali ndani ya Iran waliingizwa kwenye duara linalo mpinga Shah na sera zake za materelisim. Kupitia kwa wasomi hawa  na kupitia kwenye taasisi muhimu ya elimu ndani ya Tehran Shariati aliwafunulia vijana wa ki-Iran kazi za waandishi kama vile Jean-Paul Sartre, Frantz Fanon, Albert Camus, Jacques Berque na Louis Massignon, waandishi hawa ni wapinzani wa kubwa wa mambo ya ubeberu na materialist, hata hivyo waandishi hawa wote wanafadhiliwa na kufuata miongozo ya Club of Rome.( Dobry, Gary. The Body Politic. <http://www.onthecanvas.com/body_politic.htm>)
TAHRIR SQURE' HAIKUANZIA EGYPT, NA WALA SI LAZIMA IWE NDANI YA EGYPT, POPOTE PALE WANAPO TAKA MABWANA WAKUBWA, PAWE NI 'TAHRIR SQURE' KWA AJILI YA KUMNG'OA WASIYE MTAKA NA KUWEKA WANAYE MTAKA ...

Wanafalsafa hawa hawakuwa chochote zaidi ya wana propaganda wa Illuminanti na maandishi yao yalifuata mwongozo na matakwa ya Illuminanti. Nadharia yao ya kupambana na ukoloni ilishikilia msimamo wenye sera za vurugu, kivita na utumiaji wa nguvu kuliko njia ya amani. Waliamini ni kupitia kwa mtutu wa bunduki tu ndiyo uhuru utapatikana.
SINA HAKIKA SANA NA PICHA HII, LAKINI MTU ALIYE KUSHOTO KWENYE PICHA HII, AL MAARUF KAMA ZBIG, NDIYE 'THE BRAIN' NYUMA YA MPANGO WA WATALEBANI UPIGANA JIHAD DHIDI YA USSR, NA NDIYE ALIYEKUWA MSHAURI WA REGARN KIPINDI HICHO, NA NDIYE ALIYEMSHAWISHI RAIS HUYO KUWASAPOTI TALIBAN. NA LEO ANAYO NAFASI KAMA HIYO KWA KIJANA NAYEITWA OBAMA, NA NATUMIA MBINU ILEILE KUIWASHA DUNIA MOTO NA HASA AFRIKA KWA MASLAHI YA MAREKANI.

Si kupitia kwenye dini ya Uislamu bali kupitia kwa wanafalsafa hawa wa kimasoni na nadharia zao za vurugu kama njia ya kuleta amani ndipo vijana wa ki-Iran walipofunguliwa kwenye utaratibu wa siasa ambao leo tunauita Ugaidi. Ni kwakupitia kwenye sera hizi za vibaraka na mawakala  wa Illuminanti ndiyo Iran ikaweza kuandaliwa kama kituo muhimu cha kudhamini na kutoa misaada mbalimbali kwa wale ambao leo tunawaita ni magaidi, Sera hizo hazikutoka kwenye vitabu na mafunzo ya Kiislam bali yalitoka kwenye kabrasha na miongozo ya Club of Rome.
Wanafalsafa hawa kwenye maandishi yao wanasisitiza kuwa vurugu ni kitu kizuri, vurugu nimuhimu kwa nchi za dunia ya tatu endapo zinataka kujitoa kwenye mikono ya kikoloni, wanadai wana propaganda hao wa Illuminanti kuwa si kwamba tu vurugu zitatuletea uhuru wetu, bali pia kisaikolojia zitaturudishia uwezo wetu wa kujiamini dhidi ya mataifa ya kimagharibi.
Hichi ndicho wanacho dai vijana wa Salafi ya sasa, hichi ndicho wanacho king’ang’ania, wanakuambia hapawezi pakaeleweka hapa mpaka tuchapane kwanza! Nami narudi nyuma na kuwauliza hicho mnacho kitaka sicho ambacho walichoambiwa Talibani, wakaambiwa wa Iraq, wakaambiwa wa Iran, wakaambiwa wa Libya, wa Syria, Boko Haram, Alshabab, Seleka na wengine wengi? Hamuoni, hamtazami mambo kwa jicho pana na kuona mnachezewa? Majibu yao watazunguka na kuzunguka katika mazungumzo yao na nukta ya mwisho watarudi palepale, lazima tuchapane, nami napata hofu kuwa kile tulicho kuwa tukikihofia kipo mbele ya macho yetu kikitutazama, mitazamo ya Khawarij, Assassin, New Salafi na Wahhabi zimeshapenyezwa kwenye fikra na mitazamo ya vijana wetu. Zimepenyezwa na nani na kwa faida ya nani, hapo ndipo palipo na hekima.

 Kupitia sera hizi wapigania uhuru wa nchi mbalimbali ili wabidi kuingia msituni ili kuweza kumng’oa mkoloni, kwa mtazamo wa karibu nchi hizi zilifanikiwa kumng’oa adui yao, lakini imewachukua miaka mingi wasomi wetu kutambua kuwa hatukumng’oa mkoloni, imewachukua miaka mingi kutambua kuwa nchi zetu bado zinatawaliwa na wakoloni, nchi zetu zimewekwa chini ya mashirika ya kimataifa, wakurugenzi, ma-CO na ma-share holders wa mashirika hayo ndiyo wasimamizi, waongozaji, wasemaji wa kila kinacho zihusu nchi hizi, viongozi wa nchi zetu ni kama wamefungwa mikono, midomo na miguu na wameachiwa macho kutazama tu. Tizama http://salimmsangi.blogspot.com/2014/01/malighafi-za-afrika-na-damu-ya-waafrika.html

nimelielezea hili kwa kina, kwa mtazamo wa mbali nchi hizi zimeweza kupanda ile mbegu ya ugaidi dhidi ya mataifa ya magharibi. Mbegu hii ni muhimu kwa mataifa ya Magharibi kuliko nchi zetu zilivyo dhania. Nyingi ya nchi hizi zimeendelea kuwa ni mawakala wa vitendo vya kigaidi kwa namna mbalimbali kwa vipindi tofauti katika historia zao.

Khomein alipingana na sera za Shah, lakini yeye alitumia sura ya udini zaidi ilikuonesha mapungufu ya Shah kwa wa Iran ambao  idadi kubwa wanashikilia misingi ya dini ya Ushia kuliko siasa za kimagharibi, lakini kilichokuwa ni cha ajabu zaidi ni kuwa miongozo ya Khomein nayo haukutokea kwingine ila kwa wafadhili wake wa nchi za magharibi. Mpaka mwaka 1964 alipofukuzwa alikuwa bado anaishi kwenye mji wa kidini wa Qom na alikuwa na mawasiliano mazuri na Uingereza ambayo inasemwa walimpatia masurufu ya kifedha kila mwezi. Khomein alipofukuzwa Iran alikimbilia kuishi Iraq mpaka alipotiwa nguvuni na utawala wa Iraq. Utawala wa Ufaransa ulilazimishwa kumpa hifadhi Khomein. Alipokuwa Ufaransa mambo yaliendelea kubadilika kwa kasi, na picha kubwa ilisomeka hivi;

Bigbrotherhood / Illuminanti hawamtaki tena Shah na Khomein ndiye atakaye kuwa kibaraka wao mpya. Akiwa hapo alipokea msururu wa wageni kutoka BBC, CIA na kutoka kwenye shirika la kijasusi la Uingereza. BBC wakawa ni promota namba moja wa Khomein. (Goodgame, Globalists and the Islamists. http://www.redmoonrising.com/Ikhwan/BritIslam.htm)



BBC wakahusika vilivyo katika kusambaza kaseti za Khomein kwa watu mbalimbali wa Iran hasa kwa viongozi wa kidini. Kwenye kaseti hizo Khomein alizungumzia kuhusu ubaya wa utawala wa Shah. BBC wakaenda mbali zaidi, wakauonesha ulimwengu ubaya na mateso yanayo fanywa na kundi la kijasusi la Shah, kundi la SAVAK, asasi hii ya ujasusi hakuiunda Shah peke yake bali kwa msaada mkubwa wa nchi zilizo muwezesha kuingia madarakani, lakini kwa vile leo hatakiwi basi kila ubaya wake ambao mwanzo ulifanywa siri ulianikwa. Mchezo huu waliufanya tena kwenye miaka ya tisini na elfu mbili pale ajenda ilipomchoka Saddama Hussein.

Ilipofika September na October 1978 BBC ilianza kurusha matangazo yenye mawazo na fikra za kimapinduzi moja kwa moja Iran kwa lugha ya Kifursi, lugha ya taifa la Iran, hivyo kila mtu aliweza kumsikia Khomein kupitia lugha yao ya asili kupitia BBC. Gazeti la Washington Post likatoka na kichwa cha habari kuwa ‘BBC ni adui namba moja wa nchi ya Iran’.
MWISHO UKAWA NI WIMBO WA KILA MTU, SHAH MUST GO!!

Haikuchukua muda wimbi la watu hasa vijana wanafunzi na wasomi wakachukuliwa na vuguvugu la kimapinduzi la Khomein ambao kupitia kwa propaganda za BBC waliona kuna haja ya kurudishwa kwa utawala wa kidini wa Kishia na hivyo Shah aondoke na Khomein aingie ili atekeleze maono hayo kwa faida ya nchi yao. Lakini walikosea kitu kimoja, haikuwa kwa faida yao bali kwa faida ya Illuminanti. Utawala wa Carter kutoka kwenye White House za Marekani, ukifuata muongozo wa Zbgniew Brzezinski mwanastratejia mkubwa wa Illuminanti na kinara wa New World Order ulishirikiana na utawala wa Uingereza kumtoa Shaha Iran na kumuingiza  Khomein ndani ya nyumba.
KAMA WALIVYO WALIOMTANGULIA, NAYE MUONGOZO WAKE HAUKUTOKA PENGINE ZAIDI YA UINGEREZA, MAREKANI NA UFARANSA.

Kuanzia kipindi hicho mpaka Khomein alipofariki mwaka 1989, Iran ikawa ni kituo cha kimataifa cha kuendesha sera za chuki dhidi ya mataifa ya magharibi, kwa maneno mengine kituo cha kimataifa kwa kuendesha sera za ugaidi dhidi ya mataifa ya magharibi.

Mtu mwerevu atajiuliza ni vipi utawala wa Khomein uliosaidiwa kuingia madarakani na nchi za Magharibi leo uendeshe mapambano dhidi ya mataifa hayo ambayo ndiyo wafadhili wake wakubwa? Jibu ni kuwa utawala huo ulitakiwa uingie madarakani ili uweze kuendesha vita hivyo na hivyo kutengeneza mazingira ya kuwepo kwa makundi mbalimbali ya kigaidi ambayo yatategemea msaada wa moja kwa moja kutoka Tehran, na hapa tunakutana na Hizbullah, tunakutana na makundi mbalimbali ya kipalestina mbayo yanapokea misaada yao kutoka Tehran kupambana na adui wa Uislamu na muislamu, kupambana na mataifa ya magharibi, na hapa tunapata vita dhidi ya ugaidi na hii ndiyo picha kubwa ambayo wengi walishindwa kuiona, na wengi bado hawaioni, vita dhidi ya ugaidi si kwa faida ya Uislamu, na kama tulivyona vita hivi havikuzaliwa ndani ya Uislamu na wala havihusiani chochote na Uislamu, bali ni kwa faida ya Illuminanti, ambao kwao ni hatua muhimu kulifikia lile lengo la milenia nyingi, lengo la kuwa na serikali moja na dini moja kwa dunia yote na walimwengu wote, lengo litakalo fikiwa kupitia mapinduzi na vita vikubwa. Mapinduzi na vita hivyo yamekwisha tokea katika zama tofautitofauti, na sasa imebaki hatua moja kubwa ya mwisho, nayo ni WWIII, ambayo itafikiwa kupitia vita dhidi ya Ugaidi.
NA PUNDE MICHAKATO YA KUWAFADHILI MUJAHEEDINA NA WAPIGANIA UHURU IKAANZA ... HILI NDILO WALILOKUWA WAKILITAKA ILLUMINANTI.

Mwaka 1979 Bernad Lewis alipewa fursa ya kuhudhuria kwenye mkutano unao fanyika mara moja kwa mwaka, mkutano wa siri wa asasi ya Bilderberg, Lewis alitoa maono yake ya namna gani Mashariki ya Kati itaendelea kutawalika na wakati huohuo kutumika kuipigisha ajenda hatua kupitia vita dhidi ya ugaidi. Lewis aliwataka Illuminanti kukitengeneza kile kitakacho itwa ‘Waislam wenye siasa kali’ ndani ya Mashariki ya kati, Waislam hao watasaidia migawanyiko mbalimbali yenye sura ya kisiasa, kidini, kiuchumi na kijamii. Migawanyiko hii pia ipewe fursa ya kuanzisha vuguvugu la kimapinduzi, na kupigania uhuru wa wachache ambao wanaoneka kunyonywa au kutengwa na wengi, mfano wa Kurdu, Armeniani, Druze, Azerbaijani Turk, Copto wa Ehiopia, Sudan na makabila yao, Waarabu na makabila yao.
MWANAJESHI WA KIMAREKANI BEGA KWA BEGA AKISHIRIKIANA NA WAPIGANAJI WA TALIBANI ... JIULIZE NI NANI MLENGWA IKIWA MMAREKANI NA MTALIBANI WAKO JESHI MOJA?

Mpango huu utafanikiwa kwa kutumia mbinu zote chafu na za siri za Illuminanti kupitia kwa CIA ambao kwa mlango wa nyuma watafadhili na kutoa mwongozo kwa vikundi hivi. Kupitia mpango huu Iran ilitoa ushirikiano na kuto msaada wa kiukombozi kwa watu walio itwa wapigania uhuru wa Palestine, Ireland ya Kaskazini, Sudan na Ivory Cost.( Labeviere, Richard. Dollars for Terror. p. 215)

Illuminanti ndiyo walioitengeneza na kuipa nguvu Urusi na hatimaye kuifanya kuwa ndiyo taifa lenye nguvu duniani kuliko yote (Super Power), mchakato huo ulifanyika baada ya WWI na WWII, kati ya sababu moja wapo ya Urusi kufanywa Super Power ni ili kutengeneza taifa lenye nguvu na lisilo na dini. Hata hivyo u-super power wa Urusi ulitakiwa kufa na kile kilicho julikana kama vita baridi. 

Ajenda ilikuwa inapiga hatua nyingine kubwa, hatua ambayo itaifikisha kwenye WWIII. Nchi iliyo chaguliwa kuifikisha ajenda hapo haikuwa Urusi bali Marekani, taifa teule la Illuminanti, taifa ambalo maelfu ya miaka nyuma, hata kabla ya zama za Plato tayari lilishateuliwa kuifanikisha kazi hii muhimu na makhususi kwa Illuminanti. Hivyo vita baridi na harakati za kuliteka anga kwa njia ya kumfikisha binadamu mwenzini kwa mara ya kwanza katika historia yake vyote vilikuwa ni maagizo ya kuangusha utawala wa kisoviet na kulikaribisha taifa teule la Marekani kwenye ulingo wa u-super power.
WAS HE? SURE HE DIDNT, BUT WHY THEY TELLING US THAT HE DID?

Kwa ajili ya kumbukumbu napenda kugusia hapa kuwa hakuna binadamu aliyekwenda mwezini, si Urusi wala Marekani walioweza kumpeleka binadamu mwenzini, huu ulikuwa na bado ni uwongo mkubwa katika historia ya binaadam kupata kutolewa na mataifa makubwa duniani, na bado mpaka sasa unaendelea kufundishwa kwa namna na njia mbalimbali kuwa binaadam alikwenda mwezini, lakini ukweli ni kuwa hakuna binaadam aliye kanyaga mwezini, kifupi hakuna binaadam aliyepata kutoka nje ya orbiti ya dunia. Kwenye vitabu vya kidini mathalani Biblia na Quran kuna hadithi kuhusu mitume waliopaa kwenda mbinguni, hii ni hadithi tofauti na ninayo zungumzia , mimi nazungumzia binaadam kwenda mwezini katika zama zetu zinazoitwa za sayansi na teknolojia, katika zama zetu hizi ambazo teknolojia yetu inasemwa ipo juu. 

Nasikitika kukuambia kuwa teknolojia hii ni duni mno kiasi cha kwamba haiwezi hata kumtoa binaadam nje ya orbit ya dunia na kumrudisha akiwa hai achilia mbali kumpeleka mwezini, haiwezi kufanya hivyo ni duni mno. Hivyo safari ya kwenda mwezini ilikuwa ni danganya toto. Samahani kama na wewe ni miongoni mwa walio nunua uongo huo.
MOJA YA PICHA ZILIZOPIGWA 'MWEZINI', UNYAYO WA NAMNA HII HAUWEZI KUACHA KWENYE USO WA MWEZI AMBAPO HAKUNA NGUVU ZA MVUTANO, HIVYO USINGEONEKANA KABISA, AU ATHARI YA UNYAYO HUO INGEONEKANA KWA MBALI SANA, LAKINI KWA VILE PICHA HII IMENASWA KWENYE USO WA DUNIA, MAHALI WALIPOIGIZA TUKIO ZIMA LA KWENDA MWEZINI NDIYO MAANA ATHARI YA UNYAYO HUU, NI SAWASAWA NA MTU ANAYEKANYAGA JUU YA ARIDHI NA SIYO MWEZINI.

Hivyo sakata la vita baridi na nguvu zake zilikuwa na lengo la kumuingiza mwali mpya, Marekani kwenye ulingo wa super power na kumuondoa Urusi. Lakini Urusi haikuwa imesambaratika mpaka pale watu walio itwa kuwa ni mujaheedina kutoka Afighanistani , na kutoka katika kila kona ya dunia walipo pambanishwa na Urusi. 

ITAENDELEA HAPA INSHALLAH ...

12 comments:

  1. iyo ya mwezi ndo umeniacha hoi ucsahau na ile ishu ya ndege ya malasyia

    ReplyDelete
  2. Haupo mbali sana, kwa mtazamo wangu tukio la kwenda mwezini na hili la ndege kupotea vinawiana sawasawa, nikipata wasaa Mola akipenda huenda nikaishusha hiyo skendo ya mwezini na hapo utanipata vyema ... big up for your observation ...

    ReplyDelete
  3. Je hao neo salafy ndo hawa salafy swaleh wenye kufuata kitabu na sunna?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana! Ispokuwa wanatumia jina hilo zuri ili kuweza kuuhadaa umma.

      Delete
  4. Nimejaribu kuuliza kwa ahlul elm kuhusiana na huyo mwanzilishi wa muslim brother hood wakathibitisha kweli alikuwa freemason na pia alikuwa akijiita salafy ila katika vitabu vya masalafy wamemthibitisha kuwa yeye ni free mason, ukijaribu kupitia katika kitabu cha aliyeanzisha chuo cha Daarul hadithy (salafiya) fiy dammaj yemen Sheikh Muqbil Rahmahu Allah amemthibitisha na kusema yeye siyo katika wale wenye kujinasibisha na wema walotangulia bali lengo lao lilikuwa ni kudanganya umma ili kuwagawa makundi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Such a good comment from my reader, keep it up Abu Hudhaifa na waelimishe wengine pia.

      Delete
  5. you seem to have a good capacity in analytical journalism. Hongera, lakina hautubainishii vyanzo vya habari zako. Upande wa jinsi uislamu unavyohusishwa na ugaidi wakati magaidi ni wamarekani hapo sina shaka. Lakini hili la safari za mwezini I reserve my comment. Good job keep it up...

    ReplyDelete
  6. Nakushuru kwa maoni yako, kwenye vyanzo au 'source' ya hizi taarifa sehemu nyingi sana nimeweza kuweka, ila nitaboresha zaidi kwa kuongeza idadi ya vyanzo na kuviweka vionekane kwa wepesi. Karibu sana na endelea kutembelea blogi hii.

    ReplyDelete
  7. This is all shia propaganda.
    Hivi Iran wangekuwa chini ya ottaman wangekubali kuendeshwa kutokaa ankara?
    Basi zimbabwe au namibia wangeacha tu wazungu watawale kule kwa vile ni wakristo wenzao ?
    Ottoman ilikua dola ya kituruki zaidi kuliko ya kiislam. Hakuna cha illuminati wala nini , dunia hii ya sasa ni maslahi na wenye nguvu ndio wamehodhi rasilimali zote.
    Ghadafi na Assad wa syria hawana tofauti na Shah w iran , wote ni madictactor tu.
    Huku shah kaondolewa na mashia na ghadafi na assad ataondoles na ameondolewa na mussuni , yanayotekea sasa ya isis ni harakati za wengine kuzuia suni wasitawale kule sasa wana upaka matope uislam.
    N hi zote hizi ni maslah na zote zinafadhili vikundi vya kigaidi kuifkia maalendo y kisiasa ni kiuchumi
    Iran ina hizbollah , houthi na vikundi vya mauaji kule bahrAin, sawa na saudi na alqaeeda.
    Kuweka photo shop za bush na abdalla wakibusiana ni kuonesha kiwango cha namna gani mtu unaweza kukubali kutumiwa kufanya propaganda za kijinga ambazo hazimsaidi miislam wala mtanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakushukuru kwa maoni yako Riyadh Seif,
      Ila Umekosea Riyadh hizi siyo propaganda za Kishia hata kidogo.
      Maoni yako yako vizuri kabisa na kwa namana fulani maoni yako yapo sawa ispokuwa kwenye nukta ya HIZI NI PROPAGANDA ZA KISHIA.
      Sina cha kusema Ikiwa Ottamn ilikuwa ni dola ya Kituriki zaidi kuliko Kiislam, sababu ilibidi Wazayani kufanya njama za kuanzisha WWI na moja ya malengo yake ilikuwa ni kuiangusha dola hiyo, na Uturuki ilikuja kuzaliwa baada ya kuanguka kwa Ottaman, na wanazuoni wa Kiislam kutoka Azhar Cairo ilibidi kukutana kutoa msimamo wao juu ya hilo, na kwa miaka 2 Uingereza walipambana kumshinikiza rais wa Egypt wa wakati huo kuhakikisha mkutano huo haufanyiki, na ulipofanyika walito msisimamo wao kwamba Kuvunjwa kwa Khilafah Ya Ottaman ni Bid'aa na Haram.
      Japo Ottaman ilikuwa na mapungufu yake kama zilivyokuwa dola zingine za Kiislam baada ya makhalifa wa 4 kuondoka, lakini bado ilikuwa ni nembo na alama ya Dola ya Kiislam na Uingereza kwa kushirikiana na Ibn Saud, ndiyo waliweza kuiangusha dola hiyo.
      Kwanini basi Ibn Saud akishirikiana na Wahhab hawakuisimamisha Khilafah baada yakuanguka kwa Ottaman? Mpaka leo hakuna Khilafah, au haikuwa kwenye mpango wao kuisimamisha tena dola hiyo? Na vipi wataisimamisha ikiwa watu waliowawezasha kupambana na dola hiyo ndiyo bado wanaishikilia.

      Ni kweli unavyosema kuwa dunia ya leo ni mwenye nguvu ndiye anayefanya atakavyo, na vikundi vingi vya kigaidi vinafadhiliwa na serikali mbalimbali kama ulivyo ainisha, LAKINI KUFIKIRI KWAMBA VURUGU YA MASHARIKI YA KATI HIVI SASA NI SUNNI KUZUILIWA KUTAWALA, NADHANI UTAKUWA UMEFIKIRI CHINI YA KIWANGO CHAKO, NI KWELI KWENYE USO WA MBELE NDIVYO INAVYOONEKANA, LAKINI MALENGO MAKUU SIYO HAYO, MALENGO MAKUU NI KUWA MAREKANI SASA ANAILINDA 'PETRO DOLAR' AMBAYO MCHINA, MRUSI, MVENEZUELA, MJAPAN, MUIRAN WAMESHAITUPA, SASA MAREKANI ANAFANYA KILA ANALOWEZA KUNUSURU MKTABA BAINA YAKE NA NCHI ZA MAFUTA ULIOFANYA NA KISSINGER CHINI YA NIXXON MWAKA 1973 KUHAKIKISHA KUWA MAFUTA YOTE YATAUZWA KWA DOLA, NA MAREKANI ITATOA SILAHA NA ULINZI KWA NCHI HIZO. lIBYA ALITAKA KUUZA KWA DINAR, AKANG'OLEWA, SADDAM ALIANZA KUUZA KWA ERO, AKATOLEWA, NILIO WATAJA HAPO JUU WAMESHA ACHANA NA SARAFU YA DOLA KATIKA BIASHARA ZAO WENYEWE, SASA MAREKANI LAZIMA APAMBANE KUHAKIKISHA MAFUTA YATAENDELEA KUUZWA KWA DOLA AMA VINGINEVYO SARAFU YA DOLA HAINA THAMANI YEYOTE KOKOTE. SO KINACHOENDELEA MASHARIKI YA KATI SIYO ISHU YA SUNNI AU SHIA, AU ISIS, AU YEYOTE YULE, KINACHOENDELEA NI HARAKATI ZA KUINUSURU PETRO DOLLAR.
      KUHUSU PICHA YA BUSH NA ABDALLA KUBUSIANA SIYO USHAHIDI JUU YA POSTO HII. NADHANI SEHEMU NYINGI NIMEWEKA REFERENCE KAMA USHAHIDI, PICHA ZA KWENYE MTANDAO HATA KIDOGO HAZIWEZI KUTUMIKA KAMA USHAHIDI, ITS JUST A DECORATION, ILA NASHUKURU KWA KULIONA HILO.
      ENDELEA KUSOMA BLOGI YETU KARIBU SANA.

      Delete