Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Sunday, June 15, 2014

USICHO KIFAHAMU KUHUSIANA NA VITA DHIDI YA UGAIDI Pt 1


Ningependa kuianza makala hii kwa hadithi mbili,

Hadithi ya kwanza

Hudhaifa (ra) anasema kwamba, amesema mtume (saw): “Kwa hakika, nahofia kati yenu yule mtu ambaye ataisoma Quran kiasi kwamba nuru ya Quran itaonekana kwenye uso wake ... halafu neema hii itaondolewa pale atakapoidharau na kuipa mgongo na atabeba upanga wake kumshambulia jirani yake na kumtuhumu kuwa ni mshirikina.” Mtume (saw) akauliza ni nani kati ya wawili hao atakuwa anazistahiki hizo tuhuma? -  Mwenye kutuhumu au mtuhumiwa? Mtume (saw) akajibu ni, “mwenye kutuhumu.”

Hadithi ya pili.

Imam Bukhari (Allah amrehemu) ameeleza, “Umar ibn al-Khattab (ra), ambaye alikuwa akizungumza na masahaba, aliwauliza, ‘Ni nani kati yenu mwenye elimu zaidi kuhusiana na fitnah?’ Hudhaifah (ra) akajitokeza na kusema, ‘Mimi ewe Ameer ul-Muumini! Kisha akaanza kuzitaja baadhi ya fitnah Umar ibn al-Khattab (ra) akasema, ‘Siyo fitnah hizo ningependa kufahamu kuhusiana na fitnah ambazo wimbi lake litakuwa kama wimbi la bahari.’ Hudhaifa (ra) akauliza ‘Kwanini unataka kujua kuhusina na hizo fitnah ewe Ameer ul-Muuminin? Kati yako na hizo fitnah kuna mlango ulio fungwa.’ Umar (ra) akauliza ‘Je mlango huo utavunjwa au utafunguliwa?’ Hudhaifah (ra) akajibu, ‘Utavunjika’ Umar (ra) akajibu, ‘Basi hautafunga mpaka siku ya kiyamah..’

KUNA AMBAYE YUPO BIZE SANA KUFITINISHA IMANI HIZI MBILI.



Hadithi hizo mbili tutakuwa tukizirejelea kila pale zitakapo hitajika, lakini kwanza tuanze na hii ya pili. Hadithi hii inatuthibitishia kuwa fitnah katika Uislam imeingia baada ya kufa kwa Umar (ra) ambaye katika hadithi hiyo hapo juu mpaka mwisho wake inamtaja Umar (ra) kuwa ndiye mlango baina ya fitnah na umma wa kiislam. Fitnah ya kwanza katika umma ni kuuwawa kwa Umar (ra), kitu kinacho ashiria kuvunjika kwa mlango ulikuwapo baina ya fitnah na dini hii ya Uislamu, hivyo baada ya hapo fitnah zinazo kwenda kama mawimbi ya bahari zikaanza kumiminika.

Fitnah iliyofuatia ni kuwawa kwa khalifah watatu wa Waislamu, Uthman bin Khafan (ra), kwa kiasi kikubwa kifo chake kilitokana na Myahudi aliye ingia katika Uislam kwa nia ya kuubomoa Uislamu akiwa ndani.

Wauwaji wa Uthman (ra) wakamfuata Ali (ra) na kumtaka awe Khalifah, Ali (ra) alikataa, lakini waliendelea kumsihi na kumsisitizia mpaka akakubali.

WANASHIRIKIANA NA WASIYO WAISLAM KUUBOMOA UISLAM

Muawiyah (ra) kama ndugu wa karibu wa Othumani (ra) alikuja kutaka haki itendeke dhidi ya wauaji wa ndugu zake, lakini Ali (ra) akimsihi achukue kiapo kwanza cha  kumtii kabla hajaanza kazi ya kutafuta haki ya ndugu yake, na hapo ikawa mvutano ambao ulipelekea fitna kubwa baina ya Waislam, kwanza Mama wa Waumini Aisha (ra) na Ali, baadaye vilimalizika vita hivyo na Ali (ra) akamsindikiza Aisha (ra) kurudi nyumbani, halafu vita vya Suffin baina ya Muawiyah na Ali (ra) ambavyo pamoja na hasara kubwa iliyo patikana katika umma wa kiislam, Muawiya alisalimu amri na Ali (ra) alikubaliana na hilo.

Lakini watu waliomuwa Othaman (ra), na ambao walikuwa wamejipenyeza kwenye jeshi la Ali (ra) na ambao ndiyo waliyo anzisha vita hivyo vya Suffin, watu hawa wakaondoka kwenye jeshi la Ali (ra) kwa kutumia kauli maarufu (la hukm illa lillahi) ‘Hukmu ni ya Mwenyeezi Mungu peke yake’ na kwamba Ali amefanya makosa kupatana na Muawiya (ra), amefanya makosa kwa kutumia ‘maoni’ yake dhidi ya amri ya Allah. Hapo ndipo walipo pata jina la Khawarij, likiwa na maana ya wale wenye kujitenga.
MWISHO WA YOTE NI MUISLAM KUMUUWA MUISLAM.

Utakumbuka watu hawa ndiyo waanzilishi wa fitna hii, na ndiyo waliyo pelekea vita baina ya Waislam kwa Waislam, na kila wakiona damu wanashiriki, wakiona amani, wanajitenga.

NYUMA YAKE KUNA MNARA WA MSIKITI MKONONI KUNA KITABU CHA QURAN NA MKONO MWINGINE KUNA BUNDUKI. HII NDIYO PICHA WANAYO PANDIKIZWA WATU KUWA NAYO DHIDI YA UISLAM.

Lakini mzizi wa kundi hili ulikuwepo tangu wakati wa Rasulullah (saw), kutokana na hadithi iliyo simuliwa na Said Khudhuri, kutoka kwenye kitabu cha Bukhar, kwamba wakati mtume (saw) anagawanya ngawira, alikuja mtu kutoka kwenye kabila la Tamim na jina lake ni Dhul-Khuwaisar, mtu huyu kwa jeuri na kiburi akamuambia mtume (saw) tenda haki!, mtume wa Allah akamuambia, ole wako, ni nani atakaye tenda haki kama mimi sitaitenda. Omar (ra) akataka ruhusa kwa mtume (saw) ili aweze kukitenganisha kichwa na kiwiliwili cha mtu huyo, lakini mtume akamuambia, Muache. Atakuwa na wafuasi. Na mtakapo linganisha swala zao na zenu mtaiona ya kwenu si chochote kitu, na saumu yenu si chochote ukilinganisha na ya kwao, wataisoma Quran lakini haitavuka koromeo lao. Watatoka na kuiacha dini yao kama mshale unavyo wacha shabaha yake. Abu Saiid akaendelea kusema, Naapa nilikuwepo wakati Ali ibn Abi Talib alipopambana nao na kuwapiga. Ali (ra) alitoa amri kuwa kiongozi wao atafutwe katika maiti wao, na alipatikana kama ambavyo Mtume (saw) alivyo muelezea sifa zake.




KHAWARIJ WANAPIGANA JIHAD NA WAISLAMU WENZAO, TANGU ZAMA HIZO MPAKA LEO.


Watu hawa walikuja kupigana na Ali (ra) katika vita vya Naharwan baada ya kumkamata sahaba na familia yake na kuwaua, mke wa Sahaba alikuwa na ujauzito, walimpasua tumbo na kukitoa kichanga hicho na kukiuwa. Baada ya hapo Ali (ra) alipambana nao, na hatimaye mwili wa kiongozi wao ukaletwa mbele ya Ali (ra) kama nilivyo taja hapo juu.

Khawari waliendelea kuwepo hata baada ya vita hivyo, na wanaendelea uwepo hata mpaka sasa, na siku zote hawakuwa wakipambana na yeyote isipokuwa Waislam. Yeyote aliyewapinga walimuita ni Kafir na ni haki kwao kuwapiga watu wao na hata kuuwa wanawake zao na watoto wao na kuchukua mali zao. Nafi ibn al Azraq mmoja wa viongozi wa moja ya makundi ya Khawarij alikuwa akisema ‘wapinzani wetu ni washirikina na hivyo hatupaswi kurudisha chochote tunacho kaishikilia dhidi yao.’ (Abd al-Qahir 82-84)

Baada ya kifo chake Nafi Ibn Azraq, katika vita wafuasi wake wakampa utawala Ubaydallah ibn Ma’mun al-Tamimi. Naye huyu Ubaydallah akauwawa katika vita vingine pamoja na kaka yake Uthman ibn Ma’mun. Baada ya hapo wakampa uongozi wao bwana Qatari ibn al Fuj’a, ambaye walimuita Amir al-Muuminina. (Abd al-Qahir 85-86)
MSAHAFU NA BUNDUKI, HUU NDIYO UISLAM WA LEO.

Kwenye mikono ya watu hawa ambao nao walijiita ni ‘waislamu’, maelfu kwa maelfu ya waumini wa Kiislamu waliuwawa, mali zao kuporwa na heshima zao kuvunjwa, Khawarij walifikia kuwaita waumini wa Kiislamu ni makafiri na wenye kustahiki kuwawa kwa vile hawakukubaliana na mtazamo wao wa kiitikadi.
Lakini tumeona kisa cha Dhuli-Khuwaysira, ambaye alidiriki kusimama mbele ya mtukufu wa daraja (saw) na akamuambia kwa ukali na kwa dharau, “tenda haki” naye huyu anahisabiwa kuwa Khawarij wa mwanzo kabisa, na ambako misimamo ya viongozi wengine wa Khawarij ilifuata nyayo zake, na watu hawa hawakuwa ni fitina kwa kipindi fulani tu cha historia ya umma huu, lakini unapo itazama historia ya umma na fitina zake utaona Khawarij walikuwa ni njia au mawimbi ya fitina hizo. Mtume (saw) amesema, fitna ya watu hawa itaendelea, haikatiki. Kizazi kimoja cha watu hawa kinapo toweka, basi kingine kinakuja, mpaka katika zama za Dajjal zitakapo fika. Mtume (saw) amesema kizazi kimoja kinapo toweka kwa maana ya kuwa hawafuatani katika mstari ulionyooka, kizazi kimoja kinakuja kisha kinaondoka, sababu mwisho wa yote watu hawa wakikosa watu wakupingana nao, wanaishia kupingana, kuuwana wao kwa wao, kisha kizazi hicho kinatoweka, halafu kinakuja kuibuka tena kingine baada ya kitambo fulani, tena huenda kikaibukia sehemu nyingine kabisa. Hadithi kutoka kwa Ibn Maaja, kutoka kwa Ibn Omar anasema alimsikia mtume (saw) akisema “ ... kila kizazi kimoja kinapo tokea, hutoweka ( eidha kwa kuuana wao kwa wao au kwa nguvu pinzani) kisha kingine kitafuata nacho kitatoweka, Ibn Omar anasema mtume wa Allah alirudia hivyo zaidi ya mara 20 kisha akasema mpaka Dajjal atakapo tokea.
Ibn Omar akaendelea kusema kuwa, Khawarij ni watu wabaya zaidi, kwani wanazichukua aya za Quran zinazo walenga makafiri na kuwashambulia nazo waumini. Wanawashutumu waumini kuwa ni makafiri kwa kutumia ayah ambazo misingi yake inawalenga makafiri. Ni wepesi sana kwa kuwahukumu watu na kuwaita makafiri. Rejea hadithi ya kwanza ya mtume niliyo itaja katika makala hii nayo ikielezea jambo hilohilo kutoka kwenye kinywa cha Rasullullah.

SURA MBILI.

Nayo hiyo ndiyo moja ya sifa zao kubwa, moja kuwa na msimamo mkali kupitiliza (extremisim), pili kuwatuhumu Waislamu kuwa ni makafiri na tatu kumwaga damu ya Waislamu, kuchukua mali zao na kuwavunjia heshima zao. Na ni kwa sifa hizo kuu tatu utaona imekuwa ni rahisi kwa wao kumwaga damu ya maelfu na malaki za Waislamu kuanzia pale walipomuua Othman (ra). 

Ingawa kwa ujumla wao wanafahamika kama Khawarij, lakini kwa sifa au tabia hizo nilizo zitaja wamekuwa wakija na majina tofauti katika zama na maeneo mbalimbali kwenye historia ya umma.

HIZI NI SURA MAARUFU KWENYE HARAKATI ZA KIISLAM, LAKINI NAMNA YA HARAKATI HIZO ZILIVYO NA ZINAVYOFANYIKA ZINATIA SHAKA NA DOA KWENYE MAFUNZO HALISI YA UISLAM, NA YANABEBA KILA RANGI YA KHAWARIJ.

Kuna kundi lilikuwa likifahamika kama Assassin, kundi hili unapotembelea Mashariki ya kati basi utakutana na hadithi zao za kutosha tu.

Kundi hili la kigaidi la Assassins lilikuwa ni moja ya makundi mengi ya waliokuwa wafuasi wa dini ya kiislam ambao walijitenga na mafunzo sahihi ya dini hii na kuzitafsiri aya pamoja na mafunzo ya mtume Mohammad kutokana na maono yao. 

Kama tutakavyo kuja kuona, kundi hili la Assassins lilikuja kukutana na kikundi maarufu cha Knights Templars ambao hawa Knight Tempars ndiyo walio kuwa vinara wa vita vile vya msalaba. Kupitia kwa Assassins;  Knight Templars wakajifunza uchawi na ushirikina wa mashariki ya kati na wao wakaupeleka uchawi huo katika nchi za Ulaya. Baadaye ushawishi huo utaingia mpaka kwenye Scottish Rite Freemasonry na baadaye kwenye karne ya ishirini tutaona athari ya mahusiano haya baina ya Assassins na Knight Templar ambayo yatapelekea kuunda kwa makundi mengine ya kigaidi na Freemasonry wa Magharibi kupitia jina la Uislamu kwa malengo makubwa ya New World Order

Ugaidi ambao hauna nafasi yoyote katika mafunzo ya Kiislam ulirudishwa mara ya pili kwa freemason wa Egypt kutoka Ulaya ambapo mbinu hiyo ilipelekwa na Knights Templar ambao nao walichukua kutoka kwa Assassins. Ismailia ndiyo waliyo boresha mbinu hii ya ugaidi na baadaye itachukuliwa na Illuminanti  ambao na wataitumia kwa karne zitakazo fuata.

Ismailia haikuwa imepotea sana kwenye misingi ya Uislamu mpaka pale uongozi wa kundi hili ulipo chukuliwa na mtu aliyeitwa Abdullah Ibn Maymun mnamo mwaka 872. Jamaa huyu alipouchukua utawala wa kundi hili si kwamba Ismailiya walibadilika na kuwa ni adui wa Uislamu lakini adui wa dini zote duniani. Ibn Maymun alikuwa ni Myahudi ambaye alifuata imani za kipagani za Mesopotamia ya kale, imani ya kuabudu nyota, ushirikina, uchawi na mazingaombwe ndizo alizo fuata Ibn Maymun. Lakini jamaa huyu alikuwa pia na elimu ya dini zingine mbalimbali duniani ikiwemo Uislamu na Ukristo, hivyo alikuwa vizuri, alikuwa yupo vyema na alijua anachofanya.

Mmoja wa walio kuwa wanafunzi wazuri sana wa Ibn Maymun ni Hamdan Qarmat, ambaye alianzisha hekalu kama yale ya kimasoni, hekalu hilo liliitwa Qaramitah ambapo katika zama hizo lilipata sifa pande za Arabuni na warabu wengi walisimikwa katika asasi hiyo, mafunzo na maono yake yalikuwa sawa na ya mwalimu wake mkuu. Kwa vile wengi wa wafuasi wake walikuwa ni waumini wa dini ya Uislamu aliamua kuwafundisha namna ya kuachana na misingi ya dini hiyo lakini wakati huohuo wakiendelea kujitambua kuwa wao ni Waislamu. 

Aliwapa nadharia za upagani zilizo waruhusu kuachana na sala, ibada ya kufunga pamoja na ibada zingine. Kutokana na aina hii ya mafundisho kundi hili likawa ni kitisho dhidi ya waumini wa kweli wa Uislamu. Wale walio pinga mafunzo ya kikundi hichi waliuwawa, kikundi hichi kilisimamia kile ambacho leo tunaita ni ugaidi dhidi ya yeyote aliye onekana ni kitisho au kuwapinga. Kundi hili lilifanikiwa kuishika Iraq, Yemen na Bahrain na baadaye walilikamata jiji takatifu kwa dini ya Uislamu, jiji la Makka ambapo hapo waumini wa kweli wapatao elfu thelathini waliuwawa na kundi la Qaramitah. (David Livingstone ‘TERRORISM AND THE ILLUMINATI’ A Three Thousand Year History)

Ismailia nao wakagawanyika makundi mawili juu nani ashike uongozi wa dini hiyo baada ya kufariki kiongozi wao al-Mustansir mwaka 1094 AD. Kundi la Ismailia wa Egypti walimtambua mtoto wa al-Mustansir bwana al Mustali kuwa ndiye anayefaa kushika hatamu, kundi jingine la Ismailia kutoka Iran na Syria wao walimtaka mtoto mkubwa wa Al-Mustansir bwana Nizari ndiye ashike hatamu. Waliomuunga mkono Nizari waliongozwa na Hasan Sabbah.

Mahusiano haya baina ya Freemason wa Ulaya na wale wa Mashariki ya Kati yalitengeneza njia ambayo Illuminanti wataitumia kutengeneza kile kitakacho itwa ugaidi na baadaye vita vya tatu vya dunia vitakavyo jengwa kwenye msingi huu wa vita dhidi ya ugaidi. Mpango huu mahiri ulichorwa na vichwa vinne vya Illuminanti vya wakati huo, Alikuwepo Muzzin mwenyewe kutoka Italia, Lord Henry Palmerston wa England, Otto von Bismarck wa Ujerumani na Albert Pike mwenyewe, jamaa wote hawa walikuwa ni Freemason wa Scottish Rite wa daraja la 33. Walikubaliana kutengeneza chombo kikuu cha Freemason kitakacho kuwa na nguvu ya kuwaingilia, kuwahoji na hata kutengua maamuzi ya Freemason wengine kokote walipo duniani, chombo hichi ndicho kitakacho kuwa kikitazama na kuongoza mchezo mzima, walikiita chombo chao hichi Palladium Rite Freemason. Hivyo basi Grand Lodges, Grand Orient. Memphis Rite, Mizraim Rite, Scottish Rite na Egptian Freemason au Primitive Rite zote zililetwa chini ya Palladium Rite. (Three World Wars”. “Who Was Albert Pike?” <http://www.threeworldwars.com/albert-pike.htm>)

Wakati Freemason wa Egypt wakiwa ni msingi mzuri wa mahusiano baina yao na wale wenzao wa Ulaya, mshikamano ambao kwa karne zitakazo fuata utatengeneza vikundi na mitandao ya ugaidi kwa mbinu ileile iliyo tumiwa na Hasan Sabbah. Nadharia na sababu ya kutumika kwa mbinu hiyo ya ugaidi inazaliwa katika nchi ya Saudi Arabia kupitia kwa mtu aliye itwa Mohammed Abdul Wahhab na nadhari ya Wahhabism iliyo tengenezwa na mtumishi wa Illuminati.



 Kazi ya Abdul Wahhab dhidi ya umma haikuwa na tofauti na zile kazi za Khawarij, na hata hivyo anafahamika pia kama mtu aliyeifufua Khawarij tena.

Kabla Wahhabism haijafanya kazi nzuri iliyokusudiwa ya kuliharibu kabisa jina la Uislamu na kutilia mashaka mafunzo yake itakapofika karne ya ishirini na moja, kwanza ilitumiwa katika ile mbinu maridadi ya Uingereza ya ‘divide and rule’, ambapo Waarabu waliuwana na ndugu zao wa Uturuki,

Mwaka 1453 Waturuki waliikamata Constantinople na kuanzisha dola maarufu kwenye historia ya Uislamu, dola ya Ottoman ambayo iliweza kupanuka na kuzifikia mpaka nchi za Ulaya. Dola hii ya Ottoman ilishikilia maeneo mengi ambayo pia dola ya Uingereza iliota ndoto za kuyashika maeneo hayo. Hivyo njia iliyo kuwa bora kwa Uingereza kuweza kuizorotesha dola hii kamambe ya Ottoman ilikuwa ni kutumia njia yao marufu ya ‘divide and rule’. Freemason na jasusi wa Uingereza ndiye aliye pewa kazi hiyo ya kuwagawa na hatimaye kuwa pambanisha ndugu wawili wa Uislamu, yaani Mwarabu wa Saudi na Mturuki.


Katika Uislamu ni haram na dhambi kuu, kupigana na hatimaye kumuua ndugu yako wakiislamu. Kwa hivyo ilikuweza kumpambanisha Mturuki na Mwarabu ambao wote ni ndugu katika Uislamu, aina mpya na tofauti ya kutafsiri Quran na mafunzo ya mtume ilihitajika kufanikisha hilo, tafsiri ambayo itatoa ruhusa kwa ndugu muislamu kumuua ndugu yake.

Historia ya Uislam inathibitisha kuwa hakuna watu bora zaidi wa kufanya fitna hii zaidi ya Khawarij. Hivyo kwa mtazamo wa Uingereza hilo lingewezekana kutokea tena endapo tu atapatikana mtu muhimu wa kuanzisha moto huo, na safari hii mtu huyo hakuwa mwingine bali ni Mohammed Abdul Wahhab na mbinu au tafsiri aliyoitumia kufanikisha hilo ilikuja kufahamika kama Wahhabisim.
Kama walivyo kuwa Assassin na wengine mfano wa hao, Abdul Wahhab naye alitangaza kuwa yeyote asiye mfuata katika imani yake hiyo mpya ni kafiri na yeye Abdul Wahhab ana haki ya kumuua mtu huyo, kuteka mali zake, kumvunjia heshima yake na kumuuza kwenye soko la watumwa.

Alitumia nafasi ya hali duni waliyo kuwa nayo Waislam wa hapo kutokana na uongozi wa dola ya Ottoman na hivyo kuwataka waumini wasimtii Sultani wa Istanbul. Abdul Wahhab akasema kuzitukuza sehemu takatifu ni ushetani, akamtukana mtume na wafuasi wake waliomfuata kwa haki, wakiwemo viongozi wa kiroho na wasomi wa Kiislam. Akachochea vurugu baina ya miji na nchi za Kiislam na hasa dhidi ya dola ya Ottoman. Kokote kuliko kuwa na mwanya au jambo lenye shaka Abdul Wahhab alilitumia hilo kuwa pambanisha ndugu wawili wa Kiislam. Mwisho alitangaza jihadi dhidi ya Waislam wote. (Shaykh Juri,  Muhammad bin Abdul Wahab)

Uingereza waliweza kumshawishi Mohammad ibn Saud, kiongozi wa Dariyah kumuunga mkono Ibn Abdul Wahhab. Inasemekana pia pande hizi mbili ya Saud na Wahhab walikubaliana kuwa kuanzia hapo madaraka yatagawanya baina ya familia hizo mbili tu. Wakati Saud wao watashikiliwa utawala kwenye mambo ya siasa, Wahhab wao watabakia na nguvu kwenye masuala ya kidini. (Madawi al-Rasheed, A History of Saudi Arabia: )
TAHADHARI NA MCHUNGAJI HUYU ...

Wahhabi wakishirikiana na Saud wakatangaza kuwa utawala wa Ottoman ni wa kinafki, wakatangaza jihad kwa yoyote asiye kubaliana na madai yao kuwa utawala huo haufai. Katika mafunzo ya Uislamu ni kosa zito kumuita muislamu mwenzako mnafiki, na ili kuthibitisha uzito wa kosa hilo, mafundisho ya Uislamu yanasema, muislamu anapo mtuhumu mwenzake kwa unafiki, basi kwa uhakika anaye tuhumiwa au anayetuhumu mmoja wao ni mnafiki. Lakini uzito wa kosa hilo haukumzuia Abdul Wahhabi kuwaita wale wasiomuunga mkono kuwa ni makafiri. (The Wahhabi Threat)

Mwaka 1746 kabla hata Abdul Wahhab hajaonganisha nguvu zake na zile za Ibn Saud, yeye Abdul Wahhab alituma wanaume thelathini kwenda kuomba ruhusa ya kufanya ibada ya Hajj. Uongozi wa Makkah uliwakubalia kwani waliona huo utakuwa ni wakati muafaka kwa wanazuoni wa kweli wa Kiislam kutoka Makkah na Medina kufanya mjadala wa wazi na Abdul Wahhab mbele ya hadhara kubwa na hapo watu wote watakao hudhuria na wasio hudhuria watafahamu ukweli ni upi baina ya madai ya Abdul Wahhab na mafunzo ya kweli ya dini anayo dai kuitetea. Abdul Wahhab alishindwa vibaya katika mjadala huu na alishindwa kabisa kutetea hoja zake. (Algar, Hamid. Wahhabism: A Critical Essay, uk. 23.)
VIJANA WETU WANAKUJA WAKIWA WAZURI KABISA, LAKINI WANAPO PITA CHINI YA MTU HUYU WANATOKA WAKIWA NA MABOMU NA SHIDA ZINGINE

Tukio hili lilizidisha chuki za Wahhab dhidi ya uma wa Kiislam. Ibn Saud alipofariki mtoto wake Abdul Aziz akawa mtawala wa Dariyah. Kipindi cha miaka ishirini iliyofuata Wahhabi walizidi kutanuka, kila sehemu Mwingereza alipoingia nao walikuwa nyuma. Mara kadhaa Mwingereza alijaribu kuichukua Kuwait lakini kila wakati alizidiwa nguvu na dola ya Ottoman. Mwaka 1775 wakati Uingereza ikiuguza majeraha iliyo yapata toka kwa Ottoman, mshirika wake Abdul Wahhab alijitangaza kuwa ni kiongozi wa waislam wote duniani, na wakati huohuo akiwa ametangaza vita ya Jihad dhidi ya utawala wa Ottoman. Mwaka 1788 Uingereza ukamsaidia Abdul Aziz ibn Saud kuichukua Kuwait.

Mwaka 1792 Abdul Wahhab alifariki na Abdul Aziz akawa kiongozi wa Wahhabisim ambapo kwa miaka mitatu iliyo fuata aliweza kupenyeza vuguvugu la Wahhabisim kwenye mji wa pili kwa utukufu katika dini ya Uislamu, mji wa Medina kisha Syria na mwaka 1801 Iraq.

Saud ibn Abdul Aziz ibn Saud akawa kiongozi wa Wahhabi baada ya baba yake. Baada ya kuuvuruga vibaya mji mtakatifu wa dini ya Shiah, Wahhabi wakahamia katika mji wa kwanza kwa utakatifu kwa dini ya Kiislam, mji wa Makkah. Utawala wa Ottoman wa kwenye mji wa Makkah haukuweza kupambana na jeshi la Wahhabi bali walikimbilia kwenye ngome yao iliyoko Taif. Hata hivyo jeshi hilo la Wahhabi lilifanikiwa kuichukua ngome ya Taif. Kisha kama walivyo fanya uharibifu katika mji wa Karbala ndivyo walivyo uvuruga mji huo mtakatifu wa Makkah. Kutoka kwenye makaburi ya waumini mpaka kwenye madrassah na misikiti. Vitabu mbali mbali vya dini waliviharibu na inasemekana walitengeneza malapa kwa kutumia vitabu hivyo. ( Part Two: The Beginning and Spreading of Wahhabism, by Ayyub Sabri Pasha [1888 -1893])

Wahhabi wakiwa wameishikilia miji hiyo miwili mitakatifu ya Makkah na Medina chini ya kiongozi wao Saud ibn Abdul Aziz bin Saud wakapitisha sheria zao mpya za Uislamu. Ikiwemo kuzuia Waislamu kufanya ibada ya Hijja, walidai zama hizo hakukuwa na Waislam wasafi wa kuweza kufanya ibada hiyo, wakaifinika Al-Kabbah na kitambaa chakavu na cheusi na wakipanga namna ya kuivunja nyumba hiyo tukufu. 

Mkono wa Freemason wa Uingereza ulikuwa nyuma ya haya yote na Wahhabisim nyuma ya viongozi wao walikuwa wakitekeleza maelekezo toka kwenye nyumba za ibada za kimasoni. Wakati dola ya Uingereza ikipanuka na kuchukua aridhi za Waislam Wahhabisim wao walikuwa bize wakifanya Jihad dhidi ya uma wa Kiislam.(Ibid)

NI KAMA VIJANA WETU WANATOLEWA BONGO ZAO NA NAFASI YAKE INAWEKWA BOMUU!!!! HATARI SANA!

ITAENDELEA INSHAALAH ...

8 comments:

  1. Inalillah wainailah rajiun sasa n vipi tutazitambua jihad ya kwel na kwa namna hii xaxa uiclam utaitawalaje dunia kama umeshaharibiwa ivi inaskitisha sana

    ReplyDelete
  2. Mafunzo ya Uislam yapo wazi kabisa kwenye hili. Kwanza ni kuitafuta elimu sahihi ya kiislam, kisha ifundishe elimu hiyo kwa familia yako na jamaa zako wa karibu, na fanya juhudi kwa namna nzuri utakayo weza ya kuuelimisha umma dhidi ya njama hizo mbovu. Uma ukifahamu kipi ni kipi basi hiyo yenyewe itakuwa ni moja ya jihadi kubwa umeifanya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe shia eeh! hapana shaka shia ni wapinga jihad hakuna muumin walweli asie wafahamuni! ni nyinyi mnaotoa fatwa za uongo kupinga jihad! mkasmea kunjiahd nnafsi ambayo ni kubwa kuliko jihad ya silaha! hadithi ambayo si sahihi! muhaddithiina wote wamekosa kuipatia dalili kua ni hadithi sahihi! Shia c waislamu ninyi japokua mnakuja kwa sura za kiislamu! hilo ulifaham so hakuna unchoelezea za maana zaidi ya upotoshaji dhidi ya umma wa kiislam! Allah ndiye mjuzi zaidi!

      Delete
    2. Kuwa huru wakati unasoma posti hizi, achia akili yako ichanganue yenyewe. Usiwe na msimamo ambao hautaki utizamwe na kuoneshwa kasoro zako, msimamo wa namna hii haumsogezi mtu popote katika kutafuta elimu na uelewa zaidi ya kupingana kugombana na kuwapachika watu majina na sifa zisizo zao. Kaachini, kuwa mpole pima kwa akili yako mwenyewe, usipime kwa akili au mtazamo wa fulani, halafu mwisho njoo na utafiti wako binafsi juu ya kile unacho kisema, usikimbile kupinga tu.

      Delete
  3. asalaam alaikum, Salim, naomba nisaidie juu ya hili, UKIWAANGALIA ALSHABAAB, NI WASOMALI NA WAPO NDANI YA ARDHI YAO, NA WANANYANYASIKA NA WAGENI, NA UKIZINGATIA WANAJITAWALA ASILIMIA KUBWA KWA SHARIA YA KIISLAM, ASILIMIA TISINI NI WAISLAM, SERIKALI YAO NI CORRUPTED, ....JE KAMA ALSHABAAB HAWAPIGANI JIHAD, ....IPI ITAKUWA NI JIHAD YA KWELI? NA JE, DHULMA IWE YA KIWANGO KIPI NDIPO WAISLAM WANARUHUSIWA KUPIGANA JIHAD?,.....NA JE, JIHAD YA UPANGA KATIKA QURAN INAMAANISHA NINI?......

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu nashukuru kwa maswali yako.
      Kitu cha kwanza waislam tumehusiwa kufuata vitu viwili, Quran na Sunnah.
      Kwa kutumia viwili hivyo ndipo Mbora na mtukufu wa daraja (SAW) alifanikiwa kusimamisha Dola ya Kiislam. Sasa rudi kwenye sira na utizame sera ya bwana mkubwa huyo (SAW) na tizama falsafa ya mwenendo wake kutoka Makkah mpaka Madinah na hatimaye dola ya Kiislam ikasimama. Halafu rudi na utizame wanacho fanya hawa wanajihad wa CNN na FOX News na upime kwa akili yako mwenye halafu uniambie hiyo ndiyo JIHAD????
      Na uislam haukuenezwa kwa UPANGA, hizo ni misconception na propaganda zilizofanywa kazi kwa muda mrefu hata kabla ya first Crussade, na imeendelea hivyo na kuingizwa kwenye mafunzo mbalimbali na watu wameaminishwa hivyo, na sasa wanapotengenezwa watu wanao taka kusimamisha dola ya ‘kiislam’ kwa njia ya upanga vitendo vyao vinathibitisha na kutilia nguvu uongo na urongo na uzandiki waliopandikizwa watu kwa muda mrefu na hivyo kuichora picha mbaya ya dini yetu kwamba ilienezwa kwa upanga.
      Ukikwama rudi hapa tujadiliane.

      Delete
  4. In short JIHAD maana yake ni "STRIVING AGAINST EVILS" .........JE IWAPO MUISLAM NDIYE ANATENDA MACHAFU, NA WEWE NI MUISLAM, MAANA YAKE USIMKANYE??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unapaswa kumkanya.
      Swali linakuja,
      Unamkanya vipi?
      Kuna mengi ya kutizama katika hili na kuna njia nyingi za kupita katika hili, lakini kumkata ndugu yako shingo kwa sababu anafanya ‘machafu’ hilo litakuwa na mashaka yake makubwa. Labda ungefafanua ni aina gani ya ‘MACHAFU’ unayo yakusudia. Lakini kwa maarifa madogo niliyo nayo ni kuwa kwanza tizama aina ya kosa, pili kosa limefanywa na nani, na tatu kosa limefanywa katika mazingira gani, yote hayo matatu yatakusaidia katika aina ya njia inayofaa kuondoa uovu huo

      Delete