Wakati wa utawala wa Bush, ndani ya Nigeria kulianzishwa
kile kilicho fahamika kama ACRI, yaani Africa Response Initiative, lakini
taasisi hii ilikuwa kama msimamizi wa taasisi nyingine inayofahamika kama
ECOWAS au zaidi ilifahamika kama ECOMOG, kutokana na shughuli yake iliyofanyika
Liberia ya kutuliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Nigeria ndani ya ECOMOG mchango wake ulionekana waziwazi,
Nigeria iliweza kulimaliza sakata lile la Liberia bila msaada wowote kutoka
kwenye taasisi za kimataifa na mataifa ya kimagharibi wala Washington. Taarifa
za kijasusi kwenye mataifa ya Magharibi zinasema, mataifa hayo yalihofia endapo
Nigeria itaendelea kuyamaliza matatizo yake na nchi jirani kwa kutumia ECOMOG,
tafasiri yake ni kwamba, Nigeria itapata heshima kubwa ndani ya Afrika kiasi
kwamba umuhimu wa mataifa ya kikoloni eneo hilo kama vile Uingereza na Ufaransa
ukatoweka kabisa. Hivyo ushawishi wa mataifa hayo ya kimagharibi ukawa si
chochote si lolote kwenye eneo hilo la Afrika Magharibi.
Sababu Liberia ilikuwa ni matokeo ya kazi chafu za
Marekani, ingekuwa ni hatari sana kwa Liberia kuangukia kwenye mikono ya
Nigeria kwa kutumia ECOMOG ambayo ilionesha mafanikio makubwa ya kutatua mizozo
ya eneo hilo. Hivyo Marekani nayo haikuwa na budi ila kuingilia kati kuona
uchafu wake bado unaendelea kuwepo kwa faida yake. Kwa maneno mengine ushawishi
wa Marekani ndani ya Liberia nao ungefutwa na Nigeria, na maslahi ya mataifa ya
magharibi katika eneo la Afrika magharibi yangebakia kwa watu hao wenyewe, kitu
ambacho hakikubaliki katika sera zozote, kwenye zama zozote za mataifa ya
Magharibi.
Suluhisho ikaonekana ni lazima Marekani na washirika
wake, wahakikishe kuwa hali hiyo wanaibadilisha.
Ushawishi wa Nigeria kwenye
mataifa ya Afrika lazima uzikwe na ECOMOG lazima ibaki kama mbwa asiyekuwa na
meno. Lakini bila kuwashtua walio lala na kutengeneza mazingira ya chuki baina
ya Marekani, washirika wake na nchi za Afrika Magharibi ambapo ushawishi wa
Nigeria ni mkubwa, mpango huu ukaonekana utakuwa na tija zaidi kwa kutumia njia
za kidiplomasia.
Ndipo Marekani walipokujwa na kile kilicho kuja
kufahamika kama Africa Response Initiative (ACRI), lakini wakachagua nchi
mahususi za kuwauzia ACRI na Nigeria ikawekwa kushoto, sababu ACRI ilikuja
kufanya kazi ambayo tayari ilishamalizwa na ECOMOG, hivyo kwa Nigeria
isingeuzika.
Hivyo wakatafuta washirika muhimu ndani ya ECOMOG na kuwauzia ACRI
lengo ikiwa ni kuzitoa nchi hizo kwenye ushirika wa ECOMOG na hivyo kuibakiza
Nigeria peke yake. Hivyo Nigeria ikaachwa na zikatafutwa nchi zilizo na
ushawishi mkubwa ndani ya ECOMOG na kuuziwa ACRI ambayo iliahidi kuleta msaada
ya kijeshi na kibinaadam.
Wakati Marekani na washirika wake, ambao ni Uingereza na
Ufaransa wakiwauzia baadhi ya Waafrika ACRI, wakati huohuo walikuwa wakiziambia
nchi hizo kuna haja ya ECOMOG kutizamwa upya na kupatiwa mwelekeo mwingine.
Mwisho wa yote ECOMOG ikawekwa pembeni kwenye mgogoro wa
Liberia, na Marekani wakatengeneza AFRICOM kama kiranja wa mgogoro wa Liberia.
Kinyume na ilivyokuwa ACRI ambayo ilijaribu kila
lililowezekana kuficha maslahi ya Marekani ndani ya mpango huo, kiasi cha
kuzishirikisha nchi za Latin Amerika na Asia na mpaka UN, ilimradi tu, mapango
uonekane ni kwa ajili ya Waafrika wenyewe na maendeleo yao. AFRICOM ilikuwa ni
tofauti kabisa.
AFRICOM ilionekana kuandaliwa kufanya mipango na
stratejia za kijeshi kulinda maslahi ya Marekani kwenye eneo hilo dhidi ya
Wachina ambao ushawishi wao kidunia na ndani ya Afrika umefikia kwenye silingi
bodi. Ushawishi huo wa Wachina ni changamoto kubwa na kikwazo kwa maslahi ya
Marekani na washirika wake kwenye bara hili.
Ilikukabiliana na ukuaji huu wa ushawishi Wachina ndani
ya Afrika na upanukaji wa viwanda vya Wachina kwenye bara hili, ni kazi ya
AFRICOM kuhakikisha inayakamata maeneo yote ya kistartejia ndani ya Afrika na
kuyaweka kwenye milki ya Marekani ilikuweza kumzuia Mchina kuzifikia hizo
rasilimali na nishati kwa ajili ya uchumi wake unao kuwa kwa kasi ya ajabu.
KWENYE CHART HII WAKENYA TAYARI WAMESHAINGIZWA, NDIYO SABABU KAZI ZA ALSHABAB ZINARINDIMA HUKO, TANZANIA TUPO KWENYE ORODHA YA NZHI ZILIZO PENDEKEZWA.
HIVYO UTAONA MWISHO WA SIKU, ITS ALL ABAOUT BUSINESS,
HAKUNA SHAHADA, HAKUNA KALMA, HAKUNA
UISLAM, HAKUNA SHARIA, ITS ALL BUSINESS.
SOMALIA HAKUKALIKI SABABU LILE NI ENEO LA KISTRATEJIA.
PAKITENGENEZEKA PALE PWANI YOTE YA AFRIKA MASHARIKI ITAGEUKA KUWA HONGKONG YA
AFRIKA.
ZANZIBAR CHINI YA
SERIKALI YA MUUNGANO NAYO IMETULIZWA, NA SABABU ZA MSINGI ZANZIBAR KUINGIZWA
KWENYE MUUNGANO SI KWAMBA NYERERE ALITAKA, AU KARUME ALIPENDA, HAPANA SABABU
LILE NI ENEO LA KISTRATEJIA NA MAREKANI ALIONA NJIA NZURI YA KUISHIKILIA
ZANZIBAR NI KUILAZIMISHA IUNGANE NA TANGANYIKA.
KWANZA ILIKUWA IUNGANISHWE NA NCHI ZINGINE ZA AFRIKA
MASHARIKI, YAANI KENYA, NA UGANDA, LAKINI HILO LIKAWA GUMU, IKABIDI KARUME
ALAZIMISHWE KUPITIA NYERERE KUIUNGANISHA TANGANYIKA NA ZANZIBAR. TANGU 1964
MASLAHI YA MAREKANI ENEO HILI YAKAWA YAPO SALAMA.
LAKINI KUNAYO PWANI YA SOMALIA, NAO NI UCHOCHORO MZURI,
HATA KUSHINDA ZANZIBAR, TUTAFANYAJE? TUWAPE VITA, TANGU BAREKH AFARIKI MPAKA
SASA SOMALIA NI VITA MWANZO MWISHO, NA HAVITA KWISHA SABABU KUPITIA VITA HIVYO
MASLAHI YA MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE YANAHIFADHIKA.
NENDA KONGO, NENDA AFRIKA YA KATI, NENDA RWANDA, NENDA
SYRIA, NENDA LIBYA NENDA ... ... ... HADITHI NI ILEILE.
Sasa basi ili AFRICOM iweze kufanya kazi yake vyema,
inabidi nchi ambazo zimechaguliwa kama ni maeneo ya kistartejia, kwanza
zizoroteshwe ndani kwa ndani kiasi kwamba zenyewe zitambue kwamba katu haziwezi
kushindana na hali hiyo bila kwanza kupata msaada eidha kiufundi, kivifaa,
wataalam kutoka Marekani.
-
Kiufundi ni wanajeshi wako kwenda kupatiwa
mafunzo ya kijeshi ndani ya Marekani au kwa Washirika wake.
-
Kivifaa ni nchi yako kukopeshwa zana
mahususi za kijeshi kupambana na janga husika.
-
Kiutaalam ni nchi yako kuletewa
wataalam kutoka Marekani kama vile FBI
na wenzao kuja kukusaidia.
Nchi ambayo itakuwa imechaguliwa na
Marekani na washirika wake halafu wakawa wabishi kwamba hawaelewi au wanajua
sana na hawahitaji msaada wowote kutoka kwa mabwana wakubwa hao, itaanza
kutengwa huku na huko kama Zimbabwe, na kuwekewa vikwazo kadha wa kadha kama
Sudan na mwisho watatengenezwa watu wa kujifanya kuwa na mrengo tofauti na
serikali na kutengeneza vurugu baina ya serikali na watu hao kiasi cha kupaza
kelele kuingiliwa kwa nchi hiyo kijeshi na mataifa ya magharibi wakiongozwa na
Marekani kama ilivyo tokea Libya.
Tumeona kwa macho yetu hayo yakitoka kwenye nchi za
maziwa makuu, ambapo Marekani mara kadhaa imepeleka wanajeshi wake na bado wapo
Uganda na Rwanda kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya kuzilinda nchi hizo na
maharamia ambao wao Marekani wamewatengeneza. Wanajeshi hao utawakuta Somalia,
Kenya sasa mlango nao upo wazi kama itakuwa bado hawajaingia kupitia ‘CTU’ ya
Kenya.
Sudan tumeona kupitia blangeti la ‘Humantarian Aids’
lililoshonwa kwenye mashine ya Darfur ambapo Al-Bashir alishushiwa lawama zote.
Watu wa kawaida wanakuambia ni kwa sababu ya Uislamu wake, au Waarabu
hawawataki Wakristo. Sudan ya Kusini kunayo Mwarabu au Mwislamu? Mbona vurugu
ndiyo zinashika kasi?
Waafrika tuna nini sisi jamani? Sudan ya Elbashir
imetengwa na ulimwengu kutokana na kisanga hicho. Lakini hiyo ilikuwa ni kiboko
kwa Elbashir kutokana na kusaini kwake ‘Dili
la Mafuta’ na Wachina na ‘kuzipotezea’ kampuni za Marekani. Hakuna ishu ya
Uislamu hapo, wala Shariah, wala Uarabu, ishu ni nani kapata nini, na Mchina
hatakiwi Afrika na Obama hiyo ndiyo jukumu lake kubwa alililogewa wakati
anaachiwa ofisi na Bush.
Kwa mchezo huohuo tumemuona Gaddafi wa Libya akipotozwa.
Ishu ilikuwa na bado inaendelea kuwa ni mafuta hakuna cha udikteta wala utawala
bora, mafuta kwanza. Lakini zawadi kubwa kabisa kwa AFRICOM na malengo lake
mahususi ni kujenga dola ya Marekani ndani ya Afrika, PAX AMERICANA IN AFRICA.
Libya hayupo, nani kabaki Afrika? Mwenye jeuri kama
Libya? Mwenye utajiri na kiburi cha rasilimali na nishati muhimu kama Libya?
Hapana shaka ni jina moja tu ndilo litasimama kwenye kinyang’anyiro hicho;
NIGERIA. Hapo ndipo umuhimu wa BOKO HARAM ndani ya NIGERIA UNAPO ONEKANA.
WAKATI WEWE UNASHABIKIA KWAMBA NI SAWA HIVYO, ATI WANASIMAMISHA DOLA YA
KIISLAM, ATI WANASIMAMISHA SHARIAH, ATI ... ... ... ADUI YAKO MBAYA KULIKO WOTE
ANAWATAWALA NYOTE WEWE NA BOKO HARAM.
HII INANIKUMBUSHA KISA CHA NG’OMBE
ALIYELIWA NA SIMBA NA HUKU AKIPIGA KELELE KUWA ‘NILISHALIWA TANGU SIKU YA KWANZA NILIPORUHUSU MWENZANGU KULIWA.’
AFRIKA, WAISLAM KWA UJUMLA
TULISHAMALIZWA PALE TULIPO RUHUSU VIJANA WETU KWENDA KUPIGANA ‘JIHAD’
AFIGHANSTAN ... HAIKUWA ‘JIHAD’ ILIKUWA JUHUDI YA MAREKANI KUSIMAMISHA KITI
CHAKE CHA UTAWALA DUNIANI, NA LEO
WANAENDELEA NA MCHEZO HUOHUO KWA KUTUMIA
VIKUNDI VYA KIISLAM NA SISI TUNASHABIKIA, LAKINI TUTAKAPO GEUZA NYUSO ZETU NA
KUTAZAMANA USO KWA USO NA ADUI YETU ...
KAZI YA BOKO HARAM
Tangu Oktoba 2010 mirindimo ya mabomu imekuwa ikisikika
ndani ya Abuja, kutoka kwenye majengo ya serikali, taasisi za elimu, maeneo ya
wazi na kwenye mikusanyiko ya watu na kuuwa takribani watu 15,000 na mauaji yupo
huru kila akijisikia anatoa vidio yake na kuuambia ulimwengu kile anacho
jisikia kuambia.
Serikali ipo, inayo majeshi, vifaa, mbinu na pesa, lakini
haijaweza kufanya chochote mpaka Aprili 14 wanafunzi zaidi ya 300 wakatekwa na
Boko Haram na kutokomea nao kusiko julikana. Sasa ni kama dunia nzima imeamka,
turudishieni, turudishieni, turudishieni mabinti zetu ndiyo habari zinazo pamba
vyombo vya habari.
Kama kawaida Boko Haram wakafetua albamu yao inayo sema
hawatawarudisha kamwe mpake wapatiwe wenzao waliokamatwa na serikali, albamu
hii nayo imeuza sana kutoka kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, kitaifa,
magazeti na hata mitandao ya kijamii.
Watu tunajiuliza ni nani hao Boko Haram, wanacho taka
nini? Vipi kwa muda wote huo serikali imeshindwa hata kufahamu makazi yao, sura
zao? Mohammed Yussuf, kiongozi wa kundi asiye na maarifa na mbinu za kijeshi,
kufumba na kufumbua anaikimbiza Nigeria yote na serikali yake mchakamchaka.
Mbinu hizi za hali ya juu za kutega mabomu, kuteka watu nyara, kulipua majengo
makubwa na kutoweka bila kuacha hata unyayo wake kajifunzia wapi? Ametolea wapi
silaha hizo nzito za kivita? Anatolea wapi fedha za kuwalisha wanamgambo wake
kiasi wasiweze kumsaliti?
Maswali ni mengi, mazito si ya kudharaulika na wala
hayahitaji majibu mepesi.
Tafiti zinatambulisha kuwa, kazi inayo fanywa na Boko
Haram kwa sasa ni shughuli kivuli za CIA ambazo zinaratibiwa na ubalozi wa
Marekani ndani ya Nigeria.
Kwa kipindi sasa CIA wamekuwa wakiendesha kambi za siri
za mafunzo na kuwafunda dhana za wahabisim and new salafisim kwenye vichochoro
vya mipaka ya Niger, Chad na Cameroon. Katika kambi hizi vijana kutoka kwenye
familia masikini, kutoka kwenye tabaka lililo tengwa na kunyimwa fursa
mbalimbali na wakati mwingine vijana hawa ni wale wahanga wa mihadarati
mbalimbali na hivyo akili zao hazifanyi kazi vizuri, vijana hao ndiyo walengwa
wa kambi hizi, ambapo hapo mbali na mafunzo ya kivitendo, watapatiwa tafsiri na
maelezo ya Quran na Hadithi kutoka kwa wakufunzi wa CIA wenye asili ya
Mashariki ya kati, lakini mafunzo hayo si chochote zaidi ya kazi mahususi
zilizokuwa zikitumika tangu miaka ya mwisho ya 70 na 80 kuwaandaa vijana kwenda
kwenye Jihad ya Afghanistan. Tafsiri hizo ni kinyume kabisa na mafunzo ya Quran
na Sunnah na hazihusiani na chochote katika kuihuisha Uislamu, bali
kuuporomosha na wakati huohuo kuyalinda maslahi ya Illuminanti, a.k.a Marekani
na washirika wake.
Mkufunzi wa kazi hiyo anawatengeneza vijana hao kuamini
kuwa kazi inayo fanywa ni ya Allah kwa ajili ya kusimamisha dola ya Kiislam, na
Allah atawalipa malipo mazuri sana kwa juhudi hiyo waliyo jitolea. Baada ya
miezi kadhaa ya mafunzo ya kivitendo, namna ya kushika na kuitumia silaha,
mbinu za kijeshi na kivita, uvamizi na kujilinda, dhana za kifikra na mtazamo
wa Wahabisim na Salafisim, vijana hao wanakuwa wameiiva na sasa wanawekwa
tayari kwa hatua ya pili ya operesheni hiyo.
Hatua ya pili inahusisha na kutambua na hatimaye kuchagua
maeneo yanayo lengwa kwa ajili ya mashambulizi. Jengo ambalo linakuwa
limechaguliwa kwa ajili ya mashambulizi hayo, silaha na zana zingine
huwasilishwa hapo mapema na kuhifadhiwa kwenye chumba mahususi kusubiri wakati
wa tukio.
Tukiwa tunahesabu masaa kadhaa kabla ya tukio, kijana
aliyeandaliwa kwa shughuli husafirishwa na kwenda kuhifadhiwa kwa takribani saa
moja kwenye nyumba/chumba maalum karibu na eneo la tukio.
Baada ya shambulizi na wakati watu wameingiwa na wazimu
wa shambulizi ‘gaidi’ wetu anakimbilia kwenye nyumba ileile aliyokuwa awali
kabla ya shambulizi, huko anaziharibu zana na vifaa vilivyotumika kwenye
shambulizi kufuta ushahidi wa wapi silaha hizo zimetokea, hii ndiyo sababu hakuna
chochote polisi wa nchi husika wanachopata kuhusiana na aina gani ya bomu
lililotegwa, malighafi za bomu hilo ni kutoka nchi gani hakuna. Baada ya
kuziharibu zana hizo ‘gaidi’ anajichanganya na watu walio changanyikiwa
kutokana na mlipuko na kutokomea anapo pajua.
Hatua ya tatu baada ya hapo ni kutuma taarifa kwenye
vyombo vya habari kwa kutumia barua pepe, ujumbe mfupi wa simu ukiwa na jina la
Boko Haram/ Alshabab/Al Qaedah n.k ndiye waliyo fanya shambulizi hilo. Hatua
hii ya tatu hufanywa na mtaalam na mkufunzi wa mawasiliano ambaye anaweza kuwa
ni CIA au afisa wa Marekani mwenye dhamana na ‘project’ hiyo. Mtaalam huyo
hutumia vyombo vya kisasa vya mawasiliano ambavyo ni vigumu kuweza kufuatilia
nyayo zake.
Ikiwa bomu limelipuliwa kwa njia ya mlipuaji kujitoa
muhanga, kinachofanyika kinafahamika kama ‘MIND CONTROL PROGRAMME.’ Hili ni
darasa la aina yake, na kijana aliyeandaliwa kwa ajili ya kujitoa muhanga
huandaliwa kwa zaidi ya miezi 6, mwaka na hata miaka, tizama filamu inayokwenda
kwa jina la Munchiria Candidate kupata mwanga
kidogo wa kile ninacho zungumzia hapa. Siku zote wale wanaojitoa muhanga
hufanya kitu hicho bila kuwa na hata chembe ya kufahamu ni nini anachokifanya,
huwa kama robota la kibinadam, hii ni moja ya taaluma mbaya na inayo gofia na
silaha mahususi kwa Illuminanti, mkufunzi wa ‘MIND CONTROL SLAVERY’ huwa na
kitu kinacho tambulika kama ‘MULTIPLE PERSONALITY DISORDER’.
Huenda siku moja
tukalizungumzia somo hilo matata.
Nigeria kwenye mpango huu utakao kamilika 2015 inatakiwa
iwe chakari na si chochote si lolote kama ilivyo Pakistan leo. Moja ya taifa
kubwa na lenye nguvu za kinyuklia imegeuzwa kuwa kama mwanasesere kwenye jukwaa
la kimataifa; kuondoa uwezekano wa Nigeria kuwa ni kwakozo kwa maslahi ya
Marekani na washirika wake barani Afrika, haina budi kupigishwa magoti kama
ilivyofanya Pakistani kupitia kwa Al Qaedah na Talibani. Lakini kwa Nigeria,
mwenye zamana hiyo ni Boko Haram. Hatua tatu mahususi zimependekezwa kuifikisha
Nigeria hapo.
HATUA YA KWANZA.
Hatua ya kwanza ni kujenga mgawanyiko baina ya Wanigeria
wenyewe kwenye misingi ya UISLAM na UKRISTO. Mabomu na mashambulizi ambayo
yatakuwa yakiwalenga watu wenye imani mahususi hivyo kupalilia chuki baina ya
wafuasi wa imani hizo mbili. Utaona mabomu hayo yakilipuka kwenye makanisa na
pia kwenye misikiti na pia kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu wa imani hizo
mbili.
Kutakuwa na majibizano na maneno ya kujikweza kama
wanavyo fanya Boko Haram kila baada ya shambulizi kutokea. Hili litapelekea mauaji
ya wenyewe kwa wenyewe kwenye misingi ya kidini. Nchi itakapo fikia hapo
itakuwa iko uchi kwa yeyote kuingia eidha kwa jina ‘HUMANTARIAN AID’ au ‘WAR ON
TERROR.’ Vyovyote itakavyo kuwa hilo ndilo lengwa stahiki na lililokuwa likisubiria
kwa muda mrefu.
HATUA YA PILI.
Hatua itakayo fuatia ni kupiga ukunga kwa dunia nzima na
kusema kuwa Nigeria inamalizika lazima tufanye kitu pale. Sababu nchi itakuwa
imechanwa chanwa vipande vipende kwenye misingi ya kidini na kila ina ya
mgawanyiko na ubaguzi, na mauaji yake yatakuwa hayana kanuni wala taratibu,
ukunga utapigwa kutoka Marekani a.k.a Washington, kutoka European Union na
kutoka United Nations ukiitaka dunia kuingilia kati suala la Nigeria.
Hatua hii imeshaanza kufanyiwa kazi kwa upande mmoja,
viongozi mbalimbali wa kidunia wamepiga picha wakiwa na mabango yanayo dai
mabinti wanao shikiliwa na Boko Haram warudishwe.
Hali ikichachamaa kiasi kila mahala kuna maiti ya huyu na
yule kama tunavyo ona CAR, vikao vya dharura vitaitishwa na nchi washiriki na
hapa nikimaanisha nchi za Ulaya na Marekani pamoja na mwanasesere wao anayeitwa
UN, na mara moja vikosi vinavyo kwenda kwa jina la ‘Humantarian Aid’ vitaanza
kumiminika Nigeria, halafu wanajeshi wa kulinda amani kutoka nchi fulanifulani,
halafu ahadi wa msaada wa zana za kijeshi kwa serikali ya Nigeria, tahamaki
nchi yote iko chini ya ‘wageni.’
HATUA YA TATU.
Baada ya Marekani kujiweka kwenye kona nzuri ya
kuzinyonya rasilimali za nchi hiyo bila kuingiliwa na Mchina, aliye mpinzani
wake mkubwa leo, sakata hili sasa atarudishiwa mwanasesere UN, ambapo midahalo,
vikao na majadiliano yatakuwa yakifanyika katika kuipatia UN nafasi ya
kusimamia na ‘kutatua’ tatizo hilo. Kuna maeneo ambayo yatawekwa chini ya UN
kwa ajili ya uangalizi na kupambana na magaidi, wakati nchi washirika nao kuna
maeneo yao mahususi ambayo walikuwa wakiyahitaji tangu awali, watayakalia
maeneo hayo kwa kutumia vikosi vyao, na hivyo ndiyo itakayo kuwa historia mpya
ya Nigeria.
Muda utakapo fika sasa Nigeria irudishwe kwa wananchi
wake, nchi washirika tayari watakuwa wameshamuandaa kibaraka wao, kama walivyo
fanya Afghanistan na sehemu zingine, na kibaraka huyo ataiongoza nchi kama
wanavyo taka mabwana wakubwa wakiongozwa
na Marekani. Atakaye nufaika na utaratibu huu, si Afrika wala Nigeria, bali ni
Marekani na washirika wao ambao ndiyo waliyo tengeneza zogo hili tangu mwanzo.
Mchina atakuwa kaekewa fullstop kutia
mguu wake hapo , na Marekani itakuwa
imejiweka kwenye sehemu nyingine ya kistartejia kwa maslahi yake ndani ya
Afrika na kutengeneza njia ya kuunda Pax Amerika ndani ya Afrika.
Mwisho wa siku, hakuna Jihad, hakuna Shariah, hakuna dola
ya Kiislam wala Uislam. Mwisho wa siku kuna Marekani na maslahi yake, na sisi
wengine wote ni wanasesere tunao chezeshwa viungo vyake na kuvichezesha kama
wanavyo taka mabwana wakubwa.
Kulingana na yote hayo, na wewe uliye na akili huru,
swali la msingi la kujiuliza ni vipi taarifa kama hizi ziwe uchi kwa kila mtu
kuona? Au viongozi wa Nigeria na Afrika kwa ujumla pamoja na wakazi wake
tunaandaliwa kisaikolojia kukubaliana na hali inayo tokea na kujihesabu
hatuwezi kufanya chochote kinyume na mpango huu unao simamiwa na mataifa
makubwa duniani?
Katika utaratibu wowote wa utafiti, ushahidi usio na
shaka huwekwa mezani sambamba na tafiti hizo. Je kauli ya Marekani ya kuichakachana
Nigeria kabla ya 2015 haiwiani na kile ambacho Nigeria leo inakishuhudia
kupitia mirindimo ya mabomu na risasi mahala ambapo kabla palikuwa ni shwari na
salama?
Kwanini nchi ambayo hapo kabla iliweza kutatua matatizo
yake yenyewe, bila ushirika wowote wa kimataifa, na hata kutatua matatizo ya
nchi jirani kama Liberia leo imegeuzwa kuwa mwanasesere na kituko kwenye jukwaa
la kimataifa?
Je wananchi milioni 160 wa Nigeria watasimama pembeni na
kuwaachia Marekani waifanye nchi yao kama walivyo ifanya Libya, Iraq, Afghanistan,
Syria, Egypti, Latini Amerika na kwengineko? Ambako kote huko rekodi ya taifa
hili jeuri na lenye kiburi imekuwa ni chafu na mbaya kurekodiwa kwenye vitabu
huru vya historia.
Huu ni
mtihani kwa Wanigeria, na somo kwa Waafrika wote.
DAAH embu tueleze na kuhusu westgate tutapona kweli
ReplyDelete