Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Thursday, May 15, 2014

WASHINGTON NYUMA YA BOKO HARAM

WAKATI UKIPITIA POSTI HII NA MFANO WA HIZI NAKUOMBA UTAFAKARI MANENO HAYO YA PLATO.

Guys!

Nasikitika mwendelezo wa posti ya ‘PICHA ZA UCHI NA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME, utaendelea baada ya posti moja au mbili za KISANGA CHA ‘BOKO HARAM’,
Umma umekuwa katika kiza na lindi la ujinga kiasi ambacho hatuwezi kutofautisha katika ya KIZA na NURU. Haidithi ya Boko Haram na zingine mfano wake ni mfano hai juu ya maneno ya mtukufu wa daraja (SAW) aliposema zama karibu na Kiyaam, watu watakuwa WAJINGA MNO. Muumba atuhifadhi na hali hiyo.

Najiuliza ni kipi wanacho fanya Boko Haraam kinaonekana ni cha Kiislam kiasi waumin wa kiislam kusimamia kidedea jambo hilo na kuliunga mkono kama ni la kwetu? Ni kama vile waislam tunacheza MUZIKI USIO WA KWETU na huku tukijinasibu na kujisifia kana kwamba ni  wa kwetu na unavionjo na ladha ya kiislam. Si kweli. Lakini yapi maarifa yetu mpaka tunafika hapa na kuwashabikia Alshabaab na akina Boko Haram?


YES! MADAM NA YEYE KAGUSWA!!  UKISTAAJAB YA MUSA UTAONA YA FIRAUNI.

Maswali hayo ndiyo yaliyonisukuma kuandika posti.

Kikundi cha Kigaidi kilichopo Nigeria, kimekuwa kikiongoza kwenye vichwa vya vyombo vya habari kote Ulimwenguni. Habari kuhusu Syria zimezikwa, Iraq kimya, Afighanstan hakuna, sasa wimbo unaoshika chati na kuuzika kwenye vyombo vyote vya habari ni BOKO HARAAM!

Zi wapi akili zetu, sisi tulioitwa kwenye Quran karim kuwa WATU WENYE KUFIKIRI, WATU WENYE AKILI, na mfano wa hayo, mbona tunacheza muziki usio kuwa wa kwetu?

MTIZAME NA SILAHA YAKE NZITO NA KICHWANI AMEWEKA ANUANI YAKE KUWA YEYE NI NANI. LAKINI NI KWELI HIYO ANUANI ALIYOIVAA KICHWANI NDIYO INAMUONGOZA KUFANYA HIVYO, AU NI AJENDA ZA WASHINGTON NDIZO ZINAZOMUONGOZA?

Wimbo huu wa Boko Haraam unatofautiana gani na wimbo wa 9/11, wimbo wa Iraq, Afighanstan, Alqaeedah na wengine?

Bila maarifa na mbinu zenye kufahamika za kivita, kikundi kidogo cha Boko Haraam kimeweza kuteka watoto wa kike wapatao 300 kutoka shule iliyopo Chibok, April 14 mwaka huu.

Muda ambao tukio hili limetokea, na muda ambao vyombo vya habari vimekuja kuliripoti ni kama filamu za kuigiza kutoka Hollywood, karibu mwezi mzima ndiyo dunia inajua kwamba Boko Haraam wameshafanya mambo! Jamani hii ni kweli?

Dengu imezuka tu hapa kwetu, lakini sasa kila mtu anajua kuna ‘dengu’ Tanzania, lakini watoto 300, mwezi unaisha ndiyo dunia inafahamu jamani mi hainiingii akili hata kidogo.

Washington nadhani walikuwa bizzzzz sana kuzinyaka hizi nyuzi, lakini siunajua kwamba Obama safari hii yupo Bize sana na Urussi kule ..., halafu kuna zoezi la kugawa na kusambaza silaha kwa vikundi vya kiislam kote duniani kuendeleza vita vya kigaidi, halafu si unajua kuna ile ishi ya ndege iliyopotea ... ha ha ha dunia leo inayo vioja kama siyo viroja, ishu ya ndege nitakuja nayo soon tu, siamini kwamba kwenye uso huu wa dunia ndege inaweza potea, ajabu sana, sana, sana ..... any way tuendelee na mtanange wetu wa Boko Haraam.
KILEMBA KIKUBWA, MSWAKI WA MTI, NDEVU NYINGI, VYOTE HIVYO VINAKUAMBIA YEYE NI NANI, LAKINI NI KWELI YEYE NDIYO HUYO AU ANATUMIA MAVAZI YETU KUIPOTOSHA DINI YETU?

Lakini yote juu ya yote, FBI tayari wapo ndani ya nyumba kututatulia jambo letu, maana askari wa kila nchi na majeshi yao hawajafanya kazi yao ikakamilika kama FBI hawajaalikwa.

Lakini kama kweli FBI wanataka kutambua ukweli wa tukio zima, nadhani wangeanzia Washington ambapo, kwa muda mrefu jina la Boko Haram kwa sababu zisizo weza fahamika haraka hawakuingizwa kwenye orodha ya kikundi cha kigaidi pamoja na yote waliyo kuwa wakiyafanya.

Halafu zikaja habari zingine kuwa zaidi ya wasichana 50  wamefanikiwa kutoroka kwenye mikono ya Boko Haram na zaidi ya wasichana 200, bado wapo nao.

Bado sijapata data wasichana hao wametorokaje na nini walicho shuhudia walipokuwa kwenye mikono ya Boko Haram, nadhani watakutanishwa na FBI iliwaanze ‘kushoot’ vidio za namna walivyo toroka na urongo mwingine halafu waturishie kupitia BBC na CNN.

Kama ilivyo tabia ya vikundi vingine vya kigaidi mfano wa hivi, Boko Haram nao wapo kwa ajili ya kusimamisha dola ya Kiislam, a.k.a Sharia Law na mipango yao ni Nigeria, Cameroon na Niger. Shughuli kubwa ni kuuwa waumini wa Kikristo, kuwafanyia ugaidi, kulipua makanisa, majengo ya serikali, kuteka watalii kutoka nchi za magharibi, na lingine kwenye orodha na ingawa si la mwisho ni kuwashambulia waislam wenzao ambao wanao msimamo tofauti na wao, na sasa naona wamejiingiza kwenye biashara ya kuteka watoto. Ofcourse BBC Swahili wanatuambia wasichana wote walio tekwa sasa wamesilimu na walionekana wakisoma Quran na kushikilia bango lenye maneno ya Kalima tawhiid. Likini BBC wakapiga kimya kutuambia katika waliokamatwa wamo pia Waislaam.
WALIO KAMATWA HAO, HAPO WANAOMBA 'DUA' PICHA HII INANITIA MASHAKA MENGI, MOJA WAPO NI NAMNA BINTI HAWA WALIVYO TULIA, YAANI WAMERIDHIIKA KABISA NA DUA WANAOMBA, MH! OOOOH BBC WALITUAMBIA KUWA WOTE WAMESILIMU, DUH!

Nigeria ni moja ya nchi tajiri mno barani Afrika, tajiri wa mafuta, lakini kama yalivyo mataifa mengine barani humu nalo limegawanywa kwenye misingi ya kidini, kikabila kwa malengo mahususi. Makampuni kama BP, Shell, na Chevron wanavuna mafuta kama hawataki vile, na ili waendelee kufaidika na hili lazima Nigeria ibaki kwenye migawanyiko na kila wakati pawepo na lile la kuwa shughulisha, na leo ni Boko Haram.

Boko Haram haifanyi hayo kwa faida ya Uislam na Waislam, bali kwa faida ya Illuminati na ajenda zao. Nigeria likidorora kiuchumi, kisiasa, na kila wakati ikiwa bizz kushughulika na Alqaeeda na Boko Haram, Illuminanti wanaendelea kuingiza majeshi yao kwa kisingizio hichohicho na kuendelea kuitawala na kuinyonya.

Moja ya malengo makubwa ya US na NATO chini ya utawala wa kibaraka mweusi anayeitwa Obama ni kuhakikisha kuwa Marekani na washirika wake wanawekeza kijeshi katika bara hili kwa kuingiza majeshi yao hasa, kwenye hili tumeona story ya Rwanda na Afrika ya kati, tizama posti hii http://salimmsangi.blogspot.com/2014/01/malighafi-za-afrika-na-damu-ya-waafrika.html  

Mpango huu ulianza tangu wakati wa utawala wa Bush, 2007.
Waweza pitia dokumenti hii kupata undani wa habari yenyewe, http://www.africom.mil/downloadCenter.asp 

Lengo la mpango huo ni upi basi?

Mchina hatakiwa Afrika, It all about Power and Enomics, 

HAKUNA ISHU YA SHARIAH WALA UGAIDI, ITS ALL ABOUT POWER. SI MUZIKI WETU HUU ...

Kwenye muswada huo Washington walikuwa na bado wanahofia kwamba Mchina na yeye ataleta majeshi yake kwa ajili ya kulinda maslahi yake Afrika, ilikuondoa uwezekano huo, lazima wao watengeneze mazingira ya wao kutia mguu kwanza, Boko Haram, Alshabab, na vikundi vingine vya kigaidi ndani ya Afrika vitarahisisha hilo. 
BUSINESS HOUR AS USUAL


Nato na US wapo Libya, lakini sote tunajua wamefikaje hapo, wapo pwani ya Somali, tunajua wamefikaje hapo, na sasa FBI wapo Nigeria, hutasikia lini wanaondoka, lakini utasikia lini wanaongezwa wengine. FBI watakuwepo na Boko wataendelea kurindima kama kawaida.

Lakini kuna anaye fahamu zaidi ya Washington kwamba ukitaka kuingiza majeshi yako sehemu fulani ufanye nini? Washington wanajua ukitangaza kuna gaidi kona fulani, hakuna atakaye kuuliza chochote endapo utaamua kuweka kambi mahala hapo. Vikundi vya kigaidi Afrika vimekuwa kama migawaha ya Mcdonald au kinywaji cha Coca Cola. Kila kona utazikuta bidhaa hizi, lakini watengenezaji ni tofauti kutoka kona moja ya dunia kwenda nyingine, isipokuwa LADHA YAKE NI ILEILE. Wenyewe wanaiata ‘FRANCHISE BUSINESS’.

Ugaidi nao umekuwa franchise, mfano Boko Haram sasa ni jina la kibiashara, kama ilivyo kwa Alqaeedah, si unajua Alqaeedah baada ya Afighanstan, wakawa na maajenti, Afrika, Marekani, Ulaya, na nchi za Asia, yesss, its all about business. Ndani ya Nigeria kwenyewe kuna zaidi ya Boko Haram 5, kumbuka Franchised Business. Swali la kujiuliza ni nani anayetoa mtaji?

Tutakuja huko.

Kitu kimoja ambacho uongozi wa Obama umefanikiwa kwa kiasi kikubwa ni kugawa na kutawanya silaha kila pale zinapohitajika kupitia mawakala wake mbalimbali. Eidha ni Mexico kwa wauza unga, Libya kwa wanamapinduzi, Syria kwa ‘Free Army of Syria, Somalia kwa Alshabaab, Algeria na Mali kwa Alqaeedah, hapana shaka imekuwa ni business nzuri kwa Washington na mashirika ya silaha duniani.
KILA MTU ATASHIKA BANGO HILI, SUBIRI TU, SOON UTAWAONA VIONGOZI WA KITAIFA NAO WAKIANZA KUSHIKA BANGO HILO. LENGO NI KUKUSHIKA KIAKILI NA HIZO PROPAGANDA NA KUSAHAU KUWA ADUI NA HUYO ANAYESHIKA BANGO WOTE LAO NI MOJA.

Wakati NATO walipokuwa Libya, kulikuwa na watu waliofahamika kama Libyan Islamic Fighting Group ambao nao wakajiunga na tawi la Alqaeedah lilipo hapo Libya, na makundi yote mawili chemchem yake ni miaka ya 80 ambapo Washington walikuwa wakimuondoa Mrusi kwenye U-Super Power. Sasa Washington wameuza leseni ya ugaidi kwa Boko Haram katika mtindo ule ule wa Franchise business.

Wakati wa mahojiano na kiongozi wa Alqaeedah kwenye tawi la Libya, Abu Mousab Abdel Wadoud, kiongozi wa kundi hilo, alisema kuwa kundi lake hilo linatoa mchango wa silaha kwa Boko Haram ililiwaze kuwalinda waislam wa Nigeria. Utakumbuka kipindi fulani nyuma Alshaabab nao walisema wameungana na Alqaeedah kwa madhumuni hayohayo. Lakini mimi sina shaka na madhumuni yao, shaka yangu na kwa Washington ambao ndiyo wanao viunda vikundi hivi na kuhakikisha kuwa vinaendelea kuwepo.

Washington wanafahamu kuwa hawawezi kuimba ALQAEEDAH, ALQAEEDAH, miaka nenda rudi, wataonekana ni wendawazimu kwamba hawezi kuwashinda jamaa hao, sasa wafanyaje, tufanye Franchise kwenye business ya ugaidi, ndiyo sasa ukawaona kina Boko Haram, Alshabab, Free Syria Army, n.k.

Unapo watizama mawakala hao wa Washington waliopewa leseni ya kufanya ugaidi utaona kazi zao kubwa ni kuzorotesha nchi husika kiuchumi, kiulinzi, kisiasa na kijamii na kujenga migawanyiko na matabaka baina ya wananchi husika kiasi nchi haiwezi kukalika tena mpaka Washington na washirika wake watakapo ingia na ‘kuiweka’ nchi sawa.


Kwa uchache mawakala hao wenye leseni za kufanya hivyo kutoka Washington ni:-

-        Boko Haram leseni yao inawaruhusu kufanya kazi yao Nigeria, Niger, na Mali.
-        Alshaabab leseni yao ni Somalia na Kenya.
-        Al Qaeedah in Islamic Magreb (AQIM) hawa ni Algeria na Mali.
-        Musilim Brotherhood hawa ni Egypt.
-        Libyan Islami Fighting Group hawa ni Libya.
-        Al Qaeedah hawa leseni yao ni dunia nzima.
-        Majina hayo kwa uchache lakini yapo mengi mno.
Waweza pitia mitandao ifuatayo kwa undani wa habari hii.
http://www.theguardian.com/world/feedarticle/11322064 

WikiLeaks revealed that they are part of the US Central Inteligence Agency: 
http://imnig.org/boko-haram-cia-covert-operation-%E2%80%93-wikileaks
http://www.washingtontimes.com/news/2013/nov/13/us-designates-boko-haram-terrorist-organization/?page=all 


UMEELEWA KIKARAGOSI HICHO. ? TAFAKARI TILL NEXT TIME

No comments:

Post a Comment