Porno kwenye mtandao si sawa na picha za Playboy.
1. Picha za uchi kwenye
mtandao zinasisimua kingono zaidi kuliko picha za kwenye majarida. Hii ni kwa
sababu picha za uchi kwenye mtandao zinakila aina ya kile ambacho unaweza
kufikiria kuhusiana na suala zima la ngono. Mtazamaji wa picha za uchi kwenye
mtandao anazama katika kila aina ya uchafu wa kutisha na kugofua ambao
anaufikiri.
2. Yeyote anaweza kuwa ni teja wa picha za uchi kwenye mtandao.
Wengi kati ya wale ambao ni waathirika wa picha za uchi kwenye mtandao
hawana historia ya kuwa ni teja wa aina nyingine ya kilevi au mihadarati. Ni
watu wa kawaida tu, na wengine wenye mafanikio kimaisha au hata kiroho, na
walianza kutizama filamu za uchi na kila muda ulivyo zidi kwenda ndivyo
walivyozidi kuzama kwenye shimo hilo. Na walipo acha kutizama filamu hizo hali
zao zilirudi kawaida.
3. Kufahamu ni namna gani matumizi ya picha za uchi yanaathiri ubongo ni
muhimu sana ilikuweza kujitoa kwenye janga hilo.
Unapofahamu ni namna gani ubongo wetu unafanya kazi ni muhimu na kukusaidia
anapotaka kuchomoka kwenye uteja wa picha za uchi.
Kinachotokea kwenye ubongo wako nini pale unapokuwa ni teja wa picha za
uchi mtandaoni?
Kwanza filamu hizo za uchi zina sisimua ubongo wako zaidi ya maumbile ya
kawaida yanavyo weza kufanya na ubongo wako nao unabadilika kukubaliana na hali
hiyo kama ndiyo njia sawasawa ya msisimko wa ngono. Kuwa teja kunafika pale
ambapo ubongo wako umeshabadilishwa kiasi kikubwa na kutambua mazingira hayo kama
ndiyo sahihi kwa ngono.
Mabadiliko hayo ya ubongo ndiyo yanayotengeneza mnyororo mgumu wa kuwa teja
ambao unakuwa ni vigumu kuukata kila unapotaka kuacha, lakini mbaya zaidi
unaimarika kila pale unapotizama filamu hizo.
Hivyo utaona basi kile ambacho unakiona kwenye picha za uchi ni msisimko wa
ajabu kwenye ubongo wako ambao hauwezi kufikiwa kwa kutumia maumbile ya
kawaida.
Maisha yako ni Ubongo wako.
Sheria # 1 – Lazima niishi, hivyo ubongo unafanya kazi na mbinu na mipango
ya namna gani uishi, kusanya chakula, kula ina fulani ya chakula, kusanya kingi
huwezi jua ya kesho.
Sheria # 2
Pata watoto, ongeza ukoo, acha alama yako duniani, kopi yako n.k.
Miaka 100 iliyopita nafasi ya mababu na mabibi zetu kukutana na watu wa
jinsia nyingine ilikuwa ni ndogo sana, na pia kukutana kwa ajili ya tendo la
ndoa nayo ilikuwa ni ndogo zaidi.
Lakini muathirika wa picha za uchi ndani ya muda wa saa moja anaweza
kuwaona wanawake au wanaume wa sifa anazo taka, wakifanya aina ya ngono
anayotaka zaidi ya 100.
Katika mazingira hayo ubongo wa muathirika wa picha za uchi nao
unabadilika, unaona picha za uchi na yale yanayo fanyika ndiyo ukweli halisi wa
maisha, LAKINI OLE WAKO, SIYO UKWELI HALISI HATA KWA NUKTA MOJA.
SHE IS HOT!!! BUT IS SHE REAL?
Sehemu ya ubongo inayohusika na kujamiiana inakuwa haiwezi kufanya kazi
yake sawasawa bila picha za uchi ... shida inaanza ...
Ubongo unapoathirika, unakuwa hutosheki na kile unacho kiona, kila siku
utataka kutizama mcheza picha za uchi mpya, mwenye staili tofauti n.k. Kadiri
unavyozidi kuzama huko na mguso wa ngono kwenye maumbile halisi au kwa mwenza
wako nao unatoweka, mwisho wa siku uume wako hauwezi kusimama mbele ya mke wako
sababu UBONGO WAKO UNAYO PICHA ‘MATATA’ ZAIDI YA MWANAMKE WA KUFIKIRIKA KWENYE
MTANDAO AMBAYE ANAFANYA MAMBO YA KISHENZI YA KUFIKIRIKA, NI KWA MWANAMKE HUYO TU
NDIYO UBONGO WAKO UTAWEZA KUSIMAMISHA UUME WAKO!
HAPO NDOA INAINGIA UFA.
SOMEBODY HELP MEEEEEEEEE!!!!!!!
Hivyo basi utaona tatizo la kupoteza nguvu za kiume baada ya kutizama picha
za uchi sana, si tatizo la viungo vyetu vya uzazi, bali ni tatizo la kwenye
ubongo wetu. Ubongo umeathirika na picha za uchi.
Katika ubongo wetu kuna sehemu moja mahususi inafahamika na kazi za viungo
vya mwili, maarufu kama ‘limbic system’ katika picha hiyo hapo chini sehemu
hiyo imezungushiwa rangi ya chungwa. Wanyama wote aina ya ‘Mammal’ wanatumia au
wanayo ‘limbic’ katika bongo zao.
Ubongo ni mmoja lakini, kila sehemu ya ubongo hiyo inayo kazi yake
mahususi, na sehemu hiyo ya ‘Limbic’ ndiyo inayohusika na sheria # 1 ya ubongo.
‘survival’. Sehemu hii ndiyo inayo tawalia mambo ya hisia, kama vile woga,
furaha, huzuni n.k. Lakini pia ni sehemu ambayo hamu na msisimko wa kitu fulani
hutawaliwa hapo kama vile njaa, kuchagua mwenza na suala zima la ngono. Hamu
yako ya ngono haitokei kwenye viungo vyako vya uzazi, bali kwenye ‘limbic system’
ndani ya ubongo wako. Sehemu hii ndiyo inayohusika na wewe kupata ashki na
hatimaye uume wako kusimama, na hapo ndipo pahala ‘addiction’ zote zinapo tokea
ikiwemo hii ya picha za uchi.
Mfumo wa utendaji wa ‘limbic systeam’ ni kukwepa maumivu au kuzia maumivu
yasitokee na wakati huohuo kurudia lile lenye kuleta raha. Kuishi kunategemea
na kukwepa majanga yatakayo kuletea maumivu kimwili na kisaikolojia, lakini na
wakati huohuo, ni kupita kwenye njia ile ambayo itakuletea raha na furaha.
“Moto, mbaya; aiskrimu tamu; Mama safi; nyoka mbaya; picha za uchi safiii.”
Unanipata mpaka hapo?
Moyo wa limbic unafahamika kama ‘reward circuit’(rc), tizama picha hii hapo
chini. Utaona kwenye picha hiyo RC inatoka kwenye limbic na kwenda kwenye
sehemu ya ubongo inayofahamika kama cerebral, sehemu inayohusika na kufikiri na
kufanya maamuzi mengine baada ya kupambanua vitu kadha.
Kwenye RC ndipo unapo pata ile raha ya kitu unacho fanya ikiwemo tendo la
ngono na mwisho kupata ‘mshindo’. Pia ndipo pahala unapo amua ni kipi unakipenda
na kipi hukipendi, ni sehemu ndogo sana ndani ya ubongo, lakini ndipo penye
majibu ya mwisho, hakuna unacho fanya bila kuhusisha RC.
Kama wewe ni teja wa chochote kile, ikiwemo somo letu hili, picha za uchi,
basi hali hiyo ya kuwa teja inatokea ndani ya RC.
RC inaamshwa au kupandishwa na vitu vingi, mathalani unahisi kiu, hamu ya
kupata maji au kimiminika cha baridi inakuwa kubwa mno, unapofikiria aina
fulani ya kinywaji kwa ajili ya kiu husika, basi hamu nayo inazidi zaidi,
sehemu fulani ya ubongo wako ikikuambia pata kinywaji hicho, sehemu hiyo
inafahamika kama ‘depamine’. Unapopata kinywaji husika na ukapiga fundo la
kwanza, depamine’ inaanza kushuka, na RC nayo inakuwa imesharidhika, ukiendelea
kupata fundo jingine na jingine, basi ile hali ya kiu inatoweka kabisa na
unarudi kwenye hali ya kawaida.
Hali hiyo unaweza kuiona unapo fanya punyeto au unapofanya ngono.
Umepita mahala ambapo kuna mazingira ya wewe kutizama picha za uchi, RC
inaamka, unapofikiria ni aina gani ya picha za uchi utizame depamine inapanda
ikikuhimiza utizame picha husika nayo RC inakupa faida za kutizama picha hiyo,
kama kupata raha n.k. Unapoanza kutazama kwa vile RC imerekodi starehe ya juu
kabisa kwa wewe kutizama ni kupiga punyeto na hatimaye kupata mshindo, basi
depamine itaendelea kupanda kadiri unapotizama picha moja hadi nyingine mpaka
lengo litakapofikiwa.
Kutokana na tafiti za American Psychiatric, kama utasema ndiyo kwa maswali
matatu au zaidi kati ya haya basi wewe ni teja, sahamani mwaswali yenyewe
yataegemea kwenye suala la picha za uchi sababu ndiyo mada yetu.
1.
MUDA - Je matumizi yako ya picha za uchi kwenye mtandao yamekuwa
yakiongezeka siku baada ya siku? Umekuwa kila unapotizama unapanda chati kwa
kutumia muda mwingi zaidi au kwakuangalia mitindo na wachezaji wapya wa filamu
hizo au kwa kutizama mambo ya ajabu na yenye kinyaa zaidi kwenye filamu hizo?
2.
MADHARA YA KUACHA – Je unapo acha kutazama filamu hizo kwa muda, huwa
unajisikiaje. Wengi wa waathirika wanapoacha kutizama wanakuwa kama mazezeta,
kila kitu kinasimama, na hamu ya kutizama inakuwa kubwa ikiwataka kurudi
kutizama, wanajihisi wapo chini n.k.
3.
HUWEZI KUJITAWALA – Je wewe ashki ya kutazama picha hizo inapopanda unaweza
kuahirisha na kuendelea na kitu tofauti?
4. KUACHA SHUGHULI ZINGINE – Je umekuwa ukiacha shughuli zingine zilizo za
muhimu iliuwezea kutizama picha hizo za uchi?
5.
NATAKA KUACHA – Je umekuwa kwa muda mrefu unayo hamu na nia ya kuacha
kutizama picha hizo, lakini kila siku unajikuta umenasa kwenye mtego huohuo?
Umejaribu bila mafanikio kuacha lakini hutoki?
6.
MSAADA – Je umewahi kutafuta msaada juu ya tatizo lako, kwa ndugu, jamaa,
rafiki au kwa yeyote unayemuamini?
Kama wewe ni muathirika (teja) wa picha za uchi ni kwamba ubongo wako, hasa
sehemu ya limbic, imepata msisimko mkubwa kushinda uwezo wake kwa kutizama
picha za uchi.
Hivyo, teja wa picha za uchi kwenye ubongo wao kunawa na mabadiliko
yafuatayo.
Moja, RC inakuwa butu endapo itahitajika kufanya kazi yake kwa kitu chenye
msisimko mdogo kushinda picha za uchi, na hapo ndipo utaona tunakuwa na tatizo
kubwa la nguvu za kiume.
Pili, utaratibu wa ubongo kwenye tendo la ndoa unakuwa umetengeneza njia
mpya ya kupata msisimko nayo ni kwakutizama picha za uchi badala ya maumbile
halisi ya mwenza wako.
Hivyo basi tatizo linapokuwa kwenye hatua hiyo, ni kwamba ubongo wako
hautahitaji kingine chochote zaidi ya kile kitakacho weza kuusisimua mpaka
ufikie kileleni, nacho si kingine bali ni picha za uchi na wacheza filamu hao,
na hapo taratibu utamuona muathirika anapunguza siku za kufanya tendo la ndoa
na mwenza wake, na hamu ya kuwa naye kingono nayo inazidi kupungua siku hadi
siku, mpaka wanakuwa kama KAKA na DADA ndani ya nyumba. Ndoa inakuwa hatarini.
NINI KIFANYIKE?
Ndoa zipo hatarini, wanaume wengi wamekuwa ni waathirika wa picha za uchi, na hivyo waathirika wa 'nguvu' za kiume. Waataala wa tiba za kienyeji wanauza kila kitu chenye lebo ya 'kuongeza' nguvu za kiume. Lakini tatizo bado lipo palepale, sababu hakuna ambaye anayetibu tatizo, wote wanatibu dalili au madhara ya tatizo, lakini tatizo kuu ambalo ni PICHA ZA UCHI KWENYE MTANDAO LIKO PALEPALE ...
TUKUTANE NEXT TIME INSHAALLAH KATIKA KUATAFU SULUHU YA KUDUMU YA TATIZO HILI.
REMEMBER SHE IS NOT REAL, BUT SHE MIGHT KILL YOU AND YOUR MARRIAGE!!!!
So true
ReplyDeleteKWELI TUELIMIKE, UTEJA SI BANGI NA MADAWA TU. PICHA HIZI NI BALAA.
ReplyDelete