“Sema uwongo kwa sauti kubwa sana na rudi rudia mara kwa mara kwa muda
mrefu na watu watauamini huo uwongo. – Adolf Hitler
“Ufuate ushahidi kokote unapoelekea” – Socrates
“Ukweli inapaswa urudiwe mara kwa mara kwa sababu uwongo nao unahubiriwa
muda wote, wala siyo na wachache lakini na wengi. Uwongo unahubiriwa kwenye
magazeti na kwenye encyclopedia, kwenye mashule na kwenye vyuo, kila mahala
unaonekana kuwa wenye nguvu, unajisikia huru, raha na furaha kwa vile
unaaminiwa na wengi. – Johann Wolfgang Von Goethe
Mfumo tuliyo nao unatupotosha na kutujenga
kukubali kuwa thamani yetu iko kwenye rangi ya ngozi zetu, ukoo au kabila
fulani, na mmoja anaweza kuwa mtumwa na mwingine kuwa bwana.
Kiuhakika hatuna
tofauti, hakuna tofauti unapomtizama binaadam bila kutizama maumbile yake wala
alicho nacho, na huyo ndiyo binaadam, lakini watu wengi wanatumia rangi zao, na
au asili ya damu yao kuhalalisha matendo yao juu ya wengine. Tunapowatizama
watu wanaojinadi kuwa na uhusiano na damu ya wa-Semetik watu walioishi katika Sumeri
ya kale wakiwa wamelichukua jina la Sem na au Shem mmoja kati ya watoto wa Mtume
Nuhu katika mafundisho ya Biblia na watu hao leo wanajiita Wayahudi.
Nembo hii si haihusiani chochote na dini ya 'uyahudi, ila zaidi ni ya kishetani, tizama posti ya 666 kwa maelezo zaidi.
Dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu zote
tatu zina mizizi mikongwe ndani ya Palestina kupitia kwa mtume Ibrahim (a.s)
Abraham alihamia kutoka Iraq eneo lililoitwa Ur nakuja katika mji wa Canaan
ilipo Palestina hivi leo. Uhamiaji huu ulifanyika karibu miaka elfu nne
iliyopita. Kupitia watoto wawili wa mtume Ibrahim (as), Isaac na Ismael zikaibuka
dini hizi kuu tatu duniani, Uyahudi na Ukristo kwa Isaac na Uislamu kwa Ismail.
Hata hivyo Palestina ni ya zamani mno hata kabla Ibrahim hajatia mguu hapo
kulikuwa na mji uliopata kuishi miaka 8000 BC, mji huo uliitwa Jericho na upo
maili moja kutoka eneo ilipo Jericho ya sasa, mji huu ni wakale mno na unawezwa
kusemwa ni mji mkongwe kuliko yote duniani.
Kama
ilivyo desturi ya miji mingine mikubwa duniani na maeneo yake, eneo hili nalo
halikuachwa nyuma na utaratibu wa uhamiaji, kwa karne nyingi makabila kadha wa
kadha yalikuwa yakitafuta aridhi yenye rutuba na ahadi nzuri ya faida kwenye
biashara yalihamia eneo hili, wahamiaji hawa walijulikana kama wa-Kanaan, na
mwanzo eneo hilo likaitwa Canaan.
Kundi
jingine la wahamiaji ni lile lililokosa makazi Egypt na Mesopotamia na lilikuwa
likikimbia utawala wa mflame wa Piramidi mfalme Rameses II (Firauni),
watu hawa waliitwa Habiru, ama wakazi wa kuhama hama, hawa
ndiyo wana wa Israeli na wafuasi wa mafundisho ya dini ya Kiyahudi na mara
nyingine wanaitwa Wayahudi kwa maana ya Imani yao na siyo taifa, kama vile Mkristo,
Wakristo, na au Mwislamu, Waislamu zimaanishavyo imani na siyo utaifa ndivyo
ilivyo Myahudi na au Wayahudi.
Popote katika posti hii na mfano wake, ninapo taja Myahudi
na au Wayahudi nina maanisha wafuasi wa imani hii ya Kiyahudi bila kujali rangi
na wala utaifa, na nitajapo Israeli au Mwisraeli namaanisha mtu mwenye damu ya
asili ya Isaack na ya Jacob bila kujali dini wala utaifa. Kundi hili halikuweza
kuiteka Palestina ingawa lilifanikiwa kuishi kando, kando ya miji ya Palestina.
Wayahudi wakiokolewa na Farao akizamishwa baharini
Wahabiru
waliahidiwa aridhi hii ya ahadi kwa sharti moja, kusimamisha ufalme wa Mungu
mmoja, wa Canaan hawakutakiwa tena humo kwa sababu ya machafu yao hivyo inabidi
waondolewe na watu, wateule kwa maana ya kusimamisha ufalme wa Mungu Mmoja
wachukue aridhi hiyo, kwa maneno mengine, Wahabiru walikuwa na haki na aridhi
ile kwa muda mbao wataweza kusimamisha ufalme wa Mungu Mmoja, na
watakaposhindwa kufanya hivyo hawatakuwa na tofauti na wa Canaan ambao wao
wanaabudu mashetani.
‘ … mimi ni bwana Mungu wako,
niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa, usiwe na miungu
mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote …’
Musa (as) na watu wake, ingawa hawakuingia Caanan mpaka Musa alipofariki.
Vitisho
vya mara kwa mara na hata wakati mwingine vita kati ya Wahabiru na majirani zao
ndiko kuliko pelekea haja ya kuwa na kiongozi wao mmoja, utaratibu huu ulianza
na Sauli na kisha baadae akaja Daudi ambaye alichukua utawala mnamo mwaka 1000
BC . Baada ya Daudi kuwa shinda Wapalestina watu ambao walijulikana kuwa ni
majitu makubwa, watu wenye sifa, watu waliochanganya damu zao na
mashetani, alichagua Jerusalem kuwa
makao makuu ya Utawala wake. Jiji hili la Jerusalem lilikuwepo tangu mwanzo mwa
milenia ya pili BC lakini halijawahi mpaka hii leo kuwa makao makuu ya wa
Israeli.
“Ndipo wazee wote wa Israeli
wakakutana pamoja, wakamuendea Samweli huko Rama; wakamuambia, angalia, wewe umekuwa
mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue mfano
wa mataifa …”
Kundi
hili la wa Habiru halikuwa na sanaa za kiutamaduni na ustaarabu wa kimiji
walijifunza kutoka kwa wa Canaan. Hekalu lao la ibada lilijengwa na Wafonesia
wakazi wa hapo ambao wana damu ya nyoka, michoro, mafundisho na mashairi yaliyopatikana
ndani ya hekalu la Wahabiru yalikuwa na muundo na mitindo ile, ile ya wa Canaan
na wa Syria. Mungu ndama, Tammuz na Ishtar wakalivamia hekalu, na mantiki ya
dini ya Kiyahudi ya Mungu mmoja ikapotoshwa, na maana nzima ya kukaa kwenye
aridhi ya hadi ikapoteza sifa na hadhi yake.
Nikatika
mazingira haya ya utata ndipo vitabu vitano maarufu vinavyotengeneza Taurati
viliandikwa, vitabu hivyo vikiwemo vitabu vya ; Kitabu cha Kutoka, Mwanzo, ..... kwa karibu milenia mbili Kitabu cha
Kutoka kilifahamika kuwa ni kazi ya mtume Musa mwenyewe kwa mkono wake, mpaka
kwenye karne ya 16 ambapo maswali yalianza kuhojiwa.
“ikiwa Mussa ndiye mwandishi wa kazi ile
iweje aweze kuandika matukio ya kifo chake mpaka kuzikwa kwake?”
Lakini ni mpaka karne ya 18 ndipo ilipo bainika
kuwa kazi ile ni mkusanyiko wa kazi za kimila mbazo kizazi hadi kizazi zilikuwa
zikipitishwa kwa njia ya mdomo, kutoka kwa Wababiloni, Wasiria, Waigypti na
watu kutoka Mesopotamia, mkusanyiko huo ulikamilika katika karne ya 10BC.
Baada
ya Daudi, akaja mwanae ambaye ni mtume Suleimani naye alifariki mnamo mwaka
926-5 baada ya hapo ufalme wa Waisraeli ukaanza kuporomoka, kwanza suala la
kodi lilikuwa gumu kwao, pili mkanganyiko wa kidini nao uliwagawanya zaidi na
tatu ni nani atakaye chukua nafasi ya mtume Suleiman. Mtu mmoja aliyejitwika
sifa ya unabii ingawa haikuwa sifa yake akachukua kiti cha ufalme, mtu huyu aliitwa
Jeroboam, na hapo jamii hii ikagawanyika makundi mawili, Judah ikawa upande wa
kusini na Israeli upande wa kaskazini. Wakati wa mgawanyiko huo vita na
majirani zao vikapamba moto na vita vibaya zaidi ni vile walivyopigana mnamo
mwaka 722KK na wa Assyria, mfalme wa Assyria Tiglath –Pileser III alivamia
Israeli na kuiteka na akalifanya eneo hilo kuwa chini ya himaya yake, Judah
ilisalimika lakini ilibakia kama eneo dhaifu na tegemezi na halikuwa na nguvu
za kiutawala.
Mwaka
612KK, historia ikaandikwa tena, Assyria iliporomoka na kuchukuliwa na wa
Babilon wakati huo ikiongozwa na Nebuchadnezzar, ambaye aliivamia Jerusalem,
akaiharibu yote, akalichoma moto hekalu la mfalme Suleiman na Judah nayo
ikafutika kabisa.
Kidini
Waisraeli walikumbana na machungu haya baada ya kuacha mafundisho ya Mungu
Mmoja na hivyo hawakuwa tofauti na wa Canaan, katika vitabu vya Biblia tunaona
onyo la kutokea kwa matukio haya endapo watakengeuka na kufuata mila za
kishetani na ndivyo ilivyotokea.
Wanajeshi wa Nebuchadnezzar wakiondoka na agano baada ya kuwapiga waisrael na kulibomoa hekalu la bwana.
Wakaanza kutawanyika katika uso wa aridhi
tena, hawana mfalme, hawana nchi na mbaya kabisa hawana dini ya Mungu Mmoja.
Kila mmoja alitawanyika kutafuta hifadhi anapo pafahamu na kichwani wakiota
ndoto za kupewa tena aridhi ya ahadi.
Mungu
akawatumia tena mitume wake, lakini safari hii mitume hawakuja na maudhui ya
aridhi ya hadi na ushindi wa kivita, bali na ujumbe wa kusimamisha dini ya
Mungu Mmoja kwa amani na upendo. Zama hizi ziliwashuhudia mitume kama Ezra na
Nehemiah na wengine waliofanya kazi ya kuihuisha imani ya Jehovah. Haikuwa kazi
rahisi kwani fukuto la kisiasa lilizaa kuwagawanya Waisraeli. Kipindi cha
utawala kutoka kwa wa Persia na kuja kwa Wagiriki mnamo mwaka 333BC vyote
vilikuwa ni vipindi vya kubadilishana eneo hili kama bidhaa kutoka kwa huyu kwenda
huyu, watawala waliowekwa na wa Roma walichunga maslahi yao zaidi kuliko ya
watu wao, mfano wake ni Mfalme Herod, baba wa Mystery Force ambayo leo tunaiita Freemasons.
Mambo hayakuwa shwari kwa Waisrael wakati wa utawala wa Roma.
Utawala
wa Roma ndani ya Palestina uliwafukuzia ambali Wayahudi na kukiharibu hekalu
lao ambalo ni alama kuu ya takatifu katika historia yao. Sababu za Wayahudi
kufukuzwa zilikuwa ni zile za kisiasa na kijamii zaidi kuliko zile za kidini,
hata hivyo muda ulivyopita masuala ya kidini nayo yakawa ni msumari wa moto juu
ya kidonda kwa Wayahudi. Wayahudi waliruhusiwa kutafuta hifadhi sehemu zingine
katika dola ya Roma lakini si ndani ya Palestina. Wa Roma wakaufanya Ukristo
kuwa dini ya kitaifa dola lao, na hapo Wayahudi wakaonekana watu wabaya kuliko
wote, makanisa ya Kiroma yakaanza kampeni za kuwahusisha Wayahudi na kifo cha
Masiha, Yesu Kristo, Wayahudi wakaitwa ni wauaji wa Yesu na au wauaji wa mungu,
walimsulubu mungu msalabani.
Kuanzia
karne ya sita na kuendelea hali ilizidi kuwa ni mbaya zaidi kwa wa Israeli,
vipingamizi na vizuizi mbalimbali vikazidi kupamba moto, wakawa hawatakiwi
katika ofisi za kiserikali, na masinagogi yao yakaanza kuharibiwa, imani yao ya
Mungu mmoja ilionekana ni tusi dhidi ya imani ya Utatu Mtakatifu inayofutwa na
dola ya Roma. Sharia ikaja ikiwakataza watu kula mkate wa kimila wa Kiyahudi,
na wala wasioe kutoka kwenye familia za Kiyahudi wala kumuajiri daktari wa Kiyahudi,
zama hizo Myahudi alichukuliwa kama najisi, na Mkristo aliyekuwa na mawasiliano
na Myahudi alitengwa na kanisa.
Katika
nchi za Magharibi ambapo Wayahudi waliamua kutafuta hifadhi nako mambo hayakuwa
shwari hata kidogo, Ujerumani, Uingereza na Ufaransa kote sheria kali dhidi ya
Wayahudi zilipitishwa kuwaadhibu wauaji wa mungu. Sheria hizo ziliwabana katika
masuala ya kibiashara na kijamii. Hawakuwa na utulivu kokote walipokwenda.
Kipindi
hichi ndicho kipindi ambacho kabila la wa Turk ambalo lilikuwa likifuata imani
ya dini ya Kiislam lilikuwa likiisogelea Mashariki ya Kati na Antokia ya Asia
ya Kati, walikuwa na jeshi kubwa na lenye nidhamu, wa Islamu hawa waliisukuma
dola kubwa ya zama hizo iliyoitwa Byzantium kuelekea Constantintinople, maelfu
ya Wayahudi waliokuwa wakiishi maeneo haya walishatoweka na walibaki wachache
mno.
Dola ya Khazaria kama inavyo onekana mnamo karne ya 7
Kundi
jingine kubwa la wa Turk ambalo wao hawakuwa wa Islamu wala wa Kristo ila
walikuwa wakifuata dini zao za kimila, kundi hili liliitwa Khazair, wa Khazairi
walitawala sehemu kubwa ya Asia, hawa ni watu kutoka katika milima ya Caucasus
na maeneo ya bahari ya Caspiani na baadae walihamia Asia ya Kusini, Katika
kipindi hichi ambapo dini mbili kubwa yaani Uislamu na Ukristo zikikuwa kwa
kasi, kiongozi wa dola hili aliona hatari inayoikabili dola lake la kuangukia
katika mikono ya moja ya dini hizi, kisiasa hakuwa tayari kwa hilo, na hivyo
akaamua kufuata imani ya Kiyahudi, ni katika kipindi ambacho Wayahudi wako
katika hali ngumu sehemu mbalimbali duniani, na ni katika kipindi ambacho
wameshapoteza ile nguvu yao ya kiubaguzi ya kujibagua kuwa wao ni kizazi teule,
hawakuwa na taifa tena, lakini kiongozi wa Khazair kuamua kuingia katika dini
ya Kiyahudi.
Wa
Khazair wakaanza kuitwa Wayahudi, lakini hawa hawakuwa Wayahudi kwa maana ya
taifa lenye damu ya Israeli iliyotiririka kutoka kwa Isaac, bali Wayahudi kwa
njia ya imani, Wayahudi wachache waliobakia katika maeneo hayo nao wakapotolea
ndani ya kundi kubwa la wa Khazair, ikiwa haijulikani nani Myahudi wa kweli na
nani Mkhazairi. Kama ilivyokuwa katika nchi zingine za Ulaya waliko kimbilia,
suala la kuingiliana na kuoana na wasiokuwa Wayahudi halikuweza kuepukika na
hivyo wakapoteza ile damu yao ya asili kama watoto wa Jacob au Israeli
mwenyewe.
Mpaka hapo Wayahudi hawana nguvu ya kudai
taifa huru kwa kutumia kitambulisho cha Uyahudi kama taifa, kwani kama
tulivyoona, Uyahudi si Utaifa bali ni dini kama zile dini nyingine na mtu
yoyote anaweza kuingia katika dini ya Kiyahudi kama tunavyoona leo, kuna Wayahudi
weusi kutoka Uganda, kuna Wayahudi wakizungu na kadhalika, kama kungekuwa na
uhalali wa kuomba utaifa basi wangetumia kitambulisho cha Israeli, ikiwa na
maana wao ni kizazi cha Jacob, lakini kitambulisho hichi kimeshaharibiwa na mwingiliano
na watu wengine wasio kuwa wa Israeli, kwa hiyo tukisema tumtafute Mwisraeli
mwenye damu halisi ya Isaac na Jacob ni vigumu mno kuwapata, ingawa hili
halifanyi wanyimwe utaifa wao, lakini hakuna uhalali wa kudai utaifa nje ya
mahala ulipozaliwa. Kwa hiyo watu kutoka Milima ya Caucasua ndiyo waunda sehemu
kubwa ya watu wanaojiita Wayahudi. Mfalme wa Khaizari kuchagua dini ya Kiyahudi
kama dini ya kitaifa katika kipindi kigumu kama kile kwa Wayahudi inanipa wasi,
wasi kuwa si jambo lililotokea kwa bahati mbaya bali ni sehemu ya mpango maalum
ya kuwavisha watu wasio kuwa Wayahudi sura za Kiyahudi kwa ajili ya ajenda.
ITAENDELEA HAPA HAPA ... INSHALLAH
Nakuamin kaka mungu akupe uhai mrefu
ReplyDeleteAminnnn, na wewe ubarikiwe hivyohivyo.
ReplyDeleteHilo kundini la kutoka milimani ni milima gan lilitoka
ReplyDelete