Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Wednesday, September 25, 2013

FILAMU YA WWZ NA MIPANGO YA KUPUNGUZA IDADI YA WATU



Jana usiku (juzi)niliipata filamu inayo kwenda kwa jina la ‘WORLD WAR Z’, jina WORLD WAR ndilo lililo nivutia kuitazama filamu yake, hasa nikitaka kujua ‘Z’ inasimama badala ya nini kwenye jina hilo. Baada ya kuimaliza kuitizama nilikuwa na machache ya kushea na wasomaji wa blogi hii kuhusiana na filamu yenyewe.
Lakini kwanza kabisa kabla ya kupena mawili matu ya filamu hii, kwanza tutambue nafasi na kazi ya Hollywood kwenye soko la filamu.

Tangu Hollywood ianzishe sehemu kubwa ya zake imekuwa ni kuwarubuni mawazo ya watu, kutengeneza mawazo ya umma kukubaliana na kile wanacho kitaka.


Mathalani hakuna ushahidi wowote wenye mashiko unaothibitisha kuwa kuna viumbe wengine ‘huru’ kwenye uso wa dunia au nje ya dunia mbali na binadam na majini, lakini Hollywood wameweza kuurubuni umma kiasi kwamba kwa sasa inaaminika kuwa kuna viumbe wengine kutoka nje ya sayari hii, na kunayo uwezekano wa kuvamiwa na viumbe hao, lakini tunajua huu ni moja ya mipango kamambe ya Illuminanti ambao kwa kiasi nimeulezea kwenye posti hii http://salimmsangi.blogspot.com/2013/08/hatua-nne-kabla-ya-ujio-wa.html


Duniani hatuna tatizo la ‘UGAIDI’ kwa maana ya UGAIDI, Lakini kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na Hollywood leo dunia nzima imekubali kuwa kuna tatizo la ugaidi na kama hatua za msingi hazitochukuliwa basi tatizo hilo litaiangamiza dunia (Hatua za msingi si nyingine bali sheria zilizo na utata na zilizo juu ya katiba ya nchi na zinazo pora uhuru na haki za msingi za wananchi)


Kupitia Hollywood umma umeaminishwa kwamba Uislamu ni dini mbaya ya kigaidi, kishetani, waumini wake wana roho mbaya, wakatili na wauaji wabaya kama wao hakuna, lakini hadithi ni tofauti kabisa na Waislamu wenyewe namna walivyo.
Hivyo basi Hollywood hutumika kurubuni na kuandaa maamuzi na fikra za umma kukubaliana na jambo fulani wanalo taka kulifanya, mara kadhaa imethibitika kwa Hollywood kutengeneza filamu zenye maudhui ya jambo fulani walilopanga kulifanya



Mwaka 1954 kitabu kilicho kwenda kwa jina la  ‘I Am Legend’ kilizinduliwa. Matukio katika kitabu hicho ni baina ya mwaka 1976 – 1979. Mwaka 1957 janga la mafua likaimeza dunia na chanjo ya polio ikaanza kutumika rasmi. Kipindi ambacho kimetumika kama muda wa maudhi ya kitabu yaani miaka minne ndicho kipindi kilicho chukua kuibuka kwa janga la mafua tangu kitabu hicho kiingie sokoni.
Filamu iliyo kwenda kwa jina la ‘The Last Man on Earth’ ya mwaka 1964, maudhui yake ni matukio yaliyo chezwa kutokea mwaka 1968. Mwaka 1967 baa la mafua liliikumba dunia.
Filamu nyingine ya aina kama hii ni ‘The Omega Man’ filamu hii ni ya mwaka 1971, lakini maudhui yake ni matukio ya mwaka 1977. Mwaka 1976 liliibuka janga la mafua ya nguruwe.
Filamu ya ‘I Am Legend’ ambayo ni ya mwaka 2007, maudhui yake ni baina ya mwaka 2009 – 2012. Dunia ilikumbwa na janga la  HIN1.


Unaweza kwenda umbali wa ziada na kwakufanya tafiti binafsi, natumai utakuja na majibu mazuri zaidi.


Hadithi ya ‘Worl War Z’ na matukio kwenye filamu hiyo yanaonesha kwamba Illuminanti wanayo aina fulani ya mpango mbaya dhidi yetu. Kama ‘Z’ kwenye filamu hiyo imesimama badala ya neno ZOMBIE, Hapana shaka hivyo ndivyo tunavyo onekana kwenye macho ya Illuminanti, kwamba ni watu duni, wabaya, tusio na bongo salama, na ambao inabidi tuangamizwe kwa namna yeyote ile inayo wezekana na kwa zana yeyote ile inayo patikana kukidhi lengo hilo kwa kiwango cha kidunia, ‘globaly’ na hapo ndipo unapo pata maana ya WWZ.


Kwenye filamu hiyo zaidi ya watu bilioni 4, ‘wameathirika’ kutokana na virusi wabaya wanao badilisha maumbile ya binadamu na kama wanyama. Tetesi zipo na maandishi yapo kuwa Illuminanti wanao mpango wa kufuta asilimia 90 ya watu wote duniani, pekua mwenyewe utaona. WWZ inaonesha zaidi ya asilimia 80 ya binadamu wote wameathirika na hakuna kinga hivyo wanauwawa wote kwa  namna yeyote ile iwezekanayo.

Nyota wa filamu hii ni Brad Pitt, ambaye amesha shiriki filamu zingine zenye jumbe mahususi za kimasonia kwa wanamasonia, na pia anatarajiwa kuowana na Angelina Joel ambaye ni mwanachama wa asasi ya siri ya CFR, asasi ambayo pia inamuandaa Brad Pitt kuwa mwanachama. Katika filamu Brad Pitt kama mtu aliyepata kuwa muajiriwa wa UN, anachukua nafasi ya kutafuta njia ya kuwaangamiza ‘zombi’ (kwenye neno zombi badilisha na weka neno ‘walimwengu’).

Kutakuwa na kambi ambazo zombi itabidi waingizwe kama mahala pa salama wakati tiba yao inaendelea kutafutwa, lakini itakuwa ndiyo machinjio yao, watakuwa wanauwawa humo.
Israel itaonekana kuwa ndiyo nchi inayo weza kupambana na zahama hilo kwa kuweka ukuta mkubwa ambao utawazuia zombi wasiingie, ambao wengi ni wapalestina na mamilioni wanaonekana kuuwawa wanapo upanda ukuta huo.


Kila kona kuna miili ya binadamu iliyo lundikana baada ya kuuwawa ilipogundulika ni waathirika.

Pakistani na Iran zinamalizana zenyewe kwa silaha zao za nyuklia, baada ya Iran kuzuia kwa kuwauwa wakimbizi ambao ni zombi wasiingie Iran kutokea Pakistan, hapa kwa maneno mengine tunaambiwa kuwa Iran wanazo sila za nyuklia.

Ni kama filamu hii, inatabiri yale yatakayo kuja kwenye kila kinacho fahamika saa za mwisho, na pia inawiana na mpango wa Illuminanti, hasa linapo kuja anguko la uchumi la kidunia, ambalo nalo litakuwa ni la kupangwa, na mabilioni ya watu kumwagika mitaani wakiwa hawana kitu nyumbani wala mifukoni, kwa vile Illuminanti kupitia mabenki yao wamewapora utajiri wao, watu hawa watakuwa ni shida mitaani, sheria za kutotembea mtaani zitapitishwa kama inavyo onekana mwanzoni kabisa kwenye filamu hii, lakini hilo halitasaidia na nguvu za kijeshi ndipo zitakapo tumika, nayo itakuwa ni mauwaji ya halaki kama inavyo onekana kwenye filamu ya WWZ.

Baada ya miaka 10 ya vita, dunia imebadilika, tiba ya zombi hakupatikana zaidi ya vifo vya halaiki na walimwengu wamebakia wateule wachache.
Filamu hii ni moja ya filamu zilizo tengenezwa kwa gharama kubwa mno, lakini kikubwa ikionesha burudani ya mabilioni ya watu wakiuwawa kwa halaiki. Ni kweli suala la kuuwa watu, mabilioni ya watu ni kitu cha kukihesabu kama aina ya burudani?
Unakumbuka kazi ya Hollywood? Filamu hii inaandaa akili za umma na mawazo yao kusukumwa na nguvu hasi za kiukatili na mauwaji zaidi, kutuandaa kukubaliana na mipango ya Illuminanti hata kama itakuwa ni kuuwa mabilioni ya watu kwa sababu yeyote ile watakayo itaja kwenye vyombo vya habari.

Wakati wa utawala wa Rome, umma ulidanganywa na mambo ya kipuuzi, kulikuwa na michezo mibovu na mibaya kwa umma lakini yenye baraka za kiserikali, michezo hiyo ni kama ‘GLADIETOR’ Ambapo wafungwa waliingizwa kwenye ulingo wakapambana na kupigana mpaka kifo na wananchi walikaa majukwaani wakishangilia damu zikitiririka, Hollywood naona wanaturudishia utamaduni huo na ulimwengu umeonekana kuupenda sana. 

Leo hii tunatizama LIVE kwenye luninga taifa moja likimwaga damu za watu wasio na hatia za watu wa taifa jingine na tunaona yote hayo ni sawa tu.

 Mauwaji ya halaiki tangu lini yakawa ni burudani kwa uma? 

No comments:

Post a Comment