Jana
usiku (juzi)niliipata filamu inayo kwenda kwa jina la ‘WORLD WAR Z’, jina WORLD WAR
ndilo lililo nivutia kuitazama filamu yake, hasa nikitaka kujua ‘Z’ inasimama
badala ya nini kwenye jina hilo. Baada ya kuimaliza kuitizama nilikuwa na
machache ya kushea na wasomaji wa blogi hii kuhusiana na filamu yenyewe.
Lakini
kwanza kabisa kabla ya kupena mawili matu ya filamu hii, kwanza tutambue nafasi
na kazi ya Hollywood kwenye soko la filamu.
Tangu
Hollywood ianzishe sehemu kubwa ya zake imekuwa ni kuwarubuni mawazo ya watu,
kutengeneza mawazo ya umma kukubaliana na kile wanacho kitaka.
Mathalani
hakuna ushahidi wowote wenye mashiko unaothibitisha kuwa kuna viumbe wengine
‘huru’ kwenye uso wa dunia au nje ya dunia mbali na binadam na majini, lakini
Hollywood wameweza kuurubuni umma kiasi kwamba kwa sasa inaaminika kuwa kuna
viumbe wengine kutoka nje ya sayari hii, na kunayo uwezekano wa kuvamiwa na
viumbe hao, lakini tunajua huu ni moja ya mipango kamambe ya Illuminanti ambao
kwa kiasi nimeulezea kwenye posti hii http://salimmsangi.blogspot.com/2013/08/hatua-nne-kabla-ya-ujio-wa.html
Duniani
hatuna tatizo la ‘UGAIDI’ kwa maana ya UGAIDI, Lakini kwa kutumia vyombo
mbalimbali vya habari pamoja na Hollywood leo dunia nzima imekubali kuwa kuna
tatizo la ugaidi na kama hatua za msingi hazitochukuliwa basi tatizo hilo
litaiangamiza dunia (Hatua za msingi si nyingine bali sheria zilizo na utata na
zilizo juu ya katiba ya nchi na zinazo pora uhuru na haki za msingi za
wananchi)
Kupitia
Hollywood umma umeaminishwa kwamba Uislamu ni dini mbaya ya kigaidi, kishetani,
waumini wake wana roho mbaya, wakatili na wauaji wabaya kama wao hakuna, lakini
hadithi ni tofauti kabisa na Waislamu wenyewe namna walivyo.
Hivyo
basi Hollywood hutumika kurubuni na kuandaa maamuzi na fikra za umma
kukubaliana na jambo fulani wanalo taka kulifanya, mara kadhaa imethibitika kwa
Hollywood kutengeneza filamu zenye maudhui ya jambo fulani walilopanga
kulifanya
Mwaka
1954 kitabu kilicho kwenda kwa jina la ‘I Am Legend’ kilizinduliwa.
Matukio katika kitabu hicho ni baina ya mwaka 1976 – 1979. Mwaka 1957 janga la
mafua likaimeza dunia na chanjo ya polio ikaanza kutumika rasmi. Kipindi
ambacho kimetumika kama muda wa maudhi ya kitabu yaani miaka minne ndicho
kipindi kilicho chukua kuibuka kwa janga la mafua tangu kitabu hicho kiingie
sokoni.
Filamu
iliyo kwenda kwa jina la ‘The Last Man on
Earth’ ya mwaka 1964,
maudhui yake ni matukio yaliyo chezwa kutokea mwaka 1968. Mwaka 1967 baa la
mafua liliikumba dunia.
Filamu
nyingine ya aina kama hii ni ‘The Omega
Man’ filamu hii ni ya mwaka 1971, lakini maudhui
yake ni matukio ya mwaka 1977. Mwaka 1976 liliibuka janga la mafua ya nguruwe.
Filamu
ya ‘I Am Legend’ ambayo ni ya mwaka 2007, maudhui yake ni baina ya mwaka 2009 –
2012. Dunia ilikumbwa na janga la HIN1.
Unaweza
kwenda umbali wa ziada na kwakufanya tafiti binafsi, natumai utakuja na majibu
mazuri zaidi.
Hadithi
ya ‘Worl War Z’ na matukio kwenye filamu hiyo yanaonesha kwamba Illuminanti
wanayo aina fulani ya mpango mbaya dhidi yetu. Kama ‘Z’ kwenye filamu hiyo
imesimama badala ya neno ZOMBIE, Hapana shaka hivyo ndivyo tunavyo onekana
kwenye macho ya Illuminanti, kwamba ni watu duni, wabaya, tusio na bongo
salama, na ambao inabidi tuangamizwe kwa namna yeyote ile inayo wezekana na kwa
zana yeyote ile inayo patikana kukidhi lengo hilo kwa kiwango cha kidunia,
‘globaly’ na hapo ndipo unapo pata maana ya WWZ.
Kwenye
filamu hiyo zaidi ya watu bilioni 4, ‘wameathirika’ kutokana na virusi wabaya
wanao badilisha maumbile ya binadamu na kama wanyama. Tetesi zipo na maandishi
yapo kuwa Illuminanti wanao mpango wa kufuta asilimia 90 ya watu wote duniani,
pekua mwenyewe utaona. WWZ inaonesha zaidi ya asilimia 80 ya binadamu wote
wameathirika na hakuna kinga hivyo wanauwawa wote kwa namna yeyote ile iwezekanayo.
Nyota
wa filamu hii ni Brad Pitt, ambaye amesha shiriki filamu zingine zenye jumbe
mahususi za kimasonia kwa wanamasonia, na pia anatarajiwa kuowana na Angelina Joel
ambaye ni mwanachama wa asasi ya siri ya CFR, asasi ambayo pia inamuandaa Brad
Pitt kuwa mwanachama. Katika filamu Brad Pitt kama mtu aliyepata kuwa muajiriwa
wa UN, anachukua nafasi ya kutafuta njia ya kuwaangamiza ‘zombi’ (kwenye neno
zombi badilisha na weka neno ‘walimwengu’).
Kutakuwa
na kambi ambazo zombi itabidi waingizwe kama mahala pa salama wakati tiba yao
inaendelea kutafutwa, lakini itakuwa ndiyo machinjio yao, watakuwa wanauwawa
humo.
Israel
itaonekana kuwa ndiyo nchi inayo weza kupambana na zahama hilo kwa kuweka ukuta
mkubwa ambao utawazuia zombi wasiingie, ambao wengi ni wapalestina na mamilioni
wanaonekana kuuwawa wanapo upanda ukuta huo.
Kila
kona kuna miili ya binadamu iliyo lundikana baada ya kuuwawa ilipogundulika ni
waathirika.
Pakistani
na Iran zinamalizana zenyewe kwa silaha zao za nyuklia, baada ya Iran kuzuia kwa
kuwauwa wakimbizi ambao ni zombi wasiingie Iran kutokea Pakistan, hapa kwa
maneno mengine tunaambiwa kuwa Iran wanazo sila za nyuklia.
Ni kama
filamu hii, inatabiri yale yatakayo kuja kwenye kila kinacho fahamika saa za
mwisho, na pia inawiana na mpango wa Illuminanti, hasa linapo kuja anguko la
uchumi la kidunia, ambalo nalo litakuwa ni la kupangwa, na mabilioni ya watu
kumwagika mitaani wakiwa hawana kitu nyumbani wala mifukoni, kwa vile
Illuminanti kupitia mabenki yao wamewapora utajiri wao, watu hawa watakuwa ni
shida mitaani, sheria za kutotembea mtaani zitapitishwa kama inavyo onekana
mwanzoni kabisa kwenye filamu hii, lakini hilo halitasaidia na nguvu za kijeshi
ndipo zitakapo tumika, nayo itakuwa ni mauwaji ya halaki kama inavyo onekana
kwenye filamu ya WWZ.
Baada ya
miaka 10 ya vita, dunia imebadilika, tiba ya zombi hakupatikana zaidi ya vifo
vya halaiki na walimwengu wamebakia wateule wachache.
Filamu
hii ni moja ya filamu zilizo tengenezwa kwa gharama kubwa mno, lakini kikubwa
ikionesha burudani ya mabilioni ya watu wakiuwawa kwa halaiki. Ni kweli suala
la kuuwa watu, mabilioni ya watu ni kitu cha kukihesabu kama aina ya burudani?
Unakumbuka
kazi ya Hollywood? Filamu hii inaandaa akili za umma na mawazo yao kusukumwa na
nguvu hasi za kiukatili na mauwaji zaidi, kutuandaa kukubaliana na mipango ya
Illuminanti hata kama itakuwa ni kuuwa mabilioni ya watu kwa sababu yeyote ile
watakayo itaja kwenye vyombo vya habari.
Wakati
wa utawala wa Rome, umma ulidanganywa na mambo ya kipuuzi, kulikuwa na michezo
mibovu na mibaya kwa umma lakini yenye baraka za kiserikali, michezo hiyo ni
kama ‘GLADIETOR’ Ambapo wafungwa waliingizwa kwenye ulingo wakapambana na
kupigana mpaka kifo na wananchi walikaa majukwaani wakishangilia damu
zikitiririka, Hollywood naona wanaturudishia utamaduni huo na ulimwengu
umeonekana kuupenda sana.
Leo hii tunatizama LIVE kwenye luninga taifa moja
likimwaga damu za watu wasio na hatia za watu wa taifa jingine na tunaona yote hayo
ni sawa tu.
Mauwaji ya halaiki tangu lini yakawa ni
burudani kwa uma?
No comments:
Post a Comment