“Kama
kutakuwa na makundi mawili, badala ya kuwa benki na jamii, iwe mwana jamii
mmoja na mwingine, wasingeweza kuendesha mfumo wa ukopeshaji kwa kanuni nyepesi
tu, kwamba, mkopeshaji hawezi kukopesha kile asicho kuwa nacho, kama sinavyo
fanya benki. Ni benki za biashara tu na taasisi zingine za fedha ndizo zinazo
weza kukopesha pesa hewa wanazo zatengeneza kwa kukopesha.”
Profesa
Irving Fisher, mwanauchumi kwenye kitabu chake 100% Money
“Nipe
nguvu ya kutawala sarafu ya nchi na sitajali ni nani anaye tunga sheria”
“Somo linalo husiana na mambo ya fedha,
kwenye nyanja zote za masomo ya uchumi, ndilo somo ambalo ugumu utatiwa au
kutumiwa kwa makusudi ili kuficha au kupoteza ukweli (kuhusiana na suala zima
la fedha)”
John Kenneth
Galbraith, Mwanauchumi na Mwandishi.
“Suala ambalo limefanyiza ubaya kwa karne,
na ambalo itabidi lipiganiwe ili liondolewe, punde tu au baadaye kidogo, ni
wananchi dhidi ya taasisi za fedha (benki)”
Lord Acton (1834-1902, Mwanahistoria wa England
Pesa inatoka wapi?
Hili linaweza kuwa swali la mwaka.
Na hakuna wa kulijibu, siyo mwanauchumi
wala mfanyabiashara, wala huwezi kulipata jibu lake kwenye machapisho na
majarida ya kiuchumi, wala siyo la kiserikali, wala kwenye vipindi maalum vya
kiuchumi kwenye luninga yako, mbadala wa wapi lipo jibu la swali hilo lazima
upatikane, na ashakum siyo matusi.
Katika moja ya vitu ambavyo vimetawala au
kuendesha maisha yetu ya kila siku ni; Pesa.
Pesa ni nini, au inatoka wapi, ni
swali jepesi, lenye majibu mepesi ambayo kwa namna moja ama nyingine, huwa
hakuna anayejitolea kuyajibu, ni kama vile pesa yenyewe kupitia utaratibu wa
kuitumia au inavyo tumika inatoa jibu la maswali hayo, inajijibu yenyewe,
tunaona kwenye luninga, kwenye matangazo ya biashara, kwenye vitabu vikubwa
vilivyo vunja rekodi za mauzo na filamu, maswali haya huwa yanajijibu yenyewe
huko. Kutokana na majibu hayo ni kuwa, watu wengi unaondoka na majibu ya
kuamini kuwa pesa zinatengenezwa na serikali.
Kwamba serikali ndiyo inayo printi
noti za fedha na sarafu zake. Kwamba serikali ndiyo inayo printi sarafu na noti
ni kweli kabisa, ila huo siyo ukweli wote.
Ukweli wote ni upi?
Benki, huo ndiyo ukweli wote.
Tuashumu kuwa benki inakopesha fedha ilizo
pewa kama amana na wateja wake, ingawa huo siyo ukweli, tunaashumu tu. Unapo
kwenda benki kuchukua mkopo, benki inakupa mkopo huo baada ya kusaini mkataba
ambao utakutaka wewe kulipa fedha hizo na riba juu.
Dhamana ya ahadi hiyo,
ambayo ni maarufu kama, ‘dhamana ya mkopo’ huwa ni mali zisizo hamishika au
zinazo hamishika ambazo zinamilikiwa kihalali na mkopaji au na mdhamini wa
mkopaji. Kisha kama wanavyo fanya wana mazingaombwe, benki wanageuza mkataba
huo baina yao na mkopaji kuwa ndiyo fedha anazo pewa mkopaji. Ndiyo kama mazingaombwe
vile, huwezi kuja kwangu, tukaandikishana mkataba wa kukopeshana, nami nikaugeuza
mkataba huo kuwa ni fedha unazo taka, ila benki inafanya maajabu hayo kila
siku, ila macho yetu hayaoni.
Huwezi kuamini, ila huu ndiyo ukweli kuhusu namna
benki zinavyo fanya kazi.
Vitu hueleweka zaidi kwa mifano, ngoja ni
kupe kahadithi kidogo kama mfano wa namna ambavyo benki wanavyo fanya hayo mazingaombwe.
Hapo zamani za kale, kila kitu kilitumika
kama fedha, ili mradi kiwe kinabebeka na watu wawe na imani kuwa kinaweza
kubadilishwa na kingine chenye thamani kama yake. Hivyo mazao, mifugo, na
bidhaa nyinginezo zilitumika kama pesa. Vitu vya thamani kama vile dhahabu na
fedha vilivutia zaidi kwenye hili, navyo vilitumika katika biashara hii,
iliitwa Barter Trade.
Mtu mmoja ambaye hapa tutamuita Sonara,
kutokana na kazi yake ya kuyeyusha hivi vito vya thamani na kuviweka katika
maumbo mbalimbali, yeye alikuja na wazo, kutokana na kwamba biashara yetu ya
kubadilishana vitu inakumbana na kikwazo cha ‘thamani’ na inakuwa ni vigumu
wakati mwingine haki kufanyika katika aina hii ya biashara ni vigumu kwa sababu
hakuna kipimo maalum cha ‘thamani’ kwa bidhaa zote, Sonara akapendekeza jamii
imruhusu atumie kipaji chake atengeneze sarafu za fedha na dhahabu ambazo
zitatumika kama kipimo cha thamani kwa bidhaa mbalimbali.
Bidhaa ambazo
upatikanaji wake ulihitaji nguvu na shughuli nzito basi thamani ya bidhaa hiyo
itakuwa kubwa kuliko ile ambayo uzalishaji wake haukuhitaji nguvu na akili
nyingi. Sonara akapewa mikoba na kuanza kutengeneza sarafu za fedha na dhahabu.
Sonara akatengeneza chumba maalum chenye mlango
mkubwa na mzito, na huko akazimimina sarafu zake za fedha na dhahabu na akaweka
walinzi juu kuhakikisha hakuna anaye cheza na ‘mayai’ yake. Watu nao
wakalipenda wazo la Sonara, wakaleta fedha na dhahabu zao kwa wingi zihifadhiwe
na Sonara, naye akiwachaji malipo kidogo kwa huduma hiyo.
Sonara akapata wasiwasi, endapo watu wote
watakuja kuchukua dhahabu na fedha zao, yeye atabaki na kitu gani?
Sonara akatengeneza risiti, kwa wale wanao
leta dhahabu na fedha kwake, risiti hizo zilibeba thamani ya dhahabu au fedha
zilizo hifadhiwa na muhusika. Risiti hizo zikawa zinaweza kutumika mbadala wa
fedha na dhahabu, yaani ukiwa na risiti hizo ni sawa na kumiliki kiasi cha dhahabu
au fedha kilicho andikwa kwenye risiti hizo. Na kama ukipenda unaweza ukarudi
kwa Sonara na risiti hizo na Sonara akakupa dhahabu au fedha halisi, hii
itategemea na thamani iliyo andikwa kwenye risiti hiyo.
Nyuma ya mapazia Sonara alikuwa akifanya
biashara nyingine, alizikopesha fedha na dhahabu zake kwa wafanyabiashara mbalimbali,
lakini kwa riba. Lakini Sonara hili nalo lilimpa wazo kubwa zaidi, kwa sababu
ni watu wachache tu ndiyo waliyo amua kuzichukua dhahabu na fedha halisi,
akaona ni bora kwa kila dhahabu moja na fedha anayo miliki kuiandikia risiti,
na kwamba badala ya kukopesha fedha halisi na dhahabu atakopesha risiti hizo.
Ilimradi risiti hizo zitalipwa baadaye kama dhahabu halisi au fedha halisi kama
riba, Sonara ataendelea kufurahia ugunduzi wake huo.
Lakini mara maneno yakaanza, ikasemekana
Sonara anakopesha fedha ambazo siyo zake kwa riba, fedha alizo pewa kama amana,
Sonara hakuwa na shida, kwa vile alicho kikopesha siyo dhahabu wala fedha
halisi, bali ni risiti zenye thamani ya kile anacho kimiliki jumlisha kile
alicho pewa kama amana, akaenda kuwaonesha lango lake, akalifungua na wananchi
walipo tizama ndani waliona dhahabu na fedha zao zipo salama, watu wakamuacha
Sonara akaendelea na biashara yake.
Lakini wananchi wakarudi tena, wakamuambia
Sonara, kwa vile yeye anatumia dhahabu na fedha zao kuwakopesha watu kwa riba,
na wao walio weka dhahabu na fedha halisi wakahitaji wawe na mgawo kwenye faida
hiyo ya Sonara, wapewe kiasi fulani cha faida kama riba, na hapo kitu kipya
kikazaliwa, mfumo wa benki.
Hitajio la mkopo likazidi kuwa kubwa
kutokana na upanukaji wa biashara kwenye miji mbalimbali, naye Sonara wetu
hawezi kukopesha zaidi ya kile alicho nacho, risiti alizo zitaoa zimebeba
thamani ya kile ambacho kilichopo kwenye volti yake. Lakini akapata wazo zaidi,
wazo zuri zaidi; kwa vile hakuna yoyote isipokuwa yeye anayefahamu ni kiasi
gani hasa cha dhahabu na fedha halisi kilichomo kwenye volti yake, anaweza
kuprinti risiti nyingi zaidi kadiri awezavyo na kuzikopesha kwa wafanya
biashara, na kuzipa risiti hizo thamani yeyote ile na hakuna atakaye shuku, kwa
vile hakuna atakaye rudi muda huo, huo kwa Sonara na kuhitaji dhahabu au fedha
halisi ni nani atakaye fahamu kuwa Sonara anakopesha risiti hewa? Hakuna, ila
yeye tu mwenyewe Sonara, Bingo!
Sonara akawa tajiri, naye akawamegea siri
hiyo Sonara wenzake wa nchi zingine, duara lao likawa kubwa na lenye nguvu na
wakaja na taasisi waliyo ita benki, wakaendelea kukusanya utajiri mkubwa kwa
riba inayo patikana kwenye mikopo ya risiti hewa.
Lakini mambo yakaanza tena, wananchi
wakataka dhahabu na fedha halisi, kwa vile
zile zilikuwa ni risiti hewa, masonara hawakuwa na chochote cha kuwapa; sasa tutafanyaje?
Kimbia, kimbia, kimbia, kimbiaaaaaaa kadiri utakavyo weza, ndivyo walivyo fanya
masonara, mlango wa nyuma wakachukua dhahabu na fedha zilizobakia zikiwemo zile
walizo pewa kama amana na kutokomea.
Mara nyingi wanapo fanya hivyo huwa
hatusemi kuwa wamekimbia na fedha zetu au dhahabu zetu au mali zetu, bali
wanauchumi wetu wamekipatia kitendo hicho jina maalum, wanaita anguko la
kiuchumi.
Utajiri halisi ukabaki kwenye makaratasi,
vurugu zilifuata kama kawaida, serikali ikaingilia kati, mfumo wa Sonara
ukapitiwa, serikali ikaweka vifungu vyake na kisha ikaubariki mfumo huo. Benki
zikapewa kipimo cha mwisho cha kukopesha kutokana na fedha inazo kuwa nazo,
kipimo hicho kinaitwa Friction Reserve. Lakini bado kiwango hicho ni kikubwa
ukilinganisha na kiwango cha fedha ambazo benki inazo kwenye vitabu vyake.
Au
kama ilivyo kuwa awali kiwango hicho ni kikubwa kushinda dhahabu na fedha
halisi iliyo kuwa kwenye milki ya benki.
Benki za kitaifa zikapatikana, ambazo kazi
yake ni kusimamia taratibu za kibenki kwa vijibenki vingine ambavyo siyo
‘Central Bank’ taratibu ambazo ziliwaruhusu vijibenki vidogo dogo kukopesha
zaidi ya kile walicho nacho, vijibenki hivyo vilitakiwa kuwa na kiwango maalum
au uwiano baina ya kile walicho nacho na kile wanacho kikopesha, Loan to
deposit Ration.
Mfumo wa benki ukabadilika, suala la fedha
na dhahabu kama kipimo cha thamani ya bidhaa na huduma kikatoweka, na nafasi
yake ikachukuliwa na jinamizi jingine kubwa, Deni.
Mathalani kama unaweza
kuzipata fedha za zamani kidogo karne mbili, tatu nyuma, utaona thamani yake
ilikuwa ni sawa na kiasi fulani cha dhahabu na au fedha halisi. Lakini sasa
hivi thamani ya sarafu au noti ni sawa na sarafu au noti nyingine, yaani bati
kwa bati au karatasi kwa karatasi. Katika kipindi hicho benki binafsi ziliweza
kutengeneza risiti badala ya fedha na dhahabu halisi, lakini watu walikuwa na
uhuru wa kuzikubali au kuzikataa, kama ilivyo leo ambavyo mtu yupo huru
kuikubali au kuikataa hundi anayo pewa na mtu mwingine.. Lakini leo mabenki
yaliyo pewa leseni na serikali yanaweza kuzitoa sarafu na noti ambazo zimetiwa
baraka na serikali na benki kuu kama fedha halali kwa kiasi fulani cha malipo.
Ni kiasi gani cha fedha ambacho serikali na
benki kuu wanacho weza kukitengeneza na kukipa thamani na kukiweka katika
mzunguko?
Ni vipi aina hii ya mfumo ulivyo mzigo kwa umma?
Ni vipi mfumo huu unavyo wanufaisha wachache, hususan Illuminnati?
Je unamjua Sonara katika hadithi hii?
Uchumi wa nchi unaweza kutengemaa kwa kutegemea aina hii ya mfumo?
Hey, njoo hapa tena wakati ujao kwa majibu ya maswali hayo na mengine mengi.
No comments:
Post a Comment