AU UNAWEZA SEMA, MFUMO WA BENKI UMEPEWA LESENI YA KUWAIBIA WANANCHI.
Tumalizie
kisa cha Sonara kwanza,
Wakati
mfalme William wa Orange alipokuwa kwenye wakati mgumu wa kifedha kwa sababu ya
vita vyake na Ufaransa, ilibidi akope fedha kutoka kwa ‘SONARA’ (Goldsmiths)
lakini haikutosha kumkopesha buree tuu ukizingatia alikuwa nahitajia pauni
milioni 1.2, ambacho kipindi hichi na hata sasa hivi leo hii ni kiasi kikubwa
mno cha fedha, kikubwa si kidogo, Goldsmiths wakampatia masharti mfalme William
ambayo endapo atakubaliana nayo, basi watampatia huo mzigo anao taka.
1.
Riba ya mkopo
huo itakuwa ni asilimia 8.
2.
Mfalme
awapatie goldsmiths kibali ambacho kitawawezesha wao kukopesha fedha ambazo
hawana, kama tulivyo ona kwenye hadithi ya ‘sonara’ wetu.
Mr. William Peterson
Mfalme
alikubaliana na masharti hayo, na mwaka 1694 kibali kilitolewa kwa mtu aliyeitwa
William Paterson na benki ya kwanza duniani, ‘Bank of England’ ikafunguliwa
milango yake. Lakini haikuwa benki ya ENGLAND kama jina lake linavyo tamkwa,
wala haikuwa na mwingiliano wowote na serikali, ilikuwa ni benki inayo milikiwa
na matajiri wa dhahabu, ‘goldsmiths.
Ndani ya Frankfurt, Ujerumani. Miaka hamsini baada ya Benki Kuu ya England kufunguliwa milango yake, mfua dhahabu aitwaye Mayer Amschel Bauer akufungua duka la sarafu - nyumba kuhesabu na kubadilisha fedha - katika 1743, na juu ya mlango, aliweka bendera yenye ishara inayoonyesha ngao nyekundu, Kijerumani ilisomeka kama Rothschild.
Hiyo ndiyo alama ambayo Mayer aliitundika mbele ya nyumba yake, alama hiyo ni maarufu kama '6 Pointed Star' au 'The Star of David ' au 'The Seal of Solomon'. Alama hii haina uhusiano wowote na mitume hao watukufu wa Allah, ispokuwa kama ilivyo ada ya freemason uwongo ni sifa yao kubwa,baadaye alama hiyo ikawa ni bendera ya taifa la Israel, na hii ikiwaambia ulimwengu ni nani anaye imiliki Israeli. Hii ni nembo ya kishetani na nembo kuu katika nembo za kumuita shetani/jini kuja kwenye ulimwengu huu wa 3 dimensional.
Katika
mwaka 1785, Mayer alihamishia familia
yake yote katika nyumba kubwa,ghorofa tano na katika nyumba hiyo ilikuwemo
familia ya Schiff. Nyumba hiyo ilijulikana kama Green Shield, familia ya
Rothschilds na ile ya Schiffs
zitatasaidiana katika kuitengeneza na kuisimamia historia ya fedha kwa nchi za
Ulaya, Marekani na dunia kwa ujumla.
Mtoto wake, Mayer Amschel Bauer,
akarithi biashara, aliamua kubadili jina lake Rothschild Mayer. Na yeye ndiye aliyekuwa kichwa cha familia. Rothschild
baadaye alijuwa kuwa fedha za mikopo kwa serikali na wafalme ilikuwa faida
zaidi kuliko mikopo kwa watu binafsi.
Si tu
ilikuwa ni mikopo kubwa zaidi, lakini pia mikopo hiyo ilikuwa na uhakika wa
kulindwa kwa dhamana ya walipa kodi, yani kupitia makusanyo ya kodi za wanachi.
[Frederic Morton – ‘The Rothschilds’
:Portrait of a Dynasty]
Mayer
Rothschild alikuwa na watoto watano akawapatia mafunzo ya siri ya namna ya
kupora fedha kutoka kwa watu kwa njia ya mkopo na udanganyifu, kisha akawatuma
waende miji mikubwa ya Ulaya kufungua ofisi za tawi la benki ya biashara ya
familia. Katika moja ya miongozo yake kwa familia hiyo ni kuwa ameamuru kwamba mtoto mmoja wa kiume katika
kila kizazi ndiye atakayetawala biashara ya familia, wanawake walitengwa kwenye
hilo la uongozi.
Mtoto
wa kwanza wa kiume wa Mayer, Amschel,
alibaki katika jiji la Frankfurt kusimamia benki ya nyumbani. Mwanawe wa pili, Salomon, alitumwa Vienna.
Mtoto wake wa tatu, Nathan, alikuwa na maarifa
zaidi na mjanja; alipelekwa London katika umri 21 mwaka 1798, miaka mia
moja baada ya mwanzilishi wa Benki Kuu ya England. Mtoto wake wa nne, Karl,
akaenda Naples. Mtoto wake wa tano, Jakob (James), alikwenda Paris.
Rothschilds
akaingia kwenye biashara na mfalme tajiri kuliko wote Ulaya, -Prince William wa
Hesse. Mara ya kwanza, Rothschilds alikuwa na kazi ya kumsaidia mfalme
kutengeneza faida katika masoko ya hisa. Hata hivyo, wakati Napoleon
alipomfukuza Prince William uhamishoni, William alimtuma pauni 550,000 ambacho
kilikuwa ni kiasi kikubwa sana cha fedha kipindi hicho na kumtaka Nathan
Rothschild aziwekeze fedha hizo kwenye kununua hisa za serikali ya Ungereza.
Lakini
Rothschild akatumia fedha hizo kwenye mipango yake ambayo anajua ingemletea
fedha nyingi zaidi kwa malengo yake mwenyewe. William alipokuja kudai fedha
zake baadae Rothschild alimpatia fedha hizo zikiwa na ongezeko la riba ya
asilimia nane, faida ambayo ingepatikana kama Rothschild angeziwekeza fedha
hizo mahala ambapo Prince William alielekeza ziwekezwe, faida nyingine yote
iliyopatikana Rothschild wakaiweka kibindoni.
Nathan
Rothschild ambaye ndiye aliyepewa dhamana ya kusimamia fedha hizo za Prince William
na baba yake alidai kuwa aliweza kuongeza utajiri aliyopewa na baba yake wa
pauni 20,000 mara 2500 zaidi, yaani kufikia pauni 50,000,000 katika karne hizo,
unaweza kuona ni kiasi gani cha fedha kilitengenezwa kutokana na pauni 550,000
kutoka kwa Prince William. [http://www.rense.com/general79/tril.htm]
Kwa
nguvu ya uwepo kwao katika mataifa matano kama benki, Rothschilds walikuwa na
ufanisi uhuru, kama chombo huru kwenye mataifa ambayo wao huendesha shughuli
zao za kibenki, hawakuweza kuingiliwa na sera wala sharia za nchi husika na
kama moja ya taifa hilo sera zake zitakuwa zikipingana au kuweka kizuizi kwenye
biashara ya Rothschild basi wao waliacha kufanya biashara na nchi hiyo au
walitoa fedha kudhamini vikundi na wanaharakati ambao walipinga utawala huo.
Hivyi
ndivyo mpaka leo demokrasia inavyotumiwa na freemason wa Ulaya kuendelea
kuzinyonya nchi zetu, serikali yoyote ile duniani lazima iende na kufanya mambo
yake kulingana na wanavyo taka wao, ikijifanya yenyewe inajua zaidi itang’olewa
kupitia kile kinacho itwa demokrasia na hata wakati mwingine mapinduzi ya
silaha yaliyo dhaminiwa na freemason wa Ulaya. Jamani kuna haja ya kutoa mifano
ya nchi hizo ni zipi?
Benki
za kitaifa zikapatikana, kama vile BoT ambazo kazi yake ni kusimamia taratibu
za kibenki kwa vijibenki vingine ambavyo siyo ‘Central Bank’ taratibu ambazo
ziliwaruhusu vijibenki vidogo dogo kukopesha zaidi ya kile walicho nacho nacho,
vibenki hivyo vilitakiwa kuwa na kiwango maalum au uwiano baina ya kile walicho
nacho na kile wanacho kikopesha, Loan to deposit Ration.
Mfumo
wa benki ukabadilika, suala la fedha na dhahabu kama kipimo cha thamani ya
bidhaa na huduma kikatoweka, na nafasi yake ikachukuliwa na jinamizi jingine
kubwa, Deni. Mathalani kama unaweza kuzipata fedha za zamani kidogo karne
mbili, tatu nyuma, utaona thamani yake ilikuwa ni sawa na kiasi flani cha
dhahabu na fedha halisi. Lakini sasa hivi thamani ya sarafu au noti ni sawa na
sarafu au noti nyingine, yaani bati kwa bati au karatasi kwa karatasi.
Katika kipindi hicho benki binafsi ziliweza
kutengeneza risiti badala ya fedha na dhahabu halisi, lakini watu walikuwa na
uhuru wa kuzikubali au kuzikataa, kama ilivyo leo ambavyo mtu yupo huru
kuikubali au kuikataa hundi anayo pewa na mtu mwingine. Lakini leo mabenki
yaliyo pewa leseni na serikali yanaweza kuzitoa sarafu na noti ambazo zimetiwa
baraka na serikali na benki kuu kama fedha halali kwa kiasi fulani cha malipo.
Ni
kiasi gani cha fedha ambacho serikali na benki kuu wanacho weza kukitengeneza
na kukipa thamani na kukiweka katika mzunguko?
Kipindi
cha nyuma kiasi cha fedha au ‘risiti fedha’ zilizo kuwa kwenye mzunguko
kulitegemeana na hitajio la bidhaa ambazo zilihitajika kununuliwa na fedha
hizo. Mathalani kwa ajili ya kutimiliza hitajio la dhahabu na fedha halisi,
wachimbaji iliwabidi kuzitafuta aridhini dhahabu na fedha kwa wingi na
kuzipeleka kwa masonara ili sarafu ziweze kutengenezwa.
Lakini
leo kinacho hitajikia ili kuweka fedha nyingi kwenye mzunguko ni taasisi za
fedha ikiwemo mabenki kukopesha kwa wingi. Yaani fedha zinatengenezwa kwa
kupitia mikopo, au kama nilivyo sema awali, kwa kutumia karatasi uliyo saini
kama mkataba baina yako na benki ili uweze kupewa mkopo.
Benki
wanacho angalia ni Fractional Reserve, au Loan to Deposit Ratio, na benki kuu
ndizo zinazo simamia kuhakikisha kuwa mabenki hayapitilizi kiwango hicho,
ingawa pamoja na hayo bado yanapitiliza kiwango hicho cha ukopeshaji. Kiwango
hicho kinatofautina nchi hadi nchi. Mwanzo benki ilitakiwa kuwa na kiasi fulani
cha dhahabu kama reserve, ili iweze kukopesha kiasi flani cha pesa mara kadhaa
zaidi kushinda kiasi cha dhahabu halisi kinayo miliki, lakini leo, kiwango
hicho cha ukopeshaji kinapimwa kwa kutumia fedha ambazo benki inazo zimiliki
kwenye volti yake kwa uwiano wa mara kadhaa zaidi ya kile itakacho kikopesha
kwa wanachi.
Kwenye
buku rejea la Encyclopedia of Britannica, chapa ya kumi na nne, kuhusiana na
benki na mikopo, inasema hivi, “Benki
inatengeneza mikopo. Ni makosa kufikiri kwamba mikopo ya benki inatokana na
pesa zinazo wekwa benki na wateja. Mkopo unao tolewa na benki, hiyo ni pesa
mpya kabisa inayoingizwa kwenye mzunguko.”
Lord
Acton, Lord Chief of Justice of England, 1875.
“Suala ambalo limefanyiza ubaya kwa karne, na
ambalo itabidi lipiganiwe ili liondolewe, punde tu au baadaye kidogo, ni
wananchi dhidi ya taasisi za fedha (benki)”
Naye muheshimiwa Philip A. Bensoni,
aliyekuwa raisi wa American Bankers’ Assosiation, mwaka 1939,Juni 8, alisema
hivii, “Hakuna tena zaidi njia yeyote ya kuitawala nchi kushinda ile ya
kupitia mfumo wake wenyewe wa mikopo.”
Kidogo tutizame namna benki zinavyo fanya
kazi, kumbuka mfumo wa benki zote duniani ni mmoja, isipokuwa mfumo wa benki za
Kiislamu, hivyo hapa tutatizama mfumo wa kibenki zisizo za kiislamu namna
zinavyo fanya kazi.
Mathalani benki mpya imepewa leseni leo
ianze kazi, benki hiyo inatakiwa iwe na kiasi flani cha fedha kama mtaji wake,
kipindi cha nyuma ilikuwa ni gold, lakini kwa sasa hakuna tena gold ni pesa. Pesa hizo zinawekwa kwenye akaunti ya benki
husika iliyopo benki kuu, tuseme benki yetu hii iliyo mpya resrve yake ni
shilingi 1,111.12/-, tuseme kwenye nchi ambayo benki hii imefunguliwa
Fractional Reserve ni 9:1.
Mlango unafunguliwa, mteja wa kwanza
anaingia, anahitaji shilingi 10,000/- akanunue gari, kumbuka kwenye nchi hii
ambayo benki yetu imefunguliwa, benki inaweza kukopesha mpaka mara 9 ya fedha
ilioyo kuwa nayo. Benki itakacho fanya ni kuuchukua mkataba ambao imeingia
pamoja na mteja wake na kuigeuza kuwa fedha.
Benki haiandiki barua au Memo kwenda benki
kuu kuitaka ichapishiwe noti mpya zenye thamani ya shilingi 10,000/- Bali
itakacho fanya benki ni kuandika tarakimu hizi 10,000/- kwenye akaunti ya mteja
kwa kutumia keyboard! Kwa kufanya hivyo benki inakuwa imetengeneza pesa hewa
mpya yenye thamani ya shilingi 10,000/- katika mzunguko.
Kisha mteja husika hujaza hundi yake
10,000/- kumlipa yule ambaye anataka kumuuzia gari. Kumbuka benki haikufanya
chochote ila kuandika 10,000/- kwenye akaunti ya mteja, ambayo wakati wa
kurejeshwa benki hiyo itahitaji na ongezeko la asilimia kadhaa kama riba, hapa
kwetu benki zinatoza riba ya kuanzia 15 mpaka 24 na hata zaidi itategemea na
aina ya mkopo. Kumbuka pesa ambayo benki imemkopesha mteja huyu haipo au kwa
maneno rahisi benki haikuwa na pesa hiyo, lakini juu ya hapo benki inamtoza
mteja wake huyu riba ya asilimi 20 na zaidi kwa fedha ambayo benki haikuwa nayo
na wala haipo kwenye mzunguko fedha hiyo zaidi ya tarakimu zilizo andikwa
kwenye akaunti ya mteja.
Aliyeuza gari anaichukua ile hundi na
kwenda kuiweka (deposit) kwenye akaunti yake iliyo katika benki yake. Benki hii
iliyo pokea hundi kutoka kwenye benki yetu mpya nayo inaweza kuikopesha pesa
hii ‘mpya’ pesa hewa ambayo haipo katika mzunguko, lakini si kwa kuizidisha
mara 9, lakini kwa kuigawanya kwa ile Fractional Reserve, hivyo kwa kutumia
hundi hiyo benki hii ya pili inaweza kukopesha 9,000/- na 1,000/- itabakia kama
Reserve ya benki.
Mkopo mpya ulio tengenezwa au pesa hewa
hiyo nayo itakapo kwenda kuingizwa katika benki nyingine au hata hiyo hiyo,
inakuwa ni halali kwa benki hiyo kuikopesha fedha hiyo kwa kutumia Fractional
Reserve, nayo itatoa pesa hewa kama mkopo wa shilingi 8,100/- na shilingi 900
ikibakia kama Reserve ya benki. Hivyo kwa utaratibu huu benki zinaweza
kutengeneza mpaka 100,000/- pesa mpya ambazo hazikuwepo popote hapo kabla, na
wala hazipo kwenye mzunguko zaidi ya tarakimu katika akaunti za wateja.
Mfumo huu umebarikiwa, na asili yake ni sawa
na mfano wa Sonara tulio uona, kwa kutumia mtaji wa 1111.12 benki imeweza
kutengeneza fedha hewa kufikia 100,000/-
Hivyo mkopo unao tengenezwa na benki moja, ni deposit kwa benki
nyingine. Hivyo benki zinatengeneza riba kwenye pesa zaidi ya shilingi 100,000/-
ambazo haikuwa nazo. Benki zinakopesha fedha ambazo haikuwa nazo.
Pesa halisi iliyopo kwenye mzunguko ni 5%
na 95% ni pesa hewa inayo tengenezwa na benki kwa kubadilisha mkataba iliyo
usaini na mteja wake kuwa ni pesa, hela hiyo hapatikani popote kwenye
mzunguko zaidi ya nambari zilizomo kwenye akaunti.
Unapo kwenda kuzitoa fedha za mkopo ambazo
tunajua ni mrundikano wa tarakimu zilizo andikwa kwenye akaunti yako, ni kwamba
unakwenda kuichukua ile 5% halisi ambayo tayari ipo kwenye mzunguko, hakuna
pesa mpya halisi iliyo tengenezwa kutimiza hitajio lako la mkopo, hakuna,
kilicho tengenezwa ni tarakimu tu ambazo wewe unazisoma kwenye akaunti yako.
Ambazo zimetengenezwa kupitia mkataba wako ambao umeahidi kulipa mkopo huo,
hiyo ni pesa mpya kabisa iliyo tengenezwa na benki, lakini ni pesa mpya ambayo
hajapata kuwepo na wala haitapata kuwepo kwenye mzunguko, kwa sababu ni pesa
hewa, nawe utahitajika kuilipa hii pesa hewa kama pesa halisi na jumlisha na
riba! Benki ni waizi! Samahani nafuta usemi, mfumo wa benki ni wa uwizi mtupu.
Mkopo unapo malizika kulipwa, pesa ‘mpya’
iliyo tengenezwa na benki kwa kutumia mkataba wa mteja wake nayo inatoweka!
Mr, Regnald McKenna, wakati alipokuwa
mwenyekiti wa Midland Bank ya London, alisema haya kuhusiana na benki, “ Ninahofia kuwa
watu wa kawaida hawatapenda kuambiwa kuwa benki wana, fanya, tengeneza na
kuiharibu hela. Na kwamba wale ambao wanao simamia mikopo hiyo ya nchi
(mabenki) ndiyo wanao tengeneza sera za nchi na kwenye viganja vya mikono yao
wameshikilia hatima ya maisha ya wananchi.”
Benki zinautumia mfumo huu kwa ushirikiano
na serikali, yaani baraka za kiserikali kwanza lazima ziwepo kwa kupitisha
sheria ya fedha ambayo inawezesha makaratasi hayo kutumika kama kipimo cha
thamani kwa huduma na bidhaa zitakazo tolewa nchini au kwenye mipaka ambayo
karatasi na bati (sarafu) hizo zitatumika.
Pili serikali zina yaruhusu mabenki binafsi
kuziingiza sarafu na noti hizo zenye baraka ya serikali katika mzunguko na
ikiwemo kulipia huduma na bidhaa mbalimbali. Tatu serikali inatoa leseni kwa
mabenki hayo na taasisi zingine za pesa kukopesha makaratasi na sarafu hizo kwa
wananchi wake na nne serikali na nne inapitisha sheria kuulinda mfumo
huo na utaratibu wake wa ufanyaji kazi.
Serikali haiwaambii wananchi wake ni
wapi fedha zinapo tokea.
“Hatma ya nchi yetu ipo kwenye mikono ya watu
wa benki na biashara yao ya kutoa mikopo hewa, ambao wanakopesha ahadi ya kutoa
mkopo kwa fedha wasizo kuwa nazo. [Profesa Irving Fisher, mwanauchumi na
Muandishi.]
Bila karatasi ambayo mteja amesaini kulipa
mkopo, benki inakuwa haina cha kukopesha, yaani mkataba baina ya benki na
mteja, ambao mteja anaweka dhamana baadhi ya mali zake, kisha benki kwa kutumia
mkataba huo kwenye akaunti ya mteja wanaandika tarakimu ambazo zinalingana na
kiasi mteja anacho taka kukopa.
Kwenye mtazamo wa mteja tarakimu hizi zinakuwa
ni pesa za mkopo zilizopo kwenye akaunti yake. Kwa vile serikali inautambua
mfumo huu, na inatambua kuwa ‘pesa’ hewa za mkopo kutoka benki kwenda kwa mteja
zinaweza kubadilishwa kuwa pesa halisi, pesa ambayo ni karatasi lenye sahihi ya
viongozi wa serikali na alama za ajabu ajabu, moja kwa moja inakuwa ‘halali’
kwa benki kumpatia mteja wake makaratasi hayo kama ‘pesa’, lakini benki haijakwenda
kuprint makaratasi hayo, bali imeweka tu tarakimu pale kwenye akaunti ya mteja,
na mteja akishindwa kulipa makaratasi ambayo ni pesa hewa jumlisha na riba, alicho kiweka
kama dhamana kinakwenda.
Unaweza kusema kuwa hii siyo pesa hewa,
mbona nimezishika hapa mkononi sasa hivi baada ya kuandikiwa mkopo? Ulicho
shika mkononi ni sehemu ya pesa ambayo tayari ipo kwenye mzunguko, lakini benki
walicho fanya ni kwa nguvu waliyo pewa na serikali ni kuugeuza ule mkataba
uliyo saini wewe kuwa ndiyo tarakimu zinazo ingizwa kwenye akaunti yako na kuwa
‘pesa’ benki haina fedha hizo inazo kukopesha, haina hata kidogo, ila inayo
nguvu za kisheria kufanya mkataba wako kuwa ni tarakimu zitakazo
geuka fedha, haya ni mazingaombwe ya kibenki.
Haujiulizi ni kwa nini, serikali, mashirika,
makampuni, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, familia zote zinakuwa kwenye
deni, tena madeni makubwa makubwa. Hujiulizi ni kiasi gani kilichopo cha fedha
kwa ajili ya kukopeshea? Lakini sasa umejua, hakuna hata senti moja ambayo ipo
kwa ajili ya kukopeshea, lakini watu bado tunayo minyororo mizito ya madeni
kutoka taasisi za fedha.
Hivyo ‘pesa’ ni mkopo, kama mikopo yote
italipwa hakutakuwa na pesa, 95% ya ‘pesa’ itatoweka.
“Hivyi ndivyo mfumo wetu wa fedha ulivyo,
kama hakutakuwa na mtu anaye daiwa na benki katika mfumo wetu wa pesa,
hakutakuwa na pesa yeyote.[ Marriner S. Eccles
Mwenyekiti na Gavana kwenye bodi ya Federal Reserve.]”
Watu wanadhani kuwa ikiwa madeni yote
yatalipwa basi hali za watu na uchumi zitakaa vizuri, lakini huu ni ukweli kwa
sehemu tu ya watu, lakini endapo mikopo yote ikalipwa, hakutakuwa na hata senti
moja ya pesa, uchumi wetu unategemea fedha hewa kutoka kwenye mikopo, na kila
unapoisha unaongezwa.
Utaona benki pia zipo kwenye mikono ya
maadui zetu, na wanapo taka jambo lao lifanyike ni amri tu inatoka na benki
zinaacha kukopesha, zikiacha kukopesha mzunguko hewa wa pesa nao unatoweka, fedha za kulipa mkopo zinatoweka, kinacho fuata ni kile kinacho itwa anguko la kiuchumi, sasa itategemea maadui
zetu waliaanda nini, inaweza kuwa ni mapinduzi ya serikali, vita au lingine
lolote ambalo walilipanga, usisahau kukuibia utajiri wako halisi ambao uliuweka
kama dhamana, si hakuna pesa hewa kwenye mzunguko, unadhani utalipa huo mkopo
hewa na nini, utajiri halisi lazima uende.
NAAHIDI MTANANGE HUU WA PEOPLE vs BENKI
UNAENDELEEA HAP HAPA, CHEKI HAPA NEXT TIME TUNAPO TIZAMA BALAA HILI LA MABENKI
KWENYE ‘LEVEL’ NYINGINE ....
Kaka mi cjaelewa hapo kwenye mkopo mf nimekopa nikapewa pesa yangu cash na cio kwa hundi apo pesa hewa inapatikanaje kwa bank.
ReplyDeleteNi mchezo mdogo sana unao fanyika, lakini unahitaji akili ya ziada kuugundua.
DeleteKumbuka benki wanakopesha mpaka mara kumi ya pesa waliyo nayo. Kama kwenye vitabu vyao wanao shilingi 10, basi benki wanaweza kukopesha mpaka shilingi 100 kwa kutumia hiyo shilingi 10. Ndiyo maana benki wanawekewa kitu kinacho itwa Loan to Deposit Ration ili kuwaoongoza wasivuke kiwango cha ukopeshaji, vinginevyo hiyo shilingi 1o waliyo nayo wangeikopesha mpaka mara milioni na zaidi.
Sali linakuja ikiwa wanayo 10 iweje wakopeshe mpaka shilingi 100?
Kama wewe unayo shilingi 10 mfukoni nikija unikopeshe, huwezi nikopeshe shilingi 20, au 50 au 16, hapana utanikopesha shilingi 10 sababu hiyo ndyo unayo, lakini kwa benki ni tofauti, kile wasicho kuwa nacho benki ndicho wanacho kikopesha.
Wanacho fanya ni kui-credit accaount yako kwa tarakimu na nambari zinazofikia kiwango cha pesa unachotaka, kisha utapewa hundi au cash money haijalishi, kinachojalisha ni kuwa KWA KUINGIZA TARAKIMU HIZO KWENYE AKAUNTI YAKO KAMA MKOPO, TARAKIMU HIZO NI FEDHA MPYA ILIYOINGIZA KWENYE MZUNGUKO. VITABU VYAO HAVINA PESA HIYO, WALICHOTUMIA NI KANUNI YA LOAN TO DEPOSIT RATION NA MKATABA ULIOSAINI.
HAWAJAWAPIGIA BENK KUU WAWAPRINITIE FEDHA ZA KIASI HICHO MTEJA ANACHO TAKA. MTAJI WAO BENKI KUU HAULNGANI. YAANI NI MDOGO UKILINGANISHA NA JUMLA YA FEDHA WALIZO KOPESHA, WALA BENKI HAWAKOPESHI FEDHA ZINAZO LETWA KUWEKWA NA WATEJA HAPO, INGAWA KWA JICHO NA AKILI YA KAWAIDA NDIVYO INAVYO ELEWEKA.
KILA BENKI INAPOTOA MKOPO MPYA, UJUE HIYO NI PESA HEWA MPYA ILIYOINGIZA KWENYE MZUNGUKO, NA KILA PESA UNAYO IYONA KWENYE MZUNGUKO NI MKOPO UNAO TAKIWA KULIPWA. NA KAMA MIKOPO YOTE ITALIPWA KUSIWEPO NA MTU HATA MMOJA NAYEDAIEA NA BENKI, BASI UJUE HAPATAKUWEPO NA HATA CENTI TANO KWENYE MZUNGUKO, FEDHA ZOTE ZITATOWEKA.
ILI FEDHA ZOTE ZITOWEKE KWENYE MZUNGUKO LAZIMA WATU WENGINE WAPOTEZE ASSET ZAO KAMA NYUMBA, MAGARI NA MENGINEYO, SABABU BENKI WANAPOTENGENEZA MKOPO AMBAO NI PESA MPYA, HAWATENGENEZI NA PESA YA RIBA, HIVYO UKIJA MTAANI LAZIMA WATU WAKOPE ILI PAPATIKANE PESA YA KULIPIA RIBA, LAKINI KAMA MADENI YOTE YATALIPWA KUNA AMBAYE ATAKUTWA HANA PESA YA KULIPIA RIBA SABABU RIBA HAIKUTENGENEZWA KAMA ULIVYOTENGENEZWA MKOPO, MALI YAKO HALISI NDIYO ITAKAYO TUMIKA KULIPA RIBA.
HEWA YA UCHUMI WETU NI MIKOPO HEWA YA BENKI, NA TIZAMA ANGUKO LA UCHUMI SIKU ZOTE LINAANZIA KWENYE MABENKI, SABABU WATU WAPO, VIWANDA VIPO, MALIGHAFI ZIPO, BARABARA ZIPO, WALAJI WAPO, LAKINI KITU KIMOJA TU KIKIONDOLEWA KWENYE MZUNGUKO UCHUMI WOTE UNAPOROMOKA KAMA NYUMBA YA MAKARATASI. SABABU UCHUMI UMESHIKILIWA NA MABENKI KUPITIA MIKOPO HEWA.
tchao