Wednesday, October 16, 2013

MFUMO WA MABENKI NA HATMA YETU

AU UNAWEZA SEMA, MFUMO WA BENKI UMEPEWA LESENI YA KUWAIBIA WANANCHI.


Tumalizie kisa cha Sonara kwanza,

Wakati mfalme William wa Orange alipokuwa kwenye wakati mgumu wa kifedha kwa sababu ya vita vyake na Ufaransa, ilibidi akope fedha kutoka kwa ‘SONARA’ (Goldsmiths) lakini haikutosha kumkopesha buree tuu ukizingatia alikuwa nahitajia pauni milioni 1.2, ambacho kipindi hichi na hata sasa hivi leo hii ni kiasi kikubwa mno cha fedha, kikubwa si kidogo, Goldsmiths wakampatia masharti mfalme William ambayo endapo atakubaliana nayo, basi watampatia huo mzigo anao taka.


King William of Orange


1. Riba ya mkopo huo itakuwa ni asilimia 8.
2. Mfalme awapatie goldsmiths kibali ambacho kitawawezesha wao kukopesha fedha ambazo hawana, kama tulivyo ona kwenye hadithi ya ‘sonara’ wetu.


Mr. William Peterson

Mfalme alikubaliana na masharti hayo, na mwaka 1694 kibali kilitolewa kwa mtu aliyeitwa William Paterson na benki ya kwanza duniani, ‘Bank of England’ ikafunguliwa milango yake. Lakini haikuwa benki ya ENGLAND kama jina lake linavyo tamkwa, wala haikuwa na mwingiliano wowote na serikali, ilikuwa ni benki inayo milikiwa na matajiri wa dhahabu, ‘goldsmiths.


Ndani ya Frankfurt, Ujerumani. Miaka hamsini baada ya Benki Kuu ya England kufunguliwa milango yake, mfua dhahabu aitwaye Mayer Amschel  Bauer akufungua duka la sarafu - nyumba kuhesabu na kubadilisha fedha - katika 1743, na juu ya mlango, aliweka bendera yenye ishara inayoonyesha ngao nyekundu, Kijerumani  ilisomeka kama  Rothschild.


 
Hiyo ndiyo alama ambayo Mayer aliitundika mbele ya nyumba yake, alama hiyo ni maarufu kama '6 Pointed Star' au 'The Star of David ' au 'The Seal of Solomon'. Alama hii haina uhusiano wowote na mitume hao watukufu wa Allah, ispokuwa kama ilivyo ada ya freemason uwongo ni sifa yao kubwa,baadaye alama hiyo ikawa ni bendera ya taifa la Israel, na hii ikiwaambia ulimwengu ni nani anaye imiliki Israeli. Hii ni nembo ya kishetani na nembo kuu katika nembo za kumuita shetani/jini kuja kwenye ulimwengu huu wa 3 dimensional. 




Katika mwaka  1785, Mayer alihamishia familia yake yote katika nyumba kubwa,ghorofa tano na katika nyumba hiyo ilikuwemo familia ya Schiff. Nyumba hiyo ilijulikana kama Green Shield, familia ya Rothschilds na ile ya  Schiffs zitatasaidiana katika kuitengeneza na kuisimamia historia ya fedha kwa nchi za Ulaya, Marekani na dunia kwa ujumla.





 Mtoto wake, Mayer Amschel Bauer, akarithi biashara, aliamua kubadili jina lake Rothschild Mayer. Na yeye ndiye aliyekuwa kichwa cha familia.  Rothschild baadaye alijuwa kuwa fedha za mikopo kwa serikali na wafalme ilikuwa faida zaidi kuliko mikopo kwa watu binafsi.

Si tu ilikuwa ni mikopo kubwa zaidi, lakini pia mikopo hiyo ilikuwa na uhakika wa kulindwa kwa dhamana ya walipa kodi, yani kupitia makusanyo ya kodi za wanachi. [Frederic Morton – ‘The Rothschilds’ :Portrait of a Dynasty]

Mayer Rothschild alikuwa na watoto watano akawapatia mafunzo ya siri ya namna ya kupora fedha kutoka kwa watu kwa njia ya mkopo na udanganyifu, kisha akawatuma waende miji mikubwa ya Ulaya kufungua ofisi za tawi la benki ya biashara ya familia. Katika moja ya miongozo yake kwa familia hiyo ni kuwa  ameamuru kwamba mtoto mmoja wa kiume katika kila kizazi ndiye atakayetawala biashara ya familia, wanawake walitengwa kwenye hilo la uongozi.
Mtoto wa kwanza wa kiume wa Mayer, Amschel, alibaki katika jiji la Frankfurt kusimamia benki ya nyumbani.  Mwanawe wa pili, Salomon, alitumwa Vienna. Mtoto wake wa tatu, Nathan, alikuwa na maarifa  zaidi na mjanja; alipelekwa London katika umri 21 mwaka 1798, miaka mia moja baada ya mwanzilishi wa Benki Kuu ya England. Mtoto wake wa nne, Karl, akaenda Naples. Mtoto wake wa tano, Jakob (James), alikwenda Paris.
Rothschilds akaingia kwenye biashara na mfalme tajiri kuliko wote Ulaya, -Prince William wa Hesse. Mara ya kwanza, Rothschilds alikuwa na kazi ya kumsaidia mfalme kutengeneza faida katika masoko ya hisa. Hata hivyo, wakati Napoleon alipomfukuza Prince William uhamishoni, William alimtuma pauni 550,000 ambacho kilikuwa ni kiasi kikubwa sana cha fedha kipindi hicho na kumtaka Nathan Rothschild aziwekeze fedha hizo kwenye kununua hisa za serikali ya Ungereza.

Lakini Rothschild akatumia fedha hizo kwenye mipango yake ambayo anajua ingemletea fedha nyingi zaidi kwa malengo yake mwenyewe. William alipokuja kudai fedha zake baadae Rothschild alimpatia fedha hizo zikiwa na ongezeko la riba ya asilimia nane, faida ambayo ingepatikana kama Rothschild angeziwekeza fedha hizo mahala ambapo Prince William alielekeza ziwekezwe, faida nyingine yote iliyopatikana Rothschild wakaiweka kibindoni.

Nathan Rothschild ambaye ndiye aliyepewa dhamana ya kusimamia fedha hizo za Prince William na baba yake alidai kuwa aliweza kuongeza utajiri aliyopewa na baba yake wa pauni 20,000 mara 2500 zaidi, yaani kufikia pauni 50,000,000 katika karne hizo, unaweza kuona ni kiasi gani cha fedha kilitengenezwa kutokana na pauni 550,000 kutoka kwa Prince William. [http://www.rense.com/general79/tril.htm]

Kwa nguvu ya uwepo kwao katika mataifa matano kama benki, Rothschilds walikuwa na ufanisi uhuru, kama chombo huru kwenye mataifa ambayo wao huendesha shughuli zao za kibenki, hawakuweza kuingiliwa na sera wala sharia za nchi husika na kama moja ya taifa hilo sera zake zitakuwa zikipingana au kuweka kizuizi kwenye biashara ya Rothschild basi wao waliacha kufanya biashara na nchi hiyo au walitoa fedha kudhamini vikundi na wanaharakati ambao walipinga utawala huo.

Hivyi ndivyo mpaka leo demokrasia inavyotumiwa na freemason wa Ulaya kuendelea kuzinyonya nchi zetu, serikali yoyote ile duniani lazima iende na kufanya mambo yake kulingana na wanavyo taka wao, ikijifanya yenyewe inajua zaidi itang’olewa kupitia kile kinacho itwa demokrasia na hata wakati mwingine mapinduzi ya silaha yaliyo dhaminiwa na freemason wa Ulaya. Jamani kuna haja ya kutoa mifano ya nchi hizo ni zipi?

Benki za kitaifa zikapatikana, kama vile BoT ambazo kazi yake ni kusimamia taratibu za kibenki kwa vijibenki vingine ambavyo siyo ‘Central Bank’ taratibu ambazo ziliwaruhusu vijibenki vidogo dogo kukopesha zaidi ya kile walicho nacho nacho, vibenki hivyo vilitakiwa kuwa na kiwango maalum au uwiano baina ya kile walicho nacho na kile wanacho kikopesha, Loan to deposit Ration.



Mfumo wa benki ukabadilika, suala la fedha na dhahabu kama kipimo cha thamani ya bidhaa na huduma kikatoweka, na nafasi yake ikachukuliwa na jinamizi jingine kubwa, Deni. Mathalani kama unaweza kuzipata fedha za zamani kidogo karne mbili, tatu nyuma, utaona thamani yake ilikuwa ni sawa na kiasi flani cha dhahabu na fedha halisi. Lakini sasa hivi thamani ya sarafu au noti ni sawa na sarafu au noti nyingine, yaani bati kwa bati au karatasi kwa karatasi.


 Katika kipindi hicho benki binafsi ziliweza kutengeneza risiti badala ya fedha na dhahabu halisi, lakini watu walikuwa na uhuru wa kuzikubali au kuzikataa, kama ilivyo leo ambavyo mtu yupo huru kuikubali au kuikataa hundi anayo pewa na mtu mwingine. Lakini leo mabenki yaliyo pewa leseni na serikali yanaweza kuzitoa sarafu na noti ambazo zimetiwa baraka na serikali na benki kuu kama fedha halali kwa kiasi fulani cha malipo.

Ni kiasi gani cha fedha ambacho serikali na benki kuu wanacho weza kukitengeneza na kukipa thamani na kukiweka katika mzunguko?



Kipindi cha nyuma kiasi cha fedha au ‘risiti fedha’ zilizo kuwa kwenye mzunguko kulitegemeana na hitajio la bidhaa ambazo zilihitajika kununuliwa na fedha hizo. Mathalani kwa ajili ya kutimiliza hitajio la dhahabu na fedha halisi, wachimbaji iliwabidi kuzitafuta aridhini dhahabu na fedha kwa wingi na kuzipeleka kwa masonara ili sarafu ziweze kutengenezwa.

Lakini leo kinacho hitajikia ili kuweka fedha nyingi kwenye mzunguko ni taasisi za fedha ikiwemo mabenki kukopesha kwa wingi. Yaani fedha zinatengenezwa kwa kupitia mikopo, au kama nilivyo sema awali, kwa kutumia karatasi uliyo saini kama mkataba baina yako na benki ili uweze kupewa mkopo.



Benki wanacho angalia ni Fractional Reserve, au Loan to Deposit Ratio, na benki kuu ndizo zinazo simamia kuhakikisha kuwa mabenki hayapitilizi kiwango hicho, ingawa pamoja na hayo bado yanapitiliza kiwango hicho cha ukopeshaji. Kiwango hicho kinatofautina nchi hadi nchi. Mwanzo benki ilitakiwa kuwa na kiasi fulani cha dhahabu kama reserve, ili iweze kukopesha kiasi flani cha pesa mara kadhaa zaidi kushinda kiasi cha dhahabu halisi kinayo miliki, lakini leo, kiwango hicho cha ukopeshaji kinapimwa kwa kutumia fedha ambazo benki inazo zimiliki kwenye volti yake kwa uwiano wa mara kadhaa zaidi ya kile itakacho kikopesha kwa wanachi.



Kwenye buku rejea la Encyclopedia of Britannica, chapa ya kumi na nne, kuhusiana na benki na mikopo, inasema hivi, “Benki inatengeneza mikopo. Ni makosa kufikiri kwamba mikopo ya benki inatokana na pesa zinazo wekwa benki na wateja. Mkopo unao tolewa na benki, hiyo ni pesa mpya kabisa inayoingizwa kwenye mzunguko.”

Lord Acton, Lord Chief of Justice of England, 1875.
Suala ambalo limefanyiza ubaya kwa karne, na ambalo itabidi lipiganiwe ili liondolewe, punde tu au baadaye kidogo, ni wananchi dhidi ya taasisi za fedha (benki)”

Naye muheshimiwa Philip A. Bensoni, aliyekuwa raisi wa American Bankers’ Assosiation, mwaka 1939,Juni 8, alisema hivii, “Hakuna tena zaidi njia yeyote ya kuitawala nchi kushinda ile ya kupitia mfumo wake wenyewe wa mikopo.”

Kidogo tutizame namna benki zinavyo fanya kazi, kumbuka mfumo wa benki zote duniani ni mmoja, isipokuwa mfumo wa benki za Kiislamu, hivyo hapa tutatizama mfumo wa kibenki zisizo za kiislamu namna zinavyo fanya kazi.

Mathalani benki mpya imepewa leseni leo ianze kazi, benki hiyo inatakiwa iwe na kiasi flani cha fedha kama mtaji wake, kipindi cha nyuma ilikuwa ni gold, lakini kwa sasa hakuna tena gold ni pesa. Pesa hizo zinawekwa kwenye akaunti ya benki husika iliyopo benki kuu, tuseme benki yetu hii iliyo mpya resrve yake ni shilingi 1,111.12/-, tuseme kwenye nchi ambayo benki hii imefunguliwa Fractional Reserve ni 9:1.

Mlango unafunguliwa, mteja wa kwanza anaingia, anahitaji shilingi 10,000/- akanunue gari, kumbuka kwenye nchi hii ambayo benki yetu imefunguliwa, benki inaweza kukopesha mpaka mara 9 ya fedha ilioyo kuwa nayo. Benki itakacho fanya ni kuuchukua mkataba ambao imeingia pamoja na mteja wake na kuigeuza kuwa fedha.


Benki haiandiki barua au Memo kwenda benki kuu kuitaka ichapishiwe noti mpya zenye thamani ya shilingi 10,000/- Bali itakacho fanya benki ni kuandika tarakimu hizi 10,000/- kwenye akaunti ya mteja kwa kutumia keyboard! Kwa kufanya hivyo benki inakuwa imetengeneza pesa hewa mpya yenye thamani ya shilingi 10,000/- katika mzunguko.

Kisha mteja husika hujaza hundi yake 10,000/- kumlipa yule ambaye anataka kumuuzia gari. Kumbuka benki haikufanya chochote ila kuandika 10,000/- kwenye akaunti ya mteja, ambayo wakati wa kurejeshwa benki hiyo itahitaji na ongezeko la asilimia kadhaa kama riba, hapa kwetu benki zinatoza riba ya kuanzia 15 mpaka 24 na hata zaidi itategemea na aina ya mkopo. Kumbuka pesa ambayo benki imemkopesha mteja huyu haipo au kwa maneno rahisi benki haikuwa na pesa hiyo, lakini juu ya hapo benki inamtoza mteja wake huyu riba ya asilimi 20 na zaidi kwa fedha ambayo benki haikuwa nayo na wala haipo kwenye mzunguko fedha hiyo zaidi ya tarakimu zilizo andikwa kwenye akaunti ya mteja.



Aliyeuza gari anaichukua ile hundi na kwenda kuiweka (deposit) kwenye akaunti yake iliyo katika benki yake. Benki hii iliyo pokea hundi kutoka kwenye benki yetu mpya nayo inaweza kuikopesha pesa hii ‘mpya’ pesa hewa ambayo haipo katika mzunguko, lakini si kwa kuizidisha mara 9, lakini kwa kuigawanya kwa ile Fractional Reserve, hivyo kwa kutumia hundi hiyo benki hii ya pili inaweza kukopesha 9,000/- na 1,000/- itabakia kama Reserve ya benki.

Mkopo mpya ulio tengenezwa au pesa hewa hiyo nayo itakapo kwenda kuingizwa katika benki nyingine au hata hiyo hiyo, inakuwa ni halali kwa benki hiyo kuikopesha fedha hiyo kwa kutumia Fractional Reserve, nayo itatoa pesa hewa kama mkopo wa shilingi 8,100/- na shilingi 900 ikibakia kama Reserve ya benki. Hivyo kwa utaratibu huu benki zinaweza kutengeneza mpaka 100,000/- pesa mpya ambazo hazikuwepo popote hapo kabla, na wala hazipo kwenye mzunguko zaidi ya tarakimu katika akaunti za wateja.

Mfumo huu umebarikiwa, na asili yake ni sawa na mfano wa Sonara tulio uona, kwa kutumia mtaji wa 1111.12 benki imeweza kutengeneza fedha hewa kufikia 100,000/-  Hivyo mkopo unao tengenezwa na benki moja, ni deposit kwa benki nyingine. Hivyo benki zinatengeneza riba kwenye pesa zaidi ya shilingi 100,000/- ambazo haikuwa nazo. Benki zinakopesha fedha ambazo haikuwa nazo.

Pesa halisi iliyopo kwenye mzunguko ni 5% na 95% ni pesa hewa inayo tengenezwa na benki kwa kubadilisha mkataba iliyo usaini na mteja wake kuwa ni pesa, hela hiyo hapatikani popote kwenye mzunguko zaidi ya nambari zilizomo kwenye akaunti.

Unapo kwenda kuzitoa fedha za mkopo ambazo tunajua ni mrundikano wa tarakimu zilizo andikwa kwenye akaunti yako, ni kwamba unakwenda kuichukua ile 5% halisi ambayo tayari ipo kwenye mzunguko, hakuna pesa mpya halisi iliyo tengenezwa kutimiza hitajio lako la mkopo, hakuna, kilicho tengenezwa ni tarakimu tu ambazo wewe unazisoma kwenye akaunti yako. 




Ambazo zimetengenezwa kupitia mkataba wako ambao umeahidi kulipa mkopo huo, hiyo ni pesa mpya kabisa iliyo tengenezwa na benki, lakini ni pesa mpya ambayo hajapata kuwepo na wala haitapata kuwepo kwenye mzunguko, kwa sababu ni pesa hewa, nawe utahitajika kuilipa hii pesa hewa kama pesa halisi na jumlisha na riba! Benki ni waizi! Samahani nafuta usemi, mfumo wa benki ni wa uwizi mtupu.

Mkopo unapo malizika kulipwa, pesa ‘mpya’ iliyo tengenezwa na benki kwa kutumia mkataba wa mteja wake nayo inatoweka!


Mr, Regnald McKenna, wakati alipokuwa mwenyekiti wa Midland Bank ya London, alisema haya kuhusiana na benki, “ Ninahofia kuwa watu wa kawaida hawatapenda kuambiwa kuwa benki wana, fanya, tengeneza na kuiharibu hela. Na kwamba wale ambao wanao simamia mikopo hiyo ya nchi (mabenki) ndiyo wanao tengeneza sera za nchi na kwenye viganja vya mikono yao wameshikilia hatima ya maisha ya wananchi.”


Benki zinautumia mfumo huu kwa ushirikiano na serikali, yaani baraka za kiserikali kwanza lazima ziwepo kwa kupitisha sheria ya fedha ambayo inawezesha makaratasi hayo kutumika kama kipimo cha thamani kwa huduma na bidhaa zitakazo tolewa nchini au kwenye mipaka ambayo karatasi na bati (sarafu) hizo zitatumika.

Pili serikali zina yaruhusu mabenki binafsi kuziingiza sarafu na noti hizo zenye baraka ya serikali katika mzunguko na ikiwemo kulipia huduma na bidhaa mbalimbali. Tatu serikali inatoa leseni kwa mabenki hayo na taasisi zingine za pesa kukopesha makaratasi na sarafu hizo kwa wananchi wake na nne serikali na nne inapitisha sheria kuulinda mfumo huo na utaratibu wake wa ufanyaji kazi. 

Serikali haiwaambii wananchi wake ni wapi fedha zinapo tokea.

“Hatma ya nchi yetu ipo kwenye mikono ya watu wa benki na biashara yao ya kutoa mikopo hewa, ambao wanakopesha ahadi ya kutoa mkopo kwa fedha wasizo kuwa nazo. [Profesa Irving Fisher, mwanauchumi na Muandishi.]

Bila karatasi ambayo mteja amesaini kulipa mkopo, benki inakuwa haina cha kukopesha, yaani mkataba baina ya benki na mteja, ambao mteja anaweka dhamana baadhi ya mali zake, kisha benki kwa kutumia mkataba huo kwenye akaunti ya mteja wanaandika tarakimu ambazo zinalingana na kiasi mteja anacho taka kukopa. 

Kwenye mtazamo wa mteja tarakimu hizi zinakuwa ni pesa za mkopo zilizopo kwenye akaunti yake. Kwa vile serikali inautambua mfumo huu, na inatambua kuwa ‘pesa’ hewa za mkopo kutoka benki kwenda kwa mteja zinaweza kubadilishwa kuwa pesa halisi, pesa ambayo ni karatasi lenye sahihi ya viongozi wa serikali na alama za ajabu ajabu, moja kwa moja inakuwa ‘halali’ kwa benki kumpatia mteja wake makaratasi hayo kama ‘pesa’, lakini benki haijakwenda kuprint makaratasi hayo, bali imeweka tu tarakimu pale kwenye akaunti ya mteja, na mteja akishindwa kulipa makaratasi ambayo ni pesa hewa jumlisha na riba, alicho kiweka kama dhamana kinakwenda.

Unaweza kusema kuwa hii siyo pesa hewa, mbona nimezishika hapa mkononi sasa hivi baada ya kuandikiwa mkopo? Ulicho shika mkononi ni sehemu ya pesa ambayo tayari ipo kwenye mzunguko, lakini benki walicho fanya ni kwa nguvu waliyo pewa na serikali ni kuugeuza ule mkataba uliyo saini wewe kuwa ndiyo tarakimu zinazo ingizwa kwenye akaunti yako na kuwa ‘pesa’ benki haina fedha hizo inazo kukopesha, haina hata kidogo, ila inayo nguvu za kisheria kufanya mkataba wako kuwa ni tarakimu zitakazo geuka fedha, haya ni mazingaombwe ya kibenki.

Haujiulizi ni kwa nini, serikali, mashirika, makampuni, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, familia zote zinakuwa kwenye deni, tena madeni makubwa makubwa. Hujiulizi ni kiasi gani kilichopo cha fedha kwa ajili ya kukopeshea? Lakini sasa umejua, hakuna hata senti moja ambayo ipo kwa ajili ya kukopeshea, lakini watu bado tunayo minyororo mizito ya madeni kutoka taasisi za fedha.

Hivyo ‘pesa’ ni mkopo, kama mikopo yote italipwa hakutakuwa na pesa, 95% ya ‘pesa’ itatoweka.

“Hivyi ndivyo mfumo wetu wa fedha ulivyo, kama hakutakuwa na mtu anaye daiwa na benki katika mfumo wetu wa pesa, hakutakuwa na pesa yeyote.[ Marriner S. Eccles Mwenyekiti na Gavana kwenye bodi ya Federal Reserve.]”

Watu wanadhani kuwa ikiwa madeni yote yatalipwa basi hali za watu na uchumi zitakaa vizuri, lakini huu ni ukweli kwa sehemu tu ya watu, lakini endapo mikopo yote ikalipwa, hakutakuwa na hata senti moja ya pesa, uchumi wetu unategemea fedha hewa kutoka kwenye mikopo, na kila unapoisha unaongezwa.



Utaona benki pia zipo kwenye mikono ya maadui zetu, na wanapo taka jambo lao lifanyike ni amri tu inatoka na benki zinaacha kukopesha, zikiacha kukopesha mzunguko hewa wa pesa nao unatoweka, fedha za kulipa mkopo zinatoweka, kinacho fuata ni kile kinacho itwa anguko la kiuchumi, sasa itategemea maadui zetu waliaanda nini, inaweza kuwa ni mapinduzi ya serikali, vita au lingine lolote ambalo walilipanga, usisahau kukuibia utajiri wako halisi ambao uliuweka kama dhamana, si hakuna pesa hewa kwenye mzunguko, unadhani utalipa huo mkopo hewa na nini, utajiri halisi lazima uende.



NAAHIDI MTANANGE HUU WA PEOPLE vs BENKI UNAENDELEEA HAP HAPA, CHEKI HAPA NEXT TIME TUNAPO TIZAMA BALAA HILI LA MABENKI KWENYE ‘LEVEL’ NYINGINE ....

2 comments:

  1. Kaka mi cjaelewa hapo kwenye mkopo mf nimekopa nikapewa pesa yangu cash na cio kwa hundi apo pesa hewa inapatikanaje kwa bank.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni mchezo mdogo sana unao fanyika, lakini unahitaji akili ya ziada kuugundua.
      Kumbuka benki wanakopesha mpaka mara kumi ya pesa waliyo nayo. Kama kwenye vitabu vyao wanao shilingi 10, basi benki wanaweza kukopesha mpaka shilingi 100 kwa kutumia hiyo shilingi 10. Ndiyo maana benki wanawekewa kitu kinacho itwa Loan to Deposit Ration ili kuwaoongoza wasivuke kiwango cha ukopeshaji, vinginevyo hiyo shilingi 1o waliyo nayo wangeikopesha mpaka mara milioni na zaidi.

      Sali linakuja ikiwa wanayo 10 iweje wakopeshe mpaka shilingi 100?
      Kama wewe unayo shilingi 10 mfukoni nikija unikopeshe, huwezi nikopeshe shilingi 20, au 50 au 16, hapana utanikopesha shilingi 10 sababu hiyo ndyo unayo, lakini kwa benki ni tofauti, kile wasicho kuwa nacho benki ndicho wanacho kikopesha.

      Wanacho fanya ni kui-credit accaount yako kwa tarakimu na nambari zinazofikia kiwango cha pesa unachotaka, kisha utapewa hundi au cash money haijalishi, kinachojalisha ni kuwa KWA KUINGIZA TARAKIMU HIZO KWENYE AKAUNTI YAKO KAMA MKOPO, TARAKIMU HIZO NI FEDHA MPYA ILIYOINGIZA KWENYE MZUNGUKO. VITABU VYAO HAVINA PESA HIYO, WALICHOTUMIA NI KANUNI YA LOAN TO DEPOSIT RATION NA MKATABA ULIOSAINI.

      HAWAJAWAPIGIA BENK KUU WAWAPRINITIE FEDHA ZA KIASI HICHO MTEJA ANACHO TAKA. MTAJI WAO BENKI KUU HAULNGANI. YAANI NI MDOGO UKILINGANISHA NA JUMLA YA FEDHA WALIZO KOPESHA, WALA BENKI HAWAKOPESHI FEDHA ZINAZO LETWA KUWEKWA NA WATEJA HAPO, INGAWA KWA JICHO NA AKILI YA KAWAIDA NDIVYO INAVYO ELEWEKA.

      KILA BENKI INAPOTOA MKOPO MPYA, UJUE HIYO NI PESA HEWA MPYA ILIYOINGIZA KWENYE MZUNGUKO, NA KILA PESA UNAYO IYONA KWENYE MZUNGUKO NI MKOPO UNAO TAKIWA KULIPWA. NA KAMA MIKOPO YOTE ITALIPWA KUSIWEPO NA MTU HATA MMOJA NAYEDAIEA NA BENKI, BASI UJUE HAPATAKUWEPO NA HATA CENTI TANO KWENYE MZUNGUKO, FEDHA ZOTE ZITATOWEKA.

      ILI FEDHA ZOTE ZITOWEKE KWENYE MZUNGUKO LAZIMA WATU WENGINE WAPOTEZE ASSET ZAO KAMA NYUMBA, MAGARI NA MENGINEYO, SABABU BENKI WANAPOTENGENEZA MKOPO AMBAO NI PESA MPYA, HAWATENGENEZI NA PESA YA RIBA, HIVYO UKIJA MTAANI LAZIMA WATU WAKOPE ILI PAPATIKANE PESA YA KULIPIA RIBA, LAKINI KAMA MADENI YOTE YATALIPWA KUNA AMBAYE ATAKUTWA HANA PESA YA KULIPIA RIBA SABABU RIBA HAIKUTENGENEZWA KAMA ULIVYOTENGENEZWA MKOPO, MALI YAKO HALISI NDIYO ITAKAYO TUMIKA KULIPA RIBA.

      HEWA YA UCHUMI WETU NI MIKOPO HEWA YA BENKI, NA TIZAMA ANGUKO LA UCHUMI SIKU ZOTE LINAANZIA KWENYE MABENKI, SABABU WATU WAPO, VIWANDA VIPO, MALIGHAFI ZIPO, BARABARA ZIPO, WALAJI WAPO, LAKINI KITU KIMOJA TU KIKIONDOLEWA KWENYE MZUNGUKO UCHUMI WOTE UNAPOROMOKA KAMA NYUMBA YA MAKARATASI. SABABU UCHUMI UMESHIKILIWA NA MABENKI KUPITIA MIKOPO HEWA.

      tchao

      Delete