Kwenye tamthilia ya Lost, Eko alipoamua ‘kumpokea’ Bwana, Lock alikuwa amevutika sana akataka kujua ni kwanini
Eko kaamua hivyo, na Eko naye alitaka wafuasi kwenye ‘kanisa’ hivyo alikuwa na hamasa kumuelezea Lock, akamuambia, “Nitaanzia mwanzo”, Lock akasikiliza baada ya kitambo akamuambia Eko, “Sikujua kwamba uliposema unaanza,
mwanzo ulimaanisha MWANZO, (kitabu cha mwanzo kwenye biblia)”. Lock akaondoka
zake …..
Na mimi naanzia ‘mwanzo’, lakini haitakuwa mwanzo kama ya
Eko msije mkaondoka … ila nitapita kwa nukta moja ama nyingine kwenye kitabu
cha biblia pia.
Karibu jamvini tupo darasani na mwalimu kesha
fika.
Nukta moja ya msingi ningependa tuifaham kabla
hatujaanza darasa letu. Tukiachana na Darwin na wafuasi wake, nadhani sote
tuliobakia tunakubaliana juu ya uwepo wa vitu vitatu;
yaani, Roho, kiwiliwili,
na akili. Darwin na watu wake wanakubali viwili tu, yaani Kiwiliwili na akili,
roho wanasema haipo.
Kuhusiana na mtanange huo, rudi kwenye posti,
iliyokwenda kwa jina la ‘Namtafuta Mungu’, nilielezea kwa kina juu ya hili.
Turudi kwenye nukta ninayo taka kuitambulisha
kabla ya kupiga hatua nyingine mbele. Vitu vitatu nilivyo vitaja hapo juu,
ingawa viko pamoja lakini vina tofautiana sana kama mchana na usiku. Moja ya
vingi vinavyo tofautiana ni lugha.
Lugha ya akili na lugha ya roho, ni lugha
mbili tofauti. Asili ya vitu viwili hivi kama tutakavyo ona punde ni asili
mbili tofauti, hivyo tabia na maumbile yao ni tofauti na pia lugha ni tofauti.
Sababu dunia tunayo ishi imetawaliwa na nadharia
ya Darwin ambayo inaikataa Roho, lugha nayo tunayo itumia kwa kiasi kikubwa
nayo imegemea upande mmoja, ingawa Roho inaifaham vyema lugha ya
Akili/kiwiliwili, lakini Akili/Kiwiliwili kinapata tabu sana kuielewa lugha ya
Roho na ama haielewi kabisa; yaani ni dunia mbili tofauti.
Mwili/Akili/Kiwiliwili ni ‘Three Dimensional’ (3D) yaani Kimo, Urefu na Upana. Wakati Roho ni ‘Mult Dimensional’. Nikisema mult-didimensional
kwa lugha nyepesi namaanisha ni zaidi ya 3D.
Sababu lugha tunayo itumia inaeleweka zadi
kwenye 3D, au kwa uwazi zaidi kwenye akili zetu, kuna nukta zingine nitatoa
maelezo ya ziada pale ambapo lugha ni ‘mult dimension’ lakini imetoholewa na kuingizwa kwenye 3D.
Katika vitabu vya dini, na hasa nikizungumzia
dini kuu 3. Asili ya uumbaji ni moja.
KWAMBA ALIKUWEPO MUNGU NA HAKUKUWA NA CHOCHOTE
KINGINE.
Kisha Mungu akaanza kuumba kimoja baada ya
kingine.
“Na kumbuka aliposema Mola wako kuwaambia
Malaika kuwa anakwenda muweka msimamizi/kiongozi kwenye uso wa dunia …”(Quran: 38:71)
Katika aya hiyo limetumika neno ‘Khalifa’ ambalo
mzizi wake ni ‘Khalafu’ ambayo maana yake kilugha ni kuchukua au kushika nafasi
ya fulani baada ya kuondoka kwake.
Mathalani baada ya Mtume (saw) kufariki na
Abubakar Sidiq (ra) kushika nafasi yake, jina aliloitwa kama mtawala Abubakar
Sidiq (ra) ni Khalifat Rasullullah … ikiwa na maana kuwa yeye sasa ndiyo
kaishikilia ile nafasi ya utawala baada ya Mtume.
Hivyo aya hiyo kwenye Quran inatuambia kwamba
binadam anakuja kuishika nafasi hiyo, lakini yeye si wakwanza kupewa nafasi
hiyo, ila yeye anakuja baada ya aliye kuwa kwenye nafasi hiyo kuondolewa au
kuondoka.
Mathalani baada ya Mtume (saw) kufariki na
Abubakar Sidiq (ra) kushika nafasi yake, jina aliloitwa kama mtawala Abubakar
Sidiq (ra) ni Khalifat Rasullullah … ikiwa na maana kuwa yeye sasa ndiyo
kaishikilia ile nafasi ya utawala baada ya Mtume.
Hivyo aya hiyo kwenye Quran inatuambia kwamba
binadam anakuja kuishika nafasi hiyo, lakini yeye si wakwanza kupewa nafasi
hiyo, ila yeye anakuja baada ya aliye kuwa kwenye nafasi hiyo kuondolewa au
kuondoka.
Kulingana na mafunzo ya dini ya kiislam, kabla
ya kuja binadama katika mgongo wa aridhi, waliishi viumbe wengine waliofahamika
kama majini.
Viumbe hawa ndiyo walio kuwa wasimamizi au
viongozi kwenye uso wa dunia. Lengo la kuwepo viumbe hao kulingana na mafunzo
ya dini ya kiislam linafanana na lengo waliloumbiwa binadam ambalo ni kumuabudu
MUNGU MMOJA, BILA KUMSHIRIKISHA NA CHOCHOTE KILE NA KUSIMAMISHA UFALME WAKE
AHAPA DUNIANI.
Viumbe hao, majini walifanya fisadi kwenye uso
wa dunia na uharibifu kwenye nyanja zote za uchumi, kijamii na kiroho n.k,
mwisho wa siku waliadhibiwa na cheo hicho wakanyang’anywa.
Dunia ikabaki
kitambo kirefu bila msimamizi mpaka MUNGU MMOJA, alipompa amana hiyo binadam.
Haifahamiki ni kwa muda gani hasa utawala wa Majini
uliishikilia dunia kabla ya kuja binadam. Tofauti kubwa ya Majini na Binadam ni
kuwa Binadam tunayo roho na kiwiliwili, ikiwa majini wao wanayo roho tu bila
kiwiliwili. Majini japokuwa wanaishi kwenye uso wa dunia, lakini wanaweza
kwenda kwenye zaidi ya 3D, wakati binadam tunaishia kwenye uwanda wa 3D tu.
Binadam kupitia elimu maalum na mafunzo mahususi
anaweza pia kuifikia kwenye uwanda wa zaidi ya 3D, na mara nyingi tunakwenda
zaidi ya 3D tunapokuwa usingizini au kwenye ibada maalum au ‘meditation’, na
mtoto aliye chini ya umri wa miaka 3 na hasa miaka 2 kurudi chini wanao uwezo
mkubwa wa kuufikia uwanda wa zaidi ya 3D na mara nyingi wanafanya hivyo.
Kwa watoto, sehemu ya ubongo wa mbele, unao
husiana na mambo ya hiyari, kufanya maamuzi na kuhoji vitu inakuwa ndiyo kwanza
inajengwa, hivyo kipindi hicho mwili wake unakuwa sehemu kubwa unatawaliwa na
ubongo wa nyuma ambao kimaumbile hauathiriwi na sharia za kimaumbile kama vile
za kibaiolojia, fizikia, kemia, kijamii, kidini n.k, ubongo huu unaitwa subconscious level, na ndiyo ubongo unao utawala mwili wetu tunapokuwa tumelala, au kwenye
meditation, au tunapokuwa kwenye ibada flaniflani.
Hivyo kwa mtoto ni rahisi kuufikia uwanda wa
zaidi ya 3D sababu yuko ‘free’, wakati anapokuwa kwenye miaka 3 na kuendelea,
ubongo wa mbele, ‘front lobe’ unakuwa umeshika usikani, ubongo huu unasheria za
kutosha hivyo mambo ambayo yalikuwa yanawezekana hapo kabla sasa hivi kupitia
‘front lobe’ unaambaiwa haiwezekani.
Mathalani mtu mzima akikaa na mtoto wakatizama
filam ya Spiderman, mtu mzima atajua katu vile vitu haviwezekani, lakini mtoto
usishangae akatoka hapo na kuanza kuparamia madirisha na kusema yeye ni
Spiderman, sababu mtu mzima anatumia,
‘logic’, ambayo inakuwa ni kama kifungo wakati mtoto kila kitu kwake ni
‘possible’ …
unakumbuka ndoto zako za utotoni … ulitaka kuwa nani … je
umezifikia … au Mr. ‘Logic’ kakuambia haiwezekani?
Turidi kwenye mjadala wetu,
Ukiacha tofauti hiyo ya kimaumbile binadama na
majini hatutofautiani kitu kingine. Kulingana na mafunzo ya kiislam binadam na
majini ndiyo viumbe wawili pekee wanao itwa ‘viumbe huru’, tofauti na hayawani
wengine wote ambao wnafuata silka. Hayawani wengine wote hawana maamuzi binafsi
au uhuru alio nao binadam au jinni.
Kwenye otofauti huo ndiyo unapokuta kwa binadam
na jinni kuna lugha inayo itwa ‘halali’, ‘haram’, ‘takatifu’, ‘dini’, ‘ibada’,
mungu, miungu na mfano wa hayo, lakini kati huwezi kuikuta misamiati hiyo kwa
mnyama yoyote yule mbali na hawa wawili.
Makazi mahususi ya majini kwa ni mapangoni,
kwenye mashimo na mahandaki.
Kutokana na mafunzo ya kiislam, wakati jua
linazama (magharibi) wasilamu wana amrishwa kuwaingiza watoto wao ndani na
kufunga milango kwa kutaja jina la MUNGU MMOJA, sababu kipindi hicho ndiyo
mashetani wanatoka kwenye mashimo yao kuja kwenye uso wa dunia.
Unakumbuka hapo juu tumetaja kuwa watoto wadogo
wanao uwezo wa kuufikia uwanda wa zaidi ya 3D, na hapa utaona ni watoto ndiyo
wanatakiwa wafungiwe ndani tena kwa kutaja nina la MUNGU MMOJA, sababu watoto
wanaweza kuwaona majini na mfano wa hayo ambayo jicho la mtu mzima limepigwa
kufuli na ‘Mr. Logic’ hivyo hatuwezi kuona.
Hii ndiyo maana nyumba ambayo
imeathirika na mambo ya kichawi na ushirikina wa kwanza kuathirika anakuwa ni
mtoto.
Hivyo basi ingawa majini wanaishi kwenye mapango
na mashimo, lakini wanayo desturi ya kupanda juu ya mgongo wa aridhi, sababu
baadhi ya mahitaji yao mengine yanapatikana juu ya uso wa dunia.
Kwa mujibu wa mfululizo wa Makala hizi, mpaka
sasa hatujaona kiumbe mwingine mwenye maono huru na asiyefata silka peke yake
zaidi ya binadam na majini. Lakini si hivyo tu, mpaka sasa sayansi inayo egemea
mafunzo ya Darwin nayo haijaja na kiumbe huru zaidi ya binadam peke yake.
Ingawa uhuru wa binadam unatokana na yeye kuwa
ni roho yenye mwili, sayansi ya Darwin inasema yeye ni mwili usiyo na roho, na
hivyo uhuru wa binadam kwa upande wa sayansi ya Darwin siyo uhuru ulio kamili.
Hivyo ndiyo maana tunapata kitu kama, NWO,
Bigbrother, Illuminanti n.k ambao wanaonelea binadam ni kama hayawani wengine
isipokuwa binadam wachache kutoka kwenye familia chache mahususi wenye damu
maalum ndiyo wanaweza kuwa watawala na kuwasimamia binadam wengine wote kama
anavyo fanya mchunga kondoo kwa kondoo zake.
Mbali na filamu, vikaragosi, vitabu, tamthilia
na hadithi mbalimbali mpaka sasa ulimwengu wa Darwin na ndugu zake hawajaweza
kuthibitisha ‘beyound reasonable doubt’ juu ya kuwepo kwa kiumbe mwingine aliye
huru kama binadam, na kila wanacho kifanyia utafiti na kuja nacho kinayo kila
dalili ya kiumbe tunacho kiita ‘Jinni.’ Ingawa mbele ya hadhara sayansi hiyo ya
Darwin na jamaa zake inakana juu ya kuwepo kiumbe hicho, kama inavyo kana juu
ya kuwepo kwa roho, lakini nyuma ya mapazia mieusi wanakiri juu ya kuwepo kwa
viumbe hao na kushirikiana nao kufanikisha NWO.
Hivyo kutoka sasa nitasimamia juu ya viumbe hawa
wawili nay ale tuliyo yapita huko nyuma, sababu hadithi za ‘aliens’ na wenzao
mpaka sasa hazina mashiko, na si kwenye mfululizo wa Makala hizi tu, lakini
nenda kwenye chanzo chochote na tuletee Ushahidi ya kiumbe kilicho huru zaidi
ya binadam na majini na utaona ushahidi huo
unaangukia pua kama siyo kwenye majini.
Sababu NOW na wenzao wamefanya na bado
wanaendelea kufanya kazi kubwa ya kupotesha historia, na hili tutaligusia
kwenye hitimisho, ni kwamba kumekuwa hakuna vyanzo huru vyenye rasilimali za
kutosha kuweza kuzama kwenye bahari pana ya historia ya majini kabla ya kuja
binadama na hata baada ya binadam.
Kila tunacho kipata ni kipande cha karatasi,
tukilinganishe na mwamba Fulani wa kale, tuchanganye na hadithi ile ya zamani
ndiyo kwa mbali tupate picha ya nini hasa kilitokea, lakini pamoja na uduni wa
rasilimali na zana hizo bado picha tunazo zipata zipo ‘clear’ kushinda sokwe wa
Darwin.
Kutokana na mfululizo wa Makala hizi na kile
tulicho kiona, kuhusiana na baadhi ya kazi ambazo tumeziona kuna ambazo ni za viumbe hawa, majini, kuna zingine ni za Binadam, na zingine wamefanya pamoja kama tutakavyo ona.
Sehemu kubwa ya Maisha yao wanaishi chini ya
aridhi na mapango, ingawa mwandishi hakatai dhana kuwa sehemu ya miundo mbinu
hiyo ilikuja kutumiawa na kuendelezwa na vizazi vya Binadam baada ya kupewa
funguo za mamlaka ya aridhi.
Sehemu kubwa ya mahandaki na mashimo hayo leo
hayatumiki kwa sababu mbalimbali na iliyo kuu ni marufuku iliyopigwa na
serikali katika maeneo ambayo yapo mashimo na mahandaki hayo.
Tutarudi kwenye athari za kazi za majini kwenye
uso wa dunia, lakini kwanza turudi mbinguni kuliko tolewa taarifa ya
kuwa katika aridhi sasa atawekwa ‘Khalifa.’
Malaika wakauliza …
“... Je utawaweka wale ambao
watafanya fisadi na kumwaga damu ilihali sisi tunakutaja na kukutukuza na
kukushukuru ...?” (Quran: 2:30)
Swali la Malaika linakuja kutokana na historia
ya Majini na kile walicho kifanya, hivyo kuja kwa kiumbe mwingine ambaye
atayafanya aliyoyafanya mtangulizi wake haitakuwa sawa mbele ya Utukufu wa
MUNGU MMOJA ambaye wao malaika wanamtaja, kumtukuza na kumshukuru.
MUNGU MMOJA, akawajibu Malaika wake kuwa
‘Nayafamu msiyo yafahamu.’
“Allah mtukufu amemuumba Binadam kutokana na
udongo uliyochukuliwa sehemu mbalimbali kote duniani. Hivyo watoto wadam
wanakuja na rangi na maumbile kulingana na udongo ulipochukuliwa. Kuna ambao ni
wekundu, weupe, weusi na wengine baina ya hao (kati na kati); wengine wembamba
na wengine wanene, wengine wabaya (tabia) wengine wazuri (tabia), wapole na
wakorofi, wengine wachafu na wengine wasafi.” (Saheeh, At-Tirmidh.)
Udongo huo alio umbiwa Adam, ulichanganywa na
kufinywangwa na kutoa umbo la Adam akiwa mkamilifu likaachwa kwa kitambo
fulani, mpaka likabadilika rangi na kuwa na weusi (dark) na mkavu kiasi
ukiugonga unatoa sauti.
Ni katika weusi (dark) huo ndiyo tunapata jina
la Adam, ambalo linamaanisha Ngozi yenye weusi (dark skin). Ingawa neno Adam
kwenye baadhi ya mapokeo ya Mtume (saw) limekuja na maana mbili, ambapo maana
ya kwanza ni hiyo ya asili, likimaanisha ngozi yenye weusi (dark skin), lakini
maana ya pili, limetumika kuelezea ngozi yenye weupe (light skin).
Wakati
anatajwa Adam kwenye hadithi neno hilo linamaanisha Ngozi yenye weusi (dark
skin), na wakati anatajwa Issa/Yesu kwa neno hilohilo linamaanisha Ngozi yenye
weupe (light skin)
Hivyo basi baba yetu Adam Ngozi yake ni ‘dark
skin’, kama tulivyo ona hapo juu.
Lakini pia tumeona kwa nini watoto wake
baadae wamekuja kuwa na Ngozi tofauti, kama hiyo ya Issa/Yesu ya kwake ni light
skin, na hata ya kwako wewe msomaji ni tofauti na ya mwingine, hii ni kutokana
na aina tofauti tofauti za udongo na tabia zake zilizo tumika kumfinyangia baba
yetu, Adam (a.s).
Lakini tukirudi kwenye nukta ya msingi, hii
haimfanyi mtu mweusi kuwa bora dhidi ya mtu mweupe n.k, sababu mtu siyo mwili
au kiwiliwili chake, mtu ni Roho, na kiwiliwili ni jumba au chomb kinacho beba
roho na ambapo Roho, hakuna nyeupe wala nyeusi, nyekundu wala njano, kipofu au
kiziwi, kilema au mgonjwa, roho zote ni sawa kwa 100%.
N andiyo maana kwenye mafunzo ya dini ya kiislam
tunafundishwa kuwa
… Mola wetu hatizami miili yetu, wala mali
zetu, wala watoto wetu, lakini anatizama nafsi/roho zetu … na roho/nafsi iliyo
bora dhidi ya nyingine ni ile iliyo karibu kwa Mola wake kwa kufanya matendo
mema kwa ajili ya Mola wake ...
Ila kwasababu tunaishi kwenye dunia iliyo
tawaliwa na kushikiliwa na nadharia ya Darwin, ambayo haitambui uwepo wa Roho,
bali kiwiliwili tu, ndiyo maana leo hii, kila kitu thamani yake inapimwa kwenye
vitu, ‘materialisim’ … hata kwenye baadhi ya nyumba za ibada mwenye nacho ndiyo
anathaminiwa ambayo ni kinyume kabisa na hata malengo ya nyumba hizo za ibada.
WEWE NI ROHO YENYE KIWILIWILI NA SIYO KIWILIWILI
CHENYE ROHO.
“ … yule atakaye ingia peponi (Allah tujaalie
kuwa miongoni mwao), atapewa umbo kama la Adam, ambaye urefu wake ulikuwa ni
kubiki 60, ila watu walio fuata baada yake ukubwa wa maumbo yao umekuwa
ukipungua mpaka leo.” (Sahih Muslim)
“Allah alimuumba Adam, na akampa urefu wa kubiki
60 … watu walio fuata baada yake ukubwa wa maumbo yao umekuwa ukipungua mpaka
leo.” (Sahih Bukhar)
Kutaja hizo hadithi kwa uchache, zipo nyingi
zinaelezea umbo la Baba yetu Adam, kuwa urefu wake ulikuwa ni kubiki 60.
Kubiki 60 ukizileta kwenye lugha rahisi tunayo
ielewa ni futi 90 au mita 30!
Upo hapo?
Umbo la Baba yetu Adam, lilikuwa ni futi 90 au mita 30 kwa
urefu, nadhani ukipiga hesabu zako kichwani mwako utapata upana wake ulikuwaje!
Mtu mrefu sana leo hazidi futi 8! Kwa maneno
mengone ni kwamba tumepungua maumbile yetu kwa asilimia 90 na zaidi.
Ndugu yetu, mtanzania mwenzetu tunaye jivunia
nae kwa urefu Hasheem Thabeet, urefu wake ni futi 7 na nchi 3! Sasa hebu
fikiria kama Hasheem na urefu wote ule hauzidi futi 7, ni vipi basi ulikuwa
urefu wa futi 90!
Nadhani unaanza kupata mwanga sasa.
Kwa hiyo umbo kamili la vizazi vya Adam vilikuwa
kwenye futi 90, hawa tunaita ni MA-GIANTS.
Sema tena MA-GIANTS.
Umbo hilo la futi 90 likapuliziwa roho, ambapo
roho ndiyo kiumbe hasa kilicho kusudiwa kuishi ndani ya umbo hilo la futi 90.
Umbo hilo la futi 90 bila Roho lilikuwa ni
udongo mkavu unao toa sauti, na Roho inapohama, umbo hilo hurudi kuwa mavumbi
matupu, hurudi kwenye asili yake, hufa.
Kinacho kufa siyo Roho, kinacho kufa ni mwili,
roho inahama, ndiyo maana kwenye lugha ya Kiswahili, neno tulilo litohoa kutoka
kwenye lugha ya kiarabu, ‘Mufarakah’ au ‘Amefariki’ ‘Kufariki’, lina maana ya
kutengana, utengano, yaani mwili umetengana na Roho, na vinapo tengana ndipo
kifo hutokea, nacho huwa ni kifo cha mwili, sababu Roho itaendelea kuwa hai
kwenye kituo kinacho fahamika kama, ‘Barazaq’ kwa waislam, halafu itarudishwa
kwenye kiwiliwili mara nyingine na kusimamishwa mbele ya Mola wake akiwa na
umbo kama la awali, umbo la futi 90.
Kuna mengi yaliendelea hapo mpaka kufikia Adam
na Hawa kuteremshwa kutoka mbinguni nakuja kwenye uso wa dunia, kwenye Makala haya
nisingependa kwenda huko zaidi, ila ningependa kugusia nukta moja ya msingi
sana.
Nukta hii ni mkataba baina ya binadam wote na
MUNGU MMOJA. Kila mtu aliingia mkataba huu, wote waliokwisha pita kwenye uso wa
dunia, wote ambao wapo kwenye usi wa dunia, na wote watakao kuja mpaka siku ya
mwisho , tulisaini huu mkataba.
Kwenye Quran tunajifunza kuwa,
“Na Mola wako mlezi alipo waleta katika wana wa
Adam, kutoka migongoni mwa kizazi chao na akawashuhudia juu ya nafsi zao,
akawambia: Je Mimi si Mola wenu Mlezi? Wakasema: Kwani! (kwanini isiwe hivyo) Tumeshuhudia.
Msije mkasema siku ya kiyama sisi tumesahau makubaliano haya.” ( Quran 7:172)
Kwenye aya hiyo tunajifunza kuwa binadam wote au
watoto wote wa Adam tulisimamishwa mbele ya Mola wetu, na kuulizwa na Mola
wetu.
“Je Mimi si Mola wenu Mlezi.”
Tukajibu,
“Kwanini isiwe hivyo, hilo halina
shaka kabisa, wewe ndiye Mola wetu Mlezi.”
Tukaambiwa,
“Msije kusema siku ya kiyama kwamba
mlisahau huu mkataba.”
Je kuna yeyote anayekumbuka haya makubaliano?
Hakuna.
Swali kwanini, tusikumbuke mkataba muhimu kama
huu?
Guys Tchaoo, that is your homework …
Lakini nitalijibu swali hilo kwenye nuru ya
sayansi ya saikolojia na metaphysics …
Lakini mwalimu yoyote mzuri anapo toa ‘assignment’
kwa wanafunzi wake huwapa vitabu na rasilimali zingine zitakazo wasaidia kujibu
swali hilo…
Hivyo wanafunzi wangu wapendwa … kwa wale
wapenzi wa filamu ningeomba utizame filamu inayo kwenda kwa jina la, Déjà vu na
‘Manchuria Candidate’ zote zimechezwa na Danzel Washington, au Time Travelling
Machine.
Wale wapenzi wa series katizame series ya Lost
season 4 au 5.
Wale wapenzi wa kusoma, kasome kitabu kinacho
kwenda kwa jina la ‘The Music of Time', kimeandikwa na Preston Nicholos.
Au Project Super Man kimeandikwa na Michael Andrew Pero, au Trance - Formation of
America …
Till next time I say Tchaooo ...
Anhaaa Mbona umekatisha utamu sasa??!! Mpk lini? Ninavyokujua ww mpk miezi 2 hapo ndo tutakupata
ReplyDeleteSoon mdau, this time nataka niweke bandika bandua maana nina viporo vingi nataka viishe, so soon Inshallah ...
DeleteNataka nikutafute private Akh: Salim
ReplyDeleteHapana shaka, tuanzie hapa salimumsangi@gmail.com .. then mengine yataendelea
DeleteTupo pa1 sana
ReplyDeleteAllah akupe Fir'dausi
ReplyDeleteShukran
ReplyDeleteKaka umetoa ulibalikiwa na Allah, Allah akulinde na kila LA Shari wewe na kizazi chako
ReplyDelete