Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?
Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.
Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.
Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!
Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%
Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...
Friday, April 27, 2018
JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep 3 (Time Reference..)
Time, nyakati ni kitu cha ajabu sana … tulipo
ishia kwenye posti ya mwisho, itahitaji tujue kitu cha maajabu kinacho itwa
‘time’, bila kukijua hicho, hatuwezi kunyanyua mguu mmoja kwenda mbele.
Time ni mada pana sana, huenda siku moja nikaja
kuitiririsha hapa, lakini kwa leo nitaigusa kidogo kwa minajili ya mada yetu,
ili tuweze kulijibu swali tulilo achana kwenye posti iliyo isha.
Tumeona kuwa kile ambacho kinafikiwa na milango
yetu ya fahamu ni pungufu kwa asilimia 99.99..., dhidi ya kile ambacho hakifikiwi na
milango yetu ya fahamu kwenye ulimwengu wote.
Ulimwengu wetu tunaugawanya sehemu kuu
mbili, ulimwengu wa kiwiliwili, na ulimwengu wa roho. Asilimia 99.99 … % kwa
lugha nyepesi tunaweza kuita ndiyo ulimwengu wa roho, na kilicho bakia ndiyo
uliwengu wa kiwiliwili.
Hivyo kitu kinacho itwa ‘time’ tunaweza kukigawa
kwenye aina mbili hizi za ulimwengu, yaani ulimwengu wa kiwiliwili na ule wa
roho.
Time kwenye ulimwengu wa kiwiliwili tunaigawa
sehemu tatu, ‘past, present na future. ’Time’, kwenye ulimwengu wa roho haina
sifa hizo tatu tulizo taja, inayo sifa moja tu, ‘NOW’.
Neno ‘Present’ na ‘Now’ kama hayana tofauti,
lakini kwenye hili la kiumbe kinacho itwa ‘time’, maneno hayo yanayo tofauti,
na hapa ‘time’ tunaielezea kutoka kwenye nukta ya multdimensions.
Hivyo
tunajaribu kuitohoa ili iweze kueleweka kwenye 3D, ndiyo maana neno ‘present’
na ‘now’ nime yatofautisha ili walau kuweza kupata mwanga wa nini hasa ‘time’
kwenye multdimensions, lakini pia ‘now’ haitoshi kuelezea hasa hiyo nukta kama
ilivyo ya ‘time’ kwenye multdimensions, lakini walau itatupa mwangaza.
Mwishoni mwa WWII, Marekani walikuwa wamesha
shindwa vita vibaya mno, na walikuwa na kila sababu ya kutaka vita hiyo
imalizike.
Hivyo kipindi hicho kukawa na ‘project’ nyingi,
kubwa na za siri zilizokuwa zikifanywa kwa lengo la kutengeneza silaha ambayo
itawawezesha Marekani kuimaliza vita hiyo.
Moja ya ‘project’ hizo ni ‘Philadeliphia
Experiment’ ambayo ilifahamika kama ‘Rainbow Experiment’, lango la mradi huu
ilikuwa ni kutengeneza ‘elcotromagnetic’ kuizunguka meli ya kivita, na hivyo
kuifanya isiweze kuonekana kwenye rada ya maadui.
Meli iliyotumika kwenye zoezi hili ni meli kubwa
ya kivita ‘USS Eldridge’, ilipofika mwaka 1943 mpango ukakamilika na majaribio
yakafanyika. Lengo ilikuwa ni kuificha meli hiyo isionekane kwenye rada za
maadui, lakini jambo la maajabu likatokea, ‘mazingaumbwe,’ yakawa makubwa zaidi
ya matarajio.
Meli ya USS Eldrige, si kwamba ilipotea kwenye
rada ya maadui, lakini ilipotea mbele ya jicho la kawaida, na zaidi ilipotea
kwenye ‘time frame’ ya Philadelphia, ilitoweka kama kizuka, now you see it, now
you not. Kifupi ilitoweka kwenye 3D!
Masaa 24 baadae, meli hiyo ikaibukia Norfolk,
Virginia, mamia ya maili kutoka ilipo kuwepo awali! Napo iliibuka ghafla kama
kizuka, au utadhani imeshuka kutoka mbinguni. Hivyo kwa masaa 24 meli hiyo
ilikuwa kwenye ‘hyper space’ au multdimension, au uwanda wa zaidi ya 3D! Kisha
meli ikatoweka tena kutoka Norfolk, na kurudi Philadelphia kama kizuka.
Mradi ulikuwa umefanikiwa kwa lengo la meli
kutoweka kwenye rada, lakini ulifanikiwa zaidi sababu meli iliweza kutoweka
eneo hilo na kutokezea eneo jingine, kama kufumba na kufumbua.
Lakini mradi ulifeli kwa zaidi ya asilimia 100
kwa upande wa wanamaji na askari walio kuwemo ndani ya meli hiyo wakati
ikifanya safari zake hizo za maajabu kupitia ‘uchawi wa mzungu.’
Wanamaji, wafanyakazi na askari wote walikuwa
wendawazimu, hao ni wale walio fanikiwa ‘kurudi’ salama, wengine walirudi
lakini miili au viungo vyao vimenasa kwenye sehemu ya meli hiyo, yaani mtu
anaonekana kichwa tu, sehemu nyingine ya mwili haipo, au mkono tu, au nusu ya
kiwiliwili tu, na kuna wengine hawakurudi kabisa, walibaki kwenye ‘hyper
space’.
Si zungumzii uchawi, au ushirikina hapa, nazungumza
sayansi, tena sayansi ya daraja la kwanza, hamna bao wala ramli hapa.
Ni kama ‘science fiction’ lakini hilo ni kweli
lilitokea, fanya utafiti wako binfasi na utalipata hilo na zaidi.
Mwishoni wa miaka ya 1949 mradi wa ‘Project
Rainbow’ ulifufuliwa tena. Baada ya kile kilicho tokea hasa kwa upande wa
binadam wakati wa majaribio, serikali kwa maana ya bunge la Marekani
liliingilia kati na kuufunga mradi huo. Lakini mwishoni mwa miaka ya 1940 dude
likaamshwa tena, lakini mara hii wakiwa na lengo jingine tofauti.
The Dream Team
Mara hii wakiwa na timu ileile iliyofanikisha
‘Rainbow Project’, lengo ilikuwa ni kutizama kwanini binadam aliathiriwa na
‘electromagnetic’ kwa kiasi kile na vipi wanaweza kuliepuka hilo, sababu
walicho kivumbua kwa upande wa jeshi ni kitu adimu na lazima kiboreshwe na
kitumike, lakini kasoro zilizo jitokeza mara ya kwanza zisiweze kujitokeza
tena.
Iliwachukia miaka 10 kwa wanasayansi na
mainjinia hawa kuja na jibu au suluhisho dhidi ya kile kilicho wapata binadam
kwenye jaribio la kwanza la mradi.
Mara hii wakagundua kuwa binadam yoyote,
anapozaliwa anakuja na kitu kinacho itwa ‘time reference’, wakati wa ujauzito,
roho inapo dumbukizwa kwenye kiwiliwili inakuwa ina fungamanishwa na ‘time’ au
nukta ya kuanzia; hivyo kiwiliwili (mind), roho, na time vina fungamanishwa
pamoja.
Kumbuka kuwa time kama ilivyo roho inayo sifa za
‘multidimension’, lakini ‘time’ ambayo ina fungamanishwa hapo inakuwa ni ‘time’
yenye sifa za 3D, yaani (Past, present na future).
Lakini pia kama tulivyo sema hapo juu, time ya
kwenye 3D, siyo ukweli wote kuhusiana na kiumbe hichi tunacho itwa ‘Time’, bali
ni tuna amini hivyo kwasababu ndivyo maumbile yetu yalivyo, lakini si kila
unacho amini ni kweli, na hichi ni kimojawapo.
Time ni ‘Illussion’ iliyo jengwa kwenye
mazingira yetu haya ya 3D, na kama tulivyo ona, kwenye 3D, time inayo sifa hizo
kuu tatu, ambazo kwenye ‘hyper space’ sifa hizo hazipo.
Sasa basi kilicho wapata binadam walikuwepo
kwenye meli ile ya kijeshi ni kwamba meli ile ilikwenda kwenye ‘hyper space’
kabla yakuja kutokezea Norfolk, kisha ikarudi tena kwenye Hyper space, kabla ya
kutokezea Philadelphia tena.
Time iliyo fungamanisha na ‘roho’ na mind za
binadam wale ni 3D, lakini kwenye ‘hyper space’ hakuna 3D, ‘mind’ kiwiliwili
cha binadam hao, hakikiweza kumudu hicho; hayo maumbile mapya ya kiumbe kinacho
itwa ‘time’, sababu kwenye ‘Hyper space’ vyote present, past na future vipo
sehemu moja.
Yaani kwenye HYPER SPACE, wewe unazaliwa,
unaenda shule, unaoa, uko kazini, unakufa n.k vyote hivyo ndani ya ‘NOW’, siyo,
akili, wala kiwiliwili vinavyo weza kuhimili aina hiyo ya maumbile ya ‘TIME’,
hivyo miili yao, ikayeyuka, wengine wakapotelea huko, na wale walio himili na
kurudi kamili walikuwa wendawazimu.
Imepokewa kwa Abu ‘Abdir-Rahmaan ‘Abdullaah bin
Mas’uud (ra) kwamba:
“Ametuzungumzia Mtume wa Allaah (SAW) naye
ndiye msema kweli wa kuswadikika: Hakika kila mmoja wenu katika nyinyi
hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake kama mchanganyiko wa mbegu ya
uzazi ya mwanamme na mwanamke kwa muda wa siku arubaini; kisha kuwa kipande cha
damu kwa muda kama huo; kisha kipande cha nyama kwa muda kama huo. Kisha
hutumwa Malaika akampulizia roho ndani yake na akaamrishwa mambo manne:
Kuandika riziki yake, ajali yake, ‘amali yake na kama ni mwema au
muovu…” (al-Bukhaariy na Muslim).
Hadithi hiyo inatufundisha kile kilicho
gunduliwa kwenye ‘Rainbow Project’ na muendelezo wake, kwamba wakati ‘kiumbe’
anaye itwa roho anapoingizwa kwenye kiwiliwili kuna mambo ambayo yana fungamanishwa
naye ikiwemo, ‘Time’, hapo imekuja kama ‘ajali yake’, yaani umri wake au muda
atakao ishi mpaka umauti wake; ‘Time.’
Ndiyo utaona mara hii ya pili timu ya
wanasayansi, wakagundua kuwa, ‘time reference’ inakuwa pamoja na roho, wakati
roho inapo puliziwa.
Utakumbuka huko nyuma tumeona ‘Darwin na wenzake wanakana
juu ya uwepo wa roho, lakini utaona hapa kwenye kiwango cha kisayansi, tena
wanasayansi wa kiwango cha juu wanathibitisha juu ya uwepo wa roho.
Mradi huu kwenye hatua yake ya mwanzo, mtu kama
Albert Einstein, Testla na vichwa vingine, kwenye taaluma ya fizikia, mahesabu,
electromagnetic, metafizikia, nk; walikuwepo kwenye mradi huu, hivyo
hatuzungumzii wanasayansi wepesi wepesi.
Sasa basi ukisha mjua adui yako, umesha shinda
nusu ya vita, wanasayansi wale waligundua shida ni, ‘Time Reference’, ambayo
kwenye kiwiliwili na roho ni kama ‘orbit’ za sayari kulizunguka jua. Muda wote
sayari hizo zikiwa kwenye ‘Orbit’ zao, zinaendelea kuwa ‘hai’ na salama, na
ndivyo kwa binadam, muda atakao kuwa yupo kwenye ‘time reference’ ya 3D,
atabaki salama.
Kama nilivyo sema, dunia yetu kwenye uso wa
ulimwengu ni kama chembe moja ya chumvi, au kamchanga kamoja! Hapo binadam na
vurugu zake zote kwenye uso wa ulimwengu ni kakitu kasicho tajika, kaduchu mnooooo,
lakini mbali na yote hayo binadam huyu ame fungamanishwa na ‘network’ ya
jiulimwengu lote kupitia ‘timereference’, ambayo ni kama ‘orbit’ yake.
Kuna uwiano baina ya maumbile yetu na baadhi ya
vitu vya angani, kama nyota, mwezi n.k. Mathalani watoto wachanga wanaathirika
sana na mwezi unapokuwa kwenye vituo flani flani, kwa wale wazazi wanajua haya.
Lakini pia watu wazima kuna namna ambayo mwezi unatuathiri unapokuwa kwenye
baaadhi ya vituo. Athari hiyo moja ya sababu nyingi ni ‘time reference’, mwili
na roho zimefungamanisha na ‘time reference’ ambayo nayo inayo mafungamano na ‘electromagnetic’
za sayari yetu hii, tunayo iita dunia, ambayo nayo umefungamanishwa na
ulimwengu mzima.
Time reference ndiyo dira yako sasa kama kiumbe
kwenye ulimwengu huu wenye magalaxy, nebula, solar systems, sayari, nyota na kila
chungu ya kila tunachao kijua na tusicho kijua kwenye ulimwengu huu.
The cat in the box is dead and alive at the same time (time mystery)
Nukta yako ya maingiliano na ulimwengu huu,
kwamba wewe ni sehemu ya ulimwengu huu, ni ‘time reference.’ Ukitoka kwenye hii
‘time reference’, ni kama sayari inapo toka kwenye ‘orbit’ yake, inapotea
kwenye ‘space’, na kudhurika huko, hivyo na binadam ili asipotee kwenye ‘hyper
space’ orbit yake ni ‘time reference’ ya 3D.
Hivyo kilicho watokea watu walio kuwepo kwenye
meli ile ya kivita ya Marekani ni kwamba, walihama kwenye ‘time reference’ ya
3D, na kuingia kwenye ‘Hyper Space’ ambako nako kunazo ‘time’ za aina kwa aina
na idadi yake ni ngumu kuzidhibiti, huwenda ikawa na matrilioni kama siyo
mazilioni ya ‘time’ tofauti tofauti, na ndiyo maana kuna ambao hawakurudi mpaka
leo, kuna ambao viuongo vyao vilibaki huko na walio rudi walikuwa ni
wendawazimu.
Kwenye tamthilia ya Lost, kwa wale walio tizama,
mtakumbuka baadhi ya matukio yaliyokuwa yanahusiana na ‘electromagnetic’,
pamoja na ‘time shift’
Desmond, kwenye tamthilia hii, mwili wake
uliweza kuhimili ‘electromagnetic’ kwa kiwango cha juu mno. Hivyo aliweza
kuhimili kusafiri kwenye ‘hyper space’ na 3D lakini alihitaji kitu kinacho itwa
‘Constant’ kumfanya asiweze kupotea, anapokuwa kwenye ‘Hyper Space’ na
anaporudi kwenye 3D aweze kukumbuka nini kilimtokea kwenye ‘Hyper Space’.
Hicho kinachoitwa ‘constant’, ndicho ambacho
timu hii ya wanasayansi walikigundua na ndicho ambacho kinatakiwa kuwepo pamoja
na mtu anayesafiri kwenye ‘hyper space’ ili kumu wezesha au kumbakisha na
kumbukumbu kama vile yupo kwenye ulimwengu wa 3D.
Wanasayansi hao wakaja na suluhisho la
kutengeneza kile kitakacho fahamika kama ‘alternate reality’ au ‘artificial reality’.
Hii inatakiwa kuhakikisha kuwa wakati watu hao wakiwa kwenye ‘Hyper Space’,
kiwiliwili au akili zao ziendelee kusoma ‘time reference’ ya kwenye 3D, kama
vile bado wapo kwenye dunia yetu hii.
Walicho fanya wanasayansi wale ni ‘ku-streaming’
bila kukoma mazingira ya sayari yetu hii, kupitia kompyuta, kwenda kwa watu
ambao wako kwenye meli na hivyo kuwafanya wahisi bado wako kwenye ulimwengu wa
3D, wakati wakisafiri kwenye Hyper space.
Hilo lilifanikiwa, … mengi yaliendela
baada ya hapo lakini kwa ajili ya majibu ya swali letu haya yanatutosha.
Tururdi mbinguni
Kwenye aya ile ya Quran; (7:172), tumejifunza kuwa tulisaini
mkataba na MUNGU MMOJA, lakini kwa sababu tusizo fahamu hakuna kati yetu
anayekumbuka kuingia mkataba huo na MUNGU MMOJA, na wengine kufikia kusema
hakuna kitu cha namna hiyo!
Lakini hapa tumejifunza kitu kimoja muhimu sana,
japo kwa uchache lakini kwa muktadha wa mada yetu; tumejifunza kuwa time ni ‘mystery’,
lakini inayo mafungamano mahususi na roho na kiwiliwili chetu. Zaidi kila
ulimwengu unayo ‘time reference’ yake tofauti na ulimwengu mwingine.
Mkataba ulifanyika kwenye ulimwengu mwingine
ambao ni ‘Hyper Space’ (mbinguni), tulipokuja duniani kwenye uliwengu wa 3D,
tuka fungamanishwa na ‘Time reference’ ya
hapo. Kimaumbile kama tulivyo ona awali, nukta hiyo ya mkataba inafutika hapa
kwenye 3D, lakini haimaanishi kuwa haipo au haijatokea.
Kama tulivyo ona kwenye Hyper Space, wewe ndiyo
unazaliwa, ndiyo unakufa, ndiyo unaowa, ndiyo unapata mtoto wa kwanza, ndiyo
unapata mtoto wa pili na kuendelea, ndiyo unakufa, ndiyo tunakuzika, ndiyo
tunafanya kumbukumbu ya kifo chako na mengine na mengine, yote yanafanyika
kwenye nukta moja inayo itwa NOW.
Yote yamesha tokea na yamesha fanyika, tena kwa
ukamilifu wake.
Je kuna unalo kumbuka kati ya hayo?
Jibu ni hapana.
Kwanini?
Sababu hiyo ni nukta ambayo kwenye 3D, huwezi
kuifikia bila kuihama hii ‘Time referenece’ na kwenda kwenye ‘Hyper Space’ au ‘Hyper
Dimensional’.
Ndiyo maana kwenye ile aya, MUNGU MMOJA,
anatugusia tutakacho kisema siku hiyo, hatutasema kwamba hatuja saini huo
mkataba, bali tutasema ‘tulisahau/ tulighafilika/ tuliyafata tuliyo wakuta nao
wazee wetu, lakini hatutakana kuwa hatukufanya hayo makubaliano.
MUNGU MMOJA, kwa
Rehema zake ikawa kila zama anatuma mitume, na moja ya mengi waliyo tukumbusha
ni huo mkataba, na walikuja na dalili na hoja ambazo zilithibitisha kuwa
hawakutumwa na mwingine ila MUNGU MMOJA, hivyo ujumbe wao ni wa kweli na walilo
kuwa wakitukumbusha ni la kweli.
Tulikuwa mbinguni, kabla ya kuondoka, tukaona ni vyema, tukalizungumzia hili la 'mkataba' tuliyo usahau, ... nimeweza kuweka sababu za kwa nini tumesahau, na tena kwa kuangalia upande wa sayansi ya roho, kiwiliwili na akili bila kusahau dini kwa ujumla wake ... nadhani nimelijibu vizuri swali hilo ni kwenu nyie wasomaji kutoa dukuduku sasa ...
Next time tunarudi duniani Inshallah ... na tutakutana na ushahidi wa kushikika juu ya kuwepo kwa binadamu mwenye maumbo makubwa kama kimo cha Adam (as), ushahidi juu ya binadam kuishi na Dinosari kipindi kimoja, n.k
STAY HERE, STAY IN NOW .... See you soon Guys .... Tchaoooo ....
Mdau hii ni 'Quantum Physics' huipati ila chuo, tena inafundishwa kwa wale ambao vichwa vyao vimetulia ... kwenye elimu hii sayansi na roho zinakutana uso kwa uso.
Hata advance hawafundishwi fizikia ya namna hii, ndiyo kwanza wanafikiria namna gani wataweza kuifundisha kwenye vyuo vikuu, tena vipande vipande na siyo yotee...
Kama hii ni Phiysics Basi ni ya Advanced level,nimepata Concept ya hii Mada,ila Asante Kaka umefanya kazi,tupe uhondo na utamu
ReplyDeleteMdau hii ni 'Quantum Physics' huipati ila chuo, tena inafundishwa kwa wale ambao vichwa vyao vimetulia ... kwenye elimu hii sayansi na roho zinakutana uso kwa uso.
DeleteHata advance hawafundishwi fizikia ya namna hii, ndiyo kwanza wanafikiria namna gani wataweza kuifundisha kwenye vyuo vikuu, tena vipande vipande na siyo yotee...
DeleteHatar ila tupo pa1
ReplyDeletekaka Msangi, naitwa Kimaya tuliwasiliana kule facebook kuna mambo nahitaji tujadili kwa kina zaidi kuhusu mapokeo ya kazi unayofanya kwa jamii zetu.
ReplyDeletenaomba unitafute kaka 0625 522 322 ama facebook kwa jina la Mwinjuma Kimaya
Baba bandika bandua naona imefeli kwa kweli,nachungulia natoka mwezi huu
ReplyDeleteBaba, episodi hii ya mwisho ilikuwa ndefu nilitaka ni ikate tena lakini nikaona beta niimalize that why ikachelewa kidogo.
ReplyDeleteAseeee
ReplyDeleteHii elimu sijui binadamu wametoa WAP
Mungu ni mkubwa
Kivipi tuhukumiwe kwa mkataba tucioukumbuka nieleweshe please
ReplyDeleteRudia tena kuisoma post ... mwishoni nimeeleza kwanini bado tuko 'responsible' na tunayo yafanya a.k.a mkataba uleee ...
Delete