Kwenye mfululizo wa Makala hizi, kwenye season 1
na 2, juhudi kubwa imefanyika kuonesha kwamba, kabla historia tunayo ijua
haijaanza kuandikwa palikuwepo na jamii iliyo ishi na iliyo endelea kwenye
nyanja zote unazo zijua, kwa maendeleo makubwa ambayo leo kwenye karne ya
ishirini na moja, ya sayansi na teknolojia hatuja ‘ota’ kuyafikia!
Maarifa waliyo kuwa nayo, japokuwa ushahidi
tulio nao dhidi ya maarifa na elimu yao ni wa vipande vipande, lakini
unashangaza na kumuacha kila mmoja na maswali pasina majibu.
Mathalani ni vipi watu wa Maya walikuwa na
kalenda makini, sahihi na bora kushinda kalenda tunayo itumia leo karna ya ishirini
na moja.
Ni vipi Pyramid la Khufu linabakia kuwa moja ya
majengo makubwa, mazito kuwahi kusimamishwa kwenye uso wa dunia, n ahata leo
kwa taaluma zote tulizo nazo hatuwezi kusimamisha mfano wake?
Ni kipi kilicho wapelekea watu wa Babilon
kutengeneza betri za umeme miaka 4000 iliyopita?
Ni wapi Wagiriki na Waroma wa kale walipata
taaluma ya kuwa kuna sayari nyingine Zaidi ya Sartun?
Tunaweza kweli kuikana dhana na Zaidi ukweli wa
msingi kwamba, kabla historia haija anza kuandikwa, palikuwa na historia
nyingine kubwa kushinda ya kwetu ambayo imefichwa?
Ni vipi mtu utaweza kujibu maswali haya pasina
kukubali uwepo wa historia nyingine tofauti na hii ya Mjomba Darwin?
Ni kipi kilicho kuwa kikiwasukuma wanfalsafa wa
Kigiriki na watawa wa Brahmin India, kuzungumzia uwezekano wa kwenda kuishi
kwenye sayari nyingine? Kumbe hata kwenye hili sisi si wa kwanza?
Je watu wa kale walikuwa na taaluma ya ‘dhahabu’
kuhusiana na usafiri wa angani, hasa kile kinachoitwa, ‘antigravitation’ au ni
vipi basi utaelezea ujenzi wa Pyramid na mfano wako ambao ulihusisha ubebaji wa
mawe yenye Zaidi ya tani 1000! Ni vipi utaelezea ngano za waungu kama Isis na
wengineo walio kuwa wanarukwa angani?
Ni vipi kuhusu taaluma ya taa zinazo waka maelfu
ya miaka na hata milele, je ni nishati ipi waliyo itumia, ni wazi ni zaidi ya
umeme na hata zaidi ya nyuklia, nadhani dunia ingekuwa wapi leo kama na sisi
tungekuwa na nishati hiyo? Je taa inayo waka kwenye kaburi la Kennedy mpaka leo
inatumia nishati hiyo, au imechagizwa (inspired) na hadithi ya taa zilizo waka
milele?
Vipi kuhusu hadithi za marobotika, tumejua
Sophia siyo robotika wa kwanza kuwa na ‘artificial inteligence’ duniani, Plato
alikuwa na robotika wake ambaye ilibi amfunge asije kukimbia. Je tumeiga hili
kutoka kwenye historia iliyo fichwa kama taa ya kwenye kaburi la Kennedy na
kisha kujinadi ‘tumevumbua’?
Mbona taaluma ya kutengeneza na kuendesha ndege
imeandikwa vya kutosha na kwa lugha rahisi kwenye historia ya kale, kuliko
tunavyo andika historia ya binadam wa Darwin? Ni vipi pawepo na maelezo juu ya
ndege na aina zake kama hawakutengeneza na kuzitumia ndege hizo?
Kama binadam wa Darwin ndiyo kwanza yupo kwenye
hatua ya juu Zaidi ya kimaendeleo ni nani aliyefanya kazi zile za Sanaa zinazo
toa nuru ya kuififisha Sanaa yetu isionekane ni kitu chochote mbele ya kazi
hizo za kale za Sanaa?
Ni vipi karne arobaini na tatu zilizopita
‘wanaanga’ wa China waliweza kuuelezea mwezi kwa taarifa ambazo ndiyo kwanza
tunazithibitisha leo, na BADO HATUJAWEZA KWENDA MWEZINI.
Kwa kila hali walikuwa wameendelea kivitu kuliko
tunavyo weza kusema sisi tumeendelea.
Lakini haikuwa habari ya kona moja ya dunia, na
kona nyingine ni giza, hapana, maendeleo hayo yalikuwa kwenye pembe zote za
dunia, kila jamii, kwenye kila bara wanazo hadithi za kale zinazo fanana,
kuhusiana na ‘golden age.’
Unafaham kuwa ‘mvumbuzi’ wa simu Alexander
Graham Bell, baada ya ‘kukivumbua’ kifaa hicho alisema, ‘The old devices have been
reinvented’. Yes, ndivyo alivyo sema Bell.
Lakini mshindi
wa ‘Nobel Prize’, kwenye fizikia, ambaye ni mwanasayansi mkubwa wa Uingereza
Frederick Soddy naye alisema kuhusiana na taaluma hiyo ya kale, ‘not only have attained our present
knowledge, but a power hitherto unmastered by us?’
Kanakwamba Bell na Soddy hawajasoma kuhusiana na
evolution, ama wamesoma vyanzo vingine vya sayansi na historian a vya kale
zaidi, vyinginevyo wasinge kuwa na mawazo hayo.
Tumeona kwenye safari yote hii, tunacho kisaka, si
kwamba kimeegemea kwenye taarifa na nyaraka za kale tu, lakini pia kwenye
uvumbuzi wa kisayansi wa masalio yenye kuonekana na kushikika!
Ushahidi huo unaongezeka siku hadi siku, kwamba
siri zote za sayansi na teknolojia ya leo, vilikuwepo, vilifanyika, vikatumika
kale kwenye zama zilizo sahaulika au kwenye ukurasa uliofuta kwenye historia.
Itazame Egypt, miaka 3000 KK, ghafla kutoka
kusiko julikana Egypt ile pale, imeendelea, kiuchumi, kiasa, kijamii na hata
miundo mbinu yake.
Hakuna jamii inayo endelea ghafla namna hiyo,
hatuoni kiunganishi baina ya binadam wa Darwin na Egypt.
Hakuna kipindi cha mpito, labda imeanzia pale,
ikafika hapa ndiyo ikasogea pale, hakuna, ghafla tu Egypty inayo mahekalu,
Pyramid ambazo mpaka leo hatuwezi kuzijenga, Sanaa ya hali ya juu, mitaa na
barabara zilizo pangika, matumizi ya kuandika kwenye karatasi, matumizi ya
desimali kwenye hesabu, na matumizi ya sifuri.
Jamii tayari inayo mgawanyo
maalum, wanasiasa, wafanya biashara, wanajeshi, wafanyakazi wa kiserikali. Yote
hayo ghafla ndani ya 3000 KK?
Utazame Sumeria, Mesopotamia nazo ndani ya 3000
KK, kama zimeshuka kutoka mbinguni, zote zimekamilika, bila zile hatua za
kihistoria za kutoka kwenye hatua moja kwenda nyingine.
Nazca Peru, Uru Iraq ya leo, na miji mingine ya
kale tuliyo ipitia kwenye posti zilizo tangulia. Huoni zama za mawe, za chuma
au ujima, hakuna, wala humuoni binadam wa Darwin wala nyayo zake kwenye jamii
hizo, ni ghafla kama miji hiyo imeshushwa kutoka mbinguni ikiwa kamilifu.
Lakini ukiacha uwiano wa muda kwa maana ya 3000
KK, kwa jamii hizi pia bado pamoja na umbali na maelfu ya maili yaliyo kuwa
yaki zitenganisha jamii hizi, bado zilifanana mambo mengi kana kwamba asili
yake zote ni moja tu.
Kote kwenye jamii hizi za kale, alama na ichoro
mbalimbali imekuwa inafanana, hadithi ya mungu nyoka, mungu jua, swastika,
gharika kuu, waungu wanao ruka kwa ungo na mengine mfano wake, nenda China,
Egypt, India, Mexico kote utakutana na hadithi hiyohiyo.
Mfumo wa kuandika
Dunia nzima tukitamza mfumo wa kuandika kwa
maana ya tarakimu, herufi na alama, tukirudi nyuma 3000 KK au wakati na baada
ya 3000 KK tunakuta kote walifanana, kanakwamba tayari walikuwa na ‘globalization’
aka Utandawazi!
Lugha.
Maneno, matamshi, mizizi ya maneno na majina
kwenye jamii hiyo ya kale ni kanakwamba yote yalikuwa na asili moja. Asili ipi,
iliyo tokea wapi, lakini sote tunajua haikuanzia 3000 KK!
Ujenzi wa mahekalu na majengo mengine mfano wa
Pyramid, ulifanana si kwa muundo tu, lakini pia mali ghafi zilizo tumika,
mahesabu ya vipimo na muelekeo wake. Pyramid za Peru na Gaza zote zinazilenga
nyota fulani za angani.
Mila na desturi pia zilifanana, mathalani,
Egypty, Maya, Incas, Celts kutaja kwa uchache, walivifunga vichwa vya watoto
wakiwa wachnga ili kutengeneza fuvu la kicha kuwa kubwa kwa urefu. Mafuvu hayo
yapo, kwanini walifanya hivyo, hiyo ni habari nyingine pana.
Jamii nilizo taja
hapo juu waliwafunga maiti wao na kuwapaka vitu na madawa maalum ili wasioze,
teknolojia hii hatunayo sisi, lakini tena nukta hizi zinathibitisha kuwa jamii
hizo zilikuwa zina muingiliano wa kidunia, leo tunaita globalization.
Tunaitafuta ‘X’, tunaitafuta nukta ya msingi
iliyo anzisha yote haya, ambayo tunajua haikuwa mwaka 3000 KK.
Mwanahistoriam mwanajiografia, mwanasayansi, na
wana fani zingine wote ukiwauliza ni wapi chemchem ya taaluma aliyo nayo
imeanzia, kama hata anzia 3000 KK, basi atakuja kuanzia Egypt, Roma, Ugiriki na
mfano wa hao kama ndiyo walimu au waanzilishi wa taaluma husika, lakini swali
ambalo linakwepwa kwa makusudi na ambalo halijibiki ni yupi huyo mwalimu wa walimu wetu?
Makala hizi zimeingia season 3 sasa, na kote
huko tulikuwa tukimtafuta huyo mwalimu wa walimu wetu na hapa tupo karibu
kabisa na mlango ambao ukifunguka, tutaona maajabu ndani ya maajabu na
tutakutana uso kwa uso na mwalimu wa walimu wetu.
Mifupa, mirefu kama nyumba na kimo kama bati lake,
imekutikana kwenye kingo za mto Amazoni, Amerika ya Kusini. Wataalam wetu
wanakadiria binadam mwenye mifupa hiyo, fuvu lake la kichwa linaweza kutosha
ndani ya chumba cha mita 1.5 kwa 2.5 na mwenyewe kuwa na urefu wa mita 12!
Profesa Carl Frailey, kutoka Ovreland Park, Kansas, anasema binadam huyo
anaweza kuwa na uzito wa tani 120! “Hii
itamfanya kuwa mzito kushinda Tyrannosaurus
rex… jinyama dinosari lilikokuwa zito kushinda wote”, alisema. (The Sunday Mail, Brisbane, November 17, 1991)
Masalio haya hayapo kwenye vitabu vya Darwin,
lakini haimaanishi kuwa hayopo, au hayajapata kuwapo, kifupi kila cha kale
kilicho kusanywa kwenye historia ya kweli kilikuwa ni kikubwa kuliko tunavyo
kiona sasa. Si chura wala farasi, siyo ndege wala jongoo, historia yao ya kweli
iliyoandikwa kwenye udongo viumbe hao walikuwa wakubwa maradufu kuliko tunavyo
waona leo, na pia binadam.
Karibu kwenye historia mpya ya ulimwengu,
historia ambayo huenda ndiyo mara ya kwanza unaisoma, au uliisikia, lakini huku
isadiki, na wala mimi si kazi yangu kukufanya uisadiki, ila nitakuonesha Ushahidi,
wa maandishi na ule wa kushikika, eidha utaelewa, utaamini, au utasadiki hilo
ni lako na ubongo wako …..
Guys, Google wamenipa tabu sana, kwa mambo yao
hayo ya ‘security’ flow ya blogi imevurigika, hasa kwenye page yetu ya ‘facebook’
hivyo nilikuwa na kazi ya kuihamisha, imenichukua muda, nadhani itanichukua
muda zaidi, lakini tunahama ‘blogspot’ wapi tunakwenda soon tutajua ….
Stay tune as always ... tunakaribia kuhitimisha mtanange huu ... Tchaooo
Tupo pa1
ReplyDeleteBig up bro
ReplyDeleteAllah akupe umri mrefu wenye manufaa
ReplyDeletekila la heri kaka...ukiona wanasumbua hamia telegram.....i think it is the best place too
ReplyDelete