Tangu taifa la
Marekani lilipoanzishwa, ni bidhaa mbili tu ndiyo limekuwa likiuza kote
duniani, na hakuna yeyote aliye faida na bidhaa hiz Zaidi ya Marekani yenyewe.
Bidhaa mbili tu ndiyo zimeifanya Marekani kuwa Super Power.
Marekani imekuwa na
inaendelea kuuza makaratasi yanayo itwa ‘Dollar’ na kila nchi kwa usalama wake
lazima iwe na makaratasi haya kwenye hazina yake ama ‘UCHUMI’ wa nch hiyo uonje joto ya jiwe.
Bidhaa ya pili
inayouzwa na Marekani kwa faida kubwa sana inatwa ‘Demokrasia’ nchi lazima
inunue biadhaa hiyo itake isitake. Bidhaa hii ‘definition’ yake ya ukweli
anaijua ‘Washington’ mwenyewe, sababu unaweza kuwa ‘umeinunua’ bidhaa hii na
unaitumia vizuri lakini Washington akasema ‘Hiri rijamaa harina Demokrasia’
akaja akakung’oa au unaweza hata usiwe na hiyo bidhaa lakini wala Washington
hakufati, pia unaweza ukawa nayo na ukawa unaikanyaga kanyaga tu wala
Washington asihangaike na wewe, lakini siku unataka kitu hapo ndani kwako, hiyo
bidhaa inayo itwa ‘demokrasia’ lazima utaitafuta definition yake na hautaipata,
maana ataingia kwa mlango huo huo.
Kwa kuiuza na
kuifanyia ‘masoko’ biadhaa hiyo Marekani imezivama kijeshi nchi Zaidi ya 70
kote duniani, Marekani imejaribu kupindua nchi zisizo pungua 34 ambazo
zilichaguliwa kihalali kupita hiyo bidhaa inayo itwa ‘demokrasia’, si hivyo tu
kwa ajili ya kuuza bidhaa hiyo Marekani imejaribu kupindua bila mafanikio nchi
zisizo pungua 19 ambazo nazo pia ni wateja wa hiyo bidhaa ya ‘demokrasia’,
lakini kama nilivyo sema ni Marekani tu ndiyo inayo jua maana hasa ya
‘demokrasia’ kama ambavyo ni Marekani tu ndiyo inayo jua tafsiri ya ‘ugaidi’.
Yote haya ni lazima
yafanyike ili kuhakikisha kuwa Marekani inabakia kuwa ‘the only super power’,
lakini kama tulivyo ona kwenye post iliyo tanguliwa, wimbo huo unaweza ukashuka
‘chati’ soon, na Marekani iko tayari
kuihatarisha Amani ya dunia, ikibidi kupigana vita vya kinyuklia na mataifa
yenye silaha za nyuklia, kwa sababu tu, ‘wimbo’ huo usishuke chati. Huo wimbo
unao itwa ‘America the Only Super Power’
aka ‘Still No 1.’ Aka ‘Shoot first think later’ aka …, You got to love da song, it never got old!
Huo
wimbo huo, ndiyo unao amua ni nani atakuwa mirithi wa Mflame Obama. Lazima awe
ni mtu ambaye si tu anajua kuyaimba vizuri mashiri ya wimbo huo, lakini pia
kucheza kwenye ‘beat’ yeyote ile utakayo pigwa …, unafikiri kati ya Hillary na
Trump nani nazo sifa za kuimba na kucheza wimbo huo kwa wakati mmoja?
Tangu Marekani akae
kwenye kiti hicho juhudi kubwa iliyo fanya ni kuhakikisha kuwa inabakia hapo
basi. Marekani ndiyo nchi pekee yanye vituo vya kijeshi kote ulimwenguni kuliko
nchi nyingine yeyote, na lengo la vya vituo hivyo ni kuhakikisha Marekani
inabakia, Still No 1. Wakati Uingereza ilipokuwa Super Power na ikiitawala
dunia, mbali na kufanya wizi kwenye makoloni yake na unyonyaji, lakini kidogo
walitengeneza miundo mbinu ya kuyafanya makoloni yake yajitutumue kwenye Nyanja
mbalimbali, tuliliona hili pia wakati Mjerumani ni mtawala wa Afrika Mashariki.
Lakini Uncle Sam, yuko tofauti kabisa, yeye anabomoa na kuvunja vunja hata vile
vichache na duni vilivyo achwa na wenzake, na kuiacha nchi hoi, dhoofu, taabani
inayo hesabu siku za kuishi. Lakini ikiwa lengo ni kuhakikisha anabaki kwenye
hicho kiti milele, basi njia na utaratibu anao utumia Marekani hauwezi
kuepukika, sababu taifa lolote litakalo achiwa listawi, au litakalo kuwa ni
uchochoro wa taifa jingine kustawi, taifa hilo lazima lipigishwe magoti na
kuomba msamaha, sababu ni tishio kwa Marekani.
Barack Obama
aliahidi ‘Change’ kwenye kampeni zake. Alipo pewa usukani, jiulize nani alipewa
nafasi muhimu kwa ajili ya hiyo, ‘Change’? Alikuwa ni Hillary Rodham Clinton,
Secretary of State (SS), mara tu baada ya Hillary kupata shavu hilo, binafsi
nilijiambia, hapa rais siyo Obama, rais ni Hillary Clinton, na habari ya
‘change’ ikawa ni kitabu kilicho fungwa na kutupwa kapuni, kitabu cha zamani
tulicho kuwa tunasomewa na Bush II, kikarudishwa mezani na mwana mama akaanza
kutiririka mistari. Unaijua kazi yake ya kwanza aliyo ifanya kama SS?
Marekani ni siasa
za mambo ya nje, zingine ni blah blah tu. Unataka kuwa rais wa Marekani tuambie
utaifanyia nini Marekani kwenye siasa za mambo ya nje; full stop. Siasa za
mambo ya ndani zitafanywa na raia wa Marekani wenyewe, kama alivyo sema
Kennedy, ‘ … ask what YOU can do for your country.’ Hillary Clinton inaonekana
wimbo wa ‘still no 1’ anaumudu kuimba na kuucheza.
Ilikuwa Juni 28,
2009 jeshi lenye silaha lilimpindua raisi aliyeingia madarakani kwa kupigiwa
kura, raisi wa Honduras, Manuel Zelaya. Japo nchi ya Hondoras imeinunua ile
bidhaa ‘adimu’ inayo itwa ‘demokrasia’, lakini nabii na muuzaji wa bidhaa hiyo,
mfalme wa dunia, na serikali yake, waliuchuna kama vile hakuna kilicho tokea,
mteja wao kapata matatizo baada ya kutumia bidhaa yao, lakini ‘service line’
zao hazikuwa zikipatikana katika kumsaidia bwana Manuel Zelaya. Hondurus ni
moja ya nchi ambazo serikali ya mfalme imeweka majeshi yake yenye nguvu hapo,
ingetumia tu jeshi lake na kuwaondoa waliofanya mapinduzi na kumrudisha Zelaya
madarakani, lakini haikufanya hivyo.
Ispokuwa mapinduzi
hayo Bi. Hillary aliyaita ‘Smart Power’. Lakini ni mapema mwezi huo kabla ya
mapinduzi Bi. Hillary alikuwa kwenye ndege na kutua kwenye nchi ya Honduras na
kuhudhuria kikao cha mwaka cha Oraganization of American State (OAS) kikiwa na
ajenda kuu; ‘Namna ya kuzuia Cuba isiondolewe vikwanzo’ vilivyofikisha umri wa
miaka 47 tangu kuwekwa. Vikwanzao ambavyo wengi wa wanachma wa OAS vinaviona
vikwanzo hivyo kama ni kumbukumbu iliyo pitwa na wakati ya Cold War. Nchi kama
Venezuela, Bolivia, na Ecudor wanaviona vikwanzo hivyo kama mfano wa wazi wazi
juu ya sera za kibabe za Marekani.
Katika kusaidia
nchi yake Manuel Zelaya ilivuka mstari mwekundu uliowekwa na Washington.
Alikuja na utaratibu wenye tija juu ya kulimaliza tatizo la dawa za kulevyia nchini mwake,
mwaka 2007 Zelaya alikuwa ni raisi wa kwanza kwenda Cuba baada ya miaka 46 na
akakutana na Raul Castro na kuweka mipango ya kidiplomasia na kuiendeleza nchi
yake, mbaya zaidi akajiunga na kile kinacho fahamika Alternativa Bolivariana
para los Pueblos de Nuestra América
(ALBA), ambayo ilundwa 2004 na Cuba ikishirikiana na
Venezuela kupitia maono ya Hugo Chavez. Washington hawakupendezwa na haya yote,
na Hillary alipokuwepo hapo wakati wa mkutano wa OAS hakuwa amemtizama mwenyeji
wake huyo kwa jicho zuri, na mara baada ya Hillary kuondoka, haikuchukua muda
na serikali hiyo ya Zelaya ikaondolewa, na Hillary akaita mapinduzi hayo ‘Smart
Power.’
Utakutana na Hillary
kwenye kesi ya Libya akiimba na kucheza wimbo wa ‘Still No 1.’ Inajulikana sasa
kote ulimwenguni kuwa walioipindua serikali ya Ghadaffi walikuwa ni mamluki
walio pigana vita kwa niaba ya Marekani, lakini Zaidi imefahamika kuwa Hillary
kama SS na ofisi ilishughulika vilivyo kufanikisha hilo.
Itaendelea Inshallah ....
No comments:
Post a Comment